Hata Swali La Kwamba “lugha Ni Nini ” Siyo

2y ago
118 Views
5 Downloads
413.27 KB
14 Pages
Last View : 21d ago
Last Download : 3m ago
Upload by : Mariam Herr
Transcription

Chuo Kikuu (cha) Mzumbe (Mzumbe University)KSW101: Utangulizi wa Lugha na Isimu (Mwaka wa Kwanza 2012/2013)Mhadhiri: Mr. Simile, O.E-mail: osimile@gmail.comCHUO KIKUU (CHA) MZUMBE (MZUMBE UNIVERSITY)KITIVO CHA SAYANSI ZA JAMIIKSW 101: UTANGULIZI WA LUGHA NA ISIMUMuhadhara wa kwanza1.0.Lugha ni nini?Mtu anapouliza swali hili (Lugha ni nini?) inaweza kuonekana kana kwamba ni swali la kijinga.Labda kwa sababu huwa hatupendi kutilia maanani katika vitu ambavyo tunadhani ni vyakawaida. Kwa bahati mambo hayapo kama tunavyoweza kuyaona au kuyatafakari. Kwa maanahiyo basi, hata swali la kwamba “lugha ni nini?” siyo rahisi na wala siyo la kawaida kamaambavyo tunaweza kulichukulia. Kwa maelezo hayo tunaweza kufasili dhana ya lugha kwamitazamo miwili: Mtazamo finyu (narrow conception) na Mtazamo mpana (Broad conception).1.1.Mtazamo Finyu:i.Lugha ni chombo cha mawasilianoKuitazama lugha kama tu chombo cha mawasiliano kunawezesha ufahamu wa kawaida. Kwamaana hiyo, bado kuna taarifa muhimu zinakosekana katika fasili na hii inatupatia mapungufu yafuatayo: kwanza, kueleza lugha kama chombo cha mawasiliano ni kueleza kazi ya lugha na siolugha yenyewe. Pili, kama mtu atapiga ngoma ili kuwaita watu na watu wakaja basi milio yangoma itakuwa ni lugha. Na kwamaana hiyo kila kitakacho wawezesha watu kuwasilianakitakuwa ni lugha. Kama lugha ni chombo tu cha mawasiliano, maana yake hakuna tofautiyoyote kati ya kuzungumza na milio mbali mbali kama honi ya gari, filimbi ya refa uwanjani, aukengere ya kanisani au hata sauti inayotokana na kugonga mlango wakati mtu anabisha hodi.Hivyo jambo hili sio la kweli na linatupeleka mbali zaidi na kutufanya tuanze kuitazama fasili yalugha kwa mtazamo mwingine zaidi – mtazamo mpana.1.2.Mtazamo Mpana.Katika mtazamo huu kunawanaisimu wengi ambao wamejaribu kutoa fasili zao mbali mbali.Baadhi ya fasili hizo ni kama zifuatazo:i.ii.iii.iv.Todd (1987) anasema lugha ni mfumo wa ishara ambazo kwazo watu huwasiliana.Kamusi ya Isimu na lugha (1990) inaeleza kuwa lugha ni mfumo wa sauti nasibuzinazotumiwa na watu wa jamii wenye utamaduni unaofanana ili kuwasiliana.”Cook,1969:12 anaeleza kuwa lugha ni mfumo wa sauti nasibu na ishara za kisarufiambazo kwazo watu wa jamii Fulani ya lugha huwasiliana na kupokezana utamafuniwao.Bloch and Trager (1942): “A language is a system of arbitrary vocal symbols bymeans of which a social gorup co-operates”.1

Chuo Kikuu (cha) Mzumbe (Mzumbe University)KSW101: Utangulizi wa Lugha na Isimu (Mwaka wa Kwanza 2012/2013)Mhadhiri: Mr. Simile, O.E-mail: osimile@gmail.comv.vi.[“Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu ambazo kwazo makundi ya kijamiihushirikiana”]Noam Chomsky(1957): “Language is a set of finite number sentences, each finitein lingth and constructed out of a finite set of elements”[“Lugha ni seti ya idadi ya sentensi zinazojitosheleza, kila idadi inajitosheleza kwaurefu na hujengwa kutokana na seti za elementi zinazo jitosheleza”.]Michael Halliday (2003): “A language is a system of meaning- a semiotic system”[“Lugha ni mfumo wa maana – yaani mfumo wa ishara (semiotic system)”]vii.Muharrem Ergin(1990): “Language is a natural means to enable communicationamong people, a living entity that it has its own peculiar laws, by means of whichalone can it develop, a system of contracts whose foundation was laid in timesunknown, and a social institution interwoven with sounds”.[“Lugha ni njia ya asili ya kuwezesha mawasiliano miongoni mwa watu, ni chombohai yaani chenye sheria zake za pekee ambazo kwazo peke yake hujijenga, ni mfumowa makubaliano ambao misingi yake iliwekwa katika wakati usiojulikana, na nitaasisi ya kijamii ambayo imechangamana na sauti.]Language: “The system of arbitrary vocal symbols we use to encode our experienceof the world”[Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu ambazo tunazitumia kusimba uelewa na uzoefuwetu wa ulimwengu.]ix.Nae Sapir (1921:7) anasema: “Language is a purely human and non-instinctivemethod of communicating ideas, emotions and desires by means of voluntarilyproduced symbols.”[Lugha ni njia ya mawasiliano ambayo ni maalumu kwa mwanadamu na isiyo silikaambayo hutumiwa kuwasilisha mawazo, hisia na matakwa kwa kutumia isharaambazo hutolewa kwa hiyali].x.Mario Pei & Frank Gaynor (1954) Kamusi ya Isimu (A Dictionary of Linguistics)anasema: Language is a system of communication by sound, i.e., through the organsof speech and hearing, among human beings of a certain group or community, usingvocal symbols possessing arbitrary conventional meanings.[Lugha ni mfumo wa mawasiliano kwa njia ya sauti, yaani, kwakutumia alasauti nakusikia, miongoni mwa binadamu wa kundi fulani au jumuiya kwa kutumia isharasauti ambazo maana zake hueleweka kwa unasibu tu.2.0.Tathmini ya Fasili za LughaUkichunguza fasili hizi na nyingine nyingi ambazo hazijatolewa hapa utagundua kuwa swali letutuliloliuliza hapo mwanzo yaai “Lugha ni nini?” sio swali la kijinga wala sio swali rahisikulijibu. Hivyo basi, kutokana na fasili hizo tunaweza kusema kuna maana mbali mbali za lughaviii.2

