JINA . .NAMBARI . DARASA .

2y ago
266 Views
13 Downloads
321.96 KB
10 Pages
Last View : 1m ago
Last Download : 2m ago
Upload by : Roy Essex
Transcription

JINA . .NAMBARI . DARASA . SAHIHI .TAREHE . .102/2KISWAHILIKaratasi Ya PiliLUGHASaa: 2 ½MTIHANI WA TATHMINI WA KIDATO CHA NNE -MUUNGANOMAAGIZOAndika jina lako na mambari yako katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.Weka sahihi yako na tarehe ya mtihani katika nafasi ulizoaciwa hapo juu.Jibu maswali yoteAndika majibu yako katika nafasi ulizoachiwa katika kijitabu cha maswali.Karatasi hii ina kurasa 10 zilizopigwa chapa.Watahiniwa ni lazima waangalie kama kurasa zote zimepigwa chapa sawasawa na kuwamaswali yote yamo.KWA MATUMIZI YA MTAHINI TU:SwaliUpeo115215340410Jumla80Alama1

SEHEMU A: UFAHAMU (ALAMA 15)Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata.Ni fedheha kuona taifa ambalo halijakuwa likitambua msamiati wa shibe kwa zaidiya miongo miwili sasa limeacha chakula kiharibike mashambani kutokana na ukosefu wa soko.Taarifa kuwa ni zamu ya wakulima wa mahindi kukadiria hasara baadaya wenzao wa maziwa ni za kuhuzunisha. Inasemekana wakulima wa zao la mahindi katikamikoa ya pwani, mashariki, kati na Bonde la ufa waenendelea kuhesabu hasara kutokana naukosefu wa soko la mahindi kutoka kwa serikali.Hii ni hata baada ya serikali kuwapatia na kuwauzia pembejeo kwa bei nafuu kamanjia mojawapo ya kuimarisha uzalishaji wa chakula nchini. Kinachovunja moyozaidi ni habari kuwa serikali iyo hiyo ilitoa ahadi ya kununua mazao yote yawakulima hao kama njia mojawapo ya kuwatia moyo katika kazi yao.Kando na wakulima wa kibinafsi, ilitumia mamilioni ya pesa za umma kuzinduamiradi ya kilimo cha mahindi kwa kunyunyizia mashamba maji na mazao yakepia yanaharibikia. Wakulima wa mradi wa kilimo cha kunyunyizia mashamba waHola, kwa mfano, wameathirika pakubwa kutokana na ukosefu wa soko la mazaoyao. Imekuwa ikijikokota kutokana na sababu kadhaa ikiwemo ukosefu wa fedhaza kununua mahindi.Hii ni hata baada ya uchunguzi kuonyesha kuwa usalama wa chakula nchiniumedorora kutokana na kiangazi cha muda mrefu. Mbali na kutokuwepo kwautaratibu wa kununua mahindi kutoka kwa wakulima hao halmashauri ya nafakahaina uwezo wa kuwashughulikia wakulima wote nchini.Hii ni kwa sababu wakulima wengi hawapati huduma za halmashauri hiyo ambayo imejikitakatika maeneo yaliyokuwa yakizalisha chakula kwa wingi miaka iliyopita. Eneo la Hola, kwamfano, liko mbali kutoka kwa kituo cha halmashauri hiyo kwa sababu eneo hilo ni kame.Ni kutokana na muktadha huu serikali inapaswa ichukue hatua za haraka kuepushakuharibika kwa zao la mahindi nchini. Serikali inapaswa kutenga fedha zaidi za kununuamahindi kutoka kwa wakulima. Inakisiwa kuwa hasara zaidi inatarajiwa kutokea ikiwa pesazaidi hazitatengwa kwa sababu idadi ya wakulima wanaovuna mahindi inatarajiwa kuongezeka.Maswali(a)Kwa nini chakula kinaharibikia mashambani?(alama2)(b)Serikali ilichangia vipi katika kuimarisha uzalishaji wa chakula.2(alama 2)

(c) Eleza vile halmashari ya nafaka haijaweza kuepushia wakulima wa mahindi hasara.(alama 3)( d)Kwa nini wakulima wa maeneo kame hawajashughulikiwa na halmashuri ya nafaka?(alama 1)(e)Kutokana na taarifa hii serikali inaweza kutatua tatizo la wakulima kwa njia gani? (alama 1)(f)Pendekeza namna taifa linaweza kuepuka na kupambana na uharibifu wa chakulamashambani.(alama 3)(g)Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika taarifa.(alama 3)(i) Miongo(ii) Pembejeo( iii) Umedorora3

