COVER KANISA KUELEKEA MAONO YA PAMOJA1

3y ago
327 Views
6 Downloads
1.03 MB
96 Pages
Last View : 12d ago
Last Download : 3m ago
Upload by : Oscar Steel
Transcription

“Kamisheni ya BMD Kuhusu Imani na Utaratibu wa Ibada inatuleletea sisizawadi. Itakuwa na wajibu mkubwa katika miaka inayokuja kwa ajili yakutambua hatua nyingine kuelekea umoja unaoonekana.” - Olav Fykse Tveit,Katibu Mkuu wa Baraza la Makanisa DunianiKANISATunaweza kusema nini kwa pamoja kuhusu Kanisa la Utatu wa Mungu ilikukua katika ushirika, kupambana kwa pamoja kwa ajili ya haki na amanikatika dunia, na kushinda kwa pamoja dhidi ya migawanyiko ya zamanina sasa? Kanisa: Kuelekea Maono ya Pamoja kinapendekeza jibu lenye uzitokuhusu swali hili. Likiwa limetolewa na watheologia kutoka mapokeombalimbali ya Kikristo na tamaduni mbalimbali, andiko la Kanisa, kwanzalinashughulikia Misheni ya Kanisa, umoja, na asili yake ya kuwa katikamaisha ya Utatu wa Mungu. Baadaye kitabu hiki kinajadili juu ya kukuakwetu katika ushirika—katika imani ya kimitume, maisha ya ekaristitakatifu, na huduma—kama ilivyo kwamba makanisa yameitwa kuishindani ya na kwa ajili ya dunia.KUELEKEA MAONO YA PAMOJA“Kwa miaka ishirini, wawakilishi wa makanisa ya Kiorthodoksi, Kiprotestanti,Kianglikana, Kiinjilisti, Kipentekoste, na Kikatoliki. walifikiri kwa pamojakuanika maono juu ya asili, kusudi, na lengo la Kanisa duniani, katika tamadunimbalimbali na ushirika wa kiekumene” - Kutoka UtanguliziBarazala Makanisa DunianiiiBarazala Makanisa Duniani

KANISAKUELEKEA MAONO YA PAMOJAAndiko Kuhusu Imani na Utaratibu wa Kanisa, Na. 214.Tafsiri ya Toleo la Kiswahili naMchg. Dkt Faustin MahaliMaandiko ya Baraza la Makanisa Duniani

KANISAKuelekea Maono ya PamojaAndiko Kuhusu Imani na Utaratibu wa Kanisa Na. 214Hakimiliki 2013 Machapisho ya Baraza la Makanisa Duniani(BMD). Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kunukuusehemu ya kitabu bila ruhusu ya mpiga chapa, isipokuwa kwanukuu fupi au mapitio ya sehemu yake, omba kibali:publications@wcc-coe.org.Machapisho ya BMD ni mpango unaohusika na kuchapisha vitabuvya Baraza la Makanisa Duniani. Toka kuanzishwa kwake mwaka1948, BMD linaendeleza umoja wa Kikristo katika Imani, ushuhudana huduma kwa ajili ya kuijenga dunia inayoheshimu misingi ya hakina amani.Ikiwa ni ushirika wa dunia nzima, BMD linayaletapamoja makanisa zaidi ya 349 ya Kiprotestanti, Kiorthodiksi,Kiangalikana na mengineyo yanayowakilisha zaidi ya Wakristomilioni 560 katika nchi 110 na linafanya kazi kwa karibu naKanisa Katoliki.Mistari ya Biblia ni kutoka “New Revised Standard Version” Hakimiliki 1989 ya Dawati la Elimu ya Kikristo la Baraza laKitaifa ya Makanisa ya Kristo Marekani kwa kibali maalumu.Mchoro wa Jalada na Usanifu wa Kitabu cha Kiswahili:Mchg Dkt. Faustin MahaliISBN: 978-2-8254-1587-0World Council of Churches150 route de Ferney, P.O. Box 21001211 Geneva 2, Switzerlandhttp://publications.oikoumene.org

