KUCHUNGUZA MATUMIZI YA TAFSIDA KATIKA LAHAJA YA

2y ago
287 Views
4 Downloads
1.25 MB
73 Pages
Last View : 3d ago
Last Download : 3m ago
Upload by : Rafael Ruffin
Transcription

KUCHUNGUZA MATUMIZI YA TAFSIDA KATIKA LAHAJA YAKIPEMBA: UCHUNGUZI WA MAZUNGUMZOMAUA AME YUSSUFTASNIFU ILIYOWASILISHWA KWA AJILI YA KUTIMIZA MASHARTIYAKUPATIWA SHAHADA YA UZAMILI (M.A KISWAHILI - ISIMU) YACHUO KIKUU HURIACHA TANZANIA2017

iiUTHIBITISHOAliyetia saini hapo chini anathibitisha kuwa amesoma tasnifu hii itwayo:Kuchunguza Matumizi ya Tafsida Katika Lahaja ya Kipemba: Uchunguzi waMazungumzo”, na ameridhika kwamba imefikia kiwango kinachotakiwa na inafaakuhudhurishwa kwa utahini wa shahada ya uzamili (M.A.Kiswahili - Isimu) ya ChuoKikuu Huria cha Tanzania. . .Dkt. Anna Kishe(Msimamizi) . .Tarehe

iiiHAKIMILIKIHairuhusiwi kuiga au kunakili kwa namna yoyote ile ya Tasnifu hii kama kutoasehemu ndogo ya tasnifu hii, kielektroniki au njia nyegine yoyote ile bila ya idhini yaMuandishi wa Tasnifu hii au kwa niaba ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

ivTAMKOMimi, Maua Ame Yussuf, natamka na nathibitisha kuwa hii ni kazi yangu halisi nahaijawahi kuwasilishwa katika chuo kikuu kingine chochote kwa ajili ya kutunukiwashahada hii au nyingine ile. .Sahihi .Tarehe

vTABARUKUNatabaruku kazi hii kwa mtoto wanguFatma Hamad Abdallaili iwe kwake ni chachuya kujali elimu na kujifunza kwa bidii.

viSHUKURANIAwali ya yote sina budi kumshukuru Mwenyezi Mungu muumba wa ulimwengu navilivyomo na kunipa uwezo wakufanya utafiti huu, kuandika na kukamilisha. Pilinapenda kuwashukuru wote waliochangia kwa namna moja ama nyengine kukamilikakwa kazi hii. Hata hivyo si rahisi kuwataja wote kwa majina, ila napendakuwashukuru wote nitakaowataja na ambao hawakutajwa kwa mchango wao wakuifanikisha kazi hii.Shukurani za pekee ziende kwa msimamizi wangu Dkt Anna Kishe kwanza kwa kuwakaribu nami, lakini pia kukubali kuwa msimamizi wa kazi yangu na mwishokuniongoza kwa kila palipostahili kuongozwa juu ya kazi yangu hii hadi kukamilikakwake. Mungu amzidishie upendo na nguvu za kusaidia wengine wote wanaotakamsaada kutoka kwake.Shukurani nyingine ziende kwa Mlezi wa Chuo Kikuu Huria Tawi la Pemba, MwalimBakari Kombo kwa kuwalea wanafunzi na kuwasaidia kwa hali na mali ilikukamilisha lengo lao la kujipatia elimu. Mungu amlipe wema huo.Pia naishukuru familia yangu kwa kuwa pamoja na mimi bega kwa bega tangumwanzo wa kuanza masomo hadi kukamilika kwake na kunisaidia kwa hali na mali,familia hiyo akiwemo kwanza Mume wangu Hamad Abdalla Ali ambae ni muhimilimkuu wa kunisiadia kwaKustahamili katika kipindi chote kigumu lakini pia kunipa mawazo yanayofaa juu yamchakato wa kujisomea. Wengine ni kaka zangu Juma Ame Yussuf, Moh’d

viiAmeYussuf na Omar AmeYussuf kwa kunipa moyo na ari ya kujiendeleza kimasomo,pia bila ya kumsahau Dada Khadija Kombo kwa kuweza kunipa mawazo nakunikwamua pale nilipokwama ili kuendelea mbele juu ya wote hao siwezi kumsahauMama mzazi Siti Moh’d Shaame kwa kuwangoza wanawe wote juu ya kutodharausuala la elimu na pia kuwapa malezi bora ambayo yalitusaidia katika maisha yetuhadi leo nathubutu pia kusema Allah awalipe wema wao huo wote.Aidha ninaushukuru uongozi mzima wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania pamoja nawanataaluma wenzangu wa kitivo cha Sanaa na Sayansi ya jamii kwa kunishawishi nakunihimiza kuikamlisha kazi yangu hii.Nasema kwa pamoja Ahsanteni sana.Allah ndie muweza wa kila kitu.

