Maisha Ndani Ya Kristo 3 - WordPress

2y ago
358 Views
2 Downloads
257.85 KB
45 Pages
Last View : 2d ago
Last Download : 2m ago
Upload by : Karl Gosselin
Transcription

Maisha ndani ya KristoUtanguliziKuwa mkristo ni kuwa na uhusiano na ushirika na Bwana Yesu Kristo. Swali ni, je uhusiano huuunawezekana kwa njia gani? Je, ikiwa mtu anajitahidi sana kuishi maisha mazuri, hii itamfanya kuwamkristo? Biblia inasema kwamba, hakuna mtu ambaye anaweza kufanywa mkristo kwa kuishi maishamazuri. Je, ikiwa mtu anamheshimu Kristo kwa sababu Biblia inasema kwamba lazima tumheshimukwa sababu Yeye anastahili heshima zetu, hii itamfanya mtu huyo kuwa mkristo? Jibu ni la. Kwasababu kumheshimu tu Kristo haiwezi kumwokoa mtu yeyote.Kile kila mtu anahitaji kufanya ni kufahamu kwamba Kristo Yesu alikuja hapa ulimwenguni kuishi nabaadaye kufa kwa ajili ya wenye dhambi kama wewe. Mwamini Yesu kuwa Mwokozi wako naumtegemee Yeye pekee katika maisha yako yote ili ukubalike mbele za Mungu kwa ajili ya yaleambayo amekufanyia. Hivi ndivyo inavyomaanisha kuwa mkristo: ni yule mtu ambaye amemwaminiKristo na ambaye ana uzima wa milele (Yohana 3:16).Imani ambayo inaokoa huwa inatuleta katika uhusiano na ushirika ambao umejawa na furaha tele nautajiri mkubwa wa kiroho. Huwa tunamjua Kristo Yesu kama Mwokozi na Bwana, Kuhani na Mfalme,Rafiki na Ndugu wetu. Agano Jipya linatufafanulia vyema kuhusu uhusiano wetu na Kristo. Katikamakanisa mengi jambo hili limesahaulika sana na wengi huwa hawalielewi kamwe. Jambo hili ni siriambayo imefunuliwa kwetu leo na pia si gumu kufahamu. Tunapofahamu jambo hili, maisha yetuhubadilika kabisa na kusudi kuu la kitabu hiki ni kuwahimiza wale wote ambao ni wakristo kuhusujambo hili. Pia ninaomba sana kwamba yale ambayo ninafundisha hapa yatawasaidia wengi kuvutwana kuletwa kwa Kristo Yesu ili waweze kuokoka. Ninaomba kwamba Mungu atakupatia tamaa yakuwa na uhusiano na ushirika na Bwana Yesu Kristo na kwamba hutapumzika hadi umeokoka.Je, uhusiano huu na Kristo ni wa aina gani? Huu ni uhusiano ambao umekuja kwa sababu yakuunganishwa na Kristo Yesu. Mtume Paulo anazungumzia jambo hili kwa kutumia neno “katika.”Neno hili limetumika kama mara mia mbili katika maandishi ya Paulo. Kwa mfano kuna mahaliambapo anasema, “katika Kristo, katika Yeye, na katika Bwana.” Katika Kitabu cha Waefeso 1:1-14,anazungumza kuhusu kuwa katika Kristo Yesu kama mara kumi na moja. Wakristo katika mji waEfeso walikuwa “waaminifu katika Kristo.” Vivyo hivyo, Wafilipi walikuwa “watakatifu katika KristoYesu” (Wafilipi 1:1) na Wakolosai walikuwa “Watakatifu na ndugu waaminifu katikaKristo” (Wakolosai 1:2). Kulingana na neno la Mungu, mkristo ni mtu ambaye ako “katika Kristo.”Hii ndiyo sababu kuunganishwa pamoja na Kristo ndiyo msingi mkuu wa mafundisho ya wokovuambayo yanahubiriwa na makanisa matakatifu ya Mungu.Kuunganishwa na Kristo Yesu ni jambo kubwa sana kwa sababu lilifanyika kabla ya ulimwengukuwepo na litaendelea hadi milele. Mafundisho haya ni makuu sana kwa sababu yamejawa na barakazote za wokovu. Hata kama wengi wemesoma na kujaribu kuandika mambo mazuri kuyahusumafundisho haya, wanadamu hawayafahamu kabisa hata kama wameamurishwa na Mungu wayatiikwa imani. Kwa hivyo msomaji wangu usitarajie nikueleze kila kitu kwa sababu hata mimi sijui kilakitu.

