MTIHANI WA MWIGO KAUNTI NDOGO YA KAKAMEGA KUSINI-2016

2y ago
591 Views
29 Downloads
407.21 KB
12 Pages
Last View : Today
Last Download : 2m ago
Upload by : Tia Newell
Transcription

JINA NAMBA YAKO JINA LA SHULE .SAHIHI 102/2KISWAHILIKARATASI LA 2LUGHAJULAI/AGOSTIMUDA: SAA 2 ½MTIHANI WA MWIGO KAUNTI NDOGO YA KAKAMEGA KUSINI-2016Hati ya Kuhitimu Masomo ya Sekondari – Kenya (K.C.S.E)Maagizoa) Jibu maswali yote.b) Majibu yote yaandikwe katika nafasi zilizoachwa katika kijitabu hiki cha maswali.c) Hakikisha kuwa kurasa zote za kijitabu hiki zimepigwa hapa sawasawa na kuwa maswali yoteyamo.d) Majibu yote yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.KWA MATUMIZI YA MTAHINI PEKEESWALIUPEO115215340410JUMLA80ALAMAHii karatasi ina kurasa 10 zilizopigwa chapa.Mtahiniwa ahakikishe kuwa kurasa zote kumi za karatasi hii ya mtihani zimepigwa chapa sawasawa nakuwa maswali yote yamo.1@ 2016Kamati Andalizi Kakamega Kusini102/2 kiswahiliFungua

1. UFAHAMU(ALAMA 15)Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.Wakati wananchi katika kila pembe ya dunia waliadhimisha siku ya wapendanao maarufu kamaValentine Day, kwa mitindo mbalimbali, hali hiyo ilikuwa tofauti kwa baadhi ya wanaume nchiniKenya, baadaya ya kulalamika kuhusu kunyanyaswa na wake zao.Kulingana na mwenyekiti wa chama cha kutetea Haki za Wanaume nchini, idadi ya wanaumewanaopigwa na wake zao imeongezeka mno. Alisema juzi kuwa utafiti wa chama chake umeonyeshakuwa harakati za kumpa uwezo mwanamke zimeathiri maadili na kuwasababisha kuwadharauwanaume. Mwanaharakati huyo anadai kuwa tatizo hilo limechochewa zaidi na hali ya kuwa wanawakewengi sasa wana kipato kikubwa kuliko waume zao.Mwishoni mwa wiki polisi walimtia mbaroni mwanamke mmoja mjini Nyeri mkoani kati, baada yakumshambulia mumewe na kumjeruhi vibaya kwa panga. Mwanaume huyo bado anapata matibabuhospitalini. Yeye alirudi nyumbani kama amevaa miwani ndipo akakatwa katwa usoni na uchunguzikuhusu tukio hilo bado unaendelea.Inadaiwa kuwa zaidi ya wanaume 460,000 walinyanyaswa na wake zao mwaka jana na kwamba utafitiwa shirika la kuwatetea wanaume unaonyesha kesi nyingi za wanaume kuteswa na wake zaozinaripotiwa katika Mkoa wa Kati.Hata hivyo, baadhi ya wanaume katika eneo hilo wameunga mkono hatua ya wanawakekuwashambulia waume zao. Wanasema kuwa, wanapigwa kwa sababu wamekosa kuwajibika kwafamilia zao. Wanadai kuwa wanaume wengine hawajulikani nyumbani kwao. Wake zao wanawajuamakasisi ambao huja kuwaombea kuhusu matatizo ya nyumbani huku mabwana zao wakizama katikaulevi. Wanawake na wanaume wa Nyeri wamekata serikali ikomeshe uuzaji na unywaji pombe haramuambayo imechangia sana ugomvi wa kinyumbani.MASWALIa) Upe ufahamu huu anwani mwafaka.(al.1) b) Eleza sababu za wanaume kupigwa katika ndoa.(al.4) 2@ 2016Kamati Andalizi Kakamega Kusini102/2 kiswahiliFungua