Chuo Kikuu (cha) Mzumbe (Mzumbe University)KSW101: Utangulizi wa Lugha na Isimu (Mwaka wa Kwanza 2012/2013)Mhadhiri: Mr. Simile, O.E-mail: osimile@gmail.comkulingana na mzingira, mazoea, taaluma na hata mahala mtu alipobobea kitaaluma. Lakini,pamoja na tofauti hizi mbali mbali zinazojitokeza, tunaona kuna mambo kadhaa ya msingiambayo takribani wataalamu wote wanayagusia wanapofasili dhana ya ‘lugha’. Mambo hayo nikama yafuatayo: Lugha ni mfumo, Lugha ni mfumo wa sauti nasibu, Lugha ni maalumu kwabinadamu, Lugha ni mfumo wa ishara, Lugha hutumia sauti, Lugha ni kwa ajili ya mawasiliano.Kimsingi mambo haya ndiyo yanayogusiwa katika fasili hizi. Lakini ikumbukwe kuwa, sio kilafasili zilizotajwa hapo juu zinajumuisha vipengele vyote hivi. La hasha! Fasili moja inawezaikawa inakipengele kimoja wapo au viwili kati ya hivi. Kila kimoja kinaelezewa hapa chini kamaifuatavyo.2.1.Lugha ni mfumoIshara zinazotumiwa katika lugha zinampangilio wenye kutawaliwa na sheria na unaruwazazinazotambulika na watumiaji wa lugha hiyo. Kila lugha ya mwanadamu imeundwa katikamifumo miwili mikuu; mfumo wa sauti na mfumo wa maana. Lugha huundwa kwa sauti ambazohuunganishwa kuunda neno au sehemu ya neno, maneno nayo huungana kuunda miundomikubwa zaidi yenye maana kama virai, vishazi, sentensi na aya.Katika muunganiko huu wa maneno na miundo mbali mbali, huwa kuna kanuni na sheriazinazidhibiti mfuatano wa kila kipashio. Kuna kanuni zinazo dhibiti mfuatano wa sauti,mfuatano wa mofimu, mfuatano wa maneno na hata mfuatano wa sentensi. Hivyo basi, mtuhawezi kuunganisha tu sentensi kwa matakwa yake bila kujali kanuni hizi, akifanya hivyoatasababisha kutokea kwa kitu ambacho siyo lugha na wala hakikubaliki katika lugha. Kwamaana hiyo, lugha ya mwanadamu ni mfumo wenye kanuni, sheria na taratibu maalumu ambazozikikiukwa basi kuna kuwa hakuna utimilifu wa lugha husika. Lugha inaonesha utaratibu katikamahusiano ya viunzi vya lugha. Sheria hizi zinazotawala mpangilio wa viunzi vya lugha hiyondizo zinazowawezesha watumiaji wa lugha fulani kuelewana.2.2.Lugha ni mfumo wa sauti nasibu (Unasibu katika lugha ya mwanadamu)Lugha ni ya nasibu kwa maana kwamba, hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya neno(mathalani kiti) na kitu chenyewe tunachotumia kukalia (maana na kilejelewa). Hii ina maanakwamba, maumbo ya ishara za kiisimu hayana uhusiano wowote au mfanano wowote na maanaambazo tunayapa. Tazama mchoro ufuatao:Katika picha inayoonekana hapo juu kuna neno ‘mti’ na mmea wenyewe ambao umebatizwa jinahilo. Katika hali halisi hakuna watu waliokaa nakusema kuanzia leo huu utaitwa mti. Vile vile3

