HALl YA KUTATANISHA YA KISWAHILI HIVI LEO AFRIKA YA .

3y ago
116 Views
2 Downloads
1.15 MB
12 Pages
Last View : 9d ago
Last Download : 6m ago
Upload by : Arnav Humphrey
Transcription

AAP 42 (1995) 113-124HALl YA KUTATANISHA YA KISWAHILI HIVI LEOAFRIKA YA MASHARJKJtTIGIII SHAABAN YUSUF SENGOResumee:The essay critically discusses the confusing state of the various Swahili language policies andstudies brought fmth in the colonial and post-colonial periods and exatnines the historical factorsof the diversity within the Swahili language, which was once confined to the coastal area andlater spread to the present area of distribution The discussion focusses on the construction ofStandard Swahili and the status of Swahili in regard to other East African languages Specialcriticism is raised against recent East Mrican and other authors, who wrote on the apparent unityof the Swahili language which they see as a result of the modern Tanzanian language policy1. Utangulizi(i) Hali ya kutatanisha - hali ngumu, hali ya vurugu, hali isiyofahamika, hali ya kujiuza nakujitia vitanzi wenyewe, hali ya kinafiki, ughushi na ubanangifu wa makusudi n k(ii) Kiswahili - Kiswahili mama cha Pwani ya Afrika Mashariki, Kiswahili cha Waswahili,Kiswahili Asilia- Kiswahili Kitanganyika!Kitanzania/Sanifu- Kiswahili Kinairobi/Kikenya- Kiswahili Kiganda- Kiswahili Kirundi- Kiswahili Kinyaruanda- Kiswahili Kizaire-nk(iii) Hivi Ieo - kuanzia 1970 hadi Ieo, tangu Kiswahili k:ianze kufundishwa Vyuo Vikuu vyaAfrika ya Mashariki(iv) Afrika ya Mashariki- Tanganyika, Kenya, Uganda, Zanzibar, Burundi na RuandaLL MadhumuniMakala haya yanakusudiwa kutoa picha inayoonekana na mwandishi juu ya hali ya lughatukufu ya Kiswahili ilivyo hivi Ieo Afrika ya Mashariki Madhumuni makuu ni kuyaweka sawamapisi ya lugha hii ili wenye lugha yao, Waswahili wa asili wa Pwani ya Afrika Masharikiwasiendelee kunyang'anywa asilimali yao Aidha, kukua, kusambaa na kutumika katikamawanda mapana na makubwa zaidi si hoja ya k:inyang'anyiro kwa Kiswahili kuwa ni lugha yakila mtumiaji, kwani hiyo ingekuwa hoja, Kijarumani, Kijapani, Kif uansa, Kiingereza n k nazopia zingekuwa lugha za kuwaruhusu Wakwere, Wakerewe, Watanzania, Wachina, n k kuwa1Makala kwa ajili ya Kongamano la nane la Kiswahili, Chuo Kikuu cha Bayreuth, tarehe 26/27 mei 1995

114IIGIIJ SHAABAN YUSUF SENGOWajarumani, Wajapani, Waf uansa, Waingereza n k Pia maka1a haya yanatoa maoni kuhususera ya Kiswahi1i katika ne hi zilizotajwa na jinsi wananchi na wasomi wanavyosema juu ya halihii ya ukakafu kuhusu lugha hii muhimu duniani2.1. MapisiHoja inayoingia akilini katika nyingi zilizopata kutolewa ni:(i) Kiswahili ni kizalia cha lugha asilia za Waafrika wakazi wa mwanzo wa Pwani ya Afrika yaMashariki kabla ya majilio ya Wageni(ii) Kipwani hicho ndicho kilichokutwa na Ibn Batutta na kuitwa 'Ki-Sahil", Kingozi, Kishomvi Kipwani kwa lugha ya mgeni huyo wa Kiarabu(iii) Kipwani!Kiswahili hicho, katika kukua kwake, kilipokea wageni na lugha zao na kilitoakwa wageni hao lugha, fasihi na utamaduni wa Kiswahili 2(iv) Wapwani hao wa asili walisambaa pwani yote wakiwa ni wa mataifa mbalimbali yaKiafiika, wengi wakiwa na makwao maharani Afrika(v) Wapwani hao, baada ya majilio ya wageni, walichanganyika, kwa hali zote na wageni waona kuishi pamoja kiutamaduni, kijamii, kisiasa, kiuchumi n k. ingawa kila watu walionekana,kwa macho ya kawaida, watu maalum kama vile Waswahili, Waarabu, Wahindi, Wazungu n k(vi) Kiswahili si lugha ya mchanganyiko wa Kiarabu na lugha za Kiafiika ila Kiar abu kilitumikasana 10Jfb.ndisha Uisla.TUu (Qur'an) lava karne nyingi na kufa.nyia biashara na Waarabu pia kwakame nyingi (Mbaabu 1978:lx-x)Kwa maelezo haya, yatosha kushadidia kuwa hawapo watu ambao Waswahili wenyewewanawaita "Modem Waswahili" kama anavyojaribu kughushi msomi na mtafiti wetu DrJoshua S Madumulla (1989) Yeye anazungumza Kijarumani kwa kiasi kinacholingana kwakaribu na Kiswahili anachokitumia, lakini hajasikika akithubutu kudai kwamba na yeye nimmoja wa watu anaoweza kuwaita "Modem Germans" ambao ni pamoja na Wamakonde waNdonya, Majaluo, Wahausa n w k h ati kwa sababu watu hao nao wanakisema KijarumaniKiswahili na Waswahili anaowazungumzia Bwaa Sengo (1987:182) hawakufanya na walahawajafanya makosa kwa kuwa wakarimu na majirani zao, wageni wao na kwa binadamuwenzi wao Haiwi kwa mtu kuwa mithili ya ngarnia aliyemnyang'anya Mwarabu wake hemalake kwa kukosa moyo na hisia za shukurani Wanyasa walioko Bagamoyo mjini ni Waswahili,wa Pwani na wale waliobaki Malawi ni Waafiika wa Bara kama alivyo Mkwere wa Chalinze nanduguye Mswahili aliyeko :rvLJgotini BagamoyoJambo la ukweli 2 2 4, Mwenyezi Mungu yupo, kila binadamu atakufa, mpingo simpapai n n k h Halihitaji wapambaji wa kisiasa kama kina mwalimu Julius KambarageNyerere, ambao wameiongoza Tanganyika na Tanzania kwa miaka yote kwa kutegemeakuombaomba na bado alidai na hadi Ieo anathubutu kudai kwamba siasa yake ilikuwa ni yaKingozi lugha ya Kaskazini Mashariki mwa Kenya na Kishomvi kilichozungumzwa na watu waBagamoyo · Mzizima, Mrima wa Bandari-Salama hadi Kilwa (Tuli 1985: 11)2

