Yesu Katika India - Islam Ahmadiyya

1y ago
14 Views
2 Downloads
696.20 KB
133 Pages
Last View : 10d ago
Last Download : 3m ago
Upload by : Warren Adams
Transcription

YESU KATIKA INDIAIkiwa ni taarifa ya kuepukana kwakeYesu na kifo juu ya msalaba na safariyake ya kwenda IndiaKimetungwa na:HADHRAT MIRZA GHULAM AHMADWA QADIANMwanzilishi wa Jumuiya ya Ahmadiyya katika IslamKimetafsiriwa kutoka Kiingereza na Bwana MohammedSaidi Kibindu wa Dar es SalaamTafsiri ya Kiswahili imetangazwa na:JUMUIYA YA WAISLAMU WAAHMADIYYA TANZANIAS.L.P. 376SIMU: 2110473 FAX: 2121744DAR ES SALAAM.1

YESU KATIKA INDIAMwandishi: Hadhrat Mirza Ghulam Ahmad a.s.Mfasiri:Bwana Muhammed Said Kibindu Ahmadiyya Muslim Jamaat TanzaniaChapa ya kwanza:Nakala:20003000Kimechapwa naAhmadiyya Printing PressP.O. Box 376Simu: 2110473, Fax 2121744Dar us SalaamTanzania.2

YALIYOMO1.Neno la Mbele.42.Utangulizi.73.Sura ya Kwanza.214.Sura ya Pili.565.Sura ya Tatu.626.Sura ya Nne.72I.Sehemu ya Kwanza . . . . . . . . . . . . . . . . .72II.Sehemu ya Pili.78III.Sehemu ya Tatu.987.Viambatanisho.1123

NENO LA MBELE"YESU NCHINI INDIA" ni tafsiri ya KISWAHILI ya "MasihiHindustan Mein" ambacho ni kitabu cha Kiurdu kilichoandikwana Mwanzilishi Mtukufu wa Jumuiya ya Ahmadiyya katika Islam,Hadhrat Mirza Ghulam Ahmad a.s. (1835-1908).Mada kubwa iliyofafanuliwa katika kitabu hiki ni kuepushwakwake na kifo cha fedheha juu ya msalaba na safari yake yakwenda India kuyatafuta makabila yaliyopotea ya wana waIsraeli ambao ilikuwa lazima awakusanye na kuwaingiza katikazizi lake kama ilivyotajwa katika Agano Jipya.Ushahidi chungu nzima umekwisha patikana katika Maandikoya Kikristo na pia ya Kiislamu, vitabu vya zamani vya tiba na piavya historia, ikiwa ni pamoja na kumbukumbu za kale za Kibuddhakatika kulifafanua jambo hili.Akiwa ameianza safari yake kutoka Yerusalemu na akiwaamepitia Nasibus, na Iran, Yesu anaonyeshwa kuwa alifikaAfghanistan ambako alikutana na Wayahudi waliokaa pale baadaya kutolewa utumwani kwa Nebachadnezzar.Kutoka Afghanistan Yesu alikwenda Kashmir ambako piabaadhi ya makabila ya Waisraeli yalikaa. Alipofanya mahali hapakuwa maskani yake na ndipo mahali alipofia. Kaburi lakelimetafutwa na kukutwa katika mtaa wa Khanyar, mjini Srinagar.Kwenye sehemu inayoshughulika na ushahidi uliopatikanakatika kumbukumbu za kale za Kibuddha Hadhrat Ahmadametatua swali ambalo kutokana na hali yake ya ugumu limekuwakwa muda mrefu likiwatatiza waandishi wengi wa Kimagharibi.Waandishi hawa wamefumbwa na kufanana kwa ajabukunakopatikana baina ya mafundhisho ya Kibuddha na yale yaKikristo na kati ya matukio ya maisha ya wote wawili Yesu naBuddha kama ilivyofunuliwa katika maandiko ya kila mmoja wao.Baadhi ya waandishi hawa wanashikilia maoni kwamba kwavyo vyote vile mafundisho ya Kibudha ni lazima yawe yalifika4