viiiIKISIRIUtafiti huu ulihusu Kuchunguza Matumizi ya Tafsida Katika Lahaja ya Kipemba.Mtafiti alichagua mada hii ili kuchunguza na kuchambua utajiri mkubwa wa tafsida zalahaja ya kipemba zinavyotumika kwa Wapemba wenyewe. Utafiti huu una lengo kuumoja na malengo mahsusi matatu. Aidha mtafiti alitumia nadharia moja tu nayo ninadharia ya Simiotiki.Pamoja mtafiti alitumia njia nne za kukusanyia data nazo niusaili, Uchunguzi makini, Hojaji na mbinu ya maktabani. Data za utafiti huuzilichambuliwa kwa njia ya maelezo, Uchambuzi wa dada ulifanyika kulingana namadhumuni mahususi yaliyotajwa ndani ya utafiti huu. Utafiti umegundua kuwa zipotafsida za lahaja ya kipembaambazo hutumiwakwa lengo la kuleta heshima katikamazungumzo ya wapemba, lakini pia kulinda na kuendeleza utamaduni wa Wapembakwa kuzitumia vyema tafsida hizo. Mtafiti amegundua matumizi tofauti ya tafsidaambazo zinatumika na kuleta heshima katika mazungumzo, tafsida hizo ni kama vilekubaua, kujisaidi, utupu/ushi, msalani, kujamiiana (Kuingiliana), mja mzito namengineyo. Mwisho matafiti amehitimisha kazi yake kwa kutoa mapendekezo kwawasomi, walimu na wanajamii kwa ujumla kwa kuzilinda na kuziendeleza tafsida, piakuandaa tafiti nyingine zinazohusu tafsida kupitia lahaja na lughanyingine zamakabila.

ixYALIYOMOUTHIBITISHO . iiHAKIMILIKI . iiiTAMKO . ivTABARUKU . vSHUKURANI . viIKISIRI . viiiORODHA YA VIAMBATANISHI . xiiiSURA YA KWANZA . 1UTANGULIZI WA JUMLA . 11.1Utangulizi . 11.2Usuli wa Mada . 11.3Tatizo la Utafiti . 41.4Malengo ya Utafiti . 51.4.1 Lengo Kuu . 51.4.2 Malengo Mahasusi . 51.5Maswali ya Utafiti . 61.6Umuhimu wa Utafiti Huu. 61.7Mipaka ya Utafiti . 71.8Hitimisho . 7SEHEMU YA PILI . 8MAPITIO YA KAZI TANGULIZI NA MKABALA WA KINADHARIA . 82.1Utangulizi . 82.2Mapitio ya Kazi Tangulizi . 8

x2.2.1 Dhana ya Tamathali za Semi . 82.2.2 Dhana yaTafsida . 102.2.3 Dhana ya Lahaja . 122.4.4 Kazi Tangulizi Kuhusu Tafsida . 122.2.5 Kazi Tangulizi Kuhusu Tamathali za Semi . 142.2.6Kazi Tangulizi Kuhusu Lahaja za Kiswahili . 162.3Pengo la Utafiti . 172.4Mkabala wa Nadharia . 172.4.2 Nadharia ya Simiotiki . 172.5Hitimisho . 18SURA YA TATU . 19MBINU ZA UTAFITI. 193.1Utangulizi . 193.2Eneo la Utafiti . 193.3Mbinu za Kukusanyia Data . 193.3.1 Usaili . 203.3.2 Uchunguzi Makini . 203.3.3Mbinu ya Hojaji . 213.3.4 Mbinu ya Maktabani . 213.4Mbinu ya Uchambuzi wa Data . 223.5Usampulishaji . 223.6Sampuli . 223.7Hitimisho . 23

