JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - VPO

2y ago
212 Views
2 Downloads
2.40 MB
77 Pages
Last View : 11d ago
Last Download : 3m ago
Upload by : Cannon Runnels
Transcription

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAOFISI YA MAKAMU WA RAISMKAKATI WA TAIFA WA USIMAMIZI WA KEMIKALI NA TAKA HATARISHI2020 - 2025MUHTASARI MAHSUSIMei, 2020

YALIYOMODIBAJI. iSHUKRANI . iiYALIYOMO . iiiORODHA YA MAJEDWALI . vORODHA YA VIELELEZO . viMUHTASARI . vii1. UTANGULIZI .11.1Maelezo ya awali .11.2Umuhimu wa Mkakati .21.3Madhumuni ya Mkakati .21.4Uhusiano wa Mkakati na Mifumo ya Kitaifa na Kimataifa .21.5Misingi inayoongoza Usimamizi wa Kemikali na Taka nchini .41.6Maandalizi ya Mkakati .52. HALI YA USIMAMIZI WA KEMIKALI NA TAKA HATARISHI NCHINI .62.1Jiografia na Uchumi .62.2Mifumo ya kisera, kisheria na kitaasisi inayosimamia kemikali na taka hatarishi nchini.72.2.1Mfumo wa Kitaasisi .72.2.2Mfumo wa kisera.72.2.3Mfumo wa Sheria katika usimamizi wa kemikali na taka hatarishi.102.3Uzalishaji, Uingizaji Nchini, Usafirishaji Nje ya Nchi na Matumizi ya Kemikali .132.3.1Uzalishaji wa kemikali na bidhaa ambata .132.3.2Uingizaji Nchini wa Kemikali na Viambata .142.3.3Usafirishaji nje ya nchi wa kemikali na bidhaa ambata.162.3.4Matumizi ya kemikali na bidhaa ambata .172.3.5Taka hatarishi za Viwandani .182.4Mfumo wa Uratibu wa Wizara za Kisekta .182.5Upatikanaji, Utumiaji na Usimamizi wa Taarifa .192.5.1Hatua za Ukusanyaji na Usambazaji wa Takwimu .192.5.2Mfumo wa kitaifa wa kubadilishana taarifa .202.6Miundombinu ya maabara .202.7Kemikali zilizokwisha muda wa matumizi .202.7.1Viuatilifu vilivyokwisha muda wake na vifungashio vilivyotumika .20iii

2.7.2Kemikali za viwandani zilizokwisha muda wa matumizi .212.8Miundombinu ya kutupa na kuteketeza taka .212.9Utayari wa kukabiliana na matukio ya ajali na dharula zinazohusisha kemikali .212.10Elimu kwa umma .212.11Ushirikiano wa kimataifa katika usimamizi wa kemikali na taka hatarishi .222.12Changamoto katika usimamizi na udhibiti wa kemikali na taka hatarishi nchini .223. MASUALA MAPYA YANAYOJITOKEZA KATIKA USIMAMIZI WA KEMIKALI NA TAKA HATARISHI .233.1Bidhaa zenye viambata vya kemikali.233.2Nanoteknolojia na bidhaa zitokanazo na nanoteknolojia .233.3Kemikali hatarishi katika vifaa vya umeme na kielektroniki .233.4Madini ya Risasi katika Rangi .243.5Kemikali zinazoathiri mfumo wa homoni.243.6Dawa zinazodumu katika mazingira kwa muda mrefu .243.7Kemikali viambata vya florini na mbadala wake .243.8Viuatilifu hatarishi .254. MUHTASARI WA CHANGAMOTO, MALENGO NA VIPAUMBELE VYA MKAKATI .264.1Changamoto .264.2Malengo ya Mkakati .264.2.1Lengo Kuu .264.2.2Malengo Mahsusi .264.3Mpango kazi .274.4Mahitaji ya rasilimali na vyanzo vya fedha.644.5Mpangilio wa Utekelezaji .645. TATHMINI NA UFUATILIAJI .685.1Mpango wa Ufuatiliaji .685.2Mpango wa Tathmini ya Utendaji .68iv