Falastwini na kutumiwa na Yesu katika mahubiri yake. Lakinihakuna kabisa uthibitisho wa kihistoria wa kuunga mkono nadhariahii.Msafiri wa Kirusi aitwae Nicolas Notovitch aliishi kwa kipindikirefu na Walama wa Tibet na wakamtafsiria vitabu vyao vitakatifu.Yeye ana maoni kwamba Yesu lazima alikuja Tibet kabla yakusulubiwa kwake na kurudi Falastwini baada ya kujifunzamafundisho ya Kibuddha. Haya pia ni matamshi tu ambayohayaungwi mkono na ushahidi wa kihistoria wenye kuaminika.Akiyakanusha maoni hayo ya namna mbili, Hadhrat Ahmadanaandika kwamba Yesu alikuja India siyo kabla ya tukio laMsalaba bali baada yake na kwamba si yeye aliyekopa mafundishoya Kibuddha bali ni wafuasi wa Buddha wanaoonekana kuwawameichapisha upya picha ya Injili zote katika vitabu vyao.Kulingana na Hadhrat Ahmad, Yesu pia alitembelea Tibetwakati wa safari zake nchini India akiyatafuta makabila yaliyopoteaya Israeli. Alihubiri ujumbe wake kwa watawa wa Kibuddha ambaobaadhi yao walikuwa Wayahudi waliojiunga na dini hiyo yaKibuddha. Wafuasi wa Buddha waliathirika sana na mafundishoyake na wakamchukulia yeye kuwa ni udhihirisho wa Buddha namwalimu wao Aliyeahidiwa. Wakiwa wanamwamini kama Bwanawao, wakayachanganya mafundisho yake na yale yaliyomo katikakumbukumbu zao na wakayahesabu yote kwa pamoja ni yaBuddha. Ushahidi wa kutosha wa kuunga mkono maoni hayaunapatikana katika kumbukumbu za kale za Kibuddha.'Masih Hindustan mein' kiliandikwa mnamo mwaka 1899na ni kiishilizio cha zama ambamo kwa karne nyingi Waislamuna Wakristo waliamini Yesu kupaa mbinguni. Kikiwa ni kitabu chakwanza pekee kilichoandikwa kuhusu suala hili kwa mjio wa kiakili,kitabu hiki kilileta kishindo kikubwa.Hoja zake zilitangazwa na katika nusu karne iliyopitakimepata mafanikio ya kutosha katika kumwondolea Yesu sifaza uwongo za kiungu na kumwonyesha hadharani mbele yaulimwengu akiwa nabii mtakatifu ambavyo kwa hakika ndivyoalivyokuwa.5

Katika nyanja za Kiislamu kishindo cha kitabu hiki kilikuwakikubwa sana kiasi kwamba Mufti wa Chuo Kikuu cha Al-Azharjijini Cairo, alitoa Fatwa kwamba kulingana na Qur an Tukufu Yesualikufa kifo cha kawaida. Mvuto wake wa kuzishawishi fikra zaKikristo pia ulikuwa wa kusumbua sana.Ingawa hakuna kitabu kingine miongoni mwa maandiko yakechenye jina hili, hata hivyo Hadhrat Ahmad aliyajadili kikamilifumasuala yote haya pamoja na mengine mengi muhimu kuhusuukweli wa Islam, ukweli wa madai yake na ukweli kuhusu kifocha Yesu katika vitabu vingi tu alivyoviandika baada ya hichokilichotajwa hapo juu.Tafsiri ya Kiingereza ilifanywa na Qazi Abdul Hamidaliyekuwa mhariri wa jarida la kila juma liitwalo: "The Sunrise" laLahore ambamo ilichapishwa kwa mfululizo katika kipindi chamiaka ya 1938 hadi 1939. Ilitangazwa kwa mara ya kwanza katikasura ya kitabu mnamo mwaka 1944 na Nashrul-Ishaat SadrAnjuman Ahmadiyya, Qadian.Pamoja na wengine wote waliotusaidia kwa njia moja aunyingine katika uchapishaji wa kitabu hiki, shukrani zetu nyingizimwendee Bwana Mauloud Ahmad Khan, aliyekuwa Imam waMsikiti wa London ambaye alijitolea sana kuzikusanya nukuuzinazohusika kutoka katika vitabu vya asili vilivyorejewa na HadhratAhmad katika kulithibitisha jambo hili.Nukuu hizozimeunganishwa na kitabu hiki kwa mpangilio wa viambatanishonamba 1 hadi namba 18.Mei, 1962Wakilut - TabshirTahrik Jadid,Rabwah, Pakistan6

