UKUFUNZI WENYE NGUVU - WordPress

3y ago
294 Views
10 Downloads
1.39 MB
147 Pages
Last View : 15d ago
Last Download : 3m ago
Upload by : Tripp Mcmullen
Transcription

UKUFUNZI WENYENGUVUMMOJA-KWA-MMOJA

Dynamic Churches InternationalSimeon OyuiP. O. Box 798-00515Bukubura, Nairobi, KenyaEAST AFRICAEmail: ncc africa@yahoo.comDynamic Churches International164 Stonegate CloseAirdrie, Alberta T4B 2V2Canada.E-Mail dcioffice@shaw.caVifungu vya Biblia vilivyonakiliwa katika kitabu hiki vyote ni kutokakwa Biblia Habari Njema toleo la 1995, na ile ya muungano wamashirika 1994, 1952, 1989. 2016 Dynamic Churches International.Haki zote zimehifadhiwa.ii

UKUFUNZI WENYE NGUVUYALIYOMOUkurasa1. Kumjua Kristo kama mwokozi wangu .12. Kujua asili ya Mungu.153. Kuzungumza na Mungu .254. Kumtambua Yesu kama Bwana wangu.415. Kudai Yesu kama uzima wangu.576. Vita vya kiroho .737. Kuishi katika jamii ya kanisa langu .878. Kuwafikia wengine .1019. Mapenzi ya Mungu kuhusu maisha yangu ya usoni .119Wakati Wangu na Mungurecodi ya Kusoma Bibilia .133Fafanua njia ya Maisha Yenye Nguvu . 135Sheria za Ujumla kwa Walimu 137Cheti cha Kuhitimu 143iii

iv

MAELEZO YA SOMO LA KWANZAKwa kukamilisha somo hili la kwanza nita: (Tia alama ya kukamilisha)MATAYARISHO(Hakuna matayarisho muhimu kabla ya mkutano wa somo la kwanza namwanafunzi wako).KUTANA NA MWALIMU 1.Juaneni . Shirikianeni vile mlivyo kuja kumjua Kristo kibinafsi 2.Shiriki sababu na malengo ya Ukufunzi Wenye Nguvu.wa Mmoja-kwa-Mmoja (ona kanuni za kawaida za walimu). 3.Nakili tarehe, wakati na mahali pa ushirika ili muweze kupitiamasomo yote nane. Nakili katika kalenda yako. 4.Pitia orodha ya dibaji na uangalie jinsi kila somo limewezakujengwa na lingine. 5.Onyesha jinsi Ukufunzi Wenye Nguvu unavyo husiana na njiaya maisha yenye nguvu. Mwalimu atakamilisha na aeleze pichailiyo ukurasa wa pili. 6.Pamoja kamilisheni mafunzo yote ya somo la kwanza.Yawezekana msikamilishe katika mkutano mmoja; endeleeni wakatimtakapo kutana tena). Hakikisha kuwa unajua unao uzima wa milele. 7.Endelea kukamilisha somo la pili. Matayarisho ya kila somo lazimauyakamilishe kabla ya kukutana wakati ujao.Tarehe Saa Mahali 8.Funga kwa maombi.1

Jamii2UkufunziUshirikaUtembezi wa WageniMmoja-Kwa-MmojaKundiDogo Kikundi cha UhaiKikundi cha UhaiMisingiKukunzwa kwa KiongoziKundi DogoZingineHudumaKuabudaVijanaMfululizo wa Maishi Yenye NguvuKuingizwa katika huduma

