Maendeleo Ya Kiswahili - Mwalimu Wa Kiswahili

2y ago
604 Views
15 Downloads
1.94 MB
112 Pages
Last View : Today
Last Download : 2m ago
Upload by : Brady Himes
Transcription

Maendeleo Ya Kiswahili 2020Maendeleo Ya KiswahiliLugha ni nini?Wataalamu mbalimbali wa isimu wanakubaliana kwamba lugha nimfumo wa sauti za nasibu ambazo hutumiwa na jamii kwa madhumuniya kuwasiliana kati yao.Fasili hii inaelekea kutuambia kuwa kwa asili binadamu hazaliwi nalugha bali hukutana nayo katika jamii. Hii ina maana kwamba lugha simojawapo ya maumbile ya mwanadamu hivyo basi kwa kuwamwanadamu hazaliwi na lugha inapotokea watu wawili au zaidiwasiosema lugha moja wakikutana pamoja wanalazimika kufuatanamna fulani ya kuwasiliana.Lugha ya KiswahiliKiswahili ni lugha ambayo inatumiwa na watu ambao idadi yakeinakadiriwa kuwa zaidi ya milioni sitini (60). Miongoni mwa nchi namaeneo ambamo Kiswahili kimejikita ni Tanzania, Kenya, Uganda,Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda, Burundi, Msumbiji,Zambia, Malawi, Afrika Kusini, kutaja kwa uchache.Nje ya Afrika maeneo kinakozungumzwa Kiswahili ni kama Dubai,vituo vya utangazaji vya China, Irani, Vatikani, BBC, Dochivele, Idhaaya Redio Ngoma-Lubumbashi, Redio Isangamilo na vyuo vingi vyanchi za nje.Hivi sasa takwimu zinaonesha lugha ya Kiswahili inashika nafasi yatatu kwa kuzungumzwa katika bara la Afrika.Maeda, T.S 0717104507mwalimuwakiswahili.co.tzUk . 1

Maendeleo Ya Kiswahili 2020Pamoja na umuhimu mkubwa wa lugha ya Kiswahili, historia yakeimekuwa kitendawili ambacho kimezaa mijadala ya miaka mingi katiya wanazuoni, wasemaji wa kawaida wa lugha hii, waswahili wazawana wageni katika nchi za nje. Hali hii imejitokeza wazi katikamakongamano, semina, katika vitabu na makala kadhaa ambazozimeandikwa juu ya suala hili. Kutokana na kitendawili hicho mjadalaunaoendelea hasa ni juu ya asili na chimbuko la lugha ya Kiswahili.Mara nyingi watu wanapozungumza lugha ya Kiswahili huwawanatumia maneno asili na chimbuko kwa maana sawa. Jambo hili sisahihi kwa sababu kila moja ya maneno hayo lina maana na dhati yake.Neno asili lina maana ya jinsi kitu au jambo lilivyoanza na nenochimbuko lina maana ya mahali kitu au jambo lilipoanzia.Asili Ya KiswahiliBaadhi ya wataalamu wameibua nadharia mbalimbali zinazojadilikuhusu asili ya lugha ya Kiswahili. Nadharia hizo ni:Kiswahili asili yake ni KongoBaadhi ya wataalamu hudai kuwa asili ya Kiswahili ni huko Kongoambayo baadaye iliitwa Zaire na sasa inaitwa Jamhuri ya Kidemokrasiaya Kongo. Dai hili linaimarishwa na wazo lingine linalodai kwambakatika vipindi kongwe vilivyopata kuwako, sehemu za Pwani (Upwa)ya Afrika Mashariki hazikuwa zikikaliwa na watu. Kutokana na hali yavita, uchungaji wa mifugo na biashara, inadaiwa kuwa Wabantu tokasehemu za Kongo walisambaa na kuja pwani ya Afrika masharikiwakipitia Kigoma. Baadhi ya wabantu hawa walipitia sehemu zaUganda. Wakati wa kusambaa kwao walieneza pia lugha zao ikiwemohii ya Kiswahili.Maeda, T.S 0717104507mwalimuwakiswahili.co.tzUk . 2

Maendeleo Ya Kiswahili 2020Udhaifu wa nadharia hii ni kwamba, madai ya kuwa asili ya Kiswahilini Kongo hayana msingi kwani mpaka sasa wataalamu wanaodai hivihawajaweza kueleza na kuthibitisha kisayansi ama kihistoria juu ya linihasa watu walianza kuishi pwani ya Afrika mashariki.Kiswahili ni Pijini au Krioli(i) Kiswahili ni PijiniBaadhi ya wataalamu hudai kuwa Kiswahili ni Pijini. Wataalamuhawa hudai kwamba Pijini ni lugha ambayo huzaliwa kutokana nakukutanika kwa makundi mawili (A) na (B) yanayotumia lugha mbilitofauti. Ili makundi haya yaweze kuwasiliana kunaundwa lughaambayo kitabia ni tofauti na zile zinazozungumzwa na makundiyanayohusika. Lugha hii inaweza kuwa na msamiati mwingi kutokalugha kati ya zile mbili au inaweza kuwa na msamiati wenye uzitosawa. Lugha hiyo ndiyo inayoitwa Pijini. Mazingira ya kutokea kwaPijini ni kama vile biashara, utumwa, ukoloni, n.kAKiarabuBKibantuABPijiniMaeda, T.S 0717104507mwalimuwakiswahili.co.tzUk . 3