HALl YA KUTATANISHA YA KISWAHILI115"Ujamaa na Kujitegemea" Mwanafunzi wake F EM K Senkoro3 amejikita kwenye matamkoya kedi ya Bwaa mkubwa Nyerere ya kumwita kila mtu Mswahili Anayaona matamko hayokuwa kweli ya kitaaluma kinyume cha utafitizi anaotarajiwa kuwa nao wa kutafuta na kuteteaukweli wa jua na mwezi, ardhi na mbingu, nchi na bahaii Vipi Ieo mwanataaluma Senkoroanathubutu kutuhadaa tukubali kwamba Waethiopia nao huko kwao waliko ni WaswahiliMzee Nyerere ni mwanasiasa aliyetamani kufuatilia nyayo za Kwame Nkrumah za kuunganishaAfiika yote ingawa kwa kuwaua Waswahili wa asili Ama, Nyerere anajua fika kuwa Mzanaki,Mrmi, Msukuma si Mswahili kama vile ilivyo kwamba Mswahili si Mpare, Mkagmu, auMkwereUtetezi wa hoja za kigeni Uswahilini unapatikana pia katika makala ya Bwaa mkubwaKihore (1988) Yeye anakanusha kuwako kwa Waswahili Ieo ati kwa kuwaWatanganyika/Watanzania wote wanakitumia Kiswahili, watoto wa Ki-Bara wanasemaKiswahili badala ya lugha zao za kikwao kama lugha yao ya mama!mwanzo na ati utamaduniwa Kiswahili ni wa kigeni kwa kuwa Uislamu ambao ndio msingi mama wa utamaduni waWaswahili ni Dini ya kigeni Mwanataaluma wa kiwango chake, mradi kathubutu kuuhakikiUislamu, alipaswa ajue kauli ya Mwenyezi Mungu wa watu wote na majini yote,anapowaambia "Nisingewaumba watu na majini ila kwa kuniabudia." (YusufAli 1991:1-2)Uislamu ndio aliozaliwa nao kila mtu na kila kiumbwa Kwengine endako enda kutalii, lakinianapotalii mtalaa wa kweli wa asili yake, mja hurejea katika Dini yake ya haki kwa kukirikupwekeka na kuabudika kwa Mwenyezi Mungu mmoja na kwamba katika mitume,Muhammad ndiye mjumbe wake wa mwishoYatosha kumalizia mjadaia huu wa kuwako ama kutokuwako kwa Waswahili asilia waPwani ya Afiika Mashariki kwa kuwataja wasomi na watafiti wapenda na watetezi wa kweliMmoja ni mar'humu Shihabuddin Chiraghdin (1973) ambaye kaandika sana kuhusu "Kiswahilina Wenyewe" na kuyathibitisha maneno yake kwa ushahidi kamili kiasi cha uwezo wakeProfesa Mugyabuso M. Mulokozi, mtafiti hodari wa Kiswahili, baada ya kuitalii Pwani nakuishi na Wapwani, amekiri ukweli kwa kuutongoa kwamba ni kweli kabisa Waswahiliwenyewe wapo na ni watu na utamaduni wao mbali na ule wa majirani zao wa Mrimani na wandugu zao wa Maharani (Mulokozi & Sengo 1994: 1) Kweli hii ni kweli ya kitaaluma ambayokila mwanataaluma wa kikweli kweli anapaswa kuitetea Mifano ya utatanishi ni pamoja namakala ya SA K Mlacha (1983) ambayo yanazungumzia "Wahusika katika Riwaya zaKiswahili Tanzania" bila ya kuelezea mipaka ya Uswahili wa Riwaya hizo; zipi hasa ni zaKiswahili na zipi hasa ni za Kitanganyika katika maudhui, lugha na fasihi. Uainishi huu nimuhimu katika kuipa kila jarnii haki na hadhi yake "African literature in English" inakubalikakuvva si "English literature 11 ; v je leo, fasihi ya I'Jkerewe isem'.-ve ni FasiPi ya Kiswahili? Lughaya Kiswahili imetumika, na i huru kutumika, kuelezea Fasihi za mataifa yote ya Waafiika Hiyohaina maana kuwa Fasihi zote hizo ni za Kiswahili kwa maana ya Fasihi ya Jamii ya WaswahiliMboni na macho ya akili yamezoezwa kuutaja kila mti kwajina lake - mpingo si mkwaju; hivyoMwimo wake wa kisiasa uliojaa chuki za kimapisi na za kidini, wa kuchupa bila ya kuagana na nyonga,ni wa hatari kitaaluma. Waingereza wenyewe ndio Uingerezani na ni Waingereza wenyewe ndiowanaojuana nani hasa ndiye mahiri mbobezi wa Kiingereza Waswahili wapewe haki yao na Bwaa Senkoroaendelee tu na knishi na kupata jina kwa Kiswahili, hatanyang'anywa utumizi huo kutokana na ukanmu wakiungwana wa Waswahili halisi3