xiSURA YA NNE . 24UWASILISHAJI NA UCHAMBUZI WA DATA . 244.1Utangulizi wa sura ya nne . 244.2Kubainisha Tafsida Zinazotumika Katika Lahaja ya Kipemba . 244.2.1Tafsida zinazotumika Msibani . 254.2.2 Tafsida zinazotumika Harusin. 264.2.3 Tafsida zinazotumika Nyumbani . 274.2.4Tafsida Zinazozungumzwa Kazini. 294.3Kupambanuwa matumizi ya Tafsida zinazotumika katikaLahaja ya Kipemba . 294.3.1 Matumizi ya Tafsida katika Mazingira ya Harusini . 304.3.2 Matumizi ya aTuria katika Mazingira ya Nyumbani . 334.3.3 Matumizi ya Tafsida katika Mazingira ya Msibani . 374.3.4 Matumizi ya Tafsida katika Mazingira ya Kazi . 384.4Kuelezea Faida na Hasara ya Matumizi ya Tafsida katika Jamii HususaniJamii ya Wapemba . 384.4.1 Faida ya Matumizi ya Tafsida katika Jamii . 394.4.2 Hasara ya Matumzi ya Tafsida katika Jamii . 404.5Hitimisho . 41SURA YA TANO . 42MUHTASARI WA UTAFITI, HITIMISHO NA MAPENDEKEZO . 425.1Utangulizi . 425.2Muhtasari wa Utafiti . 425.2.1 Muhtasari wa matokeo ya utafiti . 43

xii5.2.1.1 Lengo la Kwanza. 435.2.1.2 Lengo la Pili . 435.2.1.3 Lengo la Tatu . 445.3Mapendekezo . 445.3.1 Mapendekezo ya Jumla . 445.3.2Mapendekezo ya Tafiti Zijazo . 455.4Hitimisho . 46MAREJELEO . 48VIAMBATANISHI . 51

xiiiORODHA YA VIAMBATANISHIKiambatanishi Na. I:Mwongozo wa Maswali ya Hojaji . 51Kiambatanishi Na. II:Usaili Kwa Watafitiwa Ambao Hawajui Kusoma naKuandika . 54Kiambatanishi Na. III: Kinaonyesha Orodha ya Tafsida na Maana Zake . 55Kiambatanishi Na. IV: Kinaonyesha Kisiwa cha Pemba Katika Eneo la Mkoawa Kusini Pemba . 57Kiambatanishi Na. V:Kinaonyesha Eneo la Chake Chake Mjini KisiwaniPemba. 58Kiambatanishi Na. VI: Kinaonyesha Kisiwa cha Pemba Ambapo Lahaja yaKipemba Inazungumzwa . 59Kiambatanishi Na. VII: Kinaonyesha Shughuli Mbalimbali za Wananchi katikaEneo la Mjini Chakechake Pemba Ambapo Eneo HiliNdilo Mtafiti alifanya Utafiti wake KuwakilishaPemba Nzima . 60

1SURA YA KWANZAUTANGULIZI WA JUMLA1.1UtanguliziUtafiti huu umehusu “kuchugnuza matumizi ya tafsida katika lahaja ya Kipemba”,ambapo umelenga kuchunguza mambo makuu matatu. Kwanza, kubaini kuwepo kwatafsida mbali mbali zinazotumika katika lahaja ya kipemba. Pili, kuelezea matumiziyake katika jamii ya Wapemba. Tatu, kueleza faida na hasara zake katika jamii yaWapemba. Surahii pia inatoa taarifa za awali kuhusu mada ya utafiti ambapo mtafitiataelezea kuhusu usuli wa mada,tatizo la utafiti,malengo ya utafiti yakiambatana namswali ya utafiti ,umuhuimu wa utafiti mipaka ya utafiti hatimae hitimisho , haya yoteyameelezewa juu ya kuchunguza matumizi ya tafsida katika lahaja ya Kipemba.1.2Usuli wa MadaWapemba kupitia maisha yao hutumia tafsida kama nyenzo ya kunusuru mazungumzoyao.Katika lugha ya Kiswahili hasa ya kifasihi maneno ya stasha huitwatafsida.Wataalamu wengi wameelezea kuhusu tamathali za semi ambapo ndani yakeinapatikanatafsida. Hivyo Wapemba kupitia lahaja yao ya Kipemba hawakuwa nyumakatika kutumia tafsida ili kunusuru mazungumzo yao.Wataalamu kama vile Jilala(2016), Wamitila (2003), Senkoro (1982), Masebo (2004) na wengine wamefasilidhana ya tafsida kama ifuatavyo:Senkoro (1982) amesema kuwa“Tafsida hujitokeza kwa utumizi wa maneno, msemona nahau ambayo hupunguza ukali au matusi badala ya kutumia neno,msemo aunahau kali ama ya kimatusi”, pia ameeleza dhana hii kwa kutilia mkazo wa kuonesha

