COUNTY HIGH SCHOOL - WordPress

3y ago
300 Views
30 Downloads
1.03 MB
42 Pages
Last View : 5d ago
Last Download : 5m ago
Upload by : Abram Andresen
Transcription

COUNTY HIGH SCHOOLPANELI LA KISWAHILICOMPILED BY:BURALE & FEISAL SHAKIRGafkosoft.com/swaPage 1 of 42

Isimu JamiiIsimu Jamii (social linguistcs) - ni tawi la isimu (elimu ya lugha)linalochunguza namna lugha inavyotumika katika jamii nauhusiano baina yake. Tawi hili huzingatia matumizi ya lughakatika mazingira tofauti; aina mbali mbali za lugha na mazingirayake; uhusiano kati ya lugha na utamaduni wa jamii inayoitumia. Istilahi za Isimu JamiiAina za LughaIstilahi za Isimu Jamii1. Isimu (linguistics) - ni mtalaa ambao huchunguza,huchanganua na pia kuchambua na kufafanua lugha kamamfumo wa mawasiliano baina ya wanadamu.2. Lugha - ni chombo cha mawasiliano baina ya watu.Lugha huzingatia mpangilio maalum wa sauti, maneno nasentensi.3. Sajili - ni mukhtadha/rejista mbalimbali au mitindomaalum ya lugha katika mazingira/hali mbalimbali.Mifano ya sajili ni kama vile lugha ya hospitalini, shuleni,sajili ya dini, biashara, kisiasa, michezo,4. Fonolojia - ni tawi la sayansi ya isimu linaloshughulikiauchunguzi wa mfumo wa sauti katika lugha fulani, kwamfano ugawanyaji wa irabu na konsonanti. Fonolojiahutumika kuunda alfabeti katika lugha fulani. Aghalabukila lugha hutumia mfumo fulani wa sauti mahususi katikalugha hiyo pekee.5. Fonetiki - huchunguza sauti zinazotamkwa na binadamubila kuzingatia lugha yoyote.6. Mofolojia - (au sarufi maumbo) ni tawi la isimulinalochunguza maneno ya lugha fulani, aina za manenokatika lugha, hasa upangaji wa mofimu mbalimbalizitumikazo kwa ajili ya kuunda maneno hayo. Kwa mfano,lugha ya Kiswahili hutumia mbinu kadhaa kuunda manenokulingana na mpangilio wa mofimu. Kwa mfano, neno'lima' linaweza kutumika kuunda maneno mengine katikaKiswahili k.m mkulima, kilimo, nimelima, limika n.kKatika kubadilisha mofimu hizi, tunaweza kubadilishaneno moja kutoka aina moja(kitenzi) hadi nyingine(nomino) n.k7. Sintaksi - (au sarufi miundo) ni tawi la isimu au taalumaya sarufi inayoshughulikia jinsi vikundi vya maneno nasentensi mbalimbali zinajengwa katika lugha. Sintaksiahuangazia kanuni au sheria za lugha. Kila lugha huwa nasheria zake za kuambatanisha maneno kama vile jinsi yakufuatanisha vitenzi, nomino na vielezi. Kwa mfano:Mtoto yako shiba ni sentensi isiyokuwa na sintaksi.Sentensi sawa ingekuwa: Mtoto wako ameshiba.8. Semantiki - ni tawi la isimu linalochunguza maana halisia(mantiki) ya maneno, kifungu au sentensi katika lugha.Page 2 of 42

Sentensi isiyokuwa na mantiki ni sentensi inayotoa maanaambayo haiwezekani katika uhalisia. Sentensi inawezakuwa sawa kisintaksia lakini iwe na makosa ya kimantiki.Kwa mfano: Kiatu cha mbwa kimefutwa kazi kwa sababukumi ni kubwa kama hewa.Aina za Lugha Katika Isimu Jamii1. Lafudhi - Ni upekee wa mtu katika matamshi (accent)unaoathiriwa na lugha ya mama, mazingira yake yakijiografia au kiwango ujuzi wake wa lugha.2. Lahaja - ni vijilugha vinavyoibuka kwa lugha moja kuukutokana na tofauti za kijiografia baina ya wazungumzajiwa lugha hiyo. Kwa mfano lugha ya Kiswahili ina lahajakadhaa kama vile Kimtang'ata, Kilamu, Kimvita, n.k.Tofauti baina ya lufudhi ni kama msamiati, muundo wasentensi au matamshi.3. Lugha rasmi - ni lugha inayotumika katika shughuli zakiofisi ama ya wakati wa mawasiliano rasmi katika taifafulani. Kwa mfano, lugha rasmi nchini Kenya niKiingereza.4. Lugha rasimi - ni mtindo wa lugha uliotumiwa namtu/watu fulani mashuhuri (zamani) na ambao huonekanakuwa mtindo bora wa lugha unaofaa kuigwa na wengine.Kwa mfano lugha ya Shakespeare.5. Lugha ya taifa - ni lugha inayoteuliwa na taifa fulanikama chombo cha mawasiliano baina ya wananchi, kwamaana inazungumzwa na wananchi wengi katika taifahilo. Lugha ya taifa, nchini Kenya ni Kiswahili; Uganda niKiganda.6. Lugha Sanifu - Ni lugha iliyokarabatiwa na sheria zake(k.v muundo wa sentensi, msamiati, sarufi, n.k)kubainishwa na kuandikwa, na kwa hivyo huzingatiasarufi maalum na upatanisho sahihi wa sentensi. Kwamfano: Kiswahili sanifu - ni lugha isiyokuwa na makosaya kisarufi.7. Lingua Franka - Ni lugha inayoteuliwa miongoni watuwenye asili tofauti wasiozungumza lugha moja ili iwelugha ya kuwaunganisha katika shughuli rasmi au zakibiashara.8. Pijini - ni lugha inayozaliwa kutokana na mchanganyo walugha zaidi ya moja. Kwa mfano. Sheng' (lugha ya vijanamitaani nchini ni lugha iliyoibuka kutoka kwa Kiswahilina Kiingereza.9. Krioli - Ni pijini iliyokomaa na kukubalika.10. Lugha mame - hii ni lugha isiyokua na ambayo hubakikati umbo lake la awali. Kwa mfano lugha ya Kilatinihaibadiliki na hivyo hutumika katika kubuni majina yakisayansi, n.k.11. Lugha azali - ni lugha inayozaa lugha nyinginezo.12. Misimu - ni lugha yenye maneno ya kisiri ambayohutumiwa na kikundi fulani cha watu katika jamii,inayoeleweka tu baina yao. Misimu huibuka na kutowekabaada ya muda.Sajili Katika Isimu JamiiSajili - ni mukhtadha/rejista mbalimbali au mitindo maalum yalugha katika mazingira/hali mbalimbali.Kuna sajili anuwai za matumizi ya lugha katika jamii. Hapatutazingatia mifano michache ya sajili mbali mbali.Kila sajilihuwa na sifa mbalimbali zinazoitofautisha sajili hiyo nanyinginezo. Ili kubaini sifa za lugha katika sajili fulani, nimuhimu kuzingatia baadhi ya maswali yafuatayo:Page 3 of 42