UKUFUNZI WENYENGUVUSomo la kwanzaKUMJUA YESU KAMA MWOKOZI WANGUKumjua Mungu ndilo tendo hasa kamilifu linaloweza kujulikana na mtu.Hebu jaribu kufikiri! Yeye aliye umba mbingu na nchi ametuwezesha tupatekumjua binafsi. Yesu mwenyewe alisema, "Na uzima wa milele ndio huu,wakujue wewe, Mungu wapekee wa kweli na Yesu Kristo. Yohana 17:3.Yawezekana kwamba umempokea Kristo kama mwokozi wako amaunajifunza kueleza wengine jinsi ya kumjua Mungu kibinafsi.Somo hili linaweza kukusaidia kuelewa umuhimuwa uhusiano wako na Mungu. Mungu ni mkuuzaidi ya ufahamu wako, ili hali amechaguakujionyesha binafsi kwetu.Kulingana na Mariko 12:30. Yesu anatuamurisha tumpende Mungu kwanafsi zetu zote.Kujitoa kwa nia yakoKujitoa kwa moyo wakoKujutoa kwa nafsi yakoKujitoa kwa nguvu zakoKwa sababu ya kutii sheria zake, Yesu anasema kwamba “atajidhihirishakwetu". (Yohana 14:21)Kumjua Yesu Kristo ndio ufunguo wa kumjua Mungu.3

1. KUJITOA KWA NIA YAKO - AKILITunastahili kuelewa ukweli kuhusu Yesu Kristo. Yesu Kristo alichukuliwamimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu na kuzaliwa na bikira Mariamukaribu miaka elfu mbili iliopita. Mamia ya miaka kabla, manabii wakuu waIsraeli walitabiri kuja kwake. Agano la kale, iliyoandikwa na watu wengikwa kipindi cha miaka 1,500 lina nakili ya ushahidi 300 kuhusu kuja kwake.MANABII WALITABIRI MAISHA YAKEMipangilio ya Kristo1. Alizaliwa naUnabiiIsaya 7:14UtimilifuMathayo 1:18-252. Mahali pake pakuzaliwaMika 5:2Mathayo 2:13. Aina ya kifo chakeIsaya 53:4,5Mathayo 27:26Zaburi 22:16Luka 23:33Katika umri wa miaka 30 Yesu alianza huduma yake kamili. Kwa miakamitatu alitufunza umuhimu kamili na sababu ya maisha. Maneno yakeyalikuwa kweli kuhusu maisha, uhusiano, fedha, kifo na zinginezo.JE, WALIOMJUA WALIWAZA NINI KUHUSU KRISTO?Binanu yake Yohana mbatizaji. Yohana 1:29-30Mtume Yohana. Yohana 1:1-14Tomaso. Yohana 20:25-28Je, Yesu alimaanisha nini aliposema hivi? Yohana 14:8-114

Je, maadui wa Yesu waliweza kutafsiri vipi kuhusu yale Yesu aliyoyasemakujihusu? Yohana 5:18Kumekuwa na viongozi wengi wakidini katika historia. Yesu alikuwawakipekee na tofauti.Mohammed alikuwa nabii tuBuddha (kwa ufahamisho wake) alikuwa mtu ambaye hakutambuautauaConfucius alikuwa mwalimu wa maadilili tu.Yesu alidai kuwa "Mungu"WEWE KUWA HAKIMUJe, Wafikiri Yesu alimaanisha nini?Yohana 10:30Yohana 14:9Luka 22:70, 71Je, kufufuka kwake kutoka kwa wafu yamaanisha nini kumhusu Yesu?Warumi 1:3, 4Je, wasema Yesu ni nani? Kwa nini?KUELEWA MAKUSUDIO YA KUJA KWAKEJe, kulikuwa na hitaji gani kwamba Yesu Kristo atoke Mbinguni na ajeulimwenguni kufa msalabani? Isaiah 52:2; Yohana 17:3Ni nini iliyo mshawishi kufa? Yohana 3:16Je, ni gharama gani inayostahili kwa dhambi zetu? Warumi 6:235

