MWONGOZO WA MUUNDO NA UTENDAJI KAZI WA

2y ago
2.7K Views
169 Downloads
934.86 KB
71 Pages
Last View : Today
Last Download : 3m ago
Upload by : Callan Shouse
Transcription

MWONGOZO WA MUUNDO NAUTENDAJI KAZI WA KAMATI ZASHULE ZA MSINGIOKTOBA, 2016i

Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu, 2016Umebuniwa na kutayarishwa na:Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa ElimuS.L.P 71Bagamoyo, TanzaniaSimu: 255-23-2440216Nukushi: 255-23-2440216Barua pepe: adem@adem.ac.tzTovuti: www.adem.ac.tzHaki zote zimehifadhiwaISBN: 978-9987-458-19-6ii

YALIYOMOSURA YA KWANZA . 1UONGOZI, MUUNDO NA MAJUKUMU YA KAMATI YA SHULE . 11.1Utangulizi . 11.2Umahiri Mkuu . 21.3Umahiri Mahsusi . 21.4Uongozi wa Shule . 21.5Misingi ya Utawala Bora katika Kuendesha Kamati ya Shule 31.6Uundaji wa Kamati ya Shule . 71.6.1 Muundo wa Kamati ya Shule . 81.6.2 Upatikanaji na muda wa madaraka wa Kamati ya Shule . 91.7Majukumu ya Kamati ya Shule .141.8Vikao vya Kamati ya Shule .171.9Hitimisho .20SURA YA PILI .20USIMAMIZI WA SERA NA SHERIA ZA UENDESHAJI WA ELIMU 202.1Utangulizi . 202.2Umahiri Mkuu . 202.3Umahiri Mahsusi . 202.4Dhana ya Sera . 212.4.1 Sheria ya Elimu . 212.4.2 Kanuni za uendeshaji wa elimu ya msingi . 212.4.3 Nyaraka na miongozo ya elimu . 312.5Hitimisho . 37SURA YA TATU . 38USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA SHULE . 383.1Utangulizi . 383.2Umahiri Mkuu . 38iii

ahiri Mahsusi . 38Rasilimali Fedha . 39Ruzuku Kutoka Serikalini . 40Sera na Nyaraka za Kifedha . 41Sheria na kanuni za fedha . 42Upokeaji wa fedha shuleni . 42Vitabu vya makusanyo ya fedha ya shule . 42Hundi . 43Kuchukua fedha kutoka benki . 43Utoaji wa taarifa za mapato na matumizi ya fedha . 44Usimamizi wa Manunuzi na Vifaa Shuleni . 44Hitimisho . 47SURA YA NANE .48UANDAAJI WA MPANGO WA JUMLA WA MAENDELEO YASHULE .484.1Utangulizi . 484.2Umahiri Mkuu . 484.3Umahiri Mahsusi . 484.4Washiriki katika Kuandaa Mpango . 494.5Hatua katika Kuandaa Rasimu ya Mpango . 504.5.1 Uchambuzi wa hali halisi . 504.5.2 Dira na Dhima ya Shule . 524.5.3 Kuweka malengo . 524.5.4 Malengo makuu . 524.5.5 Malengo mahsusi . 534.6Uandaaji wa Bajeti ya Mpango . 544.6.1 Mpango wa utekelezaji . 554.6.2 Mpango Kazi kwa kila mwaka . 57BIBLIOGRAFIA . 59iv