Maendeleo Ya Kiswahili 2020ZINGATIAWataalamu wa nadharia hii hudai kwamba Kiswahili ni lugha ya katiiliyozuka ili kurahisisha/kufanikisha mawasiliano katika shughuli zabiashara kwa sababu hapakuwa na mfanyabiashara hata mmoja wao (A)aliyeijua lugha ya mfanyabiashara mwenzake (B). Lugha inayozushwana makundi haya mawili (A) na (B) ndiyo huitwa Pijini.Kwa mantiki ya nadharia hii, wataalamu hawa hukiona Kiswahili kuwakilianza kama Pijini kwani ni tokeo la mwingiliano baina ya wenyejiwa pwani ya Afrika Mashariki na wageni kutoka mashariki ya katihususani Waarabu. Aidha, husisitiza kuwa lugha ya Kiswahilihaikuwepo kabla ya hapo.(ii) Kiswahili ni KrioliWataalamu hawa wanadai kwamba watu wanaozungumza Pijiniwanaweza kuishi pamoja kwa muda wa karne nyingi na kwa hiyowakaweza kuzoeana na hata kufikia hatua ya kuoana. Wakioana watotowao huikuta Pijini kama lugha yao ya kwanza,katika jitihada zakujifunza na kuizungumza hutokea tofauti hasa katika matamshi.Tofauti hizo huonekana kama upotoshi wa lugha ya kwanza. Inapofikiahatua ya aina hii kwa watoto wanaozungumza lugha hiyo, waohusemekana sasa wanazungumza lugha ya Ki-Krioli, lugha ambayo nihatua ya juu ya Pijini, yaani Pijini iliyokomaa.Nadharia hii hutumia kigezo cha msamiati wa Kiswahili kuoneshauhusiano uliopo kati ya Kiswahili na Kiarabu. Wanadai kuwa,msamiati mwingi wa Kiswahili unatokana na Kiarabu. Hivyohuhitimisha kuwa hapana shaka Kiarabu kimehusika katika kuizalishana kuikomaza lugha ya Kiswahili.Maeda, T.S 0717104507mwalimuwakiswahili.co.tzUk . 4

Maendeleo Ya Kiswahili 2020Udhaifu wa nadharia hii ni kwamba hutumia kigezo cha msamiati tubila kuzingatia vipengele vingine vya lugha kama vile matamshi,maumbo ya maneno au muundo wa sentensi za Kiswahili. Aidha,wataalamu hawa hawakuhoji suala la kufanana kwa Kiswahili na lughajirani katika hayo yaliyotajwa hapo juu na katika eneo la Kijiografiaambamo Kiswahili na lugha hizo nyingine hujikuta zikizungumzwa.Vigezo hivi ni ushahidi tosha unaoonesha kuwa Kiswahili SI Ki-Pijiniwala SI Ki-Krioli, bali ni lugha kama zilivyo hizo lugha jirani.Tofauti kati ya Pijini na KrioliPijini na Krioli zina sifa mbalimbali. Baadhi ya sifa hizo ni kwamba:(i)(ii)(iii)Pijini ni lugha inayoanzishwa na wanajamii wenye lughatofauti baada ya kuishi pamoja kwa muda mrefu katikamazingira maalumu, kwa mfano machimboni au utumwani naKrioli ni lugha inayoanzishwa na vizalia vya wanajamiiwanaotumia pijini.Mara nyingi msamiati wa pijini huwa umeathiriwa zaidi namazingira ambamo lugha yenyewe imeanzishwa na kriolimsamiati wake huwa umeathiriwa zaidi na pijini.Krioli hutumika kama lugha mama lakini pijini hutumikakama lugha ya pili. Katika jamii nyingi pijini na krioli ni lughazisizopewa hadhi sana, sababu kubwa ikiwa ni historiayenyewe ya lugha hizi ambayo inaonesha kuwa pijini na kriolizimetokana na watu duni, hususani watumwa.Ingawa mwanzoni huwa si lugha sanifu, pijini na krioli huwezakusanifiwa na hivyo kutumika kama lugha sanifu pia.Maeda, T.S 0717104507mwalimuwakiswahili.co.tzUk . 5

Maendeleo Ya Kiswahili 2020Kiswahili ni Lugha ya Jamii ya Vizalia (Chotara)Kundi la kwanza la wataalamu wa nadharia hii, ni Bishop EdwardSteer, Bwana Taylor, Dkt. R. Reusch, (Katika Maganga, 1997) hudaikwamba:Waarabu na Waajemi waliohamia pwani ya Afrika ya Masharikiwaliwaoa wanawake wa ki-Afrika.Watoto wao walijifunza maneno ya Kiarabu na ki-Ajemi kutokakwa baba zao.Aidha, watoto hao wakajifunza maneno ya ki-Bantu kutoka kwamama zao.Katika jitihada zao, watoto hao walijirekebisha kutokanana tamaduni za wazazi wao ambazo ni tofauti: utamaduni waKiarabu na utamaduni wa ki-Bantu.Vizalia hawa wakaanza kutumia lugha mpya ya mseto waKiarabu, Kiajemi na lahaja mbalimbali za ki-Bantu.Kwa kiasi kikubwa, lugha mpya ya mseto ilikuwa ni upotoshajiwa lugha ya Kiarabu na Kiajemi.Mwarabu au Mu-Ajemi alikuwa muumini wa dini ya Ki-islamu.Humo humo, vizalia hawa wakayaingiza maneno ya Kiarabu,Kishirazi na Kihindi katika hii lugha mpya.Pamoja na kuyaingiza maneno ya kigeni, lugha-mpya yao hii(Kiswahili), ilikithiri vionjo vingi vya lugha mbali mbali za kiBantu.Ndipo baadaye, lugha mpya hii ikajulikana au kuitwa Kiswahili.Kwa maoni ya wataalamu hawa, sehemu mbili kati ya tano(2/5) ya maneno yanayotumika katika lugha hii mpya ni ya kiBantu.Maeda, T.S 0717104507mwalimuwakiswahili.co.tzUk . 6