KWA JINA LA MWEZI MUNGU, MWINGI WA REHEMA,MWINGI WA UKARIMU. TUNAMHIMIDIA YEYENA TUNAMSALIA MTUME WAKE MTUKUFU S.A.W.Ee Mola! Hukumu baina ya watu wetu kwa haki.Hakika wewe U m bora wa mahakimu.UTANGULIZINimeandika kitabu hiki ili, kwa kuleta uthibitisho kutoka kwenyeukweli ambao umekwisha kubalika na kutoka kwenye ushuhudawa kihostoria usiokuwa na shaka na wenye kuthaminiwa, nakutoka kwenye nyaraka za kale za wasiokuwa Waislamu, niwezekuondoa mawazo potofu sana ambayo yamezagaa miongonimwa Waislamu na miongoni mwa takriban madhehebu zote zaKikristo kuhusu maisha ya mwanzoni na ya baadaye ya Yesu(amani juu yake) - mawazo potofu ambayo athari zake za hatarisiyo tu zimelidhuru na kuliteketeza wazo la kuwako kwa umojawa Mungu, bali pia ushawishi usiofaa na wenye sumu kwa mudamrefu umekuwa ukionekana katika maadili ya Waislamu wa nchihii (India). Maradhi ya kiroho, yaani utovu wa maadili mema,mawazo machafu, ukatili na utovu wa huruma vinaendeleamiongoni mwa firqa za Kiislamu na ni matokeo ya kuziaminihadithi na hekaya kama hizi zisizokuwa na msingi. Huruma yabinadamu, majuto na kupenda haki, upole na unyenyekevu - sifazote nzuri zinatoweka siku hadi siku, kana kwamba hivi karibunizitaiaga jamii hii. Ukatili huu na utovu huu wa maadili memaunawafanya Waislamu wengi waonekane kama wanyama waporini. Mfuasi wa Buddha ambaye katika dini ya Kibuddha huitwaJain huogopa na hujiepusha na kuua hata mmbu au kiroboto,lakini lo! wako wengi miongoni mwa sisi Waislamu ambao wanauamtu asiyekuwa na hatia au kufanya mauaji yasiyokuwa na mipaka,hawamuogopi Mwenyezi Mungu mwenye nguvu ambayeameyakadiria maisha ya binadamu kuwa ya daraja la juu kulikoyale ya wanyama wote. Lakini huu ukatili na dhuluma na utovuwa huruma vinasababishwa na nini? Vinasababishwa na jambo7

hili - kwamba tangu wakati wa utoto wao, hekaya na hadithi nafikra potofu za itikadi ya Jihadi vinaimbwa ndani ya masikio yaona kushinikizwa katika mioyo yao, matokeo yake yakiwa kwambapolepole wanakufa kiroho na kutokuhisi ubaya wa vitendo vyaovya kuchukiza; la, bali yule mtu anayemwua mtu mwingine bilakutarajiwa na hivyo kuleta maangamizi kwenye familia ya mtualiyeuawa, hudhania kwamba amefanya kitendo kinachostahili;au tuseme, kwamba ameitumia vema fursa ya kujipatiaupendeleo kutoka kwa jamii yake. Kwa vile hakuna mafundishoau hotuba zinazotolewa nchini mwetu kuzuia uovu wa namnahiyo - na iwapo kuna mafundisho yo yote ya namna hiyo yanaviini vya unafiki ndani yake - watu - wa kawaida huwa na fikra zakuviunga mkono vitendo hivyo viovu. Kwa hiyo basi, kwakuwahurumia watu wangu mwenyewe, nimetunga vitabu kadhaa,kwa Kiurdu, Kiajemi na Kiarabu ambamo nimesema kwambamaoni yanayoshikiliwa na watu wote kuhusu Jihadi ambayoyamezagaa miongoni mwa Waislamu, yaani, kusubiriwa kwaImamu mwenye kumwaga damu aliyejawa na chuki na uaduikwa watu wengine ni mfumo wa imani potofu zilizofundishwa namaulamaa wasioona mbali; vinginevyo, Islam hairuhusu utumiajiwa upanga kuieneza Imani hii; isipokuwa wakati wa vita vyakujihami au wakati wa vita zinazopiganwa ili kumwadhibumdhalimu au kutetea uhuru. Haja ya kuwepo kwa vita ya kujihamiinakuja wakati ambapo uchokozi wa adui unahatarisha maishaya mtu. Basi hizo ndizo aina tatu za Jihadi zinazoruhusiwa nasheria, na kinyume cha hizi aina tatu, hakuna aina nyingine yavita ambayo inaruhusiwa na Islam katika kuizagaza Imani. Kwakifupi nimetumia kiasi kikubwa cha fedha katika kuvichapishavitabu hivyo na nimevitangaza humu nchini, na nchini Arabia naSyria na Khurasan na kadhalika. Lakini kwa msaada wa MwenyeziMungu sasa nimegundua hoja zenye nguvu sana ambazozitatumika katika kuzifutilia mbali imani hizi potofu mioyoni mwawatu. Ninao uthibitisho ulio wazi, ninao ushahidi wa kimazingirausiokuwa na shaka, na ninao ushahidi wa kihistoria ambao nuruya ukweli wake inaleta matumaini makubwa kwamba mara baada8