VIFUPISHOMMEMMpango wa Maendeleo ya Elimu yaMsingiOR – TAMISEMIOfisi ya Rais – Tawala za Mikoa naSerikali za MitaaTSMKKKWyESTTaarifa za Shule ya MsingiKusoma, Kuandika na KuhesabuWizara ya Elimu, Sayansi naTeknolojiaADEMAgency for the Development ofEducational ManagementGPELANESGlobal Partnership for EducationLiteracy and Numeracy EducationSupportv

vi

DIBAJIMaendeleo ya taifa lolote yanategemea kwa kiasi kikubwaubora wa elimu ya watu wake. Mahitaji ya utoaji wa elimubora na usimamizi unahitaji uwajibikaji wa karibu kutokangazi ya Taifa, Mkoa, Halmashauri na Serikali ya Kijiji/Mtaa. Ugatuaji wa madaraka kutoka Serikali Kuu kwendakwenye Mamlaka ya Serikali ya Kijiji/Mtaa imekasimumadaraka ya kusimamia kwa karibu utekelezaji waMipango ya Maendeleo ya Shule kwa Kamati za Shule.Elimu ni nyenzo muhimu katika kupambana na maaduiUjinga, Maradhi na Umaskini miongoni mwa jamii. Katibaya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sera ya Elimuna Mafunzo, Dira ya Taifa ya Maendeleo na Mkakatiwa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania(MKUKUTA) vyote vinaipa elimu nafasi ya pekee nakipaumbele katika kuboresha maisha ya Watanzania wotebila kujali jinsi, rangi, kabila au dini ya mtu.Ili kufikia ufanisi unaotarajiwa, Ofisi ya Rais – TAMISEMI,Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wakishirikiana naWakala wa Maendeleo na Uongozi wa Elimu (ADEM) naWashirika wa Maendeleo ya Elimu - GPE kupitia mradiwa LANES wameweka mikakati mbalimbali ya kujengauwezo na kuimarisha utendaji wa kamati ya shule. Ilikufanikisha lengo hili, mwongozo huu umeandaliwavii

kutoa maelekezo ya kuunda Kamati za Shule na kutekelezamajukumu yake kwa ufanisi.Madhumuni ya mafunzo ya Uimarishaji wa Uwezo waKamati za Shule ni kuwaelewesha wajumbe juu ya kazina wajibu wao katika kusimamia maendeleo ya shule.Pia kuwapa nyenzo za kufanyia kazi kwa kuwapatiamiongozo mbalimbali, Sera ya Elimu na Mafunzo, Sheria,Kanuni na Taratibu mbalimbali za Serikali juu ya elimunchini.Mwisho tunachukua fursa hii kuwatakia mafunzomema wale wote watakaopata mafunzo ya kitaifa yaUimarishaji wa utendaji kazi wa Kamati za Shule.Nicolas J. BurettaKAIMU KAMISHNA WA ELIMUviii

ShukraniUtayarishaji wa Mwongozo wa Muundo na Utendaji Kaziwa Kamati za Shule ni matokeo ya juhudi na ushirikiano wawataalamu mbalimbali ambao tungependa kuwashukuru.Napenda kushukuru Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa naSerikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia (WyEST) kwa kuona umuhimu wakuandaa Mwongozo wa Muundo na Utendaji Kazi waKamati ya Shule na kuendesha mafunzo ya uimarishaji wauwezo wa wajumbe wa Kamati ya Shule za Msingi. Aidha,natoa shukrani za pekee kwa uongozi wa Wizara hizi mbilikwa kugharamia na kuwaruhusu baadhi ya watendajiwake kushiriki katika utayarishaji wa Mwongozo huu.Vile vile, nawashukuru wakufunzi wa ADEM walioshirikikatika kuandaa mwongozo huu. Aidha, nawashukuruwataalamu kutoka ngazi mbalimbali za Elimu na wadauwote walioshiriki katika kufanya mapitio na kuboreshaMwongozo huu.Dr. Siston Masanja MgullahMTENDAJI MKUUWakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM)ix