ORODHA YA MAJEDWALIJedwali 1: Uzalishaji wa baadhi ya kemikali na bidhaa ambata Tanzania Bara, 2010-2014 . 13Jedwali 2: Uzalishaji wa mbolea nchini kati ya mwaka 2013 na 2017. 14Jedwali 3: Uingizaji ndani ya nchi wa baadhi ya kemikali za viwandani, mwaka 2018 . 14Jedwali 4: Uingizaji wa mbolea nchini kati ya mwaka 2013 na 2017 . 16Jedwali 5: Usafirishaji wa mbolea nje ya nchi kati ya mwaka 2013 na 2017 . 16Jedwali 6: Uingizaji nchini wa baadhi ya viuatilifu kati ya mwaka 2013 na 2017 . 17Jedwali 7 Mpango wa utekelezaji wa Mkakati ukiainisha majukumu na taasisi husika na mudawa utekelezaji . 28Jedwali 8: Majukumu ya wadau katika utekelezaji wa Mkakati . 64v

ORODHA YA VIELELEZOKielelezo 1 Vipengele muhimu vya mzunguko wa usimamizi wa kemikali . 2Kielelezo 2 Ramani ya Tanzania ikionesha Mikoa na mipaka ya Nchi . 6vi

MUHTASARITanzania inakabiliwa na changamoto ya matumizi yasiyo salama ya kemikali na usimamiziusiosalama wa taka hatarishi katika sekta za kilimo, viwanda, afya, ujenzi, biashara, na maeneoya makazi. Hali hii inachagizwa na uelewa mdogo juu ya madhara yatokanayo na matumiziyasiyo salama ya kemikali na utupaji au uteketezaji usio salama wa taka hatarishi, pamoja nauwezo mdogo wa kitaasisi wa udhibiti na usimamizi wa taka hatarishi hivyo kuhatarisha afya zabinadamu, wanyama na mazingira. Mkakati wa Taifa wa Usimamizi Endelevu wa Kemikali naTaka Hatarishi unatoa mwongozo wa usimamizi bora na salama wa kemikali na taka hatarishinchini ili kulinda afya ya binadamu, wanyama na mazingira.Maandalizi ya Mkakati huu yamehusisha hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuchambuamfumo wa kisheria unaosimamia kemikali na taka hatarishi nchini. Baadhi ya sheriazilizochambuliwa ni pamoja na Sheria ya Kemikali za Viwandani na Majumbani (Usimamizi naUdhibiti) Na.3 ya 2003; Sheria ya Usimamizi wa Mazingira Na.20 ya 2004; Sheria ya MadiniNa.14 ya 2010; Sheria ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi Na.5 ya 2003; Sheria ya Taasisi yaUtafiti wa Viuatilifu Na. 18 ya 1979; Sheria ya Hifadhi ya Mimea Na.13 ya 1997; Sheria ya Usafiriwa Majini Na. 21 ya 2003; Sheria ya Chakula, Madawa na Vipodozi Na. 1 ya 2003; Sheria yaMipango Miji Na. 8 ya 2007; Sheria ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira Na.5 ya 2019;Sheria ya Afya ya Jamii Na.1 ya 2009; Sheria ya Usimamizi wa Viwango Na. 2 ya 2009; Sheria yaNishati ya Atomiki Na.7 ya 2003; na Sheria ya Vilipuzi Na 56 ya 1963. Aidha, maoni ya wadauyalikusanywa na kuzingatiwa ikiwa ni pamoja na kikosi-kazi cha wataalam wa kisekta, na warshaya wadau ya kitaifa kupitia, kuboresha na kuridhia Mkakati huu.Mkakati huu unalenga: Kukuza uelewa wa jamii kuhusu matumizi salama ya kemikali na atharizitokanazo na matumizi ya kemikali yasiyo salama na usimamizi wa taka hatarishi usioendelevu; Kukuza uwezo wa kitaasisi katika usimamizi endelevu wa kemikali na taka hatarishi;Kujenga uwezo wa kitaalam katika usimamizi endelevu wa kemikali na taka hatarishi;Kuimarisha uwezo wa utayari na kukabiliana na ajali au dharura zinazohusisha kemikali; Kujengauwezo na mfumo wa udhibiti wa usafirishaji haramu wa kemikali na taka hatarishi; naKuwezesha kutumika kwa dhana ya uzalishaji salama kwa kutumia mbinu bora na rafiki kwamazingira zilizopo katika sekta zote za uzalishaji.Mkakati huu umepangwa kutekelelzwa kwa miaka mitano 2020 – 2025 kwa gharama ya Dola zaMarekani 23,810,000. Wizara zinazoshiriki katika utekelezaji wa Mkakati huu ni pamoja na zilezinazohusika na: Afya; Kilimo; Madini; Maji; Ujenzi; Mazingira; Viwanda na Biashara; na Tawalaza Mikoa na Serikali za Mitaa. Aidha, taasisi zitakazohusika ni pamoja na: Mamlaka ya Maabaraya Mkemia Mkuu wa Serikali; Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu; Baraza la Taifa la Hifadhi naUsimamizi wa Mazingira; Mamlaka ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi; Taasisi ya Taifa ya Utafitivii