ya kutangazwa kwa ushahidi huo patatokea mabadiliko ya ajabukatika nyoyo za Waislamu dhidi ya imani hizo potofu. Na natumainibali nina hakika kwamba baada ya mambo haya ya kwelikufahamika, zitabubujika kutoka katika mioyo ya wachamunguwana wa Islam zile chemchem tamu na safi za unyenyekevu,huruma na amani, na kwamba yatatokea mabadiliko ya kirohoambayo yatakuwa na ushawishi mzuri na wenye baraka nyingikatika nchi hii (India). Nina uhakika pia kwamba wachunguzi waKikristo na watu wengine wote wanaoutamani na wenye kiu yakuupata ukweli huu, watafaidika sana na vitabu vyangu. Na huuukweli nilioutaja hivi punde, kwamba shabaha halisi ya kitabu hikini kuzisahihisha imani potofu ambazo zimekuwa sehemu yakanuni za imani za Waislamu na Wakristo, unahitaji maelezokidogo ambayo nayatoa hapa chini.Naifahamike kwamba takriban Waislamu na Wakristo wotewanaamini kwamba Yesu (amani ya Mungu juu yake) alipaambinguni akiwa hai; watu wote hawa waliendelea kuamini kwamuda mrefu kwamba Yesu (amani juu yake) yungali hai hukombinguni na baadaye katika siku za mwishoni atashuka ardhini.Tofauti iliyopo katika maoni yao, yaani maoni ya wafuasi waIslam na yale ya Wakristo ni hii tu kwamba Wakristo wanaaminikwamba Yesu (amani juu yake) alifia msalabani, alifufuliwa, naalipaa mbinguni akiwa na mwili wake, aliketi mkono wa kulia waBaba yake, na atakuja duniani katika siku za baadaye ili kujakuhukumu, wanasema pia kwamba Mwumbaji na Bwana waulimwengu huu ni huyu huyu Masihi Yesu na si mwingine ye yote;yeye ndiye yule ambaye katika siku za mwisho wa dunia atashukaardhini kwa mshuko wa utukufu ili kuja kutoa adhabu na thawabu;kisha, wale wote ambao hawatamwamini yeye au mama yakekama Mungu, watakokotwa na kutupwa jahanamu ambamo kaziyao itakuwa kulia na kuomboleza. Lakini firqa zilizokwisha semwaza Waislamu zinasema kwamba Yesu (amani juu yake)hakusulubiwa; isipokuwa, wakati Mayahudi walipomtia mbaroniili kumsulubu malaika wa Mungu alimchukua na kumpelekambinguni akiwa na mwili wake wa kidunia na bado yungali hai9