Chuo Kikuu (cha) Mzumbe (Mzumbe University)KSW101: Utangulizi wa Lugha na Isimu (Mwaka wa Kwanza 2012/2013)Mhadhiri: Mr. Simile, O.E-mail: osimile@gmail.comhakuna uhusiano wowote kati ya neno “MTI” an umbo linalomaanishwa. Uhusiano wake ni wanasibu tu na hutofautiana kutokana na lugha na lugha. Hii ndiyo maana Waingereza wataita tree,Wahehe wataita mubiki, Wasukuma wataita mpiki n.k. Ukweli kwamba hakuna uhusiano wa asilikati ya umbo la neno na maana ambazo umbo hilo linapewa ndiyo sababu inayofanya kuwe nanamnatofauti ya kuuelezea ulimwengu. Ferdinand de Saussure katika kile alichokiita ishara zakiisimu anabainisha sawia mbili za mahusiano haya; kwanza ni “signifie” ambacho ni kiashiriayaani umbo la kifonolojia (kutamkwa) au kiothografia (kuandikwa) na ambalo huwakilishadhana Fulani. Kitu cha pili ni “significant” ambacho ni kiashiriwa ambacho ni kitu chenyewekilicho katika ulimwengu halisi wa vitu na dhana. Hivyo basi, uhusiano kati ya kiashiria nakiashiriwa ndio unlio wa unasibu.2.3.Lugha ni maalumu kwa mwanadamu.Lugha ni chombo cha mawasiliano ambacho amejaliwa binadamu tu na kwamba hakuna kiumbemwingine ambaye si binadamu anauwezo wa kuzungumza na kutumia lugha. Hii ina maanakuwa kuna sifa Fulani za lugha za binadamu ambazo hazipatikani kwa kiumbe mwingine yeyoteyule isipokuwa mwanadamu. Ingawa ndege, mbwa, nyuki, tumbili wanawea kuwasiliana,mawasiliano yao huwa ni ya sauti au ishara ambazo kimsingi siyo lugha, pia huwa yanadhibitiwana hisia tu kama hofu, njaa, na ishara za kutoa taarifa. Binadamu anauwezo wa kujifunza lughambali mbali na kutumia katika mazingira yake na sio wanyama. Kwa mfano, ukimtoa mbwaTanzania na kumpeleka Japani, atatoa sauti ile ile sawa na mbwa wa Japani kwa kueleza shidaile ile au kutoa ishara ile ile.2.4.Lugha ni mfumo wa isharaUishara wa lugha unamaanisha kuwa maneno huambatanishwa / huhusishwa na vitu, matendo,mawazo au hisia kwa makubaliano ya unasibu tu. Vile vile, yale tunayoyasoma katika maandishini ishara tu, maana zake lazima zipatikane katika muktadha wa mawasiliano. Hivyo basi,tunapojifunza lugha lazima tufahamu mfumo wa alama za lugha hiyo na kuelewa uhusianouliopo kati ya ishara na vitu vinavyowakilisha.2.5.Lugha hutumia sautiSifa kuu ya lugha ni kutumia sauti ambazo hutengenezwa na ala za sauti. Pamoja na maendeleoambayo mwanadamu ameyafikia kwa sasa katika uandishi na uwasilishaji wa taarifa kwakutumia lugha sauti ndiyo msingi wa kila kitu. Tafiti zinathibitisha kuwa mfumo wa maandishiumekuja baadaye sana katika maendeleo ya binadamu na kwamba hutumika tu kuwasilisha yaleyanayosemwa kwa kutumia kinywa cha mzungumzaji. Vile vile, ukweli kwamba binadamuanapozaliwa huanza kujua lugha ya mahala anapokua na kuishi kabla ya kufahamu kuandika,unatuthibitishia kuwa kiunzi (msingi) cha lugha ni sauti.Kwa ujumla, kuna sababu kuu tano zinazotuwezesha kukubaliana kuwa msingi wa lugha ni sautiza kutamkwa.4

Chuo Kikuu (cha) Mzumbe (Mzumbe University)KSW101: Utangulizi wa Lugha na Isimu (Mwaka wa Kwanza 2012/2013)Mhadhiri: Mr. Simile, O.E-mail: osimile@gmail.comi.ii.iii.iv.v.vi.Mtoto hujifunza kuzungumza kablra hajajifunza kusoma na kuandikaMtoto hujifunza lugha moja kwamoja bila kufikiri kadiri anavyokuwa.Maandishi yalikuja baada ya mazungumzoMaandishi huwasilisha yale yanayozungumzwaWatu kwa kawaida hutumia muda mwingi kuzungumza kuliko kuandikaKuna mambo mengi ya muhimu katika sauti z lugha ambayo hayawezikuwasilishwa vema kwa kutumia maandishi. Mambo hayo ni kama, kiimbo,toni, mkazo, kidatu, haya ni muhimu katika mawasiliano lakini hayawezikuwasilishwa kisawa sawa kwakutumia maandishi (Habwe na Karanja, 2003).2.6.Lugha ni kwaajili ya mawasilianoKwa kutumia lugha binadamu anaweza kufanya vitu ambavyo viumbe wengine hawawezikuvifanya. Vile vile lugha hutuwezesha sisi kuzungumzia hisia zetu, matamanio yetu, kucheza,kufanya kazi n.k. Yote haya yanawezekana kwakuwa tunayo lugha ambayo ndiyo nyenzo kuu yamawasiliano.2.7.Fasili ya jumlaHivyo basi, baada ya kuchunguza fasili hizo za lugha na vipengele vinavyojibainisha kwenyekila fasili mojawapo, tunaweza kusema kuwa lugha ni mfumo wa sauti za nasibu zilizokubaliwana watu au jamii ili zitumike katika mawasiliano yao ya kilasiku kueleza hisia, mawazo,matakwa na mahitaji yao.3.0.Tabia za lugha ya binadamu ainazoitofautisha na aina nyingine za mawasilianoTumekwisha elezwa hapo awali kuwa lugha ni maalumu kwa binadamu tu na kwamba hakunakiumbe yeyote ambaye si mwanadamu mwenye uwezo wa kujua, kujifunza na kutumia lughazaidi ya binadamu. Jambo hili linatupelekea kuzitathmini sifa au tabia za lugha ya mwanadamu.Kimsingi sifa/tabia hizi ndizo zinazoitofautisha lugha ya mwanadamu na aina nyingine zamawasiliano zitumiwazo na wanyama.3.1.UnasibuKama tulivyokwisha eleza mwanzo, unasibu wa lugha ya ninadamu unaangaliwa katika mamboyafuatayo:i.ii.iii.Binadamu hazaliwi na lugha, anakutananayo kwa unasibu tuHakuna uhusiano wa moja kwa moja au wa asili kati ya kitaja (neno kamaumbo la kiisimu) na kitajwa (kitu au umbo linalomaanishwa au maana).Uhusiano wake niwa unasibu na unatokana na makubaliano ya watumialugha.Hata makubaliano haya ya kwamba kitu kiitwe au dhana fulani iitwe nakuelezwa kwa namna fulani ni ya nasibu tu. Hapa tunamaanisha kwambahakuna mkutano au kikao ambacho binadamu amewahi kukaa akasema5