116TIGIII SHAABAN YUSUF SENGOhivyo Riwaya ya Kiswahili (I anzania) katika miaka ya themanini (Madumulla 1988) shurtiisemwe ni ipi kwa misingi ipi na kwa miaka ipi Mwandishi shurti aeleze mwanzoni kabisa kwanini ameamua kumzungumzia simba akitumia jina la nyani Uandishi kama huu humsaidiamsomaji kujua, tangu mwanzoni, kuwa neno nyani au simba au Mswahili limepewa maanamaalumu isiyo ya kawaida katika matumizi ya kila sikuFikira kwamba Kiswahili ni lugha ya Watanzania wote ama Waafrika wote wa Afrika yaMashariki (16) ibakie katika kiwango cha matumizi tu Nchi nyingi duniani zinakitumiaKiingereza kikiwa ni lugha ya taifa, au rasmi, lakini hazithubutu kudai kuwa Wazimbabwe auWamalawi nao ni Waingereza Kama Kiarabu kinaruhusu kumwita kila akisemae Mwarabu(ingawa Waarabu wenyewe hawamkubali Mwarabu huyo bandia), lugha nyengine nyingihazikubali Kila lugha na wenye2.2. Kukua na kusambaaKiswahili, Kipwani, Kiafrika kilizaliwa katika eneo la Pwani ya Afrika ya Mashariki katika sikuza majilio ya watu wa mwanzo mwanzo ambao wamejikuta pamoja Pwani kwenye mavuvi, namisafara ya hatari baharini, kadhalika nchi kavu kwenye makulima, kharusi, maziko na matangan k Mtu kaumbwa azungumze na wenziwe Hivyo si suala kwamba watu hao hawakuwa nalugha. Jarnii yoyote ya watu lazima iwe na lugha yake Wapwani ni watu wa mataifa mbalimbaliwaliokuwa na lugha zao mbalimbali Kwa mfanano wa lugha hizo na tamaduni hizo, ikawawepesi kupata lugha ya masikilizano ya pamoja Wageni walipofika Pwani, walipokewa nakuhudumiwa na watu waliokuwa na lugha yao na utamaduni uliokamilika wa uongozi nautawala n k (Ibn Batutta n. d )Kila kinachozalika kina mawili, ama kufa na kusahaulika utotoni ama hukua na kunawirihadi ukubwani Kiswahili kilipata bahati ya kupendwa, hivyo kilipaliliwa na kila aliyekutananacho, tangu siku hizo za kuwapokea wageni hadi kufikia kiwango cha lugha hiyo kuifundishaQur'an yote katika Vyuo vyote vya upwa wa pwani ya Afiika Mashariki Ni jambo la wazikwamba Uislamu ulihusishwa sana na Kiswahili kwa karne zote hadi hii Ieo Utatanishi wakuyaondosha kwa makusudi maneno ya "Kiarabu" kwenye "Kitaifa" (Kitanganyika auKikenya) kinachoitwa Kiswahili Sanifu unatokana na mapisi, siasa hadi chuki za kidiniW arnisionari na Magavana wa kikoloni walijitahidi sana kukipiga vita Kiswahili kwa sababu zaDini, Uchumi na Fakhari lakini mwishowe walilazimika wao wenyewe kuamua kukitumia, siyotu kwa masuala ya biashara bali hata kufundishia InjiliSababu nyengine zilizokiHm.ya Kiswahili kikue na kusambaa :ri pam ja na (i) Majilio yawageni; (ii) kutoka kwa Waswahili kwenda nchi za majirani zao na za rnbali; (iii) Biashara; (iv)Misafara ya kitalii kwa wageni waliosindikizwa maharani; (v) Utawala wa Kifalme wa Waarabumwanzoni na baadaye; (vi) Utawala wa Kijarumani (na/au wa Kidachi kama wazee wengiwanavyoutaja hadi Ieo) Wajarumani ndio waliokuwa wageni wa mwanzo kukienzi Kiswahilikwa kukifunza kwa watu wote waliokuwa wakienda Afiika ya Mashariki ya Kidachi kwautumishi mbalimbali Aidha, Wajarumani waliamua kuwatumia Maakida katika kazi zaUtawala, uongozi, kanisa, Elimu na Biashara; (vii) Utawala wa Kiingereza ingawa ulikuwa nasera za utatanishi; (viii) Vita; (ix) Harakati za kupigania uhuru kuanzia Vita vya Maji Maji, vitadhidi ya Abushiri; (x) Vyama vya siasa kuanzia TAA; (xi) Vyama vya michezo na burudani

