MASWALI MAJIBU - Unistoretz

1y ago
11 Views
2 Downloads
643.21 KB
7 Pages
Last View : 17d ago
Last Download : 3m ago
Upload by : Giovanna Wyche
Transcription

Tunawawezesha WahitajiMASWALI&MAJIBUUTARATIBU, SIFA NAVIGEZO VYA UTOAJIMIKOPO KWA 2018/2019Tunawawezesha Wahitaji1

Tunawawezesha Wahitaji1. Swali: Ninapaswa kufanya nini ili niweze kuanza kuomba mkopo kwa njia yamtandao (OLAMS)?Jibu: Soma mwongozo uliotolewa na Bodi ambao unapatikana katika tovuti yaBodi (www.heslb.go.tz). Baada ya kuusoma Mwongozo, fungua mtandaowa maombi (www.olas.heslb.go.tz) ili ujisajili kwa kutumia namba yako yamtihani wa kidato cha nne na mwaka uliofanya mtihani huo.2. S wali: Baada ya kujisajili, napaswa kufanya nini? Jibu: Baada ya kujisajili, utapata namba ya kumbukumbu (Control Number)kutoka kwenye ‘screen’ ambayo itakuwezesha kufanya malipo ya ada yamaombi ya TZS 30,000/ kwa njia ya benki au simu. Lipa mara moja tu! Baada ya kulipa, utapokea ujumbe (sms) wa uthibitisho wa muamala wakoutakaokuwezesha kuendelea na hatua inayofuata ya maombi kwenye ‘MyApplication’. Jaza hatua kwa hatua.3. Swali: Je, nikiingiza namba yangu isiyokuwa ya NECTA, mfano ya nje ya nchi,nitawezaje kuendelea kuomba mkopo? Jibu: Wakati wa kujisajili, unatakiwa kuchagua kipengele cha ‘Non-NECTAstudents’ na kujaza kama inavyoelekezwa. Mfumo utakupatia namba yakidato cha nne tofauti na ile uliyojaza ambayo itatambuliwa na Bodi. Nambahii mpya itatokana na ile namba iliyojazwa awali (isiyokuwa ya NECTA).4. Swali: Inachukua muda gani fomu kufunguka baada ya kulipa? Jibu: Fomu inafunguka mara tu malipo yanapokamilika. Fomu inapochelewakidogo kufunguka, mwombaji anashauriwa kutoka (Sign out) na kujaribukuingia tena (Sign in) katika mtandao ili aweze kuendelea na hatuazinazofuata.5. Swali: Ikiwa nimelipa lakini sijapokea ujumbe wa kuendelea na maombi,nifanyeje? Jibu: Unatarajiwa kupokea ujumbe mara tu muamala unapokamilika. Ikiwahautapata ujumbe ndani ya saa moja (dakika 60) baada ya kufanya malipo,unashauriwa kuwasiliana nasi kwa namba ya simu 255 22 550 7910 aubarua pepe helpdesk@heslb.go.tz2

