KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global

1y ago
17 Views
3 Downloads
597.54 KB
106 Pages
Last View : 13d ago
Last Download : 3m ago
Upload by : Sasha Niles
Transcription

KUJENGA MISINGIYA IMANIBasi kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana, enendeni vivyo hivyokatika Yeye; wenye shina na wenye kujengwa katika Yeye(Wakolosai 2:6-7a)Kimetafsiriwa na Edson Kamenya kutoka katika toleo la KiingerezaLiitwalo Laying FoundationsCopyright 2002 by Cornerstone ChurchKitabu hiki chaweza kunakiliwa chote, au kwa sehemu katika mfumo wowote ule(wa maandishi, katika kanda za video au za sauti au njia nyingine sawa na hizo)Bila kupata kibali cha mchapishaji,Kwa sharti moja kwamba nakala zote hazitumiwi kibiashara.Kimechapishwa na Kanisa la Cornerstonela Afrika ya Kusini 27 11 616 4073info@cornerstonechurch.co.zaMaandiko yamenukuliwa kutoka katika BIBLIA TAKATIFU,SWAHILI UNION VERSION (SUV) Copyright 1960 (isipokuwa ilipoelezwa vinginevyo)Toleo hili ni haki miliki za Chama cha Biblia cha Kenya na Chama cha Biblia chaTanzaniaKatika kitabu hiki vifupisho kwa vitabu vya Biblia ni kama ifuatavyo:

MwaKutLawHesKumYosAmuRut1 Sam2 Sam1 Fal2 Fal1 Nya2 abuKumbukumbuYoshuaWaamuziRuthu1 Samueli2 Samueli1 Falme2 Falme1 Nyakati2 bo Ulio riaMalakiMatMkLkYnMdoRum1 Kor2 KorGalEfeFlpKol1 The2 The1 Tim2 TimTitFlmEbrYak1 Pet2 Pet1 Yoh2 Yoh3 rumi1 Wakorintho2 WakorinthoWagalatiaWaefesoWafilipiWakolosai1 Wathesalonike2 Wathesalonike1 Timotheo2 TimotheoTitoFilemoniWaebraniaYakobo1 Petro2 Petro1 Yohana2 Yohana3 YohanaYudaUfunuo

Kuweka Misingi ya ImaniKadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya YesuKristo, ndivyo kunavyokuwa na maeneo mengi maishani mwetu yanayohitajikurekebishwa na hata kubadilika. Waumini wa mwanzoni walilifanya hili kamatusomavyo katika Matendo 2:42 “Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume,na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.”Sisi sote tunataka kufikia hatua ya kukomaa kiimani, lakini ni hatua zipitunazohitajika kuzipitia kwanza? Kitabu cha Waebrania 6:1-2 kinaelezea hatuahizi za mafundisho ya msingi kama ifuatavyo: “Kwa sababu hiyo, tukiachakuyanena mafundisho ya kwanza ya Kristo, tukaze mwendo ili tuufikilie utimilifu;tusiweke msingi tena wa kuzitubia kazi zisizo na uhai, na wa kuwa na imani kwaMungu, na wa mafundisho ya mabatizo, na kuwekea mikono, na kufufuliwa wafu,na hukumu ya milele.”Masomo yote katika mafunzo haya ya msingi yameandaliwa ili kukusaidia uwezekulifikia lengo hili. “Mafunzo ya kwanza.” au ya “msingi” yote yanayopatikanakatika kifungu hiki cha Biblia yamepanuliwa. Mafunzo haya yameandaliwayawasaidie zaidi wale wanaopitia mafunzo ya Kuweka Msingi wa Imani katikaKanisa la Cornerstone maana yake kwa ni Kiswahili Kanisa la Jiwe la Pembeni.Mafunzo haya yanawawezesha kulenga zaidi katika kile wanachowezakukipokea katika mafunzo yenyewe kwa kuwa wataweza kuyakumbuka yoteambayo hawataweza kuyaandika katika wakati wa somo kupitia kitabu hiki.Vilevile, endapo mwalimu atakosa kulifundisha somo kama ipasavyo, basi kitabuhiki kitawapa mtazamo utakaofidia mapungufu.Mwisho wa kila sura kutakuwa na mfululizo wa vifungu rejea vya Maandikovitakavyoweza kuwa msaada kwako, hasa pale utakapotafuta kujifunza zaidi nahata kuwashirikisha wengine imani yako.Mwongozo huu pia umekusudiwa kuwa kitabu chenye msaada kwa Wakristo namakanisa kila mahali, na kinatolewa ili kiweze kunakiliwa na kugawanywa kwawatu wengi kadiri inavyowezekana kwa sharti moja tu kwamba yale yaliyomohayabadilishwi, na pia kitolewe pasipo kutozwa gharama yoyote. Hata hivyo,yapasa isisitizwe kwamba, mwongozo huu ni mfano ambao umeandaliwa kwaajili ya wakati huu. Mafunzo yenyewe (uchaguzi wa masomo yanayofundishwawakati wa kila somo, na walimu au wanenaji katika masomo haya), ni mamboyanayobadilika kwa haraka.Tunatarajia kwamba mafunzo haya na hata mwongozo huu vitakuwa barakakwako, na hivyo kuweza kuchangia angalau kidogo, katika jukumu zima lakuuendeleza na kuupanua Ufalme wa Mungu.Kauli Yetu Kuhusu Imani.Tunaamini katika kweli za msingi wa Ukristo kama ulivyofunuliwa katika