x

SURA YA KWANZAUONGOZI, MUUNDO NA MAJUKUMU YA KAMATIYA SHULE1.1 UtanguliziElimu ni nyenzo muhimu kwa ustawi wa jamii namaendeleo ya uchumi wa nchi kwa ujumla. Serikali yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa elimu katikangazi mbalimbali kuanzia elimu ya awali hadi elimu yajuu. Mwongozo huu ni mahsusi katika kutoa ufafanuzikwa masuala yanayohusu kamati za shule za msingi.Shule ya msingi inamjengea mtoto wa Kitanzania maarifaya awali ya kujua mazingira yake pamoja na kupata stadiza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu. Shule ya msingi nimali ya jamii inayowakilishwa na kamati ya shule katikausimamizi wa maendeleo ya shule. Kamati ya shule nichombo muhimu katika usimamizi na uendeshaji washule.Hivyo, ili kufikia malengo yaliyokusudiwa ni vizuriwajumbe wa Kamati za Shule wakatambua majukumuyao na kupata stadi za uongozi na usimamizi wa shule iliziweze kutoa elimu bora kwa watoto wote.1

1.2 Umahiri MkuuMada hii inalenga kujenga umahiri kwa wajumbe waKamati ya Shule kufahamu misingi ya uongozi nakutambua majukumu yao katika utendaji wa kila siku.1.3 Umahiri MahsusiMada hii inakusudia kumwezesha mjumbe wa kamati yashule;a) Kubaini muundo wa uongozi katika shule yamsingi na mgawanyo wa madaraka;b) Kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatiamipaka iliyowekwa; nac) Kubaini changamoto mbalimbali zinazojitokezakatika uongozi na usimamizi wa shule na namnaya kukabiliana nazoZoezi:i.Uongozi ni nini?ii. Taja misingi ya utawala bora katika shule ya msingi ?1.4 Uongozi wa ShuleUongozi wa shule ni utaratibu unaohusisha Kamati yaShule katika kupanga, kuratibu, kuongoza, kusimamiana kudhibiti rasilimali ili kuleta ufanisi katika utekelezajiwa mpango wa jumla wa maendeleo ya shule. Kamati yaShule ina mchango muhimu katika kutoa maamuzi yanamna bora ya matumizi ya rasilimali za shule.2

Baadhi ya rasilimali za shule ni walimu, vifaa vyakujifunzia na kufundishia, fedha, majengo (madarasa,vyoo na nyumba za walimu) na matumizi sahihi ya mudakatika kazi. Ili kufanikisha utekelezaji bora wa mipangoya shule, kamati ya shule inapaswa kufanya kazi kwakuzingatia na kufuata misingi ya utawala bora ambayo nipamoja na uwazi, ushirikishwaji wa jamii, uwajibikaji nakuheshimu uhuru wa maoni.1.5 Misingi ya Utawala Bora katika Kuendesha Kamatiya ShuleKamati ya Shule ina wajibu wa kufanya shughuli zakekwa kuzingatia misingi ya Utawala Bora. Misingi hiyo nipamoja na:a) ushirikishwaji;b) utawala wa sheria;c) uwazi;d) kutoa huduma kwa wakati; nae) uwajibikaji.Ni muhimu kwa kamati ya shule kufanya kazi kwa weledina kwa kuzingatia misingi ya uongozi bora na utawala washeria. Malalamiko mengi kutoka kwa wadau mbalimbalikuhusu shule yanatokana na kukiukwa kwa misingi yauongozi shirikishi na uwazi. Kamati ya shule ishirikianena mwalimu mkuu na walimu kwa ujumla kuhakikishakuwa shule inakuwa kitovu cha utoaji huduma bora kwawadau wote.3

Kamati ya Shule itimize wajibu wake kwa kufuatamiongozo mbalimbali ya elimu na taratibu za nchi kwaujumla. Kadri wadau wanavyoridhika na utolewajiwa huduma katika shule ndivyo wanavyokuwa tayarikujitolea kuisaidia shule kukabiliana na changamotombalimbali.Wadau wa ShuleWadau wa shule ni watu au taasisi zenye maslahi nashule, wanaweza kushiriki katika ujenzi wa shule namiundombinu yake au wananufaika kwa njia moja aunyingine kwa huduma zitolewazo shuleni. Wadau haowanaonyeshwa kwenye kielelezo kifuatacho.4