SEHEMU YA B: UFUPISHO: (ALAMA 15)Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata:Katika safu yangu hii sina lengo la kuzishambulia dini zetu na namuombaMungu sana asiniandikie dhambi kutokana na ninayotaka kuyaandika. Lakini nashawishikakuikumbusha jamii yangu ambayo inatufanya watu tuzione dini zetu zinamkandamizamwanamke. Dini zetu kubwa kama Uislamu na Ukristo zinatuelekeza mwanamke kumheshimumumewe na kumsikiliza anachosema, lakini kwa yeyekufuata maadili ya dini na si kukuambia uue ukakubali.Wakati dini inasema utekeleze amri ya mumeo na wao wameelezwa mamboya kuwafanyia wanawake, ikiwa ni pamoja na kuwaheshima na kuwaridhisha kadriya uwezo wao.Kutokana na hilo la amri, wanaume wengi ndio wamechukua kama tiketi ya kunyanyasamwanamke na hata kumnyima fursa ya kujiendeleza kielimu na hata kufanya shughuli zakuongeza kipato. Unakuta familia ni ya kimaskini, baba hana fedha za kutosha kuihudumiafamilia yake, lakini baba huyo anataka kujishughulishana shughuli yoyote ya kumuingizia kipato kinachoweza kuwasaidia wote na matokeo yakekuendelea kuwepo, kwenye dimbwi la umasikini. Wengine kwa hofu ya kupata changamotokutoka kwa wake zao wanawakatalia wanawake walio wao kujiendeleza kielimu au kutafutamwanamke asiyeelimika ili asiweze kuhoji mambo kadhaa ndaniya nyumba.Hili limebainishwa hivi karibuni na shirika moja lisilo la kiserikali hukokigoma ambapo katika utafiti wao asilimia 90% ya wanawake wa vijijini wanashindwa kutoahoja kutokana na uelewa wao duni na kutoa sababu ya kuwa hiyo ni kutokanana ukosefu wa elimu, masuala ya kidini yanayomwelekeza mwanamke kufuata amriza mumewe, mila na desturi kadhaa.Dini zote zinaeleza wazi umuhimu wa mtu kupata elimu bila kubagua kamaya kiislamu inavyosema; mtu anapata thawabu anapotafuta elimu na anatakiwaaitafute popote bila kujali umbali na hata ikiwezekana kufika China ambapoinaaminika ni mbali.Sijawahi kuona wala kusikia dini ikisema mwanamke asipate elimu lakinibaba zangu na kaka zangu wanaume wanalipotosha hili kutaka kuendelea kumkandamizamwanamke bila kufikiri kuwa mwanamke ni msaada mkubwakwao na kwa maendeleo ya taifa lote; ikiwa leo tupo katika harakati za kupata maendeleo nanchi hii hivi kweli tutafanikiwa?Mapambano ya kuleta maendeleo yaanze katika ngazi ya familia kwakuondoka kwa ujinga wa kumkandamiza mwanamke ili naye aelimike, awezekujenga hoja, aweze kujitafutia kipato na mwisho kusaidia katika maendeleo yafamilia ambayo kwa njia nyingine ndiyo maendeleo yenyewe ya taifa hili.4

(a) Fupisha aya tano za kwanza. (Maneno 70)(alama 8)MatayarishoJibu(b) Mwanamke anaweza kuendelezwa vipi. Rejelea aya mbili za mwisho. (alama 7)5

(Maneno 50).MatayarishoJibuSEHEMU YA C: SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA6

(a) Taja aina mbili kuu za ala za sauti kisha utoe mfano mmoja mmoja. (alama2)(b) Taja maneno yenye miundo ifuatayo ya silabi.(alama 2)(i) KKKI(ii) Irabu pekee (II)(c) Eleza ni kwa nini neno umma ni la asili ya kigeni.(alama 1)(d) Viambishi vilivyopigiwa mstari vinawakilisha dhana zipi za kisarufi?(alama 2)UdhaifuWalani?(e)Neno lifuatalo liko katika ngeli gani?(alama 1)Matukio(f)Andika kwa msemo wa taarifa:(alama 2)Askari: Ulikuwa unaelekea wapi uliposhambuliwa?Jirani: Nilikuwa nikienda sokoni jana.(g)Onyesha vishazi katika sentensi ifuatayo kisha uelezee ni vya aina gani.(alama 2)Ajapo tutamlaki kwa shangwe.(h)Sahihisha sentensi ifuatayo.7

Mtu ambaye aliyechukua kitabu chenye kilikuwa hapa arudishe.(alama 1)(i)Tumia mzizi –w- katika sentensi kama:(alama 2)(i) Kitenzi kisaidizi.(ii)Kitenzi Kishirikishi.(J)Tunga sentensi moja kubainisha matumizi ya ‘na’ kama.(alama 2)(i)Kihusishi cha ‘na’ ya mtenda.(ii)Kiunganishi(k)Weka kirejeshi ‘O’ tamati kwenye kitenzi chunga kisha ukitungie sentensi.(alama 1)(l)Eleza na utoe mifano ya mazingira mawili ambapo mstari mshazari hutumika. (alama 2)(m)Nyambua kitenzi ja kiwe katika kauli ya kutendewa kisha utunge sentensi. (alama 1)(n) (i) Eleza dhana ya shamirisho.(alama 1)(ii) Onyesha aina tofauti za shamirisho katika sentensi hii.Ali alimnunulia Asha viatu kwa pesa zake.(alama 3)8

