Serikali Ya Mapinduzi Ya Zanzibar Hotuba Ya Waziri Wa Fedha Na Mipango .

1y ago
53 Views
3 Downloads
1.20 MB
61 Pages
Last View : 2d ago
Last Download : 3m ago
Upload by : Sasha Niles
Transcription

1SERIKALI YA MAPINDUZI YAZANZIBARHOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NAMIPANGOMHE. DKT. KHALID SALUMMOHAMEDKUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETIYA SERIKALI (MAKADIRIO YAMAPATO NA MATUMIZI) KWAMWAKA WA FEDHA 2017/2018KATIKA BARAZA LA WAWAKILISHIJUNE 2017

iYALIYOMOA.UTANGULIZI . 1B.HALI YA UCHUMI NA MAENDELEO . 7C.MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA MWAKA 2016/17 . 8Mapato . 8Mapato ya Ndani. 8Mapato ya Nje. 9MATUMIZI . 9D.UTEKELEZAJI WA BAJETI KWA KIPINDI CHA MIEZI TISA (JULAI 2016 - MACHI 2017): . 10MAPATO . 10E.MFUKO WA MIUNDOMBINU (INFRASTRUCTURE FUND) . 16F.DENI LA TAIFA: . 18G.UTEKELEZAJI WA HATUA ZA KUIMARISHA MAPATO KWA MWAKA WA FEDHA 2016/2017. . 19H.MATARAJIO HADI JUNI 2017 . 21MAPATO . 21MATUMIZI . 22I.MAREKEBISHO YA MISHAHARA, 2016/2017. 23J.MWELEKEO WA BAJETI YA 2017/18 . 28K.VIPAUMBELE VYA KITAIFA: . 30L.MWELEKEO WA MAPATO: . 32Mapato ya Ndani. 32Mapato ya Nje. 33M.MWELEKEO WA MATUMIZI . 34N.UGATUZI WA MADARAKA . 37O.MAZINGATIO MAALUM YA SERIKALI . 38P.MAPENDEKEZO YA HATUA ZA KUIMARISHA MAPATO . 44Q.SURA YA BAJETI . 49R.SHUKRANI . 55S.HITIMISHO:. 58

1MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI(MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWAMWAKA WA FEDHA 2017/2018 KATIKA BARAZA LAWAWAKILISHIA. UTANGULIZI1.Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha mbele yaBaraza lako hili tukufu mapendekezo ya Makadirio yaMapato na Matumizi ya Serikali ya Mapinduzi yaZanzibar kwa mwaka wa fedha wa 2017/18. Kwakutekeleza azma hiyo, naomba kutoa hoja kwambaBaraza lako sasa likae kama Kamati Maalum ya kupokeana kujadili mapendekezo hayo.2.Mheshimiwa Spika, imani inatutaka waumini kuanzakwa jina la Mwenyezi Mungu, Muumba wetu. Naombanami nianze kwa kumtukuza na kumshukuru sana Molawetu, Subhana, kwa neema zake anazoendelea kutujaaliaambazo miongoni mwake ndio zimetuwezesha sisikuwepo hapa alasiri hii kutimiza wajibu wetu kwa jamiiiliyotupa ridhaa ya kuiongoza na kusimamia maendeleoyake. Kwangu mimi pia, bila ya neema hizo za uhai, afyana utulivu wa kila namna alionijaalia Muumba wetu,nami nisingeweza kutekeleza wajibu huu. Namshukuruna kumdhukuru sana mola wetu.

23.Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 105 cha Katiba yetuya mwaka 1984, kama ilivyorekebishwa, kinamtakaWaziri mwenye dhamana ya fedha kutayarisha nakuwasilisha mbele ya Baraza lako hili makadirio yamatumizi ya Serikali kwa mwaka unaofuatia. Kwa kuwamwaka wa fedha mpya wa 2017/18 unakaribia kuanza,nakushukuru Mheshimiwa Spika kwa kunipa nafasi hiiya kutimiza wajibu wangu wa Kikatiba kwa dhamanayangu ya Uwaziri wa Fedha na Mipango.4.Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 26 cha Katiba yetukinaweka dhima ya uongozi wa nchi yetu. Kifungundicho kinaweka uwepo wa Rais wetu, kinampadhamana ya kuwa ndie Mkuu wa nchi yetu ya Zanzibar,kuwa Kiongozi Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi na piakuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Kiongozihuyu anapatikana kwa njia ya uchaguzi unaofanywa nawananchi wenye sifa za kuchagua. Kutokana naUchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 20 Machi mwaka jana(2016), kwa sasa Rais wetu, Mkuu wa nchi ya Zanzibar,Kiongozi Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar naMwenyekiti wa Baraza letu la Mapinduzi ni Dkt. AliMohamed Shein. Ndie aliyechaguliwa na Wananchiwalio wengi kuwaongoza kwa miaka mitano hii.