Kile ninaweza kukuambia ni kwamba mafundisho haya yalinisaidia sana na yameendelea kunisaidiasana katika maisha yangu ya ukristo. Kwa hivyo ninaomba kwamba unapoendelea kuyasoma, kwaujasiri, utasema kweli “mimi niko katika Kristo,” na kwamba maneno haya yatamaanisha jambo kubwakuliko jinsi umekuwa ukiwaza.Tutaona jinsi kuunganishwa kwa Kristo kunatuletea maisha mapya na pia tutaona jinsi tunafaakumtegemea Kristo pekee katika maisha yetu tunapoishi katika ulimwengu huu mwovu. Tutasomakuhusu jamii kubwa ya Mungu ambayo ni jamii yetu sasa. Tutaona jinsi mateso na shida ni moja yanjia ambazo Mungu anatumia kutuvuta karibu na karibu kwa Kristo Yesu na kutufanya tuwe kamaKristo mwenyewe.Tutaanza na jinsi tunapoingia katika uhusiano na ushirika huu pamoja na Kristo.Sura ya KwanzaImani ndani ya KristoJe, Kristo ni nani ambaye wakristo wote wameunganishwa Kwake? Jibu la Biblia ni kwamba, Yeyendiye Mwana wa Mungu, Yeye ni yule yule ambaye kwa mamlaka na utukufu ako sawa na MunguBaba. Yeye ndiye Mesiya, Yule ambaye amepakwa mafuta na ndiyo timizo la tumaini la watu wote waMungu. Yeye ndiye Mwokozi ambaye aliishi maisha matakatifu, akafa msalabani, alifufuliwa kutokakwa wafu na alirudi mbinguni. Yeye ndiye Mfalme wa sasa na hakimu ambaye atahukumu ulimwengu.Yeye ni haya yote na mengine mengi sana. Kwa haya yote tutazingatia mambo mawili tu haswa yaleambayo Paulo anatumia katika 1 Wakorintho 15:45;47 akimfafanua Yesu Kristo, yaani “Adamu wamwisho” na “Mtu wa pili.”Adamu wa mwishoAdamu alikuwa mwakilishi wa wanadamu wote. Paul anazungumza kuhusu Adamu na Kristo kuwandiyo watu muhimu kabisa ambao wamewahi ishi katika ulimwengu wote na kwamba hakuna mtumwingine ambaye atawahi linganishwa nao. Swali ni, kwa nini Paulo katika kuandika kwake awazehivi? Jibu ni kwamba, kuna wakilishi wawili kwa watu wote wa ulimwengu: Adamu na Kristo.Hii inatuonyesha kwamba Mungu huwa hashuguliki tu na wanadamu kwa misingi ya kibinafsi balianawaona wanadamu na kuwashughulikia kama kikundi kupitia kwa mpango Wake mwenyewe.Mpango huu ni agano ambalo Mungu mwenyewe ametengeneza na watu wake.Katika agano hili, Mungu anamchagua mtu mmoja kuwa mwakilishi wa kikundi cha watu wengi.Uhusiano ambao Mungu ako nao na mwakilishi wa kikundi hicho, ndiyo ule ule ako nao na kila mtuambaye anaakilishwa katika kikundi hicho. Kila shughuli ya Mungu juu ya kila mtu wa kikundi hichoanaifanya kupitia kwa mwakilishi wa kikundi hicho. Mungu katika mipango Wake amewawekawakilishi wawili, yaani Adamu na Kristo, na kila mwanadamu amewakilishwa na Kristo au Adamu.Unaweza kufahamu hali yako ya dhambi ikiwa utafahamu kwamba wewe ulizaliwa katika Adamu nakwa hivyo yeye ndiye mwakilishi wako. Unaweza tu kufahamu na kufurahia wokovu wako ikiwa

