MWONGOZO WA MKUFUNZI - Counsenuth.or.tz

2y ago
191 Views
9 Downloads
6.92 MB
172 Pages
Last View : 1m ago
Last Download : 2m ago
Upload by : Farrah Jaffe
Transcription

United Republic of TanzaniaMinistry of Health and Social WelfareLISHE NA ULAJI UNAOFAA KWA WATU WENYEMAGONJWA SUGU YASIYO YA KUAMBUKIZAMAFUNZO KWA WATOA HUDUMA YA AFYAMWONGOZO WA MKUFUNZITanzania Diabetes AssociationNovemba 2012

Tanzania Diabetes AssociationUtayarisharishaji wa kitabu hiki ni kwa hisani ya Shirika la Kisukari Duniani kupitiaChama cha Kisukari TanzaniaThis Nutrition Manual was developed by COUNSENUTH forTanzania Diabetes Association

LISHE NA ULAJI UNAOFAA KWA WATU WENYEMAGONJWA SUGU YASIYO YA KUAMBUKIZAMAFUNZO KWA WATOA HUDUMA YA AFYAMWONGOZO WA MKUFUNZITanzania Diabetes AssociationNovemba 2012

YALIYOMOORODHA YA JEDWALI .iiiVIFUPISHO. ivFARAHASA. vSHUKURANI. viUTANGULIZI.viiMAELEZO KUHUSU MAFUNZO. viiiMODULI, MASOMO NA MUDA.xiiiUTAMBULISHO, MATARAJIO NA MALENGO.xivMODULI YA KWANZA: MASUALA YA MSINGI KUHUSU CHAKULA NA LISHE. 1Somo la 1.1: Virutubishi, Makundi ya Vyakula na Mlo Kamili. 2Somo la 1.2: Tathmini ya Hali ya Lishe, Tafsiri na Hatua za Kuchukua.15Somo la 1.3: Mtindo Bora wa Maisha.25MODULI YA PILI: ULAJI UNAOSHAURIWA KWA BAADHI YA MAGONJWA SUGU YASIYO YAKUAMBUKIZA. 33Somo la 2.1: Ugonjwa wa Kisukari.34Somo la 2.2: Magonjwa ya Moyo.49Somo la 2.3: Shinikizo Kubwa la Damu.53Somo la 2.4: Saratani.57Somo la 2.5: Magonjwa ya Figo.73Somo la 2.6: Magonjwa Sugu ya Njia ya Hewa.86MODULI YA TATU: UNASIHI WA CHAKULA NA LISHE KWA WATU WENYE MAGONJWASUGU YASIYO YA KUAMBUKIZA. 89Somo la 3.1: Stadi za Kusikiliza na Kujifunza.91Somo la 3.2: Stadi za Kujenga Kujiamini na Kutoa Msaada.98KIAMBATANISHO 1.108Jaribio la Awali. 108KIAMBATANISHO 2.112Jaribio la Mwisho. 112KIAMBATANISHO 3.115Majibu ya Jaribio la Awali na la Mwisho. 115KIAMBATANISHO 4.118i

Fomu ya Kuchukua Historia ya Ulaji na Mtindo wa Maisha. 118KIAMBATANISHO 5.121Tathimini ya Kila Siku. 121KIAMBATANISHO 6.122Tathmini ya Mwisho wa Mafunzo. 122KIAMBATANISHO 7.124Fomu ya Mpango-Kazi. 124KIAMBATANISHO 8.125Kazi ya Kikundi. 125KIAMBATANISHO 9.142Fomu ya Kujiandikisha. 142KIAMBATANISHO 10.143Fomu ya Mahudhurio ya Kila Siku. 143KIAMBATANISHO 11.144Vifaa Vinavyohitajika kwa Ajili ya Mafunzo. 144KIAMBATANISHO 12.145Ratiba Ya Mafunzo. 145KIAMBATANISHO 13.147Stadi za Unasihi. 147BIBILIOGRAFIA.148ii