c) Mwandishi anamaanisha nini anaposema kuwa wanaume wengine hawajulikani nyumbani kwao.(al.2) d) Fafanua majukumu ya makasisi katika jamii kwa mujibu wa kifungu hiki.(al.2) e) Eleza mabadiliko katika asasi ya ndoa kwa mujibu wa kifungu hiki.(al.3) .f) Eleza maana ya vifungu hivi kama vilivyotumika katika tungo.(al.3)i.Mwanaharakati ii.Amevaa miwani .iii.Waliadhimisha .2. UFUPISHO (ALAMA 15)Soma makala hii kisha ujibu maswali yote mawili.Aibu kubwa ya taifa kushindwa kukabiliana na tatizo sugu la ajali za barabarani bado inaendeleakuwafedhehesha wahusika katika sekta ya uchukuzi na mawasiliano licha ya matumizi ya vithibitimwendo na kanda za usalama. Ajali za barabarani zinaangamiza idadai kubwa ya watu kila mwaka,wakiwemo viongozi na watu mashuhuri.Miongoni mwa sababu ambazo zinaleta maafa barabarani ni pamoja na uendeshaji kasi kupitainavyotakikana, yaani kukiuka masharti yalivyowekwa na wizara ya uchukuzi na mawasiliano.Madereva wengi hung’oa vidhibiti mwendo vilivyowekwa, hawarekebishi mikanda ya usalama,wala hawayapeleki magari yao kwa ukaguzi mara kwa mara inavyopaswa. Yale yanayopelekwakwa ukaguzi mengi hushindwa kutekeleza kanuni zilizowekwa, kwa hivyo hutegemea hongo kuwabarabarani. Fauka ya hayo, madereva wa malori na matrela mara nyingi huendesha magari hayowakiwa walevi. Dawa za kulevya, kama vile miraa na bangi, hutumiwa sana na watu hawa namatokeo yake huwa ajali mbaya.Hata hivyo, lawama haiwezi kuelekezwa madereva pekee. Ukiangalia barabara nchini Kenyautapata kuwa barabara haziko katika hali nzuri. Zile za lami zimekuwa na mashimo makubwaambapo mvua ikinyesha hufanya vidimbwi mithili ya machimbo ya madini yaliyojaa maji baada yakuachwa wazi.3@ 2016Kamati Andalizi Kakamega Kusini102/2 kiswahiliFungua

Na zile barabara zisizokuwa za lami zimeharibika kiasi kwamba ni vigumu kuzitofautisha na njia zang’ombe kwenye maeneo kame. Kinachohitajika ni serikali kuzifanyia ukarabati ili kuzirudishakatika kiwango ambacho zitaweza kufaa tena.Wananchi pia inafaa waelimishwe ili wasikubali kuingia kwenye magari ambayo tayari yamejaakupita kiasi. Hii itawasaidia wananchi wenyewe kudumisha usalama wao barabarani. Pia inawafaawatambue ya kwamba wana jukumu la kuwaarifu walinda usalama endapo dereva anendesha kwakasi sana kuliko ile ya kilomita 80 kwa saa iliyokubaliwa.Inafahamika kuwa maafisa wa usalama ndio wafisadi zaidi, hivyo basi huchangia katika kuongezaidadi ya vifo barabarani. Katika vita dhidi ya ufisadi na ajali za barabarani, ni mwananchimwenyewe ambaye atawezesha kukomesha hali hii. Kwa mfano, afisa wa usalama akipatikanaakichukua hongo, yeye pamoja na Yule aliyetoa hongo wapelekwe kwenye vituo vya kukabilianana ufisadi na wachukuliwe hatua kali, matatizo haya yataisha.Lakini kabla kufikia hapo, ni muhimu kumhamasisha mwananchi kuhusu haki zake na namna yakukabiliana na suala hili la ufisadi.Hali hii inatuonyesha kwamba mipango maalumu inapaswa kufanywa na serikali ili kuwaelimishawananchi kama hatua ya kwanza ya kukabiliana na ufisadi hatimaye izilainishe sekta zote wala siya uchukuzi na mawasiliano pekee.Maswalia) Eleza mambo muhimu yanayorejelewa na mwandishi katika aya tatu za kwanza. (Maneno 70)(al.7 ut 1 8)Matayarisho 4@ 2016Kamati Andalizi Kakamega Kusini102/2 kiswahiliFungua

