MWONGOZO WA Tumbo Lisiloshiba - Newsblaze.co.ke

2y ago
2.2K Views
497 Downloads
1.41 MB
117 Pages
Last View : 7d ago
Last Download : 3m ago
Upload by : Hayden Brunner
Transcription

MWONGOZOWATumbo lisiloshibaNaHadithi NyingineUna maswali ya kudurusuUmeandikwaNaMonica NjoguSamson KeaPaul Njenga Ngethe.Peter Kamau M 2017 CLIMAX PUBLISHERS LTDi.

MwongozowaTumbo lisiloshibaNahadithi nyinginewahariri:Alifa ChokochoNaDumu KayandaKimechapishwa na shirika la uchapishaji wa vitabu la climaxIiliyoko jumba la Royal plaza, Kirinyaga rd Nairobi.Kenya0797 051 288Haki zote zimehifadhiwaHakuna sehemu yeyote ya uchapishaji huu inayopaswa kunakiliwa aukutumiwa kwa njia yoyote, Kielektroniki au kiufundi.Ni marufuku kuiga,kunakili, kuchapisha chapa au kukitoa kitabu hiki kwa mbinu zozotezile bila idhini ya mchapishaji.Kimepigwa chapa naClimax press Nairobi0722 823 142ii.

YaliyomoTumbo LisiloshibaSaid A. Mohamed.1.Mapenzi ya KifaurongoKennaWasike. 17/Shogake Dada ana Ndevu Alifa Chokocho .31Shibe InatumalizaSalma Omar Hamad .41Mame BakariMohammed Khelef Ghassany.45Masharti ya KisasaAlifa Chokocho .53Ndoto ya MashakaAli Abdulla Ali .62KidegeRobert Oduori .70Nizikeni Papa HapaKen Walibora .76Tulipokutana TenaAlifa Chokocho. 82Mwalimu MstaafuDumu Kayanda. 88Mtihani wa MaishaEunice Kimaliro. 96MkubwaAli Mwalimu Rashid .104iii.

1. TUMBO LISILOSHIBAHistoria ya Mwandishi.Hadithi hii imeandikwa na Prof. Said Mohammed, mwandishimtajika ambaye amewahi pia kuandika vitabu vingine vitajikakama vile Riwaya ya Utengano. Mwandishi huyu bila shaka ni gwijikatika ulingo huu kwani amewahi kuandika kazi zingine za fasihiandishi zikiwemo tamthilia, mashairi na hadithi fupi.DhamiraDhamira ni funzo kuu litokanalo na kazi ya sanaa au lengo kuu lamwandishi. Mwandishi wa hadithi ya Tumbo lisiloshoba alidhamiriakufunua uozo unaoletwa na ubinafsi na tamaa katika jamii. Aidhaanawajasirisha wanaoathiriwa kuwa wanaweza kukubali madhilawanayofanyiwa ama kupinga dhulma hizo na kusimama wima nakutetea haki zao.Ufupisho wa Hadithi.Hadithi hii inaangazia maisha ya watu wanaoishi katika mtaa waMadongoporomoka, mtaa ambao umepakana na jiji linalokuwakwa kasi mno. Jiji hili limeshiba kwa wingi wa mijengo iliyojengwak i a s i c h a k u a n z a k u t i s h i a u we p o wa m t a a d u n i waMadongoporomoka. Uvumi unawa kia wanamadongoporomokakwamba mtaa wao utanyakuliwa ili upanuzi wa mji u kie eneo hilo.Mwanzoni ulianza kama tu uvumi uliokuja na kupita bila yawanamadongoporomoka kuwa na uhakika nao. Ingawa uvumi huou l i i s h i a k u t ow e k a , M z e e M a g o k a t u h a k u wa r u h u s uwanamadongoporomoka kutupilia mbali wazo la uvumi huo kutimiana wao kuishia kufurushwa. Anawaleta pamoja wanakijiji wenzakeili kutafuta suluhishi kwa tatizo lililokuwa limewakodolea macho.Kwa pamoja wanakijiji wote wanakubaliana kutoondoka na liweliwalo. Hata ikiwa watafurushwa, wanaamua kutetea mtaa wao nakusalia.Kisadfa, bwana mmoja mwenye tumbo kubwa anawasili kwenyemkahawa wa Mzee Mago na kutaka kupewa chakula chotekilichoandaliwa. Ajabu ni kuwa anapokabidhiwa chakula hicho,1.