Chuo Kikuu (cha) Mzumbe (Mzumbe University)KSW101: Utangulizi wa Lugha na Isimu (Mwaka wa Kwanza 2012/2013)Mhadhiri: Mr. Simile, O.E-mail: osimile@gmail.commathalani neno “chuki” limaanishe hali ya kuto kumpenda mtu au neno“upendo” limaanishe hali ya kuonesha huba kwa mtu.iv.Kila jamiilugha ina namna yake ya kuufasili na kuuelezea ulimwengu kwalugha yake ambayo inatofautiana na jamiilugha nyingine.3.2.Uzalikaji au UbunifuUzalikaji katika lugha ya binadamu unajidhihirisha katika mambo yafuatayo:i.Uwezo wa mwanadamu kubuni na kuunganisha maneno na miundo mbalimbali ya tungo bila kikomo.ii.Uwezo wa mwanadamu kutunga na kuzielewa tungo mbali mbali ikiwa nipamoja na zile ambazo hajawahi kuzisikia wala kuzitunga.iii.Uwezo wa mwanadamu kuelewa tungo zilizotungwa na watu wengine nakufahamu maana ya kisemantiki na ile ya kipragmatiki.iv.Uwezo wa mwanadamu kuzielewa tungo sahihi na zile zisizo sahihiHivyo uwezo huu unatofautiana na aina nyingine ya mawasiliano inayotumiwa na wanyamawengine, kwamfano, “nyenje ni myama mwenye milio au ishara nne za kuchagua ili awasiliane,tumbili ana miito sita tu. Hivyo wanyama wote hawa wanaidadi isiyobadilika ya milio na sautiau ishara na hawana uwezo wa kubuni namna nyingine ya kuwasiliana au kubuni milio mingineya kuwasiliana.3.3.Uambukizaji wa utamaduniLugha ya mwanadamu inauwezo wa kuambukiza utamaduni kutoka katika kizazi kimoja kwendakizazi kingine au kutoka katika jamiilugha moja kwenda katika jamiilugha nyingine. Ielewekekuwa, uwezo huu wa kuambukiza maarifa ya lugha hufanyika kwa njia ya kusoma au kujifunzana sio kurithi. Kwa mfano, mtu anaweza kurithi maumbile kutoka kwa wazazi wake, mathalaniaina ya nywele, aina ya macho, lakini mtu hawezi kurithi lugha. Lugha inamfikia kwakuambukizwa katika jamiilugha anayokulia. Yatupasa tukumbuke kuwa, ingawa mwanadamuanazaliwa na uleuwezo (kitengo cha lugha) wa kujifunza lugha “Language Acquisition Device”kama anavyoeleza mwanaisimu Noam Chomsky, lakini hazaliwi na lugha. Hii ndiyo sababumwanadamu anaweza kujifunza lugha yoyote ile na kwa wakati wowote maadamu yupo katikamazingira na hali ya kawaida na saidizi.3.4.Uwili (utamkaji pamwe)Lugha ya mwanadamu imepangwa katika viwango viwili ambavyo vinashirikiana nakukamilishana. Kiwango cha kwanza ni kile kiwango cha utamkaji wa sauti au utoaji wa sautikama; /n/, /m/, /g/, /t/, /k/, /a/, /e/, /o/ kwa kutumia alasauti mbali mbali. Sauti hizi zikisimamapeke yake hazina maana yoyote, ni kama milio tu kama kupiga chafya, au kekele zinazotokanana kuburuza meza kwenye sakafu au kelele za injini ya piki piki. Sauti hizi zinapounganishwa(kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za lugha husika) tunapata maneno yenye maana ambapotunapata kiwango kingine cha pili cha maana. Sifa ya uwili inadhiririsha sifa ya uwekevu katika6