Maendeleo Ya Kiswahili 2020Sarufi ya lugha mpya hii ni mseto wa ki-Bantu (chenye utata nakisicho na mpangilio maalumu) pamoja na Kiarabu (chenyemantiki na kilichokomaa).Kundi la pili la wataalamu wa nadharia hii ni, B. Krumm na F. Johnsonwenye mawazo yanayodai kwamba:Kiswahili kilitokana na visiwa vya Lamu, Kilamu/Kiamu.Wageni kutoka Ghuba ya Ushirazi/Uajemi na Arabia ya Kusiniwalikuja katika Pwani ya Afrika ya Mashariki na lugha tofauti.Lakini kutokana na kuoana kwao na wenyeji, wageni hawawakaichukua lugha ya hapo walipofikia, wakaikuza kwa manenokadhaa na sentensi kadhaa kutoka lugha zao za asili, yaaniKiarabu, Kiajemi na Kihindi hususan katika masuala ya biashara,ubaharia, vyombo vya kazi zao na nguo.Aidha, utumwa na tabia ya kuoa wake wengi ilisaidia kutoakundi kubwa la masuria. Hali hii ikaondosha hisia za ugeni katikalugha zao; na maneno yote yakabatizwa kuwa ya ki-Bantu, nahata kupoteza kabisa sura ya ugeni.Kiswahili ni KiarabuKuna hoja kuu tatu ambazo baadhi ya wananadharia hii huzitumiakutetea nadharia hii kuwa Kiswahili asili yake ni Kiarabu.(i) Dai la kwanza ni kuwa maneno yenye asili ya Kiarabu yaliyomokatika Kiswahili ni ishara tosha kwamba lugha hii ilianza kamaPijini ya Kiarabu.(ii) Dai la pili linahusu neno lenyewe Kiswahili ambalo asili yake niKiarabu. Neno Kiswahili linatokana na neno “sahil” (umoja) na“swahil” (wingi) lina maana ya pwani.Maeda, T.S 0717104507mwalimuwakiswahili.co.tzUk . 7

Maendeleo Ya Kiswahili 2020(iii) Inadaiwa kwamba kwa kuwa Kiswahili kilianzia pwani, kwakuwaidadi kubwa sana ya wenyeji wa pwani ni waislamu, na kwa kuwauislamu uliletwa na Waarabu, basi Kiswahili nacho kililetwa naWaarabu.Udhaifu wa hoja hiziTukianza na dai la kwanza ‘kwamba maneno yenye asili ya Kiarabuyaliyomo katika Kiswahili ni ishara tosha kwamba lugha hii ilianzakama pijini ya Kiarabu’ tunaona wazi kwamba madai haya hayanamashiko. Lugha ya Kiswahili imetokea kuwa na maneno ya kigeniyenye asili ya Kiarabu (na kwa hakika yapo yenye asili ya Kiajemi,Kireno, Kihindi, Kijerumani, Kiingereza nk.) kutokana na ukwelikwamba kulikuwa na mawasiliano ya karne na karne baina ya wenyejiwa pwani na wafanyabiashara wa Kiarabu. Wasemaji wa lugha mbilitofauti wanapokutana hawaachi kuathiriana kilugha. Kwa hiyo lughakuwa na maneno mengi kutoka lugha nyingine, haifanyi lugha hiyoisemekane kuwa imetokana na hiyo lugha ingine.Pili, wataalamu hawa wanadai kwamba neno lenyewe Kiswahili linamaana ya Kiarabu. Kwani linatokana na neno “sahil” (umoja) na“swahil” (wingi) lina maana ya pwani. Hapa ingetupasa tuelewekwamba kila mtu binafsi au jamii binafsi aghalabu hajiiti mwenyewejina lake, yeye huitwa kwa hilo jina alilopewa na wengine: Jamii yakeau wageni waliomtembelea kwake. Na hivi ndivyo ilivyojitokeza kwaupande wa jamii ya watu wa pwani ya Afrika mashariki, yaaniWaswahili, walipotembelewa na Waarabu na kuitwa As-Sahilyy auAs-Sawahiliyy, na nchi yao kuitwa sahil (wingi wake Sawahil), yaanipwani (upwa), ufuo. Kwa mantiki hii, dai hili halina mashiko! Hebufikiria kwa mfano leo hii watu wote wenye majina ya Kiingereza kama:Johnson, Brighton, Underson, n.k waseme wao ni waingereza kwaMaeda, T.S 0717104507mwalimuwakiswahili.co.tzUk . 8