Tunawawezesha Wahitaji6. Swali: Nitanyaje ikiwa njia mojawapo ya kulipia mfano, CRDB, NMB, M-pesa, AirtelMoney, Tigo-Pesa itanigomea kulipa na kuendelea? Jibu: Kwa kuwa kuna njia zaidi ya moja ya kulipia, unashauriwa kuchaguana kutumia njia ya malipo ambayo ni rahisi kwako au inapatikana sehemuuliyopo wakati ukifanya malipo.7. Swali: Nifanyeje iwapo nimesahau neno langu la siri (Password)? Jibu: Utapaswa kubofya kiunganishi cha “Forgot Password?” na kishautaelekezwa kwenye ukurasa husika na ambako utatakiwa kujaza anuaniya barua pepe uliyotumia wakati wa kujisajili. Baada ya hapo, utapokeakiunganishi kwa ajili ya kupata neno jipya la siri kupitia kwenye barua pepeyako.8. Swali: Je, ni wapi nitahakiki cheti za kuzaliwa au kifo cha mzazi? Jibu: Vyeti vya kuzaliwa na vifo vya wazazi lazima vihakikiwe na Wakala waUsajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kabla havijapakiwa (uploaded). Kumbukakuwa RITA watawasilisha kwa Bodi orodha ya vyeti vyote vilivyohakikiwa ilikuepusha udanganyifu.9. Swali: Je kuna athari zozote ikiwa nimeambatanisha na kuwasilisha cheti ambachohakijahakikiwa na RITA? Jibu: Ndiyo. Maombi yako yatakuwa hayajakamilika na hivyo kutofikiriwakatika hatua ya upangaji mikopo. Unapaswa kuhakikisha nyaraka zote (siyovyeti vya vifo au kuzaliwa tu) zinathibitishwa na mamlaka, taasisi au maafisawaliotajwa katika mwongozo.10. Swali: Je, ikiwa kazi ya mzazi wangu haipo kwenye orodha iliyopo kwenyemtandao, napaswa kufanya nini? Jibu: Chagua kipengele cha nyinginezo (others) kisha uitaje kazi ya mzazi/mlezi wako kwa kuiandika.11. Swali: Kama sikuwahi kumfahamu mzazi wangu, nitajaza nini? Jibu: Unatakiwa kujaza taarifa za mlezi au mtu mwingine anayekulea aukusimamia masuala yako ya Elimu. Ni lazima taarifa za mlezi au msimamizizithibitishwe na Serikali ya Mtaa unakoishi. Kama mlezi anazo nyaraka rasmiza kukuasili (adoption document) nazo ziambatanishwe.3

Tunawawezesha Wahitaji12. Swali: Je, nikikosea kwenye ‘Applicant category’ natakiwa kufanya nini?J ibu: Ikiwa bado ‘huja-print’, unaweza kurekebisha kwa kurudi kwenye‘Applicant Category’ na kuchagua kipengele sahihi. Iwapo umekamilishamaombi na ku-print fomu yako, unatakiwa kuandika barua ya kuombakufanyiwa marekebisho, na kuituma HESLB kwa njia ya EMS. Barua hiyo iwenamba ya kidato cha nne yenye mwaka uliofanya mtihani huo.13. Swali: Je, kama nimehitimu kidato cha sita au diploma mwaka 2018 na sijapatacheti nitaambatanisha nini? Jibu: Unatakiwa kutaja namba ya mtihani wa kidato cha sita ambayoitatumika kuhakiki matokeo kutoka mamlaka husika. Kwa mhitimu wadiploma, unaweza kuambatanisha waraka wa matokeo (transcript).14. Swali: Kama mwaka jana au kabla nilikuwa na umri chini ya miaka 30, je mwakahuu naweza kuomba mkopo? Jibu: Kwa mwaaka wa masomo 2018/2019, umri wa juu wa mwombaji nimiaka 33. Umri umeongezwa kutoka miaka 30 hadi 33 ili kuongeza wigo wawanufaika wa mikopo.15. Swali: Iwapo niliwahi kupata mkopo zamani na nikaacha, kushindwa auufukuzwa chuoni, nitaweza kupata mkopo mwingine? Jibu: Iwapo uliwahi kuwa mnufaika wa mkopo wa fedha za Serikali,utapaswa kwanza kurejesha mkopo wote au angalau asilimia 25 ya denilako kabla ya kufikiriwa kupata mkopo mwingine. Deni hili unaweza kulipatakwa kuomba ankara ya deni kwa barua pepe repayment@heslb.go.tz aukupiga simu 0766 852 610 au 0659 748 536 kwa Idara ya Urejeshaji waMikopo.16. Swali: Kama nina wazazi wasio na uwezo, je niwasilishe uthibitisho wa ainagani ili kupata mkopo? Jibu: Muombaji ambaye ana mahitaji maalum, ni lazima mahitaji na haliyake ithibitishwe na mamlaka husika kama Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF) na taasisi za aina hii. Taarifa za aina hii zitapekuliwa kuthibitishwauhalisia na ukweli wake.17. Swali: Kama nilikosa mkopo mwaka jana, nikalazimka kuahirisha masomo,natakiwa kuomba tena mkopo mwaka huu?4