2mifano kama vile, “Kujisaidia au kwenda haja badala ya kunya au kukojoa.Gibbe(1980) ameeleza kuwa ni tamathali ambayo husema mambo kwa lugha lainiinayoambaa kuchoma na kutonesha hisia za watu. Mfano siku hiyo ya safari, kujiwana wito huo, mtu hana hiari wala uwezo.”Allan na Burridge (1991) wamesema kwamba nenotafsida limetokana na tafsiri ya“euphemism” hutokana na uambatanishi wa viambajengo vya kigiriki “eu”kumaanisha “nzuri” na “pheme” kumaanisha kuzungumza. Kwa hivyo neno tafsidakwa tafsiri ya “eupheme” kumaanisha kuzungumza kwa maneno mazuri aukuzungumza kwa usemi usioudhi na kudhuru mtu.Gatambuki (2009) akirejelea mawazo ya Bright (1985) na Allah na Burridge (1991)anaeleza kuwa”tafsida ni kutumia maneno mazuri, matamu, yanayopendeza,yaliyotiwa nakshi yakavutia”, Pia anasema ni kutokusema maneno moja kwa moja ilikuepuka kudhuru uso wa msikilizaji.Harry (1954) anasema kwamba “lugha huashiria mfumo jamii husika, na kwa hivyokuna uhusiano wa lugha na jamii ambapo lugha hiyo hutumika. Katika jamii kunanamna lugha inavyotumiwa na kuleta aibu ama hata kuwa ni vigumu kuyatumiamaneno fulani katika lugha kuwa ni mwiko. Kwa sababu hii watumizi lugha huwezakukwepa hali hiyo kwa kutumialugha inayoonekana nzuri au yenye adabu nayohuitwa tafsida. Hivyo basi kwa kuzingatia tafsiri ya Harry (keshatajwa),tunawezakusema kuwatafsida ni maneno yenye adabu.”TUKI (1990), wamesema kuwa”Tafsida au ufasidi ni matumizi ya maneno ya stahabadala ya yale halisi.Kwa mfano aga dunia ni neno la staha na lenye upolelinalotumika badala ya kufa“

3Kutokana na maelezo hayo tunaweza kusematafsida ni maneno yanayoundwa na kilajamii ili kurahisisha mawasiliano, kuyafanikisha na pia kuficha uso wawanaowasiliana. Kwa ujumla tafsida ni maneno ya heshima ambayo hutumika ilikupunguza ukali wa jambo linalosemwa ambalo aghalabu huwa aibu kutamka mbeleza watu au ni karaha .Mfano kusema sehemu za siri (uchi). Kubaua, (kukojoa), yukouani/msalani (Yuko chooni), Amechafua hewa (amejamba), n.k.tafsida hizi nanyingine hutumika ili kunusuru mazungumzo.TUKI (2004), imeeleza lahaja ni tofauti kati ya matamshi, maumbo na matumizi yamaneno katika maeneo mbali mbali kwa lugha yenye asili moja.Lahaja ya kipemba nilahaja ya Kiswahili iliyozungumzwa kisiwa cha Pemba isipokuwa eneo la Kusini laKisiwa hicho ambako yasemekana kunazungumzwa lahaja ya kitumbatu Bakari(2015). Kipemba ni lahaja ya Kiswahili iliyowekwa na Winaisimu katika kundi lakwanza la lahaja za kusini, ambazo eneo lake ni Kenya kusini ukanda wa Mrima,kisiwa cha Pemba na Unguja, lahaja zinazohusika na kundi hili ni kimtang’ata(Kimrima), Kingome (Kimafia/Kingao), kimwani, Kitumbatu, kimakunduchi (Kikae)na kipemba. Lahaja ya kipemba huzungumzwa katika maeno mbali mbali ya kisiwacha Pemba ambapo kisiwa hicho kimejigawa katika miji mikuu minne ambayoniMkoani, Chake chake, Wete na Micheweni. Mkoani na Chake Chake ipo kusini,Micheni na Wete ipo kaskazini mwa kisiwa hicho, pia Pemba imezungukwa na visiwavidogo vidogo kama vile Kojani, Fundo, Kisiwa Panza, Makoongwe nk. Maeneo hayayote yanazungumza lahaja ya kipemba, BAIKZA (2012).Utafiri huuumechunguzamatumizi ya tafsida katika lahaja ya Kipemba, ambapo kilajamii ina mfumo wake wa maisha ambao husababisha lugha kutofautiana. Utofauti

