Kutathimini Mbinu Za Ufutuhi Katika Kuelimisha Jamii Kuhusu . - Core

1y ago
46 Views
3 Downloads
530.08 KB
76 Pages
Last View : 18d ago
Last Download : 3m ago
Upload by : Jacoby Zeller
Transcription

View metadata, citation and similar papers at core.ac.ukbrought to you byCOREprovided by Digital Library of Open University of TanzaniaKUTATHIMINI MBINU ZA UFUTUHI KATIKA KUELIMISHA JAMIIKUHUSU JANGA LA UKIMWI KATIKA TAMTHILIYA YA EMBE DODONA USHUHUDA WA MIFUPALUCY CHAKUPEWA GWANKOTASNIFU ILIYOWASILISHWA IKIWA NI SEHEMU YA MASHARTI YAKUTUNUKIWA SHAHADA YA UZAMILI (M.A KISWAHILI) YA CHUOKIKUU HURIA CHA TANZANIA2017

iiUTHIBITISHOMimi, Prof. Emmanuel Mbogo, nathibitisha kwamba nimeisoma tasnifu hii iitwayo:“Kutathimini Mbinu za Ufutuhi Katika Kuelimisha Jamii Kuhusu Janga laUkimwi, katika tamthiliya ya Embe Dodo ushuhuda wa mifupa nimeridhikakwamba imefikia kiwango kinachotakiwa na inafaa kuwasilishwa kwa ajili yaUtahini wa Shahada ya Uzamili ya Fasihi kwa Kiswahili ya Chuo Kikuu Huria chaTanzania. Prof. Emmanuel Mbogo(Msimamizi) . .Tarehe

iiiHAKIMILIKITasnifu hii au sehemu yake yoyote hairuhusiwi kukaririwa, kuhifadhiwa,Kubadilishwa au kuhaulishwa kwa mbinu yoyote ile: kielektroniki, kimekanika,kunakilishwa, kurudufiwa, kupigwa picha, au kurekodiwa kwa utaratibuwowote ulekatika hali yoyote ile bila idhini ya maandishi kutoka kwa mwandishi wake aukutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, kwa niaba yake.

ivTAMKOMimi Lucy Chakupewa Gwanko, nathibitisha kwamba tasinifu hii ni kazi yanguhalisi na kwamba haijawahi kuwasilishwa na haitawasilishwa katika Chuo Kikuukingine kwa ajili ya Shahada yoyote. .Saini .Tarehe

vTABARUKUNatabaruku kazi hii kwa baba yangu mzazi Zakayo Chakupewa Gwanko na mamayangu Olipa Chakupewa Gwanko, mme wangu Livingstone Fidelis na watoto wetuwapendwa Layson, Lulu na Leonata Livingstone, pia bila ya kuwasahau wataalamuna wanafunzi wote wa fasihi ya Kiswahili.

viSHUKRANIKatika mafanikio yoyote, upo mchango wa kimawazo, kifedha ama kiutendaji nakwa sababu mafanikio ya kazi hii sikuweza kujitegemea mwenyewe kwa kila kitu,inanipasa kutoa shukrani zangu za pekee kwa watu ama taasisi zilizonifanikishakatika malengo yangu. Nikianza na shukrani za pekee kwa yeye anayetupatia pumziya uhai na kutupatia riziki kubwa kubwa na ndogo ndogo ambaye ni MwenyeziMungu kwani katika mafanikio haya si kwa nguvu zangu bali ni kwa neema yake.Wapo watu ambao inanipasa kuwafanyia iliyo haki kwa kuwataja katika kufanikishakatika tasnifu hii; shukrani za pekee kwa mwalimu na Msimamizi wangu Prof.Emmanuel Mbogo kwa juhudi zake alizonifanyia kwa kusimamia na kuisahihishakazi hii hadi kufikia ubora huu, hakika anapaswa kuheshimiwa kwa mchango wakena anastahili kuigwa kwa mazuri haya. Naweza kumbuka maneno yake ya kutiamoyo ambayo mara nyingi alikuwa akiyatumia, ‘tusikate tamaa’ neno hilo lilikuwalikinitia moyo sana kwani alikuwa ananiambia mara nyingi kuwa ukiwa na mimihauwezi choka. Mengi yaliyo katika kazi hii ni sehemu tu ya matunda ya ujuzi wakemkubwa na ushauri wake wa kitaalamu. Ninapenda pia kumshukuru Prof. EmmanuelMbogo kwa kunifanikisha katika kukamilisha tasnifu hii, kwani amekuwa akinitiamoyo na kutoa muda wake mwingi kunielekeza kwani mara nyingi nilitakakufahamu undani wa kazi yake ya tamthiliya ambayo nimeitumia katika kazi hii.Siwezi kuwasahau wasanii wa kazi ya kifasihi ziitwazo Embe dodo ya D.Z.Makukulana Ushuhuda wa Mifupa ya Ibrahim Ngozi] kwani walikubali kutoa mawazo yakeyaliyokamilisha kazi hii akiwa kama mtafitiwa, naomba Mwenyezi Mungu ambarikisana.