anafyeka chote fyuu! Ni ajabu kwani huyu jamaa ana “Tumbolisiloshiba”. Baada ya kula na kutoa bweu kubwa lenye harufumbaya, jitu linalipa na kuahidi litarejea siku iliyofuatia.Siku iliyofuata wanamadongoporomoka wanagutushwa namaporomoko yanayotokana na vibanda vyao kubomolewa namabuldoza. Wanafurushwa wote kwa nguvu. Vibanda vyaovinabomolewa na wao kuishia kufukuzwa. Ajabu ni kwamba“Bwana Tumbo” anarejea kama alivyoahidi. Ila wakati huu yukondani ya gari kubwa na dereva anayemwamrisha. Hivyo amerudikula kila kitu kama alivyoahidi ila wakati huu amekuja kulamashamba yao. Mzee Mago anawashawishiwanamadongoporomoka kutoondoka, licha ya dhulma hizo.Umoja wa wanakijiji hawa unawaokoa kwani muda mfupibaadaye, vibanda vyao vinaanza kuota tena. Wanafaulu kuzuiatamaa ya tumbo kubwa lisiloshiba la mji kutokula mashamba yao.MAUDHUIBaadhi ya maudhui yanajitokeza katika hadithi hii ni kama vile:a) Ubinafsi na tamaab) Unyanyasajic) Utetezi wa hakid) Umaskinie) Utabakaf) Migogoroa) Ubinafsi na tamaa (Tumbo lisiloshiba)Haya ndiyo maudhui makuu katika hadithi hii. Maudhui hayayanajengeka kwa kutazama jinsi ambayo wahusika fulanihawatosheki na mengi waliyokuwa nayo na hivyo basi kutamanividongo vya wengine na kutaka kuwahini. Wakubwa wa jijiwanadai kwamba jiji limejaa tayari hadi Pomoni. Halijaacha hatanafasi ya mtu kuvuta pumzi.2.

Jiji lenyewe limekuwa limesheheni usa , ujumi na tamaduni mbalimbali. Jiji limejaa hoteli, mikahawa, departmental stores, casinos,viwanja vya gofu, viwanja vya tenisi, voliboli, mpira wa vikapu,raga, kabumbu, vyuo vikuu, mahakama, hospitali, majumba ya o sina mengine mengi. Haya yote yamekuwa yamesimama wima jijini.Hapajasalia hata nafasi kidogo ya kuvuta pumzi. Hivyo basiwakubwa wa jiji waonelea vyema kwa ardhi ya watu waMadongoporomoka kutwaliwa. Hii ni tamaa ya hali ya juu.Wanataka wajenge majumba ya kifahari huko. Hawataki kuwalipawenye ardhi hiyo dhamana inayofaa bali wanataka tu kuwafurushawanamadongoporomoka.Mhusika “Bwana Tumbo” anaingia kwenye mkahawa wa MzeeMago. Ukubwa wa tumbo lake unashangaza wengi. Ni dhahiri kuwahuyu mtu ni mlaji hodari. Jamaa huyu anaishi kuulizia chakulakilichopo kwenye mkahawa na kukila. Anakula chakula chotekilichoandaliwa kwa walaji wengine wote. Anamaliza chakula nakuongezewa kingine. Anakula nyama ya kuchoma, mchuzi wanyama, wali wa nazi, samaki wa kukaanga, chapatti kadhaa nakuishia kuteremshaa na chupa mbili za Coca cola. Anafagiamkahawa wote. Anaahidi kurejea siku itakayofuata na kutakachakula kipikwe mara mbili Zaidi ya kile kilichopikwa siku hiyo. Hii nitamaa ya ajabu. Watu waliokuwepo kwenye mkahawa wanabakikushangaa ni vipi mtu anakula chakula chote kilichoandaliwa walajiwote kwenye mkahawa?Bwana mwenye tumbo ana tamaa ya mashamba. Anajaribukuwafurusha wanamadongoporomoka kutoka kwenye makaaziyao. Anawarausha asubuhi na mapema kwa mabuldozayanayobomoa makaazi yao. Inakusudiwa kuwa majengoyatajengwa katika ardhi hii inayotamaniwa sana na wenye jiji.Anwambia Mzee Mago kuwa amekuja kula mashamba yao. Hii nitamaa ajabu ya mashamba yaliyo na wenyewe.3.