4ambao husababishwa na mambo mengi yakiwemo utamaduni, lugha, mazingira nahata shughuli zakimaisha kama vile biashara, kilimo, uvuvi n.k.Kwa kuwa tafsida nimoja kati ya vipengele vya tamathali za semi hivyo basi ipo hajaya kujua ni nini tamathali za semi “Tamathali za semi ni vifananishi au viwakilishivya dhana moja kwa dhana nyingine zinazofanana Jilala (2016). Mtafiti baada yakupitia mandiko tofauti aliona maelezo yanayozungumzia tafsida katika muktadhamwingine kama vile maana na mifano ya tafsida, ila hakupata kuona maelezoyaliyoelezea tafsida za lahaja ya kipemba.Hivyo basi utafiti huu umeshughulikia zaidina kuchunguza matumizi ya tafsida katika lahaja ya Kipemba.1.3Tatizo la UtafitiHakuna shaka ipo tofauti ya mazungumzo katik

Wapemba. Surahii pia inatoa taarifa za awali kuhusu mada ya utafiti ambapo mtafiti ataelezea kuhusu usuli wa mada,tatizo la utafiti,malengo ya utafiti yakiambatana na mswali ya utafiti ,umuhuimu wa utafiti mipaka ya utafiti hatimae hitimisho , haya yote yameelezewa juu ya kuchunguza matumizi ya tafsida katika lahaja

Related Documents:

Data zilirekodiwa katika kinasa sauti na kunukuliwa kwa maandishi. . Tofauti za Matumizi ya Lugha katika Miktadha Mbalimbali ya Mazungumzo 13 sehemu ya pili inahusu tofauti ya matumizi ya lugha katika miktadha mbalimbali. Sehemu ya tatu inafafanua mkabala wa kinadharia uliotumika katika uch

Nyenzo za kufundisha huwa viungo muhimu wakati wa utoaji wa mafunzo. Utafiti ulichunguza matumizi ya nyenzo katika ufundishaji wa Kiswahili katika shule za msingi za umma katika Jimbo la Nyandarua, Kenya. Madhumuni ya utafiti yalikuwa: Kuainisha nyenzo zinazotumika kufundisha Kiswahili, Kutathimini kiwango cha matumizi ya

mawazo ya wanamsambao hususani katika ugawaji wa ngano bila kuchunguza kwa umakini sifa ya kila kundi. Propp anaamini kuwa ili kuchunguza asili ya ngano ni vema kuanza kuchunguza aina za ngano kwa kuangalia maumbo ya ngano. Hivyo mtazamo huu unaangalia asili ya ngano kwa kuchunguza maumbo ya ngano husika. Ubora wa nadhairia hii, nadharia hii inasaidia kujua aina za ngano kutokana na dhima zake .

tamko la tatizo la utafiti, lengo kuu na madhumuni mahususi ya utafiti. Aidha maswali ya utafiti, umuhimu wa utafiti, mipaka ya utafiti na mpangilio wa tasnifu pia vimewasilishwa katika sura hii. 1.1 Usuli wa Tatizo la Utafiti Binadamu katika kuishi

kundi ,fanya jukumu la maana katika masomo yote.Umahiri wa maelezo maalum na wa baina ya mitaala yameshikanishwa pamoja katika muktadha wa maelezo. . baina ya mitaala katika muda wa mwaka wa shule. Kwa kufanya hivo wanaangazia kusoma kwao . na wanachukua jukumu la mchakato wao wa kimasomo. Tathmini ya kibinafsi hufanywa katika

katika tamthiliya za Kinjeketile na Nyerere na Safari ya Kanaani: Utafiti linganishi. Ili kufanikisha utafiti huu, mtafiti ametumia mbinu za maktabani katika kukusanya na kuwasiilisha data kimaelezo. Pia marejeleo mbalimbali kutoka tamthiliya za Kiswahili yalipitiwa. Nadharia ya fasihi ya jamii ndiyo iliyotumika katika

v Ramani ya Yaliyomo Mada 1: Kuelewa Mazungumzo na Kujieleza Kimazungumzo Mada 2: Msamiati katika Mazingira ya Shule Mada 3: Msamiati katika Mazingira ya Nyumbani Mada 4: Msamiati katika Mazingira ya Utawala Mada 5: Msamiati katika Mazingira ya Sokoni Mada 6: Matumizi ya Msamiati kuhusu Usafi wa Mwili Idadi ya Vipindi

The effects of using a more efficient insulation don’t appear to be much at face value, but factor in a minimum 30-year life-cycle cost of operating