ORODHA YA MAJEDWALIJedwali 1: Baadhi ya virutubishi; umuhimu, vyanzo vyake na dalili za upungufu. 6Jedwali 2: Hatua za kuchukua kufuatana na tafsiri ya vipimo.24Jedwali 3: Glycaemic index ya baadhi ya vyakula.41Jedwali 4: Baadhi ya vyakula vinavyoweza kupunguza au kuongeza uwezekano wakupata saratani mbalimbali.68Jedwali 5: Kiwango cha virutubishi vinavyohitajika na mgonjwa wa acute renal failure.79Jedwali 6: Kiasi cha protini kinachoshauriwa kutegemea hali ya figo.80Jedwali 7: Jedwali linaloonyesha baadhi ya vyakula na baadhi ya virutubishi.82Jedwali 8: Kiasi cha Calcium, Phosphorus, Potassium na Sodium katika baadhi ya vyakulakwa kila gram 100 inayoliwa. 84iii

VIFUPISHOAIDSAcquired Immuno Deficiency SyndromeBMIBody Mass TVVUWCRFWDFWHOAnti RetroviralThe Centre for Counselling, Nutrition and Health CareCare and Treatment ClinicHuman Immunodeficiency VirusMinistry of Health and Social WelfareMid-Upper Arm CircumferenceReproductive and Child HealthTanzania Diabetes AssociationTanzania Food and Nutrition CentreUnited States Agency for International DevelopmentVoluntary Counselling and TestingVirusi Vya UKIMWIWorld Cancer Research FundWorld Diabetes FoundationWorld Health Organizationiv

:Nishati-lishe:Virutubishi:Lishe:Afya:Kiasi kidogo cha chakula ambacho sio mlo kamili, kinachoweza kuliwa bilamatayarisho makubwa. Mara nyingi huliwa kati ya mlo mmoja na mwingineKipimo kinachotumika kupima kiasi cha nishati lisheAina ya mafuta inayopatikana hasa kwenye vyakula vyenye asili ya wanyama napia hutengenezwa mwilini. Lehemu inayotokana na vyakula ikizidi mwilini huletamadhara hasa katika mishipa ya damu kwani huwa na tabia ya kujikusanya katikakuta za ndani za mishipa hiyo kidogo kidogo na kuifanya kuwa myembamba.Aina ya kabohaidreti ambayo mwili hauwezi kuiyeyusha. Makapi-mlo hupatikanakwa wingi kwenye matunda, mbogamboga na nafaka zisizokobolewaNguvu inayouwezesha mwili kufanya kazi mbalimbaliViini vilivyoko kwenye chakula ambavyo mwili hutumia kufanya kazi mbalimbaliMchakato unaohusisha hatua mbalimbali za jinsi mwili unavyokitumia chakulakilicholiwa. Hatua hizi ni tangu chakula kinapoliwa, jinsi mwili unavyokisaga nakukiyeyusha na hatimaye virutubishi kufyonzwa na kutumika mwiliniKwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), afya ni hali ya kuwa mzimakimwili, kiakili na kijamii, na wala sio tu hali ya kutokuwepo na ugonjwa au kuwadhaifuv

SHUKURANIChama cha Ugonjwa wa Kisukari Tanzania (Tanzania Diabetes Association/TDA) kinatoa shukuraniza dhati kwa Shirika la Kisukari Duniani (World Diabetes Foundation - WDF) kwa kufadhiliutayarishaji na uchapishaji wa Moduli hii ya Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wenye Magonjwa SuguYasiyo ya Kuambukiza.TDA inaishukuru COUNSENUTH kwa utaalamu na usimamizi katika utayarishaji wa kitabu hiki.Aidha, COUNSENUTH na TDA wanatoa shukurani za dhati hasa kwa Wizara ya Afya na Ustawiwa Jamii, Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC), International Medical and Technological University(IMTU), Hospitali ya Amana, Hospitali ya Temeke, Hospitali ya Hindu Mandal, taasisi, wataalammbalimbali na watu binafsi ambao wamechangia kwa njia mbalimbali katika kutayarisha nakukamilisha moduli hii.Tunawashukuru wataalam wafuatao ambao walishiriki katika kutayarisha moduli hii:Dr Margareth Nyambo- Hospitali ya AmanaDr Boniface Venance- Hospitali ya TemekeDr Shadrack BusweluDr Abidan MgangaDr Ali A. MzigeDr Lunna KyunguRestituta ShirimaGelagista GwarasaMary J. MsangiElizabeth LicocoBeatrice P. MhangoMary NghumbuPeter Mabwe- Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii- Hospitali ya Taifa ya Muhimbili- Hospitali ya IMTU- COUNSENUTH- COUNSENUTH- Taasisi ya Chakula na Lishe- Taasisi ya Chakula na Lishe- Hospitali ya Taifa ya Muhimbili- Chama cha Kisukari – Tanzania- Hospitali ya Hindu Mandal- Elimu ya Afya kwa Umma – Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamiivi

UTANGULIZIMagonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza yanayohusiana na mtindo wa maisha yamekuwayakiongezeka kwa kasi katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania. Awali, magonjwa hayayalikuwa yakiwaathiri watu wenye rika mbalimbali hasa wenye umri mkubwa (zaidi ya miaka45) lakini kwa sasa magonjwa haya yanazidi kuathiri watu wenye umri mdogo wakiwemo watoto.Magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza huwa yanachukua muda mrefu kujitokeza.Magonjwa sugu makuu sita yasiyo ya kuambukiza – kisukari, shinikizo kubwa la damu, magonjwaya moyo, magonjwa ya figo, saratani, magonjwa sugu ya njia ya hewa yanajitokeza kwa wingikatika nchi zenye uchumi mdogo na wa kati. Hali hii inatokana na mtindo wa maisha na ulajiambao umebadilika kwa kasi kulinganisha na hali ilivyokuwa huko nyuma. Kwa mujibu ya Shirikala Afya Duniani (WHO), mitindo ya maisha isiyo bora ndio chanzo kikubwa cha kuongezeka kwamagonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza duniani ambayo yamekuwa yakisababisha mamilioni yavifo vya mapema kila mwaka.Maendeleo ya kiuchumi ambayo ni pamoja na kuongezeka kwa kipato, ambacho huwapa watuuwezo wa kumudu gharama za nyenzo mbalimbali za kurahisisha kazi za kutumia nguvu ikiwani pamoja na magari, vifaa vya kutendea kazi, kompyuta, televisheni nk ni miongoni ya mamboyanayochangia kuongezeka kwa magonjwa haya. Matumizi ya nyenzo za kufanyia kazi au kutofanyamazoezi ya mwili huwafanya watu kulimbikiza nishati-lishe mwilini ambazo husababisha ongezekola uzito wa mwili ambao huchangia kuongeza uwezekano wa kupata magonjwa hayo.Mambo mengine yanayochangia magonjwa haya ni kuongezeka kwa watu wanaohamia mijini namabadiliko ya tabia ya ulaji. Mabadiliko ya tabia na mtindo wa ulaji yamefanya jamii kubadilishanamna ya ulaji na aina ya vyakula vinavyoliwa. Mabadiliko haya huifanya jamii kuachana nautaratibu wa kutumia vyakula vya asili, kutopika chakula kwa njia za asili, kutumia kwa wingivyakula vyenye mafuta mengi, sukari na chumvi nyingi pamoja na nafaka ambazo zimekobolewa.Matokeo ya mabadiliko haya ni ongezeko la magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza ambayo huathiriubora wa maisha.Mwongozo huu unatoa maelezokuhusu lishe na ulaji unaofaa kwa watu wenye magonjwa suguyasiyo ya kuambukiza kwa ajili ya kuwawezesha watoa huduma ya afya kutoa unasihi kwa ufanisikwa wagonjwa wanaowahudumia. Mwongozo pia umejadili kwa kina namna ya kuzuia baadhi yamagonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza ambayo yanajumuisha shinikizo kubwa la damu, kisukari,magonjwa ya moyo, saratani na magonjwa sugu ya njia ya hewa.Walengwa wa mwongozo huu ni wakufunzi wa watoa huduma ya afya hususan wanaotoa hudumakatika kliniki zinazohudumia watu walioathirika na magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza.vii