35.Mheshimiwa Spika, Sisi sote ni mashahidi wa uongozithabiti, wenye subra, hekima na uadilifu mkubwa waMhe. Dkt. Shein. Tumeshuhudia mwaka mwengine wamafanikio ya pekee chini ya uongozi wake. Naomba tuuniruhusu, kwa sasa, nitumie fursa hii kumpongeza sanaMhe. Dkt. Shein kwa uongozi mahiri na kumaliza vyemamwaka mmoja wa kipindi cha pili cha uongozi wake.Kwangu mimi sina budi pia kumshukuru sana kwa imaniyake inayoendelea kwangu inayodhihirika katika uamuziwake wa kuendelea kunipa dhamana kubwa yakuiongoza Wizara hii roho ya Serikali, Wizara ya Fedhana Mipango. Kwa dhati ya nafsi yangu namuombeaMheshimiwa Rais kuendelea kuwa mfano wa uongozi wauadilifu, uongozi uliojaa hekima na uongozi wakuwapenda bila ya ukomo watu wote anaowaongoza.6.Mheshimiwa Spika, mafanikio tunayoyaona kwa Mhe.Rais yanachangiwa pia na ushauri na usaidizi mzurikutoka kwa msaidizi wake wa karibu, MheshimiwaBalozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Pili wa Rais nakiongozi wa shughuli za Serikali hapa Barazani. Mhe.Balozi Seif nae amejipambanua kwa uongozi imara,usioyumba na usaidizi wa dhati kwa Rasi wetu. Nasitunampongeza sana na kumshukuru kwa miongozo yake

4anayotupatia katika kuhakikisha uwepo wa utendaji uliobora.7.Mheshimiwa Spika, niruhusu pia nitumie fursa hiikuwakaribisha na kuwapongeza sana mwenzetu,Mheshimiwa Dkt. Sira Ubwa Mamboya na MheshimiwaAhmada Yahya Abdulwakil ambao wameteuliwa naMheshimiwa Rais, kuwa Wajumbe wa Baraza hilimuhimu. Pili kwa Mheshimiwa Dr Sira kuwa Mjumbewa Baraza la Mapinduzi na hivyo Waziri asiye na WizaraMaalum. Namkaribisha tena Dr Sira nikijua kuwa siomgeni katika Baraza hili na nikitambua mchango wakemkubwa katika Baraza lililopita. Tunawaombea kwaAllah Mtukufu utumishi shupavu na imara kwa wananchiwote.8.Mheshimiwa Spika, Baraza letu hili limeonesha utendajiimara wa kuisimamia Serikali. Mwaka mmoja wa uhaiwa Baraza hili la tisa umeweka viwango vipya vyautendaji wa chombo hiki muhimu kwa uhai namaendeleo ya Zanzibar. Nachukua fursa hii kukupongezawewe binafsi, Mheshimiwa Zubeir Ali Maulid, Spika waBaraza la Wawakilishi, Naibu wako Mheshimiwa MgeniHassan Juma, Wenyeviti wa Baraza, Mheshimiwa SheheHamad Mattar na Mheshimiwa Mwanaasha Khamis

5Juma na Wajumbe wote wa Baraza hili. Utendaji wamwaka huu mmoja umedhihirisha kuwa tukishirikianavyema, kwa umoja wetu tuna nafasi kubwa yakuwatumikia vyema Wananchi wote wa Zanzibar.9.Mheshimiwa Spika, umoja wetu huo unadhihirika tenakatika kikao hiki cha Bajeti kwa Waheshimiwa Wajumbekuisimamia vyema Serikali, kuihoji na kuwakilishamaslahi ya Wananchi wa Majimbo wanaowawakilishabila ya kusahau maslahi makubwa zaidi ya Taifa.Hongereni sana Waheshimiwa Wajumbe wote.10. Mheshimiwa Spika, Katiba yetu, chini ya Kifungu cha9, imeweka bayana kuwa mamlaka ya kuendesha nchi niya wananchi wenyewe. Kwamba nguvu na uwezo waSerikali kufuatana na Katiba unatoka kwa wananchiwenyewe. Ni dhahiri kuwa, pamoja na kutoa ridhaa yaokwa Chama na viongozi wa kuwaongoza, wananchi ndiowenye mamlaka ya kuongoza nchi na hivyo wana nafasimuhimu sana katika utawala na maendeleo yao.11. Mheshimiwa Spika, Kwa mukhtadha huu, pongezizangu haziwezi kukamilika bila ya kutambua, kushukuruna kupongeza mchango adhimu wa Wananchi wote wakila kona ya Zanzibar, ukiwemo wa kuendelea kuiparidhaa Serikali ya kuwaongoza na kusimamia maendeleo

6yao. Katika ridhaa hiyo, wananchi pia wameendelezautulivu ambao unaipa Serikali murua wa kutekelezawajibu wake na wamedumisha Amani inayowezesha naokila mmoja kufanya shughuli zake za kijamii na zakujiimarisha kiuchumi. Nawashukuru sana wananchiwote kwa imani yao, utulivu na mchango wao mkubwakatika kuiendeleza mbele nchi yetu.12. Mheshimiwa Spika, tumo katika Baraza hili tukiwaWajumbe ama wa kuchaguliwa na Wananchi katikaMajimbo yetu ya uchaguzi, kupitia viti maalum au kwauteuzi wa Mheshimiwa Rais na Mwenyekiti wa Baraza laMapinduzi. Kwa upande wangu, mimi ni muwakilishiniliechaguliwa na Wananchi wa Jimbo la Donge. Kwafursa hii, kwa mara nyengine tena, naomba kuwashukurusana viongozi na Wananchi wote wa Jimbo la Dongekwa mashirikiano makubwa wanayoendelea kunipa.Wananchi wa Donge waendelea kunivumilia na kunipaari na nguvu kubwa za kutekeleza majukumu yangukwao na kwa Taifa langu. nasema sitoacha kuwashukurusiku zote kwa imani yao isiyoyumba kwangu mimi.13. Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo yautangulizi, pongezi na shukurani, niruhusu sasa