viiIKISIRILengo la utafiti huu ni kuchunguza mbinu za ufutuhi katika kufikisha maudhui katikatamthiliya kwa kulinganisha kazi mbili za tamthiliya ya Embe dodo na Ushuhuda waMifupa ili kubaini mbinu za ufutuhi zinavyowafananisha na kuwatofautisha wasaniiwa vitabu hivyo katika kuliwasilisha suala la ugonjwa wa ukimwi na njia za kueneakwa ugonjwa wa ukimwi. Utafiti huu ulitumia mbinu moja ya ukusanyaji dataambazo ni; maktaba. Aidha data za utafiti huu zilichambuliwa kwa kutumia mbinuya uchambuzi linganishi. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Elimumitindokatika Uchambuzi wa Matini za Kifasihi. Utafiti umegundua kuwa, tamthiliya hizizinatofautiana katika mbinu za kisanii na ubunifu. Tamthiliya ya Embe dodoimetumia mbinu za ufutuhi ubeuzi zaidi wakati tamthiliya ya Ushuhuda wa Mifupaimetumia mbinu ya ufutuhi uzimbwe zaidi, rahisi na ya wazi zaidi. Aidha utafiti huuumebaini kuwa, tamthiliya hizi zinatofutiana katika kuwasilisha suala la ugonjwa waukimwi na njia za kuenea kwake katika jamii ya Tanzania katika vipindi viwilitofauti. Embe dodo anawasilisha suala la mila na desturi linavyopingana na njia zakujikinga na ugonjwa wa ukimwi wakati Ushuhuda wa Mifupa inajadili kwa uhalisiajuu ya njia mbali mbali ambazo zilisababisha zaidi kuenea kwa ugonjwa wa ukimwi,ambazo ni ujinga, umaskini na jamii kutokujali. Kwa upande mwingine, ilibainikakuwa tamthiliya hizi kwa vile zimeandikwa na wasanii wa jamii moja ambaowameshuhudia na kupata kuona na masimulizi ya historia ya jamii yao juu zaugonjwa wa ukimwi. Wasanii hawa wanafanana katika kuwasilisha maudhui ya kazizao ambapo wote kwa pamoja wanajadili juu ya mambo mbalimbali yaliyopo katikajamii kama vile; rushwa, harakati za ukombozi, usaliti, mfumo dume, nafasi yamwanamke, suala la ugonjwa wa ukimwi.

viiiYALIYOMOUTHIBITISHO . iiHAKIMILIKI . iiiTAMKO . ivTABARUKU .vSHUKRANI. viIKISIRI . viiORODHA YA MAJEDWALI . xiSURA YA KWANZA.11.0UTANGULIZI .11.1Utangulizi.11.2Historia Fupi ya Watunzi wa Tamthilia ya Embe Dodo na Ushuhuda waMifupa.11.3Usuli wa Tatizo la Utafiti.21.4Tamko la Tatizo la Utafiti .51.5Malengo ya Utafiti.51.5.1 Lengo Kuu .61.5.2 Malengo Mahususi .61.6Maswali ya Utafiti .61.7Umuhimu wa Utafiti .61.8Mipaka ya Utafiti.71.9Matatizo ya Utafiti.71.10Muundo wa Tasnifu .8

ix1.11Hitimisho .8SURA YA PILI .92.0MAPITIO YA KAZI TANGULIZI NA KIUNZI CHA NADHARIA .92.1Utangulizi.92.1.1 Futuhi .92.1.2 Maandiko Yahusuyo Ufutuhi .102.1.3 Dhima ya Futuhi . 142.1.4 Futuhi wakati wa Ukoloni. 192.1.5 Futuhi Wakati Ww Sasa Nchini Tanzania . 202.2Pengo la Maarifa . 212.3Kiunzi cha Nadharia . 212.3.1 Dhana ya Nadharia . 222.4Nadharia ya Fasihi Linganishi .232.5Nadharia ya Elimu Mitindo .252.6Hitimisho . 27SURA YA TATU.293.0MBINU ZA UTAFITI . 293.1Utangulizi. 293.2Mkabala wa Utafiti . 293.3Eneo la Utafiti . 293.4Mbinu ya Usomaji wa Maktabani . 303.5Matini.303.6Uchambuzi wa Data . 313.7Hitimisho . 31