Chuo Kikuu (cha) Mzumbe (Mzumbe University)KSW101: Utangulizi wa Lugha na Isimu (Mwaka wa Kwanza 2012/2013)Mhadhiri: Mr. Simile, O.E-mail: osimile@gmail.comlugha ya mwanadamu kwani kwa kutumia sauti hizi chache mzungumza lugha anaweza kutoa aukuzungumza sentensi nyingi au tungo nyingi na zenye maana tofauti tofauti bila kikomo.Suala jingine la msingi ni kwamba, tunaposema kuwa lugha imegawanyika katika viwangoviwili, kiwango cha sauti na kiwango cha maana haimaanishi kwamba binadamu anatumiaviwango hivi kiupeke peke. Hata sikumoja mwanadamu hasemi kwamba sasa naanza kutamkasauti, mathalani, baba halafu ndiyo niweke maana yake. La hasha! Binadamu hutamka kwamaramoja sauti pamoja na maana vikiwa vimebebana ndani kwa ndani (hutamka sauti pamwe namaana). Yaani, wakati anatamka sauti na kuziunganisha ndiyo wakati anaambatanisha na maanandani yake. Hii ndiyo sifa ua uwili katika lugha ya mwanadamu.3.5.Uhamisho au UrejeleziUhamisho ni sifa ya lugha ya mwanadamu inayomaanisha kwamba lugha ya mwanadamuinaweza kutumika katika kuzungumzia au kurejelea kitu ambacho hakipo katika upeo wa machoya mzungumzaji kiwakati na kimazingira. Tofauti na mawasiliano ya wanyama, binadamuanaweza kuzungumza juu ya matukio yaliyopita, matukio yajayo, na hata yale anayoyatarajiakufanya kwa kutumia lugha. Kwa mfano, myana kama ng’ombe hawezi kuelezea kwa njia yakeya mawasiliano, aina ya chakula alichokula jana, au anachotamani kula, au anachotarajia kula, aukwa nini jana alikwenda kunywa maji, au hata kujua sababu ya kuumia. Lakini mambo hayabinadamu anayaweza kwa kutumia lugha yale ya asili. Hii ndiyo sifa inayoitwa uhamisho auurejelezi (displacement).3.6.Uwezo wa kubadilishana taarifa/Ubadilishanaji taarifaSifa hii inamaanisha kuwa binadamu wenyewe kama watumia lugha wanauwezo wakubadilishana taarifa. Kila mmoja wao anaweza kuwa mtumaji au mpokeaji wa taarifa kwakutumia lugha.3.7.UpekeLugha hundwa na viunzi vidogo vidogo ambavyo ni peke peke na haipo katika mfululizo. Kilakipashio kinachotumika kuunda tungo za lugha kipo peke peke na kinaweza kuunganishwa navingine kupata muundo wa juu mkubwa zaidi. Hivyo, lugha inawezwa kugawanywa tena kwakukusayna vipashio hivyo kuunda tungo kubwa zaidi.4.0.Asili ya LughaHakuna maafikiano kati ya wanaisimu juu ya wapi, lini, namna gani na nani hasa alianzishalugha. Hii inatokana na ukweli kwamba binadamu alianza kuishi tangu kale wakati ambapo hatahivyo bado hauja julikana. Suala ambalo lina uhakika ni kuwa lugha inatumiwa na mwanadamu7

Chuo Kikuu (cha) Mzumbe (Mzumbe University)KSW101: Utangulizi wa Lugha na Isimu (Mwaka wa Kwanza 2012/2013)Mhadhiri: Mr. Simile, O.E-mail: osimile@gmail.comna kila jamii ina lugha yake. Hata hivyo kuna nadharia mbali mbali zinazoeleza chanzo na asiliya lugha. Baadhi ya nadharia hizo ni kama zifuatazo:4.1.Nadharia ya UUngu/mtazamo wa kidiniMsingi wa nadharia hii ni kwamba lugha iliumbwa na Mungu na akapewa mwanadamu kwanguvu za Mwenyezi Mungu. Nadharia hii inaeleza kuwa, haja ya Mungu kuwasiliana na kiumbewake Binadamu ndiyo iliyomfanya aumbe lugha. Inaaminika kuwa Mungu ndiye alikuwawakwanza kutumia lugha, aliumba ulimwengu kwa kutumia neno, na kwa neno kila kituakiwemo mwanadamu likifanyika. Inaaminika kuwa lugha zote zilitokana na lugha mojailiyoumbwa na Mungu. Hata hivyo kuna visasili mbali mbali vinavyoeleza asili ya lugha katikanadharia ya Uungu. Kwanza ni, pale Mungu alipompa Adamu uwezo wa kuzungumza kwakuwatajia majina wanyama wote na pale ndipo lugha ilipoanza (Mwanzo 2:19).Nadhari hii ya uungu pia huchagizwa na kisasili kingine cha Wamisri, Wababiloni, na Wahindi.Kwa mujibu wa kisasili cha Wababiloni, inasemekana hapo kale Mfalme wa Babeli aliamurukujenga mnara mrefu ulioitwa Mnara wa Babeli ili kumfikia Mungu. Kwa lengo hilo Mungualikasirishwa sana akaamua kuwachanganya lugha wajenzi wa mnara huo hivyo wakashindwakuelewana na hatimaye azma yao ikasitishwa. Kwa hiyo kutokana na imani hiyo waaminiwengine wanakubali kuwa yawezekana lugha nyingi zinazoonekana leo ni tokeo la mnara waBabeli.Kama hivyo haitoshi, Wamisri wanachagiza nadharia hii kwakuwa na Mungu wao aliyeitwaThoth ambaye ni Mungu wa Lugha. Wahindu walihusisha uwezo wa mwanadamu wakuzungumza na mungu wao wa kike aliyeitwa Brahma ambaye kwa imani yao Brahma ndiyeMungu muubaji wa ulimwengu lakini lugha alipewa mwanadamu kutoka kwa mke wakealiyeitwa Sarasvati.Suala la msingi katika nadharia hii ni kwamba lugha za mwanadamu zinakianzo kimoja na ndiomaana wanaisimu wa baadaye wamekuwa wakizungumzia suala la sarufi bia. Udhaifu wakenikwamba zinashindwa kujibu maswali kama- kwanini lugha nyingine zinazuka tu sikuhizi bilaya kuwa nazo zimetoka kwa Mungu. Vile vile, mtazamo huu haujajikita katika tafiti za sayansiya lugha yaani Isimu, pia haujafuata taratibuza kiuchunguzi wa kiisimu ambayo ndio sayansi yalugha.4.2.Nadharia ya Wigo wa Sauti za Asili/ kianzo asiliaNadharia nyingine inayoeleza juu ya asili ya lugha ni ile ya Wigo. Kwa mujibu wa Yule (2010),nadharia hii inashikilia msimamo kuwa sauti za awali kabisa za lugha ya binadamu ni matokeobinadamu kuiga sauti asilia ambazo wanawake na wanaume walizisikia katika mazingira yao.Nadharia hii inapigiwa upatu na baadhi ya maneno ambayo yanatokana na sauti asilia za milio yavitu kama vile vitu vinapodondoka, au kugongana ambayo huitwa onomatopoeia.8

