NADHARIA ZA CHIMBUKO LA NGANO/MASIMULIZI

3y ago
720 Views
4 Downloads
396.69 KB
9 Pages
Last View : 11d ago
Last Download : 3m ago
Upload by : Bennett Almond
Transcription

NADHARIA ZA CHIMBUKO LA NGANO/MASIMULIZIKazi hii tumeigawa katika sehemu tatu, ambazo ni, Utangulizi, katika sehemu hii tutatoa fasili yanadharia na fasili ya ngano kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali. Sehemu ya pili itakuwa nikiini cha swali ambapo tutajikita kuzielezea nadharia mbalimbali zinazozungumzia asili ya fasihisimulizi/masimulizi kwa mujibu wa Okpewho (1992), Miruka (1994/1999) na Finnegan (1970).Na sehemu ya mwisho ni hitimisho.Tukianza na fasili ya Nadharia, Massamba (2009:63) anasema, nadharia ni taratibu kanuni namisingi ambayo imejengwa katika muundo wa kimawazo kwa madhumuni ya kutumiwa kamakielelezo cha kuelezea jambo. Sarantakos (1997: 9) amefasili nadharia kama jambo linalofanywana kuthibitishwa kwa utaratibu maalum kwa njia ya utafiti kwa ajili ya kuelezea jambo fulanikatika jamii. Martin E. Amini (2005:10) anasema nadharia ni jumla ya mambo yote ambayomtafiti amekusudia kuelezea, kuchambua, kuelewa au hata kutabiri jambo fulani kwa utaratibumaalum.Hivyo basi, nadharia huchukuliwa kama dira au muongozo wa kumuongoza mtafiti/mchambuziili kulielezea vema jambo fulani kwa mtazamo unaotarajiwa kuwa imara zaidi kuliko mtazamomwingine. Hivyo tunaweza kujumuisha kuwa nadharia ya fasihi simulizi ni chombo kinachotoamwongozo kuhusu mwelekeo wa jamii fulani.Maana ya nganoSenkoro (2011:53) anasema, ngano ni utanzu wa kifasihi simulizi ambao ulipitishwa toka kizazikimoja hadi kingine kwa njia ya mdomo.King’ei (2005:65) anasema ngano kuwa ni hadithi fupi na zenye masimuliziyasiyoyakishairi. Kwa upande wake,Wamitila, K.W. (2003:165) anasema ngano ni hadithi ya kaleambayo ni moja kati ya tanzu maarufu za fasili simulizi. Ni moja kati ya vipera au vitanzu vyahadithi au simulizi. Ngano nyingi huwa na mwanzo wa hapo zamani za kale.Kwa fasili yetu, tunaweza kusema kuwa, ngano ni utanzu wa hadithi fupi fupi ambazohuelezea/kusimulia matukio mbalimbali yanayoleta mafunzo katika jamii husika na kurithishwakutoka kizazi kimoja hadi kingine.1