Kielelezo na. 1 Wadau wa ShuleMuundo wa Uongozi wa ShuleZoezii.Uongozi wa Shule unaundwa na watu gani?ii.Kamati ya Shule inawajibika kwa nani katikamuundo wa uongozi wa shule?Muundo wa Uongozi wa shule ni mfumo unaooneshamahusiano ya kiutawala na uwajibikaji. Ufuatao nimuundo wa uongozi wa shule ya msingi;5

Kielelezo Na 2. Muundo wa Uongozi wa /MtaaMratibuElimuKataKamatiyaShuleMwalimu MkuuMipangoFedhanaMalezi naUshauriNasahaTaalumanaNidhamuMwalimu MkuuMsaidiziMwalimuw aTaalumaMwalimu wavifaa unziWanafunzi6Mwalimuw amiradinaMazingiraMiundombinu naMazingira

Muundo huu unaonesha mahali ilipo kamati ya shule,hivyo wajumbe wa kamati ya shule watambue nawajitambue kama sehemu muhimu ya uongozi katikashule.1.6 Uundaji wa Kamati ya ShuleZoezii. Je Kamati ya Shule ipo kisheria?ii. Je kamati ya shule inapaswa kuwa na wajumbewangapi?iii. Kamati ya Shule itakaa madarakani kwa muda ganitangu kuchaguliwa?iv. Je mjumbe wa Kamati ya Shule anaweza kuitumikiakamati kwa vipindi vingapi?v. Je mwenyekiti wa mtaa/kijiji, diwani au mbungeanaweza kuwa mjumbe wa Kamati ya Shule?Kamati ya Shule ni chombo kilichoundwa kisheria kwaSheria ya Elimu Na. 25 ya mwaka 1978 na Rekebisho Na.10 la mwaka 1995 ikisomwa pamoja na Waraka wa ElimuNa. 4 wa mwaka 2016 unaohusu mwongozo wa uundajiwa Kamati ya Shule.Ibara ya 3 kifungu cha 39 cha Sheria ya Elimu Na. 25ya mwaka 1978, inazitaka Mamlaka za Serikali za Mitaakuunda Kamati ya Shule kwa kila shule ya msingi. Ibara7

hii ikisomwa pamoja na Waraka wa Elimu Na. 4 wamwaka 2016 inaainisha idadi ya Wajumbe wa Kamati yaShule, wajibu wa kamati na muda wa wajumbe wa Kamatiya Shule kuwa madarakani. Kwa maana hiyo, kamati yashule imeundwa kisheria na ina nguvu ya kisheria katikauendeshaji, usimamizi na uongozi wa shule.1.6.1 Muundo wa Kamati ya ShuleKwa mujibu wa Waraka wa Elimu Na. 4 wa Mwaka 2016Kamati ya Shule inatakiwa kuwa na wajumbe kumi nawatatu (13) kutoka katika makundi yafuatayo:a) Wajumbe watano (5) waliochaguliwa na wazazikutoka miongoni mwa wazazi au walezi wawanafunzi wanaosoma katika shule husika;b) Mwenyekiti, awe ni mkazi wa eneo hilo na piaawe na kiwango cha elimu kisichopungua kidatocha nne, cheti cha kuhitimu elimu ya sekondari auzaidi;c) Makamu Mwenyekiti, awe na sifa kama zaMwenyekiti;d) Katibu, atakuwa Mwalimu Mkuu wa shule husika;e) Wajumbe wawili (2) kutoka serikali ya mtaa au kijijishule ilipo kwa kuzingatia jinsi;f) Mwalimu wa taaluma katika shule;g) Mwalimu mmoja (1) anayechaguliwa na walimukutoka miongoni mwao; nah) Afisa Elimu kata wa kata husika.8

