KUCHUNGUZA UFASIHI SIMULIZI UNAOJITOKEZA NDANI YA HADITHI .

3y ago
224 Views
3 Downloads
777.91 KB
124 Pages
Last View : 14d ago
Last Download : 3m ago
Upload by : Braxton Mach
Transcription

KUCHUNGUZA UFASIHI SIMULIZI UNAOJITOKEZA NDANI YA HADITHIZA KUSADIKIKA NA ADILI NA NDUGUZEMUHAMMED ALI SALIMTASINIFU ILIYOWASILISHWA KWA AJILI YA KUTIMIZA SEHEMU YAMASHARTI YA KUTUNIKIWA SHAHADA YA UZAMILI YA CHUO KIKUUHURIA CHA TANZANIA2015

iiUTHIBITSHOWalioweka saini hapa chini wanathibitisha kuwa, wameisoma Tasnifu hii iitwayo:Kuchunguza Ufasihi Simulizi unaojitokeza Ndani ya Hadithi za Kusadikika na Adili naNduguze, na kupendekeza ikubaliwe na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kwa ajili yakukamilisha masharti ya kupatiwa Digrii ya Uzamili M.A (Kiswahili) ya Chuo KikuuHuria cha Tanzania.Mohamed Omary Maguo(Msimamizi)Tarehe

iiiHAKI MILIKITasnifu hii ni mali yangu binafsi, hairuhusiwi kuihifadhi na kuibadili kwa namnayoyote, kielektroniki, kimekanika, kwa kupigwa picha, kuirekodi kwa utaratibu wowoteila kwa ruhusa ya mwandishi wake au ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

ivTAMKOMimi, Muhammed Ali Salim nathibitisha kwamba, hii ni kazi niliyoifanya mimimwenyewe na kwamba haijawahi kuwasilishwa katika chuo kikuu chochote kinginekabla kwa minajili kutunukiwa shahada nyingine yoyote ile.SignatureDate

vTABARUKUNaitabaruku kazi hii kwa wazazi wangu wapenzi, Ali Salim Rashid na Fatma SalimJuma wa Mibrani Chake Chake - Pemba.

viSHUKURANIKwanza kabisa, kabla sijasema neono lolote, ninapenda nitoe shukurani zangu zisizo naukomo kwa ALLAH SUBHANAHU WATAALAH kwa kunijaalia afya njema katikakipindi chote cha masomo yangu, kunipa nguvu, uwezo, akili, busara na maarifa katikamuda wote wa masomo yangu ya Uzamili. Ninasema, kwa unyenyekevu, AlhamdulillahRabbillaalamina.Pili, napenda kuwashukuru kwa dhati wasimamizi wangu Prof. Sengo na Dktr.Mohamed Omary Maguo kwa kunilea kitaaluma na kunikuza katika misingi ya nadhariana vitendo katika fasihi ya Kiswahili. Sina neno ila kuwaombea duwa ya kheri.Tatu, ninawashukuru sana wazazi wangu, kwa kunizaa, kunilea, kunisomesha nakunifunza maisha ya dunia na Akhera. Vile vile, shukurani za pekee ni za mke wangukipenzi, Salma Othman Suleiman na watoto wangu Abdul-Aziz Muhammed, RaifaMuhammed, Sumaiya Muhammed, Mudrik Muhammed, Mukrim Muhammed, Mukhtar Muhammed, Mudathir Muhammed na Ulfat Muhammedkwa uvumilivu wao,huruma na kunitia moyo katika kuendeleza masomo yangu. Nne, ninapendakuwashukuru wafuatao; Prof. E. Mbogo, na Bw. Bakar Kombo Bakar kwa msaada waowa ushauri kimasomo. Mwisho ninawashukuru ndugu zangu na wanachuo wenzanguwote, walioshiriki moja kwa moja na kwa namna yoyote nyingine, katika kuikamilishakazi hii.