Tunawawezesha Wahitaji Jibu: Unaruhusiwa kuomba upya mkopo mwaka huu. Maombi yakoyatapimwa kwa mwongozo na vigezo vya mwaka 2018/19. Unashauriwausome mwongozo kwa makini na kuuzingatia. Aidha, kama unasoma mwakawa pili au wa tat una kuendelea na una uhitaji wa mkopo, unaruhusiwakuomba kwa kuzingatia vigezo vya mwaka huu.18. Swali: Nitafanyaje nisipoweza kumfikia mtoa huduma kwa njia yasimu inayoonyeshwa kwenye mtandao? Jibu: Kuna njia mbili za kuwafikia watoa huduma wa kitengo cha usaidizi(Helpdesk) Njia ya kwanza ni kwa simu 255 22 550 7910 na nyingine nikwa barua pepe helpdesk@heslb.go.tz. Unashauriwa kuwasilisha taarifa au changamoto husika kwa njia ya baruapepe ili wataalamu waifanyie kazi na kukupigia kama itahitajika. Kumbukakuandika mawasiliano yako ya simu itakayotumika kukupigia.19. Je, mwombaji atajuaje kama fomu yake ya maombi imejazwa kwa ukamilifu?Mwombaji ana wajibu wa kuhakikisha nyaraka zote muhimu zimepakiwa kwenyemfumo wa maombi katika nakala laini. Nyaraka hizo ni pamoja na:i.Picha ya mwombaji;ii. Vivuli vya nakala za vyeti vya kitaaluma zilizothibitishwa na Wakili auHakimu; iii. Vivuli vya nakala za vyeti vya kuzaliwa au kifo zilizothibitishwa naRITA;iv.Nakala za barua za ufadhili kutoka katika taasisi zinazotambulika;v. Nakala ya fomu ya maombi iliyosainiwa na kugongwa muhuri naSerikali ya Mtaa, Hakimu au Wakili kama inavyoelekezwa;vi. Aidha, nakala halisi ya fomu ya maombi inapaswa kusainiwa namwombaji na mdhamini wake vii. Maelezo ya kina yanapatikana katika mwongozo uliopo kwenye tovutiya Bodi ya Mikopo (www.heslb.go.tz)20. Swali: Fomu za maombi ya Mikopo zinawasilishwaje Bodi ya Mikopo yaWanafunzi wa Elimu ya Juu? Jibu: Baada ya kuzi-upload na kukamilisha fomu yake ya maombi, mwombajia-print fomu iliyokamilika na kuituma kwenda kwa:5

Tunawawezesha WahitajiMkurugenzi Mtendaji,Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,Barabara ya Sam Nujoma – MwengeS.L.P. 7606814113 DAR ES SALAAM21. Mwombaji atajuaje iwapo amepata mkopo?Jibu: Baada ya Bodi kupokea, kuhakiki na kuchambua maombi ya Mikopo, majinaya Wanafunzi watakaofanikiwa kupangiwa Mikopo yatatangazwa kupitia tovuti yaBodi ya Mikopo (www.heslb.go.tz) kabla ya kufunguliwa kwa vyuo vya elimu ya juuwalikodahiliwa Wanafunzi husika.Imetolewa na:Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juuinfo@heslb.go.tzMei 20186

Tunawawezesha Wahitaji46 Barabara ya Sam Nujoma - Mwenge, S.L.P 76068, 14113Dar es Salaam, Tanzania Simu: 255 22 2772432/2772433; Nukushi: 255 222700286; Barua pepe: info@heslb.go.tz; Tovuti: www.heslb.go.tz7