Kwa sababu ya kifo chake, ni dhawabu ipi anayotupa badala ya kifo(Kutengwa na Mungu)?Je, Yesu alitekeleza nini kwa ajili yetu? 1Petro 1:3, 4naJe, kufufuka kwake kulileta nini kati yetu na Mungu? 1Petro 3:18Soma Waebrania 9:22. Kama Kristo angekufa kwa ajili ya dhambi zetu, je,ingewezekana wewe kusamehewa na Mungu?Kwa nini? / Kwanini hapana?Maisha bilaKristoYesu KristoYako na:DhambiUtengamanoKusumbukaMaisha ndaniya KristoYako na:AmaniMsamahaUzima wa mileleKwa akili yako lazima uelewe ukweli kumuhusu Yesu Kristo na madai yakena kwa imani, uyatambue kwamba ni ya kweli. Yeye hawezi tukupokelewa kama mtu mwema. Anapaswa kukubalika kama yuleMungualiyesema ndiye au akataliwe kama mwongo mkubwa ulimwenguni.2.KUJITOA KWA MOYO WAKO - HISIASote tumeumbwa kwa mfano wake Mungu. (Mwanzo 1:26, 27)Kwa hivyo "tumeumbwa kwa jinsi ya ajabu". (Zaburi 139:14) Kila mtuameumbwa kwa kipekee na hisia tofauti. Utu tofauti na kuishi tofauti. Mtummoja aweza kuwa na hisia zenye nguvu zaidi, hali mwingine yawezekanakuwa mtulivu na mpole. Hisia zako zitatofautiana wakati mwingine nahazipaswi kuzingatiwa mno. Watu wengine wanakosa kuwa na uhusianosawa na Mungu kwa sababu ya kutegemea hisia zao badala ya kile Munguasemacho kwa neno lake.6

Hebu fikiria watu wawili tofauti na jinsi walivyo chukulia maisha yaowalipompokea Kristo.Mtume Paulo. Matendo 22:6-10 Je, ungeeleza vipi kuhusu maisha yake?Je, maisha ya Lidia yalitofautiana vipi na ya Paulo? Matendo 16:14, 15Je, wote walikuwa na maisha makamilifu mbele ya Mungu?Je, umepitia nini kuja kumjua Kristo zaidi kama Paulo ama Lidia?Imani sio Hisia - FunguoWarumi 1:17 "Mwenye haki ataishi kwa imani"Waebrania 11:6 "Lakini pasipo imani haiwezekanikumpendeza Mungu"Warumi 14:23 "Kila tendo lisilo toka katika imani ni dhambi"Hisia yaweza ama yaweza kosa kuambatana na maisha yako ya wokovu.Hisia zinatufautiana na wakati; sio yakutegemewa katika imani. Kilichomuhimu ni, Je waweza kuamini kile ambacho Mungu amesema? Imani kwaMungu inamaanisha kuamini na kusadiki kile anachosema.3.KUJITOA KWA NAFSI YAKO - AKILIKutumia akili nikuchagua utakacho. Chaguo lako litakuwa la sawa kamalitaambatana na neno la Mungu.Soma Yohana 3:36 . Je, changuo la sawa litakuwa lipi?Matokeo yatakuwa gani?Chaguo gani litakalokuwa halifaiNi nini kitakachotokea?7

Je, tunawajibika kutenda nini? 1 Yohana 3:23Tukiamua kutomuamini Kristo, basi kamwe hatutajua mapenzi yake.(1Yohana 7:17)Chagua kuamini ukweli huu!KRISTO AMEKUJA MAISHANI MWAKO.Soma ufunuo 3:20Je, mlango ni nani?Ahadi ya Kristo ni nini?Wajibu wetu ni nini?Wajibu wake ni nini?Kulingana na fungu hili, kama, kwa imani, utafungua mlango wa moyowako na kumkaribisha Yesu Kristo aingie maishani mwako awe Bwanana mwokozi wako, je, ataingia?DHAMBI ZAKO ZILISAMEHEWASoma Wakolosai 2:12-14Ni dhambi ngapi zako zilizosamehewa?Jinsi yakukabiliana na hisia za majuto baada ya kuwa na uhakika kwambaMungu amekusamehe.(a)Tambua yanatoka wapi (Ufunuo 12:10) - Shetani.(b)Dai/Kiri ushindi (Warumi 8:1) hakuna hukumu(c)Ishi kwa imani (1Yohana 1:7) - Tembea katika nuruUnapotenda dhambi, yakupasa kufanya nini? 1Yohana 1:9Hebu tukome sasa na kwa ukimya kukiri dhambi zetu na tudai ahadi yaMungu ya msamaha wa dhambi zote ambazo tunazijua maishani mwetu.8