Maandiko pamoja na haya kama ifuatavyo: Umoja wa Utatu Mtakatifu - Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. (Kum 6:4,Mat 28:19, 2 Kor 13:14) Mamlaka na enzi ya Mwenyezi Mungu katika uumbaji, ufunuo, ukombozina hukumu ya mwisho. (Mwa 1:1, Ebr 1:1-2, Tit 3:4-5, Mdo 17:31) Uvuvio kamili wa Agano la Kale na Jipya kama kila moja lilivyotolewamwanzoni, na kwamba Maandiko haya ndiyo yenye mamlaka ya mwishokatika maswala yahusuyo imani na mwenendo. (2 Tim 3:16, 2 Pet 1:21, 1Kor 2:13) Hali ya anguko la mwanadamu kupitia dhambi ya Adamu, haliinayomuweka mwanadamu kuwa chini ya hasira na hukumu ya Mungu.(Rum 5:12, 2 The 1:7-9) Ukombozi kutoka dhambini kupitia kifo cha kidhabihu (sadaka takatifu) nacha kipatanishi cha Bwana wetu Yesu. (Rum 3:25-26, 5:15-21, 2 Kor 5:19,Mk 10:45) Ufufuo wa kimwili wa Mwokozi wetu, kupaa na kuketishwa kwake katikautukufu mkono wa kulia wa Mungu Baba. (1 Kor 15:4, Ebr 8:1) Roho Mtakatifu aliye nguvu ya utendaji wa Mungu ambaye kwa njia yakemtu mwenye dhambi anahuishwa, na muumini kuwezeshwa katika maishana huduma. (Yn 3:5-6, Rum 8:9, 2 The 2:13) Kuhesabiwa haki kwa njia ya neema ya Mungu pekee. (Gal 2:16, Efe2:8-9) Kanisa moja tu ulimwenguni lililo mwili wa Kristo linalowaunganisha ndaniyake waumini wote wa kweli. (Efe 1:22-23, 1 Kor 12:12-13, Mdo 2:41-47) Tumaini la baraka la kurudi tena kwa Kristo katika nguvu na utukufu. (Mdo1:11, Ebr 9:28, 2 Pet 3:10)Sisi wenyewe tunaweza tukajiita kuwa ni “kanisa la kiroho”, lakini tunatambuaumuhimu wa kuepuka kujiweka katika mafungu ya utambulisho. Tunaamini katikavipawa au karama za Roho Mtakatifu (1 Kor 12) na kuendelea kujazwa na RohoMtakatifu. (Efe 5:18)Tumejitoa kwa dhati kutimiza wajibu wa “kuwafundisha mataifa” (Mat 28:19-20,Mdo 1:8), na kwa hiyo wewe utapata mafundisho na pia kuambukizwa maonohaya.Yaliyomo

Sura ya Kwanza: Wokovu1A.B.C.D.E.F.G.H.1233Hitaji la Mwanadamu la WokovuMungu Ametuletea MwokoziNani Awezaye Kuokolewa?Mtu Anaokolewaje?Kuufanya Wokovu Uonekane NjeUhakika wa Wokovu – Hisia.Mnyororo wa WokovuUhakika wa Mnyororo wa Wokovu4455Sura ya Pili: Ubatizo wa Maji6A.B.C.D.E.F.G.H.I.6677Ubatizo ni nini?Kwa nini Yatupasa Kubatizwa?Nani Astahiliye Kubatizwa?Wakati Gani Inapotupasa Kubatizwa?Tukabatizwe Wapi?Nani Awezaye Kubatiza?Tunabatizwaje?HitimishoMnyororo wa Ubatizo wa Maji88888Sura ya Tatu: Ubatizo wa Roho Mtakatifu9A.B.C.D.E.F.91112121315Roho Mtakatifu ni Nani?Ubatizo wa Roho Mtakatifu ni Nini?Ninapokea Ubatizo Huu kwa Njia Gani?Nani Abatizaye, Wakati Gani, Na Lipi Litokealo?Kuna Nini Katika Kunena kwa Lugha?Mnyororo wa Ubatizo Katika Roho Mtakatifu.Sura ya Nne: Kiini cha Ubaba wa Mungu16A.B.C.D.E.F.161618181922UtanguliziKwa Nini Mungu Awe na Moyo wa Ubaba?Nini Kinachotusukuma Kumtumikia Mungu?Kuupokea Upendo Alionao Mungu KwetuBaba Yako AmefunuliwaMnyororo: Moyo wa Ubaba wa MunguSura ya Tano: Tumaini Letu23A.B.C.232325UtanguliziUelekeo WetuMnyororo wa Ufufuko

D.E.F.Vipi Kuhusu Hukumu, Thawabu na Jehanamu?Mnyororo wa Hukumu ya MileleJe, “Hizi ni Siku za Mwisho”?252626Sura ya Sita: Ibada28A.B.C.D.E.2829303232Moyo wa IbadaVielelezo vya Ibada Katika Agano la KaleVielelezo vya Ibada Katika Agano JipyaHitimishoMnyororo wa IbadaSura ya Saba: Maombi na 93940414243Maombi ni Nini?Kwa Nini Twapaswa Kuomba?Mifano ya MaombiMafundisho ya Yesu Juu ya MaombiTuombeje?Vikwazo Dhidi ya maombiMnyororo wa MaombiKufungaKufunga ni Nini?Kwa Nini Tunapaswa Kufunga?Kufunga - Tufungeje?Tufunge Wakati Gani?Tahadhari na Miongozo Katika KufungaSura ya Nane: Biblia44A.B.C.D.E.F.444648485050Kile Tukiaminicho Kuhusu BibliaMuundo wa BibliaKwa Nini Tujifunze Biblia – Sababu kumiItupasavyo Kuikaribia BibliaHitimishoMnyororo wa BibliaSura ya Tisa: Fedha na Utoaji51A.B.C.D.58E.F.Mungu Ndiye Chanzo cha VyoteUtoajiFedha na UaminifuKutengeneza Mambo ya Nyumba Zetu515356Thawabu au Tuzo za UtiiMnyororo wa Fedha na Utoaji5859