Chuo Kikuu (cha) Mzumbe (Mzumbe University)KSW101: Utangulizi wa Lugha na Isimu (Mwaka wa Kwanza 2012/2013)Mhadhiri: Mr. Simile, O.E-mail: osimile@gmail.comPamoja na uthibitisho unaoweza kutolewa kwa maneno hayo machache ambayo huenda kilalugha inayo, bado kuna udhaifu katika nadharia hii. Nadharia hii haijitoshelezi kwakuwa kunamaneno mengi tu mbayo kwa asili yake hayatokani na milio ya vitu, kama majina, na vitenziambayo ni matokeo ya njia nyingine za uundaji wa maneno na siyo uigo wa sauti asilia.4.3.Nadharia ya mchangamano wa na mahusiano ya kijamiiNadharia hii inashikilia msimamo kuwa, wakati Fulani katika maisha ya mwanadamu, alihitajimsaada wa mwanadamu mwingine katika kufanya kazi. Katika kazi hizo binadamu hao walitoamilio na sauti mbali mbali za kuhamasishana. Kutokana na sauti hizo yasemekana ndipo lughailipoanza. Hatahivyo nadharia hii inatupa wazo moja muhimu kwamba maendeleo ya lugha yamwanadamu yanatokana na mazingira ya kijamii alimoishi mwanadamu. Kwa hiyo wanadamulazima waliishi katika makundi ya kijamii, kama hilo linaweza kukubalika, lazima tukubali kuwayamkini kulikuwa na kanuni maaumu ambazo zilitawala mfumo wao wa mawasiliano katikamaisha yao na mahusiano yao ya kijamii.Pamoja na hayo, nadharia hii bado inatunyima majibu ya swali letu la msingi juu ya asili ya hizosauti zilizozalishwa. Kama chanzo cha lugha ni mahusiano ya kijamii, kuna wanyama wenginewanaoishi katika makundi makundi kama tumbili na ngedere lakini mawasiliano hayahayaendelei kuwa matamshi ya lugha.4.4.Nadharia ya Ki-maumbile ya MwanadamuBadala ya kuchunguza asili ya sauti za mwanadamu na kutoa tamko kuwa huenda ndizo chanzona asili ya lugha ya mwanadamu, nivema tukaangalia sifa za kimaumbile alizonazo mwanadamu.Uchunguzi huu unajikita katika zile sifa ambazo viumbe wengine (wanyama) hawana (RejeaYule, 2010). Msimamo wa nadharia hii ni kuwa tofauti ya kimaumbile kati ya mwananadamu nawanyama kama Nyani ndiyo uliokuwa chanzo cha lugha y mwanadamu.5.0.Utangulizi wa Isimu5.1.Isimu ni nini?Fasili iliyozoeleka na pengine inakubalika na wataalamu wengi wa lugha ni kuwa Isimu ni elimuya sayansi ya lugha. Ni uchunguzi wa kisayansi na wa kimantiki kuhusu vipengele na sifa mbalimbali za lugha. Swali ambalo tunaweza kujiuliza ni kwamba; “Kwa nini isimu ni sayansi?”Verma et al (1989:29), wanasema kuwa isimu ni sayansi kwakuwa hufuata na kutumia mbinu zakimsingi za utafiti wa kisayansi. Mbinu hizo ni kama zifuatazo:i.ii.iii.iv.v.Uchunguzi uliodhibitiwaUundaji wa mabunioUchanganuziUjumlishi/ujumuishiUtabiri9