Nakala safi .5@ 2016Kamati Andalizi Kakamega Kusini102/2 kiswahiliFungua

b) Kwa kurejelea aya nne za mwisho fafanua hatua zinazofaa kuzingatiwa kupunguza ajali zabarabarani (maneno 60)(al 6 ut 1 7)Matayarisho Nakala safi 6@ 2016Kamati Andalizi Kakamega Kusini102/2 kiswahiliFungua

.3. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)a) Sauti /p/ ni kipasuo, sauti hizi ni gani?i.(al.2)/f/ ii./l/ b) Ainisha viambishi katika sentensi ifuatayo;(al.3)Alituogofya c) Tunga senetensi yenye muundo ufuatao wa maneno(al.2)W V T E E d) Nyambua vitenzi vifuatavyo vya silabi moja ili kujaza mapengoi.Mgeni ali (pa, kutendewa) kiti ili akae.ii.Ame (la, kutendesha) moto chakula.(al.2)7@ 2016Kamati Andalizi Kakamega Kusini102/2 kiswahiliFungua

e) Andika kwa usemi halisi(al.4)Cherotich aliwahakikishia wazazi wake kwamba angetia bidii katika masomo yake ili apitemtihani wake wa mwisho wa mwaka huo. f) Eleza matumizi mawili ya parandesi(al.2) g) Kiambishi –ji- kimetumiwa vipi katika sentensi ifuatayo;(al.2)Binti mdogo anajishaua kwa jiatu la mamake. .h) Eleza maana ya kihusishi katika sentensi ifuatayo;(al.1)Alhamdulilahi! Nimefaulu katika mtihani wangu. i) Huku ukitoa mfano mmoja andika miundo yoyote matatu ya virai vivumishi.(al.3) j) Changanua sentensi kwa njia ya vistari(al.3)Mto uliofurika jana umezoa taka nyingi.8@ 2016Kamati Andalizi Kakamega Kusini102/2 kiswahiliFungua

k) Sahihisha kwa namna mbili tofauti;(al.2)Angalifika mapema angelimuona mkurugenzi. l) Kanusha sentensi katika hali ya kuamrisha wingi.(al.2)Kimbia haraka Amka .m) Tambua kiima chagizo na shamirisho katika sentensi ifuatayo;(al.3)Mtoto aliletewa cheti mapema na mzazi. n) Unda nomino mbili kutokana na neno mwigo.(al.2) o) Kwa kutunga sentensi, tofautisha vitate hivi.i.Bakaii.Paka(al.2) p) Andika sentensi ifuatayo katika wakati ujao, hali timilifu(al.1)Miti hupandwa na wanakandarasi wale. 9@ 2016Kamati Andalizi Kakamega Kusini102/2 kiswahiliFungua

q) Unganisha sentensi zifuatazo kwa kutumia “o” rejeshi.i.Mshukiwa alipelekwa mahakamani.ii.Mshukiwa alichukuliwa hatua.(al.2) r) Weka neno lifuatalo katika ngeli yake.(al.1)Malezi 4. ISIMU JAMII (ALAMA 10)a. Eleza maana ya istilahi zifuatazo;i.Isimu jamii ii.Lafudhi iii.Lahaja iv.Lingua franka v.Pigini 10@ 2016Kamati Andalizi Kakamega Kusini102/2 kiswahiliFungua

11@ 2016Kamati Andalizi Kakamega Kusini102/2 kiswahiliFungua

12@ 2016Kamati Andalizi Kakamega Kusini102/2 kiswahiliFungua

MTIHANI WA MWIGO KAUNTI NDOGO YA KAKAMEGA KUSINI-2016 Hati ya Kuhitimu Masomo ya Sekondari – Kenya (K.C.S.E) Maagizo a) Jibu maswali yote. b) Majibu yote yaandikwe katika nafasi zilizoachwa katika kijitabu hiki cha maswali. c) Hakikisha kuwa kurasa zote za kijitabu hiki zimepigwa hapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.