xSURA YA NNE .334.0UWASILISHAJI NA UCHAMBUZI WA DATA . 334.1Utangulizi. 334.2Uteuzi na Matumizi ya Mbinu za Ufutuhi . 334.2.1 Mbinu za Ufutuhi Katika Tamthiliya ya Embe Dodo .334.2.2 Mbinu za Ufutuhi katika Ushuda wa Mifupa . 394.3Kulinganua na Kulinganisha Uteuzi wa Mbinu za Ufutuhi Katika KuwasilishaUeneaji wa Ukimwi . 514.3.1 Kutofautiana . 514.3.2 Kufanana .534.3.3 Sababu za Kufanana na Kutofautiana Kwa Mbinu za Ufutuhi . 544.3.4 Hitimisho . 55SURA YA TANO .575.0MUHTASARI, HITIMISHO NA MAPENDEKEZO . 575.1Utangulizi. 575.2Muhtasari wa Matokeo ya Utafiti. 575.3Hitimisho . 605.4Mapendekezo . 61MAREJELEO .63

xiORODHA YA MAJEDWALIJedwali Na 2.1: Mbinu za Ufutuhi . 16Jedwali Na 4.1: mbinu za Ufutuhi katika Embe dodo na Ushuhuda wa Mifupa .50

1SURA YA KWANZA1.0 UTANGULIZI1.1UtanguliziSura hii ni sura tangulizi ambayo imetoa usuli wa tasnifu hii. Katika kubainishatatizo la usuli wa tatizo na tatizo lililofanyiwa utafiti. Sura hii inahusu usuli watatizo, tatizo la utafiti, malengo ya utafiti, maswali ya utafiti, umuhimu wa utafiti,mipaka ya utafiti na hitimisho.1.2Historia Fupi Ya Watunzi wa Tamthilia ya Embe Dodo na Ushuhuda waMifupaKabla ya kuanza tupate historia fupi ya mtunzi wa tamthiliya ya Embe dodo naUshuhuda wa Mifupa. Tamthiliya ya Embe dodo imeandikwa na Dominicus Z.Makukula (2015) ni mzaliwa wa nchi ya Tanzania katika mkoa wa Ruvuma.Tamthiliya ya Embe dodo imeandikwa katika malengo ya kuwashawishi Watanzaniakubadili tabia au kutumia kinga katika kupambana na ugonjwa wa Ukimwi. Mchezohuu ulichezwa kwa mara ya kwanza na wanachuo mbali mbali katika Chuo cha sanaaBagamoyo kati ya mwaka 2000 hadi 2005 kwa ubunifu mkubwa wenye matukio yakufurahisha na kuelimisha. Wakati tamthiliya ya Ushuhuda wa Mifupa imeandikwana Ibrahim Ngozi (1990) iliyolenga kuhamasisha au kufanya kampeni dhidi yaugonjwa wa Ukimwi. Kampeni hii ililengwa kuwa ya kudumu katika maisha yaWatanzania ili kuwaweka wananchi kuwa makini au kujihadhari na ugonjwa waUkimwi. Hizi ni juhudi za kupambana na ugonjwa wa Ukimwi ambao hauna tiba nadunia nzima ingali ikitafuta dawa za ugonjwa huu hatari, aidha watu wengi wa

2vijijini bado hawajaufahamu vyema ugonjwa huu wa Ukimwi. Kazi hii imeangaliakuhusu mchango wa ufutuhi katika uelimishaji wa jamii yetu ya Kitanzania juu yakupambana na ugonjwa wa Ukimwi, nanma ya kujikinga, unavyoenezwa na nanmaya kuwahudumia watu waliopatwa na ugonjwa huo. Tumechunguza jinsi waandishihawa walivyotumia ufutuhi katika kuwasilisha suala la ugonjwa wa Ukimwi katikajamii ya Tanzania. Tamthiliya hizi mbili zilichanguliwakwasababu zotezinazungumzia ugonjwa wa Ukimwi unavyoambukizwa na namna ya kujikinga nao,tena zimeandikwa na waandishi wawili tofauti. Aidha, tamthiliya hizi zimechaguliwakwa sababu zote zimetumia mbinu ya ufutuhi katika kuwasilisha suala la ugonjwawa Ukimwi.1.3Usuli wa Tatizo la UtafitiTatizo la Ufutuhi ni kutaka kutathimini mbinu za kifutuhi zilivyotumika katikakuelimisha jamii kuhusu janga la Ukimwi. Mtunzi yeyote kwa kazi ya fasihi hutumiaubunifu au ujuzi fulani ili kuwasilisha ujumbe katika jamii husika. Hivyo basi,Ufutuhi ni mbinu iliyotumiwa na waandishi wote wa tamthiliya ya Embe dodoiliyoandikwa na Makukula,D.Z (2015) na tamthiliya yaUshuhuda wa Mifupailiyoandikwa na Ngozi,I (1990). Tamthiliya kama ilivyofasiliwa na Wamitila (2002)ni kazi ya kimantiki na kimaongezi ambayo hutendwa mbele ya hadhira. Anaendeleakusema kwamba, nitamthiliya ya kimuundo imegawanyika katika matendo nautendaji, mazungumzo ya kusemwa huchukua nafasi kubwa katika uwasilishaujumbe. TUKI, (2013:538), wanaeleza kuwa, Tamthiliya ni utungo wa kisanaaambao huweka wazo Fulani katika matendo na mazungumzo, agh.huweza kuigizwa.Hivyo tamthiliya ni utanzu wa fasihi ambao hutendwa jukwaani mbele ya hadhira na