Maendeleo Ya Kiswahili 2020sababu majina yao yana asili ya lugha ya Kiingereza, nadhani hakunaatakayewaelewa.Kigezo cha dini nacho hakikubaliki, lugha haiwi lugha kwa sababu yaimani. Hata hivyo lugha ya Kiarabu yenyewe ilikuwepo karne nyingikabla ya kufunuliwa dini ya Uislamu. Hali kadhalika, lugha nyingineza Kimagharibi zilikuwepo karne nyingi kabla ya kufunuliwa imani yaukristo. Kama ilivyo kwamba Kiingereza au Kijerumani si ukristo, basindivyo vivyo hivyo ilivyo kwamba Kiswahili hakiwezi kuwa dini yauislamu, asilani! Wala Kiarabu nacho si uislamu. Tunachowezakufanya ni kuitumia lugha kuifasili dini, lakini hatuwezi kuitumia dinikuifasili lugha.Kiswahili ni KibantuVipengele vinavyotumika katika kuihalalisha nadharia inayodaikwamba Kiswahili ni Kibantu ni ushahidi wa ki-Isimu, ushahidi wa kiHistoria na kuichunguza lugha ya Kiswahili katika mfumo mzima wahistoria ya mgawanyiko wa kusambaa kwa lugha za ki-Bantu.Wataalamu wa nadharia hii wanahitimisha kwa kudai kwambaKiswahili ni mojawapo kati ya lugha katika jamii kubwa ya lugha zaki-Bantu.Baadhi ya wataalamu muhimu wanaoiunga mkono nadharia hii ni Prof.Malcon Guthrie, Dkt. C. Meinholf na Dkt. C. Rohl na Prof. ClementMaganga.Ushahidi wa ki-IsimuUshahidi huu unatumia sayansi ya lugha (isimu) kuthibitisha ubantu walugha ya Kiswahili.Maeda, T.S 0717104507mwalimuwakiswahili.co.tzUk . 9

Maendeleo Ya Kiswahili 20201. Utafiti wa Profesa Malcom Guthrie: huyu ni mtaalamu(mwanaisimu) mashuhuri kutoka Chuo Kikuu cha London, Uingereza.Alitumia miaka 20 kuchunguza uhusiano uliopo baina ya lugha zaKibantu zilizoko katika eneo lote ambalo hukaliwa na wabantu.Sehemu hii ni ile ambayo inajulikana kama Afrika, Kusini mwaJangwa la Sahara.Alifanya uchunguzi wa mashina/mizizi (viini) ya maneno 22,000kutoka lugha 200 za Kibantu. Katika uchunguzi wake alikuta mizizi(mashina) 2,300 imezagaa katika lugha mbalimbali za Kibantu naKiswahili kikiwemo. Mashina/mizizi 500 yalilingana katika lugha zote200. Mashina haya yalipatikana katika lugha zote za Kibantu. Mashinahaya yalikuwa ya asili moja. Baadhi ya lugha hizo 200 zilizofanyiwauchunguzi Kiswahili kilionesha kuitikia ulinganifu sawa na Kikongokwa asilimia arobaini na nne (44%).Katika kuchunguza ni asilimia ngapi za mashina hayo 500 yaliyomokatika kila lugha, mgawo uliojitokeza ulikuwa kama ifuatavyo:Kiwemba kizungumzwacho Zambia ------------------------------ 54%Kiluba kizungumzwacho Katanga------------------------------- 51%**Kikongo kizungumzwacho Zaire------------------------------ 44%****Kiswahili kizungumzwacho Afrika Mashariki ----------------- 44%**Kisukuma kizungumzwacho Tanzania ------------------------------ 41%Kiyao kizungumzwacho Tanzania/Msumbiji ---------------------- 35%Kisotho kizungumzwacho Botswana ------------------------------- 20%*Kirundi kizungumzwacho Burundi ------------------------------- 43%*Kinyoro kizungumzwacho Uganda ----------------------------------37%Maeda, T.S 0717104507mwalimuwakiswahili.co.tzUk . 10

Maendeleo Ya Kiswahili 2020Kizulu kizungumzwacho Afrika Kusini ------------------------------29%Baada ya kupata matokeo haya, Profesa Malcom Guthrie anaiungamkono nadharia hii ya kwamba Kiswahili ni ki-Bantu kwa kudaikwamba:(i) Kiswahili kilikuwepo kabla ya ujio wa wageni;(ii) Anaonesha kwamba Kiswahili kina uhusiano mkubwa na lughazaKibantu;(iii) Mwisho anasema Kiswahili kilianzia Pwani ya Afrika Mashariki.2. Utafiti wa Dkt. C. Meinholf na Dkt. C. Rohl: Wataalamu hawawanaamini kwamba:(i) Wakati wa utawala wa Shirazi katika upwa wa mashariki ya Afrikakulikuwa na kabila la Waswahili;(ii) Kabila hili ni dhuria ya Wazaramo wa leo.(iii) Kwa kuwa hawa Wazaramo walikuwa wamezaliwa katika harakatiza kibiashara, kwa hivyo wakafuata nyayo za wazazi wao.(iv) Lugha yao ilikuwa ya aina ya ki-Bantu.(v) Kwa kuwa Wabantu ni wengi zaidi kuliko jamii ya makabilamengine, lugha yao ya Kiswahili ikaanza kutumika na kueneakatikamakabila mengine, hususan katika ukanda wa pwani ya AfrikaMashariki.(vi) Baadaye, Waswahili hawa hawa wakafanya biashara na wageniwaliokuja kuvinjari Afrika Mashariki, hususan Waarabu,Washirazi,Wamalaysia, Wahindi na Wareno ambao tayari walikuwawamefurika katika pwani hii ya Afrika Mashariki miaka kadhaakabla.(vii) Vifaa na majina ya vitu vya biashara vya wageni hao vikaseleleana kuingizwa katika mfumo wa lugha hiyo ya WaswahiliambayoMaeda, T.S 0717104507mwalimuwakiswahili.co.tzUk . 11