UMEFANYIKA KUWA MWANA WA MUNGUSoma Yohana 1:12, 13Ni watu gani ambao wamezaliwa kiroho katika jamii ya Mungu?Ulipompekea Kristo, ulifanyika nini?ULIPOKEA UZIMA WA MILELESoma I Yohana 5:11-13Kulingana na fungu hii, ni nani aliye na uzima wa milele? (Fungu la 1112)Kama mtu hajampokea Kristo maishani mwake, je, ni nini lingine anakosa?(Fungu la12)Kulingana na Fungu 13, Je, waweza kujua kana kwamba una uzima wamilele?Je, wajua kwamba una uzima wa milele?Kwa ratibu gani?4. KUJITOA KWA NGUVU ZAKO - MWILIKILE TUNACHOTENDA KAMA WAKRISTO NI MUHIMUSoma Wakolosai 3:9, 10Je, sasa hatupaswi kutenda nini?Yatupasa tuwache nini?9

Tumevaa nini?Je, twauwishwa kwa ufahamu wa umbo la nani?Kama vile buu anavyogeuka kuwa kipepeo na hamu mpya ya maisha mapya pia sisitunageuzwa kutoka kwa "ufalme wa giza kuelekea katika ufalme wa Mwana mpendwa waMungu ". (Wakolosai 1:13, 14). Warumi 12:2 yasema "Wala msimfuatishe namna yadunia hii, bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu". Yatupasa kuishi kama watoto waMungu wenye tamanio mpya na maisha mapya. (1 Yohana 4:17)HUWEZI KUOKOKA KWA SABABU YA MATENDO MEMA!Soma Waefeso 22:8-10Ni kwa ratiba gani ulipokea wokovu? (Fungu la 8)Je, matendo mema yanauhusiano upi na wokovu wako? (Fungu la 9, 10)Kama hauna uhakika na wokovu wako, waweza kumpokea Kristo sasa hivi kwa chaguolako?Hapa kuna ombi la kuomba.Bwana Yesu, mimi ni mwenye Dhambi na siwezi kujiokoa mwenyewe. Nakushukurukwa kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zangu. Sasa ninakukaribisha maishanimwangu na kukupokea kama Mwokozi na Bwana wangu. Asante kwa kusameheDhambi zangu na kunipatia uzima wa milele. Sasa ninakupatia usukani wa maishayangu na kukuamini kuishi "Maisha yako ya milele" kunipitia mimi kamaupendavyo.Kama umemkaribisha Kristo maishani mwako, sasa au mbeleni, yuko wapi sasa katikaushirika nawe?Ufunuo 3:20Ni kwa mamlaka yapi unajua?USHAHIDI WA KUMJUA YESU KAMA MWOKOZI WANGUMarko 12:30 yasema "Nawe umpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, nakwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote".Tumetazama sehemu yetu, ambavyo ni kujitoa kabisa kwa utu wetu kwakujitoa kwake katika ukamilifu kwetu. Tutokapo nje kwa imani Mungu anahahikisha kwamba tumezaliwa kiroho.10

USHAHIDI WA NENO LA MUNGUTunapokamilisha matarajio ya Mungu yanavyofunuliwa kwa neno lakeutajua kwamba umtoto wa Mungu.1Yohana 5:13 yasema; utajua kwamba una uzima wa milele.USHAHIDI WA ROHO MTAKATIFU.Warumi 8:16 yasema; Roho Mtakatifu anatueleza sisi ni watoto wa Mungu.USHAHIDI WA UPENDO WETU1Yohana 4:7, 8 na I Yohana 3:14 yasema; kwamba tutajua tumepita kutokakwa mauti hadi uzima tunapopenda Wakristo wengine.USHAHIDI WA MAISHA YALIYO BADILIKA.Soma 1Yohana 2:3-6Tunapotii amri zake, inaonyesha nini? (Fungu la 3)Tunapotii neno lake matokeo yatakuwa yapi? (Fungu la 5)Tutajuaje kwamba tuko ndani yake? (Fungu la 5, 6)11

MAWAIDHAISHI KATIKA UJASIRI WA UHUSIANO WAKO NA KRISTO!Wiki hii nakili ushahidi/mabadiliko yako ya kumjua Kristo kama Mwokozi.Nakili hasa mifano katika.1.Upendo wako kwa Wakristo wengine.2.Mabadiliko maishani mwangu.12

MAFUNZO ZAIDI KATIKA SOMO HILINDANI YA KRISTO MIMI .20.21.22.23.Mtoto wa Mungu kwa sababu nimezaliwa mara ya pili. 1 Petro 1:23Nimesamehewa dhambi zangu zote. Waefeso 1:7; Waebrania 9:14Wakolosai 1:14; 1 Yohana 1:9, 2:12Mimi ni kiumbe kipya. 2Wakorintho 5:17Mimi ni hekalu la Roho Mtakatifu. 2 Wakorintho 6:19Nimekombolewa na laana ya sheria. 1 Petro 1:18, 19; Wagalatia 3:13Nimebarikiwa. Kumbukumbu la torati. 28:1-4; Wagalatia 3:9Mimi ni Mtakatifu. Warumi 1:7; 1 Wakorintho 1:2; Wafilipi 1:1Mtakatifu na asiye na hatia mbele zake. 1Petro 1:16, Waefeso 1:4Nimechaguliwa. Wakolosai 3:12; Warumi 8:33Nimetiwa nguvu hadi mwisho. 1Wakorintho 1:8Nimeletwa karibu kupitia damu ya Kristo. Waefeso 2:13Mimi ni mridhi pamoja na Kristo. Warumi 8:17Nimetiwa muhuri na Roho Mtakatifu wa ahadi. Warumi 8:17Ndani ya Kristo kwa kazi yake. 1 Wakorintho 1:30Nimekubaliwa na wapendwa. Waefeso 1:6Nimekamilika ndani yake. Wakolosai 2:10Nimepatanishwa na Mungu. 2 Wakorintho 5:18Nimeitwa kwa Mungu. 2 Timotheo 1:9Limbuko la viumbe vyake. Yakobo 1:18Tumechaguliwa. 1Wathesalonike 1:4; Waefeso 1:4; 1Petro 2:9Kwa mapigo yake Yesu tumepona. 1Petro 2:24; Isaiah 53:5Tunapendwa na Mungu. Wakolosai 3:12; Warumi 1:7;Tumefichwa na Kristo ndani ya Mungu. Wakolosai 3:3NIMEPOKEA24. Nimepokea Uridhi. Waefeso 1:1125. Nimepata kumkaribisha Baba kwa Roho Moja. Waefeso 2:18.13

14

MAMBO YA KUTIMIZA KWA SOMO LA PILIKukamilisha somo hili nita: (tia alama ya kukamilisha)MAANDALIZI 1. Tayarisha kunakili kutoka kwa ufahamu wako. Yohana 3:16 2. Soma Zaburi 23 3. Nakili chini mafundisho ya mchungaji. Ukitumia“maandalizi ya ujumbe”. 4. Kamilisha matayarisho yote katika somo la pili, "Kujua asiliya Mungu."IKAMILISHE NA MWALIMU (KIONGOZI) 1. Kwa ufupi eleza maelezo muhimu katika somo la Kwanza.Jadilianeni mambo ya kutenda. 2. Nakili kutoka kwa akili yako Yohana 3:16. 3. Kagua kwa kusoma Zaburi 23. 4. Jadilianeni mafundisho yaliyo nakiliwa katika funzo lamchungaji. 5. Nakili somo la pili. Ukitilia mkazo ukuu wa Mungu wetu. 6. Rudia "Mambo ya kutimiza kwa somo la tatu" "maandalizi "ya somo yastahili kukamilishwa kabla ya mkutano ujao.Tarehe Wakati Mahali 7. Funga kwa maombi.15

16

UKUFUNZI WENYENGUVUSomo la PiliKUJUA ASILI YA MUNGU.Ukweli wa ajabu umepewa kwetu katika Danieli 11:32b. “Lakini watuwamjuao Mungu wao watakuwa hodari na kutenda mambo makuu !”Sote twapenda kuishi maisha yaliyo na mazao na yenye nguvu katika tabia.Kwa hivyo, yatupasa, "Kumjua Mungu wetu". Kutomjua Mungu ni kuishimaisha kama kipofu, asiye na mwelekeo wa kule aendako na kukosaufahamu wa kile kinacho endelea miongoni mwetu.Katika somo hili, tutaangalia asili ya Mungu na kutambua kinacho mtengayeye kando na tofauti nasi. Kumuelewa Mungu kutatusaidia kuelewa maanaya maisha yetu ya kila sikuJE, WAMJUA MUNGU KIASI GANI?Je, wang’ang’ana na mambo ya maisha ama waishi kwa ujasiri kuwaMungu ameshikilia usukani? Hautakuwa wa kawaida utakapoanza kuishikatika nuru ya yale utakayojifunza kuhusu Mungu wako. Wale ambaowameweza kuishi maisha ya ushindi kupitia wakati mgumu wao ni zaidi yawashindi, kwa sababu wamemjua Mungu wao, wameelewa ukuu wake nawakatii.Kila utu wa uungu - Baba, Mwana na Roho Mtakatifu wanafanana katikahali na asili.Uasili wa mungu unaweza kuonekana kwa njia mbili:1.TABIA ZINAZO NA UKWELI UNAOMUHUSU MUNGU.NI MKUUNI WA MILELEMWENYE NGUVU ANAJUA KILA KITUHABADILIKIYUKO KILA MAHALI2.TABIA ZINAZODHIHIRISHA MUNGUANAPOLINGANISHA NA VIUMBE VYAKE.UTAKATIFUHAKIKUTOBAGUA17UPENDO

Soma vifungu vifuatavyo kisha unakili alama muhimu utakayojifunzakuhusu kila asili ya uungu. Eleza vile utakavyoishi kulingana na kileulichofahamu kumuhusu Mungu.1.TABIA ZINAZO MUHUSU MUNGU.NI MKUU - Mungu ni kiongozi mkuu juu ya viumbe vyake vyote.Biblia inasema.Zaburi 103:19Warumi 9:20,21Yamaanisha: Vitu vyote viko mikononi mwake. Mungu hutendaapendavyo na nguvu zake mbinguni na watu wake duniani. Hatuwezikumsimamisha wala kuwa na mamlaka ya kumuuliza maswali. (Danieli 4:35na Isaya 55:8, 9)Mungu ananifunza mimiNIWA MILELE Mungu alikuwa wa milele na atakuwa wamilele siku zote.Biblia yaeleza:Isaya 44:6Ufunuo 1:81Timotheo 1:17Yamaanisha: Kwa kuwa Mungu ni Mungu, njia zake, asili yake, na vitendovyake viko juu ya Ufahamu wetu. Maelezo yote ya kuishi kwake yako ndaniyake. Mungu hana vipimo au mipaka ya aina yeyote katika asili yake auUfalme wake.18

Mungu ananifunza mimiHABADILIKI - Asili ya Mungu haibadiliki, hali yake na mapenzi yake.Yeye hana sababu ya kubadilika, na hawezi kamwe kubadilishwa.Bibilia yatueleza:Zaburi 102:25-27Waebrania 13:8Yamaanisha: Mapenzi ya Mungu kamwe hayatabadilika. Mapenzi yake nikuwabariki watu wake na kuwavuta watu wote kwake. Twawezakumuamini yeye kulitimiza neno lake tunapotii kanuni zake.Mungu ananifunza mimiNI MUWEZA YOTE - Mungu anazo nguvu zote. Anaweza kutenda vyotena chochote kulingana na mapenzi yake.Biblia yatueleza:Ayubu 42:2Waefeso 3:20Yamaanisha: Nguvu za Mungu zinaonyeshwa kwa;1.2.3.4.Kuumba Mbingu na Dunia (Mwanzo 1:1)Kutunza vitu vyote (Waebrania 1:3)Kutoa wokovu (Warumi 1:16)Kutujali sisi (I Petro 5:6, 7)19