ni mazungumzo baina ya nani na nani?kuna uhusiano gani baina ya wanaozungumza?yanapatikana wapi?yanatumika katika hali gani?yana umuhimu ama lengo ganini istilahi zipi istilahi (maneno maalum) zinazopatikanakatika mazingira hayo?umaizi wa lugha baina ya wazungumzaji ni wa kiwangogani?ni mtindo gani wa lugha unaotumika?Sajili ya Matanga"Waombolezaji wenzangu, kama mnavyojua tumekusanyika hapakwa ajili ya kumsindikiza rafiki yetu amabye amelala hapa. Ikiwakuna mtu alifikwa zaidi na msiba huu ni mimi. Marehemualikuwa rafiki wangu wa dhati tuliyeshirikiana naye sana.Nilimjua marehemu tukifanya kazi katika soko la Mauzoduni natangu siku hiyo tumeishi kama ndugu; kuomba radhi ukikosewa;kusaidiana, na kadhalika. "Habari za kifo chake zilinipiga kwa mughdha. Sikuamini kwambaamekufa; kwamba sitamwona tena aushini mwangu. Ninasikitikasana lakini kwa kuwa Mungu hakosi, ninaamini kwambaalimpenda zaidi ya tulivyompenda. Ombi langu kwa Mungu nimoja, kwamba amweke rafiki yangu mahali pema peponi; aupopote alipojitafutia siku zake za uhai; nami nitakapokufaanipeleke papo hapo tuendelee kuwa marafiki. Mwenzangu lala.Lala salama tutaonana siku moja"Ni lugha inayotumiwa katika shughuli za mazishi au nyumbanikwa marehemu.Sifa za Lugha ya Matanga/Mazishi1. Hutumia msamiati wa maneno ya huzuni kama vilewaombolezaji, makiwa, kifo, mauti, pole n.k.2. Hutumia lugha ya kuliwaza/kufariji na kupa matumainihasa kwa waombolezaji.3. Ni lugha yenye unyenyekevu isiyotumia manenoyanayokera.4. Hudhihirisha unyonge wa mwanadamu, kama asiye namamlaka juu ya uhai wake.5. Huwa na mbinu rejeshi kurejelea maisha ya marehemualipokuwa hai.6. Kwa mara nyingi hutumia maneno ya kusifu marehemukutokana na aliyotenda.7. Wakati mwingine huwa ni lugha inayodhihiri hali yakukata tamaa.Mfano wa Sajili ya MatanganiSajili ya AjaliHii ni lugha inayotumiwa katika ambalo ajali imetokea. Wahusikawanaweza kuwa majeruhi, polisi, walioshuhudia au wananchiwengine n.kSifa za lugha inayopatikana katika sajilihii1. Msamiati wa kipekee unaohusiana na ajali kama vilemajeruhi, hudumanya kwanza, damu, mkasa.Page 4 of 42