viiIKISIRILengo la utafiti huu ni kuchunguza Ufasihi Simulizi unaojitokeza katika hadithi za Adilina Nduguze na Kusadikika za Shaaban Robert. Ili kukamilisha lengo hili, utafiti ulikuwana malengo mahususi matatu ambayo ni; kufafanua vipengele vya fasihi simulizivinavyojitokeza ndani ya hadithi za Kusadikika na Adili na Nduguze, kujadili mbinuzilizotumika katika kuhifadhi ufasihi simulizi uliomo ndani ya kazi husika, na kuelezeadhamira zinazojitokeza ndani ya hadithi za Kusadikika na Adili na Nduguze. Data zautafiti huu zimekusanywa kwa kutumia mbinu za usomaji makini na upitiaji wa nyarakamaktabani. Mkabala wa kimaelezo sambamba na nadharia za Mwitiko wa Msomaji naUjumi ndizo zilizotumika katika kuchambua data za utafiti.Matokeo ya utafitiyamebaini kuwa fani za fasihi simulizi kama vile methali, misemo, hadithi ndani yahadithi, nyimbo na masimulizi zimejitokeza kwa kiasi kikubwa katika kazi teule zaShaaban Robert. Vile vile, matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa mbinu za kisanaa kamavile; muundo, mtindo, wahusika, mandhari na matumizi ya lugha zimetumika katikakuhifadhi ufasihi simulizi katika riwaya husika. Pia, matokeo ya utafiti yamegunduakuwa, katika kazi hizo kunajitokeza dhamira kama vile; umuhimu wa elimu, kilimo,uongozi bora, umuhimu wa sheria, mapenzi, choyo na husda, ndoa, malezi na kodi.Kwa ujumla, utafiti huu umegundua kuwa fasihi ni moja tu. Maandishi au Masimulizi ninamna za uwasilishaji wa fasihi ya Kiswahili na nyinginezo duniani. Aidha, utafitiumegundua kuwa, Fasihi ya Maandishi hutumia vipengele vile vile vya Fasihi yaMasimulizi ili kufikisha ujumbe kwa jamii. Hivyo, mpaka uliopo ni namna yauwasilishaji wa kazi hizo.

viiiYALIYOMOUTHIBITSHO . iiHAKI MILIKI . iiiTAMKO . ivTABARUKU . vSHUKURANI . viIKISIRI . .viiYALIYOMO . viiiORODHA YA MAJEDWALI. xiiSURA YA KWANZA . 1UTANGULIZI WA JUMLA . 11.1Utangulizi . 11.2Usuli wa Tatizo la Utafiti . 31.3Tatizo la Utafiti . 41.4Madhumuni ya Utafiti . 51.4.1Lengo kuu la Utafiti . 51.4.2Madhumuni Mahususi ya Utafiti . 51.4.3Maswali ya Utafiti . 61.5Umuhimu wa Utafiti . 61.6Mipaka ya Utafiti . 61.7Vikwazo vya Utafiti. 71.7.1Utatuzi wa Vikwazo . 7SURA YA PILI . . 8MAPITIO YA KAZI TANGULIZI NA MKABALA WA KINADHARIA . 82.0Utangulizi . 82.1Dhana ya Fasihi Simulizi . 8

ix2.2Tanzu za Fasihi Simulizi . 142.2.1Semi . 142.2.2Mazungumzo . 142.2.3Masimulizi . 152.2.4Maigizo . 152.2.5Ushairi Simulizi . 162.2.6Ngomezi . 172.3Dhamira . 172.4Kazi Tangulizi kuhusu Riwaya za Shaaban Robert. 182.5Mkabala wa Kinadharia . 212.5.1Nadharia ya Mwitiko wa Msomaji . 212.5.2Nadharia ya Ujumi wa Mwafrika . 222.6Hitimisho . 23SURA YA TATU . . 24MBINU ZA UTAFITI . 243.0Utangulizi . . 243.1Umbo la Utafiti . 243.2Eneo la Utafiti . 253.3Data za Utafiti Zilizokusanywa . 253.3.1Data za Msingi . 253.3.2Data za Upili . 263.4Mbinu za Kukusanya Data . 263.4.1Upitiaji wa Nyaraka . 263.3.1Usomaji Makini . 273.4Uteuzi wa Watafitiwa . 283.5Wateuliwa . 29