Jiji lina tumbo ambalo halishibi. Jiji hili limepambwa vyema namajumba ya kifahari. Jiji limejaa hoteli, mikahawa, departmentalstores, casinos, viwanja vya gofu, viwanja vya tenisi, voliboli, mpirawa vikapu, raga, kabumbu, vyuo vikuu,mahakama na hatahospitali. Ajabu ni kuwa jiji hili halijatosheka kwa usa wake. Jijilinataka kupanua tumbo lake hadi katika mtaa waMadongoporomoka.a) UnyanyasajiHii ni hali ya wahusika kuhiniwa haki ambayo wanastahili nabadala yake wengine kupewa haki hiyo kwa haramu.Wanamadongoporomoma wananyanyaswa na viongozi wa jiji.Licha ya wao kuwa wamiliki halisi wa mashamba yao,wanapangiwa hila ya kunyang'anywa vipande vyao vya ardhi.Ardhi hiyo inapangiwa njama ya kunyakuliwa bila ya wao kulipwa dia inayostahili. (Uk 4)WanaMadongoporomoka pia wananyanyaswa kisheria. Ni mujibuwa sheria kuwatetea watu wote ambao wamehiniwa au kutendewaisivyo haki. Mzee Mago anafahamu vyema kwamba kunauwezekano mkubwa wa wao kupokonywa mali zao ilhali shariaitumiwe kuwakandamiza yeye na maskini wenzake.Anaombawaishie kumpata hakimu ambaye ni mpenda haki ili haki isiuliwe naasiyestahili kuishia kutetewa na sharia mbovu. (Uk 2)Majengo makubwa yaliyoko jijini yananuia kuwanyanyasawanamadongoporomoka na kumeza vipande vyao vya ardhi.Vipande hivi vya ardhi vinanuiwa kutumika ili kuwahi kujengamajengo bora Zaidi. b) Utetezi wa hakiMzee Mago ametumiwa na mwandishi kama kielelezo cha mteteziwa haki ya wakaazi wa kijiji wa madongoporomoka. Mhusika huyuanawatetea madongoporomoka kutokana na maonevu ya wakuuwa jiji.alijitahidi kuzuia njama ya watu wakubwa kutaka kuchukuaardhi za watu wadogo. Mzee Mago aliwafuata wengine ilikuzungumza kuhusu haki ya unyang'anyaji wa mashamba yao. Yeyehupiga mbio huku na kule kujaribu kuzuia haki isiangamizwe. (Uk 2)4.

