MADA YA UTAFITI: ATHARI ZA LUGHA YA KIJITA KATIKA .

3y ago
566 Views
9 Downloads
1.13 MB
101 Pages
Last View : 6d ago
Last Download : 3m ago
Upload by : Baylee Stein
Transcription

iMADA YA UTAFITI: ATHARI ZA LUGHA YA KIJITA KATIKAKUJIFUNZA KISWAHILIMASHAKA WENCESLAUSTASNIFU HII IMEWASILISHWA KWA AJILI YA KUKAMILISHAMASHARTI YA SHAHADA YA UZAMILI M.A (KISWAHILI) KITIVOCHA SANAA NA SAYANSI YA JAMII.CHUO KIKUU HURIA CHATANZANIA.NOVEMBA, 2015

iiUTHIBITISHOAliyetia saini hapa chini anathibitisha kuwa, amesoma na anapendekeza Tasnifu hii inayohusuAthari za lugha ya Kijita katika kujifunza Kiswahili, ipokelewe na ikubaliwe na Chuo KikuuHuria cha Tanzania, kwa ajili ya kukamilisha matakwa ya kuhitimu shahada ya Uzamili yaKiswahili ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. .Dktr Anna. M. KisheMsimamiziTarehe .

iiiTAMKO LA MTAHINIWAMimi Mashaka Wenceslaus, ninatamka na ninathibitisha kwamba,Tasnifu hii iitwayo Athariya lugha ya Kijita katika kujifunza Kiswahli ni kazi yangu mimi mwenyewe kwamba,haijawahi kuwasilishwa na wala haitawasilishwa katika chuo kingine chochote kwa ajili yakutunukiwa shahada yoyote .Saini------------------------Mashaka WenceslausTarehe---------------------------

ivHAKI MILIKISehemu yoyote ya Tasnifu hii hairusiwi kukaririwa, kunakiliwa, kuhifadhiwa kwa njia yoyoteile au kuhawilishwa kwa mbinu yoyote ile au kurudufu katika hali yoyote bila kupata idhiniya mwandishi wa Tasnifu hii au Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kwa niaba yake.

vTABARUKUKazi hii ninaitabaruku kwa wazazi wangu wapendwababa Karisti Mwanga Etonya na mamayangu Scholastika Nyanjugu Mulungu kwa kunisomesha toka darasa la kwanza hadi ChuoKikuu .Walinilea kwa kunitia moyo na kunihimiza kusoma kwa bidii, wamenipa msingi wamaisha katika dunia hii.Pia, bila kumsahau mke wangu mpendwa, Beatrice Bwire pamoja nawatoto wangu.Mwenyezi Mungu awabariki sana.

viSHUKURANIKwanza kabisa, ninapenda kumshukuru mwenyezi Mungu mwingi wa rehema ambayeamenisaidia na amenibariki katika kufanikisha kazi yangu hii. Shukurani zangu za pekeezimwendee msimamizi wangu wa utafiti huu Dktr. Anna.M.Kishe kwa kubeba jukumu lakuisimamia vyema kazi hii. Nimemshukuru kwa ujasiri na uvumilivu wake mkubwa tokeahatua ya kuandika pendekezo la utafiti hadi kumalizika kwa kazi hii. Ninaamini kuwaamenivumilia vya kutosha kwa udhaifu wangukama binadamu na kama mwanafunziMafanikio yaTasnifu hii yametokana na juhudi yake kubwa ya kusoma, kukosoa , kurekebisha,kuelekeza na kushauri yale yote yanayofaa kuzingatiwa katika utafiti huu. Licha yamajukumu mengi aliyonayo hakusita hata mara moja kusoma kazi yangu kwa umakinimkubwa kwa wakati na kutoa maelekezo yanayojenga kazi hii kwa muda wote nawakati ufaao. Sina cha kumlipa ila nina muombea dua kwa mwenyezi Mungu ampemaisha marefu na amzidishie nguvu na imani ili aweze kutoa mchango kwa wanataalumana taifa kwa ujumla. Nawashukuru wahadhiri wote wa Idara ya Kiswahili katika ChuoKikuu Huria cha Tanzania kwa mchango wao walionipa: Prof. Mbogo, Prof .Mdee, Prof.Sengo, Dktr. Zelda, Dktr .Simpasa, na Dktr. Lipembe, Mungu awape maisha marefu na yafuraha katika maisha yao yote ili waendelee kutoa mchango wa kitaaluma na wa kijamiikatika Taifa letu. Vilevile ninatoa shukurani zangu za dhati kwa wanafunzi wenzangu wotewa shahada ya uzamili ya Kiswahili wa mwaka wa masomo 2014\ 2015. Shukurani hizi zapekee zimetokana na ushirikiano waowa dhati kwa kipindi chote cha masomo yauzamili. Mwenyezi Mungu awazidishie moyo wa kupendana na kusaidiana. Vilevile ,ninatoashukurani zanguza dhati kwa wazaziwangu, mzee KarisitiMwangaEtonya naScholastika Nyanjugu Mulungu pamoja na familia yangu kwa kuniendeleza kielimu hadi

viikufikia hatua hii ya juu. Nawashukuru kwa msaada wao wa hali na mali, MwenyeziMungu awajalie afya na rehema tele.

viiiIKISIRILengo la Tasnifu hii ni kuchunguza Athari ya lugha ya Kijita Katika Kujifunza lugha KiswahiliKwa Wanafunzi wa Shule za Msingi, sababu za athari hizo na mbinu za kutatua athari hizo.Utafiti huu umefanywa Wilaya ya Musoma vijijini na Manispaa ya Musoma katika mkoa waMara. Kata mbili zilishirikishwa ambazo ni kata ya Suguti na Makoko. Shule za msingi zaSuguti, Kusenyi, Buhare, Nyarigamba na Mtakuja zilichunguzwa ili kubaini athari za lugha yaKijita katika kujifunza Kiswahili.Utafiti huu umetumia nadharia ya Fonolojia Zalishi Asiliaambayo huchunguza bayana athari hizo za lugha ya kwanza ( Kijita) katika kujifunza lughaya Kiswahili. Aidha nadharia hii huchukulia kuwa makosa katika lugha ya pili ( Kiswahili)husababishwa na athari ya lugha ya kwanza. Utafiti huu ulitumia mbinu tatu za ukusanyajidata ambazo ni; hojaji, mahojiano, na majadiliano ya vikunndi. Sampuli ya utafiti huuiliteuliwa kwa kutumia mbinu ya; madhumuni maalumu, kimfumo na uteuzi wa nasibutakabishi. Matokeo ya utafiti huu umegundua kuwa, athari za matamshi zinazojitokeza kwawanafunzi wanapojifunza lugha ya Kiswahili ni pamoja na udondoshaji wa sauti , kutumiasauti zinazokaribiana, na kuongeza viambishi visivyohitajika. Aidha utafiti huu umegunduasababu zinazotokana na athari hizi ni lugha mama na athari ya kimazingira. Utafiti huuuligundua mbinu za kutatua tatizo hili ni watoto wafundishwe Kiswahili wakiwa badowadogo na wazazi wawe mfano bora kwa watoto wao katika kuzungumza Kiswahili nakuwapa zana malimbali za ujifunzaji kwa mfano kamusi na kadhalika. Matokeo ya utafiti huuyaliwasilishwa katika sura ya nne, yanaweza kutumiwa na Taasisi ya ukuzaji mitaala kutoamapendekezo kwa wanaojifunza Kiswahili kwa kuwashirikisha wanafunzi kimazungumzokwa lengo la kuinua kiwango cha umilisi wa lugha.

ixYALIYOMOUTHIBITISHO. .ITAMKO LA MTAHINIWA . .IIHAKI MILIKI . .IVTABARUKU. .VORODHA YA VIFUPISHO MUHIMU VIORODHA YA MAJEDWALI VIIYALIYOMO VIIIIKISIRI .IXSURA YA KWANZA . 11.0UTANGULIZI 11.1Utangulizi 11.1.1Lugha ya Kijita . . 1-21.1.2Historia ya Wajita ,21.1.3.Asili yaChimbuko la Wajita 1.1.4Lugha ya Kiswahili . .3-51.2 .2-3Usuli wa Tatizo . . 5-7

x1.3Tatizo la Utafiti .7-91.4Malengo yaUtafiti . 91.4.1Lengo kuu la Utafiti 91.4.2Malengo Mahususi . . 9-101.5Maswali ya Utafiti . .101.6Umuhimu wa Utafiti .10 -111.7Yaliyoandikwa kuhusu Mada hili . .111.8Mipaka ya Utafiti 11 -121.9Vikwazo vya Utafiti . . 131.10Hitimisho . .14SURA YA PILI .152.0MAPITIO YA KAZI MBALIMBALI .152.1Utangulizi .152.2Mapitio ya kazi mbalimbali . .15-162.2.1Mapitio ya kazi za kitaaluma kuhusu mada hii 16-262.3Pengo la Utafiti. . .262.4Kiunzi cha Nadharia . .27-31

xiSURA YA TATU .323.0.323.1NJIA NA MBINU ZA UTAFITI Utangulizi . .323.2Eneo la utafiti 333.3Mbinu za utafiti 3.4 .1.Mbinu ya Hojaji 3.4.2Mbinu ya Mahojiano 35-363.4.3Majadiliano ya vikundi 363.5Aina za data zilizokusanywa . .363.5.1Data za msingi /Awali . .3.5.2Data za Upili /Fuatizi .3.6Wahusika Lengwa . . 33 .33-3536-37.-37 -38.383.7Sampuli na Usampulishaji wa Kundi Lengwa . .383.7.1Sampuli ya Utafiti 3.7.2Mchakato wa Usampulishaji 3.8Mbinu za Kuchanganua Da . 41 -4238-40.40-41

xii3.9Uthabiti na Kuaminika kwa Mbinu zfiti 423.9.1Uthabiti wa Mbinu za Kukusanyia Data .42-433.9.2Kuaminika Kwa Data 433.10Ukusanyaji wa Data . 433.11Zana za kukusanyia Data .43-443.12Maadili ya Utafiti 3.13Hitimisho SURA YA NNE 4444-45464.0UWASILISHAJI NA UCHAMBUA DATA 464.1Utangulizi .464.2Uwasilishaji wa Data . . 474.3Uchambuzi wa Data kwa Njia ya Majedwali . 49-494.4Athari za lugha ya Kijita katika kujifunza Kiswahili 494.5.1Athari za Kifonolojia Katika Matamshi 49-504.5.2Athari Katika Matumizi ya /h/ .504.5.3Athari katika matumizi ya /z/ badala ya /dh/ . 514.5.4Athari za matumizi ya /s/badala y a /dh/ 52

xiii4.5.5Athari za Matumizi ya /s/ badala ya /z/ 524.5.6Athari za Matumizi ya /r/badala ya /l/ 53-544.5.7Athari za Matumizi ya /g/ badala ya /gh/ .544.5.8Athari za Matumizi ya /bh/ badala ya /b/ .54-554.5.9Kuongeza Viambishi Visivyohitajika .554.5.10Mwalimu Kutojua Lugha Vizuri 59-624.6Sababu za Wanafunzi wa Kijita Kuathiriwa Katika Kujifunza Kiswahili 624.6.1Lugha Mama . 63 -664.6.2Mazingira . 4.766-68Njia za Kuondoa Athari za Kimatamshi Katika Lugha ya Kijita Katika KujifunzaKiswahili 4.7.14.7.268Watoto Wafundishwe Lugha ya Kiswahili Tangia Utotoni . 68-69Kuwaelekeza Wanafunzi juu ya Utamkaji Sahihi wa Maneno yaKiswahili 4.7.34.869Wazazi wawe Vielelezo Katika Ujifunzaji waLlugha ya -------------------------------------70-71SURA YA TANO 72

xiv5.0MUHTASARI, MAPENDEKEZO NA HITIMISHO 725.1Utangulizi 725.2Muhtasari wa Matokeo ya Utafiti ----72-735.3Mapendekezo ya utafiti . 735.4Mchango wa utafiti sho . 75Marejeo .76-79Viambatanisho 80-90

xvISHARA NA VIFUPISHO MUHIMU[]Mabano ya Fonetiki//Uwasilishaji wa FoimuFZFonolojia ZalishiNFZANadharia ya Fonolojia Zalishi AsiliaSPESound Patterns of EnglishAGPAspects of Generative PhonologyINGPNGMZIntroduction to Natural Generative PhonologyNadharia ya Geuza Maumbo Zalishi

xviORODHA YA MAJEDWALIJedwali 2.1:Uhusiano Kati ya Lugha ya Kiswahili na Kibantu .22Jedwali 2.2 :Maumbo Kati yaLugha ya Kiswahili na Kijita 23Jedwali 3.1:Mgawanyo wa Sampuli .40Jedwali 4.1 :Athari za Kifonolojia Katika Matamshi . 56Jedwali 4.2 :Majibu Kutokana naLugha Mama 64Jedwali 4.3 :Utumiaji wa Lugha ya Kijita na Kiswahili Jedwali 4.4:Majibu Kutokana na Mazingira 6665

1SURA YA KWANZA1.01.1UTANGULIZIUtanguliziSura hii ni sura tangulizi ambayo inazohusiana na mada ya utafiti ambayo ni athari ya lughaya Kijita katika kujifunza Kiswahili. Utafiti huu unabainisha na kuelezea juu ya tafasiri yadhana ya lugha ya Kijita, historia ya lugha ya Kijita,chimbuko la Wajita,lugha yaKiswahili,usuli wa tatizo, tamko la tatizo la utafiti,malengo ya utafiti,maswali yautafitiambayo utafiti huu ulikusudia kuyajibu na umuhimu wa utafiti. Aidha, sura hii inaelezeakuhusu mipaka ya utafiti, matatizo ya utafiti tuliyokumbana nayo katika utafiti.1.1.1Lugha ya KijitaKijita ni lugha inayozungumzwa na watu waitwao Wajita nchini Tanzania wanaoishi mkoa waMara, hasa wilaya ya Musoma vijijini na Manispaa ya Musoma. Heinne (1980) wakimnukuuGuthrie (1948), waliainisha wazungumzaji wa lugha ya Kibantu katika makundi matano.Kijita kikiwa miongoni mwa lughaza Kibantu katika tapo la kati la E 20.Pia Wajitawanajishughulisha na uvuvi, kilimo, ufugaji, na wana mila, desturi na tamaduni zao.Chachage (2002) katika makala yake kuhusu juuya ‘utandawazinamigogoroyautamaduni’’ akimnukuu Nyerere (1962), katika hotuba yake ya uzinduzi wa Jamhuri yaTanganyika pamoja na masuala mengine kwamba,nchi isiyokuwa na utamaduni wake nikuhusu historia ya utamaduni wa Tanganyika. Kwamba,nchi isiyokuwa na utamaduni

2wake ni sawa na mkusanyiko wa watu ambao hawana roho iwezayo kuwa Taifa’’.Utamaduniwa Wajita ni moja ya tamaduni zinazochangia kuwepo na Taifa la Tanzania.1.1.2Historia ya WajitaKwa mujibu wa manyama (2013) wajita ni kabila mojawapo la Tanzania wanaoishikatika mkoa wa Mara Wilaya ya Musoma vijijini. Manyama (2013:1-3) aliendelea kusemakuwa, neno majita lilitokana na mlima “Masita” ambao ndio chimbuko la jina la kabila laWajita, na sehemu yao wanayokaa inaitwa majita. Mlima huu mpaka leo unaitwa Masita(mtiro) ambao ni mlima mrefu mkoani Mara wenye futi 4,916, kutoka usawa wa bahari. Hiiilitokana na kwamba, wazungu yaani Wadachi (Wajerumani) walishindwa kutamka neno“masita” badala yake wakatamka “Majita”. Kufuatia matamshi hayo watawala wa kikoloniwaliweka katika maandishi, watu wote sasa wanaita sehemu hiyo Majita na kabilalinaitwa Wajita.1.1.3Asili ya Chimbuko la WajitaAsili ya chimbuko la Wajita ni kutoka eneo la kushi nchini Ethiopia. Kutoka Ethiopiawalipitia Sudani, mpaka Uganda, na kupitia visiwa vya Sese kwa mtumbwi mpakaBuhaya (Bukoba), Uzinza (Geita), Bugalika(Mwanza), Emulambo, Bhukerebe(Ukerewe), kisiwa cha Ukara mpaka Majita iliyoko wilaya ya Musoma. Vievile,wengine wanaishi Mkoani Geita, mwambao wa Wilaya ya Sengerema na Biharamulo.Hivyo, kila jamii huwa na lugha mama ambayo mtu amekuwa akiiongea na hivyo