Sura ya Kumi: Kanisa60A.B.C.D.E.6065656667Sura ya kanisa Ndani ya Barua kwa WaefesoUtume na AgizoKanisa Ulimwenguni na Kanisa la MahaliWewe na KanisaMnyororo wa KanisaSura ya Kumi na Moja: Kuwekewa Mikono68A.B.C.D.68707273Kutoa Baraka, Mamlaka na UponyajiKupokea Roho Mtakatifu na Vipawa vya KirohoWatumishi Kuwekwa WakfuMnyororo wa Kuwekewa MikonoSura ya Kumi na Mbili: Unabii74A.Maandiko na Roho ya UnabiiB.Unabii Kwa Watu BinafsiC.Hamu ya Kuwa na Huduma ya KinabiiD.Je, Hivi Twaweza Kutarajia Kumsikia Mungu Akinena?E.Kuitambua Sauti ya MunguF.Ni Wakati gani Mungu Anasema Nasi na Kwa Njia Gani?Tunafanya Nini na Neno la Mungu?78H.HitimishoI.Mnyororo wa Unabii747475767677.7979Sura ya Kumi na Tatu: Uenezaji Injili80A.B.C.D.E.8080838384Njia Ngumu ya Mashaka Kuelekea UinjilishajiTabia Tatu za Uenezaji InjiliKanuni Zifaazo kwa Uenezaji InjiliDondoo Zinazoweza Kusaidia Kwa UinjilishajiMnyororo wa Uenezaji InjiliSura ya Kumi na Nne: Vita ya Kiroho85A.B.C.D.E.8587909090UtanguliziVitaMaombi (Sala) na KufungaHitimishoMnyororo wa Vita ya KirohoSura ya Kumi na Tano: Maono, Mali na Magari Yetu91A.B.C.919194UtanguliziKichwa (Uongozi/Mamlaka)Moyo Wetu (Kiini au Roho ya Utamaduni Wetu)

D.E.F.Tumaini (Maono)Vyombo vya Kusafirishia Maono, ThamaniMuhtasari na Hitimisho959898

Sura ya Kwanza: WokovuLakini andiko limeyafunga yote chini yanguvu ya dhambi, makusudi haowaaminio wapewe ile ahadi kwa imaniya Yesu Kristo. (Gal 3:22.)A. Hitaji la Wokovu Kwa MwanadamuNia aliyokuwa nayo Mungu mwanzoni ilikuwa ni kuwa na uhusiano wa kiagano na wanadamu. Hata hivyo, “anguko” na “dhambi” vilisababisha utengano na hivyo kuwezeshakifo kitawale. Hitaji la wokovu kwa mwanadamu ni matokeo ya dhambi, kwa kuwaMungu mtakatifu hawezi kuigusa dhambi.A.1. Dhambi Hutenganisha“Lakini maovu yenu yamewafarakanisha ninyi na Mungu wenu” (Isa 59:2a)A.2. Dhambi ni Tatizo Kwa Ulimwengu Wote“Hakuna mwenye haki hata mmoja.” (Rum 3:10b)Wanadamu wote wameishiriki dhambi: Kwa kuzaliwa:“Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyomauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi.” (Rum5:12)“Na kama kwa kutotii kwa mtu mmoja watu wengi walifanywa wenye dhambi.” (Rum5:19)“Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; Mama yangu alinichukua mimba hatiani.”(Zab 51:5)Kwa hali hii, dhambi ni urithi wetu wa kuzaliwa tangu hapo anguko lilipotokea. Kwa tendo:“Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.” (Rum3:23)A.3. Ipo Adhabu Kwa Ajili ya DhambiAdhabu ya dhambi ni hukumu ya Mungu na kifo. “Kwa maana mshahara wa dhambi nimauti;” (Rum 6:23a)“Roho ile itendayo dhambi itakufa.” (Eze 18:4b)A.4. Muhtasari1

Wanadamu wote wako chini ya dhambi. Dhambi humtenga mwanadamu ikimuwekambali na nia ya Mungu ya uhusiano wa kiagano na ukaribu. Dhambi hukiwezesha kifokitawale.B. Mungu Ametuletea MwokoziB.1. Mwanadamu Hana Uwezo wa Kujiokoa“Matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi.” (Isa 64:6a)“Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana nanafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.”(Efe 2:8-9)B.2. Hali Hii Haituachi Tukiwa Hatuna Tumaini“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ilikila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” (Yn 3:16)“Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu.” (1 Yn 3:16a)B.3. Nini Kimpacho Yesu Uwezo wa Kuondoa Dhambi? Alizaliwa toka kwa mwanamke bikira na hivyo hakuwa chini ya dhambi iliyoendelezwa kwa njia ya urithi toka kizazi hadi kizazi (dhambi ya asili, angalia, kwamfano, Rum 5:12). Yeye mwenyewe hakupata kufanya dhambi yoyote (Ebr 4:15). Yesu alivumilia mateso ya adhabu (ghadhabu) ya Mungu kwa ajili ya dhambi.Kwa kulifanya hilo alifanyika kuwa dhabihu au sadaka ya upatanisho kwa ajili yadhambi na kusimama kama afanyaye malipizi badala ya wanadamu watendadhambi: “Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwakuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. Basi zaidisana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwayeye.” (Rum 5:8-9)“Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu.”(Isa 53:5a/Mat 4:12) Aliiharibu nguvu ya kifo kwa kuwa alifufuka kutoka katika wafu. (angalia 1 Kor 15:3-6na Ebr 2:14-15).B.4. MuhtasariMungu alimuumba mwanadamu, mwanadamu akaanguka dhambini, na hivyo watu wotewako chini ya nguvu ya dhambi. Mungu ametupatia Mwokozi awe suluhisho: Mwokozialikufa akiwa dhabihu au sadaka mbadala kwa mwanadamu mtenda dhambi. Ni jambolililo wazi, hata hivyo, kwamba ukombozi huu haumuhusu kila mmoja kwa sababu Bibliainatamka wazi kwamba baadhi ya wanadamu watatupwa katika jehanamu ya moto pindiwakati wa hukumu utakapowadia.2