YaliyomoDibaji . vNeno la Utangulizi . viiUtangulizi . 1Sura ya I . 6Misheni ya Mungu na Umoja wa Kanisa . 6A. Kanisa Limekusudiwa na Mungu. 6B. Misheni ya Kanisa katika Historia . 9C. Umuhimu wa Umoja . 11Sura ya II. 14Kanisa la Utatu Mtakatifu . 14A. Kutambua Mapenzi ya Mungu kwa Kanisa . 14B. Kanisa kama Ushirika wa Utatu wa Mungu . 15Uwezo wa Mungu, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu . 15Unabii, Utume na Ufuasi wa Watu wa Mungu . 18Mwili wa Kristo na Hekalu la Roho Mtakatifu . 22Kanisa Moja, Takatifu, la Kikatoliki na la Kimitume . 23Jinsi muendelezo wa mapokeo na mabadiliko yanavyohusiana namapenzi ya Mungu . 26C. Kanisa kama Ishara na Mhudumu wa Mpango wa Mungukwa ajili ya Dunia . 26Usemi kuhusu "Kanisa kama Sakramenti". 29D. Kanisa kama Ishara na Mhudumu wa Mpango wa Mungukwa ajili ya Dunia . 29Uhalali na Hali ya Tofauti Iletayo Mgawanyiko . 32E. Ushirika wa Makanisa ya Kikanda . 32Uhusiano wa Kanisa la Eneo na la Kiulimwengu . 35Sura ya III . 36Kanisa: Kukua katika Ushirika . 36iii

A. Tayari lakini Bado . 36B. Kukua Katika Mambo Muhimu ya Ushirika: Imani,Sakramenti, na Huduma . 38Imani . 39Sakramenti. 42Sakramenti na Taratibu za Ibada . 46Huduma ndani ya Kanisa . 47Sura ya IV . 62Kanisa: Duniani na kwa ajili ya Dunia . 62A. Mpango wa Mungu kwa ajili ya Uumbaji: Ufalme . 62B. Changamoto ya Kimaadili ya Injili. 65C. Kanisa katika Jamii . 67Hitimisho . 71Mchakato Ulioleta Andiko la Kanisa: Kuelekea Maono yaPamoja . 73iv

DibajiKatika ziara zangu za kuzungukia makanisa duniani, nimeonachangamoto nyingi juu ya umoja kati ya makanisa na makanisana ndani ya makanisa yenyewe. Mazungumzo ya pamoja yakiekumene kati ya makanisa na taasisi zake ni ukweli ulio wazina yanachangia pia katika mahusiano kati yake hata nje yamipaka yake. Katika hali hii, mahusiano mapya hujengwa. Hatahivyo kuna hali ya wazi na ya msingi miongoni mwake yakukosa uvumilivu kwani yanahitaji kuona vuguvugu zaidikatika kufikia mazungumzo ya pamoja na maridhiano. Baadhiya makanisa na taasisi zake yanaona kuwa kuna maswali mapyaambayo yanaweza kuleta mpasuko zaidi. Vuguvugu lakiekumene linaonekana kukosa nguvu katika baadhi yamakanisa hakuna wasemaji wenye utayari kulisemea kamavipindi vya nyuma. Kuna hali ya kuelekea kwenye mipasuko nakuangalia zaidi vitu vinavyounganisha watu wachache kulikowatu wengi. Bila shaka, wito wa kuungana hauishii tu kwakuzaliwa kwa changamoto mpya, bali kinyume chake. Hatahivyo tunahitaji pia kuona mihimili mingine ya wito wakuelekea umoja wenye nguvu na kujikumbusha wenyewe kuwatunakumbatiwa na upendo na tunaitwa kupendana (1 Kor. 13).Katika mukitadha huu, Kamisheni ya BMD juu ya Imani naUtaratibu wa Kanisa inaleta kwetu tuzo, ambayo ni tamkokuhusu Kanisa: ni tunda la miaka mingi la kazi kuhusu elimuya kanisa. Kama chimbuko kutoka chapisho la Ubatizo, Ekaristina Huduma (1982) na itikio la makanisa la chapisho hili,chapisho la Kanisa: Kuelekea Maono ya Pamoja lilipokelewakwenye Kamati Kuu ya 2012 na kisha kupelekwa kwenyemakanisa ili kuendeleza mjadala zaidi kuhusu Kanisa nakuomba majibu yao kuhusu andiko hili. Utafiti huu namchakato wa majibu yake utachangia kwa kiwango kikubwakwa miaka ijayo kuamua juu ya hatua zaidi kuelekea umoja uliowazi zaidi. Kazi ya utafiti wa kikanisa unahusu mambo yotev

yahusuyo Kanisa na kazi zake za misheni ndani yake na kwaajili ya ulimwengu wote. Hivyo, chapisho hili la Kanisa linamizizi yake katika asili na misheni ya Kanisa. Linaakisi malengoya kikatiba na utambulisho wa BMD kama ushirika wamakanisa ambao unayaita makanisa kufikia lengo la umojaunaoonekana.Umoja ni kipawa cha maisha, na pia ni kipawa kitokanacho naupendo, na wala hautokani na misingi ya kufikia miafaka aumakubaliano kati ya kanisa na kanisa. Kama ushirikauliojengwa na makanisa tunaitwa kuueleza umoja unaohusumaisha ambao tumepewa kwa njia ya Yesu Kristo aliyejitoamaisha yake pale msalabani na katika ufufuko wake ili tuwezekushinda dhidi ya ubaya wetu, dhambi zetu na maovu yetu.Kwa kuwa kama andiko hili la Kanisa linavyotangaza: “Ufalmewa Mungu ambao Yesu ameufunua kwa njia ya Neno la Mungukwa mifano na kuusimika kwa njia ya matendo yake yenyenguvu, na hasa kwa njia ya fumbo la pasaka katika kifo naufufuko wake, ndio hasa lengo la mwisho la ulimwengu wotekuufikia. Kanisa limekusudiwa na Mungu si kwa ajili yakelenyewe, lakini kwa ajili ya kutumikia mpango wa Mungu wakuubadili ulimwengu” (§ 58).Olav Fykse TveitKatibu MkuuBaraza la Makanisa Dunianivi

Neno la UtanguliziMuunganiko wa andiko hili la Kanisa: Kuelekea Maono yaPamoja ni sehemu ya malengo ya kibiblia juu ya umoja waWakristo: “Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungovingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwilimmoja; vivyo hivyo na Kristo. Kwa maana katika Roho mmojasisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi,au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru;nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja” (1 Kor 12:12-13).Kusudi la msingi la Kamisheni juu ya Imani na Utaratibu waKanisa ni “kuyahudumia makanisa wakati yakiitana kwa ajili yaumoja ulio wazi kwa njia ya imani moja na kwa njia ya ushirikawa pamoja katika Ekaristi Takatifu, unaojieleza katika ibada namaisha ya pamoja katika Kristo; kwa njia ya ushuhuda nahuduma kwa dunia nzima, na kuelekea katika utimilifu waumoja huo ili ulimwengu uweze kuamini” (Kanuni 2012).Lengo la huu wito wa pamoja kuelekea umoja wa waziunaambatana na ulazima wa kutambuana kama makanisa,kama kielelezo cha kweli cha Ukiri wa Imani unaotuita kuwakanisa “lililo moja, takatifu, la ulimwengu wote [katoliki], na lakimitume.” Pamoja na Ukiri huu wa Imani bado katika haliisiyo ya kawaida ya mgawanyiko wa kikanisa, tafsiri za kanisajuu ya asili na misheni ya Kanisa vimeongeza mashaka kuwamafundisho mbalimbali ya makanisa si tu yanatofautiana, balipia hayapatani. Hivyo kufikia muafaka juu ya mafundisho nijambo lililotambuliwa kwa muda mrefu kuwa ni lengo lamsingi la kitheologia katika kutafuta umoja wa Kikristo. Kitabuhiki cha pili kinachounganisha Imani na Utaratibu wa Kanisa nimatokeo ya kitabu cha kwanza juu ya Ubatizo, Ekaristi, naHuduma (1982), na majibu rasmi juu yake, ambayoyaliyatambua maeneo ya msingi katika mafundisho ya kanisavii

yaliyohitaji utafiti zaidi;1 na pia kinatokana na maswaliyaliyotokana na mafundisho ya kanisa yaliyojitokeza katikaandiko la kitafiti kiitwacho Ubatizo Mmoja: KuelekeaKutambuana na Kuheshimiana (2011).Kwa miaka ishirini sasa, uwakilishi toka makanisa yaKiothodoksi, Kiprotestanti, Kianglikana, Kiinjili, Kipentekostena Kikatoliki, katika Kongamano la Dunia kuhusu Imani naUtaratibu wa Kanisa (1993), vikao vitatu vya ndani vyaKamisheni juu ya Imani na Utaratibu wa Kanisa (1996, 2004,2009), na mikutano kumi na nane ya Kamisheni iliyosimikwa,na vikao vya kutengeneza rasimu mbalimbali vilitafutakuyafunua maono ya asili, kusudi, na misheni ya Kanisakiulimwengu, kimataifa, na kiekumene. Makanisa yametoamajibu ya kina na ya kujenga katika hatua mbili za mwanzo juuya njia ya namna ya kuwa na tamko la pamoja. Kamisheni yaImani na Utaratibu wa Kanisa inaitikia wito wa makanisa naandiko hili, Kanisa: Kuelekea Maono ya Pamoja, ni andiko lapamoja, linalokutanisha, na ni tamko juu ya mafundisho yaKanisa. Muunganiko huu uliofikiwa katika andiko hili laKanisa yanawakilisha matokeo yasiyo ya kawaida ya kiekumene.Kuna malengo mawili tofauti, lakini yanayohusiana katikautume wa andiko la Kanisa kwa makanisa kwa ajili ya utafiti naitikio rasmi la makanisa hayo. Lengo la kwanza ni uamshompya. Andiko hili la Kanisa, ambalo ni la kimataifa nakiekumene, haliwezi kuhusishwa na utamaduni wa mafundishofulani ya pekee. Tangu mwaka 1993 had 2012, maelezo yakitheologia na uzoefu wa makanisa mbalimbali yamewekwapamoja kiasi kwamba makanisa yanayosoma andiko hiliyanaweza kujikuta yakipewa changamoto ya kuyaishi maisha ya1Linganisha, Baptism, Eucharist & Ministry, 1982-1990: Report on the Process andResponses. Faith and Order Paper No. 149. WCC: Geneva, 1990, 147-151.viii

kikanisa kwa ukamilifu; mengine yataona baadhi ya mamboambayo yamekuwa yakipuuzwa au kusahauliwa; na makanisamengine yanaweza kuona yameimarishwa na kuthibitishwa.Kama Wakristo wanaoendelea kukua katika maisha ya imaniyao katika Kristo, watajikuta wakisogeleana wenyewe kwawenyewe kwa ukaribu zaidi, na pia kuishi katika mfano wakibiblia wa mwili mmoja: “Kwa maana katika Roho mmoja sisisote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, aukwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru;nasi sote tulinyweshwa katika Roho mmoja.”Lengo la pili ni la makubaliano ya kitheologia juu ya Kanisa.Kama ilivyo kwenye umuhimu wa mapatano yaliyofikiwa katikaandiko la Imani na Utaratibu wa Kanisa kwenye Ubatizo,Ekaristi na Huduma, majibu rasmi ya makanisa katika mchakatohuu yana nafasi yake pia. Machapisho sita ya itikio la makanisayameonyesha maeneo mbalimbali ya muafaka kati yao kwenyemasuala ya msingi ya ubatizo, ekaristi na huduma. Atharichanya ya mapatano ya makanisa yaliyojitokeza katika andikola Ubatizo, Ekaristi na Huduma kuelekea umoja wa Kikristo,nyaraka zake zimetunzwa vizuri na mchakato wake ni endelevu.Itikio miongoni mwa makanisa kutokana na andiko la Kanisa:Kuelekea Maono ya Pamoja halitatathimini tu mapatano yayaliyofikiwa kwenye andiko la Imani na Utaratibu wa Kanisa,bali litatafakari pia kiwango cha makubaliano juuyamafundisho ya Kanisa. Kama ilivyo katika mapatano kuhusuubatizo, itikio la andiko la Ubatizo, Ekaristi na Huduma lililetamwamko mpya kuhusu kutambuana kati ya makanisa,yakihimizana kuwa na umoja ulio wazi katika imani moja naekaristi moja.“Majibu ya kikanisa” yaliyotokana na Kamisheni ya Imani naUtaratibu wa Kanisa yalihusisha makanisa ambayo yalikuwasehemu ya Kamisheni na jumuiya za makanisa ya Baraza laix

Makanisa Dunia. Inatumainiwa kuwa hata makanisa mapyayaliyojumuika katika vuguvugu hili la kiekumene yataukubalimwaliko wa kutafiti na kutoa maoni juu ya andiko hili.Kamisheni pia inaalika mawazo toka katika taasisi za makanisa,kama vile mabaraza ya kitaifa na kikanda na Jumuiya zaKikristo Duniani, ambazo mazungumzo ndani ya vyombo vyakeyamechangia sana katika kufikia mapatano ya tafsiri iliyopokwenye andiko hili la Kanisa. Maswali ya kipekee yaliyoulizwakwa makanisa kwenye andiko la Imani na Utaratibu wa Kanisaili kuuongoza mchakato huu yanapatikana mwishoni mwaUtangulizi wa Andiko hili la Kanisa. Maswali kwa ajili ya utafitini ya kitheologia, kivitendo, na kichungaji. Kamisheni iliombakuwa majibu rasmi yatumwe kwa sekretarieti iliyopo katikaBaraza la Makanisa Duniani kufikia tarehe 31 Desemba 2015.Kwa kuwa kuandaa andiko hili imechukua miongo miwili,tunapenda kutoa shukrani zetu kwa wale wote ambaowameubeba mchakakato huu kwa maombi na kwa njia yavipawa vyao vya kitheologia: tunawashukuru Wanakamisheniwa Imani na Utaratibu wa Kanisa, makanisa na watheolojiawaliotoa majibu ya utafiti wa andiko la Asili na Kusudi la Kanisa(1998) na Asili na Misheni ya Kanisa (2005), wajumbe wasekretarieti ya Imani na Utaratibu wa Kanisa, na wenzetuwaliotangulia kuongoza mchakato huu na kuuratibisha nawakuu wa idara za Kamisheni ya Imani na Utaratibu waKanisa.Canon John GibautMkurugenzi wa Kamishenijuu Imani na Utaratibu waIbadaMetropolitan Dr Vasilios waConstantia AmmochostosMsimamizi wa Kamishenijuu ya Imani na Ibadax

Utangulizi“Mapenzi yako yatimizwe” ni maneno wanayoomba kilasiku waumini wengi wasiohesabika kutoka makanisa yaKikristo. Yesu mwenyewe aliomba maneno haya katika bustaniya Getsemane muda mfupi kabla hajakamatwa (ling. Mt 26:3942; Marko 14:36; Luka 22:42). Katika injili ya Yohana, Yesuanayafunua mapenzi ya Baba kwa Kanisa pale alipoomba juu yawanafunzi wake kuwa wamoja, ili ulimwengu upate kuamini(ling. Yohana 17:21). Kuomba ili mapenzi ya Bwana yatimizwekunahitaji juhudi zitokazo moyoni ili kuyakubali mapenzi yakekwa ajili ya na kwa kipawa cha umoja. Andiko la sasa – Kanisa:Kuelekea Maono ya Pamoja–linajaribu kutatua moja ya matatizoyanayofikiriwa kuwa ni magumu yanayoyakabili makanisakatika kuondoa vikwazo vilivyobaki katika kukiishi kipawa chaushirika kitokacho kwa Bwana: yaani uelewa wa asili wa Kanisalenyewe. Umuhimu mkubwa wa kipawa na lengo hiliunaangazia maana ya mambo ambayo yanatakiwayashughulikiwe katika kurasa zinazofuata.Lengo letu si kutoa andiko la muungano, maana yake,andiko ambalo, wakati likiwa halielezei makubaliano kamilijuu ya masuala yote yaliyofikiriwa, ni zaidi ya chombo kwa ajiliya tu kuamsha utafiti zaidi. Bali, kurasa hizi zinaeleza ni kwakiwango gani jumuiya za Kikristo zimefikia katika uelewa wapamoja kuhusu Kanisa, kuonyesha hatua zilizofikiwa na piakuonyesha kazi ambayo bado inahitajika kufanywa. Andiko lasasa limechambuliwa na Kamisheni ya Imani na Utaratibu waKanisa, ambayo kusudi lake, kama lilivyo kusudi la Baraza laMakanisa Duniani kwa ujumla, ni kuyahudumia makanisa“yanapoitana kwa ajili ya umoja ulio wazi katika imani moja naushirika wa ekaristi moja, inayojieleza katika ibada na katikamaisha ya pamoja katika Kristo, kwa njia ya ushuhuda nahuduma kwa dunia nzima, na katika kusonga mbele kuelekea1

umoja kamili ili dunia iweze kuamini.”1 Umoja huu ulio waziunapata maelezo yenye ustadi wakati wa kushiriki ekaristitakatifu, ushiriki ambao unamtukuza Mungu wa Utatu nakuliwezesha Kanisa kushiriki katika Misheni ya Mungu kwaajili ya kuleta mabadiliko na wokovu wa dunia nzima. Tamkola sasa limetumia majibu ya makanisa kwa kazi ya andiko laImani na Utaratibu wa Kanisa juu ya mafundisho yake katikamiaka ya karibuni na nyaraka za mwanzoni za makubaliano yakiekumene ambazo zote zilitafuta makubaliano kwa njia yakutafakari Neno la Mungu, kwa matumaini kuwa, kwakuongozwa na Roho Mtakatifu, kipawa cha Mungu cha umojakinaweza kufikiwa. Kwa hiyo haya ni matokeo ya mazungumzokatika ngazi ya kimataifa, na hasa majibu ya makanisayaliyotokana na utafiti juu ya Asili na Misheni ya Kanisa,michango ya mawazo iliyotolewa katika mkutano wa wazi wakamisheni juu ya Imani na Utaratibu wa Kanisa uliofanyikaKrete mwaka 2009 na michango mbalimbali toka kanisa laOrthodoksi katika kongamano liliyofanyika Cyprus mwaka2011. Kwa kuongezea, andiko hili linajenga msingi wakekwenye mazungumzo mengi yaliyofanyika kati ya kanisa mojana jingine yaliyojikita kwenye hoja ya “Kanisa Moja” hasakatika miongo ya hivi karibuni.2Ni matumaini yetu kuwa kitabu hiki cha Kanisa:Kuelekea Maono ya Pamoja kitayasaidia makanisa kwa njia tatu:(1) kwa kutoa majumlisho ya matokeo ya mazungumzo yakiekumene kuhusu mada mbalimbali za mafundisho ya kanisakatika miongo ya karibuni; (2) kualika mada ili kutathiminimatokeo ya mazungumzo haya – kuyathibitisha matokeo1L. N. Rivera-Pagán (mhariri.), God in Your Grace: Official Report of the NinthAssembly of the World Council of Churches, Geneva, WCC, 2007, 448.2Kwa ajili ya maelezo zaidi juu ya mchakato huu, angalia maelezo ya kihistoriayanayopatikana mwisho wa kila andiko.2

mazuri, kuainisha mapungufu na au kuonyesha maeneoambayo hayajaangaliwa kwa kina; na (3) kutoa fursa kwamakanisa kutafakari kuhusu uelewa wa makanisa yenyewe juuya mapenzi ya Bwana ili kukua pamoja kuelekea umoja mpanazaidi (ling. Ef. 4:12-16). Nimatumaini kuwa kwa mchakato huuwa habari, majibu na ukuaji, kwa kukubali, kuboresha na kutoachangamoto kwa makanisa yote, andiko hili litaleta mchangomkubwa na hata kuwezesha kufikiwa kwa baadhi ya hatua zakimaamuzi kuelekea kufikia umoja ulio kamili.Kitabu hiki kimepangwa kwa kufuata madazinazojadiliwa kuhusu masuala ya kikanisa. Kitabu hiki chaKanisa: Kuelekea Maono ya