2. Hutumia lugha ya kudadisi dadisi ili kubaini chanzo chaajali.3. Huwa na masimulizi – walio na habari kuhusu kisa hichohueleza waliyoshuhudia4. Kutokana na hali ya msukosuko, lugha hii haina utaratibu– watu huwa katika hali ya hofu, kwa juhudi za kuwaokoamajeruhi.Mfano wa Sajili ya ijiji2:Mwanakijiji1:Nimesikia twa! Kisha kishindo kikubwa sana(akihema hema) Nikaambia kuna mlipuko tukimbie.Lilio la muhimu ni kuyaokoa maisha ya majeruhikwa kuwapa huduma ya kwanza.Tuondoeni miili ya waliofariki kwanza.hatuwezi kuishika miili iliyobanwa katika gari hadipolisi wafike. Na ndio hao wanaokuja!(akikimbia) Ndio hao! Acheni kuiba mafuta! Polisiwanakuja!Wakitawanya wananchi walioliparamia gari kuibaPolisi:bidhaa mbali mbali.Liinueni hili gari! Wapi dereva?(ambaye amelala akihema kwa maumivu, damuikichuruzika miguuni na mikononi) Nilisitishwa naDereva:ng'ombe waliokuwa wakivuka barabara. Nilijsribukukwepa lakini usukani ukanishinda gari likapotezamwelekeo Alikuwa akiendesha gari kwa kasi sana. TukampigiaAbiria:kelele apunguze mwendo lakini hakutusikia.Matunda yake Niliona gari likibingiria mara kadhaa mpakaMwanakijijilikaingia humu mtaroni, ndiyo tukakimbia2:kuwaokoa.Nyamazeni! Achieni polisi kazi iliyobaki. IkiwaPolisi:kuna yeyote anayejuana na waathiriwa aandamanenasi.Sajili ya NyumbaniHii ni lugha inayotumiwa na watu katika familia. Wanaohusikasana katika mazungumzo ya nyumbani ni mama, baba, watoto,majirani na watu wa ukoo. Maswala yanayorejelewa sana ni yaleyanayoiathiri jamii/boma hilo.Sifa za Sajili ya NyumbaniSifa za sajili ya nyumbani hubadilika kulingana na madainayorejelewa, wanaozungumza na hali katika boma.Mfano wa Sajili ya NyumbaniBaba: Mama Kadara! Huyo mtoto wako amekuja?Mama: Kadara ni mtoto wetu; mimi na wewe.Hapana! Mimi sizai malaya. Huyo ni wako. Hata Bahati niBaba:wako! Hakika wote sita ni wako Mume wangu unanifanya nikasirike bure tu. MbonaMama:umeanza mafarakano tena.Mafarakano! Mafarakano! Ni mimi niliyekwambia uzaeBaba:wasichana sita Mama: Lakini sikuzaa pekee. Tulizaa na wewe, mume wangu .Hapana! Uliniona na mimba? Uliniona na maumivu yauzazi? Umeniona nikinyonyesha mtoto? Mwanamke kuwaBaba:na adabu. Nitakurudisha kwa wazazi wakufunze heshima.Na nitaoa sioni tukikaa pamoja.(baada ya kimya) Niambie ulichotaka kuniambia kuhusuMama:Kadara (akijipangusa machozi kwa kitambaa) unajuaPage 5 of 42

mume wangu, nakuheshimu. Yangalikuwa mapenzi yangutungepata wavulana pia. Lakini haya ni mapenzi yaMungu.Kadara akija umpe kuku apeleke vileoni kwa MzeeMagoti. Nina deni lake kubwa baada ya kunywa temboBaba:siku kadhaa bila kulipa. (akicheka) Hakika hata anastahilimbuzi.Hatuwezi kulipia pombe kwa mbuzi wala kuku. KukuMama: waliobaki hapa ni wangu na wa watoto wangu. Kukuwako uliwauza.Kelele za chura hazimkatazi ng'ombe kunywa maji.Baba: Endelea kupayuka kama wanawake wengine wa kijijini.Nikirudi nikute chakula na maji moto tayari.Mama: (akinuna) Haya nimesikia.Mfano wa Sajili ya SimuSajili ya SimuSajili ya BiasharaHii ni lugha inayotumiwa katika mazungumzo ya simu.Lugha ya biashara huzungumzwa na wauzaji na wanunuzi katikasehemu za kibiashara. Inapaswa ikumbukwe kwamba lugha hiiinaweza kubadilika kidogo kulingana na mazingira. Kwa mfano,katika mikutano ya kibiashara, lugha rasmi hutumiwa ilihalikatika soko, lugha ya mitaani inaweza kutumika.Sifa za lugha ya simu1. Mazungumzo ya simu ni mafupi, hutumia sentensi fupizenye muundo rahisi.2. Hoja hutajwa moja kwa moja bila maneno mengi kwani ilikudhibiti gharama ya simu3. Huwa na kukatizana kwa maneno kati ya wazugumzaji.4. Huwa ni mazungumzo baina ya watu wawili pekee;anayepiga na anayepokea.5. Hutumia istilahi maalum za lugha ya simu kama neno'hello'6. Huchanganya ndimi (kutumia maneno yasiyo ya lughanyinginezo) ili kuwasilisha ujumbe kwa upesi.7. Ni lugha ya kujibizana.Sera: Hello. Ningependa kuongea na Mika.Sauti: Subiri kidogo nimpatie simu.Sera: HelloMika: Hello. Sema Sera. Niko kwa mkutano Sera: Pole kwa kukusumbua. Unakumbuka safari yetu ya kesho?Mika: Siwezi kusahau. Tunakutana saa ngapi?Sera: nampendekeza saa tano machana Mika: Katika Hoteli ya Katata MaaSera: enhe. Hapo kwa heriMika: Haya. Bye!Sifa za Lugha ya Biashara1. Hutumia msamiati wa kibiashara kama vile:o Fedhao Faidao Hasarao Beio Bidhaa2. Hutumia misimu ili kuwavutia wanunuziPage 6 of 42