Mungu ananifunza mimiANAJUA VYOTE - Mungu nimkamilifu na ana ufahamu kamili kuhusu kilekilicho pita, sasa na usoni.Biblia yatueleza:Zaburi 139:1-6Waebrania 4:13Yamaanisha: Mungu anajua mawazo yetu, hisia zetu, tamanio zetu, na sirizetu. Hakuna kinacho mpata Mungu kwa ghafla. Kwa mfano, Mungualipokukubali kama mwanawe na akakupa uzima wa milele alikuwa naufahamu kamili wa jinsi utakavyo kuwa na utakayoyatenda.Mungu ananifunza mimiYUKO KILA MAHALI - Mungu yuko kila mahali ulimwenguni wakatiwote katika asili yake kamilifu.Bibilia yaeleza:Methali 15:3Yeremia 23:23, 24Yamaanisha: Kwa wakati wa hitaji, tunahakika kua Mungu yuko karibunasi sana hata ijapokua hatumuhisi. Hatuwezi kujificha kutokana na Mungu.Anajua kamili yanayotendeka katika mataifa, katika kanisa na maishanimwetu binafsi.20

Mungu ananifunza mimi2. TABIA ZINAZOMFUNUA MUNGU ANAVYOSHIRIKI NAVIUMBE VYAKE.MTAKATIFU. Tabia ya Mungu ni kamilifu na safi kabisa katika asili yautu.Biblia inasema:Ayubu 34:10Isaya 57:15I Petro 1:14-16Yamaanisha: Mungu ni Mtakatifu kabisa katika kila wazo na kitendo. IPetro 1:16 yasema, “mtakuwa watakatifu kwa maana mimi ni mtakatifu"Haya yanawezekana tu ninapo mruhusu Roho Mtakatifu aishi ndani yanguapendavyo.Mungu ananifunza mimiNI MWENYE HAKI - Mungu kila wakati hutenda yaliyo ya sawa. Kwamaana yeye ni Mungu. Chochote atendacho ni chema kabisa kwa kuwa yeyeni ukweli mtupu. Matendo yake yanasukumwa na upendo wake.Biblia inasema:Kumbukumbu la Torati 32:3, 4Warumi 8:28Yamaanisha: Mawazo ya Mungu kamwe ni mema. Anapo tupatiamwelekeo maishani mwetu, twaweza kuhakikisha kwamba ni ya kweli na21

sawa, hata kama yanaonekana kinyume cha mapenzi yetu na hekima yetu.Mungu ananifunza mimiHABAGUI - Mungu hana ubaguzi na ni mwenye haki katika matendo yake.Katika uamuzi wake (mwamuzi wa haki). Yeye hutunuku haki nakuhukumu dhambi.Biblia yaeleza:Nehemiah 9:13- 332 Wathesalonike 1:3-10Yamaanisha: Mungu, aliye hakimu wa wote, atahakikisha kwamba hakiyote imetimizwa. Hii ni ya kuwapa moyo wale ambao wanagandamizwakatika maisha haya. Na ni onyo kwa wale watendao maovu. Munguhuchukia uovu na atawaadhibu watendao maovu. Mungu anatuuliza tuishimaisha ya sawa yenye haki na ametuwezesha sisi kupokea haki yake kupitiakifo cha Yesu Kristo. (2 Wakorintho 5:21)Mungu ananifunza mimiUPENDO - Mungu ni mkamilifu na mwenye upendo wa milele. Yeye hutoaupendo wake bure na bila kuangalia wema wa yule ampendae. Tendo kuu laupendo lililo onyeshwa na Mungu kwetu sisi ni kumtuma Yesu afe kwa ajiliya dhambi zetu. (Warumi 5:8)22