utafahamu kwamba umeondolewa katika Adamu na kwa hivyo yeye sasa si mwakilishi wako. Wewesasa kuletwa katika Kristo na sasa ni mwakilishi wako. Paulo anazungumza juu ya jambo hili katikaWarumi 5:12-21.Kile ninamaanisha kwa mfano ni, mtu mmoja anaishi katika eneo la mbunge fulani ambaye ni adui waRais. Kwa hivyo eneo lake halifaidiki hata kidogo kutoka kwa serikali kwa sababu mbunge ni adui waRais. Lakini siku moja huyo mtu anahamia eneo lingine ambalo mbunge wake ni mtoto wa Rais. Niwazi kwamba atafaidika sana kwa sababu mbunge wake ni mtoto wa Rais. Vivyo hivyo wale ambaohawajaokoka wako katika Adamu ambaye ni mwakilishi wao na ambaye alianguka dhambini. Kwahivyo wao pia wanahesabiwa kuwa wenye dhambi na maadui wa Mungu. Lakini yule ambayeanaokoka anaondolewa kutoka katika Adamu na kuletwa katika Kristo ambaye ndiye Mwana waMungu. Kwa hivyo wao sasa wanapata baraka zote kutoka kwa Mungu kwa sababu Mwakilishi waondiye Mwana wa Mungu.Mtu mmojaKatika kifungu hiki cha Warumi 5, neno la kuzingatia sana ni “Mtu mmoja.” Kila jambo ambaloAdamu alifanya, kila mtu anahesabiwa amelifanya. Adamu baada ya kuanguka dhambini, hakuwa nauhusiano na Mungu, na kwa hivyo wale ambao wako katika Adamu pia hawana uhusiano wowote naMungu. Kwa njia hiyo hiyo kila jambo ambalo Kristo alifanya akiwa mtu Mmoja, limehesabiwa kwawale wote ambao anawakilisha, pia maisha Yake matakatifu yamehesabiwa kwa wale ambaoanawakilisha. Kile ninamaanisha ni kwamba kulingana na mafundisho ya Biblia, wakati Adamualitenda dhambi, kila mwanadamu alitenda ile dhambi. Hii ndiyo sababu Biblia inasema, “Kwa hiyokama vile dhambi ilivyoingia ulimwenguni kupitia kwa mtu mmoja na kupitia dhambi hii, mautiikawafikia watu wote, kwa sababu wote wamefanya dhambi” (Warumi 5:12). Vilevile, wakati Kristoalitii sheria ya Mungu wale wote ambao wameokoka walitii pamoja naye. Hii ndiyo sababu Bibliainasema, “Kwa tendo la mtu mmoja la haki huleta kuhesabiwa haki kule kuletako uzima kwawote.vivyo hivyo kwa kutii kwa mtu mmoja wengi watafanywa wenye haki” (Warumi 5:18,19).Tunaona hapa hali ya mwanadamu kwamba yeye amenaswa katika dhambi. “Hakuna mwenye haki,hakuna hata mmoja.Kwa kuwa wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu waMungu” (Warumi 3:10;23). Je, kwa nini ikawa hivi? Je, ni kwa sababu kwamba kila mwanadamumwenyewe amechagua kutenda dhambi? Biblia inasema, la. Jibu lile Biblia inapeana katika Warumi3:10;23 ni kwamba, kila mwanadamu ni mwovu kwa sababu ya dhambi ya Adamu ambaye ndiyemwakilishi wa kizazi chote cha mwanadamu. Paulo anasisitizia jambo hili katika Warumi 5. Anasema,dhambi iliingia ulimwenguni kupitia “kwa mtu mmoja” (mstari wa 12), “Wengi walikufa kwa sababuya kosa la mtu mmoja” (mstari wa 15), “Hukumu ilikuja kwa njia ya mtu mmoja” (Mstari wa 16),“Kwa maana ikiwa kutokana na kosa la mtu mmoja, mauti ilitawala” (Mstari wa 17), “Kwa hivyo kamavile kosa la mtu mmoja lilivyoleta hukumu kwa watu wote” (Mstari wa 18), “Kwa maana kwa vile kwakutotii kwa yule mtu mmoja wengi walifanywa wenye dhambi” (Mstari 19).Je, unafahamu kusisitizwa kwa maneno haya: “Mtu mmoja”? Sisi sote ni watenda dhambi kwa sababuya uhusiano wetu na Adamu. Kwa ufupi ni kwamba, “Wanadamu wote ambao wametoka kwa Adamu,kwa asili, wamefanya dhambi ndani mwake na wakaanguka naye katika dhambi ya kwanza.” Sisi sotetulikuwa ndani mwa Adamu wakati alipoanguka katika dhambi na mauti ilitufikia na hukumu kwa