Maendeleo Ya Kiswahili 2020ni ki-Bantu.Madai ya nadharia hii yakichunguzwa, tunagundua kwamba inazingatiamitazamo miwili yaani, mtazamo wa ki-Isimu na mtazamo wa kiHistoria. Kwa mantiki hii, nadharia hii inaelekea kukubalika nawataalamu wengi kuwa ndiyo sahihi kuhusu asili au historia yaKiswahili.3. Utafiti wa Profesa C. Maganga, na uthibitisho wake kwambaKiswahili ni ki-Bantu. Kama tulivyoona, lugha ya Kiswahili ilifanyiwautafiti na uchambuzi na wanataaluma kadhaa kwa madhumuni yakuiainisha kama ilikuwa yenye misingi ya ki-Bantu au la. Prof.Maganga alifanya uchambuzi wa ki-Isimu na wa ki-Historia kuhusulugha hii. Matokeo ya utafiti wake wa ki-Isimu kuhusu lugha yaKiswhili (au lugha kwa ujumla) unadhihirisha mambo mengi,mojawapo ni asili ya lugha hiyo. Amethibitisha kwamba Kiswahili nilugha ya Kibantu; na kwa hivyo, kuthibitisha kwa ushahidi thabiti hojaya Dkt. C. Meinholf na Dkt. C. Rohl kama ilivyoelezwa hapo juu.(i) Ushahidi wa Kiisimu (kwa mujibu wa Prof. Maganga)(a) MsamiatiMatokeo ya utafiti alioufanya kuhusu msamiati wa Kiswahili ulibainikwamba 60% ya maneno yote yanayoweza kuandikwa na kutamkikakatika lugha ya Kiswahili asili yake ni lugha za Kibantu, 30% ni lughaya Kiarabu na 10% ni lugha nyingine za kigeni kama vile Kiingereza,Kireno, Kijerumani, Kihindi, Kiajemi, Kifaransa, nk. Kinyume chakeni kwamba msamiati wa Kiswahili na ule wa Kibantu hautofautiani.Maeda, T.S 0717104507mwalimuwakiswahili.co.tzUk . 12

Maendeleo Ya Kiswahili 2020Mfano:Kiswahili MotoUmuliloMotoOmulilo OmoroMwoto(b) Tungo (Sentesi) za KiswahiliMiundo ya tungo (sentesi) za Kiswahili inafanana sana na miundo yatungo za ki-Bantu. Sentesi za Kiswahili na za lugha za ki-Bantu zinakiima na kiarifu.Mfano:Lugha za KibantuKiimaKiswahiliJumaanakula ugali.KiziguaJumaadya ugali.KisukumaJumaalelya bugaliKindaliJumaakulya ubhugali.KijitaJumakalya ubusima.KindendeuleJumaKiarifuilyeughale(c) Ngeli za MajinaWataalamu wanakubaliana kuhusu ngeli za majina kwa mujibu wa:Maeda, T.S 0717104507mwalimuwakiswahili.co.tzUk . 13

Maendeleo Ya Kiswahili 2020maumbo ya nomino (umoja na wingi wa majina) pamoja; naupatanisho wa kisarufi katika sentesi.Kigezo cha maumbo ya majina: Kigezo hiki hufuata maumbo ya umojana wingi katika kuyaainisha majina. Majina yaliyo mengi katika lughaya Kiswahili na lugha za ki-Bantu hufuata mkondo wa umoja na wingi.Majina ya lugha ya Kiswahili na lugha za ki-Bantu yaliyo mengi yanamaumbo dhahiri ya umoja na wingi.Mfano:Lugha za ojaWingimtuwatumtotowatotoomantobanto wanabhandumundubhanamwanaβhanduβhanaKigezo cha upatanisho wa kisarufi katika sentesi: Katika kigezo hikitunaangalia uhusiano uliopo kati ya kiima (jina na viambishi awali vyaMaeda, T.S 0717104507mwalimuwakiswahili.co.tzUk . 14

Maendeleo Ya Kiswahili 2020nafsi) na vivumishi katika vitenzi vya Kiswahili na ki-Bantu.Vivumishi, majina pamoja na viambishi hivyo vya vitenzi hubadilikakutokana na maumbo ya umoja na uwingi.Mfano:Lugha za KibantuUmojaKiswahiliBaba analimaKindaliUtata akulima Abbatata bbakulimaKikuryaTata araremaBatata(Tata)bararemaKijitaTata kalimaBatata abalimaKindendeuleTate ilimaWingiBaba wanalimaAkatate βhilima(d) Vitenzi vya Kiswahili na KibantuKuna uhusiano mkubwa sana kati ya vitenzi vya Kiswahili na vile vyalugha zingine za ki-Bantu. Vipengele vinavyothibitisha uhusiano huuni: Viambishi, mnyumbuliko, pamoja na mwanzo au mwisho wavitenzi, kama ifuatavyo:Viambishi: vitenzi vya lugha ya Kiswahili na vya lugha zingine za kiBantu hujengwa na mzizi (kiini) pamoja na viambishi vyake vya awalina vya tamati.Maeda, T.S 0717104507mwalimuwakiswahili.co.tzUk . 15

Maendeleo Ya Kiswahili 2020Mfano:Kiswahili-analimaa - na - lim - aKikuyu-areremaa - re - rem - aKindali-akulimaa - ku - lim - a1 - 2- 3 - 4Sherehe:1 -Kiambishi awali kipatanishi cha nafsi.2 -Kiambishi awali cha njeo (wakati uliopo).3 -Mzizi/Kiini.4 -Kiambishi tamati maana.Mnyumbuliko wa vitenzi: Mnyumbuliko wa vitenzi vya Kiswahilihufanana na ule wa vitenzi vya lugha za ki-Bantu.Mfano:Kiswahili-kucheka - kuchekesha - kuchekelea.Kindali-kuseka- kusekasha- kusekelela.Kibena-kuheka- kuhekesha- kuhekelea.Kinyamwezi -kuseka- kusekasha- kusekelela.- kuseka- kusekesha- kusekelelaKikaguluMaeda, T.S 0717104507mwalimuwakiswahili.co.tzUk . 16