C. Nani Awezaye Kuokolewa?Uwezekano upo, kwamba watu wote wanaweza kuokolewa. Yategemeana na mwitikiowao binafsi juu ya ufunuo ambao Mwenyezi Mungu ameutoa. Ni hamu ya Mungu kuonakwamba watu wote wangeokolewa (1 Tim 2:4), Yesu alikufa kwa ajili ya “ulimwengu” (Yn3:16). Lakini, kwa hali halisi si kila mmoja ameokolewa. Swali ni kwamba, “Mtu anapataje kuokolewa?”D. Mtu Anaokolewaje?Paulo aliwasihi na kuwatia moyo watu “wamtubie Mungu, na kumwamini Bwana wetuYesu Kristo.” (Mdo 20:21). Yesu alianza mahubiri yake kwa kusema, “Wakati umetimia,na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili.” (Mk 1:15). Vifungu hivi viwilivyote vinaonyesha mahitaji makuu mawili ya kibiblia yanayohitajika ili mtu aweze kupatawokovu: toba na imani (angalia pia Ebr 6:1-2). Mahitaji haya yanajumlisha mambo gani?D.1. TobaNeno la Kiyunani “metanoia” maana yake ya moja kwa moja ni “ni mtu kubadili mawazo/akili/nia.” Hii ina maana kwamba toba si hali ya kujisikia vibaya au kusikitika bali ni haliya uamuzi, uamuzi wa kubadilika. Ni tendo la dhamira na wala si la hisia. Ni kwelikabisa, kwamba tendo lenyewe laweza kuandamana na hisia kali lakini toba yenyewe nimabadiliko ya mawazo, akili au nia.Mabadiliko haya ya mawazo, akili au nia na hatimaye mabadiliko ya maisha yetu katikakila eneo ni:Utambuzi wa hali yetu halisi ya dhambi.Uamuzi wa kuishi kulingana na mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa kwa ajili ya watu wakewateule.“‘Wakati umetimia,’ Yesu alisema. ‘Tubuni na kuiamini Injili!’ ” (Mk 1:15; Mdo 2:38a)D.2. ImaniHii inatutaka tuweke tumaini letu ndani ya Yesu – na kujiambatanisha na ufunuo waYesu Kristo kama Mwokozi. Hakuna kazi au tendo ambalo mtu aweza kulifanya linaloweza kumfanya astahili kupewa haki na Mungu.“Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana nanafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.”(Efe 2:8-9a)Zawadi haifanyiwi kazi, inaweza tu kupokelewa.“Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani.” (Rum 5:1a) Kufanywa kuwawaadilifu au kuhesabiwa haki ni neno la kisheria linalotumika kwa wale ambao hatia yaoimeondolewa. Ili kuondolewa hatia iliyo juu ya wanadamu wote mtu lazima awe na imanikatika kazi ya uokozi ya Yesu Kristo. Imani, kwa hivyo ni kuliamini Neno la Mungu.3

“Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki yaMungu katika Yeye ” (2 Kor 5:21)Neno la Mungu ni Kweli (Yn 17:17) na halina uongo hata kidogo. Kwa hivyo tunawezakulitumainia kwa mioyo yetu yote.E. Kuufanya Wokovu Wako Uonekane NjeToka wakati ule tunapotubu na kumwamini Yesu, tunaingia ndani ya ufalme wa Mungu.Tendo hili linaelezwa kama “kuzaliwa upya au kuzaliwa mara ya pili ” (Yn 3:3). Tokea kipindi hiki cha kuingia ndani ya ufalme hadi mwisho wa maisha yetu duniani, tunakuwa nawajibu wa kuishi maisha yetu katika hali ya toba (hali ya kuendelea kujiweka chini yaNeno la Mungu) na kuwa na imani kwa Yesu Kristo kama Mwokozi.Yesu alisema katika Yn 10:27-30, “Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua,nao wanifuata. Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakunamtu atakayewapokonya katika mkono wangu. Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu kulikowote; wala hakuna mtu awezaye kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu. Mimi naBaba tu umoja.” Hivyo, mara tunapokuwa tumeokolewa wokovu wetu unalindwa naYesu – hakuna yeyote awezaye kutuibia wokovu huo. Lakini Biblia inatuonya katika 2Tim 2:12b, “Kama tukimkana yeye, yeye naye atatukana sisi.”Kwa hivyo tunatiwa moyo kuvumilia tukidumu katika imani yetu hadi kufa, au hadi Kristoarudipo. Waebrania 10:35-36 inatuambia, “Basi msiutupe ujasiri wenu, kwa maana unathawabu kuu. Maana mnahitaji saburi, ili kwamba mkiisha kuyafanya mapenzi yaMungu mpate ile ahadi.” Tunapovumilia tukiishi katika uadilifu, matendo mema, uaminifuna mateso, tunalipwa kwa kupewa hazina za milele na Mungu mwenyewe (angalia, kwamfano, Ebr 11:26, Mat 6:1-6, Mat 6:16-21, Mat 10:41-42, Mat 16:27 na Lk 6:22-23).F. Uhakika wa Wokovu – Hisia.Maisha ya Kikristo hayahusu tu kujizoeza katika imani pasipo kujipatia "uzoefu".Muumini anaweza kuhisi na kuwa na hisia au misisimko inayompa kujua kwa hakikakwamba yeye ni mtoto wa Mungu. Biblia inatuonyesha wazi kwamba Roho Mtakatifuaweza kushuhudia pamoja na roho zetu kwamba sisi ni watoto wa Mungu katika Warumi8:16, “Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto waMungu.” Uzoefu wa jinsi hii utahusisha hata hisia zetu pia.Hata hivyo, ni lazima tusisitize wazi kwamba misisimko hii na hisia si vitu vya kuendeleaau vya kudumu. Misisimko na hisia hizi ni MATOKEO tu ya imani katika Neno la Munguna kuifanyia kazi Kweli iliyo katika Neno lenyewe. Nyakati huja ambapo Mkristo binafsihujihisi kama mtu ambaye hajaokolewa. Misisimko au hisia zetu zinaathiriwa na hali yamazingira yanayotuzunguka, na tunaweza kujikuta tukiwa wapweke sana, na nyakatizingine hata tukajiona kuwa Mungu mwenyewe ametuacha. Katika nyakati kama hizihatuwezi kuzitegemea hisia zetu, lakini katika hali ya ukomavu wa kiroho tuziambie nafsizetu kwamba tunapaswa kuliamini Neno la Mungu.Misisimko na hisia ambazo ni matunda ya imani kwa kweli ni ziada tu au nyongeza, nikama, "rojo ya maziwa inayowekwa juu ya keki". Haitakiwi tuifanye kuwa msingi waimani yetu, wala hatutakiwi tuifanye misisimko hiyo na hisia kuwa ndiyo lengo letu. Inakuja yenyewe pale sisi tunapotafuta kulitii Neno la Mungu, lakini ITAKUJA, na tunaweza4

kutegemea kujipatia uzoefu wa hisia zinazosisimua, hali ya amani na kujiona kuwa namaisha yenye utoshelevu.G. Mnyororo wa WokovuYnRumRumYn1 YohYnEfeRum3:163:236:2314:61:91:122:8-910:9-10H. Uhakika wa Mnyororo wa Wokovu1 27-295

Sura ya Pili: Ubatizo wa Maji“Tazama, maji haya; ni nini kinachonizuia nisibatizwe?”(Mdo 8:36b)A. Ubatizo ni Nini?A.1. Ishara ya NjeUbatizo ni ishara ya nje inayoashiria tendo la ndani na lisiloonekana, la kuzaliwa maraya pili au kuzaliwa upya. Wakati wa uongofu wetu tunabatizwa kwa kuunganishwa na“Kristo” (Gal 3:27), na hivyo ubatizo huonyesha maana ya ubatizo wa kiroho ndani yamwili wa Kristo. Ubatizo wa maji unakuwa kama taswira au picha ya kile kilichomtokeamtu ambaye amekuwa Mkristo. Wanapozamishwa chini ya maji wanaashiria kifo chaKristo na hali yao ya kufa kuelekea matakwa ya nafsi zao wenyewe. Wanapoinuliwa juuya maji wanaonyesha picha ya ufufuko wa Kristo na kufufuka kwao wenyewe kwakuingia katika uzima mpya (Rum 6:1-14).Katika Agano la Kale, tukio katika kitabu cha Kutoka la kuvuka bahari ya Shamu lilikuwani mfano wa Ubatizo ambao kupitia huo Wana wa Israeli waliwekwa huru toka katikautumwa wa Misri (1 Kor 10:2, 1 Pet 3:21).A.2. Ukiri HadharaniUbatizo ni ukiri wa hadharani wa hali ya ndani ya kujitoa kwa mtu binafsi. Katika maishaya waumini wengi, hutokea kwamba mara tu baada ya kubatizwa mateso makali huwaandama kutokana na hali halisi ilivyo ya ukiri huu wa imani.B. Kwa Nini Yatupasa Kubatizwa?B.1. UtiiYesu aliamuru ubatizo: “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi,mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hataukamilifu wa dahari” (Mat 28:19-20a).B.2. Kufuata Mfano wa YesuYesu alionyesha mfano kwa kubatizwa na Yohana Mbatizaji (Mat 3:13-17). Yohana Mbatizaji alipojaribu kumzuia Yesu asibatizwe yeye alimjibu, “Kubali hivi sasa; kwa kuwandivyo itupasavyo kuitimiza haki yote.”Ubatizo ulionyesha kwamba Yeye alikuwa amejitoa wakfu kwa Mungu na sasa alikuwaamekubaliwa “rasmi” na Baba (jambo linaloonekana katika kushukiwa na Roho Mtakatifu, na maneno aliyotamka Baba kumthibitisha).Ilikuwa wakati wa ubatizo wake, pale Yohana Mbatizaji alipomtangaza mbele ya watuwote kwamba Yeye ndiye aliyekuwa Masihi. Yesu alijifananisha na mwanadamu6