kupitia kwake. Dhambi ndiyo hali ya kila mwanadamu ulimwenguni kote kwa sababu sisi kwa asili niwatoto wa Adamu.Hata katika hali hii, tunamshukuru Mungu kwamba huu siyo mwisho wa kila mwanadamu kwa sababukuna wokovu ambao umeahidiwa pamoja na uzima wa milele na baraka tele tele. Je, wokovu huuunatufikia aje? Je, ni kwa njia gani mtu anaweza kupata wokovu huu? Hapa ndipo mtume Pauloanatueleza ukweli wote ambao unapatikana katika Biblia. Hapa ndiyo kuna mabishano ya wengiambao wanawaza kwamba wokovu hupatikana kwa kufanya matendo mazuri na kwa kujitahidi kwaokuwa wazuri. Maoni ya watu hawa ni kwamba, Mungu ni kama ametengeza mtihani na kwamba mtulazima ajitahidi kibinafsi apite mtihani huu. Na wanawaza kwamba ni juhudi za mtu ambazozitamsaidia kupita mtihani huu. Ikiwa mtu atajitahidi sana kwa kufanya vizuri sana, basi atapitamtihani huu na ataokoka.Lakini Paulo anauliza, je, ni namna hii tulipotea kwanza? Jibu ni la, kwa sababu tumepotea kupitiakwa mtu mmoja, yaani Adamu, ambaye ni mwalikishi wa kizazi cha wanadamu wote. Ikiwa tulipoteakwa njia hii, je, tutaokolewa aje? Jibu ni kwamba tunwaweza tu kuokolewa kupitia kwa Mtu Mmoja,kwa sababu tulianguka dhambini kupitia mtu mmoja.Warumi 5 inaendelea kusema, “Neema ya Mungu na ile karamu iliyokuja kwa neema ya mtu mmoja,yaani Kristo imezidi kuwa nyingi kwa ajili ya wengi” (mstari wa 15), “Wale wanaopokea wingi waneema ya Mungu na karamu Yake ya kuhesabiwa haki, watatawala katika uzima kwa njia ya huyo mtummoja, yaani, Yesu Kristo” (mstari wa 17), “Tendo la mtu mmoja la haki huleta kuhesabiwa haki kulekuletako uzima wa wote” (mstari wa 18) na “Kwa kutii kwa mtu mmoja wengi watafanywa wenyehaki” (mstari wa 19).Je, unaona hapa jinsi Mungu mwenye hekima yote anavyodhihirishwa? Yeye ni Mungu ambaye anajuamwanzo hadi mwisho na ambaye amepanga kila kitu kwa njia kuu zaidi. Njia tunapaswa kutumiakurudi kwa Mungu ndiyo ile ile ambayo tulitumia wakati tulitoka Kwake. Njia ya wokovu wetuambayo ni kuu zaidi kuliko kuanguka kwetu dhambini, inaweza kudhihirisha jinsi tulianguka dhambini.Katika Adamu tulianguka dhambini. Katika Adamu tulikufa kiroho na tulihukumiwa, lakini katikaKristo tumetii sheria zote za Mungu na kwa hivyo tunaishi kiroho. Katika Kristo tumeishi maishamakamilifu, katika Kristo tumelipa deni la dhambi, katika Kristo tumefufuliwa na katika Kristotunaishi milele. Kila kitu ambacho Kristo alifanya kwa wokovu wetu, Mungu Baba anahesabukwamba sisi wenyewe tumekifanya. Mateso yake yote yanahesabiwa yetu na ushindi Wake msalabanini ushindi wetu.Hii ndiyo sababu Mungu anatazama wanadamu wakiwa katika vikundi viwili, yaani wale ambao wakokatika Adamu, na wale ambao wako katika Kristo Yesu. Ukweli ambao uko katika Biblia ni kwambakuna watu wawili ambao waliishi hapa ulimwenguni na kila maisha ya mwanadamu yanategemea hawawawili. Biblia inasema kwamba, “Kwa maana kama vile katika Adamu watu wote wanakufa, vivyohivyo katika Kristo wote watafanywa hai” (1 Wakorintho 15:22). Mimi na wewe tuko katika Adamuau Kristo, na kwa hivyo mwishowe kuishi au kufa kwetu kunategemea ni nani mwakilishi wetu. Kwahivyo sasa tunaweza kufahamu ni nini Paulo anamaanisha wakati anamwita mwokozi “Adamu wamwisho au Mtu wa pili.” Kristo ndiye kichwa cha kila mtu ambaye ameokoka na amewafanya kuwawatu wapya. Yeye ndiye kichwa cha mwanamume na mwanamke ambao wako katika uhusiano na