x3.6Mkabala wa Uchambuzi wa Data za Utafiti . 293.7Hitimisho . . 29SURA YA NNE . 31UWASILISHAJI, UCHAMBUZI NA MJADALA WA DATA ZA UTAFITI . 314.0Utangulizi . 314.1Vipengele vya Fasihi Simulizi katika Kusadikika na Adili na Nduguze . 314.1.1Methali katika Kusadikika na Adili na Nduguze. 324.1.2Misemo katika Kusadikika na Adili na Nduguze . 364.1.3Nyimbo,,,,,,,,,,,, . 404.1.4Hadithi Ndani ya Hadithi . 424.1.5Hadithi Simulizi . 464.2Vipengele vilivyotumika kuhifadhi Ufasihi Simulizi ndaniKusadikika na Adili na Nduguze . 494.2.1Muundo,,,,,,,,,, . 504.2.2Mtindo . 564.2.2.1 Mtindo wa Barua . 574.2.2.2 Motifu za Safari za Kisimulizi. 584.2.2.3 Mtindo wa Masimulizi. 614.2.2.4 Mtindo wa Nyimbo . 644.2.2.5 Matumizi ya Korasi . 644.2.2.6 Matumizi ya Vilio na Vicheko . 674.2.3Wahusika wa Kisimulizi. 694.2.4Mandhari ya Kisimulizi . 774.3Dhamira katika Kusadikika na Adili na Nduguze . 824.3.1.1 Dhamira ya Umuhimu wa Elimu . 834.3.1.2 Dhamira ya Choyo . 84

xi4.3.1.3 Umuhimu wa Sheria . 854.3.1.4 Umuhimu wa Kilimo . 874.3.1.5 Dhamira ya Ukombozi. 884.3.1.6 Ubadhirifu wa Mali za Umma . 904.3.1.9 Malezi Mazuri ya Watoto . 934.3.1.10 Dhamira ya Israfu . 944.3.2Dhamira katika Adili na Nduguze . 954.3.2.1 Dhamira ya Wivu na Husda. 954.6.2Dhamira ya Ndoa . 964.6.3Dhamira ya Mapenzi . 974.6.4Dhamira ya Ujasiri. 984.6.5Dhamira ya Ukweli . 994.6.6Dhamira ya Uongozi Bora . 1004.6.7Dhamira ya Kodi . 100SURA YA TANO . 102MUHTASARI, HITIMISHO NA MAPENDEKEZO . 1025.0Utangulizi . 1025.1Muhtasari . 1025.1.1Dhumuni Mahususi la Kwanza. 1035.1.2Dhumuni Mahususi la pili . 1035.1.3Dhumuni Mahususi la Tatu . 1055.2Hitimisho . 1055.3Mapendekezo . 1065.3.1Kwa Watunga Mitaala . 1065.3.2Kwa Wahadhiri na Walimu . 1065.3.3Kwa Wachapishaji . 106

xii5.3.4Kwa Watafiti. 1075.3.5Kwa Watunzi . 1072.3.6Kwa Wahakiki . 107MAREJELEO . 108ORODHA YA MAJEDWALIJedwali 1 : Fani za Fasihi Simulizi katika Kusadikika na Adili na Nduguze . 32Jedwali 2 : Fani katikaAdili na Nduguze na Kusadikika . 49Jedwali 3 : Mtindo katika Kusadikika na Adili na Nduguze . 56Jedwali 4 : Dhamira katika Kusadikika . 83