mwenye dhambi japo Yeye mwenyewe hakuwa na hitaji la kutubu. Ubatizo wakeulikuwa ni mfano kwa wafuasi wake.B.3. Mfano wa Kanisa la KwanzaWaongofu wa kwanza katika Yerusalemu (Mdo 2:37-41).Wasamaria (Mdo 8:12-13).Towashi (Mwethiopia) Mkushi (Mdo 8:36-38).Paulo (Mdo 9:17, Mdo 22:16).Kornelio pamoja na nyumba yake (Mdo 10:33-48).Mwanamke Lidia pamoja na nyumba yake (Mdo 16:13-15).Askari wa gereza Mfilipi (Mdo 16:31-34).Krispo na Wakorintho wengine (Mdo 18:8).Ni muhimu kuelewa kwamba ubatizo wenyewe peke yake, hauwezi kumwokoa mtuyeyote, lakini wenyewe huo ni hatua ya utii wa nje iliyo ya lazima kwa ajili ya kuthibitishatoba ya ndani.C. Nani Astahiliye Kubatizwa?Waumini wote sharti wabatizwe: Si ubatizo wa watoto wala ubatizo wa watu wazima, baliubatizo wa wote waaminio. Ni waumini pekee wanaopaswa kubatizwa. Ubatizo ni isharaya mabadiliko yaliyopo na wala si kisababishi cha mabadiliko.C.1. Vipi Kuhusu Ubatizo wa Vitoto Vichanga?Watoto hawawezi kutubu. Yesu hakubatizwa akiwa mtoto mchanga, bali aliwekwa wakfukwa Bwana katika Luka 2:22. Watoto wenye umri wa kuielewa injili na kuonyesha kuwana imani yao binafsi wanaweza kubatizwa. Jambo hili laweza kutokea katika umri mdogosana kwa sababu injili ni rahisi kiasi cha mtoto kuweza kuielewa. Waumini wanaorudinyuma hawapaswi “kubatizwa upya” wanapomrudia Kristo kwa kuwa ubatizo ni tendolifanyikalo mara moja tu, sawa na vile ambavyo tendo la kuzaliwa linatokea mara mojamaishani.D. Wakati Gani Inapotupasa Kubatizwa?Ni wakati tunapopata uongofu. Katika kanisa la kwanza watu walibatizwa mara tu walipoamini. Katika siku ya Pentekoste, “Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na sikuile wakaongezeka watu wapata elfu tatu.” (Mdo 2:41). Paulo alibatizwa mara tu baadaya kuamini. Uongofu na ubatizo vilikuwa vitu viwili vilivyokwenda sambamba katikakanisa ka kwanza, mara nyingi vyote viwili vikitokea katika siku moja. Angalia, kwamfano, Matendo 10:47-48.E. Tukabatizwe Wapi?7

Popote! Hatuhitaji vyombo maalumu vilivyojengwa kwa ajili ya kubatizia. Maji yoyote yaliyo karibu na hapo mtu apatiapo uongofu yanafaa. Angalia kwa mfano, Matendo8:38-40.F. Nani Awezaye Kubatiza?Muumini yeyote aweza kubatiza. Si lazima awe mzee au kiongozi. Filipo aliyembatizatowashi wa Kiethiopia alikuwa muenezaji wa injili (muinjilishaji).G. Tunabatizwaje?G.1. Kwa KuzamishwaTunabatiza kwa kuzamisha, na si kwa kunyunyizia (Mdo 8:38-39). Filipo na towashi,wote walishuka na kuingia majini na Filipo akambatiza. “Walipotoka majini.” (Mdo 8:39a).Neno “ubatizo” linatokana na neno la Kiyunani, “baptiso”, lenye maana ya “kuzamisha,kuchovya, kutumbukiza au kuzika” na daima hutumika likiwa katika muundo wenyenguvu unaoonyesha tendo la kuzamisha kitu kabisa.G.2. Katika Jina la Baba, Mwana na Roho MtakatifuSisi hubatiza katika jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu (Mat 28:18, Gal3:27). Msisitizo ulikuwa kwamba huu ulikuwa ubatizo wa Kikristo , na si wa Kiyahudi, kipagani au ubatizo wa Yohana Mbatizaji.H. HitimishoKwa kuhitimisha, ubatizo ni tendo rahisi la utii kwa Neno la Mungu lililofunuliwa. Tendohili hukaribisha baraka za Mungu ndani ya maisha yetu na kutuweka hali imara juu yamsingi wa kimungu. “Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba.” (Mat 7:24)I. Mnyororo wa Ubatizo wa MajiMdo2:38-39Mat3:13-17Mat28:19-20Mdo 10:47-48Rum 6:1-14Kol2:9-151 Pet 3:218