7niwasilishe taarifa ya utekelezaji wa Bajeti ya Serikalikwa miezi tisa ya kwanza ya mwaka 2016/17.B.HALI YA UCHUMI NA MAENDELEO14. Mheshimiwa Spika, maelezo ya kina juu ya mwenendowa uchumi wa dunia, kanda na Zanzibar niliyatoa leoasubuhi wakati nikiwasilisha Mapitio ya Hali ya Uchumikwa mwaka 2016 na Utekelezaji wa Mpango waMaendeleo kwa mwaka 2016/17. Si azma yangukuyarudia tena maelezo yale bali niruhusu tu kutaja tenamambo muhimu yaliyojitokeza katika uchumi wetu.Kwanza, ni ukweli kwamba uchumi wetu umeendeleakukua. Kwa ukuaji halisi wa Pato la Taifa wa asilimia 6.8mwaka 2016 kutoka asilimia6.5 mwaka 2015inadhihirisha kuwa tumeendelea kupata mafanikiomakubwa zaidi ya kiuchumi mwaka 2016, kushindamwaka 2015. Kwa ujumla sasa Pato letu la Taifalimefikia TZS 2,628 bilioni kwa bei za mwaka 2016.15. Mheshimiwa Spika, inatia moyo zaidi kuona kuwamafanikio haya ya ukuaji wa uchumi yametokea wakatimwenendo wa uchumi wa dunia na wa Kanda ya Kusinimwa Jangwa la Sahara umeonesha kudorora. Aidha,mafanikio yamepelekea wastani wa pato la mtu kupandakutoka TZS 1,633,000 (Dola za Kimarekani 818) hadi

8TZS 1,806,000 (Dola 830). Kilimo cha mazao, hoteli namikahawa, na ujenzi ndio sekta ndogo zilizoongoza kwamchango mkubwa katika Pato la Taifa.C. MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA BAJETI YAMWAKA 2016/17Mapato16. Mheshimiwa Spika, Sura ya Bajeti ya Serikali kwamwaka wa fedha 2016/17 ilihusisha jumla ya TZS 841.5bilioni iliyotokana na mapato ya ndani ya TZS 482.4bilioni na mapato kutoka nje ya TZS 324.8 bilioni. Kiasikilichobakia cha TZS 34.3 bilioni kilitarajiwa kitokanena mikopo ya ndani ya TZS 33.0 bilioni na fedha zamsamaha wa madeni (MDRI) TZS 1.3 bilioni.Mapato ya Ndani17. Mheshimiwa Spika, itakumbukwa kuwa Baraza lakoliliidhinisha makadirio ya mapato ya ndani ya TZS 482.4bilioni kwa mgawanyo wa ukusanyaji ufuatao:a) Bodi ya Mapato (ZRB) TZS 237.4 bilioni;b) Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) TZS 188.8bilioni;c) Mapato ya Mawizara TZS 26.4 bilioni;

9d) Kodi ya Mapato kwa wafanyakazi wa SMT TZS 21.0bilioni;e) Gawio la faida kutoka Benki Kuu (BoT) TZS 4.0 bilioni;naf) Gawio la faida kutoka Mashirika ya SMZ TZS 4.8 bilioni.Mapato ya Nje18. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa mapato ya nje,Serikali ilikadiria kupata jumla ya TZS 324.8 bilioni,ikiwemo ruzuku ya TZS 93.3 bilioni na mikopo ya TZS231.5 bilioni.MATUMIZI19. Mheshimiwa Spika, kutokana na mapato hayo ya TZS841.5 bilioni, Baraza lako liliidhinishia Serikali kutumiajumla ya TZS 445.9 bilioni kwa kazi za kawaida na TZS395.6 bilioni kwa kazi za maendeleo. Matumizi hayoyamegawanyika kwa utaratibu ufuatao:a) Mishahara ya wafanyakazi TZS 223.7 bilionib) Matumizi mengineyo TZS 80.6 bilionic) Matumizi ya kazi za maendeleo TZS 395.6 bilioni ambapomchango wa SMZ ni TZS 71.1 bilioni na Washirika wamaendeleo ni TZS 324.8 bilioni.d) Matumizi ya Mfuko Mkuu ni TZS 82.3 bilioni.