Maendeleo Ya Kiswahili 2020Mwanzo wa vitenzi: Vitenzi vyote vya Kiswahili na vile vya lugha zaki-Bantu huanza na viambishi ambavyo ni viwakilishi vya nafsi, -ngendaKiyao-N-gwendaKindendeule -Ni-yendaMwishilizo wa vitenzi: Vitenzi vya lugha za ki-Bantu na Kiswahilihuishia na irabu - a.Mfano:Kiswahilikukimbi-a-kuwind-a- kushuk-aKindalikukind-a-kubhing-a- huk-a-kuhig-a-kising-akuhwim-a- kuhuk-aKindendeule kuβhutuk-a -Utafiti wa Prof. Maganga kuhusu ushahidi wa ki-Isimu wa kuthibitishakama Kiswahili ni ki-Bantu au la ungeweza kuelezwa kimuhtasari kwamifano mingine ifuatayo:Maeda, T.S 0717104507mwalimuwakiswahili.co.tzUk . 17

Maendeleo Ya Kiswahili 2020Mfano wa 1:LughaSentesiKiswahiliJongoanafuga g’ombeKindambaJongokafugha menengukunasenga.KichagaJongonao hengukunaumbeKihayaJongon’afuga embuzi enkoko n’KikaguruJongokachima m’ehengu’kuna eng’ombeKatika mfano huu inaonekana kwamba mpangilio wa maneno katikasentesi una ufanano kwa sababu katika kila sentesi kuna kiima nakiarifu. Katika kiima kuna nomino, yaani jina la mtenda (Jongo) nakatika kiarifu kuna kitendo kinachofanyika na nomino mtendwa. Pianafasi ya viunganishi ni ile ile kwa lugha zote zilizooneshwa katikamfano huu.Kuna mfano mwingine wa ufanano wa mpangilio huu.Mfano wa 2:LughaSentesiKiswahiliSitamkuta keshoKihayaTimushangemu nyenkyaMaeda, T.S 0717104507mwalimuwakiswahili.co.tzUk . 18

Maendeleo Ya Kiswahili 2020KisukumaNatusanga intondoKinyaturuTumuhanga fadyuKipareNesikemkiche yavoKiziguaSirambila luviKatika sentensi hizo mpangilio wa maneno una ufanano kwa sababukila sentensi ina kiima na kiarifu chenye kitenzi na kielezi. Piakiambishi cha nafsi cha nomino ya mtenda kinajitokeza mwanzonimwa neno la kwanza la kila ;Nesikamkiche;Sitambila.Viambishi hivyo vya nafsi ya mtenda pia vinaonesha hali ya ukanushikatka kila sentesi na nafasi yake ni ile ile kwa kila sentesi.Viambishi vya urejeshi navyo vinajitokeza katika kitenzi cha kilasentesi.Viambishi {m}, {m}, {ti}, {tu} sitamkuta, timushangemu, natusanga,tumuhanga, nesikamkiche, na sitambwila ni vya urejeshi;vinawakilisha nomino tendwa.Kwa hivyo, hali hii inadhihirisha kwamba miundo ya sentensi hiziinafanana na vitenzi vyake vina tabia mbalimbali, kama vile:Maeda, T.S 0717104507mwalimuwakiswahili.co.tzUk . 19

Maendeleo Ya Kiswahili 2020(i)kubeba viambishi vya nafsi, mtenda na mtendwa(ii)kuoneshga hali ya ukanushi njeo na kitendo kinachofanyika.Mfano wa 3:LughaSentesiKiswahiliAkija mwambie anifuateKiziguaAkeza umugambe anitimile.KihayaKalaija omugambile ampondeleKisukumaUlu nahali anikubijeKinyaturuNewaja mwele ang’onge.KipareEkiza umti aniratereKindendeuleAnda ahikite n’nongerera esizotezinafanana kimpangilio. Pia maneno yake yanakubali uambishaji, kwamfano:(i) Katika maneno ya mwanzo: akija, akeza. kalaija, akuja, newaja,ekiza, herufi zilizopigiwa mstari ni viambishi vya nafsivinavyowakilisha dhana ya mtenda.(ii) Vivyo hivyo katika maneno: anifuate, ampondele, anitimile,ang’onge, aniratere, angobhekeraye, viambishi vilivyoko katikaviarifu vya sentesi hizo vinawakilisha nafsi za watenda.(iii) Pia vitenzi vya sentesi hizo vina tabia ya kubeba virejeshi vyanafsi kama ilivyo katika,mwambie, omugambile, nahali,mbwelena umti, vinaonesha njeo na hali ya uyakinifu- hali inayooneshaufanano wa maumbo ya maneno.Maeda, T.S 0717104507mwalimuwakiswahili.co.tzUk . 20