HALl YA KUTATANISHA YA KISWAHILI117kama vile Young African Sports Club, Egyptian Music Club, Sundeiland n.k; (xii) Pilikapilikaza uhuru na jitihada za makusudi za Viongozi kama vile J K Nyerere ingawa kwa miaka mingiyeye alikiona "Kiingereza kuwa ndicho Kiswahili cha Dunia", 4 na Rashidi Kawawa, na kablayao Abeid Amani Karume n w ; (xiii) Elimu ya Biblia Kanisani na baadaye Elimu ya Msingi,Stadi za kazi na za kiufundi - zote zilitolewa kwa Kiswahili. Leo, Elimu ya Juu inajadiliwa kwaKiswahili ingawa inafundishwa kwa "Kiingereza cha Kiswahili " Elimu ya 1 iba inatolewa kwaKiswahili; (xiv) "Natural Beauty and Love" - Mapenzi ya uzuri wa kimaumbile yamekipitishaKiswahili katika vihunzi mbalimbali na kukisambaza duniani kote Titi la mama li tamu hatalikiwa la m-bwa Karibu Vyuo Vikuu vyote vya Dunia vina idaJa au wasomi wanaokisema,kukiandika, kukichambua katika taaluma zao za lughawiyati na fasihi au sanaajadiiya yaWaswahili Wasomi wengi wameandika tasnifu zao na kupata PhD zao Vyama vya Kiswahilivimezagaa kuanzia Afrika, U1aya, Marekani hadi Mashaiiki ya mbali. Pongezi KiswahiliKongole Kiswahili Hongera Kiswahili I2.3. SemBaada ya kushindwa kwa jitihada za kuzuia lugha ya Kiswahili kukua na kusambaa, Serikali yaKiingereza ilitumia mbinu ya kukibadili Kiswahili kwa kuwatumia wataalamu wageni kuanzakutunga lugha mpya ambayo Ieo inaitwa "Kiswahili cha Shuleni au Kiswahili Sanifu", 5 tafautikwa masafa mapana na lugha mama asilia ya Waswahili (Wangozi na Washomvi) na Kingozi 6na Kishomvi chao Mbinu hii ndiyo iliyokifanya Kiswahili kiendelee kusimamiwa nakuendeshwa na wageni au ugeni (kama vile Idara karibu zote za Kiswahili, kwenye Shule,Vyuo vya Ualimu, Vyuo Vikuu; kadhalika Wahariri wa magazeti ya Kiswahili, Mwengoya,Runinga na Pataninga, Asasi za lugha hii kama vile BAKIT A, IUKI, n n kote Afrika yaMashariki zimeshikwa na wageni wa eneo la upwa wa Pwani) Asasi kama vile BAKIZA,TAKILUKI za Zanzibar na Baraza la Kiswahili la Kenya lililoko Mombasa, vyaendeshwa kwamisingi ya kigeni Kanuni za lughawiyati na za kifasihi na hata zile za sanaajadiiya kwa wenyekuimaizi taaluma hiyo, ni zile za lugha kama vile Kiingereza, Kifaransa na kidogo sana lughanyengine kama vile Kireno, Kibelgiji, Kijammani, Kishambaa, Kinyamwezi n k4Julius K. Nyerere ni mturniaji mzuri sana wa Kiswahili katika mazungumzo, utnnzi na uandishi lakinikwenye Sera, kachangia sana kuiflflsha na kuifuja hadi kniflkisha kwenye utatanishi uliopo sana. Kenya,mwenziwe ni Bwana Njonjo ambaye kwa siku zake hakumwamini 111iombaake, mamaake au babaakeMwafrika kuendesha ndege ambayo yeye angeisaflria5 Pera Ridhiwani katika mahojiano baina ya I S.Y Sengo na yeye 23/03/1995: "Ndio, kiko Kiswahili chaShulerj na KiswaJ jJi cha Uswahilini Kiswahili cha Shuleni ni !ugha iliyopangwa yenye kufuata sheria zaona Kiswahili cha Waswahili ni vile walivyokikuta toka kwa wazazi wao Neno "Sanifu" maana yake ni"Kutunga" Hivyo, ukisema Kiswahili Sanifu ni Kiswahili kilichotnngwa na watu, na inawezekana kuwahivyo kwa sababu maneno mengi ya Kamusi hayaeleweki " (Kurasa 1-2 kidadisi)6Ahmed Sheikh Nabhany Kandi ya Kiswahili Mss wenye siia nyingi za uasili wa utaflti na ushahidi waasili ya Kiswahili (kwamba kweli ni lugha ya kingozi-Kiafrika) . kabila la Waswahili wenye mila nadesturi zao jina lao la asili ni Wangozi na lugha yao ni Kingozi Mfano wa maneno: Ngeu au mweni nidamu (dam ya Kiarabu); Ng'andu ni dhahabu (dhahab ya Kiarabu); Matayo ni lawama (lawa-mah yaKiarabu); Mapisi ni historia (Kiingereza) au tareikh (Kiarabu), sehemu za mwili zote ni Kiswahili cha asrhkitupu (utosi, kichwa, nyele, maeneleo ya nyele, uso, nahi, kope, Puwa, Jicho-Mboni, Miyomo, kidevu,kishogo, sikiyo, ndewe, shingo, taya, kidaka tonge, koo, mtulinga, kidari, bubu au titi, kifuwa, mkono, kiwiau kisukusuku, tumbo, kitovu, kinno, mkono, boti, kiwiko, zanda au vidole, kiweo au paja, mtoki, nndo augoti, tafu, mundi, ito la guu, kisigino, wayo/nyayo) Wapenzi wa Kiswahili wanaombwa kuchangia kwa halina mali gharama za kuutoa mss huu kitabu (kama US 5000 tu)