Baada ya kuangalia fasili mbalimbali za nadharia na ngano, sehemu inayofuata ni kuzielezeanadharia mbalimbali zinazozungumzia asili ya fasihi simulizi/masimulizi kwa mujibu waOkpewho (1992), Miruka (1994/1999) na Finnegan (1970). Tukianza na Okpewho (1992)ameanisha aina sita za nadharia zinazoelezea asili ya fasihi simulizi/masimulizi ambazo ni,nadharia ya mabadiliko, nadharia ya msambao, nadharia ya uamilifu, nadharia ya urasimi,nadharia ya Saikochanganuzi na mwisho ni nadharia ya Umuundo. Kwa upande wake, Miruka(1994) ameanisha aina tano za nadharia ambazo ni, nadharia ya Mabadiliko, nadharia yamsambao, nadharia ya urasimi, nadharia ya uamilifu na nadharia ya umuundo, wakati Finnegan(1970) ameanisha aina tatu za nadharia ambazo ni nadharia ya Mabadiliko, nadharia ya msambaona nadharia ya Umuundo.Tukiangalia uanishaji wa nadharia hizo za wataalamu hapo juu, tunaona kuwa, wataalamu haowanatofautiana katika idadi ya nadharia hizo, lakini kimsingi wataalamu wote wanakubalianakuhusu nadharia fulani fulani, mathalani, wote wanakubaliana uwepo wa nadharia yamabadiliko, nadharia ya msambao na nadharia ya umuundo. Lakini Okpewho na Mirukawanakubaliana juu ya uwepo wa nadharia ya mabadiliko, nadharia ya msambao na nadharia yaumuundo, nadharia ya urasimi na nadharia ya uamilifu. Okpewho anainisha aina nyingine yanadharia ya Saikochanganuzi ambayo haijitokezi kwa hao wataalamu wengine. Hivyo katikauwasilishaji wetu, tutazigawa nadharia hizo katika aina sita kama ifuatavyo:Nadharia ya wanamabadiliko, nadharia hii iliasisiwa na Charles Darwin ambaye alikuwamwana bailojia karne ya 19, alifanya utafiti kuhusu mabadiliko ya viumbe ambao waliishi kuwaviumbewalioendeleakuishi imewezekana tu kwa sababu ya kumudu mapambano dhidi ya uhaba wa vyakula, hivyoDarwin aliita jambo hili kama “Uhai kwa wanaofaa”. Pia aligundua viumbe walioendelea kuishikwa sababu ya maumbo yao na mazingira yaliyosababisha wao kuwepo.Mawazo ya utafiti wa Darwin yalishadadiwa na wanazuoni mbalimbali waliokuwawanachunguza utamaduni wa binadamu, katika utafiti wao walikusanya simulizi kutoka jamiimbalimbali za Afrika, Asia na Amerika ambapo baada ya kukusanya simulizi hizo waligundua2

zilikuwa na ufanano wa kimaudhui. Wanamabadiliko wanaamini kuwa ngano/masimulizituliyonayo leo yana asili moja isipokuwa zimekuwa zikibadilika kutokana na mabadiliko yawakati. Zaidi ya haya wanamabadiliko wanaamini kuwa viumbe wote tumetokea kwenye asilimoja hivyo tuna uwezo wa akili sawa na maendeleo tutakuwa sawa.Ubora wa nadharia hii, nadharia hii ndiyo msingi wa nadharia nyingine zilizofuata kamanadharia ya msambao, urasimi na uamilifu. Vilevile imesaidia kuelezea asili yangano/masimulizi hasa ngano zinazofanana kimaudhui, na mwisho nadharia imesaidia kuoneshakuwa ngano zina asili moja isipokuwa zinabadilika kutokana na mabadiliko ya wakati namazingira.Mapungufu ya nadharia hii, wanamabadiliko waliamini kila kilichokusanywa katika fasihisimulizi kilihesabika kama masalia ya zamani/mabaki ya fasihi zilizotangulia, kwa maanakwamba kila kitu kilichosalia kitakuwa na dosari hakiwezi kuwa kitu halisi. Wanamabadiliko piawameangalia tu upande wa maudhui na kuacha kipengele cha fani kama vile muundo na mitindoya fani husika. Mwisho, pamoja na ufanano wa huo wa kimaudhui kuwa ngano zina asili mojalakini kuna tofauti kubwa hasa katika utendaji wa fanani hivyo fanani hutofautiana.Nafasi ya nadharia hii katika ngano za Kiswahili, nadharia hii inahusiana na ngano zaKiswahili katika sanaa za jadi ambayo ni elimu inayohusu asili ya binadamu pamoja naumuhimu wake ambao ilihusishwa na usimulizi wa ngano ambayo ilitokana na jamii husikakatika shughuli mbalimbali za jamii kama vile jando na unyago, miviga, vyanzo vya vyakula,sherehe, matambiko kwa kutaja kwa uchache.Nadharia ya msambao, nadharia hii imeasisiwa na wataalamu kama Jacob na Wilhem Grimm,baadaye mawazo yao yaliendelezwa na Maxmuller na Mmarekani Stere Thomson. Pamoja nakwamba kulikuwa na tofauti ndogondogo lakini wataalamu wa nadharia hii wanamwelekeommoja ambao wanaamini kuwa chimbuko la fasihi simulizi ni moja lakini kutokana namaingiliano ya kijamii ndiyo yaliyosababisha kusambaa kwa hii ngano hasa kutoka katika jamiizilizostaarabika (Ulaya) kuja katika jamii zisizostaarabika (Afrika).3