10D. UTEKELEZAJI WA BAJETI KWA KIPINDI CHAMIEZI TISA (JULAI 2016 - MACHI 2017):MAPATO20. Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha miezi tisa chautekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2016/17, jumla ya TZS448.2 bilioni zimekusanywa, sawa na asilimia 110 yamatarajio ya kukusanya TZS 406.9 bilioni. Makusanyohaya yanajumuisha makusanyo ya ndani ya TZS 389.6bilioni na mapato kutoka nje ya TZS 58.6 bilioni. Kwaujumla, mapato yamekuwa kwa asilimia 12.3ikilinganishwa na TZS 399.0 bilioni zilizokusanywa hadiMachi 2016.21. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mapitio,mafanikio mazuri zaidi yamejitokeza katika ukusanyajiwa mapato ya ndani kwa kufikia TZS 389.6 bilioni, sawana asilimia 108 ya lengo la kipindi hicho. Ikilinganishwana kipindi kama hicho mwaka 2015/16 ambapo mapatoya ndani yalifikia TZS 306.1 bilioni, mapatoyameongezeka kwa asilimia 27.3.22. Mheshimiwa Spika, Mapato ya kodi ndio yamefanyavizuri zaidi ambapo jumla ya TZS 366.0 bilionizimekusanywa sawa na asilimia 108.6 ya makisio yajumla ya TZS 337.0 bilioni.Ukusanyaji huo

11unamaanisha ukuaji wa makusanyo ya kodi kwa asilimia27 kutoka TZS 288.5 bilioni zilizokusanywa hadi Machi2016. Aidha, mapato yasiyo ya kodi nayo yamekuwakwa asilimia 34 kutoka TZS 17.6 bilioni za mwaka janahadi TZS 23.6 bilioni, sawa na asilimia 94 ya makisio yajumla ya TZS 25.2 bilioni kwa miezi tisa ya mwaka huu.23. Mheshimiwa Spika, taswira ya jumla ya utendajiinaashiria kuimarika kwa mapato kutokana na ukusanyajimzuri wa mapato ya ndani uliochangiwa na mamboyafuatayo:i.Kuimarika kwa usimamizi kwa ZRB na TRA;ii.Kuimarika kwa uchumi kutokana na ukuaji wa asilimia6.8;iii. Kuongezeka kwa idadi ya watalii waliotembeleaZanzibar ambapo mwaka 2016 tulipokea watalii 82,000zaidi na kufikisha watalii 376,242 kutoka watalii 294,243wa mwaka 2015, sawa na ongezeko la asilimia 28.iv. Kuimarika kwa shughuli za biashara kutokana na,miongoni mwa mambo mengine, amani na utulivu ulioponchini.Utendaji wa Mapato yasiyo ya kodi umeathiriwa nakuchelewa kulipwa kwa gawio la SMZ kutokana na faida

12ya Benki Kuu ambalo hatimae limelipwa katika robo yanne badala ya robo ya tatu ya mwaka.24. Mheshimiwa Spika, kutokana na mwenendo huo mzuriwa ukusanyaji wa mapato yetu, Serikali haikuhitajikutumia sana fursa ya kukopa ndani iliyoidhinishwa naBaraza lako. Utakumbuka kuwa mwaka jana, serikaliiliomba na Baraza lako liliidhinisha kukopa ndani jumlaya TZS 33.0 bilioni ili kuziba nakisi ya Bajeti ya kiasihicho. Hadi Machi 2017, fedha zilizokopwa ndani ni TZS8.1 bilioni tu, sawa na asilimia 24.5 ya Bajeti ya mwaka.25. Mheshimiwa Spika, wazee wetu waliotanguliawametutaka kuwatunza wachezao kwao. Mwenendo wautendaji wa taasisi zetu za ukusanyaji wa mapato kwamwaka huu unaoendelea umeonesha utendaji mzuri naulioimarika sana. Naomba nitumie fursa hii kuwatunzakwa kuwapongeza sana viongozi na watendaji wote waMamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) hapa Zanzibarpamoja na Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB). Utendajiwao pamoja na jitihada za Serikali za kudhibiti matumiziya fedha za umma zimesaidia sana katika kuimarishahuduma za Serikali. Naamini kuwa jitihada hizizitaendelezwa katika mwaka ujao kwa kuziba mianyailiyobakia na kuimarisha zaidi mapato yetu.

1326. Mheshimiwa Spika, Kwa upande wa mapato ya nje,kukwama utekelezaji wa baadhi ya miradi mikubwa,ikiwemo ujenzi wa jengo jipya la abiria, kumepelekeataswira ya utekelezaji tofauti na iliyoonekana katikamapato ya ndani. Kwa sababu hii, uingiaji wa mikopo naruzuku kutoka nje ni chini ya matarajio. Hadi kufikiaMachi 2017, ni TZS 58.6 bilioni tu zimekusanywakutokana na mikopo na ruzuku kutoka nje, sawa naasilimia 18 ya matarajio ya mwaka. Kiasi hichokinatokana na TZS 30.8 bilioni za ruzuku na TZS 27.8bilioni za mikopo. Ikilinganishwa na kipindi kama hichomwaka jana ambapo jumla ya TZS 82.8 bilionizilipatikana, kunajitokeza pia kushuka kwa mapato ya njekwa asilimia 29.3.27. Mheshimiwa Spika, kuhusu uendelezaji wa ujenzi waJengo jipya la Uwanja wa Ndege, bado Serikali inaupamradi huu umuhimu wa kipekee kutokana na mchangounaotarajiwa kiuchumi na kijamii. Kwa mnasaba huu,jitihada maalum zimechukuliwa kuhakikisha kuwa mradiunakwamuka na ujenzi wa jengo hilo unaendelea.Mazungumzo zaidi yamefanyika baina ya Serikali yaMapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Watuwa China pamoja na Benki ya Exim ambayo inagharamiaujenzi huo kwa mkopo.

