KUTATHIMINI MBINU ZA USAWIRI WA WAHUSIKA KATIKA RIWAYA YA .

3y ago
678 Views
16 Downloads
562.56 KB
134 Pages
Last View : 17d ago
Last Download : 3m ago
Upload by : Jerry Bolanos
Transcription

KUTATHIMINI MBINU ZA USAWIRI WA WAHUSIKA KATIKA RIWAYA YADUNIA UWANJA WA FUJO NA ASALI CHUNGU: UTAFITI LINGANISHIALI VUAI HAJITASNIFU ILIYOWASILISHWA IKIWA NI SEHEMU YA MASHARTI YAKUTUNUKIWA SHAHADA YA UZAMILI (M.A.KISWAHILI - FASIHI) YACHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA2018

iiUTHIBITISHOAliyeweka saini hapa chini anathibitisha kuwa, ameisoma tasnifu hii yenye mada:Kutathimini Mbinu za Usawiri wa Wahusika katika Riwaya ya Dunia Uwanjawa Fujo na Asali Chungu: Utafiti Linganishi: na kupendekeza ikubaliwe na ChuoKikuu Huria cha Tanzania kwa ajili ya kukamilisha masharti ya kupatiwa shahada yaUzamili ya Sayansi ya jamii katika Kiswahili Fasihi ya Chuo Kikuu Huria chaTanzania. .Profesa Emmanuel D. Y. Mbogo(Msimamizi) . Tarehe

iiiHAKIMILIKITasnifu hii ni mali yangu binafsi, hairuhusiwi kuihifadhi, kuibadili na kuiga kwanamna yoyote, kielektroniki, kirudufu nakala, kwa kupigwa chapa, kuirikodi kwautaratibu wowote ila kwa ruhusa ya mwandishi wake au ruhusa ya Chuo Kikuu Huriacha Tanzania kwa niaba.

ivIKIRARIMimi, Ali Vuai Haji, nathibitisha kuwa tasnifu hii ni kazi yangu binafsi na halisi nakwamba haijawahi kuwasilishwa wala haitawasilishwa, katika Chuo Kikuu kinginechochote kwa ajili ya kutunukiwa shahada ya Uzamili au Shahada nyengine yoyote. . .Saini .Tarehe

vTABARUKUKwa heshima na udhati wa moyo wangu natabaruku tasnifu hii kwa wazazi wanguwapenzi: Mama yangu Subira Omar Makame na marehemu baba yangu Vuai HajiAme kwa juhudi zao za kunizaa, kunilea na kunisomesha bila ya kuchoka hadi sasa.Nawaombea kwa Mwenyezi Mungu awasamehe makosa yenu na awajaalie wawemiongoni mwa waja wa Peponi kwa rehema na mapenzi yake (Amiin).

viSHUKURANINaam, ni dhahiri shahiri anayestahiki kushukuriwa ni Mwenyezi Mungu mtukufu(Subhaanah Wataalahah kwa kuniumba binadamu na kunijaalia uzima, afya,uvumilivu, uwezo, busara na hekima ya kuifanya kazi hii ya utafiti hadikuimaliza.Kwa ufupi nastahiki kusema Alihamdulillah Rabbil Allamiin. NamuombaMwenyezi Mungu (SW) anijaalie ziada za kheri.Shukurani zangu za dhati ziwafikie wazazi wangu wapenzi: Mama yangu SubiraOmar Makame na marehemu baba yangu Bwana Vuai Haji Ame kwa juhudi zao zakunizaa, kunilea na kunisomesha bila ya kuchoka hadi sasa. Nawaombea kwaMwenyezi Mungu (SW) awasamehe makosa yaona awajaalie wawemiongoni mwawaja wa peponi kwa rehema na mapenzi yake ( Amiin).Shukurani zangu zisizo na ukomo zimfikie msimamizi wangu Profesa EmmanuelMbogo, ambaye amekuwa msaada na kiongozi mahiri katika tasnifu hii.ProfesaMbogoamenilea na kuniongoza bila kuchoka kinadharia na kitaaluma hadi kufikiakiwango kizuri,hatua ambayo hapo awali sikuwa nayo. Amekuwa akiisimamia nakufanya kazi hii bila ya kuchoka na kunitia hamasa kubwa niweze kumaliza kazi hiikwa wakati muwafaka; Sinabudi kumuombea kwa Mola amlipe malipo mema(Amiin).Shukurani zangu za pekee ziufikie uongozi mzima wa Chuo Kikuu Huria chaTanzania (OUT) makao makuu Dar es Salaam na tawi lao la Pemba.Kwa heshimakubwa naombakuwashukuru kwakuwataje baadhi ya walimu / wahadhiri chuoni hapo:

viiProfesa James Saleh Mdee, Dkt. Muhamed Omary Maguo, Dkt. Peter Lipembe, Dkt.N. Ligembe, Dkt. Anna Kishe, Dkt. Hadija Jilala, Dkt Zelda Elisifa, Mwalimu BakarKombo, Mwalimu Nassor Ali Suleiman na wengineo. Hawa wote juhudu zao,mwamko, hamasa na maelekezo yao yamekuwa ni dira katika kufanikisha tasnifu hiikwa kiwango kizuri. Mungu awajaalie umri mkubwa wenye mafanikio.Shukurani zangu za ziada zimfikie Mwalimu Bakari Kombo Bakari, Mwalimu MatiAli Matina Mwalimu Sharif Juma Fakih kwani wamekuwa wakinisisitiza kusoma kwabadii bila kukata tamaa.Wengine wanaostahiki kushukuriwa ni walimu na wanafunziwenzangu wote. Naomba niwataje baadhi yao:Mwalimu Hemed Said Massoud, AliSaid Haji, Haji Kh. Mbwana, Mussa Kh.Mussa, Riziki A. Hamad, Zaina O.Othman.Kwa ujumla hawa na wengineo tumeshirikiana vyema na kuelekezana haditukaweza kufanikiwa katika elimu na tasnifu hii.Mwisho na kwa umuhimu mkubwa shukurani zangu za dhati ni kwa familia yangu;mke wangu kipenzi Bimize Hamad Juma pamoja na watoto wangu Sahil,Yahya,Haroun,Yasir,Sabah na Sarah kwa uvumilivu mkubwa waliokuwa nao katikakipindi chote cha masomo hadi sasa. Vile vile napenda niwashukuru viongozi wanguwa kazinikwa kunipa mashirikiano na mapenzi makubwa kwangu ambayo nayoyamenisaidia kufanikisha vyema tasnifu hii.Mungu awape kila lenye kheri naBaraka.Zaidi ya hayo yote naomba radhi kwa wote waliochangia kwa namna yeyotekufanikisha tasnifu hii ambao sikuwataja.Natambua thamani na juhudi zao.Natoashukurani zangu kwenu na M/Mungu (SW) awaelekeze katika kheri na neema.Amiin.

viiiIKISIRILengo la utafiti huu ni Kutathimini Mbinu za Usawiri wa Wahusika katika Riwaya yaDunia uwanja wa fujo na Asali chungu: Utafiti Linganishi. Ili kukamilisha lengohili,utafiti ulikuwa na malengo mahususi matatu ambayo ni; Kuainisha Mbinu zaUsawiri wa Wahusika katika Riwaya ya Dunia Uwanja wa fujo, Kuainisha Mbinu zaUsawiri wa Wahusika katika Riwaya ya Asali chungu na mwisho ni Kulinganisha naKulinganua Mbinu za Usawiri wa Wahusika katika riwaya teule za Dunia Uwanja wafujo na Asali Chungu.Data za utafiti huu zimekusanywa kwa kutumia mbinu zausomaji makini na upitiaji wa nyaraka maktabani. Mkabala wa kimaelezo sambambana Nadharia ya Mwitiko wa Msomaji na Fasihi Linganishi ndizo zilizotumika katikakuchambua data za utafiti. Mtafiti alitumia nadharia hii kwa lengo la kuwasawiriwahusika na alitumia nadharia ya Fasihi Linganishi kwa lengo la kulinganisha nakulinganua mbinu za usawiri wa wahusika katika riwaya hizi mbili. Matokeo ya utafitiyamebaini kuwa mbinu za usawiri wa wahusika ambazo mtafiti amezibaini ni pamojana Mbinu ya Kimaelezi, mbinu ya Uzungumzi nafsi, mbinu ya kidrama, mbinu yakuwatumia wahusika wengine, mbinu ya motifu ya safari, mbinu ya taharuki, nambinu ya majazi au majina.Mtafiti alibaini kuwa riwaya hizi zimetafautiana sanakatika kumsawiri mhusika kwani watunzi wa riwaya hizi wanatoka na wana asili yajamii mbili tofauti na bila shaka hata mitazamo ya dini, hisia zao ni tofauti.Kwamfano Said A.Mohamed ni mwandishi kutoka Zanzibar na ni muumini wa dini yaKiislamu na Kezilahabi ni mwandishi kutoka Tanzania bara, Kisiwa cha Ukerewe nani muumini wa dini ya Kikristo.