Okpewho anasema, wanamsambao walijishughulisha na kuhusianisha ngano za jamii mbalimbalina kugundua kuwa ngano zina ufanano unaokaribiana sana. Uhusiano huu unahusishwa nakipindi cha kihistoria ambacho kulikuwa na mawasiliano baina ya jamii moja hadi nyingine.Katika utafiti wao wanamsambao wamegawanywa katika shule mbili, kwanza ni kundi la shuleya India, kundi hili lilianzishwa na Jacob na Wilhelm ambapo walikusanya hadithi mbalimbalihuko ujerumani na kwingineko barani Ulaya na kugundua kuwa ngano hizo zilikuwa nauhusiano na kuhitimisha kuwa ngano za Ulaya kama zilivyo lugha za Ulaya zimeonekana narangi ya nasaba bora iliyopata kuishi huko kati ya kaskazini na Asia, rangi ya nasaba bora sirangi ya ngozi bali ni familia ya lugha ambayo lugha zote za Ulaya zinahusishwa nayo. Hivyoaligundua kuwa ngano zilikuwa zinasambaa na makundi ya wahamiaji. Wao waliona chimbukola ngano ni huko India na zikafika huko Magharibi kwa njia ya msambao.Kundi la pili ni kundi la shule ya Kifini, shule hii ilianzishwa na Eliasi Lonnrot ambaye mwaka1825 alianza kukusanya ngano za mashujaa katika nchi ya Finland, kupitia maudhuiyanayohusiana na kuziweka katika kundi moja.Ubora wa nadharia hii, wanamsambao waliipa hadhi fasihi simulizi kwa kuchunguza muktadhakwa undani, vilevile, nadharia hii ilionekana kuwa ni ya kisayansi zaidi, hivyo inawezakuchunguzika tofauti na wanamabadiliko kwani akili ya mtu haiwezi kuchunguzika.Upungufu wa wa nadharia hii, kufikiria kuwa ngano zimeenea toka kundi moja la watu hadikundi jingine, inaonesha kuwa jamii ya Kiafrika haikuwa na ngano. Nadharia hii inaona kuwaAfrika haikuwa na ngano kwani ngano zilitoka katika jamii zilizostaarabika (Ulaya) jamboambalo si kweli kwani hata kabla ya ujio wa wakoloni Waafrika walikuwa na ngano zao.Vilevile, licha ya kuipa fasihi simulizi upekee katika kipengele cha muktadha lakinihawakuchunguza kwa undani vipengele vya kisanaa vya fasihi simulizi, mfano hawakuangaliavipengele muhimu vya fasihi simulizi ya Kiafrika hususani sanaa ya jadi kama vile, miviga,jando na unyago, matambiko, n.k.4