3yaweza kuwa katika maandishi mfano Embe dodo na Ushuhuda wa Mifupa. Tatizohili la ugonjwa wa Ukimwi kwa sasa ni tatizo kubwa katika nchi yetu ya Tanzania.Katika kuthibitisha hilo kuwa ni tatizo kwa sasa, kuna waandishi kadhaa ambaowameandika tamthiliya zao juu ya ugonjwa wa Ukimwi, baadhi yao ni Medical AidFoundation (2005) Kilio chetu, Jilala (2003) Giza,Mapalala (2006) Passed like ashadow na Steve (2007) Orodha.Tamthiliya hizo na zingine ambazo hatujazitaja katika utafiti wetu zote zinaongeleajuu ya ugonjwa wa Ukimwi na njia za kuenea kwa ugonjwa huo. Hivyo idadi hiyo yavitabu ambavyo tumeviorodhesha, vyote kuongelea suala moja, ni ushahidi toshauliomsukuma mtafiti kufanya utafiti wake katika tamthiliya za Embe dodo naUshuda wa Mifupa ambavyo navyo vinaongelea suala ugonjwa wa Ukimwi.Kazi hii inahusu Ufutuhi au ucheshi,hivyo tunalazimika kuelezea maana ya futuhikwa vile ndicho kiini cha utafiti wetu. Tunaomba kukazia kwamba,futuhi havinalengo la kuchekesha peke yake lakini ucheshi huo unaopatikana katika futuhiumekusudia kutoa ujumbe mbali kwa jamii, kama tutakavyoona katika kipengele chadhima ya futuhi. Dhana ya Ufutuhi imeelezwa na wataalamu mbali mbali kwa njia yakukaribiana; Senyamanza,(h.t:76), akinukuu Oxford Dictionary: Thesaurus andWordpower Guide (2007),anaeleza kuwa, neno futuhi wamalifafanua kwa mitazamomitatu;i)ii)iii)Entertainment consisting of jokes and sketches intended to make anaudience laugh.A film, play or programme intended to arouse laughter.A humorous of satirical play in which the characters ultimatelytriumph over adversity.

4Tafsirii)ii)iii)Ni kiburudisho ambacho hujumuisha utani na vibonzo kwa lengola kuchekesha hadhira.Ni filamu, mchezo wa kuigiza au vitendo ambavyo hulenga kuibuaucheshi.Ni mchezo wa dhihaka unaojumuisha vichekesho, kejeli ambaohatima yake ni kuibua furaha kwa wahusika.Maelezo haya yanabainisha wazi kuwa futuhi ni kazi ya kisanaa ambayo imebuniwaili kuleta furaha au ucheshi miongoni mwa wanajamii au hadhira inayotazamamchezo husika.FUTUHISenyamanza (h.t) anasema; “Lengo la msingi la futuhi ni kuchangamsha na huishiakwa namna ya kufurahisha. Lazima tukumbuke kwamba, kusema futuhi inafurahishahaina maana kuwa dhamira yake haina uzito. Utuhihuweza kuwa na sifazinazotofautiana, jambo ambalo hutumiwa kama kigezo cha kuainisha aina mbalimbali za ucheshi. Lakini, vyovyote iwavyo, futuhi hujikwepesha na maswala yakuhuzunisha au kushtua”.Kwa mujibu wa utafiti huu, ufutuhi ni mchezo wa kuigiza au tamthiliya ambaohuyaweka mawazo mbali mbali katika matendo ili yaweze kuigizwa katika mtindowa kuchekesha au kushangaza ili jamii iweza kupata ujumbe uliokusuiwa. Wamitila(2002) anasema, tofauti na katuni, Ufutuhi ambao kwa Kiingereza ni comedyinatokana na neno Komos la lugha ya Kiyunani likimaanusha sherehe za matambikoya watu wa Uyunani ya kale ambapo watu walifurahi kugonga ngoma kwa kuchezangoma, kuimba na kutambamajigambo ili kumshukru Mungu wao aitwaye