Kwa kuwa Mzee Mago anafahamu kwamba haki inauzwa nakupewa watu wasiostahili. Anajua kuwa haki itauzwa. Anafahamukwamba haki itapewa wengine wasiostahili. Hivyo basi anamtafutawakili mzuri ambaye hatasaidiana na viongozi dhalimu ili kuwahinimashamba yao.Mzee Mago anawahamasisha wanamadongoporomoka kutokubalikufurushwa kutoka maeneo yao. Hawaruhusu watu kusahau uvumiwa wao kufurushwa. Anawaita katika kikao na kuwakumbushauwezekano wa hao kufurushwa. Anawaongoza kutokubalikufurushwa ikiwa wakubwa wa jiji watakuja kuwaondoa kwenyemakaazi yao. Baadaye wanamadongoporomoka wanapovamiwa,wanakataa kuondoka hadi wiki tatu baadaye ambapo makaaziyao yanarudi kuchomoza kama uyoga. (Uk 11)a) UmaskiniNi hali ya kukosa mali/hali ya ufukara au ukata. Umma waMadongoporomoka unaishi katika hali mbaya ya kimaskini.Mandhari ya kijiji hiki ni ya kimaskini na kufedhehesha mno. Kunamashonde na vinyesi. Kuna vibanda vya uchwara vinavyozungukwana uoza na bubujiko la maji machafu. Kuna uvundo unaopasuamianzi ya pua. (Uk 4). Bila shaka, mandhari haya sio ya mahaliambapo mtu anaweza kufurahia kuwa. Ni mandhari ya mahaliambapo ni masikini tu ndio wanaishi.b) UtabakaHii ni hali ya wahusika kugawika katika makundi tofauti tofaautikulingana na uwezo wao wa kiuchumi. Kuna tabaka la matajiri namasikini. Kila tabaka limejikita katika shughuli zao wenyewe zakutetea matumbo yao. Masikini wanapigania kutetea makaazi yaoya kimaskini. Wanakataa kata kata kuhiniwa na wachache matajiriambao wanamiliki mali nyingi. Kwa upande mwingine, matajiriwana matumbo yasiyoshiba. Wananyakua mashamba ya masikinikwa minajili ya kutaka kuendeleza ujenzi wa majumba ya kifahari.Hivyo basi, matajiri wanaishi kuwafurusha masikini kutoka kwenyemakaazi yao. (Uk 10-11)5.

a) MigogoroKatika hadithi hii panazuka migogoro mbali mbali baina yawahusika tofauti. Kuna tofauti nyingi ambazo zinazuka kati yawahusika mbali mbali katika hadithi. Baadhi ya migogoro hii nikama vile:a) Mgogoro baina ya Wakuu wa Jiji na wanakijiji waMadongoporomoka.Mgogoro huu unatokana na hali ya jiji kupanuka nakusheheni kila aina ya majumba kiasi cha kukosa nafasi yamtu kuvuta pumzi. (Uk 4)Kutokana na hali hii, wakuu wa jijiwanaonelea kuwa mahali pazuri pa kupanua shughuli za jijilile ni huko Madongoporomoka. Huko ndiko kuna vijishambaambavyo havina kazi. Vishamba ambavyo vinapaswakupambwa na majumba mazuri ya kifahari. Kwa upandemwingine, maskini hawa wanaenzi vijumba vyao pamoja namazingira yao na hawako tayari kuondoka kwa njia yoyoteile. Hali hii inazua mgogoro kati yao na wakuu wa Jiji.b) Mgogoro baina ya Bwana mwenye tumbo na wanaMadongoporomoka.Bwana Mwenye tumbo ananuia kula mashamba ya wanaMadongoporomoka. Kwa upande mwingine, wanakijiji hawawanakaidi amri ya kuondoka, pamoja na madhila yakubomolewa makaazi yao wanamoishi. Licha ya mateso yotewanayoelekezewa wana-Madongoporomoka, wanakataakuondoka katika mashamba yao na kuruhusu ujenzi wamajumba ya kifahari kutekelezwa. Ni wazi kuwa huu nimwanzo tu wa mgogoro kati ya wahusika hawa hawa namporaji huyu wa ardhi.6.