ixYALIYOMOUTHIBITISHO . iiHAKIMILIKI . iiiIKIRARI . ivTABARUKU . vSHUKURANI . viIKISIRI . viiiORODHA YA MAJADWELI . xvORODHA YA VIFUPISHO . xviSURA YA KWANZA . 1UTANGULIZI WA JUMLA . 11.1Utangulizi . 11.2Usuli wa Tatizo la Utafiti . 11.3Tamko la Tatizo la Utafiti . 41.4Malengo ya Utafiti . 51.4.1Lengo Kuu la Utafiti . 51.4.2Malengo Mahsusi ya Utafiti . 51.5Maswali ya Utafiti . 51.5.1Umuhimu wa Utafiti . 61.6Vikwazo vya Utafiti na Utatuzi Wake . 61.7Mipaka ya Utafiti . 71.8Mpangilio wa Tasnifu . 91.9Hitimisho . 10

xSURA YA PILI . 11MAPITIO YA KAZI TANGULIZI NA MKABALA WA KINADHARIA. 112.1Utangulizi . 112.2Ufafanuzi wa Istilahi Mbalimbali. 112.2.1Dhana ya Riwaya . 112.2.2Chimbuko la Riwaya na Mapinduzi ya Viwanda . 122.2.2.1Kuzuka kwa Utanzu wa Riwaya Barani Ulaya . 122.2.2.2Historia ya Riwaya Barani Afrika . 132.2.2.2.1 Riwaya Nchini Uganda . 132.2.2.2.2 Riwaya Nchini Kenya . 142.2.2.2.3 Riwaya Nchini Tanzania . 142.2.3Dhana ya Wahusika . 152.2.3.1Aina za Wahusika . 162.2.3.2Uainishaji wa Kwanza wa Wahusika. 162.2.3.3Uainishaji wa Pili wa Wahusika . 182.2.4Dhana ya Usawiri . 192.2.5Usawiri wa Wahusika . 192.2.5.1Mbinu za Usawiri wa Wahusika. 202.2.5.2Mbinu Nyengine za Usawiri wa Wahusika . 232.2.6Maana ya Fujo . 262.3Mapitio ya Kazi Tangulizi . 272.3.1Mapitio ya Kazi Tangulizi Kuhusu Wahusika kwa Ujumla . 282.3.2Mapitio ya Kazi Tangulizi kuhusu Riwaya za Said A.Mohamed . 312.3.3Mapitio ya Kazi Tangulizi Kuhusu Riwaya za E.Kezilahabi . 34

xi2.4Mkabala wa Kinadharia . 352.4.1Nadharia ya Fasihi Linganishi. 362.4.1.1Chimbuko la Nadharia ya Fasihi Linganishi na Waasisi Wake . 382.4.1.2Mihimili/ Misingi ya Nadharia ya Fasihi Linganishi . 412.4.2Pengo la Utafiti . 422.5Nadharia ya Mwitiko wa Msomaji . 432.6Hitimisho . 44SURA YA TATU . 45MBINU ZA UTAFITI . 453.1Utangulizi . 453.2Maana ya Mbinu za Utafiti . 453.3Eneo la Utafiti . 463.4Usanifu wa Utafiti. 463.6Sampuli na Usampulishaji. 473.6.1Maana ya Sampuli . 473.6.2Maana ya Usampulishaji . 483.6.2.1Usampulishaji Lengwa. 483.7Ukusanyaji wa Data . 493.7.1Data za Msingi . 493.7.2Data za Upili. 503.9Mbinu za Kukusanyia Data . 513.9.1.1Upitiaji wa Nyaraka mbalimbali . 523.9.1.2Usomaji Makini wa Matini . 523.12Mbinu za Uchambuzi wa Data . 53