linashughulikia Misheni ya Kanisa, umoja, na asili yake ya kuwa katika maisha ya Utatu wa Mungu. Baadaye kitabu hiki kinajadili juu ya kukua kwetu katika ushirika—katika imani ya kimitume, maisha ya ekaristi takatifu, na huduma—kama ilivyo kwamba makanisa yameitwa kuishi ndani ya na kwa ajili ya dunia.

Related Documents:

na maisha ya uadilifu na usafi, ambayo yamedhibitishwa na wakati kuwa yanafaa kwa Mkristo. Toleo hili la Kitabu cha Mwongozo la 2017-2021 lina taarifa fupi ya kihistoria ya kanisa, Katiba ya kanisa inayofafanua Kanuni za Imani yetu, ufahamu wetu wa kanisa, Agano la Maadili ya Kikristo ya kuishi kitakatifu,

Lindi 6.30-6.50 Chikonji Mwenge kuweka jiwe la msingi Mradi wa Maji. 0 Mkuu wa Wilaya ya Lindi 6.50-7.00 10Chikonji Mwenge kuelekea S/M Kineng‟ene. Mkuu wa Wilaya ya Lindi 7.00-8.00 S/M Kineng‟ene. CHAKULA CHA MCHANA 0 Mkuu wa Wilaya ya Lindi 8.00-8.15 S/M kineng‟ene Mwenge kuelekea Shule ya Sekondari Mkonge. 15 Mkuu wa Wilaya ya Lindi 8. .

Somo la 7: Kanisa la Kristo Somo la 8: Maisha mapya katika Kristo . mafundisho ya Kristo, bali akayaacha, yeye hana Mungu. Ye yote anayedumu katika mafundisho ana Baba na Mwana pia” . ndani Yake, vivyo hivyo amempa Mwana kuwa na uzima ndani Yake. Naye amempa Mwanawe mamlaka ya kuhukumu kwa kuwa Yeye ni Mwana wa .

mafundisho potofu ndani ya makanisa mbali mbali). Kwa sababu ya hali hii, viongozi wa makanisa wanapaswa kujua “tunda” la maisha yao na ya maisha ya watu ndani ya kanisa (ona Math 7:16-20; 21:43; Luka 6:43-44; Yoh 15:4-5; Gal 5:22-23; 1 Tim 4:15-16); vifungu vya Biblia “vinavyoonya”

"Mafunzo ya kwanza." au ya "msingi" yote yanayopatikana katika kifungu hiki cha Biblia yamepanuliwa. Mafunzo haya yameandaliwa yawasaidie zaidi wale wanaopitia mafunzo ya Kuweka Msingi wa Imani katika Kanisa la Cornerstone maana yake kwa ni Kiswahili Kanisa la Jiwe la Pembeni. Mafunzo haya yanawawezesha kulenga zaidi katika kile .

URITI WETU Kitabu hiki kitachangamoto dhana yako na mawazo ya kanisa ni nini na sehemu yako ndani yake. Yesu alisema nao waniabudu bure, wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu Mariko 7:7 Soma kitabu hiki ufahamu: Kufanyika mwana Kuwa sehehu ya kikundi cha kitume Siri ya kanisa Kuhusiana na Yesu kama Mtume

Mwito Mkuu "Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote . Mafundisho yaliyobaki yameundwa kuwapa viongozi wetu wa kanisa maarifa rahisi yenye nguvu yawezayo kufanya kanisa lenye kufanya wanafunzi. Mwito mkuu unahusu idadi ya watu ulimwenguni kote. Yaweza kutimizwa na Roho wa

Immersive Adventure Tourism is about building up to the adventure activity with soft immersion in the natural and culture assets that make a place distinct from any other. The aging population is a big driver of this trend. 2/3 rd’s Of travellers cite adventure 42% costs, on avg. are spent directly in activities as the focus of their holidays, the lions share of which are “soft .