5Dionysius ambaye alikuwa mungu wa rutuba na mavuno . Hivyo katika utafiti huuumeliangalia suala Ufutuhi linavyojitokeza katika tamthiliya hizo mbili na watafitiwatabainisha ujitokeza wa matukio ya ufutuhi katika tamthiliya zote mbili nakubainisha maudhui au ujumbe uliobebwa na Ufutuhi huo katika tamthiliya hizo.1.4Tamko la Tatizo la UtafitiWaandishi wa kazi za fasihi wanaweza kuelezea suala moja katika jamii kwakutumia ubunifu wa namna mbali mbali. Ingawa wataalamu wanaeleza kuwa kilamwandishi ana namna yake ya kuwasilisha ujumbe kwa jamii yake. Waandishiwanaweza kuwa wawili au zaidi na wakaongelea suala lile lile, lakini wakatofautiananamna ambavyo kila mmoja anavyowasilisha ujumbe wake kwa jamii. Hivyo basibado kuna haja ya kujua kuwa mwandishi wa tamthiliya za Ufutuhi wanawezakutumia mbinu zile zile au tafauti katika kufikisha ujumbe kwa jamii kwa kutumiaUfutuhi?(uchekeshaji). Ubainishaji wa mbinu za kifutuhi na kunafanana amakutofautiana kwa mbinu hizo za Ufutuhi. Hivyo basi tatizo la utafiti ni kwambatamthiliya nyingi za Ufutuhi hazijafanyiwa uchunguzi wa kina na kuweka bayanajinsi mbinu za Ufutuhi zinavyoweza kubainishwa katika uwasilishwaji wa ugonjwawa ukimwi kwa jamii husika. Waandishi wawili tofautiwa tamthiliya za Embedodo na Ushuhuda wa mifupa wanaweza kuwa na mbinu zile zile au zikatofautianakatika tamthiliya ya Embe dodo na Ushuhuda wa mifupa?1.5Malengo ya UtafitiUtafiti huu una lengo kuu na malengo mahsusi kama ifuatavyo:

61.5.1 Lengo KuuLengo kuu la utafiti huu kulinganisha mbinu za kifutuhi zilivyotumika katikakuelimisha jamii ya Watanzania kuhusu janga la ugonjwa wa Ukimwi katikatamthiliya za Ufutuhi za Embe dodo na Ushuhuda wa Mifupa1.5.2 Malengo MahususiUtafiti huu una malengo mahususi mawili:i)Kubainisha mbinu za kifutuhi katika tamthiliya ya Embe dodo na Ushuhudawa Mifupa.ii)Kulinganisha na kutofautisha mbinu za ufutuhi katika tamthiliya ya Embedodo na Ushuhuda wa Mifupa.1.6Maswali ya UtafitiUtafiti huu unajibu maswali yafuatayo:i)Ni mbinu zipi za kifutuhi zilizotumika katika Embe dodo na Ushuhuda waMifupa?ii)Kuna kulingana na kutofautina gani katika mbinu za ufutuhi zilizoonekanakatika tamthiliya ya Embe dodo na Ushuda wa Mifupa?1.7Umuhimu wa UtafitiUmuhimu wa utafiti huu umejikita katika nyanja kuu tatu; kwanza, matokeo yautafiti huu yataongeza maarifa katika nadharia na mbinu za utunzi wa tamthiliyahususani tamthiliya za Ufutuhi wa tathiliya za Kiswahili. Pili, utafiti huu utatoamchango katika maarifa ya taaluma ya fasihi linnganishi. Hivyo basi, utafiti huu

7utaweza kutumiwa kama marejeo, hususani katika fasihi linganishi. Kwa maanahiyo, utawasaidia wanafunzi na watafiti wengine kupata marejeo kuhusu fasihilinganishi na tamthiliya Ufutuhi ya Kiswahili kwa ujumla wake. Tatu, utafiti huu piautakuwa ni changamoto kwa watafiti wengine kufanya utafiti kuhusu tamthiliya zaKiswahili hususani tamthiliya za Ufutuhi zilizoandikwa na waandishi wawili tofautina vilevile utatajirisha maktaba ya chuo.1.8Mipaka ya UtafitiUtafiti huu unalenga kuchunguza na kulinganisha ujumbe uliojitokeza katikatamthiliya za kifutuhi. Zipo tamthiliya nyingi zenye kuongelea tatizo la ugonjwa waUkimwi, kama vile Orodha ya Steve Rynolds,(2007), Kilio chetu ya Medical AidFoundation(2005), Giza ya Jilala,(2003),hatukuweza kuzishughulikia tamthiliya zotehizo za ufutuhi. Utafiti huu utajikita katika kubainisha vipengele vya ufutuhiambavyo ni kejeli,ubeuzi,vijembe, dhihaka na utani katika tamthiliya ya Embe dodona Ushuhuda wa mifupa. Aidha utafiti huu umejikita katika kubainisha tofauti nakufanana kwa mbinu za Ufutuhi katika tamthiliya ya Embe dodo ya DominicusMakukula na Ushuda wa Mifupa yaIbrahim Ngozi tu kwasababu ndivyo mtafitialivyovilenga.1.9Matatizo ya UtafitiKatika utafiti huu, mtafiti alikutana na matatizo kadhaa ambayo yameifanya kazi yakiutafiti kuwa ngumu, ila alijitahidi kuyatatua. Tatizo moja lilikuwa upatikanaji wakitabu cha tamthiliya cha ushuhuda wa mifupa cha Ibrahimu Ngozi. Kitabu hikihakijaenea sana katika maduka ya vitabu ya mikoa mingine,tofauti na Dar es Salaam