xii3.12.1Mkabala wa Kimaelezo . 533.14Maadili ya Utafiti. 543.15Hitimisho . 55SURA YA NNE . 56UWASILISHAJI NA UCHAMBUZI WA DATA ZA UTAFITI . 564.1Utangulizi . 564.2Usuli wa Mwandishi: Euphrase Kezilahabi . 564.3Muhtasari wa Riwaya ya Dunia Uwanja wa Fujo (1975) . 574.4Usuli wa Mwandishi: Said Ahmed Mohamed . 584.5Muhtasari wa Riwaya ya Asali Chungu. 594.6Mbinu za Usawiri wa Wahusika katika Riwaya ya Dunia Uwanja wa Fujo604.6.1Mbinu ya Kimaelezi / Kisimulizi . 614.6.2Mbinu ya Uzungumzaji Nafsi . 644.4.6.3Mbinu ya Majigambo. 664.6.4Mbinu ya Motifu wa Safari . 674.6.5Mbinu ya Kivisasili. 694.6.6Mbinu ya Kutumia Wahusika Wengine. 694.6.7Mbinu ya Mwingilianomatini. 704.6.8Mbinu ya Kidrama . 744.6.9Mbinu ya Taharuki . 784.7Mbinu za Usawiri wa Wahusika katika Riwaya ya Asali Chungu . 794.7.1Mbinu ya Kimaelezi/Kisimulizi . 804.7.2Mbinu ya Uzungumzi Nafsi . 824.7.3Mbinu ya Majigambo. 85

xiii4.7.4Mbinu ya Motifu wa Safari . 864.7.5Mbinu ya Kuwatumia Wahusika Wengine . 874.7.6Mbinu ya Mwingilianomatini. 884.7.7Mbinu ya Kidrama . 904.7.8Mkondo wa Ung’amuzi au Tayashuri . 934.7.9Mbinu ya Majazi au Matumizi ya Majina. 954.8Kulinganisha na Kulinganua Mbinu za Usawiri wa Wahusika katikaRiwaya ya Dunia Uwanja wa Fujo na Asali Chungu . 984.8.1Kulinganisha (Kufanana) kwa Mbinu za Usawiri wa Wahusika katikaRiwaya ya Dunia Uwanja wa Fujo na Asali Chungu. 984.8.1.1Mbinu ya Kimaelezi . 994.8.1.2Mbinu ya Uzungumzi Nafsi . 1004.8.1.3Mbinu ya Majigambo. 1004.8.1.4Mbinu ya Motifu wa Safari . 1014.8.1.5Mbinu ya Kuwatumia Wahusika Wengine . 1014.8.1.6Mbinu ya Mwingilianomatini. 1024.8.1.7Mbinu ya Kidrama . 1024.9Kulinganua (Tofauti) ya Mbinu za Usawiri wa Wahusika katika Riwaya yaDunia Uwanja wa Fujo na Asali Chungu . 1044.9.1Mbinu ya Taharuki . 1044.9.2Mbinu ya Kivisasili / Kitendi . 1054.9.3Mbinu ya Ulinganuzi na Usambamba . 1054.9.4Mbinu ya Majazi au Matumizi ya Majina. 1064.9Mkondo wa Ung’amuzi Tayashuri . 107

xivSURA YA TANO . 109MUHTASARI, HITIMISHO NA MAPENDEKEZO . 1095.1Utangulizi . 1095.2Muhtasari . 1095.2.1Lengo Muhsusi la Kwanza . 1105.2.2Lengo Mahususi la Pili . 1105.3Hitimisho . 1125.4Mapendekezo. Error! Bookmark not defined.5.4.1Mapendekezo ya Kitaaluma . Error! Bookmark not defined.5.4.2Mapendekezo kwa Serikali kupitia Wizara ya Elimu. 1135.4.3Mapendekezo kwa Watafiti Wengine . 1135.4.4Mapendekezo kwa Wahakiki . 1135.4.5Mapendekezo kwa Jamii . 113MAREJELEO . 115

xvORODHA YA MAJADWELIJadweli Na. 4.1: Muhtasari wa Mbinu za Usawiri wa Wahusika katika Riwaya yaDunia Uwanja wa Fujo .79Jadweli Na.