3. Ni lugha yenye malumbano hasa watu wanapojadilianakuhusu bei4. Ni lugha legevu - haizingatii kanuni za lugha.5. Huchanganya ndimi kwa kuingiza maneno ya lugha zakigeni6. Ni yenye heshima na unyenyekevu kwa wanunuaji7. Msamiati katika lugha ya KibiasharaMfano wa Sajili ya tu kwa mia! Tatu kwa mia! Leo ni bei ya hasara!Unauza hii briefcase kwa pesa ngapi?Hiyo ni seventy bob mtu wanguHuwezi kunipunguzia. Niuzie hamsini hivi.Haiwezekani mtu wangu. NItapata hasara nikiuza hivyo.Ongeza mkwaja, mama.Basi hamsini na tano.Tafadhali ongeza kitu kidogo. Unataka nikule hasara leo?Fikisha sitini na tano.Basi sitanunua hii. Sina pesa hizo zote. Unajua uchumi nimbaya siku hizi.Tafadhali mtu wangu. Huu mkoba ni mzuri sana. UmetokaGermany. Angalia. Unaweka pesa hapa, kitambulisho hapaMtu halafu unafunga hivi. Hauwezi kupoteza chochote ukiwa naX: mkoba huu. Angalia wewe mwenyewe. Hakuna mahalipengine utaweza kununua mkoba huu kwa bei ghali kamahii.Mtu Nimekwambia sina hizo pesa. Nitanunua baadayeY: ukipunguza bei.Mtu Lete sixty bob. Lakini utakuwa umeniumiza. NakufanyiaX:MtuY:MtuX:hivyo kwa kuwa wewe ni customer poa.Sawa basi nitanunua. Shika sixty bob.Asante Customer. Mungu akubariki. (akimfungia) Hey! Tatukwa mia. Bei ya hasara! Tatu kwa mia!Sajili ya BungeniHii ni lugha inayozungumzwa wakati wa kikao cha bunge. Sajilihii ni tofauti na na sajili ya siasa, ambayo huhusisha wanasiasawakipiga kampeni.Sifa za Lugha ya Bungeni1. Ni lugha yenye ushawishi – wabunge hutumia vishawishiili kuwahimiza wenzao waunge ama kupinga msalaba2. Ni lugha ya mjadala yenye waungao na wapingao.3. Ni lugha yenye heshima na nidhamu. Maneno ya heshimakama mheshimiwa, tafadhali na samahani hutumika sana.4. Hutumia maneno maalum yanayopatikana katikamazingira ya bunge kama vile kikao, mswaada, kuungamkono, kujadili, kupitisha, n.k.5. Lugha ya bungeni ni rasmi na sanifu.6. Hulenga maswala mbalimbali ya kisiasa na maendeleokatika taifa.7. Huwa na maelezo kamilifu8. Ni lugha yenye maswali na majibu miongoni mwawabunge.Mfano wa sajili ya BungeniSpika:Waheshimiwa, muda unayoyoma. Nawaomba mfanyemazungumzo yenu sauti ya chini tumsikize huyu.Page 7 of 42

Endelea mheshimiwa.Asante Bwana spika. Hii siyo mara ya kwanza yakuuwasilisha mswaada huu hapa. Kila mbungeanayethamini raia wa taifa hili ni lazima auunge mkonoMbungemswada huu. Katika kikao kilichotangulia, mliupinga1:mkidai kwamba hauna heshima kwa rais. Leo tumefanyaukarabati wote mliotaka. Hamna budi kuuunga mkono.Bwana spika .Muda wako umekwisha tafadhali keti. Wabungewataamua hatima ya mswada huu ikiwa utapitishwaSpika:kama sheria. Lakini kumbukeni uamuzi wa mwisho niwa rais.Sajili ya HospitaliniSifa za Lugha ya HospitaliniKichwa kilianza kuniuma jana jioni baada ya chajio.Mgonjwa: Nilipoamka asubuhi nikatambua kwamba hata tumbolilikuwa likiuma pia.Ulipoanza kuumwa na mwili mzima, ulichukua hatuaDaktari:gani? Hukunywa dawa yoyote?Nilichukua tembe zilizokuwa zimepatiwa kakanguMgonjwa:miaka mitano iliyopita alipokuwa akiumwa na malaria.Kila ugonjwa unahitaji matibabu mbalimbali. Tembeza malaria haziwezi kutumika kutibu maumivu yaDaktari: kichwa na tumbo. Pia ni hatari kutumia dawa ambazozimepitwa na wakati. Zinaweza kukuletea madharazaidi.(akikohoa) Sijui kama una tembe za kifua pia. HiiMgonjwa:baridi inaniletea homa mbaya.Hatuwezi kukupatia dawa kabla ya kutambua ugonjwaulio nao. Itabidi tupime joto lako, damu na pia mateDaktari:yako ili kupata tatizo linalokusumbua. Kishatutakupatia dawa. Je, una umri wa miaka mingapi?Mgonjwa: Nikichukua hizo dawa nitapona?Matokeo hubadilika kutoka kwa mgonjwa mmoja hadimwengine. Inaweza kuchukua muda. Huenda ukalazwaDaktari:kwenye wadi kwa siku mbili tatu hivi. Umri wako,mama?1. Hutumia msamiati wa hospitalini kama vileo dawao magonjwao Daktario Wadio Mgonjwao Dawao Kipimo2. Ni lugha yenye upole na heshima3. Huwa na maswali mengi hasa daktari anapotaka kutambuaKatika sajili ya kidini tunaangazia lugha inayozungumzwa nakiini cha ugonjwa unaomhadhiri mgonjwa wakewaumini/washiriki wa imani fulani wakati wa ibada, sala, katika4. Ni lugha yenye hofu na huzuninyumba takatifu au mahali popote pale ambapo wanazungumziamambo yanayorejelea imani au Mwenyezi Mungu.Sajili ya KidiniMfano wa Sajili ya HospitaliniDaktari:Ulianza kuumwa hivi lini?Sifa za Lugha ya KidiniPage 8 of 42