TANBIHI: Waheshimiwa Wabunge, Madiwani naWenyeviti wa Serikali za Vijiji/Mitaa wasiwesehemu ya wajumbe wa Kamati ya Shule.1.6.2Upatikanaji na muda wa madaraka wa Kamati yaShulea) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti waKamati ya Shule wachaguliwe katika kikao chawazazi;b) Wajumbe wakishachaguliwa Mwalimu Mkuuwa shule husika amtaarifu Mkurugenzi waHalmshauri juu ya uundaji wa kamati ikioneshajina na cheo kwa kila mjumbe, nakala ya baruahiyo ampe Afisa Elimu Kata;c) Mkurugenzi wa Halmashauri atoe barua yautambulisho wa wajumbe wa kamati ya shulekwa kila shule;d) MwenyekitinaMakamuMwenyekitiwanatakiwa wawe na angalau kiwango chaelimu ya kidato cha nne na wawe ni wakaziwa kudumu katika Kijiji / Mtaa ambamo shuleipo. Wajumbe wengine wawe na sifa ya kuwezakusoma, kuandika na kuhesabu;e) Wajumbe wa kamati watakuwa madarakanikwa muda wa miaka mitatu (3);f) Baada ya muda wa miaka mitatu (3) kumalizika,mjumbe anaweza kuchaguliwa tena lakini si9

g)h)i)j)zaidi ya vipindi viwili mfululizo;Nafasi inayoachwa wazi kwa sababu maalum(kama uhamisho, kifo, kutohudhuria vikao3 mfululizo n.k) itajazwa kwa kumchaguamjumbe mpya kupitia kikao cha wazazi, naatakuwa mjumbe kwa kipindi kilichobaki chakamati;Mjumbe anayetaka kujiuzulu anatakiwakumtaarifu Mwenyekiti kwa maandishi;Kila mjumbe wa kamati anatakiwa kuwa nakazi halali zinazompatia kipato kwa ajili yamaisha yake; naUwiano wa wajumbe unatakiwa uzingatie jinsi(me/ke) wakati wa uchaguzi.1.6.3 Kamati ndogondogo za Kamati ya ShuleKamati ya Shule itakuwa na kamati ndogondogo zifuatazo:a) Mipango na Fedha;b) Miundombinu na Mazingira;c) Taaluma na Nidhamu;d) Afya na Chakula; nae) Malezi na Ushauri Nasaha.Majukumu ya kila kamati ndogo ya Kamati ya Shule nikama ifuatavyo;10

a)Kamati ya Fedha na Mipangoi)kusimamia Mpango wa Jumla waMaendeleo ya Shule pamoja na MpangoKazi;ii) kufuatilia utekelezaji wa mpango;iii) kusimamia manunuzi na kuhakikiubora wa vifaa vinavyonunuliwa; naiv) kubuni na kusimamia vyanzo vyamapat.,b)Kamati ya Afya na Chakulai) kuhamasisha na kusimamia upatikanajina utoaji wa chakula shuleni;ii) kuhakikisha uwepo wa huduma yakwanza;iii) kuhakikishashuleinachumbamaalumu cha wasichana; naiv) kuhakikisha upatikanaji wa maji safina salama, viwanja vya michezo, vyoona uimarishaji wa Haki za Mtoto.Kuwa na uhakika wa chakula cha mchana shulenikutaimarisha mahudhurio na wanafunzi kuwepo shuleni.Kamati ya Shule ikishirikiana na walimu na wazaziinaweza kuwasaidia wanafunzi kuzalisha mazao kwa ajiliya chakula chao.11