Maendeleo Ya Kiswahili 2020(iv) Licha ya kuwa na mpangilio unaofanana na wa lugha nyingineza kibantu, kwa mfano, katika mifano tuliyoiona hapo juu, baadhiya maneno yanafanana: tazama maneno: kafugha (Kindamba);nafuga (Kihaya); nifuga (Kindendeule); anafuga (Kiswahili).Pia maneno:nkuku (Kipare); nguku (Kindamba);nguku (Kichaga); enkoko (Kihaya);ng’uku (Kikaguru); nguku(Kindendeule);nguku (Kindendeule)Katika mfano wa 3, maneno yafuatayo yana ufanano:Akeza (Kizigua); kalaija (Kihaya); alize (Kisukuma),newaja (Kinyaturu); ekiza (Kipare); anda ahikite,. (Kindendeule);akija, (Kiswahili.)Pia maneno;umugambe (Kizigua); omugambile (Kihaya); unongeraye(Kindendeule); na mwambie (Kiswahili).Mfanano huu wa msamiati, maumbo ya maneno pamoja na mpangiliowa maneno katika sentensi, vyote vinathibistisha kwamba lugha yaKiswahili ni ya kibantu kama zilivyo nyingi lugha nyinginezo.(ii)Ushahidi wa Kihistoria Kwamba Kiswahili ni KibantuBaada ya kuangalia ushahidi wa kiisimu kuhusu asili ya Kiswahili,katika sehemu hii Maganga (1997) aliendelea kuchambua ushahidi waKihistoria unaothibitisha kuwa lugha ya Kiswahili ilizungumzwaMaeda, T.S 0717104507mwalimuwakiswahili.co.tzUk . 21

Maendeleo Ya Kiswahili 2020katika upwa wa Afrika Mashariki hata kabla ya ujio wa wageni kamavile Waarabu na Wazungu. Ushahidi huu ulitolewa na wagenimbalimbali waliofika hapa Afrika Mashariki. Wote wanathibitishakuwa lugha ya Kiswahili ilizungumzwa hapa Afrika Mashariki kablaya ujio wa wageni.(a) Ugunduzi wa Ali-Idris (1100-1166)Ugunduzi huu yasemekana ulifanywa huko Sicily yapata mwaka 11001166. Kwenye mahakama ya mfalme Roger II. Licha ya kufahamikakuwa Kiswahili, kilipata kuandikwa kabla ya 10BK. Ali-Idris alikuwawa kwanza kugundua jina la zamani la Zanzibar kuwa ni Ungudya.Katika maelezo yake anaandika pia majina kama vile kikonde, mkonowa tembo, muriani, na kisukari, ambayo ni majina ya ndizi mbalimbalizilizokuwa zikipatikana huko ungudya.(b) Ushahidi wa Marco PoloHuyu ni mzungu ambaye alijishughulisha sana na masuala mbalimbaliya kijiografia na alisafiri sehemu nyingi duniani. Marco Polo aliandikahivi:“Zanzibari ni kisiwa kizuri ambacho kina ukubwa wa mzunguko wamaili 200. Watu wote wanaabudu (Mungu), wana Mfalme nawanatumia lugha yao, na hawalipi kodi (ushuru) kwa mtu.” Maelezohaya yanapatikana katika kitabu cha Safari za Marco Polo 1958:301Marco Polo anasemekana aliandika pia kitabu cha jiografia ambachohakikupata kuchapishwa lakini sehemu zake zimepata kufasiriwa kwaKirusi na Kifaransa. Mfano mmojawapo ni huu unaofuata:“Katika visiwa vya djawaga vilivyoshughulikiwa katika sura hii, ni kilekisiwa cha Andjaba ambacho mji wake mkuu unaitwa katika lugha yaMaeda, T.S 0717104507mwalimuwakiswahili.co.tzUk . 22

Maendeleo Ya Kiswahili 2020kwao Zanguabar/Ungudya, na wakazi wake, japokuwa nimchanganyiko, kwa sasa wengi wao ni Waislam chakula chao kikuukikiwa ndizi. Kuna aina tano ambazo zinajulikana kama kundi, fili,ambazo uzito wake waweza kuwa wakia 12, Omani, Muriani,Sukari.”Maelezo haya ya Marco Polo yanathibitisha mambo ya msingi kuhusuwakazi wa Pwani ya Afrika ya Mashariki na lugha yao; mintaarafudini, chakula na utamaduni wao kwa ujumla.(c) Ushahidi wa Al-Masudi (915 BK)Katika moja ya maandiko yake, Al-Masudi anazungumzia juu yawakazi wa mwambao ambao walijulikana kwa jina la “wazanji”. Kwadhana hii, neno Zanzibar linatokana na Zenj’bar yaani “Pwani yaZenji”. Katika maelezo yake Al-Masudi anaonesha kwamba Wazenjiwalikuwa na “Watawala Wa-kilimi” ambao waliaminiwa kuwawalitawala kwa nguvu za ki-Mungu. Kuna maelezo kuwa huenda neno“wakilimi” lina maana ya “wafalme”. Al-Masudi alisisitiza katikamaelezo yake kuwa Wazenji walisema lugha kwa ufasaha na walikuwana viongozi waliowahutubia kwa lugha yao. Kutokana na neno “zenji”kuna uwezekano kuwa kabla ya majilio ya Waarabu, Kiswahili kiliitwa“Kiazania” au “Kizanji” na wageni waliofika pwani.(d) Historia ya Mji wa KilwaKimsingi habari zinazoeleza historia ya mji wa Kilwa katika karne ya10-16BK zinataja majina ya utani kama vile: mkoma watu, nguonyingi, nk. ambayo walipewa Masultani wa kwanza wa Kilwa Ali IbnHussein na mwanawe Mohamedi Ibn Ali. Kutokana na habari hizihuenda lugha ya Kiswahili ilishaanza kusemwa mnamo karne ya 10 auMaeda, T.S 0717104507mwalimuwakiswahili.co.tzUk . 23