1428. Mheshimiwa Spika, Naomba nitumie fursa hiikuishukuru sana Serikali ya Jamhuri ya Watu wa Chinakwa kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali yetukatika kupiga hatua zaidi za maendeleo. Baada yamazungumzo ya pande mbili hizi inatarajiwa kuwa sasaujenzi utaendelea tena mapema mwaka ujao wa fedha nahatimae kukamilika mwishoni mwakani.MATUMIZI29. Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha mapitio,matumizi halisi yalifikia jumla ya TZS 424.8 bilioni,yakijumuisha matumizi ya vyanzo vya ndani ya jumla yaTZS 378.3 bilioni na TZS 46.5 bilioni kutoka kwaWashirika wa Maendeleo. Ikilinganishwa na kipindi kamahicho kwa mwaka 2016/17, kunajitokeza ongezeko lamatumizi la asilimia 20.4 kutoka TZS 352.9 bilionizilizotumika kwa miezi tisa hadi Machi 2016.Kati yamatumizi hayo, TZS 338.8 bilioni zimetumika kwaMatumizi ya Kawaida sawa na asilimia 100 ya lengolililowekwa.30. Mheshimiwa Spika, Mgawanyo wa matumizi hayo nikama ifuatavyo:

15i.Mishahara TZS 149.5 bilioni sawa na asilimia 99 yalengo;ii.Matumizi ya Mfuko Mkuu wa Serikali ya TZS 80.6bilioni sawa na asilimia 112 ya lengo;iii. Ruzuku kwa Taasisi TZS 42.2 bilioni sawa na asilimia97; naiv. Matumizi mengineyo ya kuendeshea ofisi (other charges)TZS 66.5 bilioni sawa na asilimia 102 ya lengo.31. Mheshimiwa Spika, tokea mwezi wa Aprili mwaka janaSerikali ilianzisha Pencheni ya Wazee ambapo wazeewote waliofikisha umri wa miaka 70 hulipwa Shilingielfu ishirini kila mwezi. Katika kipindi cha mapitio,Serikali imetekeleza vyema utaratibu huo ambapo malipoyamekuwa yakifanyika tarehe 15 ya kila mwezi nchinikote, Unguja na Pemba. Malipo haya yamesaidia sanawazee wetu sio tu kwa mahitaji yao madogo madogo balipia kuongeza imani kwa Serikali yao inayowajali.32. Mheshimiwa Spika, katika kipindi hicho Serikali piaimetumia jumla ya TZS 39.5 bilioni ikiwa ni mchangowake katika utekelezaji wa kazi za maendeleo, sawa naasilimia 93 ya lengo la TZS 42.7 bilioni. Kazi hizozinajumuisha matengenezo makubwa katika sekta ya

16habari kwa lengo la kuwa na studio za kisasa zautangazaji ili kuimarisha huduma zinazotolewa naShirika la habari Zanzibar. Matengenezo hayo ni pamojana Uimarishaji wa Shirika la Utangazaji Redio naTelevisheni ikiwemo kampuni ya usambazaji maudhui(ZMUX), kuimarisha vifaa vya kurushia matangazo kwakutumia “Microwave link” na mkonga wa Taifa kwavituo vyote vya Unguja na Pemba, kulifanyiamatengenezo makubwa jengo la ZBC Televisheni kwakuweka mfumo mpya wa umeme na hewa baridi,kununua vifaa vya kisasa vya kurikodia na kurushiamatangazo pamoja na kutengeneza studio zote za rediona televisheni.E.MFUKO WA MIUNDOMBINU(INFRASTRUCTURE FUND)33. Mheshimiwa Spika, Serikali ilianzisha Mfuko u ya Msingi kwa kutumia vyanzombalimbali vya mapato. Lengo ni kuharakishamaendeleo ya miundombinu muhimu kwa kutumiarasilimali zetu wenyewe. Kwa mwaka unaoendelea wafedha, jumla ya TZS 26.6 bilioni zimetarajiwakupatikana na kuingizwa katika Mfuko huo. Hadi Machi

172017, jumla TZS 21.0 bilioni zimekusanywa sawa naasilimia 105 ya lengo la miezi tisa hiyo. Makusanyo hayoyanajumuisha TZS 13.3 bilioni kutoka ZRB na TZS 7.7bilioni kutoka TRA.34. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa matumizi, fedhakutoka Mfuko wa Miundombinu zilitarajiwa kugharamiautekelezaji wa Miradi kumi na moja (11) kamanilivyoiainisha katika Hotuba yangu ya Bajeti ya mwakajana. Hadi mwishoni mwa Machi 2017, jumla ya TZS17.1 bilioni zimetumika kutoka Mfuko wa Miundombinukwa kugharamia Miradi ya uwekaji wa Kamera na Vifaavya Ulinzi, kulipa fidia barabara ya Ole – Kengeja, naujenzi wa Maabara ya Mkemia Mkuu.35. Mheshimiwa Spika, Serikali pia ilitoa ahadi yakuwapelekea nishati ya umeme wananchi wenzetuwanaoishi katika visiwa vyote vidogo vidogo, awamukwa awamu. Kwa mwaka unaoendelea wa fedha(2016/17), Baraza lako liliidhinisha matumizi ya TZS 2.0bilioni kwa ajili ya kupeleka umeme katika Kisiwa chaFundo ili kuanza utekelezaji wa azma hiyo. Nina furahakulijuulisha Baraza hili kuwa hadi Machi 2017 tayariSerikali imeipatia ZECO jumla ya TZS 1.8 bilioni kutokaMfuko wa Miundombinu kwa madhumuni hayo.