MBINU ZA LUGHA NA UANDISHI.Hizi ni mbinu ambazo mwandishi hutumia ili kuleta mvuto katika kaziyake. Mbinu za uandishi ni sawa na mtindo wa mwandishi. Hizizinahusu upekee wa mwandishi kwa namna anavyoichora kaziyake. Mbinu za uandshi ni mbinu ambazo mwandishi hutumia ilikutupa sisi wasomaji ujumbe wa ziada. Mbinu hizi ni kama vilematumizi ya ndoto, barua, mbinu rejeshi,n.k. mbinu zilizotumiwakatika hadithi hii ni pamoja na:1. TakririTakriri ni mbinu ya kifasihi ya kurudiarudia neno au kifungu chamaneno ili kusisitiza au kulitilia mkazo. Mifano ya takriri ni kamaifuatayo:a) Ulianza uvumi. Uvumi ukageuka nong'ono. Nong'onozikafumbua kinywa kueneza wasiwasi. Wasiwasi ukawahofu (Uk 1).b) gwa sahau hiyo ni tokeo la lile lile la umoja katika uwili.(Uk 1)c) Mzee Mago kajifunza kutosahau. Kutosahau hamkumpi hatakidogo (Uk 2)d) Itikadi ya wakubwa ilikuwa bado ni ile ile. (Uk 2)e) Hawawezi hawawezi, hawawezi, kabisa hawawezi! (Uk 5)2. KinayaKinaya ni hali ambayo mhusika anasema au kutenda kinyumena matarajio. Mifano ya kinaya ni kama ifuatayo:a) maana siku hizi wanasheria waaminifu ni adimu kamahaki yenyewe. (Uk 2)b) Ilishikilia kwamba jiji halina nafasi tena. Yaani limejaa kilapahala. Limejaa hiki na kile, hili na lile. Limejaa hadipomoni. (Uk 3-4)7.

c) Halikuacha hata nafasi ya kuvuta pumzi. (Uk 4)d) “sharia gani hiyo iko mikononi mwetu?” Aliuliza MzeeMago. “Sheria kila wakati iko mikononi mwao.” (Uk 6)a)“Nitakula chakula chako chote ulichopika kuwauziawateja wako leo.” (Uk 8)1.TaswiraTaswira ni maelezo ambayo yanaunda picha fulani katika akili zamsomaji. Mifano ya taswira ni kama ifuatayo:a) Kuna mashonde na vinyesi. Kuna vibanda vya uchwaravinavyozungukwa na uozo na bubujiko la maji machafu. Kunauvundo unaopasua mianzi ya pua. (Uk 4).b) Wakati huu ndipo pua za wazungumzaji hawa ziliponasaharufu za vyakula vilivyotoka jikoni. Harufu mchanganyikozilizowaingia puani na kukaanza kulambatia na kukaza matevinywani mwao. (Uk 6)c) Jitu lilikuwa limevaa suti nyeusi na shati jeupe. Limekabwashingoni na tai ya buluu iliyozama kwenye misuli ya shingofupi nene (Uk 7)d) Naam. Vyakula vilipakuliwa. Wali na nazi. Mchuzi na nyama.Nyama ya kuchoma kwa mkaa na bakuli la kachumbari.Samaki wa kukaanga. Chapatti kadhaa za duara (Uk 8)1. Maswali ya BalaghaBalagha ni mbinu ambapo mwandishi huuliza maswali yasiyohitajimajibu. Maswali haya hulenga kumfanya mhusika au msomaji ku kirikwa kina. Kwa mfano:a) Aaa, kuna jabu gani lakini mvua ikinyesha? Si kila sikuhuanguka kupunguza joto ? Si huanguka kuburudisha nafsizinazohaha na kukata tamaa? (Uk 1)b) Nani angewashauri wao mburumatari? Sauti zao hazikustahikusikika, seuze kusikizwa? (Uk 3)8.