3kujikusanyia msamiati mwingi wa lugha hiyo. Lugha hii huitumia katika mawasilianoya kila siku. Pia kutumia lugha mama kulisaidia sana kuleta maendeleo ya Taifa kwasababu ilirahisisha katika kuwasiliana na kuelewana. Aidha itakayo waunganisha watuhao kwa pamoja, mfano,Tanzania kuna lugha nyingi lakini lugha teule ni Kiswahili.Massamba (2006) alisema kwamba, Wajita ni jamii mojawapo kati ya jamiizinazopatikana katika nchi ya Tanzania, wanaishi mkoa wa Mara. Katika Mkoa huukuna, wajita, Waruri, wakwaya, wazanaki,Waikizu, Wakurya, wanaata, waisenye,wakebhwa, Wawaluo, Walkorua, Washashi, Wangoreme, Wasukuma, wahachanawatatiru kwa kutaja baadhi tu.1.1.4Lugha ya KiswahiliLugha ya Kiswahili ni lugha ya Afrika Mashiriki na kati iliyoenea na kujulikana na wengikatika eneo hili kuliko lugha nyingineyo ya Afrika. Ali (2010), anaeleza kuwa Kiswahili nilugha ya Kibantu inayotumiwa kwa mawasiliano sehemu za Afrika mashariki na Kati .Aidha,ni lugha ya taifa nchini Tanzania, Kenya na Uganda.Vilevile, ni moja kati ya lugha nne za taifanchini Kongo Mwita (2009). Whiteley (1969), alitafiti kuhusu lahaja ya Kimtang’ata nakubainisha kwamba,kuwepo kwa lahaja anuai katika lugha ya Kiswahili kuonesha tofauti zakilugha kutoka lahaja moja na nyingine.Tofauti hizo za kilugha ni pamoja na tofauti zakimsamiati katika lahaja za lugha ya Kiswahili. Hata hivyo, lahaja zifuatazo zimetajwa nawengi wao zikiwemo Kiunguja, Kiamu, kimvita, Kihadimu, Kitumbatu, Kipemba,

4Kimtang’ata, Kivumba, Chichifundi, Kisu, Kitikuu, Chimini, na Kingwana. Kiswahili sanifu ni. Hivyo waswahili hupatikana sehemu ya mwambao wa Pwani ya Afrika ya Masharikiambapo wengi wao ni wafuasi wa dini ya Kiislam Mwita (2009). Kwa kuwa wamekuwa nadini hiyo kwa karne nyingi, maisha yao kwa ujumla, ndoa, ushirika. itikadi na desturi zote zawaswahili,haziwezi kuzungumza kwa undani bila kugusia dini ya kiislamu.Msingi waKiswahili sanifu ni lahaja ya Kiunguja. Lakini kwa vile Kiswahili sanifu ni lugha inayotumiwana watu wengi wenye tofauti za kiutamaduni, kiuchumi na kisiasa,vimeathiriwa sana namsamiati kutoka lugha mbalimbali Zawawi (1979-36). Ni vigumu kuifahamu idadi kamiliya watu wanaozungumza Kiswahili. Lugha hii inatumika kama lugha ya kwanza na wakaziwa mwambao wa Afrika Mashariki kuanzia Somalia upande wa kaskazini hadi visiwa vyaKomoro upande wa kusini Massamba (1990). Kiswahili ni mojawapo ya lugha za kiafrikazilizoenea zaidi barani Afrika.Hatua ya kuchaguliwa kwa Kiswahili kuwa mojawapo ya lughazinazotumika katika muungano wa nchi za Kiafrika kumeipa lugha hii hadhi kubwa. Lugha yaKiswahilii inakuwa na kuvuka mipaka. Haitumiki Afrika Mashariki pekee bali ulimwengunikote, hasa katika vyuo vikuu. Isitoshe Kiswahili kimetumika katika matangazo kwenye idhaambalimbali ulimwenguni kwa mfano Marekani, Japani, Ufaransa, Uchina, na Uingereza. Pia,lugha ya Kiswahili ni Lugha ya mawasiliano katika Afrika ambapo Kiswahili kinatumika kamalugha ya pili na mamilioni ya watu hasa nchini Kenya, Tanzania, Uganda,na hata Zaire

