TATHMINI YA MWISHO WA MUHULA-MUHULA WA KWANZA-KIDATO CHA .

3y ago
375 Views
5 Downloads
453.19 KB
8 Pages
Last View : 1d ago
Last Download : 2m ago
Upload by : Melina Bettis
Transcription

TATHMINI YA MWISHO WA MUHULA-MUHULA WAKWANZA-KIDATO CHA PILI -KISWAHILIKIDATO 2Jina .Darasa Nambari .Tarehe .Sahihi MUDA: SAA 2MAAGIZO:Jibu maswali yote katika mtihani huu.Compiled & distributed by Schools Net Kenya, P.O. Box 15509-00503, Nairobi Tel: 254202319748E-mail: infosnkenya@gmail.com ORDER ANSWERS ONLINE at www.schoolsnetkenya.com

TATHMINI YA MWISHO WA MUHULA-MUHULA WAKWANZA-KIDATO CHA PILI -KISWAHILIUFAHAMUSoma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuatia.KIDATO 2(ALAMA 15)Macho ya Abdul yalipigwa na mwali mkali wa jua la asubuhi. Ilikuwa ndiyo mara yake yakwanza kuuona mwanga halisi wa ombwe lijiitalo dunia tangu alipohukumiwa kifungo gerezani.Punde tu komeo la mlango wa seli lilipofunguliwa, ilimlazimu Abdul ayafumbe macho kabla yakuyafumbua tena taratibu ili yazoee mabadiliko yake.Ilikuwa ndiyo siku ya Abdul ya kuachiliwa huru kutoka kwenye kifungo kirefu kilichoyapamacho yake mazoea ya giza la kaburi mle gerezeni. Macho yake yalipokwishaizoea ile hali nakumhakikishia kuwa kila alichokuwa akikiona si kizuka ila uhalisia, alipiga hatua. Akatoka njeya mlango wa seli, kisha kwa kutoamini, akageuka nyuma kulitazama tena lile pango alimokuwaametikwa katika muda huo wote. Akayafikicha macho kwa kutoamini huku machoziyakimdondoka asijue kama yalikuwa ya furaha au ya huzuni. Alipogeuka kuanza safari ya uhuruwake, macho yake yalikumbana na lango la gereza. Hapo, akasita kidogo, labda kuhakikishakama kweli alikuwa huru. Bila shaka, hakuna askari wa gereza aliyemshikia bunduki aukumuamuru asimame. Walimtazama tu na kumpa tabasamu.Taratibu, Abdul aliendelea kupiga hatua. Mhemko aliokuwa nao kutokana na hewa safiiliyompenya mapafuni uliufanya moyo wake upige kwa kasi. Ghafla, tabasamu ikapasuamashavuni pake. Akasita. Akaiinua pua yake iliyompa hakikisho kuwa uvundo na uozo wa selihaukuwa naye tena. Ingawa mwili wake ulijaa mabaka ya uchafu na matambara yaliyoufichauchi wake kuvunda, hilo halikumkera tena. Kwa hivyo, akatia tena tabasamu. Lake kuu lilikuwashukrani kwa kuepuka yale madhila ya joto na rundo la wafungwa. Na kama hilo halikutosha,aligeuka tena ili sasa kuliangalia lile gereza. Bila kutarajia, alipiga magoti, akainua mikonokupiga dua, ―Ewe Mungu, niepushe na balaa nyingine.Safari ya Abdul kutoka katika majengo ya gereza ilikumbwa na mseto wa mawazo. Alipokuwakatika ujia uliomwelekeza katika barabara kuu, mambo mengi yalimpitikia mawazoni asipatejawabu. Hakujua kama wazazi wake walikuwa wangali hai, na kama walikuwa bado wanaishikatika nyumba ile ya kukodi kwa miaka hiyo kumi aliyokuwa jela. ‗Je, nikiwakosa, nitaendawapi? Nitaanzia wapi kuwatafuta?„ Mawazo hayo yaliifungua mifereji ya machozi, kisha ile yamakamasi. Balagha hiyo ilimfikisha katika kituo cha magari ya uchukuzi kwa ule aliouona kuwamuda wa kufumba na kufumbua. Aliyafuta machozi yake haraka kwa kiganja kisha akazibatundu la pua, tayari kupenga kamasi. Hata hivyo, kabla hajafanya hivyo, nafsi yakeilimtahadharisha kuwa hatua hiyo ingekatiza uhuru aliopewa kwa kuchafua mazingira. Kwahivyo akaghairi. Akavuta ncha ya shati lake na kuitumia kama hankachifu kutimiza azma yake.Hapo kituoni, matatu iliyokuwa mbele ilikuwa na watu wachache. Abdi akaingia na kukaaupande wa kioo ambapo tafakuri nyingi zilimjia. Akakumbuka jinsi kesi yake ilivyoendeshwaCompiled & distributed by Schools Net Kenya, P.O. Box 15509-00503, Nairobi Tel: 254202319748E-mail: infosnkenya@gmail.com ORDER ANSWERS ONLINE at www.schoolsnetkenya.com