MASWALI & MAJIBU UTARATIBU, SIFA NA VIGEZO VYA UTOAJI MIKOPO KWA 2018/2019. Tunawawezesha Wahitaji 2 1. Swali: Ninapaswa kufanya nini ili niweze kuanza kuomba mkopo kwa njia ya mtandao (OLAMS)? Jibu: Soma mwongozo uliotolewa na Bodi ambao unapatikana katika tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz). Baada ya kuusoma Mwongozo, fungua mtandao

Related Documents:

MASWALI NA MAJIBU ميِحِرلا َّنِمَٰحْرلا َِّالل َّمِسِْب NENO LA MCHAPISHAJI M aswali na Majibu ni kitabu kinachotoa mwongo-zo kwa njia ya maswali na majibu. Kitabu hiki ni mkusanyiko wa maswali aliyoulizwa Sheikh Hasan al-Saffar katika programu yake ya maswali na majibu ili-yoandaliwa katika tovuti yake.

4. Biblia inajibu maswali tunayojiuliza Mwanamke fulani alitambua kwamba Biblia ina majibu ya maswali yaliyomhangaisha kwa miaka mingi.OnyeshaVIDEO,kisha mzu-ngumzie maswali haya: Katika video hiyo, mwanamke huyo alijiuliza maswali gani? Kujifunza Biblia kulimsaidiaje? Biblia inatutia moyo tuulize maswali.SomaMathayo 7:7, kisha mzungumzie .

MWALIMU ONYANGO #DIRA SERIES, USHAIRI# KCSE 2007-2019. MASWALI NA MAJIBU. 0707311302 Soma shairi hili kisha ujibu maswali yayofuata: Kila Mchimba Kisima; Musa Mzenga 1. Tenda utendapo tendo, tenda tendo kwa hekima, Lindamane mwenendo, sawa na yakio kalmia, Kalmia yenye upendo, kufurahisha mtima, Kila mchimba kisima, budi hungia mwenyewe. 2.

maswali yako mengi iwezekavyo kuhusu Australia Tuanze kwa kujua nini haswa WEWE unachotaka kujua Tumia nafasi ya mstari iliyopo hapo chini ili kuandika maswali yako Wakati unaposikia majibu ya moja wapo ya maswali yako wakati upo kwenye AUSCO, andika majibu hayo AUSCO hukupatia wewe maelezo mengi na inaweza kuwa vigumu kukumbuka maelezo yote!

1. Pata orodha ya maswali yako na uifungue kwenye ukurasa wa kwanza. 2. Tumia habari katika mwongoza huu wa Kiswahili kuweka alama kwa majibu yako kwenye karatasi ya orodha ya maswali la Kiingereza. USIANDIKE MAJIBU YAKO KWENYE MWONGOZO HUU. 3. Kabla ya kujibu swali la kwanza, hesabu watu wanaoishi katika nyumba

Kitabu Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafa-nyayoKazi,Bukula2,kimekusudiwakumpamtotowenu kanuninzurisana za Kimaandiko. Ukitazama Yaliyomokati-ka ukurasa wa 4na 5utaona habari mbalimbali zinazozungu-mziwa katika kitabu hiki. Hata hivyo, kitabu hiki kimekusudi-wa kutimiza mengi zaidi. Fikiria mamboyafuatayo: (1) Kitabu hiki kinamhusisha .

Maswali na majibu Ufafanuzi Uchambuzi Maelezo Mifano Maswali na majibu Majadiliano JUMA 5. 219 KIPINDI SHABAHA NJIA ZA KUFUNDISHIA NYENZO ZA KUFUNDISHIA MADA KUU MADA NDOGO MAONI HAKIUZWI Yatumiwe na Kiswahili Fasaha Kiswahili, Kidato cha 2 Maazimio ya Kazi Muhula wa Kwanza 1 2 3

Ballet music for piano This collection, the third of a trilogy (the others being A Night at the Opera and The Piano at the Carnival ) owes its inception to a welcome commission from pianophile and ex-ballet dancer Geoffrey Walters to make piano transcriptions of four pas de deux from Russian ballets. In classical ballet the pas de deux is typically a four-part set piece involving two .