Related Documents:

2015 Mtihani wa Tathmini eneo la Bondo 102/1 Insha Fungua ukurasa 102/1 KISWAHILI Karatasi ya 1 Julai/Agosti - 2015 MUDA: SAA 1 ¾ MTIHANI WA KUTATHIMINI WILAYA YA BONDO - 2015 . Ardhi ndiyo chanzo cha riziki zote. Fauka ya hayo, ardhi ni dafina kubwa. . Fupisha aya ya kwanza kwa maneno 50.

4.0 KISWAHILI (102) 4.1 MATOKEO YA MTIHANI WA SOMO LA KISWAHILI Jedwali hili linaonyesha matokeo ya mtihani wa somo la Kiswahili katika muda wa miaka minne (2005 hadi 2008). Jedwali 6: Matokeo ya mtihani wa Kiswahili (2005 - 2008) Mwaka Karatasi Watahiniwa Alama ya Juu Alama ya Wastani Alama ya Tanganisho 2005 1 2 3 Jumla 259,301 40 80

RIWAYA YA CHOZI LA HERI NA ASHUMTA K. MATEI . 4. Matatizo mengi yanayowakumba wahusika wengi katika riwaya hii ni mwiba wa kujidunga. Jadili (al.20) 5. Kwa kurejelea riwaya hii, fafanua mbinu zifuatazo. (al.20) (i) Kinaya (ii) Mbinu rejeshi (iii) Sadf

Ni kinaya Kenga kumwacha Majoka ilhali ndiye aliyenufaika na uongozi wake. (8x1) d) Eleza changamoto zinazoikumba elimu. (alama 4) Ukosefu wa ajira kwa waliosoma, mfano Tunu na Ashua Matumizi ya dawa za kulevya- wanafunzi katika shule ya Majoka wanadungana sumu ya nyoka.

Kwa jina Ia Mwenyezi Mungu Mwenye kuneemesha neema Jcubwa kubwa na M wenye kuneemesha neema ndogo ndogo. I . Alif Lam Ra. Hizi ni Aya za Kitabu kilichoku nya kila yanayohitajiwa na kikayadhihirisha kwa vizuri. 2. Mara nyingi wale walio

FASIHI Julai / Agosti 2018 Muda: Saa 2½ MTIHANI AW MWISHO AW MUHULA AW PILI Kidato cha Nne KISAW HILI Karatasi - 102/3 Julai / Agosti 2018 Muda : Saa 2½ MAAGIZO 1. Jibu maswali MANNE pekee. 2. Swali la KWANZA ni la LAZIMA. 3. Kisha chagua maswali mengine matatu kutoka sehemu zilizobakia; yaani Riwaya, Hadithi Fupi, na Ushairi 4.

MTIHANI WA PAMOJA WA SHULE ZA EKSIKA Hati ya kuhitimu kisomo cha sekondari Kenya(K.C.S.E) MAAGIZO: a) Jibu maswali yote. b) Andika majibu yote katika nafasi zilizoachwa. c) Karatasi hii ina alama 30. d) Hakikisha kurasa zote zimepigwa chapa. Swali Upeo Alama Ufahamu 15 Ufupisho 15 Lugha 40 Isimu Jamii 10 Jumla 80

planning a business event D1 evaluate the management of a business event making recommendations for future improvements P2 explain the role of an event organiser [IE] P3 prepare a plan for a business event [TW] P4 arrange and organise a venue for a business event, ensuring health and safety requirements are met [SM, EP] M2 analyse the arrangements