TATHMINI YA MWISHO WA MUHULA-MUHULA WAKWANZA-KIDATO CHA PILI -KISWAHILIKIDATO 2kinyume kabisa na ukweli na hukumu kutolewa kinyume cha haki. Mimi Abdul, mtoto twaatangu kuzaliwa kwangu hata mdudu sijawahi kumponda kwa udole wangu, ndiyo sasa nijekusingiziwa kuua mtu? Mungu wangu! Kwa nini dunia hii haina wema? Kwa nini wanaodaiwakuwa wasomi hata wakapewa jukumu la kuwakilisha maslahi ya raia ndio wanaowadhulumu haoraia? Hivi, hata hukimu na tajiriba yake aliamua kufuatilia zile porojo za wanaojiita majasusi?Angeahirisha hukumu yake ili kufanya uchunguzi zaidi, bila shaka nisingepata mapigo nadhuluma hizo zote. Kwa kweli, hii ni dunia ya mwenye nguvu mpishe! Abdul alijisemea.Maswali(a) Kwa nini Abdul alifungwa?(alama 2) (b) Kwa kurejelea kifungu eleza mashaka katika asasi za kurekebisha tabia.(alama 4) (c) Ni kinyume kipi kinachoonekana katika kifungu hiki?(alama 2) (d) Ni mambo yapi yaliyomtia Abdul machugamachuga alipoachiliwa huru.(alama 2) (e) Abdul anaelekea kuwa na hulka gani? Fafanua kwa kurejelea kifungu.(alama 2)Compiled & distributed by Schools Net Kenya, P.O. Box 15509-00503, Nairobi Tel: 254202319748E-mail: infosnkenya@gmail.com ORDER ANSWERS ONLINE at www.schoolsnetkenya.com

TATHMINI YA MWISHO WA MUHULA-MUHULA WAKWANZA-KIDATO CHA PILI -KISWAHILIKIDATO 2 (f) Msamiati ufuatao una maana gani kwa mujibu wa kifungu hiki.(alama 2)(i) Ombwe .(ii) Mhemko .MATUMIZI YA LUGHAa) Eleza tofauti kati ya sauti hizi.i)ALAMA 35Alama 4/y/ na /z/ ii)/t/ na /h/ b) Andika katika ukubwa wingi.Alama 2Ndovu amezaa ndama mkubwa sana. c) Toa mfano wa neno lenye silabi ya konsonanti pekeealama 1 d) Akifishaalama 2Tupa kifaa cha kunolea kisu na air conditioner huuzwa kwa bei ghali. e) Amrisha katika nafsi ya tatu wingi.Alama 2Uandike insha ndefu. .f) Badilisha sentensi hii katika usemi wa taarifa.Alama 2Compiled & distributed by Schools Net Kenya, P.O. Box 15509-00503, Nairobi Tel: 254202319748E-mail: infosnkenya@gmail.com ORDER ANSWERS ONLINE at www.schoolsnetkenya.com

TATHMINI YA MWISHO WA MUHULA-MUHULA WAKWANZA-KIDATO CHA PILI -KISWAHILIKIDATO 2“Itakubidi urauke alfajiri iwapo unataka kusafiri nami kesho,” mjomba alisema. g) Andika vinyume vya vitenzi katika sentensi ifuatayo.Alama 2Chebet aliingia garini na kufunga kioo. h) Viorodheshe vipashio vya lugha ukianza na cha juu Zaidi.Alama 2 i) Ainisha mofimu katika:alama 3Alinywewa maziwaj) Tambua wakati na hali katika sentensi ifuatayo.Alama 3Mhazigi atakuwa ameiunganisha mifupa iliyovunjika k) Unda nomino mbili kutokana na kitenzi „tahini‟.Alama 2 l) Neno hili limo katika ngeli gani?Alama 1Kinda m) Tumia nomino ya jamii badala ya maneno yaliyopigiwa mstari.Alama 1Kundi la wachawi lilitiwa mbaroni jana. n) Andika katika wingialama 2Mtoto wake alilelewa kwenye ukoo huuCompiled & distributed by Schools Net Kenya, P.O. Box 15509-00503, Nairobi Tel: 254202319748E-mail: infosnkenya@gmail.com ORDER ANSWERS ONLINE at www.schoolsnetkenya.com

TATHMINI YA MWISHO WA MUHULA-MUHULA WAKWANZA-KIDATO CHA PILI -KISWAHILIKIDATO 2 o) Yakinishaalama 2Wakulima wasipopalilia mahindi yao hawatapata mazao. p) Pambanua sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha mstarialama 4Mwanahamisi alilishona rinda lake vizuri.q) Ainisha viambishi katika neno lifuataloalama 3WaliochezewaISIMUJAMIIALAMA 10“ maandiko yanasema kwamba siku ya kiama tutapaa angani na mwenye uwezo.”a) Tambua sajili ya kauli iliyopo hapo juu.(alama 2) b) Kwa kutoa mifano mwafaka, taja sifa bainifu za sajili uliyoitambua hapo juu.(alama 8) Compiled & distributed by Schools Net Kenya, P.O. Box 15509-00503, Nairobi Tel: 254202319748E-mail: infosnkenya@gmail.com ORDER ANSWERS ONLINE at www.schoolsnetkenya.com

TATHMINI YA MWISHO WA MUHULA-MUHULA WAKWANZA-KIDATO CHA PILI -KISWAHILIKIDATO 2 FASIHI SIMULIZIa) Eleza sifa zozote tano za hadithiALAMA 20(alama 10) b) Eleza sifa za mtambaji bora wa ngano(alama 10) Compiled & distributed by Schools Net Kenya, P.O. Box 15509-00503, Nairobi Tel: 254202319748E-mail: infosnkenya@gmail.com ORDER ANSWERS ONLINE at www.schoolsnetkenya.com

TATHMINI YA MWISHO WA MUHULA-MUHULA WAKWANZA-KIDATO CHA PILI -KISWAHILIKIDATO 2 Compiled & distributed by Schools Net Kenya, P.O. Box 15509-00503, Nairobi Tel: 254202319748E-mail: infosnkenya@gmail.com ORDER ANSWERS ONLINE at www.schoolsnetkenya.com

KWANZA-KIDATO CHA PILI -KISWAHILI KIDATO 2 Compiled & distributed by Schools Net Kenya, P.O. Box 15509-00503, Nairobi Tel: 254202319748 E-mail: infosnkenya@gmail.com ORDER ANSWERS ONLINE at www.schoolsnetkenya.com UFAHAMU (ALAMA 15) Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuatia. Macho ya Abdul yalipigwa na mwali mkali wa jua la asubuhi. Ilikuwa ndiyo mara yake ya kwanza kuuona .

Related Documents:

FASIHI Julai / Agosti 2018 Muda: Saa 2½ MTIHANI AW MWISHO AW MUHULA AW PILI Kidato cha Nne KISAW HILI Karatasi - 102/3 Julai / Agosti 2018 Muda : Saa 2½ MAAGIZO 1. Jibu maswali MANNE pekee. 2. Swali la KWANZA ni la LAZIMA. 3. Kisha chagua maswali mengine matatu kutoka sehemu zilizobakia; yaani Riwaya, Hadithi Fupi, na Ushairi 4.

JARIBIO LA TATHMINI YA PAMOJA MTIHANI WA CEKENAS MUHULA WA PILI MWAKA 2015 Hati ya Kuhitimu Elimu ya Sekondari KISWAHILI INSHA KARATASI YA KWANZA MUDA: SAA 1 ¾ MAAGIZO 1. Andika insha mbili. 2. Insha ya kwanza ni ya lazima. 3. Chagua insha nyingine moja kutoka hizo tatu zilizosalia. 4. Kila insha isipungue maneno 400 5. Kila insha ina alama 20.

Juma Kipindi Funzo Mada Malengo Shughuli Za Mwalimu Na Mwana Funzi Nyenzo Asilia Maoni 1 1 . Kusikiliza na kuongea Hadithi Kufikia mwisho wa kipindi: Mwanafunzi aweze . Sarufi Nomino Kufikia mwisho wa kipindi: Mwanafunzi aweze kutambua nomino kutokana na nomino -kueleza -kutaja -kuandika -kuiga -kadi -picha michoro Tujivunie UK 183-185 .

ni wa kazi za sanaa za fasihi simulizi Vipindi 32 mada ndon-go 1.Na - dharia ya fasihi sim - ulizi ya Kiswa - hili na tanzu zake Mada kuu 1.Uwan-ja wa fasihi kama sanaa A. MPANGILIO WA MASOMO KWA MUHULA WA KWANZA. 3-Tathmi-ni ende-lezi au tathmini ya ujif - unzaji: Inayo - fanyiwa darasani-Tathmi-ni ende-lezi au tathmini ya ujif - unzaji: Inayo

kumeendelea kushuhudiwa matatizo mengi hali iliyopelekea kushuhudiwa kwamsururu . wamelazimishwa kulipa ushuru kwa kutaka tu kuona maiti za jamaa zao kwenye vyumba vya kuhifadhi maiti. . Eleza sifa sita za fasihi simulizi. .

wizara ya elimu, sayansi na teknolojia cheti cha ualimu elimu ya awali matokeo ya mtihani wa mwisho wa muhula wa ii juni 2019 wanachuo wa mwaka wa kwanza i i ja ict ja i ja ills ja u ja ct ja hili ja a ja ia ja o ja ia ja la ni ja i oni e512/283 nicodem herry swetala me 78 a 67 b 74 b 66 b 8

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali; (Watu wamesimama nusu mduara chini ya mti mkubwa. Wanafanya kelele na kuinua silaha zao. Mbele yao kuna viongozi. Hivi ndivyo mambo yalivyoendelea.) Mkuu wa wilaya: Ningependa kiongozi wenu awasilishe matatizo yenu. Tafadhali ketini . tumsikilize.

Animal Nutrition & Health addresses the nutrition additives segment of the feed and pet food markets. Human Nutrition & Health largely addresses nutrition and functional ingredients segment of the food markets. Personal Care is focusing on the actives and ingredients in the sun care, skin care and hair care industries. DSM is the only producer who can supply the lawsuits, and public rejection .