1836. Mheshimiwa Spika, Kama nilivyoeleza katika Mapitioya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo, tayari ZECOimeshatekeleza matayarisho yote kwa kufanikishaupelekaji wa umeme katika kisiwa hicho. Hatuailiyobakia ni uwekaji wa waya wa chini ya bahari ambaoutakamilika kutengenezwa mwishoni mwa mwezi huuwa tano. Mradi unatarajiwa kukamilika katika robo yakwanza ya mwaka wa fedha 2017/18. Kukamilika kwamradi huo ni hatua muhimu sana ya kuharakishamaendeleo ya wananchi wenzetu, wakaazi wa kisiwa chaFundo.F.DENI LA TAIFA:37. Mheshimiwa Spika, Hadi kufikia mwezi Machi, 2017,Deni la Taifa limefikia TZS 377.1 bilioni, kutoka deni laTZS 398.6 bilioni lililokuwepo mwezi Machi 2016. Denihili limejumuisha deni la nje TZS 270.2 bilioni ambalolimeongezeka kwa asilimia 1.3 kutoka TZS 266.8 bilioni.Aidha, deni la ndani ni TZS 106.8 bilioni ambalolimepungua kutoka TZS 130.2 bilioni, ambapo upungufuhuo ni sawa na asilimia 21.9. Mafanikio yanatokana namkazo uliowekwa na Serikali katika ulipaji wa madeniikiwemo deni la kiinua mgongo cha wastaafu Serikalini.Katika kipindi hicho, jumla ya TZS 19.1 bilioni

19zimetumika kulipa kiinua mgongo cha Wastaafu 1,455.Serikali pia imelipa deni la Hati Fungani iliyoiva pamojana kulipa riba kwa mikopo mingine ya ndani.38. Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia Pato letu la Taifakama nilivyoeleza awali, deni hilo ghafi ni sawa naasilimia 14.3 ya Pato la Taifa. Kutokana na ukuaji wauchumi na mwenendo mzuri wa mapato ya ndani nahadhari kubwa inayochukuliwa ya kudhibiti kuongezekasana deni la Taifa, uwiano huo wa deni na Pato la Taifaunaonesha kuwa: (i) Serikali inahimili deni hilo; (ii) nchiinakopesheka; na (iii) tuna uwezo wa kulipa.G. UTEKELEZAJI WA HATUA ZA KUIMARISHAMAPATO KWA MWAKA WA FEDHA 2016/2017.39. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2016/17,Serikali ilichukua hatua mbalimbali za kuimarishamapato ya ndani. Matokeo ya utekelezaji wa baadhi yahatua hizo ni kama ifuatavyo:i.Ada ya Ukaguzi wa Bidhaa katika kituo (DestinationInspection Fee) na Uthibitishaji wa Bidhaa (CustomsDeclaration-TANSAD)40. Mheshimiwa Spika, hatua hii imehusisha utozwaji waAda ya Ukaguzi wa bidhaa (Destination Inspection Fee)

20kwa asilimia 0.6 ya thamani ya bidhaa iliyoingizwa naAda ya Uthibitishaji wa Bidhaa (Customs DeclarationTANSAD) ambayo ni 10 USD kwa kila kadhia yaForodha kwa ajili ya kuimarisha TRA na ZRB. Jumla yaTZS 1.4 bilioni zimekusanywa hadi kufikia Machi 2017sawa na asilimia 21 ya lengo la mwaka la kukusanyaTZS 6.68 bilioni.ii.Vibali vya Kodi kwa Wazabuni (Tax ClearanceCertificate)41. Mheshimiwa Spika, Jumla ya TZS 32.4 bilionizimekusanywa kutokana na utekelezaji wa hatua hiiambapo TZS 31.8 bilioni zimetokana na Kodi yaOngezeko la Thamani (VAT) na TZS 0.6 bilioni nikutokana na Kodi ya Zuio (Withholding Tax).iii. Uhaulishaji wa magari kutoka Zanzibar kwendaTanzania Bara42. Mheshimiwa Spika, hatua imehusisha kukusanya tofautiya kodi wakati magari hayo yanapotaka kuhaulishwakwenda Tanzania Bara. Hatua hii imeiningizia Serikalijumla ya TZS 6.8 bilioni hadi Machi 2017.iv. Usajili wa Vyombo vya Moto