5Mashariki. Vilevile, kuna wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili katika nchi za Burundi,Rwanda, Zambia, Malawi na hata katika nchi za Uarabuni Massamba (1990).1.2Usuli waTatizoMada inayoshughulikiwa katika utafiti huu, ni athari za lugha ya Kijita katika kujifunza lughaya Kiswahili. Kwa mujibu wa wataalamu na watafiti mbalimbali wa Kiswahili. Lugha mama nilugha ambayo mtu alijifunza kwanza maishani mwake kabla ya lugha nyingine. Lugha hiiilitumika katika mawasiliano ya kila siku, Lugha mama ilisaidi sana katika kuleta maendeleoya Taifa kwa ujumla, kwani huirahisishia katika kuwasiliana na kuelewana kwa harakazaidi. Hata hivyo, ni vigumu sana kwa jamii moja kutumia lugha moja katika mawasilianokwa watu wasioifahamu au kwa wazawa wa lugha hiyo. Hivyo ni lazima pawepo na lughateule inayounganisha watu hao, mfano Tanzania kuna lugha nyingi sana lakini lugha teuleiliyowaunganisha ni lugha ya Kiswahili. Kwa msingi huu utafiti ulilenga kuchunguza athariza lugha ya Kijita katika kujifunza lugha ya Kiswahili ambayo ndiyo lugha inayotumikakatika kuwaunganisha watu ambaoKijita sio lugha yao ya kwanza lengo ni kupataukweli kuhusu athari . Mekacha (2011), anasema kwamba lugha moja huathiriwa kutokana namuktadha wa matumizi yake.Mekacha, (ameshatajwa) anabaini kuwa lugha ya Kiswahilihutumiwa hasa katika shughuli za kijamii zaidi kama vile ofisini, shuleni, sehemu zabiashara na sehemu ambazo kuna makabila mengi. Watu wanapokuwa nyumbani kwao kwaasilimia kubwa hutumia lugha zao za asili. Mekacha anaendelea kusema kuwa, matumizi ya

6lugha katika maeneo mbalimbali kama maeneo ya nyumbani na miongoni mwa wanafamiliataratibu za matumizi ya lugha kwa mfano yawezekana wajita ikiwa ni sababu mojawapo yakuwaathiriwawaokatikakwamba kwa kawaidakujifunzalughayaKiswahili. Wajita wengimawasiliano yanayofanyika nyumbanindugu na marafiki hufanyikawameripotibaina ya familia moja,kwa lugha ya kijamii. Idarus (2005wanaeleza makosambalimbali yanayofanywa mara kwa mara katika matumizi ya Kiswahili, pamoja na athariza lugha mbalimbali katika Kiswahili.Athari hizo zimechangiwa na vitu vingi kama vilevyombo vikuu rasmi vya habari vinavyotumia Kiswahili mathalani magazeti, radio naofisikuuzaserikali. Masebo(2008:31-33) anasema kwamba, lugha ya Kiswahilikiliingiliana na lugha nyingine ya Kibantu kwa kuwa, lugha ya Kiswahili ni ya pili katikajamii nyingi za Kibantu, athari ya lugha ya kwanza inaonekana katika matamshi. Vilevile, lugha za Kibantu huziathiri lugha ya Kiswahili katika maana, msamiati na sarufi.Kwa mfano kuna baadhi ya lugha za Kibantu kikiwemo Kijita zilionyesha athari katikalugha ya Kiswahili, Watu wengi sana wameathiriwa na lugha za kikabila wanapozunguzaKiswahili sanifu. Kuna baadhi ya watu wanapozungumza Kiswahili hawaoni tofauti iliyopokatika matamshi kati ya \r \ na \ l\ kwa mfano Wajita. Vile vile, kisarufi wakati mwingine,hutokana na muundo wa lugha ya kwanza, muundo huo wa kwanza huliweza kumuathiri mtukatika kuzungumza lugha ya pili. Pia lugha ya Kiswahili ina maneno mbalimbaliambayo yamechukuliwa kutoka katika makabila mbalimbali na kuwa katikamsamiati