1. Hutumia msamiati wa kidini kama vileo Bibiliao maombio mbingunio jehanamuo Madhabahuo Paradisoo Mbingunio Mwenyezi Munguo Mwokozi2. Ni lugha inayonukuu sana hasa wazungumzajiwanaporejelea Kitabu kitakatifu3. Lugha yenye heshima, upole na unyenyekevu4. Lugha sanifu5. Ni lugha iliyojaa ahadi nyingi kwa wanaoandamana namafunzo ya kidini na vitisho kwa wanaoenda kinyume namafundisho6. Huwa imejaa matumaini7. Ni lugha yenye kutoa maneno ya sifa, kumtukuza nakumshukuru Mwenyezi MunguMfano wa Sajili ya KidiniBoriti: Bwana asifiwe Bi.BiAmina, mchungaji. Watoto wanaendeleaje?Rangile:Karita hana neno. Mwenyezi Mungu ametunyesheaBoriti:rehema na neema zake. Je, wajukuu wako wa hali gani?BiWanaendelea vizuri isipokuwa hawataendelea naRangile: masomo. Sijui nilimfanyia Mungu dhambi gani.Nasikitika sana kusikia hivyo. Mungu atawalindaBoriti: mayatima hao. Yeye ndiye baba wa mayatima. Munguni mwenye huruma.BiSijui hayo, mchungaji. Hata sijui maana ya kuishi hapaRangile: duniani. Kila siku ni matatizo.Boriti: Usife moyo. Mungu anasema katika kitabu cha Yohana14:18, "Sitawaacha nyinyi kama mayatima." Kwahivyo, ukiwa na imani, Mungu atakuonekania.BiBasi niombee mchungaji ili Saumu na Neema wapateRangile: karo ya kurudi shuleni.Funga macho tusali. Ewe Rabuka uliyejaa neema nabaraka tele. Tunakushukuru na kulitukuza Jina lakotakatifu kwa baraka zako za ajabu. Tunajua kwambaBoriti: wewe ndiye Mungu uliyewatoa wana wa Israeli kutokaMisri. Sisi wenye dhambi tunakuja mbele yakotukiomba ukafanya miujiza katika nyumba hii ya BiRangile.Wote: Amina.Sajili ya MahakamaniHii ni lugha inayozungumzwa na wanasheria, mahakimu,mawakili, washitakiwa na mashahidi katika mahakama.Sifa za Lugha ya Mahakamani1. Hutumia msamiati wa kipekee unaorejelea sheria kamavileo katibao sheriao mashtakao Hakimuo Ushahidio Wakilio Jelao MshitakiwaPage 9 of 42

o Kiongozi wa mashtakiwaikiwa ni yeye mwenyewe au ikiwa ni rafiki yake.2. Huwa na maelezo marefu na ya kina ili kutafuta ushahidiHivyo basi jaribio la kujiua ni hatia kulingana nawowote uliopokanuni za nchi hii. Una jingine la kuulizia?3. Ni lugha yenye kunukuu sana hasa vipengele katika vitabuJe, sheria yetu inaruhusu mtu kuadhibiwa kwa kosaKisaka:vya sheria kama vile katibaambalo hakufanya?4. Ni lugha rasmi na sanifuKiongozi: La hasha.5. Ni lugha iliyojaa maswali na majibizanoBasi tutakuwa tumekiuka kanuni za nchi yetu iwapo6. Ni lugha yenye heshimaKisaka: tutamhukumu Musa kwa kujiua ilhali hakujiua bado.Tunawezaje kutambua kama angekufa?Mfano wa Sajili ya MahakamaniInafaa ahukumiwe kinyonga au kifungo cha maishaKatili:gerezani. Hata alivunja simu yangu.Musa Kasorogani, mwanaye Bi Safina na MzeeOrder! Lazima kutii mpangilio wa mahakama. KatiliMpotevu Kasorogani; umeshtakiwa kwa kosa la jaribioKiongozi: hauruhusiwi kuongea bila ruhusa ya hakimu auKiongozi: la mauaji mnamo tarehe 23/08 mwaka huu. Unawezakiongozi wa mashitaka. Polisi, mpelekeni nje.kukubali mashitaka, kukana au kunyamaza. Je,unakubali mashitaka.Musa:Naomba kukanusha mashtaka hayo, bwana mkubwa.Kiongozi: Je, kuna shahidi yeyote katika kesi hii?Hapa mkubwa. Siku hiyo ya tarehe 23/08, Musaalipatikana akiwa akijinyonga usiku wa maneno. Kijijichote kilikusanyika hapo kwenye boma ya Kasorogani. Lugha ya michezoni hutumiwa wakati wa mashindano yaKatili:Nilipoleta polisi, wakamkamata na kumpelekamichezo kama vile kandanda, ukimbiaji n.k Hii inaweza kuwahospitalini atibiwe kwanza. Ndiposa ameletwa hapalugha ya watangazaji/wasimulizi wa mchezo, watazamaji,siku ya leo.mashabiki au wachezaji.Je, mshitakiwa una tetesi lolote. Ama pia unawezaKiongozi:kuleta wakili wako azungumze kwa niaba yako.Sifa za Lugha ya MichezoniBwana mkubwa, mimi ndiye wakili na shahidi waMusa. Musa hakuua mtu. Alikuwa akijinyonga1. Hutumia msamiati wa kipekee unaohusu michezo kamakutokana na mkasa uliomfika tarehe hiyo ya Agosti 23vile mpira, goli, mchezajibaada ya bibi harusi wake kubadilika. Mimi na2. Huchanganya ndimi na kuingiza maneno ya lughaKisaka:mamake, Bi Safina Kasorogani tulijaribu kumtulizanyingine kama vile Kiingereza. mfano 'goal!!!'jioni hiyo. Asubuhi nilipoamka siku iliyofuatia,3. Ni lugha ambayo hutumia vihisishi na mshangao kwanikapata habari kwamba alikuwa amepelekwawingihospitalini. Je, alipojaribu kujiua, alimwua mtu yeyote?4. Sentensi nyingi katika lugha hii huachwa bila kukamilikahasa hali inapobadilika uwanjaniKulingana na katiba ya nchi hii, kifungu cha 12.ab,Kiongozi:kuua ni kutoa uhai wa binadamu yeyote. HaijalishiSajili ya MichezoniPage 10 of 42