Mungu, na Mungu anawashughulikia kwa njia mpya kabisa.Sasa kila mkristo ameondolewa kutoka kwa Adamu na ameletwa katika Kristo, ambaye ndiyemwakilishi wa Agano Jipya. Tumeunganishwa kwa “Mtu wa pili.” Kwa sababu ya Kristo Yesu kunawanaume na wanawake wengi wapya, idadi ambayo isiyohesabika: “Umati mkubwa wa watu ambaohakuna ye yote awezaye kuuhesabu. Kutoka kila taifa, kila kabila, kila jamaa na kila lugha” (Ufunuo7:9). Kristo ndiye mwokozi ambaye tunaitwa kuamini. Kuungana na Kristo kunamaanisha kuwasehemu ya mpango wa Mungu wa kufanya kila kitu kuwa kipya.Mabadiliko makubwaWokovu ni kuondolewa katika Adamu na kuletwa katika Kristo Yesu. Haya ni mabadiliko makubwasana ambayo yanaweza tu kufanywa na Mungu pekee. Wale wote ambao wameokoka sasawanawakilishwa na Kristo mbele ya Mungu na wamefanywa watu wapya. Wokovu ni kuunganishwakwa Kristo Yesu Mwenyewe. Ni Mungu Roho Mtakatifu mwenyewe ambaye anafanya kazi hii, niYeye mwenyewe ambaye anatuwezesha tuwe katika Kristo milele. Yeye ndiye anayetuondoa kutokakatika Adamu na kutuleta katika Kristo. Wakati Paulo anaandika kuhusu kanisa anasema, “KatikaRoho mmoja wote tulibatizwa katika mwili mmoja” (1 Wakorintho 12:13).Je, jambo hili linafanyika aje? Je, tunawezaje kujua kwamba mtu ameunganishwa kwa Kristo na RohoMtakatifu? Ishara ni imani. Kile Roho Mtakatifu anafanya ni kwamba anatuleta katika wokovu wetuambao uligharamiwa na Kristo Yesu Mwenyewe. Wakati Roho Mtakatifu anatufanya tuzaliwe mara yapili, huwa anatuwezesha kumwamini Kristo na hili ndilo jambo muhimu sana kwetu. Ni kwa imanitunakuja kwa Kristo na bila imani hatuwezi kuja kwake na kuokolewa.Haya ni mafundisho ya undani sana, na hakuna yeyote ambaye anaweza kuyaelewa kabisa, zaidi yajinsi Mungu ameyafunua kwetu. Ukweli ni kwamba wateule wa Mungu wamekuwa katika Kristokabla ya Mungu kuweka misingi ya ulimwengu (Waefeso 1:4). Kabla hajasulibishwa, Bwana YesuKristo alimwomba Baba, “Nimewajulisha Jina Lako wale ulionipa kutoka katika ulimwengu.Walikuwa wako, ukanipa Mimi, nao wamelitii Neno Lako” (Yohana 17:6). Wale wote ambaowataokoka milele, Mungu Baba aliwachagua kabla ya Yeye kuumba ulimwengu, na alimpa Kristo watuhawa. Hii ndiyo sababu wao wameunganishwa kwa Kristo tangu milele. Hii inamaanisha kwambakabla ya Mungu kuweka misingi ya ulimwengu, Yeye aliwachagua wakristo wote wawe katika KristoLakini pia hatuwezi kuingia katika ushirika huu au kufurahia baraka zake hadi wakati tunaamini. Pauloaliwakumbusha wakristo wa mji wa Efeso ambao walikuwa wamechaguliwa kwamba kulikwa nawakati ambapo wao walikuwa wafu katika makosa na dhambi zao ambazo walizitenda (Waefeso2:1-2). Pia Paulo anasema hivi kuhusu Andronico na Yunia katika waraka wa Warumi kwamba,“walikuwa katika Kristo kabla yangu”(Warumi 16:7). Sababu ya Paulo kusema hivi haikuwa kwambayeye hakuwa amechaguliwa na Mungu, bali ni kwa sababu yeye hakuwa ameamini wakati huo. Yaanimtu anaweza kuwa katika Kristo kwa sababu amechaguliwa na Mungu aokoka, lakini awe badohajamwamini Kristo na kuokoka. Kuamini ni jambo muhimu sana, na hii ndiyo sababu Biblia inasema,“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu

amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16).Kuamini katika Kristo.Je, inamaanisha nini kuamini? Huwa mara mingi tunaamini mambo ambayo tunaambiwa au kuona.Kwa mfano tunaamini kwamba Kampala ni mji mkuu katika nchi ya Uganda kwa sababu tumeambiwajambo hili. Lakini kuamini jambo hili hakuwezi kubadilisha maisha yetu au kutuletea furaha. Hili nijambo kweli lakini halileti mabadiliko maishani mwetu.Hii siyo ukweli wakati tunazungumza kuhusu kumwamini Kristo. Kumwamini Kristo ni zaidi yakukubali kwamba Yeye aliishi hapa ulimwenguni na akateseka na kufa kwa ajili ya watenda dhambi.Kumwamini Kristo ni kuishi ndani Mwake na kufanya yale ambayo yanamtukuza Yeye mwenyewe.Kunamaanisha kujitambulisha kwamba wewe ni mtu wa Kristo na kujitolea kabisa kwa ajili Yakepekee. Ikiwa unamwamini Kristo, basi wewe unategemea Yeye kwa kila kitu. Ni Yeye pekee ambayeunamtazama na kumtegemea kwa kila kitu. Wewe ni mmoja wa mwili Wake sasa na kwa milele yote.Yeye ni kila kitu kwako, uaminifu wako sasa ni Kwake. Wewe uko ndani Mwake na Yeye ndiyemaisha yako ya milele. Ndani Mwake wewe ni kiumbe kipya. Waza juu ya mitume, je kumwaminikulimaanisha nini kwao? Kuamini kulimaansiha kubadilishwa kabisa kutoka ndani mwao.Walijitambulisha naye mbele za watu na walimsikiza na kuzungumza naye. Kila kitu ambachoaliwaambia waliamini na walijaribu kukitii. Yesu Kristo na wanafunzi wake walitembea nchini kotepamoja. Walitembea pamoja, wakafanya kazi pamoja na walitatizwa pamoja. Walikuwa pamoja nayena walisimama naye. Kwao kuamini kulimaaninisha kujitolea kabisa kwa ajili ya Bwana Yesu Kristomilele. Hii ndiyo sababu Petro alimwambia Kristo, “Tazama, sisi tumeacha kila kitu nakukufuata” (Mathayo 19:27).Tunapokuja kwa Kristo Yesu kwa imani, tunaweza kukosa kujua kwamba tunafaa kujitolea kabisa.Bwana arusi huwa hafahamu kabisa siku ya ndoa jinsi maisha yake yatakavyobadilika, kwamba ujanawake unabadilika na mke ambaye anaoa ako na mipango mingi juu ya maisha yake. Sasa bwana arusihuyu hajui kabisa kwamba pesa ambayo alikuwa anatumia kwa starehe zake sasa mke wake atazitumiakwa mahitaji ya nyumba. Masaa ambayo alikuwa akimaliza kwa kutazama mpira kwa runinga, baadaya kuoa anapaswa kuyatumia kuwa pamoja na mke wake. Sasa yeye hayuko peke yake, na kwa hivyoni lazima ajifunze kuishi kwa ajili ya mke wake. Lakini hata kama haelewi kabisa majukumu hayayote, ukweli ni kwamba majukumu haya yako hapo hadi afe. Aliapa kuyatekeleza kikamilifu katikahali zote za maisha. Hivi ndivyo ilivyo kujitolea kwa ajili ya Kristo Yesu.Imani ambayo inayohubiriwa katika makanisa mengi leo ni imani ya kuwapotosha watu. Watuwanaambiwa kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu na kile wanahitaji kufanya ni kukubalikwamba kweli jambo hili lilifanyika na kwamba dhabihu yake ilikuwa kwa ajili yetu. Wanaambiwakwamba hii ni imani ya wokovu ambayo kila mtu anahitaji ili awe mkristo. Ni kama mtu ambaye akona deni kubwa sana na siku moja anasikia kwamba kuna mtu ambaye ako tayari kumlipia deni hilo.Anaambiwa kwamba kile anahitaji kufanya ni kukubali kwamba ako na deni hilo na mara mojalitalipwa hata kama mtu mwenye kulilipa hamfahamu. Yeye bora tu aelewe kwamba deni lakelimelipwa na mtu mwingine.Imani iletayo wokovu kulingana na Biblia ni tofauti sana na mafundisho haya. Imani iletayo wokovu