7wake. Tena mara nyingi kuna athari za maana kwa watu wanaozungumza lugha mbili auzaidi.1.3Tamko la Tatizo la UtafitiSuala la athari za lugha ya Ki

mada ya utafiti: athari za lugha ya kijita katika kujifunza kiswahili mashaka wenceslaus tasnifu hii imewasilishwa kwa ajili ya kukamilisha masharti ya shahada ya uzamili m.a (kiswahili) kiti vo cha sanaa na sayansi ya jamii.chuo kikuu huria cha tanzania. novemba, 2015

Related Documents:

Wapemba. Surahii pia inatoa taarifa za awali kuhusu mada ya utafiti ambapo mtafiti ataelezea kuhusu usuli wa mada,tatizo la utafiti,malengo ya utafiti yakiambatana na mswali ya utafiti ,umuhuimu wa utafiti mipaka ya utafiti hatimae hitimisho , haya yote yameelezewa juu ya kuchunguza matumizi ya tafsida katika lahaja

tamko la tatizo la utafiti, lengo kuu na madhumuni mahususi ya utafiti. Aidha maswali ya utafiti, umuhimu wa utafiti, mipaka ya utafiti na mpangilio wa tasnifu pia vimewasilishwa katika sura hii. 1.1 Usuli wa Tatizo la Utafiti Binadamu katika kuishi

v Ramani ya Yaliyomo Mada 1: Kuelewa Mazungumzo na Kujieleza Kimazungumzo Mada 2: Msamiati katika Mazingira ya Shule Mada 3: Msamiati katika Mazingira ya Nyumbani Mada 4: Msamiati katika Mazingira ya Utawala Mada 5: Msamiati katika Mazingira ya Sokoni Mada 6: Matumizi ya Msamiati kuhusu Usafi wa Mwili Idadi ya Vipindi

majelis wali amanat universitas gadjah mada peraturan majelis wali amanat universitas gadjah mada nomor 1 tahun 2021 tentang rencana induk kampus universitas gadjah mada tahun 2017—2037 dengan rahmat tuhan yang maha esa majelis wali amanat universitas gadjah mada, menimbang : bahwa guna melaksanakan ketentuan dalam pasal 57 ayat (3)

tabianchi katika maendeleo ya sasa na unatia maanani fursa za kupunguza ongezeko la hewa mkaa. Katika kutathimini athari za muda mrefu za mabadiliko ya tabianchi ya siku za baadae ,hasa maeneo ambayo yanahitaji hatua za mapema, yaani miundombinu (ya kudumu ) kwa ajili ya athari kubwa na kuc hukua hatua za kukabiliana na hali hiyo

Ikiwa una wasiwasi kuhusu dalili zozote zisizo za kawaida ambazo unaweza kuwa nazo, au una maswali kuhusu mchanganyiko wa athari kutokana na kupata chanjo zaidi ya moja kwa wakati mmoja. Ikiwa una wasiwasi kuhusu athari zako au ikiwa athari haziishi baada ya siku chache.

Naisinyai kati ya Juni 2016 na Februari 2017, ikiwa ni pamoja na ziara za awali, utafiti wa awali na utafiti shirikishi.Tunawashukuru watu wote wa kijiji cha Naisinyai kwa ushiriki na ukarimu wao wakati wote wa utafiti na msaada mkubwa uliotolewa na Halmashauri

ASME BPV CODE, EDITION 2019 Construction Code requirements Section VIII, Div. 1, 2 a 3 ; Section IX ASME BPV Section V, Article 1, T-120(f) ASME BPV Section V, Article 1, Mandatory Appendix III ASME BPV Section V, Article 1, Mandatory Appendix II (for UT-PA, UT-TOFD, RT-DR, RT-CR only ) SNT-TC-1A:2016; ASNT CP-189:2016 ASME B31.1* Section I Section XII ASME BPV Section V, Article 1, Mandatory .