2143. Mheshimiwa Spika, Serikali ilidhinishiwa kusajili kwanamba za Zanzibar vyombo vyenye usajili wa TanzaniaBara vilivyopo Zanzibar ili kuleta usawa katikautekelezaji wa sheria na usajili. Hatua hii ilichelewakutekelezwa hivyo hadi Machi 2017 ni TZS 90 milioni tuzimeweza kukusanywa.H. MATARAJIO HADI JUNI 2017MAPATOMatarajio ya Mapato Julai – Juni 2016/2017.44. Mheshimiwa Spika, inatarajiwa kwamba hadi kufikiaJuni 2017, mapato kwa ujumla, yatafikia TZS 668.3bilioni sawa na asilimia 86 ya Bajeti ya mwaka ya TZS841.5 bilioni. Kati ya fedha hizo, kutokana na kuimarikakwa utendaji wa TRA na ZRB na mwenendo mzuri wauchumi wetu, mapato ya ndani yanatarajiwa kuvukalengo na kufikia TZS 530.2 bilioni, sawa na asilimia 110ya makisio ya mwaka ya TZS 482.4 bilioni.45. Mheshimiwa Spika, matarajio ya ukusanyaji wa mapatohayo Kitaasisi ni kama ifuatavyo:i.TRA inatarajiwa kukusanya TZS 211.3 bilioni nahivyo kuvuka lengo kwa TZS 22.5 bilioni, sawa nautendaji wa asilimia 112 ya lengo;

22ii.ZRB inatarajiwa kuvuka lengo kwa utendaji waasilimia 113 sawa na nyongeza ya TZS 35.3 bilionikwa mapato kufikia TZS 307.9 bilioni. Kati yamapato hayo, mapato ya kodi ni TZS 265.3 bilioni,sawa na asilimia 117 ya lengo la kukusanya TZS237.4 bilioni na mapato yasiyokuwa ya kodi ni TZS42.6 bilioni sawa na asilimia 131 ya lengo la TZS32.5 bilioni;iii. PAYE kutoka SMT inatarajiwa kufikia TZS 21.0bilioni sawa na asilimia 100 ya lengo; naiv. Mikopo ya ndani inatarajiwa kufikia TZS 8.1 bilionisawa na asilimia 24.5 ya Bajeti ya kukopa TZS 33.0bilioni.46. Mheshimiwa Spika, kutokana na sababu nilizoelezaawali, mikopo na ruzuku kutoka nje inatarajiwa kufikiajumla ya TZS 150.0 bilioni sawa na asilimia 46.2 yamakadirio ya mwaka.MATUMIZI47. Mheshimiwa Spika, inatarajiwa kwamba hadi kufikiaJuni 2017, kwa ujumla, matumizi yatafikia TZS 687.2bilioni sawa na asilimia 81.7 ya Bajeti ya mwaka ya TZS

23841.5 bilioni. Matumizi hayo yamejumuisha ongezeko lamshahara kwa kipindi cha April hadi Juni 2017.48. Mheshimiwa Spika, Mchanganuo wa matumizi hayo nikama ifuatavyo:Matumizi ya kawaida yatafikia TZS 470.2 bilioni kamaifuatavyo:i.ii.iii.iv.v.Mishahara (Wizara) TZS 223.8 bilioniMishahara (Ruzuku) TZS 26.7 bilioniMatumizi Mengineyo (Wizara) TZS 90.0 bilioniMatumizi mengineyo (Ruzuku) TZS 31.1 bilioniMfuko Mkuu wa Serikali (CFS) TZS 98.6 bilioniMatumizi ya maendeleo yatafikia TZS 217.0 bilioni kwamgawanyo ufuatao:I.i.Mchango wa Serikali TZS 67.0 bilioniii.Mikopo na Ruzuku TZS 150.0 bilioniMAREKEBISHO YA MISHAHARA, 2016/201749. Mheshimiwa Spika, katika Kampeni za Uchaguzi Mkuuwa mwaka 2015, Mheshimiwa Rais wa Zanzibar naMwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliahidi kupandisha

24kima cha chini cha mshahara ndani ya mwaka mmoja wauongozi wake katika awamu hii ya pili. Nyongeza hiyo nikutoka TZS 150,000/ hadi kufikia TZS 300,000/ kwawafanyakazi wa kawaida Serikalini na kutoka TZS203,000 za sasa hadi TZS 406,000/- kwa mwezi kwaWafanyakazi wa Idara maalum za SMZ ili walingane nawenzao wa vikosi vya SMT. Kwa makundi yote mawili,ongezeko hili ni sawa na nyongeza ya asilimia 100 yakima cha chini cha mishahara.50. Mheshimiwa Spika, huu ni muendelezo wa jitihada zaMheshimiwa Rais za kuimarisha maslahi na hivyo kuletaufanisi kazini ambazo amekuwa akizichukua tokeakuingia madarakani. Katika Hotuba yangu ya Bajeti yaSerikali ya mwaka jana nilieleza kuwa ahadi hiyo yaMheshimiwa Rais itatetekelezwa kwa kufanyamarekebisho hayo ya mshahara kuanzia mwezi waAprili, 2017. Sambamba na nyongeza hiyo, niliahidi piakupunguza Kodi ya Mapato (PAYE) kwa kundi la kipatocha chini kutoka asilimia 13 hadi asilimia tisa, ilikuimarisha zaidi maslahi ya wafanyakazi wa kima chachini cha mshahara kwa kuzingatia gharama za maisha.51. Mheshimiwa Spika, tuna wasia wa wazee wetu. Wazeewalitusisitiza kuwa ahadi ni deni. Wakatuambia pia