Sura ya Tatu: Ubatizo wa Roho Mtakatifu“Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili yatoba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvukuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.” (Mat 3:11)Hakuna “hatua” tatu za mtu kupata kuwa Mkristo, bali ipo hatua moja tu: toba inayooandamana na imani. Hata hivyo, Biblia inazungumzia ubatizo wote wa aina mbili, yaani wamaji na wa Roho Mtakatifu kuwa ni majaliwa ambayo mwongofu wa kweli sharti apitie.Kwa hali hii, kupata ubatizo wa Roho kunafanya “mchakato” wa uongofu uwe umekamilika.Itakuwa vigumu kukielewa na kukitamani kitendo hiki kitokee maishani mwetu endapokwanza tutakuwa hatuna maarifa ya kumjua Roho Mtakatifu ni nani, naye hufanya nini.Kwa hiyo tunatakiwa kuanza kwa “kumtambulisha” Roho Mtakatifu.A. Roho Mtakatifu ni Nani?A.1. Nafsi YakeRoho Mtakatifu ni nafsi ya tatu ya Mungu aliye nafsi tatu, ni mshiriki aliye sawa na aliyewa milele sawa na Baba na Mwana. Kwa karne nyingi Yeye alikuwa nafsi ya UtatuMtakatifu iliyosahauliwa na kanisa; lakini katika wakati huu wetu amerejezwa katika nafasi anayostahili ndani ya mawazo na uzoefu wa maisha ya Kikristo.Roho Mtakatifu si nguvu ya hivihivi tu au nguvu fulani ya Mungu inayofanya kazi ulimwenguni (wazo potofu la kawaida la wengi), lakini yeye ni nafsi hai: Biblia inamzungumzia kama “Yeye” na “Yake,” na wala si “kitu” na “ya kitu” na Biblia inamwonyeshaakiwa na tabia za mwenye nafsi (akili na mawazo, usemi na lugha, kama vile pia hisiana misisimko) akifanya vitendo vya aliye na nafsi (kwa mfano, kuonyesha njia, kuongoza, kutenda kazi, kutoa, kufanya ushirika, kutia hatiani, kufundisha, kufariji, kushaurina kuomba).Roho Mtakatifu si mdogo kuliko Mungu (wazo lingine lililokuwa potofu) bali ni Mungukamili. Anaitwa Mungu katika Maandiko yaliyo wazi na ndani ya mengine ambayo kutokana na utendaji wake katika Maandiko hayo inakuwemo maana iliyojificha inayomwonesha kama Mungu kamili; Anazo sifa za kimungu (kwa mfano, kuweza yote, kuwa mahali pote, kujua yote na kutokufa) na anatenda au kushiriki katika kazi ya Mungu (kwamfano, uumbaji, kufunua, kuonyesha hatia, kubadilisha, kutakasa na kufufua).Roho Mtakatifu ni mwenye nafsi na pia Mungu, na kwa kuwa yeye anayo nafsi twawezakuwa watu wanaohusiana naye au wasio na uhusiano naye (hatuwezi kuhusiana nanusu ya mtu mwenye nafsi), na kwa hali hii hatuwezi kuuliza swali “Hivi, mimi nina kiasigani cha Roho Mtakatifu?” Lakini badala yake swali linalofaa ni “Roho Mtakatifu anatawala kiasi gani cha maisha yangu”Kwa sababu Yeye ni Mungu anayefanya kazi maishani mwetu kwa kuangalia matakwayake na si yetu. Yeye hufanya apendavyo na hivyo haiwezekani tumuamrishe afanyetutakacho; Yeye ni mtakatifu na hivyo hataweza kukijaza chombo kisicho safi.9

Ufahamu mwingine juu ya Roho Mtakatifu waweza kupatikana kutokana na majinamengi anayoitwa katika Maandiko na pia alama zinazotumika kumuelezea (moto, upepo,maji, mafuta na hua).A.2. Kazi YakeYeye kama sehemu ya utatu wa Mungu, Roho Mtakatifu anahusika katika kazi zote zaMungu. Yeye alihusika na alikuwa mwenye sehemu muhimu katika kazi ya uumbaji,kutoa ufunuo, katika matendo makuu ya Mungu kwa Israeli na pia katika tendo maalumuambalo kwa hilo Kristo alifanyika kuwa mwanadamu. Anashughulika ndani ya kanisa;Anakaaa ndani yake, analiunganisha, anatoa vipawa kwa washiriki na pia anaujengamwili, anawaweka na kuwawezesha viongozi wake, na kuelekeza katika lengo la utumewa kanisa. Atakuwa mwenye kuhusika kwa karibu katika matukio ya siku za mwisho, napia katika milele ijayo.Kwa vyovyote vile, kazi ya Roho Mtakatifu inaonekana zaidi katika kipindi hiki kwa kulekuhusika kwake ndani ya maisha ya muumini binafsi. Hata kabla ya wokovu ni RohoMtakatifu ampaye mwanadamu kujiona ni mwenye hatia na kumfanya amkaribie Kristo(Yn 6:44, Yn 16:8-11). Wakati mtu kupata anapoongoka, Roho ndiye afanyaye mabadiliko ndani ya roho ya mtu huyo na kumfanya azaliwe mara ya pili (Yn 3:5-8, Tito3:5). Tangu wakati huo na kuendelea, kila muumini hukaliwa ndani yake na Roho Mtakatifu (Rum 8:9) na kwa hali hii, anakuwa amepigwa muhuri na Yeye Roho: ambaye uwepowake ni kama malipo ya kwanza yanayokuwa ni dhamana kwa ajili ya malipo kamili ya(wokovu) yatakayotolewa mara Kristo ajapo (Efe 1:13-14, Efe 4:30, 2 Kor 1:22).Baada ya kupata uongofu kwa maisha yote ya mtu husika, Roho Mtakatifu anatembeana muumini, akimpa uhakika, akimtakasa, akishirikiana naye, akimwongoza, akimshauri,akimfundisha, akimvuvia na kumpa vipawa. Tunaweza kusema kwamba Roho Mtakatifuhuchukua jukumu la msingi kwa ajili ya maisha ya muumini, akichukua hatua kwa hatua,toka mwenye dhambi aliyetiwa hatiani hadi kuwa mtakatifu aliyekamilishwa na kufikishwa katika kilele cha wito wake.Huu hasa ni utambulisho wa kukupa uelewa juu ya Roho Mtakatifu tuliyepewa na Yesu(Yn 14:16-18). Yeye ni mfariji/mshauri/mtetezi (hakuna tafsiri maalumu kwa neno la Kiyunani “parakletos,” linalomaanisha ‘mmoja atembeaye nasi akitupa ushauri katika kilahatua tunayoipiga njiani). Yesu aliposema “nitawatumia msaidizi mwingine” neno la Kiyunani lililotumika siyo heteros (lenye maana ya mwingine), bali neno “allos” (neno laKiyunani lenye maana ya “mwingine aliye sawa kabisa).Kwa hivyo kama ilivyo kwambakumjua Yesu ni kumjua Baba (Yn 14:7-9), vivyo hivyo, kumjua Roho ni kumjua Yesu (nakinyume chake).Roho Mtakatifu hutuwezesha kuzitimiza amri za Kristo kwetu na kutupa vipawa ili kutupauwezo wa kuyatimiza yale tuliyoitwa kuyatimiza. Kugundua vipawa vyetu tulivyopewa nisehemu muhimu ya maisha yetu ya kutembea na Bwana, na jambo hili litatiliwa maananikatika majadiliano yatakayofuata.Sasa kwa kuwa tumemjua Roho Mtakatifu ni nani na ni nini anachokitaka kukifanya kupitia katika maisha yetu, tutakuwa na uwezo zaidi wa kuelewa, kutamani na kuupokeaubatizo wa Roho Mtakatifu.B. Ubatizo wa Roho Mtakatifu ni Nini?10 page