Chuo Kikuu (cha) Mzumbe (Mzumbe University)KSW101: Utangulizi wa Lugha na Isimu (Mwaka wa Kwanza 2012/2013)Mhadhiri: Mr. Simile, O.E-mail: osimile@gmail.comvi.Majaribio na uthibitishajivii.Urekebishaji au ukataaji wa mabunio5.2.Misingi ya kisayansiKwa hatua hizi, tunathubutu kusema kuwa isimu haichunguzi lugha kiholela tu bali kwamwelekeo maalumu. Katika kuchunguza lugha wanaisimu hutumia misingi ya kisayansi kamazifanyavyo sayansi nyingine, misingi hii ni kama vile; uwazi, utaratibu na urazini.5.2.1 UwaziDhana hii inamaanisha kuwa maswala katika isimu huelezwa kwa udhahiri usio na utata wowote.Hoja huelezwa bila kuleta vugu vugu lolote la kimaana hii ni kinyume na mawasiliano yasiyokisayansi.5.2.2. UtaratibuHabwe na Karanja, (2003) wanaeleza kuwa utaratibu na uwazi ni dhana zinazokaribiana sana.Bila kuwa na uwazi ni vigumu kuwa na utaratibu na kinyume chake. Utaratibu ni kufanya jambokwa mpangilio mzuri wenye kubainika. Utaratibu unaweza kuhusisha wakati, idadi, umuhimu nahata ukubwa5.2.3. Urazini/UhoromoMtafiti hatakiwi kughosha hisia zake na kuzitumia kueleza jambo fulani. Hii ina maanisha kuwamtafiti hatakiwi kuruhusu hisia zake kuathiri utafiti wake wa kisayansi hatakama suala la mgusolinatafitiwa. Katika utafiti, kitu chamsingi ni data na matokeo ya uchunguzi yanayotokana nadata zilizotumika. Utetezi wa matokeo vile vile lazima utokane hatua madhubuti za kisayansi nakiutafiti.5.3. Upeo wa IsimuHabwe na Karanja, (2003) wansema kuwa, katika kushughulikia lugha wanaisimu hujaribukujibu maswali kama vile:i.Lugha ni nini?ii.Asili ya lugha ni nipi?iii.Lugha hufanya kazi namna gani katika mawasiliano?iv.Lugha inahusiana namnagani na asasi nyingine maishani?v.Kujua lugha ni nini?vi.Namna gani mtoto anajifunza lugha?vii.Kwa nini lugha hubadilika?viii. Lugha zinatofautiana kwa kiasi gani?Hivyo katika kujaribu kujibu maswali haya, mwanaisimu hujikuta akiwa na kazi ya kutimizamajukumu yafuatayo:i.Kueleza maana na asili ya lugha10

Chuo Kikuu (cha) Mzumbe (Mzumbe University)KSW101: Utangulizi wa Lugha na Isimu (Mwaka wa Kwanza 2012/2013)Mhadhiri: Mr. Simile, O.E-mail: osimile@gmail.comii.iii.iv.5.4.Kuchambua muundo wa lughaKueleza uhusiano kati ya lugha na asasi nyingine za mwanadamuKuibua nadharia mbali mbali za lughaIstilahi za msingi katika uchunguzi wa kiisimuKatika sehemu hii ni muhimu kwa kila msomaji wa lugha au mwanaisimu kuzifahamu nakuweza kuzitofautisha istilahi zifuatazo kama zinavyotumika katika taaluma ya lugha.5.4.1. Sikronia na DaikroniaKatika sinkronia, lugha huchunguzwa kwa kuangalia namna ilivyotumika katika kipindi fulanimaalumu cha wakati bila kujali mabadiliko yake yanayotokea. Kwa upande mwingine katikadaikronia lugha huchunguzwa katika mtazamo wa historia ya mabadiliko yake. Hapa wanaisimuhulinganisha lugha kwa kuangalia tofauti zake zinazotokana na mabadiliko ya kihistoria nakuzielezea tofauti hizo. Kwa mfano mabadiliko yaliyoko kati ya Kiswalihi cha kale (mathalanimiaka ya 1900) na Kiswahili cha sasa yanawezwa kuelezewa kifonolojia, kisarufi, na kimaana.5.4.2. Umilisi (langue) na utendi (parole)Umilisi ni ujuzi alio nao mjua lugha kuhusu lugha yake. Ni ujuzi alio nao mjua lugha ambao upokatika ubongo wake. Ujuzi huo huhusu kanuni zinazotawala lugha hiyo husika. Ujuzi huuhumwezesha kutambua sentensi sahihi, zisizosahihi na kupambanua sententi zenye utata. Ujuzihuo humwezeha kupuuza makosa ya kiutendaji katika mazungumzo kama vile kuteleza kwaulimi, kukatisha sentensi n.k.(Rubanza, 2003).Utendi (aji) ni kile asemacho mjua lugha katika muktadha wa mawasiliano ikiwa ni pamoja namakosa ya kiutendaji ya bahati mbaya nay ale ya kukusudiwa. Vile vile tunaweza kusema niudhihirikaji wa ujuzi wa lugha alionao mjua lugha.5.4.3. Utumizi (functionalism) na Urasmi (formalism)Utumizi au isimu tumizi ni elimu inayohusu muundo wa lugha kwa kurejelea kazi zake za kijamiikatika mawasiliano. Inamchukulia mtu binafsi kama kiumbe-jamii na kuchunguza namnaanavyojifunza lugha na kuitumia katika mawasiliano na wanajamii wenzake. Urasmi au isimurasmi ni elimu ya maumbo dhahania ya lugha na mahusiano yake ya ndani. Huzingatia maumboya lugha kama uthibitisho wa kimalimwengu bila kuzingatia namna jamii inavyowasiliana.5.4.4. Uelezi na UelekeziUelezi (isimu elezi) ni mtazamo ambao huelezea ukweli wa lugha jinsi ilivyo na inavyotumika najamiilugha husika. Na siyo namna inavyotakiwa kutumika. Isimu elezi haiweki kanuni ngumu ausheria ngumu zozote zinazotokana na mawazo ya mtu juu ya lugha fulani bali huelezea lughakwa kuangalia namna lugha hiyo inavyojidhihirisha yenyewe. Huelezea sheria na kanuni ambazomzungumzaji mzawa ameziweka kichwani na zinazoakisi uwezo wake wa lugha. Kwa kifupi,11