wa Magonjwa ya Binadamu; Shirika la Viwango Tanzania; Ofisi ya Taifa ya Takwimu; Mamlakaya Dawa na Vifaa Tiba; Tume ya Nishati za Atomiki; na Kituo cha Usimamizi wa Uzalishaji BoraViwandani.Tathmini na Ufuatiliaji wa utekelezaji wa Mkakati huu utahusisha ukusanyaji wa takwimu,uchambuzi na uandaaji wa taarifa. Taarifa hii itasaidia kutoa mwenendo na mwelekeo wautekelezaji wa Mkakati huu. Aidha, tathmini ya utekelezaji itafanyika kwa awamu mbili. Awamuya kwanza itafanyika kila baada ya miaka miwili kupima maendeleo ya utekelezaji na tathimniya mwisho itafanyika kwa lengo la kupima mafanikio yaliyofikiwa kulingana na lengo la Mkakati.viii

1. UTANGULIZI1.1Maelezo ya awaliKemikali hutumika katika sekta mbalimbali za uzalishaji ikiwa ni pamoja na:- Afya, Nishati,Usafirishaji, Kilimo, Ujenzi, Viwanda na Biashara na Mafuta na gesi. Pamoja na kuwa na faidakubwa za kiuchumi na kijamii, matumizi yasiyo salama ya kemikali yana athari kwa afya yabinadamu, wanyama, mazingira na ni tishio kwa maendeleo endelevu. Kwa kuzingatia atharizitokanazo na matumizi yasiyo salama ya kemikali, pamoja na uwezo mdogo wa kukabiliana naathari hizo, usimamizi endelevu wa kemikali na taka hatarishi ni changamoto mtambukainayohitaji juhudi za pamoja kukabiliana nayo.Juhudi mbalimbali zimefanyika kuwezesha usimamizi bora wa kemikali na taka hatarishi kwalengo la kulinda afya za binadamu na mazingira. Kimataifa, miongoni mwa juhudi hizo ni pamojana, Mkataba wa Basel Kuhusu Udhibiti wa Usafirishaji na Utupaji wa Taka hatarishi baina yaNchi na Nchi; Mkataba wa Rotterdam kuhusu taratibu za utoaji taarifa za awali kwa baadhi yakemikali hatarishi na viuatilifu katika biashara za kimataifa; Mkataba wa Stockholm KuhusuUdhibiti wa Kemikali Zinazodumu kwa Muda Mrefu kwenye Mazingira; Mkataba wa MinamataKuhusu Udhibiti wa Zebaki; na Itifaki ya Montreal Kuhusu Kemikali Zinazomong’onyoa Tabaka laOzoni.Tanzania kama mwanachama wa mikataba na itifaki zilizoainishwa ina Sera na mfumo wakisheria unaosimamia uzalishaji, uingizaji, usambazaji, matumizi, usafirishaji na uhifadhi wa ainambalimbali za kemikali. Hata hivyo, usimamizi madhubuti na endelevu wa kemikali bado nichangamoto nchini katika ngazi zote. Changamoto nyingine ni pamoja pamoja na uwezo mdogowa kitaasisi katika kudhibiti; uelewa mdogo wa jamii kuhusu athari zinazotokana na kemikali nataka hatarishi katika mzunguko wa matumizi ya kemikali (Kielelezo 1); Miundombinu hafifu; nauratibu hafifu. Kwa muktadha huo, Mkakati huu umeandaliwa ili kutoa mwongozo wa kitaifa wakuboresha uratibu na usimamizi wa kemikali na taka hatarishi katika ngazi zote.1