118TIGITI SHAABAN YUSUF SENGONadharia ya "Ndani - Nnje" badala ya "Nnje - Ndani" (Sengo 1985) ndiyo inayofaa kutafitiakweli ya watu na lugha yao ama ya lugha na watu wake Haimkiniki kuturnia kanuni zaKishambala kwa kupatia kweli halisi za lugha ya Kiswahili Ni muhali Rata lugha nazo zinanyago zakeHivyo katika rniaka ya 1920 Gavana wa Tanganyika, Sir Donald Cameroon aliitisha kikaocha wataalamu wa lugha Dar es Salaam kutoka Uganda, Kenya na Tanganyika Kikaokilielekezwa kichague lugha moja ya Kiafrika ambayo kwa kedi ya kitaalamu ilianza kuitwalugha ya "Ki-Bantu" Miaka ya 1925 - 1930 ilishuhudia juhudi hizo za kuunda au kutungaKiswahili Sanifu Ndipo ikapatikana Kamati ya kusanifu Kiswahili ambayo iliamkuliwa "TheIntertenitorial Language (Swahili) Cornittee " Kamusi za Kiingereza - Kiswahili na Kiswahili Kiingereza za Frederick Johnson (1939),7 Kiswahili Sanifu kutokana na Ki-Unguja cha mjini(lugha ambayo kwa wakati huo ilipwaya kimapisi, kimashiko na kiutamaduni ikilinganishwa nanduguze wa Kaskazini na Kusini kama vile Kiamu, Kipate, Kimvita, Kimtang'ata hata Kimrimacha "Bwaga-moyo wako", "Bagamo-umoyo" na Pangani, Mafia na Kilwa ama Kishomvi chaKunduchi Bandari ya Salama Ni dhahiri kwamba uteuzi wa lugha hiyo changa ulikuwa nasababu za uwepesi kwa wataalamu wa kigeni na kwa athari ya vizazi na vizazi vya baadayekwa wenye lugha kutokana na utohozi wa utajiri mkubwa wa ndirni za Kiswahili zilizoachwanyuma "Bandagala ng'onyo!"Wizara ya Maendeleo ya Jarnii, Utamaduni, Vijana na Michezo, mwezi Juni 1988ilipendekeza sera yenye madhumuni ya (i) kuainisha lugha zinazoturnika katika nchi yetu nakufafanua nafasi, hadhi na mipaka ya maturnizi ya lugha hizo katika jarnii ya Watanzania; (ii)maturnizi yake ili iwe ni chombo halisi cha kuleta umoja, ukombozi na maendeleo ya kisasakatika Taifa; (iii) Kutoa mwongozo ulio wazi kwa Taifa na vyombo vyote vinavyohusika nalugha kuhusu rnipango ya lugha hapa nchini, malengo yake na namna ya kuyafikiaJe, kuna utatanishi gani katika madhumuni ya Wizara mama hii kwa ne hi yoyoteinayotharnini watu wake na tamaduni zao ? Wizara, tangu Uhuru, 9 Desemba 1961,ilibadilishiwa jina mara kadha wa kadha ili isiwe na mashiko ya kulielekeza taifa kwa kwendaMaendeleo ya jarnii kwa maana ya kumbadilishia hali yake Mtanzania wa kawaida binafsisijayaona Utamaduni umepewa maana ya ngoma, mpira wa rniguu, ujana, starehe na asasi zakuvunjia uadilifu wa Mwafrika Hivyo, vijana na rnichezo ndio vitu vilivyotiliwa nguvu na siyolugha, uadilifu, juhudi na mapenzi ya kazi, adabu, amani, dini n k Majumba ya MaendeleoTanganyika, kwa muda mrefu, yaliashiria ulevi, uasherati, starehe chafu chafu na njia yakughusbi vipato vya haraka haraka vinavyotoka11a na kazi har amu(i) Lugha za Afrika Mashariki za Kiasili ziko nyingi Kila watu wana yao Lugha za kigeni naHizi za kigeni hazihitajiKiarabu, Kiingereza, Kidachi au Kijarumani, Kireno n n. ckuainishwa Kila moja ina kazi yake kihistoria, kielimu, kidiplomasia, kibiashara n kTanganyika peke yake ina lugha zaidi ya 130 Si ajabu zikafikia 250 kwa Afrika Mashariki hadiIeo hii; Kipare, Kisukuma, Kihehe, Kizaramo, Kijaluo, Ki-Baganda, n k - Lugha hizi7Krapf, Madan and Steere na wenzao wamefanya kazi kubwa katika kukikuza na kukisambaza Kiswahili,kazi ambazo hazipaswi kupuuzwa wala kusahaulika. Athari zao za Kizungu zilzoleta "Kiswahili-Kizungu"ni suala mbali la majadiliano Mcheza kwao hutuzwa