Nafasi ya nadharia hii katika ngano za Kiswahili, ukiangalia kwa jicho la ndani nadharia hiiinasaidia kutambua kuwa mfanano wa ngano katika jamii nyingi za kiafrika ulitokana namaingiliano ya shughuli za kijamii kama vile, biashara, kilimo,ufugaji, uwindaji na kazimbalimbali za jamii.Nadharia ya umuundo, nadharia hii iliasisiwa na Claude Levis Strauses, alidai kuwa utamaduniunajumuisha vitu mbalimbali vinavyofanana, alichunguza visasili na kusema kuwa visasili hivyovinatumika katika kuelezea na kutatua matatizo katika jamii. Hadithi hizo zilikuwa zinaelezeafalsafa ya jamii husika, alidai kuwa visasili hivyo vilisaidia jamii katika kuyaelewa na kutatuamatatizo ambayo yalileta mtanziko katika maisha ya binadamu, matatizo hayo ni kama vile, uhaina kifo.Strauses, alidai kuwa muhusika wa ngano anajengwa katika kupambana na tatiziko ambaloanashindwa kulipatia majibu. Dominique Zahen aliongeza kuwa ngano zinahusu uhai na kifo naziishie kwa kuona kuwa uhai na kifo vimetoka kwa mungu (mfano: ngano inayoelezea namnakifo kilivyoingia duniani) (rejea Miruka 1994:138)Ngano zinatakiwa kutazamwa kama mfumo wenye kanuni zake ambazo kila msanii anatakiwakuelewa pia aelewe mfumo unavyoweza kutumiwa katika mawasiliano na hata kimuundo.Mfano katika ngano lazima kuangalia matumizi ya lugha na kaida zinazotawala utunzi huo.Ubora wa nadharia hii, nadharia hii inasisitiza kuwepo kwa kanuni/kaida maalumu zakiutambaji, kiutunzi na matumizi ya lugha. Hapa wanaona kuwa ngano zisichukuliwe kama kitupekepeke bali ni utanzu unaoongozwa na kaida maalumu katika uumbaji, kiutambaji namatumizi ya lugha. Hivyo kutakuwa na sifa zinazofanana katika ngano zote. Vilevile, inasaidiakujua chimbuko la ngano katika jamii fulani.Udhaifu wa nadharia hii, kwanza kwa kutumia nadharia hii hatuwezi kupata kanuni rasmi yakiutambaji, kiutunzi na matumizi ya lugha toka jamii moja hadi nyingine. Hii ni kutokana naukweli kwamba kila jamii ina namna yake ya kuwasilisha ngano zao, kuziumba ngano zao namatumizi ya tofauti ya lugha. Mfano; maumbo ya ngano yanatofautiana toka jamii moja hadi5

nyingine, mfano, muingiliano wa tanzu moja katika nyingine, utambaji pia hutofautiana, mfanowatambaji na tabaka tawala na watambaji na tabaka duni. Hata wahusika wa ngano piahutofautina mhusika anaweza kuwa mtu duni kwenda bora au mtu bora kuwa mtu duni. Nadhariahii pia inatalia mkazo muundo kuliko dhima ya ngano katika jamii.Nafasi ya nadharia hii katika ngano za Kiswahili, nadhairia inasaidia wanafasihikutambua/kuelewa ngano kama utanzu wa fasihi una muundo wake rasmi katika uumbaji,kiutambaji na matumizi ya lugha kiulemwengu lakini muundo huo si wa kimajumui kwa maanahuweza kutofautiana kutoka jamii moja hadi nyingine.Nadharia ya urasimi, nadharia hii iliasisiwa na mwanazuoni wa Kinesi Vladimir Propp(1928,1968) katika chake cha “The Morphology of the folktale.” Nadharia hii ilizuka ili kupingamawazo ya wanamsambao hususani katika ugawaji wa ngano bila kuchunguza kwa umakini sifaya kila kundi. Propp anaamini kuwa ili kuchunguza asili ya ngano ni vema kuanza kuchunguzaaina za ngano kwa kuangalia maumbo ya ngano. Hivyo mtazamo huu unaangalia asili ya nganokwa kuchunguza maumbo ya ngano husika.Ubora wa nadhairia hii, nadharia hii inasaidia kujua aina za ngano kutokana na dhima zake,mfano ngano za urafiki, miadi, ukatili, ugunduzi na mwisho wa urafiki, (Alan Dunde’s)Udhaifu wa nadharia, nadharia hii inaonekana kutomzingatia mtambaji ambaye ni sehemu yangano yenyewe ambaye anaweza kubadilisha umbo la ngano kadri ya utendaji wake.Nafasi ya nadharia hii katika ngano za Kiswahili, nadharia hii inatusaidia kuziweka ngano katikamakundi kutokana na kazi zake. Mfano tunapata ngano zinazohusu wahusika wajanja mfanosungura na wahusika wasiowaelevu/wajinga mfano fisi.Nadharia ya saiko-changanuzi, muasisi wa Nadharia hii ni Sigmund Freud raia wa Australia,mtaalamu huyu alikuwa tabibu wa magonjwa ya akili, alifanya uchunguzi wa nafsia, alichunguzahasa sehemu ya nafsi iliyofichika yaani sehemu ya ung’amuzi bwete ili kujua asili ya tatizo lamgonjwa husika, alieleza kuwa ung’amuzi bwete ni sehemu ya akili ya binadamu ambayohuhodhi fikra, mawazo, hofu na mitazamo hasi ambayo haiwezi kukubalika na jamii. Hofu na6