Kielelezo 1 Vipengele muhimu vya mzunguko wa usimamizi wa kemikali1.2Umuhimu wa MkakatiPamoja na kuwa na faida za kijamii na kiuchumi, ni muhimu kudhibiti athari zinazoweza kutokeakwa afya ya binadamu, wanyama na mazingira kutokana na matumizi yasiyo salama ya kemikalina taka hatarishi ili kufikia maendeleo endelevu. Mkakati huu utatumika kama mwongozo wakitaifa utakaowezesha usimamizi bora na salama wa kemikali na taka hatarishi nchini. Aidha,utekelezaji wake utachangia kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, hususan yaleyanayohusu hifadhi ya mazingira, kulinda afya ya jamii na kupunguza umasikini.1.3Madhumuni ya MkakatiMadhumuni ya Mkakati huu ni kutoa mwongozo wa kitaifa wa kuwezesha usimamizi bora wakemikali na taka hatarishi ili kufikia maendeleo endelevu.1.4Uhusiano wa Mkakati na Mifumo ya Kitaifa na KimataifaMkakati huu umeandaliwa kwa kuzingatia misingi, kanuni, miongozo na mapendekezo yaliyomokatika mifumo ya kitaifa, kimataifa na kikanda na mipango ya maendeleo inayohusu usimamiziwa kemikali na taka hatarishi kama ifuatavyo:a) Ajenda 21 (1992) inayohimiza usimamizi endelevu wa kemikali kama nyenzo muhimu yakufikia maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi katika ngazi ya kitaifa, kikanda nakimataifa;2

b) Jukwaa la Kimataifa la Usalama wa Kemikali (1994) linaloweka mfumo wa ushirikianobaina ya Serikali na Mashirika yasiyo ya kiserikali, katika kufanya tathmini ya atharizitokanazo na kemikali na kuhamasisha usimamizi bora na salama wa kemikali;c) Mpango wa Utekelezaji wa Johannesburg (2002) uliolenga kupunguza athari za kiafyakwa binadamu na mazingira zitokanazo na uzalishaji na matumizi ya kemikali ifikapomwaka 2020;d) Mfumo Linganifu wa Kimataifa wa Kuainisha na Kuweka Alama za Utambulisho kwenyeKemikali (2002) unaohimiza kuainisha na kuweka alama za utambulisho kama sehemuya usimamizi bora na salama wa kemikali;e) Mpango Mkakati wa Bali wa Msaada wa Teknolojia na Kujenga Uwezo (2005) ambao nimfumo uliokubaliwa na nchi wanachama kwa ajili ya kuimarisha uwezo wa nchizinazoendelea kushughulikia mahitaji, vipaumbele na majukumu katika utekelezaji waMikataba ya kimataifa ya Mazingira;f) Mwongozo wa Kimataifa wa Usimamizi wa Kemikali Kimkakati (2006) chini ya Mpangowa Utekelezaji wa Johannesburg ambao unapendekeza mfumo wa kisera wakuhakikisha kwamba, ifikapo 2020, kemikali zitatengenezwa na kutumiwa kwa njiazinazopunguza athari kwa binadamu na mazingira;g) Azimio la Libreville kuhusu Afya na Mazingira (2008) ambalo linahimiza masuala yaathari za mazingira kwenye afya kuhuishwa na kujumuishwa katika sera, mikakati,kanuni na mipango ya maendeleo ya kitaifa; nah) Malengo ya Maendeleo Endelevu yanaelekeza na kutilia mkazo usimamizi bora wakemikali na taka hatarishi ili kulinda afya za binadamu na viumbe wengine wa nchi kavuna majini, na kuhakikisha uzalishaji salama.Pamoja na hayo, maandalizi ya Mkakati huu yamezingatia mipango ya maendeleo ya kitaifaikiwa ni pamoja na:a) Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 ambayo imeweka malengo ya maendeleo ya kitaifakwa kipindi cha miaka 25 kutoka 1999 hadi 2025. Dira hiyo inalenga kuiwezesha nchikutoka kwenye nchi masikini na kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo 2025. Piainakusudia kubadilisha uchumi unaotegemea kilimo peke yake kwenda kwenye uchumiwa kati wa viwanda;b) Mpango wa Taifa wa Muda Mrefu wa Kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025unaotumika kama mwongozo mpya wa utekelezaji wa miaka 5 iliyobaki ya Dira yaMaendeleo ya Taifa ya mwaka 2025. Pamoja na mambo mengine unatoa, mwongozo3