5. Husimuliwa kwa haraka haraka ili kuambatana na kasi yamchezo6. Ni lugha yenye sifa na na chuku kwa mfano msimulizianaposimulia sifa za mchezaji fulani7. Hutumia misimu kama vile 'wametoka sare'8. Hutumia kwa ya kulinganisha ili kuelezea matokeo yamechi k.m 'walitoka mbili kwa nunge'9. Ni lugha yenye kukariri (kurudia rudia) hasa mchezajianapoumiliki mpira kwa muda mrefu au mwanariadhafulani anapoelekea kushinda katika mbio.10. Huwa na sentensi fupi fupikwamba unapata matangazo haya moja kwa moja kupitia idhaayako uipendayo, redio nambari moja kote nchini. Mpiraunarudishwa uwanjani. Akienda kuurusha pale ni.Sajili ya MtaaniMfano wa Sajili ya MichezoniNakwambia ndugu msikilizaji hapa mambo yamechachakwelikweli. Hawa wachezaji wa Manyuu hawacheki na watu leo.Wameamua kuishambulia timu ya Cheusi bila huruma. Kumbukakwamba hii ni mara yao ya. Lo! Anauchukua mpira pale,mchezaji nambari tisa. Matiksta. Matiksta, Matiksta na mpira.Anaucharazacharaza pale. Anamwangalia mwenzake. Anaupigampira kwa kichwa pale! Lo! Mwenzake anaukosa. Akiushikampira pale ni mchezaji wa timu ya Cheusi, Romana. Romana,Romana anaelekeza mpira kwenye lango la Manyuu. Anaupigampira kwa nguvu! Lo! Hatari sana. Hatari sana katika lango laManyuu. Hatari! hatari! Gooooaaaaaal! Noooo ooh! Wameukosa!Goal keeper ameudaka mpira huo. Pole sana wachezaji wa .Mlinda lango anaupiga mpira huo kwa hasira. Juu kabisa.Anauchukua pale nambari saba, Saruta. Huyu ni mchezajimachahari sana. Mwaka uliopita, alipewa tuzo la mchezaji borawa mwaka. Ananyang'anywa na mchezaji mwingine hapa.Wanakabiliana kidogo. Huyu mchezaji anaupiga mpira kwa mguuwa kushoto. Lo! Mpira umekuwa mwingi na ukatoka nje.Mashabiki wa timu hizi mbili wanasubiri kwa hamu na ghamukutambua ni nani atakayeibuka mshindi. Katika mechizilizotangulia, timu hizi zimekuwa zikitoka sare. Lakini leolazima mshindi atapatikana. Hawa ni fahali wawili. KumbukaLugha ya mitaani ni lugha inayozungumzwa na vijana mtaani.Sifa za Lugha ya Mtaani1.2.3.4.Ni lugha legevu isiyozingatia kanuni za kisarufiHuchanganya ndimiHutumia misimu kwa wingiHukosa mada maalumMfano wa Sajili ya MtaaniChali: Hey, niaje msupaa?Katosha: Poa. So, mathee yako alikushow naweza kuja?Chali: Ha! Masa hana noma. Si unajua nita.Katosha: Chali! Unataka aniletee problem?Mimi ni boy wa maplans. Ngoja nifikirie venyeChali:tutamshowNa by the way, kwani umejipaka mafuta ya manzi. AmaKatosha:ulikuwa na msichana mgani?Chali: Oh! Niliscoop mafuta ya Anita. Si unajua natakaPage 11 of 42