mawazo hayo hujitokeza kwa ndoto. Pia ung’amuzi bwete huhusisha matukio yaliyotendekazamani lakini mgonjwa huyaingiza katika maongezi yake kama yanatendeka muda huo.Kutokana na utafiti wake aligundua kwamba ndoto zote husheheni ukweli kuhusu maisha yamgonjwa.Freud anaifananisha kazi ya fasihi na ndoto kwa kuwa visasili huwa ni hadithi za kubuni basiubunifu huo unashabihi ndoto kwani wahusika wake na maudhui yake kwa ujumla huwa katikaulimwengu wa kufikirika ambao ni kama ndoto katika ulimwengu halisi sawa sawa na mgonjwawa akili anayeumba ulimwengu wake.Freud alisisitiza mambo yote katika akili ya binadamu yanatawaliwa na ngono (libido). Mawazoyake yaliungwa mkono na mwanafunzi wake Carl Gustav Jung ambaye pia alifanya kazi pamojana Freud katika kuwatibu wagonjwa wa akili kwa kutafsiri ndoto ingawa Gustav alitofautiana naFreud kwa msimamo wake kuwa akili ya binadamu inatawaliwa na ngono.Carl Gustav Jung alifanya utafiti na kuunda dhana ya kikale ambayo ni mtiririko au pichakongwe inayojitokeza mara kwa mara katika tajriba anayopitia mwanadamu , alisema kunasehemu ndani ya akili isiyokuwa na fahamu ya mtu mwenyewe lakini ina athira kubwa juu yamawazo na matendo yake. Alitofautisha sehemu hiyo kama, sehemu ya kwanza ni sehemubinafsi inayofunza maarifa yaliyokusanywa na kila mtu katika maisha yake na sehemu ya pili nisehemu ya kijamii inayofunza maarifa ya kibinadamu yaliyokusanywa na watu katika historiayao na kuendelezwa kwa karne nyingi. Anasema sehemu hii husika na matambiko muhimuambayo mtu anapitia kama sherehe za kumpa mtu jina, sherehe za kuingia jandoni na unyagoni,sherehe zinazoigizwa wakati wa ndoa na hatimaye sherehe zinazohusu maziko ambazo sherehezote hii ndizo huibua ngano.Gustav alifafanua kwa undani masuala ya ngano katika tamaduni mbalimbali za dunia. HivyoFreud na Gustav wanasema masimulizi ni kama ndoto au mvurugiko wa akili kwani picha,taswira na maudhui vyote ni vya kubuni havitoki katika ulimwengu halisi.7