unaolenga kubadilisha uchumi wa nchi kuwa uchumi wa kati unaozingatia utawala bora,maendeleo ya viwanda, rasilimali watu na maendeleo ya teknolojia; nac) Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016/17 - 2020/21) wa KuendelezaViwanda, kukuza Uchumi na Maendeleo ya Watu unaolenga kukuza uchumi nakupunguza umasikini kwa kuimarisha ufanisi katika sekta za kipaumbele zinazohusika namafuta, gesi, kemikali, dawa, ujenzi, kilimo na usindikaji wa bidhaa za kilimo, makaa yamawe na chuma.1.5Misingi inayoongoza Usimamizi wa Kemikali na Taka nchiniMisingi muhimu iliyowekwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inalenga kulindaafya ya binadamu na mazingira ambayo kwa maudhui yake inaelekeza usimamizi bora nasalama wa kemikali na taka hatarishi. Misingi hiyo ni pamoja na:a) Mazingira ni urithi wa kizazi cha sasa na vizazi vijavyo;b) Haki ya Mazingira safi na salama ikiwa ni pamoja na haki za raia kutembelea sehemumaalum za mazingira kwa shughuli za burudani, elimu, dini au kitamaduni;c) Wajibu wa kulinda na kutunza mazingira na kutoa taarifa kwa Mamlaka husika endapokuna vitendo au tukio lolote linaloweza kuathiri mazingira;d) Kuzuia au kupunguza athari mbaya kwa afya na mazingira kwa kuweka mipango nauratibu jumuishi na jitihada za pamoja zinazozingatia mazingira kwa ujumla;e) Msingi wa kinga na tahadhari unaelekeza kulinda mazingira, pale ambapo kuna hatari yakutokea athari kubwa zisizorekebishika, hata pale ambapo ushahidi wa kisayansiunakosekana;f) Msingi wa mchafuzi kulipia gharama, unaomtaka mtu yeyote anayesababisha athari kwamazingira kulipa gharama kamil

vii MUHTASARI Tanzania inakabiliwa na changamoto ya matumizi yasiyo salama ya kemikali na usimamizi usiosalama wa

Related Documents:

wa aya ya 112(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Aidha, kwa mujibu wa Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama Na. 4/2011, Tume ya Utumishi wa Mahakama mbali na kuwa na majukumu mengine inalo jukumu la kuajiri watumishi wa kada mbalimbali wa Mahakama.

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA THE CONSTITUTION OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA OF 1977. CHAPTER 2 OF THE LAWS. 2005 . The following is the official Revised version in English of “KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 1977”. This revised edition of the

Utafiti wa THIS wa mwaka 2016-17 umeongozwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Tume ya Kuthibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) na Zanzibar (ZAC), na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee . MATOKEO YA AWALI UTAFITI WA VIASHIRIA NA MATOKEO YA UKIMWI TAN

kwa kuzingatia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977; Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025; Mpango wa Taifa wa . /12 hadi 2015/16; Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA II); Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2010 hadi 2015; Malengo ya Maendeleo ya Milenia; Sera ya Taifa

CCM - Chama cha Mapinduzi CHADEMA - Chama cha Demokrasia na Maendeleo CSO - Civil Society Organization CUF - Civic United Front DC - District Council . (NEC). Ibara ya 74(6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeipa Tume jukumu la kusimamia na kuratibu uandikishaji wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani .

TARP Tanzania Agricultural Research Project TAWIRI Tanzania Wildlife Research Institute TAWLAE Tanzania Association of Women Leaders in Agriculture and Environment TBC Tanzania Broadcasting Cooperation TBS Tanzania Bureau of Standard TCC Tanzania Communications Commission TCCIA Tanzan

(2019). Muhtasari wa Somo la Maarifa ya Jamii Elimu ya Msingi Darasa la III-VII. Dar es Salaam: Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kunakili, kurudufu, kuchapisha wala kufasiri andiko hili kwa namna yoyote ile bila idhini ya maandishi ya Kamishna wa Elimu,

avanzados de Alfredo López Austin, Leonardo López Lujan, Guilhem Olivier, Carlos Felipe Barrera y Elsa Argelia Guerrero con la intención de mostrar si existió ó no el sacrificio humano entre los aztecas y si los hubo con qué frecuencia y crueldad. Por otra parte, he de mencionar que la elaboración de este trabajo ha sido una ardua tarea de síntesis de diferentes fuentes sobre la .