Ni haki ya mtotokuangaliwa afya yake.Mwalimu akiwakaguawanafunzi wake usafiwa menoc)Kamati ya Miundombinu na MazingiraMajukumu ya Kamati ya Miundombinu naMazingira ni kama ifuatavyo:i) Kufuatilia ujenzi wa miundombinu muhimushuleni ikiwemo ya wenye mahitaji maalum;ii) Kuhamasisha na kufuatilia utunzaji wamazingira ya shule ikiwa ni pamoja nakupanda miti ya vivuli na matunda;iii) Kusimamia ukarabati wa majengo na samaniza shule;iv) Kuhakikisha kuwa shule ina madarasa yawanafunzi wa elimu ya awali;v) Kufuatilia na kuhakikisha kuwa maeneo yashule yanapimwa na kupata hati miliki; navi) Kuhakikisha kuwa mazingira ya ndanina nje ya darasa ni salama na rafiki kamayanavyoelezewa hapa chini.12

d)Mazingira ya ndani ya darasaKamati ya Shule inapaswa kuhakikishakuwa shule ina madarasa ya kutoshaambayoyanakidhimahitajiyakufundishia na kujifunzia kwa kuzingatiaviwango vilivyowekwa na Wizaraya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Piayanapaswa kuwa na samani za kutoshakwa wanafunzi wa kawaida na wenyemahitaji maalumu. Mazingira ya nje ya darasaNamna shule inavyoonekana kwa njehutoa taswira ya kinachoendelea ndaniya madarasa. Shule yenye mazingiramazuri huwavutia wanafunzi, walimu najamii kwa jumla. Madarasa, ofisi, ghala,nyumba za walimu, viwanja vya michezombalimbali, barabara, vitalu vya maua,upandaji wa miti, matangi ya kuvunamaji ya mvua, barabara zinazotenganishasehemu mbalimbali, ikiwa ni pamojana mashimo ya takataka lazima vyotevipangwe kitaalamu.Kamati ya Malezi na Ushauri NasahaMajukumu ya Kamati hii ni kuhakikisha kuwawanafunzi:13

i)ii)iii)iv)v)vi)wanapata malezi bora shuleni;wanatengewa chumba maalum cha ushaurina unasihi;wanapata huduma ya ushauri na unasihi;haki zao zinalindwa;mazingira ya shule ni rafiki; nawanapata fursa ya burudani zinazozingatiamaadili mema na wanajiepusha na makundimabaya.1.7 Majukumu ya Kamati ya ShuleZoezi:i) Je kamati ya shule ina majukumu gani?ii) Je kamati ya shule inapaswa kukaa vikao vingapi kwamwaka?iii) Kamati ya shule iwe na kamati zipi ndogo ndogo?Kamati ya Shule iko kisheria, hivyo majukumu yakeyanatambuliwa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa.Yafuatayo ni miongoni mwa majukumu ya Kamati yaShule:a) Kuandaa Mpango wa Maendeleo ya Shule nab)c)Mpango Kazi wa Shule;Kubuni na kupanga mikakati ya maendeleo yashule;Kusimamia utekelezaji wa utoaji wa elimu bora;14

d) Kuhimiza uwajibikaji na nidhamu katika shule;e) Kuitisha vikao vya wazazi na kutoa taarifa yamaendeleo ya shule;f) Kuandaa bajeti na kusimamia matumizi ya fedha zashule;g) Kuidhinisha matumizi ya fedha za shule;h) Kusimamia ujenzi na ukarabati wa miundombinuya shule;i) Kuhimiza usafi, afya bora za wanafunzi na utunzajiwa Mazingira;j) Kusimamia matumizi bora ya fedha ya uendeshajiwa shule;k) Kutoa taarifa kwenye Serikali ya Kijiji/Mtaa juu yamaendeleo ya shule;l) Kusimamia upatikanaji wa chakula cha mchanakwa wanafunzi;m) kusimamia uandikishaji wa wanafunzi wenyeumri wa kuanza shule wakiwemo wenye mahitajimaalum kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa naSer