HALl YA KUTATANISHA YA KISWA HILI119Kwa nini? "Hatutakizinafundishwa Ulaya, Marekani, Mashaiiki ya mbali kama vile Japankyusa wamejazanaukabila?" Makabila je? Hayapo. Wasukuma je? Aa Aee ! Mbona Wanyatu? Aa Ae ! MbonaBenki ya 1aifa ya Biashara? Aa, Ae I Mbona Jeshini kumejaa akina fulaniwanaosoma ni watu wa makabila na imani fulani tu? Aa Ae!izi ya lugha hizoNi dhahiri kuwa lengo la 1988 si la kuainisha lugha wala kufafanua matumau I aasisi ya lugha nabali ni kukanganya na kuzidi kutatanisha wananchi Kiko wapi Chuoriki ambapo utafitiTamaduni za Tanganyika, Tanzania, Kenya, Uganda, Afiika ya Mashaya Mashariki na jamiiungefanywa, watu wangejifunza, vitabu kumechapishwa na Afrikakidini Leo 1995 watunyengine kunufaika? Badala yake kukakuzwa chuki za kikabila na zaua Viongozi kutokanawanazungumzia uzawa, wahubiri wanelekeza watu wa imani zao kuchagMuingilikani, je, Mchana ucha- Mungu. Kama Mwingereza alimwiita pagan i kila asiyekuwaaMungu kwa Mwingereza atakuwa Mwiislamu, Mroma au Mluteri? Hapanuwanja wake Labda(ii) Kiswahili, 1 anzania, kilikuwa hakihitaji kukuzwa wala kupanuliwaeusi" ilitawala Nikwa Kenya na Uganda, ambako Kiingereza na kasumba ya "Wazungu-Wmadhumuni ya kukifimyautatanishi mkubwa sana wa kisera kuihusisha lugha ya Kiswahili naya kisasa katika Taifa laKiswahili chombo halisi cha kuleta umoja, ukombozi na maendeleowaliwa na Waswidi naTanzania 1988 Kweli akutukanae hakuchagulii tusi Finland iliyotakuwa mtumwa wabaadaye Warusi kwa takribani karne moja kwa kila dola, iliamua haitakiifanya kwa lugha yaonchi nyengine kwa masuala ya lugha na tamaduni. Kila kitu chao wanaka Kiswahili HatariSisi Watanzania 1988, tunaazimia kufafanua haja na umuhimu wa kukuzkubwa sana hii!mwendo umekuwa wa(iii) Juu ya mwongozo wazi na mipango ya lugha nchini,4 ya sera (Serikali yakisengerenyuma, kwenda twendao lakini kufika, hatufiki Sura yaTanzania 1988) ilijaribu kupendekeza yafuatayo:a) Kiswahili kupewa hadhi kamili;b) Kiswahili kikuzwe katika hali zote;Utamaduni wa Taifa;c) Lugha za asili (za makabila) zikuzwe kwa madhumuni ya kuhifadhid) F asihi na Sanaajadiiya ishughulikiwe;e) Machapisho yato!ewe kwa wingi na yasambazwe kwingi;f) Kiswahili kitumike katika kumbi za Kimataifa;Vyuog) Kiswahili kianze kutumika 1993 kufundishia masomo yote Upili nakarnili kitaifa KiswahiliHadi Ieo hii, Kiswahili hakijapata hadhi yake achilia mbali hadhina kukiendeleza hasalr.inakuzwa na watafutaji kazi lakini wenye uwezo wa kukikuzaia kama kuna asasiwananyimwa nafasi Lugha za asili bado zinajikongoja zenyewe, sijasikga wa madogori nayoyote ya kuzifundisha ama kuzifanyia utafiti rasmi Wana-ushirika, waganu nzima kwenye Vyuowaghushi wengi tu wamejitia katika uwanja na Ieo ni Maprofesa chunghakupitishwa kwenyeVikuu vya Afiika ya Mashariki; wa F asihi, Sanaajadiiya (hata kama mtuluglia, taaluma naunyago huu) mradi ana jina linaloelekea Uprofesa Ni utatanishi katikabobezi lililotopea katikamaisha kwa ujumla Profesa ni mtu wa hadhi, ni mtu wa umri, nika vitabu vingi vyaketaaluma yake; kagundua vitu na mambo, nadharia na misingi, kaandimambo na watu Leo hiimwenyewe, si mzushi wala mghushi, si mcheza shere wala fatani wanenda salama" atarudituna Maprofesa wa Kiswahili wakiambwa "karibu" kwa maana ya "haya

120TIGITI SHAABAN YUSUF SENGOaketi kitako na akenda, ataaga, "ninaharakia kukamata basi " Si utatanishi huu? Machapishoyatolewayo hivi Ieo ni ya mjomba kwa shangazi, hayapimi taaluma, yanapima kaandika naniHivyo, hata yakitolewa mengi na kusambazwa kwingi, bado hayatusaidia kwani yatakuwayanamsaidia mama wa kambo aliyemficha binti aliyestahiki kuolewa na Mfa1me kwa kutakaao1ewe binti aliyemzaa yeye Mwishowe, mwenye haki ana haki, binti wa kambo kaolewa nabinti wa mama kaishia kupunguzwa wayo ili uenee kwenye kiatu cha kumtafuta mwenyeweBatili haikai mbele ya hakiKiswahili hadi Ieo hakijafika kutumika kwenye kumbi za kitaifa Mfano Chuo Kikuu chaDar es Salaam, lugha ya wanataaluma ni Kiingereza cha kujiumauma na kujikosesha raha nauhuru wa kucheka na kuchekelea, kujimwayamwaya kwa Kiswahili ambacho wengi waowanakiweza zaidi kuliko hicho Kiingereza kinachowalazimisha kukenuliana meno badala yakuchekeana Mbali ya Chuo Kikuu Huria cha I anzania, Kiswahili hakijakaribishwa kwenyeShule za Upili, Vyuo, Vyuo Vikuu na azma ya kuanza kukitumia kufundishia masomo yote1993 inaelekea haipo tena Kwa nini?(i) "Lugha ya I aifa" ni jina la kisiasa, halikuwa na halina ufuatiliaji na wanasiasa viongoziwenye uwezo wa maamuzi(ii) Hakujawa na malengo thabiti kwa muda maalumu wala kauli thabiti na za wazi mbali yapropaganda na uchezaji shere tu(iii) Kutetea Kiingereza kama kushughulikia Ukimwi ni mr adi wa kujinufaisha Kielimu, kilamtu mwenye nayo anakubali kuwa, lugha ya kufundishia chochote kiwacho ni ile lughainayofaharnika vizuri sana na wanafunzi, walimu na jamii Kiingereza, Afiika ya Mashariki nilugha ngeni, ina dhana nyingi, mbinu zake ngeni na pia walimu wageni ama kutoka Uingerezawasiojua na kuthamini Uafrika ama Wazungu-Weusi walioiva kikasumba kucheza Waltz(Hussein 1971 :8) kijijini kwao Kudimoze-Mdaula Bagamoyo au Mbale Uganda au KisiwaniPate Kenya Je, si utatanishi huu? Vipi Mwingereza huyu anayesemwa kazuia biashara yaWatumwa 1873 katika Bahara ya Hindi (ingawa tunasikia hadi Ieo watumwa wangalikoMarikani ya Kusini na kati!) Ieo hii amuachie Afisa au Kiongozi au kikundi cha viongozi kuuzanchi zao na kuuza watu wao kwa Karnisheni ya kupendelea Kiingereza na siyo lugha mama yaTanzania, Kenya, Uganda, Zimbabwe, Malawi, Nigeria, n n? Je, Waingereza Ieo hawajui kuwahakuna nchi yoyote Ulaya inayotumia Kiingereza kama lugha mama isipokuwa Uingerezayenyewe Scotland na Ireland ambazo zote ni nchi moja hiyo hiyo? Kwa nini wamkubalieMwafrika aliyelala kwa kujidanganya kuwa atajua Sayansi na 1 ekinolojia ya kisasa kwaKiingereza? Wajarumani, Waswidi, Wadachi, Wajapani, Wamalei n w k h wanawezajekuendelea kisayansi na kitekonolojia k-wa lugha zao wenyewe? Je, huu si utatanishi? Amakweli, alalaye usimwamshe, ukimwamsha utalala wewelKitambo cha 1994/95 wanaasasi za Kiswahili waliitana ili kasisi "Siku ya Kiswahili", siku yakiutamaduni ya kuienzi lugha ya Kiswahili na utamaduni wake. Mara hii ya mwanzoalikusudiwa Shaaban Robert, aenziwe kwa kazi yake kubwa aliyoifimya ya kukiendelezaKiswahili na taaluma zake Utatanishi uliotokea ni wa kutokubaliana juu ya dhana yenyewe yaSiku ya Kiswahili, Kiswahili na "Waswahili A,B, C "wa kupewa zawadi kutoka kote Afiikaya Mashariki na wapigaji upatu kutoka kote duniani Nani kapata zawadi, zawadi gani, kwanini, haijafahamika kwa wengi wetu hadi Ieo Je, si utatanishi huo?'