na Nadharia ya Mwitiko wa M somaji na Fasihi Linganishi ndizo zilizotumika katika kuchambua data za utafiti. Mtafiti alitumia nadharia hii kwa lengo la kuwasawiri wahusika na alitumia nadharia ya Fasihi Linganishi kwa lengo la kulinganisha na kulinganua mbinu za usawiri wa wahusika katika riwaya hizi mbili. Matokeo ya utafiti yamebaini kuwa .

Related Documents:

Mbinu zifuatazo matokeo yake ni ya chini kuliko mbinu zote zilizotajwa mbeleni: Kondomu ya wanaume, kondomu ya wanawake, shanga za mwezi au mzunguko wa shanga, mbinu ya siku mbili. Mbinu hizi nizitumiwe vizuri sana kukuzuiya kupata mimba. Zikitumika kwa uaminifu na vizuri, si lazima kutumia mbinu ya pili. Unapohisi uko katika hatari ya kupata

"Kutathimini Mbinu za Ufutuhi Katika Kuelimisha Jamii Kuhusu Janga la Ukimwi, katika tamthiliya ya Embe Dodo ushuhuda wa mifupa nimeridhika kwamba imefikia kiwango kinachotakiwa na inafaa kuwasilishwa kwa ajili ya Utahini wa Shahada ya Uzamili ya Fasihi kwa Kiswahili ya Chuo Kikuu Huria cha . 4.2.2 Mbinu za Ufutuhi katika Ushuda wa Mifupa .

Lugha huja katika sehemu za maneno Maneno huweza kuvunjwa kuwa silabi Silabi huweza kuvunjwa kuwa sehemu ndogo zaidi zinazoitwa fonimu Baadhi ya mbinu ambazo walimu wanaweza kutumia kuwafundisha watoto dhana kuhusu kusoma na kuandika ni mbinu ya Uzoevu wa Lugha, Kushirik

Katika nchi nyingi za Afrika, "hitaji lisilofikiwa" la upangaji uzazi liko juu. Kwa kweli, chunguzi zinaonyesha kwamba kuna watu zaidi ambao wanaweza kutumia mbinu za kupanga uzazi kama wanaweza kuzipata zaidi ya watu ambao wanazitumia tayari. Kwa maneno mengine, kama aina mbalimbali za mbinu za kupanga uzazi ambazo watu

2015 Mtihani wa Tathmini eneo la Bondo 102/1 Insha Fungua ukurasa 102/1 KISWAHILI Karatasi ya 1 Julai/Agosti - 2015 MUDA: SAA 1 ¾ MTIHANI WA KUTATHIMINI WILAYA YA BONDO - 2015 . Ardhi ndiyo chanzo cha riziki zote. Fauka ya hayo, ardhi ni dafina kubwa. . Fupisha aya ya kwanza kwa maneno 50.

katika tamthiliya za Kinjeketile na Nyerere na Safari ya Kanaani: Utafiti linganishi. Ili kufanikisha utafiti huu, mtafiti ametumia mbinu za maktabani katika kukusanya na kuwasiilisha data kimaelezo. Pia marejeleo mbalimbali kutoka tamthiliya za Kiswahili yalipitiwa. Nadharia ya fasihi ya jamii ndiyo iliyotumika katika

Ufupisho I. Utangulizi II. Sera ya Ujumla III. Mfumo wa Kisheria . Ofisi itatumia mbinu nyeti kuhusu watoto katika nyanja zote za kazi zake zinazohusisha watoto. Mbinu hii huchukulia mtoto kama mtu binafsi na hutambua . waathirika peke yake huenda sambamba na Mkataba wa Roma. 2 Dibaji ya Mkataba, aya. 9. Angalia Mfuko wa Kimataifa wa Watoto .

Russian Origin" 500 AD the Slavic peoples separated into Western, Eastern, and Southern groups Later, on unknown date, the Eastern Slavic language divided into Ukrainian, Byelorussian, and Russian!