c) Kwani si kila mtu anafaa kujua kuwa kimya kirefu kinamshindo mkuu? (Uk 3)d) Tuondoke twende wapi? (Uk 5)e) Kuwe na mazungumzo gani hasa yatakayomchangamshakila mtu wakati huu kuliko uvumi ulioanza tena kuvuma? (Uk 5)f) Aaa, nani anayejua hatimaye? Kesho yenyewe haijazaliwaseuze fumbato ndani ya kesho yenyewe?g) Chupa mbili za Coca cola zifae nini kwa jitu kuza kama hilo?(Uk 8)h) Wakawa wanatazamana kwa wakionyesha hawaamini ninikinachotokea. Itawezekanaje?1.Kuchanganya NdimiHii ni mbinu ya uandishi ambapo wahusika huzungumza kwakutumia lugha zaidi ya moja ili kuonyesha hali yao na hisia zaokatika mazungumzo. Mbinu hii humwezesha mhusika kujielezavyema Zaidi kwa kutumia msamiati ambao hauko katika lughafulani. Kwa mfano:a) Chupa mbili za Coca cola zifae nini kwa jitu kuza kama hilo?(Uk 8)b) Jitu hilo lilikuwa limeketi nyuma ya gari kubwa aina ya AudiQ7 (Uk 10)c) Simama kidogo Chauffer (Uk 11)9.

2. TaharukiTaharuki ni mbinu inayotumiwa na waandishi ili kuteka hisia nahamu ya wasomaji kutaka kuendelea kusoma zaidi. Katikakufanikiwa kujenga taharuki, mwandishi husuka matukioyalito na mshikamano na mtiririko ambao humvutia msomajiasiiweke chini kazi hiyo pindi aanzapo kuisoma hadi a kiekikomo chake.a) Ulianza uvumi. Uvumi ukageuka nong'ono. Nong'onozikafumbua kinywa kueneza wasiwasi. Wasiwasi ukawahofu (Uk 1). Msomaji anajiuliza, Ni jambo gani hili ambalolinatarajiwa kutendeka?b) Kwa Mzee Mago, iliyobaki sasa ni kutazamia siku yakulipuka mambo (Uk 3)Ni mambo yepi yatalipuka? Hii inasalia kama taharuki.c) Kesho nita ka hapa tena. Niwekee chakula mara mbilikuliko hiki cha leo (Uk 9)Tunashangaa ikiwa jitu hilo kweli litarudi.1.Jazanda/ Istiari.Jazanda ni mbinu ambayo inaonyesha fumbo lililotumiwa namwandishi kurejelea hali fulani kwa njia che. Istiari kwa upandemwingine inalinganisha moja kwa moja kitu au hali na nyinginelakini bila ya kutumia maneno ya ulinganisho. Mifano:a) Angepoaje na ule moto unaomlipukia kila mtu pale mtaaniumeacha mpaka sasa kovu bichi moyoni ? (Uk 2)10.

b) Wakubwa hawatambui kuwa kwamba jambo hilo lakuwafanya wao takataka tu ndilo linalowakasirisha (Uk 3)c) Sahau imebaki vilevile kutanda giza na kufunga milango yawasiwasi vichwani mwa watu (Uk 5)d) Bweu likapasuka na kutoa uvundo wa mnyama aliyeoza (Uk 9)Hii ni ishara ya jinsi jitu hili litawahangaisha wanakijiji hawabaadaye.2. Tashbihi/MshabahaTashbiha/Tashbihi/Mshabaha ni maneno yanayofananisha kitu,jambo au kitendo na kingine kwa kutumia vihusishi kama vile 'kama','mithili', 'ja', 'mfano wa' na kadhalika. kwa mfano:a) maana siku hizi, wanasheria waaminifu ni adimu kamamaziwa ya kuku! (Uk 2)b) Ulikuwa ukitukuta ndani kwa ndani kama moto ya makumbi.(Uk 3)c) Umebaki tu ukining'inia hewani kama mvua inayotarajiwakunyesha (Uk 4)d) Kauli ya jitu hilo ilimwinua Mzee Mago kama mtualiyechapwa na bakora. (Uk 7)e) Lilipokula, lililamba sahani zote kana kwamba lilikuwa najukumu la kuziosha.(Uk 9)f) vibanda vya Madongoporomoka viliota tena hapo kamauyoga. (Uk 11)11.

1.Tashihisi/Uhuishaji Hii ni mbinu ya lugha ya kuweka hisia na uhai katika vituvisivyokuwa na uhai. Pia kuna uwezekano wa kuwapa wanyamauwezo na hulka za binadamu. Mifano:a) Nong'ono zikafumbua kinywa kueneza wasiwasi. (Uk 1)b) Maisha ndugu yangu ndiyo- maisha ndiyo yanayotukabakoo akina sisi! (Uk 1)c) Yeye hupiga mbio huku na kule kujaribu kuzuia hakiisiangamizwe (Uk 2)d) Mzee Mago lakini hairuhusu sahau iketi na kutawalakichwani mwake. (Uk 2)e) Aliwakumbusha kuwa maendeleo yanadai mchango wa kilamtu (Uk 2)f) Kesho yenyewe haijazaliwa, seuze fumbato (Uk 5)g) Sahau imebaki vilevile kutanda giza na kufunga milango yawasiwasi vichwani mwa watu (Uk 5)h) Kauli ya jitu hilo ilimwinua Mzee Mago kama mtualiyechapwa na bakora. (Uk 7)i) Haikuchukua muda mrefu akili zilipowaamsha kuwapelekamaana ya kile (Uk 10)2. ChukuNi mbinu ya kutilia mazungumzo chumvi ili kuyafanya yavutieZaidi. Kwa mfano:a) K w a m i u j i z a , n d i p o j i t u l a m i r a b a m i n elilipoingia halikujulikana lilipotoka. Liliingia tu gha a.(Uk6)b) Lile tumbo lake limezidi kufura na ndani ya tumbo, ugomvi wavyakula ukawa unapwaga kwa mingurumo ya radi iliyosikikahadi nje. (Uk 9)12.

c) Mstari huo ulikuwa umefuatana na mpasuko mkali wa radi naumweso uliomulika mpaka ndani ya mioyo ya watu. (Uk 10)d) Jitu hilo lilimwaga tabasamu mfululizo iliyoenea eneo lote laMadongoporomoka. (Uk 10)1. NidaaNi mbinu ya kuonyesha hisia aliyo nayo mhusika. Hujulikana kwakutumia alama ya hisi. Kwa mfano:a) Maisha ndugu yangu ndiyo- maisha ndiyo yanayotukaba kooakina sisi! (Uk 1)b) maana siku hizi, wanasheria waaminifu ni adimu kamamaziwa ya kuku! (Uk 2)c) Pale lilipoketi, lilionekana kupapa jasho ovyo! (Uk 7)d) Halikubakisha hata chembe moja ya chakula chochotealichopewa! (Uk 9)e) Hazitatuhamisha kabisa hizi fujo zenu! (Uk 11)2. Tanakuzi.Ni mbinu ya kutaja vitu viwili ambavyo sifa zao zimepingana.Kwa mfano:a) “Hata hivyo, kila mtu, mdogo kwa mkubwa, kike kwa kiume (Uk 2)b) Aliwakumbusha kuwa maendeleo yanadai mchango wa kilamtu, maskini au tajiri. (Uk 2)c) Lile jitu lilimkata maneno Mzee Mago, Wakubali,wasikubali (Uk 8)d) Watu wanakimbia huku na huku, huku na kule, mbele nanyuma (Uk 10)e) Kike kwa kiume, vijana kwa wazee, watoto kwa watuwazima (uk 10)13.

WAHUSIKA NA UHUSIKAa) MZEE MAGOHuyu ndiye mhusika mkuu ambaye ametumiwa na mwandishi kamakielelezo cha watetezi wa haki. Ametumika kuwatetea wanyongekutokana na madhila ya matajiri wanaotaka kuwapokonyamashamba yao. Sifa zake ni kama zifuatazo:i) Ni mtetezi wa haki.Anakataa kutazama huku wanakijiji wakihiniwa mashamba yao.Anamtafuta wakili ambaye hajahongwa ili kutetea haki yawanyonge. Isitoshe, anakataa kuwaruhusuwanamadongoporomoka kusahau uvumi uliokuwepo hapo awalikuhusu uwezekano wa vipande vyao vya ardhi kuchukuliwa.ii) Ni mwenye hekima/busara.Anafahamu vyema matokeo ya wingu linalotarajiwa kutua. Hivyoanajiandaa na pia kuwaandaa wanakijiji ili yatapowasili madhila,wawe tayari wameungana kupigania haki zao.iii) Ni mwenye bidii.Ni yeye tu aliye na mkahawa pale madongoporomoka, ishara yakwamba

TUMBO LISILOSHIBA Historia ya Mwandishi. Hadithi hii imeandikwa na Prof. Said Mohammed, mwandishi mtajika ambaye amewahi pia kuandika vitabu vingine vitajika kama vile Riwaya ya Utengano. Mwandishi huyu bila shaka ni gwiji katika ulingo huu kwani amewahi kuandika kazi zingine za fasihiFile Size: 1MB

Related Documents:

1.1 Tumbo Lisiloshiba Said A. Mohamed 5 1.2 Mapenzi ya Kifaurongo Kenna Wasike -.15 1.3 Shogake Dadangu ana Ndevu Alifa Chokocho 26 1.4 Shibe Inatumaliza Salma Omar Hamad 34 1.5 Mame Bakari Mohammed K. Ghassany 41 1.6 Masharti ya Kisasa 1.7 Ndoto ya Mashaka 1.8 Kidege 1.9 Nizik

zozote nne katika diwani ya Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine (alama 20) 6. Eleza nafasi ya vijana katika jamii ukerejelea hadithi fupi zifuatazo. a) Mapenzi ya kifa urongo (alama 5) b

Sehemu ya 3: Hutoa mwongozo au maelekezo ya ufundishaji kwa kila dha-na iliyotolewa ndani ya kitabu . Ingawa mwongozo huu wa mwalimu una majibu kwa kila kazi zote zilizotolewa katika kitabu cha mwanafunzi, unaombwa kupitia kila swali na kazi kabla ya ku-tathmini matokeo ya utafiti.

Namba ya Mkataba: AID-621-C-15-00003 Mwongozo Wa Mkufunzi Wa Mfumo Wa Ujifunzaji Wa Kieletroniki (MUKI) Agosti, 2019. KANUSHO Chuo cha Serikali za Mitaa (Hombolo) ndicho kitawajibika na matokeo ya kazi hii. Mwongozo Wa Mkufunzi Wa Mfumo Wa Ujifunzaji Wa Kieletroniki (MUKI) ni maoni ya

SEHEMU C: TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI ZINGINE SHIBE INATUMALIZA 5. “Ndugu yangu kula kunatumaliza” “Kunatumaliza au tunakumaliza” a) Eleza muktadha wa dondoo hili (al. 4) b) Fafanua maana kitamathali katika kauli „Kula tunakumaliza‟ (al. 10) c) Kwa mujibu wa hadith

A. Chokocho na D. Kayanda: Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine 4. “Madhila ya mtoto mvulana katika karne ya ishirini na moja ni mengi.” Tetea kauli hii kwa hoja ishirini ukirejelea hadithi ya Mapenzi ya Kifaurongo, Masharti ya Kisasa na Ndot

Nunua diwani ya TUMBO LISILOSHIBA na Hadithi nyingine kisha usome hadithi zifuatazo na kuandikia muhtasari wa hadithi hizo:Mame Bakari,Mapenzi Kifaurongo,Mtihani wa Maisha,Ndoto ya Mashaka na Mkubwa.Maswali kwenye mtihani wa kiingilio yatatoka

ANNUAL REVIVAL, ANNIVERSARY, AND INSTALLATION SERVICE REVIVAL SERVICE Wednesday, November 28, 2012 – Friday, November 30, 2012 7:00 P.M. - NIGHTLY THEME: “Changing the Method, Not the Message” 1 Corinthians 9: 20-23 ANNIVERSARY AND INSTALLATION SERVICE Sunday, December 2, 2012 4:00 P.M. THEME: “Changing the Method, Not the Message” 1 Corinthians 9: 20-23 Fort Foote Baptist Church .