8na hata maktabani hakipatikani na hata wanafunzi wa sekondari hawakisomi kamakitabu cha kiada. kitabu hiki ni cha zamani, hivyo mtafiti amekipata kutoka kwamwanafunzi aliyetunza kopi ya kitabu hicho katika Chuo kikuu Huria cha Tanzania,Dar es Salaam akapata nakala, ambayo imenisaidia katika utafiti huu. Tatizo la pili,ni upatikanaji wa pesa,kazi zote za kitafiti zitahitaji fedha za kutosha, hivyo mtafitialilazimika kukopa fedha katika banki ili kukamilisha utafiti huu. Hivyo, ilikuwa nikazi ngumu kwa mtafiti kukamilisha utafiti huu.1.10 Muundo wa TasnifuMuundo wa utafiti huu umegawanyika katika katika sura tano, sura ya kwanzainahusu utangulizi wa jumla wa utafiti, masuala yanayohusiana na tatizolililofanyiwa uchunguzi katika utafiti huu, yamejadiliwa na kutolewa maelezo yakina. Sura ya pili inahusu utalii wa kazi tangulizi na mkabala wa kinadharia, ambaposura ya tatu inahusu mbinu za utafiti. Katika sura hii, imeonesha mbinu ya usomajiwa maktabani. Sura ya nne, inahusu uwasilishaji na uchambuzi wa data na sura yatano, ambayo ndiyo sura ya mwisho, inahusu muhtasari wa matokeo, hitimisho namapendekezo.1.11 HitimishoSura hii imejadili juu ya usuli wa tatizo, tatizo la utafiti, malengo ya utafiti, maswaliya utafiti, umuhimu wa utafiti, mipaka ya utafiti, masuala ya kimaadili na muundowa tasnifu. Aidha katika sura hii ya kwanza tatizo la utafiti litakuwa limebainishwana kuelezwa wazi na kwa undani zaidi. Sura inayofuata ni sura ya pili, ambayoinahusu Mapitio ya kazi tangulizi na Kiunzi cha Nadharia.

9SURA YA PILI2.0 MAPITIO YA KAZI TANGULIZI NA KIUNZI CHA NADHARIA2.1UtanguliziSura hii inatalii mapitio ya maandiko tangulizi, katika sura hii maandiko na tafitimbalimbali zinazohusiana na mada ya utafiti zitajadiliwa kwa kina na hatimayekuibua pengo la maarifa ambalo liliweka msukumo kufanya utafiti huu. Sura hiiimegawanyika katika sehemu kuu nne ambapo sehemu ya pili inahusu dhana yafasihi linganishi, sehemu ya kwanza inajadili juu ya dhana ya Ufutuhi , ya tatu nipengo la kimaarifa na sehemu ya nne kiunzi cha nadharia.2.1.1 FutuhiSenyamanza,(h.t:77-78), akiwanukuu Kennedy na Gioia, (2007: 1257), anaelezakuwa, Futuhi / Komedia (comedy)linalotokana na neno Komos la lugha yaKiyunani. Komos linamaanisha sherehe za matambiko ya jamii ya watu wa Uyunaniya kale katika sherehe, sherehe hizo watu walifurahi na kuimba, kucheza ngoma nakutamba majigambo ili kumshukrumungu wao aitwaye Dionysius ambaye nimungu wa rutuba na mavuno. Wamitila, (2003) anaelezea kuwa, futuhi ni dhana yaucheshi inayotumia kuelezea uwezo wa kazi ya fasihi na sanaa ya maonyeshokusababisha vichekesho kwa msomaji au mtazamaji.Senyamanza,(h.t:76), akitoa maelezo katika, Oxford Dictionary: Thesaurus andWordpower Guide (2007),anasema kuwa, neno futuhi wamalifafanua kwa mitazamomitatu;Entertainment consisting of jokes and sketches intended to make an audience