25kuwa uungwana ni vitendo, tutende watu wataona.Nina furaha kulijuilisha Baraza lako hili kuwa Serikaliimetekeleza ahadi zake. Mosi, kama ilivyoahidi,imepandisha mshahara wa kima cha chini kwa makundiyote mawili kwa asilimia 100. Pili, nyongeza hiyoimeanza April 2017. Na tatu, kiwango cha kodi kwakundi la mwanzo linaloanza kutozwa kodikimepunguzwa kutoka asilimia 13 ya kabla hadi asilimia9.52. Mheshimiwa Spika, huo ndio uungwana, na hivyo ndiovitendo vya Serikali ya Dkt. Ali Mohamed Shein.Ameahidi na ametenda; Muungwana. Sasa ni jukumuletu watumishi wa umma kuuenzi uungwana huu kwakuongeza jitihada zenye ufanisi katika kuwahudumiavyema zaidi wananchi wote.53. Mheshimiwa Spika, kwa sasa marekebisho hayoyatawahusu, kwa viwango tofauti, wafanyakazi wote waSerikali na taasisi zake zipatazo ruzuku ya Mishaharakutoka Serikalini isipokuwa wale ambao mishahara yaokwa mwezi inafikia TZS 1,500,000.00 au zaidi. Hatahivyo, marekebisho hayo yanaambatana pia namarekebisho ya kiasi cha kipato ambacho kitasamehewaKodi ya mapato kwa wafanyakazi wote wa Serikali na

26taasisi binafsi. Ili kuleta uwiano baina ya sekta hizo mbilina kwa azma ya kupunguza athari kwenye mapato yaSerikali, kiasi cha kipato kutokana na ajira ambachokitasamehewa kodi ni hadi TZS 180,000/ kwa mwezisawa na TZS 2,160,000 kwa m

10. Mheshimiwa Spika, Katiba yetu, chini ya Kifungu cha 9, imeweka bayana kuwa mamlaka ya kuendesha nchi ni ya wananchi wenyewe. Kwamba nguvu na uwezo wa Serikali kufuatana na Katiba unatoka kwa wananchi wenyewe. Ni dhahiri kuwa, pamoja na kutoa ridhaa yao kwa Chama na viongozi wa kuwaongoza, wananchi ndio

Related Documents:

hizi, ulizingatia Mipango Mikuu ya Kitaifa ikiwemo Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015 - 2020, MKUZA, pamoja na Mpango Mkakati wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. 2.1 UPATIKANAJI WA FEDHA 15. Mheshimiwa Spika, mwaka wa fedhakwa 2017/2018, Ofisiya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ilitengewa jumla ya TZS .

THE CONSTITUTION OF THE STATE OF ZANZIBAR , ¿.vVST¡ncftèrà. 1. Zanzibar subjects by birth. 2. Subjects by descent. 3. Naturalisation of aliens. 4. Registration of minors. 5. Registration of wives of Zanzibar subjects. 6. Women who have ceased to be Zanzibar subjects on marriage. 7. Deprivation of status as Zanzibar subject.

Maana ya Serikali za Mitaa na Dhana ya kupeleka Madaraka kwa Wananchi 2 Mfumo na Muundo wa Serikali za Mitaa 3 Mamlaka za Wilaya 3 Mamlaka za Miji 5 Muundo wa Serikali za Mitaa mbalimbali 6 Kitongoji 6 Mtaa 6 Kijiji 7 Kamati ya Maendeleo ya Kata 7 Mamlaka ya Mji Mdogo 8 Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Jiji (kama vile Mwanza) 8

ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2020 utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015. Vilevile, maudhui ya Ilani hii yamezingatia Mwelekeo wa Sera za Chama Cha Mapinduzi wa 2020-2030, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na Dira ya Maendeleo ya Zanzibar 2020-2050. Aidha, Ilani hii imezingatia fursa na changamoto

KATIBA YA BARAZA LA DIASPORA LA WATANZANIA DUNIANI . umoja na mshikamano, ili kushirikiana na kukuza, hamasa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambayo ni Nchi yetu. Tutazidi kuimarisha mahusiano mazuri, ushirikiano katika kukuza tamaduni, shughuli za kijamii . Halitakua na mlengo wa chama cha .

tunakuandikia, kwa niaba ya Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kukushauri kutumia mamlaka yako chini ya ibara ya 97(2 . Kiongozi katika muundo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Katiba ya sasa ya Zanzibar imefuta nafasi hiyo na kuunda nafasi mbili

1.1 Importance of the Zanzibar Coastal Zone 1 1.2 Zanzibar s Coastal and Marine Resources 3 1.3 The Increasing Pressure on Coastal Areas and Resources 4 1.4 The need for ICAM and Government Policy Commitment 5 1.5 The Chwaka Bay-Paje Area: A Step Towards ICAM in Zanzibar 5 CHAPTER 2: THE CHWAKA BAY-PAJE AREA 9AJE AREA 2.1 Introduction 9

men’s day worship service. It is recommended that the service be adjusted for specific local needs. This worship service is designed to honor men, and be led by men. Music: Led by a male choir or male soloist, young men’s choir, intergenerational choir or senior men’s choir. Themes: Possible themes for Men’s Day worship service include: