ULINGANISHI WA TABIA ZA WAHUSIKA WAKUU NA DHAMIRA KATIKA .

3y ago
119 Views
3 Downloads
534.69 KB
84 Pages
Last View : 21d ago
Last Download : 3m ago
Upload by : Macey Ridenour
Transcription

ULINGANISHI WA TABIA ZA WAHUSIKA WAKUU NA DHAMIRAKATIKA RIWAYA ZA KUSADIKIKA NA UTENGANOMIZA OMAR MOH'DTASNIFU ILIYOWASILISHWA KWA AJILI YA KUTIMIZA BAADHI YAMASHARTI YA KUTUNUKIWA SHAHADA YA UMAHIRI YA KISWAHILI(M. A. KISWAHILI - FASIHI) YA CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA2017

iiITHIBATIAliyetia saini hapa chini anathibitisha kwamba ameisoma kazi hii na anaidhinishaikubaliwe kwa utahini na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania tasnifu yenye mada:“Ulinganishi wa Tabia za Wahusika Wakuu na dhamira katika Riwaya zaKusadikika na Utengano" na kupendekeza ikubaliwe na Chuo Kikuu Huria chaTanzania kwa ajili ya kukamilisha masharti ya Shahada ya Umahiri katika Kiswahiliya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.Dkt. Hadija Jilala(Msimamizi).Tarehe

iiiHAKIMILIKIHairusiwi kuiga au kumiliki kwa namna yoyote ile sehemu ya tasnifu hii kwa njiayoyote kama vile, kielektroniki, kurudufu nakala, kurekodi au njia yoyote nyinginebila idhini ya mwandishi au Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kwa niaba.

ivTAMKOMimi Miza Omar Moh'd, nathibitisha kwamba tasinifu hii ni kazi yangu halisi nakwamba haijawahi kuwasilishwa na haitawasilishwa katika Chuo Kikuu kinginechochote kwa ajili ya masharti ya kupata shahada yoyote. .Saini .Tarehe

vTABARUKUNatabaruku kazi hii kwa wazazi wangu, Bw. Omar Moh'd Shoka na Bibi HabibaHamad Ali kwa kunizaa, kunilea, kunisomesha, na kunipa moyo katika kipindichote cha masomo yangu, tangu darasa la kwanza mpaka sasa ninapokamilishamasomo yangu ya Shahada ya Umahiri. Mawazo yao na busara zao katika elimunitazikumbuka daima na kuwa chachu ya kujiendeleza zaidi.Aidha, ninaitabaruku kwa wanangu Habiba Abubakar na Haabil Abubakar, piawakwe zangu Makame Fakih na Dawa Fakih, kwa uvumilivu wao katika kipindichote cha masomo yangu.

viSHUKURANIKwanza, napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu muweza wa kila kitu, kwakunijaalia afya njema, nguvu, uwezo, akili, busara, maarifa, utulivu na uvumilivukatika kipindi chote cha masomo yangu ya uzamili na utafiti huu. Namshukuru tenakwa unyenyekevu kwa kusema, Alhamdulillah Rabbilaalamina.Pili, napenda kumshukuru kwa dhati Msimamizi wangu Dkt. Hadija Jilala kwakuniongoza vyema katika kila hatua ya utafiti huu. Siku zote, hakusita walahakuchoka kunishauri na kuirekebisha kazi hii katika hatua zote mpakailipokamilika. Amenilea kitaaluma na kunipa misingi ya nadharia za fasihi, fasihilinganishi na mbinu za utafiti ambazo zimezaa kazi hii. Namuomba MwenyeziMungu ambariki na ampe afya njema na amzidishie kila la kheri, Amin.Tatu, napenda kuishukuru familia yangu kwa uvumilivu waliouonyesha kwa kuelewakuwa nilikuwa masomoni, kwani wakati mwingi waliukosa upendo wa mama.Aidha, napenda kumshukuru kwa dhati mume wangu mpenzi, Dkt. AbubakarMakame, kwa subira, msaada wake wa hali na mali, ushirikiano na ustahamilivu wahali ya juu aliouonesha katika kipindi chote cha masomo na utafiti huu. Shukrani zapekee kwa ndugu zangu Moh'd O. Moh'd na Said O. Moh'd kwa misaada yao ya halina mali iliowezesha kutoka kazi hii katika hali ilionayo.Mwisho, napenda kuwashukuru walimu wangu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzaniakwa kunilea kitaaluma na kunikuza kinadharia na vitendo. Walimu hao ni Prof. E.Mbogo, Prof. T. Y. Sengo, na Dkt. M. Omary. Bila kuwasahau wanafunzi wenzanguwa Shahada ya M. A. Kiswahili wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Tawi laZanzibar kwa ushirikiano wao.

viiIKISIRILengo la utafiti huu lilikuwa ni kulinganisha tabia za wahusika wakuu nadhamirakatika riwaya ya Kiswahili kwa kutumia mifano kutoka riwaya ya Kusadikika naUtengano. Pia, malengo mahususi yalikuwa matatu; ambayo ni kueleza muhutasariwa riwaya za Kusadikika na Utengano, kubainisha tabia za wahusika wakuu wariwaya za Kusadikika na Utengano na kulinganisha tabia za wahusika wakuu wariwaya za Kusadikika na Utengano. Data ya utafiti huu imekusanywa kutokamaktabani na uwandani. Kwa upande wa data za maktabani zimekusanywa kwakutumia mbinu ya usomaji maandiko na data za uwandani zimekusanywa kwakutumia mbinu tatu za ukusanyaji data. Mbinu hizo ni majadiliano ya vikundi, usailina hojaji. Nadharia ya Uhalisia na Nadharia ya Uasilia zimetumika katika ukusanyajina uchambuzi wa data za utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwawahusika wakuu katika riwaya zote mbili ya Kusadikika na Utengano,wamesawiriwa katika tabia za aina mbili; yaani tabia nzuri na tabia mbaya kwawahusika hao. Pia, waandishi wa riwaya mbili hizi wameathiriwa na mapokeosimulizi ya visakale vya watu wa pwani. Riwaya zote mbili ya Kusadikika naUtengano zinafanana, sambamba na kutofautiana. Zaidi ya hayo, utafiti huuumebaini kuwa waandishi kwa kiasi kikubwa wanawatumia wahusika wakuukuwasawiri matendo ya watu katika jamii inayohusika. Wahusika wakuu haowengine hupambwa kwa tabia nzuri na wengine huvikwa tabia mbaya ili kuakisitabia za binadamu katika jamii. Mwisho kabisa utafiti huu umetoa hitimisho la jumlana mapendekezo kwa watafiti wengine watakaopenda kuchunguza tabia za wahusikawakuu katika kazi za fasihi.

viiiYALIYOMOITHIBATI . iiHAKIMILIKI . iiiTAMKO . ivTABARUKU . vSHUKURANI . viIKISIRI . viiYALIYOMO . viiiSURA YA KWANZA . 1UTANGULIZI . 11.1Utangulizi . 11.2Usuli wa Utafiti . 11.3Tatizo la Utafiti . 31.4Malengo ya Utafiti . 41.4.1 Lengo Kuu . 41.4.2 Malengo Mahususi . 51.5Masuali ya Utafiti . 51.6Umuhimu wa Utafiti . 51.7Mawanda ya Utafiti . 61.8Mpangilio wa Tasnifu . 71.9Uzingatifu wa Maadili ya Utafiti . 8

ix1.10Hitimisho . 11SURA YA PILI . 12MAPITIO YA KAZI TANGULIZI NA KIUNZI CHA NADHARIA . 122.1Utangulizi . 122.2Historia Fupi ya Riwaya ya Kiswahili . 122.4Dhana ya Wahusika . 152.5Kiunzi cha Nadharia . 192.5.1 Nadharia ya Uhalisia . 192.6Pengo la Utafiti . 242.7Hitimisho . 24SURA YA TATU . 26MBINU ZA UTAFITI. 263.1Utangulizi . 263.2Eneo la Utafiti . 263.2.1 Mbinu ya Mapitio ya Maandiko . 263.3Zana za Utafiti . 273.3.1 Shajara . 273.3.2 Kompyuta . 283.3.3 Simu ya Mkononi . 283.3.4 Vifaa vya Kunukulia . 283.4Uchambuzi wa Data . 283.5Uzingatifu wa Maadili ya Utafiti . 303.6Hitimisho . 32

xSURA YA NNE . 33UWASILISHAJI NA UCHAMBUZI WA DATA . 334.1Utangulizi . 334.2Muhutasari wa Riwaya ya Teule . 334.2.1 Muhutasari wa Riwaya ya Kusadikika . 334.2.2 Muhutasari wa Riwaya ya Utengano . 354.3Kubainisha na Kujadili Tabia za Wahusika . 374.3.1 Tabia za Wahusika Wakuu wa Kusadikika . 374.3.1.1 Karama . 384.3.1.2 Majivuno . 394.3.1.3 Wajumbe Sita . 394.3.2 Tabia za Wahusika Wakuu wa Utengano . 414.3.2.1 Makusudi. 414.3.2.2 Maimuna . 424.3.2.3 Kazija . 434.3.2.4 Farashuu . 444.3.2.5 Mussa . 454.4Kulinganisha na Kutafautisha Tabia za Wahusika. 464.4.1 Makusudi na Majivuno . 464.4.2 Karama na Maimuna . 484.4.3 Kazija na Buruhani . 504.4.4 Fadhili na Mussa . 514.5Data ya Kuonesha Tabia za Wahusika . 534.6Dhamira . 53

xi4.6.1 Uongozimbaya . 534.6.2 Uzalendo na Ujasiri . 544.6.3 Uonevu na Ukandamizaji (Kukosekana kwa Haki) . 544.7Dhamira katika Kitabu Cha Utengano . 544.7.1 Nafasi ya Mwanamke . 544.7.2 Uongozi Mbaya . 554.7.3 Usaliti . 554.9Hitimisho . 58SURA YA TANO . 59MUHUTASARI, HITIMISHO NA MAPENDEKEZO . 595.1Utangulizi . 595.2Muhtasari wa Mjadala . 595.2.1 Kujibu Maswali ya Utafiti . 615.2.2 Mchango wa Utafiti. 645.3Hitimisho . 655.4Mapendekezo . 66MAREJEO. 67KIAMBATANISHO . 71

1SURA YA KWANZAUTANGULIZI1.1UtanguliziUtafiti katika sura hii ya kwanza unahusu utangulizi wa jumla ambao unabainishavipengele vya awali vya utafiti. Vipengele hivyo ni usuli wa utafiti, tatizo la utafiti,malengo ya utafiti; lengo kuu na malengo mahususi, maswali ya utafiti, umuhimu wautafiti, mawanda ya utafiti, mpangilio wa tasnifu, uzingativu wa maadili ya utafiti nahitimisho.1.2Usuli wa UtafitiWaandishi mbalimbali wa fasihi ya Kiswahili (Wamitila, 2002; Ntarangwi, 2004; naSenkoro, 2011) wamechambua wahusika katika kazi za fasihi. Katika kazi zaowataalamu hao wanakubaliana kuwa wahusika katika kazi za fasihi huwa ni viumbeambao huwakilisha tabia za watu katika jamii.Kwa mujibu wa Mlacha (1985) wahusika ni watu ambao msanii mwenyewehuwabuni kutokana na maisha ya jamii yake kulingana na kile anachotakakukifafanua. Kwa upande mwingine, Msokile (1982) anafafanua kuwa wahusikakatika kazi yoyote ya sanaa ni watu, wanyama au vitu. Mara nyingi, wahusika haomwandishi huwasawiri kisanaa ili waweze kuwakilisha nyanja mbalimbali za maishaya jamii. Waandishi huwasawiri wahusika wao kwa kuwapa sifa pambanuzi ambazohuakisi dhamira maalumu zinazokusudiwa na mwandishi ziifikiye jamii.Tunapozungumzia kuhusu wahusika mara nyingi tunarejelea viumbe waliopewa sifaya kutenda kama washiriki katika kazi ya fasihi. Kama tutakavyoona hapo baadayekuwa wahusika wamegawanyika katika makundi mawili makuu. Makundi hayo ni

2wahusika wakuu wa kazi ya fasihi na wahusika wadogo. Wahusika hao ndiowanaoipamba kazi fasihi na kuifanya iweze kuakisi mambo ya yaliyomo katika jamii(Msokile, 1992). Kwa muktadha huo tabia za wahusika wa kazi ya fasihi ndio ambaohusawiri matukio na mambo mbalimbali yanayofanywa katika jamii inayohusika.Waandishi wa riwaya, nao huwasilisha masuala mbalimbali yanayoibuka katikajamii zao ambayo yanahusu nyanja tofauti za maisha ya wanajamii zao kama vilenyanja za kisiasa, kiuchumi, kielimu, kijamii na kiutamaduni. Pia, wahusika wa ainambalimbali wamekuwa wakibuniwa katika kazi hizo kulingana na dhamirazinazojitokeza katika riwaya. Kawaida, wahusika huchukuliwa kuwa ndiowanaoijenga riwaya na tabia za wahusika hao ndizo ambazo huibua dhamira.Dhamira ni jumla ya mambo yanajadiliwa katika kazi ya fasihi (senkoro, 1982).Dhamira za kazi ya fasihi hujitokeza kulingana na matukio ya jamii, wakati,mabadiliko ya jamii na historia ya jamii. Kwa mfano Dhamira zilizoibuliwa kipindicha ukoloni zililenga kuibua suala la ukoloni na unyonyaji mfano ni riwaya yakusadikika (1991) ya Shaaban Robert. Dhamira hizi zinatafautiana na dhamira zakazi za sanaa za kipindi cha kipindi baada ya uhuru, ujamaa na kujitegemea ambazozilijikita katika ujenzi wa jamii mpya. Jamii isiyo na matabaka, uongozi mbaya,ukoloni mambo leo. Dhamira ni kipengele ambacho kinaweza kuhusishwa akuoneshawasaniiwanavyotafautiana katika kuibua matukio ya kijamii kwa tochi ya kisanii. Kwakulinganisha dhamira za kazi mbali mbali za fasihi, tunaweza kubaini muingiliano namahusiano ya dhamira kulingana na mazingira na wakati.

3Dhamira ya kusadikika.Dhamira kuu ya muandishi ni ukombozi.Dhamira hii ndio kuu katika riwayayakusadikika iliyojikita kwenye ukombozi wa kifikra na ukombozi wa kisiasa.Mwandishi mwandishi amemtumia mwandishi karama alieanzisha elimu ya sheriayenye lengo la kuwezesha wananchi ili waweze kushiriki katika mambo mbali mbaliya nchi. Katika kazi za fasihi, wahusika wakuu na wahusika wadogo hujengwa kwatabia ambazo zinaakisi sifa halisi zinazowakilisha matendo ya binadamu. Kunawahusika ambao huwakilisha sifa kamili za watu. Wahusika hao hutenda mambomazuri na mabaya. Hivyo basi, wahusika hao huwa wa aina mbili za tabia; kunawahusika wenye tabia mzuri ambazo huakisi matendo mazuri yanayowakilisha watuwema na kuna wahusika wenye tabia mbaya ambao huwakilisha watu waovu katikajamii inayohusika (Senkoro, 1982).Kwa kuwa, wahusika wa aina mbalimbali hujitokeza katika kazi za fasihi nawahusika hao husawiriwa wakiakisi maisha ya wanajamii, hivyo, tumehamasikakufanya utafiti wa kuchunguza tabia za wahusika wakuu katika riwaya za Kusadikikaya Shaaban Robert na Utengano ya Said Ahmed Mohamed. Hatimayetumelinganisha tabia za wahusika hao zilizobainishwa na mwandishi mmoja namwingine ili kuona kufanana na kutofauti kwa wahusika hao.1.3Tatizo la UtafitiWataalamu mbali mbali wamefanya tafiti zinazohusiana na riwaya miongoni mwawataalamu hao Pamoja na Sengo na Kiango (1973), Senkoro (1977), Mulokozi(1996) na Wamitila (2011). Watafiti wote hawa wamejikita katika kuchunguzamasuala ya kifani na kimaudhui pamoja na kusawiri maisha na mazingira halisi ya

4jamii lengwa, uchunguzi kuhusu mlingano wa wahusika na dhamira katika fasihihaujachambuliwa kwa kina. Licha ya hali hii bado jamii imekuwa na tatizo lakutokujua kwa undani tabia za wahusika hawa, umuhimu wake pamoja na faidazakekwa jamii yetu. Kwa kuwa kazi za Shaaban Robert zimesawiri na kuakisi mojakwa moja jamii ya Waswahili wa Bara na zile za Said Ahmed Mohamed nazozimeakisi na kusawiri moja kwa moja tabia na desturi za

wahusika wakuu wa kazi ya fasihi na wahusika wadogo. Wahusika hao ndio wanaoipamba kazi fasihi na kuifanya iweze kuakisi mambo ya yaliyomo katika jamii (Msokile, 1992). Kwa muktadha huo tabia za wahusika wa kazi ya fasihi ndio ambao husawiri matukio na mambo mbalimbali yanayofanywa katika jamii inayohusika.

Related Documents:

(d) Wahusika Katika Fasihi, wahusika ni vitu, watu au viumbe wengine waliokusudiwa kuwasilisha dhana, mawazo au tabia za watu. Usawiri wa wahusika na majukumu ya uhusika wao hufanywa katika namna inayoleta mvuto wa kisanaa. Kwa mfano, wahusika wasio binadamu kama vile mti au sungura wanapopewa uwezo wa

Wahusika - jinsi mwandishi alivyo wasawili wahusika wake Usimulizi wa kazi za fasihi Wahusika ni binadamu wanaopatikana katika kazi ya kifasihi na ambao wanasifa za kimaadili, kitabia, kiitikadi na kifalsafa ambazo hutambulishwa na wanayoyasema (mazungumzo) na wanayoyatenda (matendo) (Wamitila, 2002).

na Nadharia ya Mwitiko wa M somaji na Fasihi Linganishi ndizo zilizotumika katika kuchambua data za utafiti. Mtafiti alitumia nadharia hii kwa lengo la kuwasawiri wahusika na alitumia nadharia ya Fasihi Linganishi kwa lengo la kulinganisha na kulinganua mbinu za usawiri wa wahusika katika riwaya hizi mbili. Matokeo ya utafiti yamebaini kuwa .

3. Fafanua mchango wa fasihi simulizi katika fasihi andishi. Wahusika wa fasihi simulizi Fasihi simulizi huweza kujengwa kwa wahusika wafuatao: i) Msimuliaji (Fanani): Huyu ni mhusika katika fasihi simulizi, kazi yake kubwa ni kuwaslisha mawazo aliyonayo kwa hadhira. Msimuliaji hujitahidi kutumia mbinu mbalimbali kwa ajili ya kuijenga kazi yake.

c) Fasihi simulizi ni mali ya jamii ilhali fasihi andishi ni mali ya mtu binafsi/mwandishi. d) Fasihi simulizi ina wahusika wa kila aina k.v binadamu, wanyama na ndege, mazimwi na majitu, miungu, mizimu, mashetani na vitu visivyo na uhai k.v. mawe na miti ilhali fasihi andishi ina wahusika binadamu kwa kiasi kikubwa.

Unapofanya maamuzi ya ajira kulingana na uwezo na sifa, na sio tabia za binafsi zisizohusiana na kazi. Unapoheshimu haki za kila mmoja. Unapotoa nafasi ya kutosha kwa watu wenye ulemavu au mahitaji maalum. Unapokataa aina yoyote ya Ukatili au matumizi mabaya ya madaraka. Unapoendelea kufahamu masuala ya usalama, kufuata itifaki za ulinzi na usalama wa ndani na kusimamisha kazi yoyote ambayo si .

Kaani ndani mwangu 122 Appendix A: Asili ya Kristo 129 . waliohudhuria mikutano yao ya uvuvio maisha yao yaliweza kubadilika na kuwa maisha mapya.Katika mwaka wa 1978, wiki la maombi liliandaliwa katika chuo kikuu cha Andrews, . nalo linawakilisha tabia ya kristo, kwa manufaa ya yule mgeni yeyote atakayehudhuria harusi kama atakubaliwa na .

The following summary highlights the basic effective counseling skills useful for positive interactions with patients; 1. Listening – The act of listening is further delineated into the following two components; a. Attending - Orienting oneself physically to the patient to indicate one is aware of the patient, and, in fact, that the client has your full, undivided attention and that you care .