kunukia hmmmm.Ok. So, umefikiria tumshow nini masa yako? AmaKatosha:nikona idea poa.Nishow hiyo plot, na by the way, nataka unisaidieChali:kuhusu ile deal yangu na Kaunda. Ile ya siz yangu.Kwanza tutaplan na huyo siz yako, niwe ndiye nimekujaKatosha:kuvisit. Mamako atakubaliWow! Idea poa. Utakuwa umekuja kufanya homework.Chali: Halafu masa akiishia kwa bed. Homework tutaitupambali.Katosha: So, utamshow Anita nakuja tufanye homework.Sajili ya KisayansiKwanza, viluwiluwi, ambao ndio tunaotafiti wamekuwa habasana wakati huu wa ukame. Pili, kutokana na kufungwa kwamaabara ya kisayansi katika taasisi hii, ni muhali kufanyamajaribio yoyote ya kazi yetu. Tatu, kumekuwa na pingamizikubwa kutoka kwa baadhi ya wanakijiji kwamba kukusanyaviluwiluwi kunawatia hofu. Aidha, tume yetu imepungukiwa nafedha baada ya serikali kusitisha kudhamini utafiti huu.Baada ya kujadiliana kwa vikao tatu mfululizo, tume yetuinapendekeza haya: Muda wa kufanya utafiti uongezewe kwakipindi cha miezi sita; serikali kupitia kwa taasisi hii ifadhiliwachunguzi. Wananchi wahamasishwe kuhusu umuhimu wakuwafanyia viwavi utafiti na maabara ya utafiti ikaraatiwe harakaiwezekanayo.Sajili ya ShuleniSifa za Lugha ya Kisayansi1. Hutumia msamiati wa kipekee unaoambatana na taalumainayorejelewa.2. Huwa na maelezo kwa ukamilifu.3. Huwa na mpangilio maalum na maendelezo ya hoja naujumbe.4. Huchanganya ndimi na kutumia maneno ya kisayansi aulugha mbalimbali.5. Hutumia lugha sanifu.6. Ni lugha yenye udadisi mwingi (wakati wa kufanyautafiti)Mfano wa Lugha ya KisayansiKwa sababu zisizoweza kuepukika, kikundi chetu hakitamalizautafiti ulioratibiwa kukamilishwa mwishoni mwa mwezi ujao. Hiini kwa sababu ya changamoto kadhaa ambazo tumekutana nazo.Hii ni rejista ya lugha inayopatikana katika mazingira ya shule.Wahusika wake huwa walimu, wazazi na wanafunzi.Sifa za Sajili ya Shuleni1. Matumizi ya istilahi (maneno maalum) yanayopatikanakatika mazingira ya shule kama vile darasa, mitihani,vitabu, elimu, muhula, masomo2. Lugha yenye heshima kutokana na utofauti baina yamwanafunzi na mwalimu, mzazi na mwalimu;3. Takriri - mbinu ya kurudiarudia maneno. Katika darasamwalimu hurudia rudia maneno ili kusisitiza anachofunza4. Ni lugha yenye maswali mengi na majibu. Mwalimuhuuliza maswali wakati wa mafunzo. Wanafunzi piahuuliza maswali ili kujua/kupata ufafanuzi.5. Hutumia lugha ya kukosoana na kurekebishana.Page 12 of 42

Mfano wa Mazungumzo katika Sajili yaShulenia) Mazungumzo kati ya Mzazi na MwalimuToeni vitabu vyenu vya Historia mnakili haya. NiMwalimu: nani atakayetukumbusha tulichosoma wiki jana?Naam Halima!Halima:Tulisoma kuhusu Chama cha Mapinduzi(Wakiinua mikono na kupiga kelele) MwalimuWanafunzi:MwalimuInueni mikono nitawaona. Msipige kelele. HalimaMwalimu:umenoa. Simama! Mwanafunzi mwengine?Tulisoma kuhusu kundi asi la Maji Moto lililopingaJadaha:wakoloni.Wanafunzi: Mwalimu! Mwalimu! Kundi la Maji Maji.Naam mmepata. Lakini nimewaambia msijibu kwapamoja. Ukitaka kujibu uinue mikono. Jadaha, nikundi la Maji Maji siyo Maji Moto. Leo tutasomaMwalimu: athari za kundi katika taifa letu la Tanzania na namnalilivyoshindwa nguvu. Lakini kabla hatujaendeleaningependa mniambie, ni matatizo yepiyaliyochochea kuchipuka kwa kundi hilo.Mwalimu nina swali. Kiongozi wa kundi hilo alikuwaKirata:nani?Kirata hukuwa darasani wiki jana. Nione baada yakipindi hiki. (wanafunzi wakicheka) Nawe wafanyaniMwalimu: na kitabu cha Hisabati katika somo la Historia.Kimbia ofisini uniletee kiboko. Ninyi ndiomnaorejesha nyuma darasa langu katika mitihani.Mzee Kundu, ningetaka tuzungumze kwa mudakuhusu hali ya mwanao, Machome Kundu.Machome? Ana nini mwanangu. Kuna nafasiMzee:imepatikana ya Mwanako amebadilika sana kitabia. Alikuwa akifanyaMwalimu:vizuri sana katika masomoKweli kabisa. Mimi ni mlezi mwema sizai watoto mbuMzee:mbu mbu darasani.Ndivyo. Lakini sasa naona ameanza kubadilika.Mwalimu:Ameanza kulegea katika mitihani na kuzembea kazini.Unamaanisha nini? (akiinuka) Inaonekana siku hiziMzee:hamjui kuwapa adabu watoto. Ni lazima mtoto wanguamepotoshwa na wengine, katika vikundi vibaya!Hakika, mwanako ndiye anayepotosha wanafunziwengine. Yeye ni kiongozi wa makundi haramushuleni, yanayovuruga masomo, kuuza dawa zaMwalimu:kulevya na mambo kama haya. Hii ndiyo sababunimekuita tujadiliane. Ni lazima mienendo hiiimechipuka nyumbani.Ajapo nyumbani, mwanangu huzingatia vitabu pekeeMzee:hata mamake anaweza kuthibitisha haya. Ikiwa kunautovu wa nidhamu nina hakika haya yanatoka darasani.FASIHI SIMULIZITafadhali keti mzee (akichungulia dirishani) Mtindi!Mwalimu:FasihiUtanzu waNiitie Machome Oral LiteratureKiingerezab) Mazungumzo katika Sajili ya Darasani Hadithi / NganoTanzu za Fasihi NyimboSimuliziMwalimu:Fasihi SimuliziPage 13 of 42