10laugh.A film, play or programme intended to arouse laughter, ahumorous ofsatirical play in which the characters ultimately triumph over adversity.Tafsiri; Ni kiburudisho ambacho hujumuisha utani na vibonzo kwa lengo lakuchekesha hadhira.Ni filamu, mchezo wa kuigiza au vitendo ambavyo hulengakuibua ucheshi. Ni mchezo wa dhihaka unaojumuisha vichekesho, kejeli ambaohatima yake ni kuibua furaha kwa wahusika.Maelezo haya yanabainisha wazi kuwafutuhi ni kazi ya kisanaa ambayo imebuniwa ili kuleta furaha au ucheshi miongonimwa wanajamii au hadhira inayotazama mchezo husika.Mbogo, (2015:11), katika nukuu za darasani, anaeleza kuwa, futuhi au Komedia niutungo ambao unachekesha na kuchangamsha. Tamthiliya ya aina hii inawezakutusawiria picha yakini katika maisha yetu kwa undani ikitumia dhihaka na iinavyoendeleakutuburudisha. Futuhi hulenge kurekebisha tabia inazozidhihaki au inazozichekesha.2.1.2 Maandiko Yahusuyo UfutuhiMiongoni mwa waandishi walioandika kuhusu suala la matumizi ya ufutuhi katika zafasihi ni Senkoro (1982:30). Alitumia msamiati wa ucheshi, na kusema:Ucheshi ni mbinu ya kifani ambayo wasanii huitumia katika kazi zao za fasihikuzichekesha hadhira zao, au walau kuzifanya hadhira hizo zitabasamu Wenginehutumia ucheshi ili kuwafurahisha wasomaji, wasikilizaji au watazamaji wa kazi zao;na wengine wanatumia ucheshi ili kuiepushia uchovu hadhira ya kazi zao. Wako paiawasanii ambao hutumia ucheshi ili kujenga kejeli katika kazi zao.

11Aidha, amebainisha matumizi mengine ya ucheshi kuwa ni kuundia komedia(futuhi). Pamoja na kwamba maelezo haya yanatupatia mwangaza juu ya matumiziya ufutuhi katika kazi za fasihi, kwa upande mwingine, yanatuachia maswalimuhimu kuhusiana na ufutuhi uliomo katika kazi zingine za kifasihi mfano, kwambaje, tamthiliya ya Embe dodo na Ushuhuda wa mifupa kwa upande wake zinazombinu za ufutuhi? Na kama zimo, ni aina ya mbinu ipi ya ufutuhi iliyotumikakwasilisha suala la elimu juu ya ugonjwa wa ukimwi?Kezilahabi, (1976), amegusia dhana ya ufutuhi kupitia kipengele cha ubeuzi.Alieleza ubeuzi kwa maana ya kumtania au kumchezea mtu( kwa kufanya dhihaka).Alijenga hoja zake kupitia riwaya za Kusadikika (1948) na Kufikirika (1946)alibainisha kuwa Shaaban Robert ni mwandishi aliyebobea katika matumizi yambinu ya ubeuzi kufikisha maudhui kama vile utu,amani n.k. Katika kubainishatofauti kati ya ubeuzi na vichekesho anasema: Katika ubeuzi ukweli wake unauma nakuamsha hasira. Katika vichekesho ukweli wake hauumi sana. Ubeuzi unahitajimuda wa kufikiri kwa mtu ambaye kichwa chake ni kizito Katika vichekeshotunacheka ghafula na katika ubeuzi tunafikiri na kucheka baadaye.Knapper, (1970) katika kazi yake ya Myths and Legends of the Swahili, ameoneshakwamba suala la ufutuhi lilijitokeza hata katika kazi za mwanzo za fasihi yaKiswahili. Ufutuhi huo ulijikita katika hadithi fupi na mashairi yaliyojaa kejeli namafumbo baina ya jamii moja na nyingine. Ufutuhi huo haukukusudia kuishia katikakuchekesha tu, bali pia ulitoa mafundisho fulani. Mathalani, anaonesha kuwa MrClever man and Mr simple ni miongoni mwa hadithi fupi maarufu za wakati huo.

12Kiini cha hadithi hiyo kipo katika msigano baina ya ujanja wa Mr. Cleverman nauzubavu wa Mr. Simple katika kutongoza wanawake. Mr. Cleverman anamfundishaMr. Simple mbinu mbali mbali za kuwapata wanawake. Baadaya Mr. Simpleanafuzu kukubuhu katika hilo. Hatimaye anazitumia mbinu hizo kumpata kimapenzimke wa Mr.Cleverman mwenyewe. Mr.Cleverman anaanza ugomvi dhidi yaMr.Simple baada ya kubaini uhusiano huo.Kazi hii inatupatia mwanga juu ya mambo kwamba, ufutuhi umo katika fasihisimulizi. Pili ufutuhi hutumia mbinu za kukejeli wenye lengo la kutoa ujumbe fulanikwa jamii na tatu ni kwamba ufutuhi huwa na utani ndani yake. Kwa mfano MrCleverman alikuwa akimtania Mr Simple kwa uzoba wake wa kushindwa kutongozawanawake na alipofunzika vizuri alimtongoza mke wa Mr Cleverman na hivyokuwepo ungomvi tena kati yao. Jambo hilo linachekesha.Nanjekho,(1998) alishughulikia suala la fani katika tamthiliya za Emmanuel mbogo.Katika tasnifu yake, amezungumzia umuhimu wa wasomaji kuvitambua vipengelembalimbali vya kazi ya fasihi utambuzi huo hujumuisha pia uhusishaji wa mambombalimbali kama vile mazingira na wakati wa utunzi wa kazi husika pamoja namaisha ya mtunzi kwa jumla. Kwa kufanya hivyo msomaji atakuwa katika nafasinzuri ya kuyafikia malengo na maana alizozikusudia fanani kwa hadhira yake. Kazihii ilitusaidia sana na kutusukuma zaidi katika azima yetu ya kuchunguza mbinu zaufutuhi katika tamthiliya ya Embe dodo na Ushuhuda wa mifu