kulingana na Biblia inafanya kazi na iko. Agano Jipya linazungumza kuhusu kuamini katika Kristo aujuu ya Kristo. Maneno haya yote yanafundisha kwamba imani ya ukweli inatuleta katika uhusiano wakaribu sana na Kristo na inatuunganisha kwa Kristo. Kuamini kunamaanisha kuja kwa Kristo Yesu,kumpokea Kristo Yesu na kumwamini Kristo Yesu kwa wokovo wetu. Kristo alisema kwambakumwamini ni kama kunywa damu Yake na kula mwili wake (Yohana 6:53). Kuamini kunamanishakuingia ndani ya Kristo, kuwa Wake, kuwa pamoja naye na kuunganishwa Kwake milele. Imani yawokovu si kupokea baraka za mtu ambaye hatumjui na hatujawahi kutana naye. Badala yakeinamaanisha kuwa na uwezo wa kusema “Kwa maana kwangu mimi, kuishi ni Kristo” (Wafilipi 1:21).Hii ndiyo sababu maandiko yanatuonyesha kwamba uhusiano wetu na Kristo ni wa karibu sana. Sisindiyo mawe katika jengo na Yeye ndiye jiwe kuu (Waefeso 2:19-22; 1 Petro 2:4-8); sisi ni matawi naKristo nd