"Mafunzo ya kwanza." au ya "msingi" yote yanayopatikana katika kifungu hiki cha Biblia yamepanuliwa. Mafunzo haya yameandaliwa yawasaidie zaidi wale wanaopitia mafunzo ya Kuweka Msingi wa Imani katika Kanisa la Cornerstone maana yake kwa ni Kiswahili Kanisa la Jiwe la Pembeni. Mafunzo haya yanawawezesha kulenga zaidi katika kile .

Related Documents:

1. maisha mapya katika kristo 1 2. maisha mapya katika ushindi 5 3. maisha mapya yenye uweza 9 4. maisha mapya yenye usawa 13 5. ukufunzi wenye nguvu - nafasi nzuri 17 6. misingi yenye nguvu taratibu ya viongozi 19 7. cheti cha kuhitimu ukurasa wa nyuma

KITABU CHA MISINGI YA BIBLIA Carelinks, PO Box 152, Menai NSW 2234 AUSTRALIA www.carelinks.net email: info@carelinks.net . YALIYOMO 1) Biblia 2) Mungu 3) Mpango na nia ya Mungu 4) Mauti 5) Ahadi za Mungu 6) Bwana Yesu Kristo 7) Ahadi ya Mungu kwa Daudi 8) Ufufuo wa Yesu 9) Kurudi kwake Yesu Kristo .

MISINGI YA BIBLIA Bible Basics: Kiswahili KITABU CHENYE MAFUNZO . AMANI KWA UKRISTO ULIO WA KWELI DUNCAN HEASTER Carelinks, PO Box 152 Menai NSW 2234 AUSTRALIA www.carelinks.net . 2 DIBAJI Watu wote ambao wamekubali kuwa Mungu yupo, na kwamba Biblia ni ufunuo wake kwa mwanadamu, Kwa kusema kweli wanahitaji . wamekuwa ndio chanzo cha msaada .

KITABU CHA MISINGI WA BIBLIA. Kama umefurahia kitabu hiki na ungependa kuendeleza masomo yako, kuna kitabu kingine kiitwacho MISINGI WA BIBLIA kinachoweza kupatikana kutoka kwa anwani hii: Christadelphian Advancement Trust, P.O. Box 3034, SOUTH CROYDON, SURREY CR2 OZA ENGLAND Wavuti: www.carelinks.net Barua pepe: info@carelinks.net

Kikristo ya kwamba watu wanaokolewa kwa neema ya Mungu tu kwa njia ya imani katika Yesu Kristo—na hii huifanya familia yote ya Kikristo (Wayahudi na Mataifa pia) kuwa moja; (3) Kisha kinajadili ile maana hasa ya huu msimamo wa wokovu kwa ile jamii mpya: watu wanapaswa kuishi maisha mapya kwa imani inayotiririka

IMANI Telecom Series: Why you are paying so much for broadband Internet and what should be done about it. Ghana’s largest revenue sources since independence has been from the export of natural resources such as Gold, Cocoa, Timber and until recently crude oil. . This still remains a pipe dream in Ghana.

all about the incredible explanation of who He is, and that He is . A.W Tozer said that we are to 13. CHRIST-CENTERED CHURCH - CAPTIVATED have an eternal pre-occupation with Christ. This is a way to live. There’s a s

Sarjana Akuntansi Syariah (S.Akun) Pada Program Studi Akuntansi Syariah Menyetujui Pembimbing I Pembimbing II Drs. Sugianto, MA Kamilah, SE, AK, M.Si NIP. 196706072000031003 NIP. 197910232008012014 Mengetahui Ketua Jurusan Akuntansi Syariah Hendra Harmain, SE., M. Pd NIP. 197305101998031003 . LEMBARAN PERSETUJUAN PENGUJI SEMINAR Proposal skripsi berjudul “PERLAKUAN AKUNTANSI TERHADAP .