MaigizoTungo FupiTamathali za UsemiPrevFasihi AndishiNextVIPERA VYA TANZU ZA FASIHI SIMULIZI Khurafa Hekaya Mighani / Visakale Usuli / VisaviiniHADITHI / NGANO Visasili Hadithi za Mtanziko Hadithi za MazimwiNYIMBO MashairiKimaiWawe/HodiyaNyimbo za NdoaNyimbo za KidiniNyimbo za KisiasaZa Tohara/JandoniNyimbo za Kizalendo MethaliVitendawiliMafumboVitanza Ndimi na VichezeaManenoSemiLakabuMisimu Michezo ya KuigizaNgomeziMivigaTUNGO FUPIMAIGIZO Malumbano ya i Simulizi ni utanzu wa fasihi ambao unawakilisha sanaa yalugha inayopitishwa kutoka kwa kizazi hadi kizazi kwa njia yamaneno/masimulizi ya mdomo.Sifa za Fasihi Simulizi1. Hupitishwa kwa njia ya mdomo2. Ufanisi wa sanaa katika fasihi simulizi hutegemea uwezowa msimulizi, au wahusika3. Masimulizi yake yanaweza kuathiriwa na mazingira, hisiana hali4. Ni mali ya jamii. Hakuna mtu fulani anayemiliki sanaakatika fasihi simulizi.5. Inaweza kubadilika kutoka kizazi hadi kizazi, aumazingira mbalimbali kwa sababu hutegemeakumbukumbu ya msimulizi.6. Aghalabu huwa na funzo fulaniUmuhimu wa Fasihi Simulizi1. Kuburudisha - Hufurahisha na kuchangamsha hadhira2. Kunasihi- kutolea mawaidha na kuonyesha mwelekeounaotarajiwa katika jamii3. Kuelimisha watu kuhusu vitu mbalimbali hasa mazingirayao4. Kutambulisha jamii - jamii mbalimbali husifika kutokanana sanaa zao katika fasihi simulizi kama vile nyimbo5. Kuhifadhi na kudumisha utamaduni wa jamii6. Kuunganisha watu - huleta watu pamojaPage 14 of 42

7. Kukuza lugha - fasihi huimarisha lugha kwa kuwahutumia mbinu mbalimbali za lugha.8. Kuliwaza - hutoa huzuni na kuleta matumaini.9. Kupitisha muda - wakati mwingine fasihi simulizihutumika kupitisha muda.Ngano Katika Fasihi SimuliziHADITHI / NGANOFasihi SimuliziUtanzu waNarrativesKiingereza Khurafa Hekaya Mighani / Visakale Usuli / VisaviiniVipera vya Hadithi Visasili Ngano za Mazimwi Ngano za MtanzikoPrev Sifa za Mtambaji wa HadithiVipera vya NganoTunaweza kuainisha ngano kulingana na vipengele vifuatavyo:1. Wahusika k.v khurafa, hekaya, mighani, mazimwi,2. Maudhui k.v usuli, visasili, mtanzikoUtanzu huu wa fasihi simulizi umegawanyika katika vipera ezea chanzo

kila lugha hutumia mfumo fulani wa sauti mahususi katika lugha hiyo pekee. 5. Fonetiki - huchunguza sauti zinazotamkwa na binadamu bila kuzingatia lugha yoyote. 6. Mofolojia - (au sarufi maumbo) ni tawi la isimu linalochunguza maneno ya lugha fulani, aina

Related Documents:

Chatham County Chattahoochee County Chattooga County Cherokee County Clarke County Clay County Clayton County Cobb County Coffee County Colquitt County Columbia County Cook County Coweta County Crisp County 320 6 2 1 2 4 1 10 12 6 4 43 1 1 3 2 4 11 4 1 5 6 6 5 60 1 1 7 22 1 58 51 7 3 8 4 6 5 19.80% .37% .12% .06% .12% .25% .06% .62% .74% .37% .

adams county 376,750 alamosa county 18,435 boulder county 23 costilla county 334 delta county 464 jackson county 28,172 jefferson county 50,160 lake county 762 larimer county 522 mesa county 60 moffat county 12,075 rio grande county 24,304 saguache county 33,128

1.1.3 WordPress.com dan WordPress.org WordPress menyediakan dua alamat yang berbeda, yaitu WordPress.com dan WordPress.org. WordPress.com merupakan situs layanan blog yang menggunakan mesin WordPress, didirikan oleh perusahaan Automattic. Dengan mendaftar pada situs WordPress.com, pengguna tidak perlu melakukan instalasi atau

Data Profile for Orange County 2018-1003 1. Orange County 140,853 County average in NC 56,087 a Source: 2. Orange County 398 County average in NC 463 a Source: 3. Orange County 6 County average in NC 6.7 c Source: 4. Orange County 1 Source: 5. B Orange County 45,190 County average in NC 34,568 a Source: 6. B Orange County 3 County average in .

Ansbach Middle High School Ansbach Germany Baumholder Middle High School Baumholder Germany . Lee County High School Sanford NC Lugoff Elgin High School Lugoff SC North Brunswick High School Leland NC . Liberty High School Bealeton VA . Mallard Creek High School Charlotte NC Mount Tabor High School Winston Salem NC Myers Park High School .

300 Amite County School District 4821: Amory School District 400 Attala County School District 5920: Baldwyn School District . Tate County School District 7100 Tishomingo County Schools 7200. Tunica County School District 4120 Tupelo Public School District 7300. Union County School District 5131 Union Public School District 7500.

Data Report C.S. Hardaway, Jr. D.A. Milligan G.R. Thomas C.A. Wilcox . James City County, King and Queen County, King George County, Middlesex County, New Kent County, Newport News, City of, Prince George County, Richmond County, Stafford County, Surry County, Westmoreland County, and York County . The p

Millikan High School Murrieta Valley High School Palisades Charter High School . Samueli Academy School of Business and Tourism South High School View Park Preparatory Charter HS Florida Apollo Middle School Cooper City High School Coral Springs High School Cypress Bay High School . Morris Knolls High School The