Biblia inasema:Yohana 3:16Warumi 8:37-39Yamaanisha: Upendo wa Mungu hauna mpaka. Upendo wake haubadiliki,yeye hutupenda kikamilifu. Na ameweka upendo wake ndani yetu.(Warumi 5:5) Yesu Kristo yuaishi ndani yetu na anatuwezesha sisi kupendawenzetu kama vile atupendavyo sisi.(1Yohana 4:7)Mungu ananifunza mimiJINSI YA KUTENDA KAZIWAJIBU WANGUSasa rudia somo hili. Chagua kitu kimoja maishani mwako ambachoungependa kuishi tofauti katika nuru ya ufahamu wa Mungu wako.Juma hili nitaKumbuka "Lakini watu wamjuao Mungu wao watakuwa hodari nakutenda makuu" (Danieli 11:

Maisha ndani ya Kristo Yako na: Dhambi Utengamano Kusumbuka Yako na: Amani Uzima wa milele Yesu Kristo. 7 . Kama vile buu anavyogeuka kuwa kipepeo na hamu mpya ya maisha mapya pia sisi tunageuzwa kutoka kwa "ufalme wa giza kuelekea katika ufalme wa Mwana mpendwa wa Mungu ". (Wakolosai 1:13, 14).

Related Documents:

1. maisha mapya katika kristo 1 2. maisha mapya katika ushindi 5 3. maisha mapya yenye uweza 9 4. maisha mapya yenye usawa 13 5. ukufunzi wenye nguvu - nafasi nzuri 17 6. misingi yenye nguvu taratibu ya viongozi 19 7. cheti cha kuhitimu ukurasa wa nyuma

Yesu aliwaacha waamini na utume mkuu wa kuufikia ulimwengu kwa Injili ya Ufalme. Kazi hii haitakamilishwa kwa maneno pekee. Kama katika kanisa la kwanza, lazima pia kuwe na . Hizi zote ni nguvu kubwa zinazofanya kazi katika ulimwengu wetu wa leo. Lakini mwito kutoka kwa Yesu sio kwa mamlaka ya kidunia. Ni kwa nguvu za kiroho. Ni nguvu ambayo .

1.1.3 WordPress.com dan WordPress.org WordPress menyediakan dua alamat yang berbeda, yaitu WordPress.com dan WordPress.org. WordPress.com merupakan situs layanan blog yang menggunakan mesin WordPress, didirikan oleh perusahaan Automattic. Dengan mendaftar pada situs WordPress.com, pengguna tidak perlu melakukan instalasi atau

WordPress Themes WordPress Premium Themes WordPress Free Themes WordPress Plugins ite Templates WordPress Hosting WordPress.com CreativeMarket.com . with crowdfunding b Astoundif plugin and fundif theme. Plugin will empower o

Lesson 2. Install Wordpress On Your Domain Lesson 3. How To Log In And Out Of Wordpress Lesson 4. The Design Of Your Wordpress Website Lesson 5. First Steps To A Perfect Website Lesson 6. Add Your First Wordpress Page Lesson 7. Add Your First Wordpress Post Lesson 8. All About Widgets IN-DEPTH GUIDE - DRILL DOWN TO THE WONDERS OF WORDPRESS .

waliojitolea kwa mwito mkuu wa Bwana wetu Yesu Kristo, na wamejitoa mhanga kuhakikisha kwamba wanashiriki kuwafanya wengineo hadi kila mmoja kote ulimwenguni atakapomjua Mungu kibinafsi. SHUKURANI Nakala hii imetayarishwa ili kueleza mafunzo kamili jinsi wakriso wachanga wanavyoweza kukomaa katika mwenendo wao na Mungu na kuweza kusaidia wengine.

Mwito Mkuu "Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote . Mafundisho yaliyobaki yameundwa kuwapa viongozi wetu wa kanisa maarifa rahisi yenye nguvu yawezayo kufanya kanisa lenye kufanya wanafunzi. Mwito mkuu unahusu idadi ya watu ulimwenguni kote. Yaweza kutimizwa na Roho wa

CHATEAUBRIAND, ATALA : « Les funérailles d’Atala » (XIX e s) Nous convînmes que nous partirions le lendemain au lever du soleil pour enterrer Atala sous l’arche du pont naturel, à l’entrée des Bocages de la mort. Il fut aussi résolu que nous passerions la nuit en prière auprès du corps de cette sainte.