HALl YA KUIATANISHA YA KISWAHILI1212.3 Maoni ya JumlaWatanganyika wengi watokao juu ya Mrima wana haki ya kudai kuwa Kiswahili ni lugha yaokwa kuwa wameitumia kwa miaka mingi Wengine, kwa kuwa watoto wao hawazijui tenalugha zao za asili Wengine, wamejiuza katika tamaduni za miji kwa kuzungumza na kuishikimji Swali la msingi la kujiuliza ni: Kunani Uswahilini hata sote sisi tudai kunatuhusu Ieo hiiwakati kwenye miaka ya 1960 (kwa Tanganyika), 1970 (kwa Kenya), ya 1990 (kwa Uganda),tulikipuuza na kukitukana Kiswahili?Leo, Wasudani wakidai Uarabu kwa kukitumia Kiarabu, kesho Wazaire wakiamua,wakijifunza na kukitumia Kiarabu vizuri, pengine vizuri zaidi kuliko Wasudani, watakubalikakuwa ni Waarabu na wao? Rwanda, kabla ya vita, ilikazania sana kukisambaza KiswahiliKitanganyika ambacho kingegeuka kuwa Kiswahili-Kinyaruanda Je, nao wangeweza kudaiKiswahili ni chao? Sisi watu wa Afiika ya Mashariki tunatumia sana Kiingereza, tulipata kuotandoto ya kudai kuwa tu Waingereza siku moja?Ni wazi kwamba Kiswalrili-Kiswahili ni cha Wapwani wenyewe, ndio wakizungumzao kiwena athari za Kiarabu au za Kiingereza, kila lugha ina athari zake Wasomaji na watumiaji waKiingereza, si sote tuhusikianao na kanisa la lugha hiyo, na bado hatujasema tuyatohoe manenoyote ya Biblia yaliyomo kwenye lugha na utamaduni huo Kiswahili cha Waswahili hakinanarnna ya kukwepa maneno ya Kiarabu (yatokanayo na Qur'an na mawasiliano ya kibiashara yakarne nyingi za kusafiriana huku na huko na Waarabu, Wahindi na watu wa Mashariki yambali Athari zitajipunguza zenyewe na hasa kwa marejezi ya lugha hiyo Uswahilini kwenyeweambako kina Mufti Nabhany, Pera, Ridhiwani, Maulid Moh'd Omar, Hamisi Akida na wenginekama hao, wanayajua maneno mengi ya asili ambayo Ieo yamenyang'anywa nafasi na lugha zakigeniMkanganyiko na utatanishi huu umepata wasaa mzuri wa kujadiliwa na Dkt Z S Mochiwakatika makala yake, "Kiswahili Sanifu: Fasili na Vidokezo vyake" (1986) ambamo:(i) Kiswahili kimepewa nafasi na hadhi yake ya mwanzo na ya asili kuwa ni lughainayozungumzwa katika upwa wa Afrika ya Mashariki Waswahili ni wazungumzaji wa lughahiyo na ni wanakikoa wa utamaduni huo(ii) Kiswahili Sanifu au Kiserikali kimepewa nafasi yake Hapa sharti tuongezee fikira za lughahizi za Kiserikali Tusipojihadhari tutakuwa na "Vi-Serikali" vingi: Ki-Kenya, Ki-Uganda, KiNa tukichanganya chuki zetu za Kiarabu naRwanda, Ki-Burundi, Ki-Ianganyika, n kUarabu lakini tukashikilia upendeleo wetu wa Kizungu na Uzungu, ni wazi kwamba Kiserikalicha kila nchi kitakuwa ni Kiswahili cha aina yake mbali na Kiswahili-Kiswahili ambacho kipona hakina chuki wala upendeleo kwani lugha siku zote ni chombo cha kutumiwa na wote(iii) Ili Kiswahili Sanifu kiendelee kuwa karibu na Kiswahili-Kiswahili, utafiti wa Viswahili vyaPwani ni aula, wataalamu wazawa waachiwe kazi yao hiyo ya kukiendeleza Kiswahili nautamaduni wao bila ya chuki wala upendeleo wa makusudi Lugha zote zinakuzwa nawenyewe, kwa nini Kiswahili kiendelezwe na Wakwere, Wapare, Wanyamwezi, Wahaya,Wakerewe, Wazungu? Kwa nini? Kwa nini hii si ya lawama, ni kwa nini ya kweli Mchaggaanaweza kushiriki katika Idara ya Kichina Chuo Kikuu cha Beijing, lakini ni kweli aliyejifunzaKichina atamshinda Professa wa Kichina Mchina kwa hali zote za taaluma ya Kichina? Mbona,