xiii

1SURA YA KWANZAUTANGULIZI WA JUMLA1.1UtanguliziUtafiti huu unahusu kuchunguza ufasihi Simulizi unaojitokeza ndani ya kazi zaShaabani Robert za Kusadikika na Adili na Nduguze. Utafiti una sura tano; Sura yakwanza, inaelezea mambo ya msingi kuhusu mada, tatizo la utafiti, madhumuni yautafiti, maswali ya utafiti, umuhimu wa utafiti, vikwazo vya utafiti na namna vikwazohivyo vilivyotatuliwa. Aidha, sura ya pili imeelezea kazi zilizosomwa na mtafiti,zinazohusiana na mada iliyotafitiwa. Pia, sehemu hiyo imeelezea nadhariazilizomuongoza mtafiti katika utafiti huu. Sura ya tatu imeelezea mbinu zilizotumikakukusanyia data na kuzichambua, mbinu hizo ni pamoja na mbinu za maktabani, uteuzilengwa, kazi zilizoteuliwa ambazo ni hadithi za Kusadikika na Adili na Nduguze. Aidha,imeelezwa kwamba, data za utafiti huu, ziliwasilishwa kwa majadweli nazilichambuliwa kwa njia ya maelezo. Sura ya nne imeshughulikia uchambuzi wa datazilizokusanywa na mtafiti. Sura ya tano inaelezea matokeo ya utafiti, ambapo suraimetathmini madhumuni mahususi ya utafiti huu na kumalizia kwa kutoa mapendekezo.Mulokozi (1996) anaeleza kwamba kabla ya Afrika Mashariki kuingiliwa na wageni,fasihi kama fasihi nyengine za jamii ya Kiafrika, ilikuwa ni ya masimulizi kwa njia yamdomo bila kuandikwa. Fasihi hiyo, ya masimulizi ilikuwa na tanzu kama vile, ngano,methali, vitendawili, nyimbo nakadhalika. Wahusika katika tanzu hizi walikuwawanyama, mizimu, mashetani, majini na hata binaadamu, lakini tabia zao ziliwakilishatabia za binaadamu. Kwa upande wa hadithi, hadithi za kigeni kama za Kiarabu naKiajemi zilianza kutafsiriwa na kuingizwa katika Fasihi ya Kiswahili.

2Aidha, Mulokozi (ameshatajwa), anaeleza kuwa Fasihi ya Kiswahli ilianza kuandikwakwa kutumia hati ya Kiarabu na baadae Kilatini. Hati hizo zilifungua fasihi ya Kiswahiliikaingizwa na Waafrika wenyewe katika maandishi. Mathalan, utanzu wa Riwayaulianza kushughulikiwa kwa kuingizwa katika maandishi wakati wa Mwingereza.Wazungu waliwashawishi Waafrika kuanza kuandika hadithi zao. Walifanya hivi kwakutumia halmashauri ya kusanifisha lugha, mnamo 1930, ambayo iliandaa mashindanoya waandishi wa Kiafrika. Mashindano hayo yalizua waandishi kama vile JamesMbotela, Shaaban Robert, M.S. Jemedaar nakadhalika. Kazi za waandishi hao ni kamavile; Uhuru wa Watumwa, Adili na Nduguze, Kurwa na Doto, Mzimu wa Watu wa Kale,Nahodha Fikirini mutawalia.Aidha, Mulokozi (ameshatajwa), anaeleza kwamba miaka thelathini baadae, baada yariwaya ya kwanza ya, ilitawaliwa na kazi za Shaaban Robert na riwaya yake ya kwanza,Utu bora Mkulima, yasemekana ilitungwa mwaka 1946, lakini haikuchapishwa hadimwaka 1968. Kazi iliyofuata ilikuwa ni Kufikirika, iliyoandikwa mwaka 1947, nakuchapshwa 1967. Kazi ya tatu ilikuwa hadithi ndefu ya Kusadikika, ilichapishwamwaka 1951 na ya nne Adili na Nduguze, ilichapishwa mwaka 1952. Hadithi ndefuyake ya mwisho ni Siku ya Watenzi Wote, iliandikwa kama 1960-62 na kuchapishwamwaka 1968. Karibu riwaya zote za Shaaban Robert ziliathiriwa sana na ngano nahekaya, hasa katika muundo wake na uchoraji wa wahusika.Pamoja na kwamba kazi hizi ni miongoni mwa kazi za mwanzo mwanzo za Fasihi yaMaand

Mathalan, chimbuko la hadithi za fasihi ya Kiswahili linatokana na chimbuko la ngano za Kiswahili (Kenguru, 2013). Baada ya wageni wa Kimagharibi kuingia Afrka mashariki, hasa Wamishionari, ngano kadhaa wa kadhaa zilifasiriwa na kuwa ndio msingi wa hadithi ndefu za Kiswahili. Baina ya mwaka 1940 na kuendelea hadi miaka ya 1960, hadithi ndefu nyingi za Kiswahili zilifuata mkondo wa ngano za .