Ubora wa Nadharia hii, Nadharia hii inaonesha utofauti wa msimulizi mmoja hadi mwinginehutokana na historia ya mtu binafsi na uwezo wake binafsi hata kama kisa kitakachosimuliwa nikimoja, hii imedhihirishwa kwa wagonjwa waliokuwa wanasimulia mambo yao kwa utofautikutokana na historia zao. Lakini pia imesaidia kutuonesha chimbuko la ngano kwa miktadhatofauti tofauti kama sherehe za jando na unyago, sherehe za kutoa jina, n.k.Upungufu wa Nadharia hii, Nadharia hii imesisitiza zaidi masuala ya hisia za kingono katikaubunifu wa masimulizi kitu ambacho hakina ushahidi wa kutosha kwani siyo kila hadithiinatarajia kujiridhisha kutoka hali ya ngono iliyofifizwa katika ung’amuzi bwete kamaanavyosema Freud.Nadharia ya kiuamilifu, Nadharia hii iliasisiwa karne ya 20 na Poland Bronislav Malinowsk.Uamilifu uliibuka kama njia yal kuyatazama maisha na utamaduni wa jamii, kwa kuchunguzadhima za vipengele vya kijamii pamoja na njia ambazo kwazo dhima hizi zinahakikisha uwepowa jamii. Malinowsk alifanya utafiti Australia na kugundua kuwa ngano ni kumbukumbu zakweli za mila na desturi za jamii zilizopita, unyago, jando, mazishi, harusi, tohara, matambiko,kusalia miungu, n.k.Ubora wa Nadharia hii, Nadharia hii imesaidia kuondoa mawazo kuwa chimbuko la fasihimbalimbali zikiwemo ngano ni mahali fulani bali ni kila jamii imekuwa na simulizi ambazozinasawiri tajriba (uzoefu) wao wa kila siku katika Nyanja mbalimbali kama vile, kiuchumi,kisiasa, kiutamaduni na kijamii. Vilevile Nadharia hii, inatusaidia kujielewa na kuzielewa jamiizetu vizuri, kwa kuyaelewa mazingira ya mila na desturi zetu katika jimii.Nafasi ya Nadharia hii katika ngano za Kiswahili, inatusaidia kujua tamaduni zetu katika somola ngano, pia inatusaidia kujua kuwa kila jamii ilikuwa na tamaduni zao zenye kuwaongozakatika maisha yao ya kila siku kama vile, jando na unyago, harusi, matambiko, mazishi, miviga,kusalia miungu kuwa ndiyo chimbuko la ngano.8

Hitimisho, kila nadharia tuliyoiangalia ina umuhimu wake katika kujifunza chimbuko la ngano,hivyo ni muhimu kila mwanataaluma wa ngano kuzisoma na kuzielewa nadharia zotezinazozungumzia chimbuko la ngano kwa sababu kila nadharia ina misingi yake ambayo kwanamna moja ama nyingine inatusaidia kujua na kuelewa chimbuko la ngano, Nadharia hizi nimuhimu pia kujifunza kwa sababu kuanzishwa kwa nadharia inategemea na upungufuunaojitokeza katika nadharia nyingine. Kwa ujumla licha ya mtenguo wa nadharia moja dhidi yanyingine tunaona kuwa Nadharia hizi zinakamilisha, Nadharia moja inakamilisha Nadharianyingine. Kwa maana hiyo, hatuwezi kujua au kuthibitisha chimbuka la ngano kwa kutumianadharia moja.9

mawazo ya wanamsambao hususani katika ugawaji wa ngano bila kuchunguza kwa umakini sifa ya kila kundi. Propp anaamini kuwa ili kuchunguza asili ya ngano ni vema kuanza kuchunguza aina za ngano kwa kuangalia maumbo ya ngano. Hivyo mtazamo huu unaangalia asili ya ngano kwa kuchunguza maumbo ya ngano husika. Ubora wa nadhairia hii, nadharia hii inasaidia kujua aina za ngano kutokana na dhima zake .