122IIGITI SHAABAN YUSUF SENGOMwafiika kashindwa kumuiga Mwingereza kukenua meno? Kwa sababu yeye kazoea kuchekabadala ya kukenea meno tu Na lugha yoyote ina siri nyingi ambazo mwenye kujifunza hazipatizote Hivyo Wasanifu wa lugha wakiwa wenye lugha, hawatakuwa wanatungatunga tu manenomapya ambayo hayana msingi kabisa na Kiswahili-Kiswahili kwani kunga na mizungu yotewanayo, si wasungo nayo mambo hayo(iv) Wazawa wa lugha hawaleti khitilafu kwa kung'ang'ania taratibu zao za usemajikwenye maandishi Kama Kiswahili k:inaandikwa kama kinavyotamkwa, kifimyweHaiwezekani bwa ya ku-bwa iwe ni bwa lakini bwa ya mbwa isemwe ni MBWA kwakanuni za k:igeni za lughawiyati zinalazirnisha hivyo Haikubaliki thatha badala ya sasa,badala yajamani na kama hayo hasa katika mazingir a ya U swahilinimpakahivyosababujemeni(v) Dkt. Mochiwa ni jirani ya Waswahili Atufimyie utafiti zaidi kuhusu Ki-Unguja hichoanachokisema ni cha kame ya kurni na tisa na cha h

kwa wageni hao lugha, fasihi na utamaduni wa Kiswahili 2 (iv) Wapwani hao wa asili walisambaa pwani yote wakiwa ni wa mataifa mbalimbali ya Kiafiika, wengi wakiwa na makwao maharani Afrika (v) Wapwani hao, baada ya majilio ya wageni, walichanganyika,

Related Documents:

Kiswahili dialects are endangered by, among other factors, the onslaught of standard Kiswahili, English, and Sheng, and so they are likely to be dying. The paper holds the position that the Kiswahili dialects are vital for the development of standard Kiswahili and, therefore, their endangerment is the endangerment of standard Kiswahili.

Introduction to Kiswahili Poetry KSX 2102 Kiswahili Oral Literature KSX 2104 (with Mr Innocent Yerindabo) Introduction to Kiswahili Novels KSX 2202 History and Development of Kiswahili KSX 3101 Kiswahili Teaching Methods KSX 3201 Drafts Reviewed: Advanced Proficiency in Kiswahili KSX 1102 by Boaz Mutungi.

Song as an aspect of Kiswahili poetry. Origin and development of modern Kiswahili classics such as taarab. Leading founders of Kiswahili popular song in East Africa, history and development of Kiswahili solo, choral and orchestra composition. Themes, style and language use in popular Kiswahili songs.

Kiswahili) na Shahada ya Umahiri/Uzamili ya Sanaa katika Kiswahili (MA. Kiswahili – akitamilikia Fasihi) zote kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania. Chuoni anafundisha kozi za Kiswahili - Lugha, Isimu na Fasihi ikiwemo kozi ya Uandishi wa Kubuni. Pia, hufundisha Kiswahili

4.0 KISWAHILI (102) 4.1 MATOKEO YA MTIHANI WA SOMO LA KISWAHILI Jedwali hili linaonyesha matokeo ya mtihani wa somo la Kiswahili katika muda wa miaka minne (2005 hadi 2008). Jedwali 6: Matokeo ya mtihani wa Kiswahili (2005 - 2008) Mwaka Karatasi Watahiniwa Alama ya Juu Alama ya Wastani Alama ya Tanganisho 2005 1 2 3 Jumla 259,301 40 80

AKS 301: Kiswahili Structure AKS 302: Theories of Literary Criticism AKS 303: Contemporary Kiswahili Novel and Play AKS 400: Sociolinguistics AKS 401: Second Language Learning AKS 402: Kiswahili Poetry AKS 403: Oral Literature in Kiswahili History AHT 102: Introduction to Political Science AHT 200: A History of Kenya AHT 201: Themes in African

Mchango wa Fasihi ya Kiswahili katika Kuudumisha Utambulisho wa Kiswahili : Mifano Kutoka Kazi za Fasihi za Kiswahili Dk. Wael Nabil Ibrahim Othman* Abstract This study emphasizes that the Swahili literature has a very big role in consolidating and maintaining Swahili identity. In the field of Swahili poetry

ASTM International, 100 Barr Harbor Drive, P.O. Box C700, West Conshohocken, PA 19428-2959. . Second Revision No. 2-NFPA 501-2016 [ Section No. D.1.2.2 ] D.1.2.2ASTM PublicationPublications. ASTM International, 100 Barr Harbor Drive, P.O. Box C700, West Conshohocken, PA 19428-2959. ASTM E903, Standard Test Method for Solar Absorptance, Reflectance, and Transmittance of Materials Using .