(o)Tumia kivumishi kionyeshi cha karibu pamoja na nomino katika ngeli ya I-ZI kisha utungesentensi katika ukubwa - wingi.(alama 2)(p)Yakinisha sentensi ifuatayo katika wakati ujao hali timilifu wingi.(alama 2)Msomi hakutuzwa siku hiyo.(q)Eleza matumizi ya kwa katika sentensi hii.(alama 3)Kwa nini umeishi kwao kwa miaka mingi?(r)Eleza maana tatu zinazopatikana katika sentensi hii.(alama 3)Alikuwa amenijuza kuwa angefika kwao.(s)Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya mishale.(alama 4)Kuku na mbuzi ni mifugo.(t)Eleza maana ya nomino.(alama 1)9

SEHEMU YA D: ISIMU JAMII: (ALAMA 10)Ali:Ebo:Ali:Ebo:Ali:Ebo:Ali:Wee kuja hapa. Wewe ni nani? Sema haraka!Mimi ni afande ni EboUnatoka wapi sa ii? Hapa hakuna sheria?Samahani mkubwa. Mimi niku Mkubwa wa nani? Wakubwa wako ofisini.Pole mzee.Mzee gani? Hii mtu lazima niiweke store. Yaani self-contained.Toa viatu.Ebo: Tafadhali Bwana Askari, nilichelewa Ali: Mimi sitaki hadithi! Hizo pelekea nyanya yako, eh! Fanya haraka!Ebo: Naomba mkubwa Ali:Hapa si kanisani. Unaomba! Hata (a) Hii ni sajili gani?(alama2)(b)Fafanua sifa tano za sajili hii.(alama 5)(b)Eleza maana ya istilahi zifuatazo za isimu jamii.(alama 3)( i)Lugha ya taifa.( ii)Lugha ya ishara( iii)Lugha mwiko10

Kando na wakulima wa kibinafsi, ilitumia mamilioni ya pesa za umma kuzindua miradi ya kilimo cha mahindi kwa kunyunyizia mashamba maji na mazao yake pia yanaharibikia. Wakulima wa mradi wa kilimo cha kunyunyizia mashamba wa Hola, kwa mfano, wameathirika pakubwa kutokana na ukosefu wa soko la mazao yao.

Related Documents:

wa somo la Kiswahili wa mwaka 2016 ulioanza kutumika Januari 2017, ambao ulizingatia muhamo wa ruwaza. Aidha, fomati hii imezingatia malengo ya Upimaji wa Elimu Msingi Darasa la Tatu na Darasa la Nne ambayo ni pamoja na kufuatilia kiwango cha ujifunzaji wa wanafunzi wa Darasa la Tatu na Darasa la Nne katika somo la Kiswahili.

sn jina la kwanza jina la pili jina la tatu jinsi index n0. csee elimu somo la 1 somo la 2 mkoa halmashauri kata shule 1 abasi amiri omari me s0413-0001/2010 stashaha

MTIHANI WA PAMOJA -MECS 2021 Jina: _ Nambari ya mtahiniwa:_Darasa: _ Tarehe: _ Sahihi: _ 102/2 Kiswahili Karatasi ya 2 Muhula wa Pili - 2021 Muda: Saa 2½ . kweli kwamba sera ya elimu bila malipo katika shule za msingi nchini humu inaendelea kutekelezwa. Hata hivyo, asilimia ya watoto na hata watu wazima wasiojua kusoma na .

TIE (2018). Mtaala na Muhtasari wa Elimu ya Awali,Dar – es – Salaam: MoEST TIE (2015). Mtaala wa Elimu ya Msingi Darasa la I & II; Dar – es – Salaam: MoEST TIE (2016). Mtaala wa Elimu ya Msingi Darasa la III & IV;

Msimbo wa mwalimu: _ 5. Is the class being observed multi-grade? a. Yes Ndio b. No Hapana ; Jee! darasa lenye kuangaliwa ni darasa lenye wanafunzi wa viwango tofauti? 6. Subject of class to

SEHEMU C: TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI ZINGINE SHIBE INATUMALIZA 5. “Ndugu yangu kula kunatumaliza” “Kunatumaliza au tunakumaliza” a) Eleza muktadha wa dondoo hili (al. 4) b) Fafanua maana kitamathali katika kauli „Kula tunakumaliza‟ (al. 10) c) Kwa mujibu wa hadith

WIZARA YA ELIMU SAYANSI, TEKNOLOJIA NA MAFUNZO YA UFUNDI DARASA IV – KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA MWANAFUNZI: _ MAELEKEZO 1. Kumbuka kuandika majina yako matatu kwa usahihi. 2. Jibu maswali yoe kulingana na maelekezo. 3. Soma maswali kwa ufasaha kabla ya kuyajibu

1 Advanced Engineering Mathematics C. Ray Wylie, Louis C. Barrett McGraw-Hill Book Co 6th Edition, 1995 2 Introductory Methods of Numerical Analysis S. S. Sastry Prentice Hall of India 4th Edition 2010 3 Higher Engineering Mathematics B.V. Ramana McGraw-Hill 11 th Edition,2010 4 A Text Book of Engineering Mathematics N. P. Bali and Manish Goyal Laxmi Publications 2014 5 Advanced Engineering .