MAELEZO KUHUSU MAFUNZOLENGOLengo la mafunzo haya ni kuwajengea watoa huduma ya afya uwezo katika masuala ya chakula nalishe kwa wateja wenye magonjwa sugu yasiyoambukiza ili waweze kutoa unasihi kwa ufanisi kwawateja. Pia itawawezesha kutoa elimu ya jinsi ya kuchukua tahadhari mapema ili kuzuia magonjwahaya kwa wale ambao hawajaathirika.MATAYARISHO NA UTARATIBU WA KUENDESHA MAFUNZO Matayarisho kwa wakufunziWakufunzi wakutane siku mbili kabla ya mafunzo kuanza, ili kujadili ratiba, kutayarisha vipindina vifaa vya kufundishia, pia kukagua sehemu ya kufanyia mafunzo. Mafunzo haya ni ya siku nneyakijumuisha nadharia na vitendo. Kila kipindi kinaainisha muda utakaotumika, malengo, mamboya kujifunza na kazi ya kikundi. Njia za kufundishiaNjia mbalimbali zitatumika katika kuendesha mafunzo haya ikiwa ni pamoja na: kutoa mhadhara,majadiliano ya vikundi, igizo dhima, maswali na majibu, kuonyesha kwa vitendo, bungua bongo namazoezi ya mtu mmoja mmoja au katika vikundi. Mafunzo haya yanahusisha watu wazima hivyoyatazingatia kupeana uzoefu na kuheshimu mawazo ya kila mmoja. Mahali pa kufanyia mafunzoMuda wote wa mafunzo, washiriki wanatakiwa waishi sehemu moja ili waweze kufanya mazoezi,kusaidiana na kujadiliana kwa pamoja baada ya saa za masomo. Ni vyema pia mafunzo yakafanyikamahali ambapo pana nafasi kuwawezesha kufanya kazi katika vikundi. Inashauriwa uwiano wawakufunzi na washiriki uwe ni mkufunzi mmoja kwa kila washiriki sita. Darasa lisiwe na washirikizaidi ya 25. VifaaLebo za majinaChati pinduNotebookKalamuKalamu zenye wino mzitoVifaa vya mazoezi kwa vitendoIdadi ya vifaa vinavyohitajika vimeoredheshwa katika somo husikaviii

Sifa za mkufunziMkufunzi anatakiwa awe na sifa zifuatazo: Angalau awe na shahada ya kwanza ya Lishe au amepitia mafunzo ya kuwa mwezeshajikatika masuala ya lishe Awe na stadi za unasihi na mawasiliano Awe na uzoefu wa kufundisha watu wazima Awe amepitia mafunzo ya uwezeshaji Awe na ufahamu kuhusu miongozo ya kitaifa inayohusiana na masuala ya lisheNi muhimu mmoja wa wakufunzi awe amesomea masuala ya afya katika ngazi ya utabibuau zaidi. Sifa za washirikiMshiriki ni lazima awe: Amemaliza elimu ya sekondari Mtoa huduma ya afya Awe ana ari ya kujifunzaKUENDEDSHA MAFUNZOMafunzo haya yataendeshwa kwa siku 4; kila siku muda wa saa 8. Kila siku asubuhi kutakuwana muhtasari wa masomo yaliyofundishwa siku iliyotangulia. Mkufunzi ataeleza malengo ya kilakipindi na njia zitakazotumika kufundishia. Mkufunzi anaweza kufanya mabadiliko kulinganana uzoefu wake au aina na uzoefu wa washiriki wa mafunzo. Kila kipindi kina maelezo kuhusumatayarisho ya kufanya kabla ya kipindi.Kitabu cha mshiriki kina muhtasari wa vipindi vyote na kitamuwezesha mshiriki kufanya rejeawakati wa mafunzo na baada ya kumaliza. Mafunzo haya yametayarishwa kuwa shirikishi ilikuwawezesha washiriki kutoa mawazo yao. Kila mkufunzi ni lazima awe na nakala ya mwongozona kitabu cha mshiriki.KAZI YA KIKUNDIKutakuwa na kazi ya kikundi kila baada ya kipindi ili kuwawezesha washiriki kujadili kwa kina.Inapobidi washiriki wapewe kazi za kufanya baada ya masomo. Ni vyema washiriki wajiandaekutayarisha mpango wao wa kazi ili kuboresha huduma baada ya mafunzo. Mpango huu piautatumika wakati wa kufuatilia utekelezaji. Inabidi mwezeshaji atoe mwongozo ili kuwezeshakutayarisha mpango unaotekelezeka (rejea kwenye kiambatanisho namba 7)VITABU VYA REJEAMkufunzi anatakiwa asome vitabu kadhaa vya rejea ili aweze kuwa na uelewa mpana katika madaanayofundisha. Katika kila kipindi orodha ya vitabu vya rejea imeainishwa. Mshi