"Kutathimini Mbinu za Ufutuhi Katika Kuelimisha Jamii Kuhusu Janga la Ukimwi, katika tamthiliya ya Embe Dodo ushuhuda wa mifupa nimeridhika kwamba imefikia kiwango kinachotakiwa na inafaa kuwasilishwa kwa ajili ya Utahini wa Shahada ya Uzamili ya Fasihi kwa Kiswahili ya Chuo Kikuu Huria cha . 4.2.2 Mbinu za Ufutuhi katika Ushuda wa Mifupa .

Related Documents:

Mbinu zifuatazo matokeo yake ni ya chini kuliko mbinu zote zilizotajwa mbeleni: Kondomu ya wanaume, kondomu ya wanawake, shanga za mwezi au mzunguko wa shanga, mbinu ya siku mbili. Mbinu hizi nizitumiwe vizuri sana kukuzuiya kupata mimba. Zikitumika kwa uaminifu na vizuri, si lazima kutumia mbinu ya pili. Unapohisi uko katika hatari ya kupata

na Nadharia ya Mwitiko wa M somaji na Fasihi Linganishi ndizo zilizotumika katika kuchambua data za utafiti. Mtafiti alitumia nadharia hii kwa lengo la kuwasawiri wahusika na alitumia nadharia ya Fasihi Linganishi kwa lengo la kulinganisha na kulinganua mbinu za usawiri wa wahusika katika riwaya hizi mbili. Matokeo ya utafiti yamebaini kuwa .

katika tamthiliya za Kinjeketile na Nyerere na Safari ya Kanaani: Utafiti linganishi. Ili kufanikisha utafiti huu, mtafiti ametumia mbinu za maktabani katika kukusanya na kuwasiilisha data kimaelezo. Pia marejeleo mbalimbali kutoka tamthiliya za Kiswahili yalipitiwa. Nadharia ya fasihi ya jamii ndiyo iliyotumika katika

Nyenzo za kufundisha huwa viungo muhimu wakati wa utoaji wa mafunzo. Utafiti ulichunguza matumizi ya nyenzo katika ufundishaji wa Kiswahili katika shule za msingi za umma katika Jimbo la Nyandarua, Kenya. Madhumuni ya utafiti yalikuwa: Kuainisha nyenzo zinazotumika kufundisha Kiswahili, Kutathimini kiwango cha matumizi ya

Katika nchi nyingi za Afrika, "hitaji lisilofikiwa" la upangaji uzazi liko juu. Kwa kweli, chunguzi zinaonyesha kwamba kuna watu zaidi ambao wanaweza kutumia mbinu za kupanga uzazi kama wanaweza kuzipata zaidi ya watu ambao wanazitumia tayari. Kwa maneno mengine, kama aina mbalimbali za mbinu za kupanga uzazi ambazo watu

kundi ,fanya jukumu la maana katika masomo yote.Umahiri wa maelezo maalum na wa baina ya mitaala yameshikanishwa pamoja katika muktadha wa maelezo. . baina ya mitaala katika muda wa mwaka wa shule. Kwa kufanya hivo wanaangazia kusoma kwao . na wanachukua jukumu la mchakato wao wa kimasomo. Tathmini ya kibinafsi hufanywa katika

Lugha huja katika sehemu za maneno Maneno huweza kuvunjwa kuwa silabi Silabi huweza kuvunjwa kuwa sehemu ndogo zaidi zinazoitwa fonimu Baadhi ya mbinu ambazo walimu wanaweza kutumia kuwafundisha watoto dhana kuhusu kusoma na kuandika ni mbinu ya Uzoevu wa Lugha, Kushirik

Safety-sensitive employees of city, county or other public transit services are subject to alcohol and drug testing requirements under rules issued by the Federal Transit Administration (FTA), a DOT agency. Additionally, employees who operate a vehicle requiring a commercial driver's license (CDL) are subject to substance abuse testing. This expansion of the scope of the Federal Motor Carrier .