Maisha ndani ya Kristo Utangulizi Kuwa mkristo ni kuwa na uhusiano na ushirika na Bwana Yesu Kristo. Swali ni, je uhusiano huu . Tutaona jinsi kuunganishwa kwa Kristo kunatuletea maisha mapya na pia tutaona jinsi tunafaa kumtegemea Kristo pekee katika maisha yetu tunapoishi katika ulimwengu huu mwovu. Tutasoma

Related Documents:

MAISHA MAPYA NDANI YA KRISTO-SOMO LA KWANZA 7 Uamuzi wa muhimu Sana katika maisha yako, ni kumkubali Yesu Kristo awe bwana na mwokozi wa maisha yako. Yohana 3:3 inasema, mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuona ufalme wa mbinguni. Ulipomuamini Yesu awe mwokozi wako, ulizaliwa mara ya pili.Kuzaliwa kwako upya kwa roho wa Mungu, .

7. Onyesha kwa vitendo maisha yako mapya kwa kuonyesha upendo na shauku ya kuwajali wengine. Maisha inayotawaliwa na Kristo Maisha ya Mkristo yanaweza kuwakilishwa na picha ya msalaba. Kristo ndiye kiini cha maisha yetu mapya. Tunaishi kwa kujisalimi-sha kwake.Mstari ulio wima, unawakilisha ushirika wetu pamoja na Mungu kwa maombi na kwa kusoma .

Sasa Kristo anaishi ndani yako. Tamaa yako ya kumpendeza itaongeza kumpendeza Yeye zaidi ya wewe. Katika mfululizo wa masomo ya Maisha mapya ndani ya Yesu, ulifundiswa juu ya maombi na kusoma biblia. Tutatazama kwa undani sana nguzo hizi mbili muhimu ambazo zitabadilisha maisha yako na kukuwezesha kumpendeza Kristo ambaye kwa hiari yake

kwamba maisha ya dhambi yatamharibu kabisa, na maisha ya wokovu katika Kristo yatamletea faida kubwa sana. Kwa hivyo alikuwa na vita hivi ndani yake: kuendelea kufuata maisha ya dhambi na kujiharibu au kufuata maisha matakatifu katika Kristo na kupata furaha nyingi kwa kuokoka. Augustine aliandika, “Vita hivi viliendelea ndani yangu hadi .

Hili ni toleo la kwanza la Kiswahili la Maisha mapya ndani ya Kristo. Toleo hili lilitolewa kwa mara ya kwanza kabisa kwa Kiispaniola kama NUEVA VIDA EN CRISTO. Kusudi lake ni kukupa msingi imara katika maisha yako ya Kikristo.Epuka kunakili moja kwa moja kutoka kwenye Biblia unapojibu maswali baada ya kila somo. Jaribu

Somo la 7: Kanisa la Kristo Somo la 8: Maisha mapya katika Kristo . mafundisho ya Kristo, bali akayaacha, yeye hana Mungu. Ye yote anayedumu katika mafundisho ana Baba na Mwana pia” . ndani Yake, vivyo hivyo amempa Mwana kuwa na uzima ndani Yake. Naye amempa Mwanawe mamlaka ya kuhukumu kwa kuwa Yeye ni Mwana wa .

Kuishi maisha kutoka kwa chanzo mapya Kitabu cha kwanza katika mfululizo Kuishi maisha iliyobadilika . nilikuwa na mapambano makubwa ya ndani ya uhaba, uoga, . Anasema kwamba maisha ya Kristo ni Zaidi ya uzima wa milele aliokupa katika wokovu. Anasema kwamba Yesu ni maisha yako leo, wakati huu.

The first concert showcases one of Australia’s best pianists, with a special ballet accompaniment, and the second will star the just announced winner of the Sydney International Piano Competition. Head of Piano Studies at the Australian National Academy of Music, Timothy Young will perform the first concert in the series on Tuesday 7 August. Young will challenge the audience with the .