Related Documents:

a) Dhihirisha kuwa ngano hii ni; (alama 3) i. Ngano ya usuli ii. Ngano ya kiayari iii. Hurafa b) Eleza sifa tano za ngano zinazojitokeza katika ngano hii. (alama 5) c) Hii ngano ina mafunzo mbalimbali. Eleza yoyote manne. (alama 4) d) Tambua shughuli zozote mbili za kiuchumi na mbili za kidini zinazojitokeza kwenye ngano hii. (alama 2)

Mathalan, chimbuko la hadithi za fasihi ya Kiswahili linatokana na chimbuko la ngano za Kiswahili (Kenguru, 2013). Baada ya wageni wa Kimagharibi kuingia Afrka mashariki, hasa Wamishionari, ngano kadhaa wa kadhaa zilifasiriwa na kuwa ndio msingi wa hadithi ndefu za Kiswahili. Baina ya mwaka 1940 na kuendelea hadi miaka ya 1960, hadithi ndefu nyingi za Kiswahili zilifuata mkondo wa ngano za .

2.Asilimia 75 ya Walioteuliwa kwenye utafiti huu na wenye umri wa miaka 19-25 walishiriki katika shughuli za nyimbo za ngoma. Zipo nadharia kadhaa zililyotumika katika Tasnifu hii, kuhusu uwasilishaji na uchanganuzi wa takwimu,Nadharia hizo ni Nadharia ya fasihi ina kwao, Nadharia ya

na Nadharia ya Mwitiko wa M somaji na Fasihi Linganishi ndizo zilizotumika katika kuchambua data za utafiti. Mtafiti alitumia nadharia hii kwa lengo la kuwasawiri wahusika na alitumia nadharia ya Fasihi Linganishi kwa lengo la kulinganisha na kulinganua mbinu za usawiri wa wahusika katika riwaya hizi mbili. Matokeo ya utafiti yamebaini kuwa .

Kiyahudi waliohuisha mwito wa watu wa msalaba. Na hapa tunawaambia ya kwamba: Je, inajuzu na kusihi kuifanya chimbuko letu katika 'Ibaadah ni kutoka kwa watu hawa? Nasi tunarudia mara nyingine tena kuwa zile karne zilizo bora na kufadhilishwa ambazo waliishi watangu wetu wema hakukuwa na athari wala kufanywa mfano wa hizi 'Ibaadah.

Sifa za Ngano f) Zina fomyula ya kuanzia/mwanzo maalum. g) Zina fomyula ya kumalizia/mwisho maalum. h) Zina wahusika aina mbalimbali. i) Zina matumizi ya nyimbo. j) Hutumia takriri (us ambamba) i li kusisitiza k.m. zimwi likakimbia, likakimbia. k) Huwa na na maadili/mafunzo l) Hutumia maswali ya balagha kuongeza taharuki. m) Hutumia tanakali za sauti. n) Zina matumizi ya fantasia au matukio .

a) Eleza maana ya ngano. ( alama 2) b) Tambua sifa sita za masimulizi. ( alama 6) c) Je, formula ya ufunguzi huwa na umuhimu upi katika kuwasilisha hadithi? ( alama 5) d) Fafanua sifa za mtambaji bora za hadithi. ( alama 7) IDARA YA LUGHA APRILI MWAKA 2020 KIDATO CHA NNE 102/3 – KISWAHILI – Karatasi ya 3 FASIHI Maagizo:

austin, tx 78758 3 day blinds, corp. 1583 sloat blvd. san francisco, ca 94132 3 day blinds, corp. 2220 e. cerritos ave. anaheim, ca 92806 3 day blinds, corp. 25 technology drive irvine, ca 92618 337078 ontario ltd. attn: sheldon silverberg 5799 yonge street suite 1100 north york, on m2m 4e7 canada 34 strong, inc. 2020 hurley way #145 sacramento, ca 95825 page 1 of 1963 case 15-10952-kjc doc .