Maendeleo Ya Kiswahili 2020ya 11 BK. Maelezo ya kihistoria yanaeleza juu ya Sultani aliyeitwaTalt Ibin Al Husaini ambaye alipewa jina la utani “Hasha Hazifiki”.(e) Utenzi wa Fumo Liyongo (13 BK) kama UshahidiShairi la zamani kabisa lililopata kuandikwa kwa lugha ya Kiswahili,linalojulikana ni lile la Utenzi wa Fumo Liyongo. Utenzi huuinasemekana uliandikwa karne ya 13BK. Kuweko kwa shairi hilikunadhihirisha kuwako kwa lugha ya Kiswahili kabla ya karne hiyo, nakwa hivyo, huenda Kiswahili kilianza kutumika kabla ya karne ya10BK. Baadhi ya beti za utenzi wa Fumo Liyongo ni hizi zifuatazo:Ubeti 6:Liyongo Kitamkali,Akabalighi vijaliAkawa mtu wa kweliNa hiba huongeya.Ubeti 7:Kilimo kama mtukufuMpana sana mrefuMajimboni yu maarufuWatu huja kwangaliya.Ubeti 10:Sultani pate BwanaPapo nae akanenaWagala mumemwonaLiyongo kiwatokeya.(Kutoka E.A. Swahili Committee 1973)(f) Ushahidi wa Ibn Batuta Karne ya 14 BKHuyu ana asili ya kiarabu, alifika miji ya Pwani ya Afrika masharikimwaka 1331BK. Katika maelezo yake anaeleza kwa kirefu maisha yanyakati hizo,anazungumza kuhusu maisha ya Mogadishu pamoja naKilwa anasema:Maeda, T.S 0717104507mwalimuwakiswahili.co.tzUk . 24

Maendeleo Ya Kiswahili 2020“.basi nilianza safari toka Mogadishu kwenda kwenye nchi yawaswahili na mji wa Kilwa ambao umo katika nchi ya Zanji. TulifikaMombasa kisiwa kikubwa mwendo wa siku mbili toka nchi yawaswahili.watu hawajishughulishi na kilimo, huagiza nafaka kutokakwa waswahil.” Katika maelezo haya ingawa anaongelea nchi yawaswahili bila kutaja lugha yao lakini lazima walikuwa na lugha yaona tunaweza kusema lugha hiyo ilikuwa ndicho Kiswahili cha leoingawa si sawa na Kiswahili cha sasa.(g) Maandishi ya Morice Karne ya 18BKMaandishi hayo yalijitokeza mwaka 1776 katika, katika maandishihayo Morice anawagawa wakazi wa Afrika mashariki katika makundimatatu ambayo ni Waarabu, Suriyama (chotara) na Waafrika. Moriceanasisitiza kuwa Suriyama na Waafrika walishakaa na kuungana kamajumuiya na wakaoleana

Kwa mantiki ya nadharia hii, wataalamu hawa hukiona Kiswahili kuwa kilianza kama Pijini kwani ni tokeo la mwingiliano baina ya wenyeji wa pwani ya Afrika Mash

Related Documents:

Kiswahili dialects are endangered by, among other factors, the onslaught of standard Kiswahili, English, and Sheng, and so they are likely to be dying. The paper holds the position that the Kiswahili dialects are vital for the development of standard Kiswahili and, therefore, their endangerment is the endangerment of standard Kiswahili.

Introduction to Kiswahili Poetry KSX 2102 Kiswahili Oral Literature KSX 2104 (with Mr Innocent Yerindabo) Introduction to Kiswahili Novels KSX 2202 History and Development of Kiswahili KSX 3101 Kiswahili Teaching Methods KSX 3201 Drafts Reviewed: Advanced Proficiency in Kiswahili KSX 1102 by Boaz Mutungi.

Song as an aspect of Kiswahili poetry. Origin and development of modern Kiswahili classics such as taarab. Leading founders of Kiswahili popular song in East Africa, history and development of Kiswahili solo, choral and orchestra composition. Themes, style and language use in popular Kiswahili songs.

Kiswahili) na Shahada ya Umahiri/Uzamili ya Sanaa katika Kiswahili (MA. Kiswahili – akitamilikia Fasihi) zote kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania. Chuoni anafundisha kozi za Kiswahili - Lugha, Isimu na Fasihi ikiwemo kozi ya Uandishi wa Kubuni. Pia, hufundisha Kiswahili

4.0 KISWAHILI (102) 4.1 MATOKEO YA MTIHANI WA SOMO LA KISWAHILI Jedwali hili linaonyesha matokeo ya mtihani wa somo la Kiswahili katika muda wa miaka minne (2005 hadi 2008). Jedwali 6: Matokeo ya mtihani wa Kiswahili (2005 - 2008) Mwaka Karatasi Watahiniwa Alama ya Juu Alama ya Wastani Alama ya Tanganisho 2005 1 2 3 Jumla 259,301 40 80

AKS 301: Kiswahili Structure AKS 302: Theories of Literary Criticism AKS 303: Contemporary Kiswahili Novel and Play AKS 400: Sociolinguistics AKS 401: Second Language Learning AKS 402: Kiswahili Poetry AKS 403: Oral Literature in Kiswahili History AHT 102: Introduction to Political Science AHT 200: A History of Kenya AHT 201: Themes in African

Mchango wa Fasihi ya Kiswahili katika Kuudumisha Utambulisho wa Kiswahili : Mifano Kutoka Kazi za Fasihi za Kiswahili Dk. Wael Nabil Ibrahim Othman* Abstract This study emphasizes that the Swahili literature has a very big role in consolidating and maintaining Swahili identity. In the field of Swahili poetry

Grade 2 must build on the strong foundation of Grades K-1 for students to read on grade level at the end of Grade 3 and beyond. Arkansas English Language Arts Standards Arkansas Department of Education