Chuo Kikuu (cha) Mzumbe (Mzumbe University)KSW101: Utangulizi wa Lugha na Isimu (Mwaka wa Kwanza 2012/2013)Mhadhiri: Mr. Simile, O.E-mail: osimile@gmail.comhaielezi wala kuagiza namna mtu anavyotakiwa kutumia lugha bali namna lugha ilivyo nainavyotumika na wamilisi wa lugha hiyo.Uelekezi (isimu elekezi) ni mtazamo unaojaribu kuweka kanuni za usahihi wa namna watuwanavyotakiwa kutumia lugha.5.5. Matawi ya Isimu5.5.1. Isimu ubongo – ni tawi la isimu linalochunguza mahusiano kati ya lugha namichakato ya kiakili (ubongo), uzalishaji wa matamshi katika ujifunzaji wa lugha.Msingi mkubwa katika tawi hili la isimu ni kuwa mchakato wa uzungumzajihuanzia katika akili ya mtu. Hivyo mwanaisimu ubongo hujaribu kutafitina kuelezani nini hasa kinatokea katika ubongo ambacho kinamwezesha mwanadamukuzungumza. Pia hutafiti na kueleza matatizo katika lugha yanayotokana namatatizo katika ubongo wa mwanadamu.5.5.2. Isimu jamii - Isimu Jamii (social linguistcs) - ni tawi la isimu (elimu ya lugha)linalochunguza namna lugha inavyotumika katika jamii na uhusiano baina yake.Tawi hili huzingatia matumizi ya lugha katika mazingira tofauti; aina mbali mbaliza lugha na mazingira yake; uhusiano kati ya lugha na utamaduni wa jamiiinayoitumia. King’ei (2010), anaeleza kuwa, kwanza lugha ni zao la jamii, na nikipengele muhimu sana cha utamaduni wa jamii husika. Pili, lugha hutumiwa najamii kuhifadhi amali na utamaduni wake na hasa kama chombo maalumu chakuwezesha wanajamii kuwasiliana. Hivyo isimu jamii hueleza na kufafanuamahusiano ya karibu kati ya lugha na jamii ambayo ndiyo mama wa lugha.5.5.3. Isimu anthropolojia – tawi hili la isimu hukijita katika kutafiti na kueleza historiaya na miundo ya lugha ambazo bado hazijaandikwa.5.5.4. Isimu kompyuta – huchunguza matumizi ya kompyuta katika kuchakata nakuzalisha lugha ya

[“Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu ambazo kwazo makundi ya kijamii hushirikiana”] v. Noam Chomsky(1957): “Language is a set of finite number sentences, each finite in li

Related Documents:

KI 214 UFUNDISHAJI KISWAHILI KWA WAGENI MBINU ZA UFUNDISHAJI KISWAHILI KWA WAGENI I. Malengo ya ufundishaji lugha kwa wageni Lengo kubwa ni kwamba ili mwanafunzi aweze kujua lugha hiyo kwa stadi zote za lugha ile. Stadi za lugha ni 1. Kusikiliza 2.kuzungumza

inafuata mchango wa baadhi ya wanaisimu wa lugha ya Kiingereza, Kiarabu na Kiswahili walivyobainisha uwepo wa kategoria ya nomino (majina) katika lugha hizi. 1.1.2 Majina Katika Lugha ya Kiingereza Wataalamu mbalimbali wa lugha ya kiingereza wamebainisha kuwepo kw

Kukuza lugha. Aghalabu tungo zote za fasihi hutumia lugha. Isitoshe, fasihi hutumia mbinu nyingi za lugha. Wasimulizi na waandishi wa fasihi huhitaji kuwa na ukwasi wa lugha. Kuhifadhi mila, tamaduni na itikadi za jamii. Aghalabu kazi za fasihi (hasahasa Fasihi Simulizi) huambatanishwa na desturi mbalim

2.2 COST 231 Hata model COST 231 Hata model is an empirical model used for calculating path loss in cellular mobile system. This model is an extension of the Okumura-Hata model designed to cover frequency ranges from 1700Mz to 2300MHz with receiving antenna heights up to 10m and transmitting antenna heights of 30m-200m. COST 231

i UTHIBITISHO Aliyeidhinisha hapa chini anathibitisha kwamba ameisoma tasnifu hii inayoitwa ; "Upimaji wa ufahamu wa kiswahili kama lugha ya kufundishia shule za msingi : mifano kifani toka halmashauri ya wilaya ya Geita", na ameridhika kwamba imefikia kiwango kinachotakiwa na inafaa kuwasilishwa kwa ajili ya

lugha ya Kimunakiiya buutsa (kuchukua) na karibu kama TS katika neno la Kiingereza cats (paka); Ĝ hutamkwa kama J katika lugha ya Kigogo: -inji (ingi), lakini bila sauti ya N; basi hutamkwa kama J ya Kiswahili katika neno njaa, bila sauti ya n. Angalia pia kwamba sauti hiyo ni tofauti sana na sau

iii) Sauti iv) Ishara za mwili. Ni mfumo wa sauti za nasibu zinazotumiwa na wanadamu katika mawasiliano. Sifa za lugha. i) Hakuna lugha iliyo bora kushinda zingine. –zote ni sawa. ii) Kila lugha ina sifa zake. iii) Lugha hubadilika kutegemea mazingira, aina ya

Grade 2 Home Learning Packet The contents of this packet contains 10 days of activities in paper copy. Students should be completing this packet, along with completing lessons on their math/reading online programs daily. If we surpass the 10 days without school, students should continue using their online math and reading programs for 45 minutes per day per program unless otherwise specified .