Sheria ya Elimu Na. 25 ya mwaka 1978 na Rekebisho Na. 10 la mwaka 1995 ikisomwa pamoja na Waraka wa Elimu Na. 4 wa mwaka 2016 unaohusu mwongozo wa uundaji wa Kamati ya Shule. Ibara ya 3 kifungu cha 39 cha Sheria ya Elimu Na. 25 ya mwaka 1978, inazitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa kuunda Kamati ya

Related Documents:

kuhusu suala la utendaji wameshughulikia utendaji katika fasihi simulizi, tamthilia na sanaa za maonyesho. Ingawa riwaya imetafitiwa kwa kina, tafiti nyingi ni zile zinazoegemea fani na maudhui. Tofauti na tafiti hizi, utafiti huu umejikita katika utendaji wa kidrama katika riwaya, mintarafu riwaya ya Haini ya Shafi Adam Shafi

Maana ya Serikali za Mitaa na Dhana ya kupeleka Madaraka kwa Wananchi 2 Mfumo na Muundo wa Serikali za Mitaa 3 Mamlaka za Wilaya 3 Mamlaka za Miji 5 Muundo wa Serikali za Mitaa mbalimbali 6 Kitongoji 6 Mtaa 6 Kijiji 7 Kamati ya Maendeleo ya Kata 7 Mamlaka ya Mji Mdogo 8 Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Jiji (kama vile Mwanza) 8

FASIHI MWONGOZO WA KUSAHIHISHIA FASIHI TATHMINI YA PAMOJA MACHI/APRILI 2017 SEHEMU YA A: FASIHI SIMULIZI (a)i Utungo wa kishairi ambao hutungolewa kwa kutumia sauti iliyo kati ya uimbaji na uzungumzaji (kalima) 1 x 2 alama 2 (ii) Sifa za maghani (i) Yana muundo wa kishairi. (ii) Tamathali za semi hutumika kwa wingi.

Sehemu ya 3: Hutoa mwongozo au maelekezo ya ufundishaji kwa kila dha-na iliyotolewa ndani ya kitabu . Ingawa mwongozo huu wa mwalimu una majibu kwa kila kazi zote zilizotolewa katika kitabu cha mwanafunzi, unaombwa kupitia kila swali na kazi kabla ya ku-tathmini matokeo ya utafiti.

Namba ya Mkataba: AID-621-C-15-00003 Mwongozo Wa Mkufunzi Wa Mfumo Wa Ujifunzaji Wa Kieletroniki (MUKI) Agosti, 2019. KANUSHO Chuo cha Serikali za Mitaa (Hombolo) ndicho kitawajibika na matokeo ya kazi hii. Mwongozo Wa Mkufunzi Wa Mfumo Wa Ujifunzaji Wa Kieletroniki (MUKI) ni maoni ya

Muhtasari wa Elimu ya Awali umeandaliwa ili kuwawezesha watoto kujenga umahiri uliokusudiwa. Muundo wake una vipengele . 2 vitano ambavyo ni: umahiri mkuu, umahiri mahususi, shughuli za kutendwa na mto

Ms. Fika Mwakabungu - Mkurugenzi Idara ya Mafunzo na Mitaala . kuwasiliana kwa lugha ya Kiswahili, Utambuzi, Kuhusiana, Kujenga Mwili na Kuthamini Mazingira. Aidha mwongozo huu unatoa maelekezo ya kutumia . Kufanya upimaji na tathmini ya maendeleo ya watoto kwa kutumia mbinu zilizopendekezwa katika mwongozo.

REKONSILIASI EKSTERNAL DATA SISTEM AKUNTANSI INSTANSI SATUAN KERJA Universitas Pendidikan Indonesia repository.upi.edu perpustakaan.upi.edu BAB I PENDAHULUAN 1.1 Latar Belakang Penelitian Masa reformasi menyadarkan masyarakat akan pentingnya pengelolaan keuangan pemerintah yang harus dilaksanakan dengan prinsip pemerintahan yang baik, terbuka dan akuntanbel sesuai dengan lingkungan .