Amemaliza elimu ya sekondari Mtoa huduma ya afya Awe ana ari ya kujifunza KUENDEDSHA MAFUNZO Mafunzo haya yataendeshwa kwa siku 4; kila siku muda wa saa 8. Kila siku asubuhi kutakuwa na muhtasari wa masomo yaliyofundishwa siku iliyotangulia. Mkufunzi ataeleza malengo ya

Related Documents:

Namba ya Mkataba: AID-621-C-15-00003 Mwongozo Wa Mkufunzi Wa Mfumo Wa Ujifunzaji Wa Kieletroniki (MUKI) Agosti, 2019. KANUSHO Chuo cha Serikali za Mitaa (Hombolo) ndicho kitawajibika na matokeo ya kazi hii. Mwongozo Wa Mkufunzi Wa Mfumo Wa Ujifunzaji Wa Kieletroniki (MUKI) ni maoni ya

Sehemu ya 3: Hutoa mwongozo au maelekezo ya ufundishaji kwa kila dha-na iliyotolewa ndani ya kitabu . Ingawa mwongozo huu wa mwalimu una majibu kwa kila kazi zote zilizotolewa katika kitabu cha mwanafunzi, unaombwa kupitia kila swali na kazi kabla ya ku-tathmini matokeo ya utafiti.

FASIHI MWONGOZO WA KUSAHIHISHIA FASIHI TATHMINI YA PAMOJA MACHI/APRILI 2017 SEHEMU YA A: FASIHI SIMULIZI (a)i Utungo wa kishairi ambao hutungolewa kwa kutumia sauti iliyo kati ya uimbaji na uzungumzaji (kalima) 1 x 2 alama 2 (ii) Sifa za maghani (i) Yana muundo wa kishairi. (ii) Tamathali za semi hutumika kwa wingi.

Ms. Fika Mwakabungu - Mkurugenzi Idara ya Mafunzo na Mitaala . kuwasiliana kwa lugha ya Kiswahili, Utambuzi, Kuhusiana, Kujenga Mwili na Kuthamini Mazingira. Aidha mwongozo huu unatoa maelekezo ya kutumia . Kufanya upimaji na tathmini ya maendeleo ya watoto kwa kutumia mbinu zilizopendekezwa katika mwongozo.

Sheria ya Elimu Na. 25 ya mwaka 1978 na Rekebisho Na. 10 la mwaka 1995 ikisomwa pamoja na Waraka wa Elimu Na. 4 wa mwaka 2016 unaohusu mwongozo wa uundaji wa Kamati ya Shule. Ibara ya 3 kifungu cha 39 cha Sheria ya Elimu Na. 25 ya mwaka 1978, inazitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa kuunda Kamati ya

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU MWONGOZO WA UTOAJI MIKOPO NA RUZUKU KWA WANAFUNZI KWA MWAKA WA . (malipo ya 25% ya mkopo wa awali si dhamana ya kupangiwa mkopo). . programu (ii) Waombaji wapya lazima wawe wamehitimu elimu ya Kidato cha Sita (ACSEE) au Stashahada ndani ya miaka mitatu, kua

na maisha ya uadilifu na usafi, ambayo yamedhibitishwa na wakati kuwa yanafaa kwa Mkristo. Toleo hili la Kitabu cha Mwongozo la 2017-2021 lina taarifa fupi ya kihistoria ya kanisa, Katiba ya kanisa inayofafanua Kanuni za Imani yetu, ufahamu wetu wa kanisa, Agano la Maadili ya Kikristo ya kuishi kitakatifu,

Andreas Wagner { Integrated Electricity Spot and Forward Model 16/25. MotivationFrameworkModel and ResultsConclusions Volatility of supply-functional This observation motivates the following volatility structure (as in Boerger et al. [2009]) Volatility structure ( ;t) e (t ) 1; 2(t) ; where 1 is the (additional) short-term volatility, is a positive constant controlling the in .