Related Documents:

mawazo ya wanamsambao hususani katika ugawaji wa ngano bila kuchunguza kwa umakini sifa ya kila kundi. Propp anaamini kuwa ili kuchunguza asili ya ngano ni vema kuanza kuchunguza aina za ngano kwa kuangalia maumbo ya ngano. Hivyo mtazamo huu unaangalia asili ya ngano kwa kuchunguza maumbo ya ngano husika. Ubora wa nadhairia hii, nadharia hii inasaidia kujua aina za ngano kutokana na dhima zake .

3. Fafanua mchango wa fasihi simulizi katika fasihi andishi. Wahusika wa fasihi simulizi Fasihi simulizi huweza kujengwa kwa wahusika wafuatao: i) Msimuliaji (Fanani): Huyu ni mhusika katika fasihi simulizi, kazi yake kubwa ni kuwaslisha mawazo aliyonayo kwa hadhira. Msimuliaji hujitahidi kutumia mbinu mbalimbali kwa ajili ya kuijenga kazi yake.

Fasihi simulizi imeelezwa kwa namna tofauti na wataalamu mbalimbali wa fasihi. Finnegan (1970) anaeleza kuwa fasihi simulizi ni sanaa ambayo hutegemea msanii ambaye huiumba kwa maneno katika tukio maalumu. Katika fasili hii Finnegan hajagusia mambo muhimu katika fasihi simulizi kama vile muktadha, namna ya

c) Fasihi simulizi ni mali ya jamii ilhali fasihi andishi ni mali ya mtu binafsi/mwandishi. d) Fasihi simulizi ina wahusika wa kila aina k.v binadamu, wanyama na ndege, mazimwi na majitu, miungu, mizimu, mashetani na vitu visivyo na uhai k.v. mawe na miti ilhali fasihi andishi ina wahusika binadamu kwa kiasi kikubwa.

Ukongwe wa fasihi simulizi waaidha imo katika mbinu za kuhifadhi. Hapo zama . Page 3 za zama fasihi simulizi ilikuwa ikihifadhiwa kichwani. Ilihifadhiwa humo kwa . fanani, kwani hii ni fasihi ambayo uwasilishaji wake si lazima wahusika wote wawili wawepo yaani fanani na Hadhira. Hadhira inaweza kuwepo lakini fanani

FASIHI SIMULIZI Fasihi ni sanaa inayotumia lugha kuwasilisha ujumbe unaomhusu binadamu. Sanaa ni ufundi wa kuwasilisha fikra na hisia za binadamu kama vile maneno, maandishi, uchoraji, uchongaji, ufinyanzi n.k. Fasihi simulizi ni sanaa kwa vile: a) Huwasilisha ujumbe kuhusu binadamu kuhusu utamaduni na uchumi. b) Huwa na umbo mahsusi k.m .

kuna mambo anuwai yanayoshirikisha wanajamii na yanayosheheni vipengele vya fasihi simulizi. Tamasha za urembo ni miongoni mwa shughuli zinazowakilisha fasihi simulizi ya jadi pamoja na kusawiri hali halisi ya ulimwengu wa sasa. Baadhi ya sifa katika sanaa ya maonyesho ya mitindo na urembo zinazosawiri sifa za fasihi simulizi ni kama utendaji .

The themes of pilgrimage and welcome are central to The Canterbury Journey. A lasting part of its legacy will be the new free-to-enter Welcome Centre with dedicated community and exhibition spaces and viewing gallery. The journey to our new centre is underway, to open in 2019. A New Welcome In 2017, the face of the Cathedral has changed .