huko mbinguni - ambayo wanaiita mbingu ya pili ambako pia yukonabii Yahya, yaani Yohana. Zaidi ya hayo Waislamu wanasemapia kwamba Yesu (amani juu yake) ni nabii mashuhuri waMwenyezi Mungu, lakini si Mungu wala si mwana wa Mungu nawanaamini kwamba katika siku za akheri zamani atashuka ardhinikaribu na Mnara wa Demeshki au karibu na sehemu nyingineakiwa amebebwa juu ya mabega ya malaika wawili, na kwambayeye na Imam Muhammad Mahdi ambaye atakuwa tayari yukoulimwenguni, na ambaye atakuwa ametokana na uzao waFaatimah, watawaua wote wasiokuwa Waislamu bila kumwachaye yote hai isipokuwa wale ambao pale pale na bila kuchelewawatasilimu.Kwa ufupi shabaha halisi ya kushuka duniani kwa Yesu(amani juu yake) isemwavyo na firqa za Kiislamu ziitwazo AhliSunna au Ahli-Hadithi ambazo watu wa kawaida wanaziitaWahabii - ni hii kwamba, kama alivyofanya Mahadev wa Wahindu,ni lazima auteketeze ulimwengu wote; kwamba ni lazima kwanzaawalazimishe watu kusilimu na kisha iwapo wataendeleakutokuamini awaue wote kwa upanga; zaidi ya hayo wanasemakwamba yeye yu hai mbinguni akiwa na mwili wake wa kidunia ilinguvu za Kiislamu zitakapodhoofika ateremke na kuwauawasiokuwa Waislamu au kuwalazimisha kwa kuwatia uchungumkali ili wasilimu. Kuhusiana na Wakristo, hususan viongozi wafirqa hizo zilizokwisha tajwa, wanasema kwamba wakati Yesu(amani juu yake) atakapoteremka kutoka mbinguni atavunjamisalaba yote ulimwenguni, atafanya vitendo vingi vya kikatili kwakutumia upanga, na ataujaza ulimwengu kwa mafuriko ya damu.Na kama nilivyokwisha sema, hawa watu, yaani Ahli-Hadithi nakadhalika watokao miongoni mwa Waislamu wana jazba kubwasana kuhusu hii imani yao kwamba muda mfupi kabla yakuteremka Masihi atatokea Imam kutoka miongoni mwa BaniiFaatima ambaye jina lake litakuwa Muhammad Mahdi. Huyu ndiyeatakayekuwa Khalifa na Mfalme wa wakati ule, na kwa kuwaatatokana na Wakureshi, shabaha yake halisi itakuwa kuwauawote wasiokuwa Waislamu isipokuwa wale ambao wataitamka10

Kalima mara moja. Yesu (amani juu yake) atateremka ilikumsaidia huyu Imam katika kazi hiyo; na ingawa Yesumwenyewe (amani juu yake) atakuwa Mahdi, la, bali Mahdimkubwa zaidi -hata hivyo kwa kuwa Khalifa wa zama hizo lazimaawe Mkureshi, Yesu (amani juu yake) hatakuwa Khalifa wa zamahizo. Khalifa wa zama hizo atakuwa huyo huyo Muhammad Mahdi.Wanasema kwamba hawa wawili kwa pamoja wataijaza duniakwa damu ya binadamu, na watamwaga damu nyingi zaidi kulikoiliyowahi kumwagwa hapo kabla katika historia ya ulimwengu huu.Mara tu watakapojitokeza wataanza kampeni hii ya umwagajidamu. Hawatahubiri wala kumsihi mtu wala kuonyesha isharayo yote. Na pia wanasema kwamba ingawa Yesu (amani juu yake)atakuwa kama mshauri au naibu wa Imam Muhammad Mahdi,na ingawa hatamu za uongozi zitakuwa miongoni mwa Mahdipeke yake, Yesu (amani juu yake) atamchochea Hadhrat ImamMuhammad Mahdi kuua watu wote ulimwenguni na atamshaurikuchukua hatua kali, yaani atayafanyia marekebisho yalemafundisho yake ya kuhurumiana aliyoyatoa hapo kabla, yaani,usishindane na shari yo yote na maovu, na "ukipigwa shavu mojaugeuze jingine pia."Hivi ndivyo Waislamu na Wakristo waaminivyo kumhusuYesu (amani juu yake), na wakati ambapo ni kosa kubwawafanyavyo Wakristo kumwita binadamu mnyonge "Mungu,"imani za baadhi ya wafuasi wa Islam, miongoni mwao ikiwamohii firqa inayoitwa Ahli-Hadithi ambayo pia inajulikana kamaWahabii, kuhusu Mahdi mwenye kumwaga damu na Masihimwenye kumwaga damu, zinaathiri maadili yao vibaya sana, kwakiasi hiki ambapo kutokana na ushawishi mbaya wa imani hizo,ushirikiano wao na watu wengine hauko katika misingi ya uaminifuna nia nzuri wala hawawezi kuwa watiifu kikwelikweli na kikamilifukwa serikali isiyokuwa ya Kiislam. Watu wote wenye busarawatatambua kwamba imani kama hiyo, yaani kwamba wasiokuwaWaislamu washurutishwe, kwamba imma wasilimu mara mojaau wauawe ni lazima itapingwa kwa njia zote. Kila mtu mwenyekupenda mema atakubali mara moja kwamba kabla mtu11

hajatambua vya kutosha ukweli wa imani fulani, na kablahajatambua uzuri wa imani hiyo na mafundisho yake safi, haifaikabisa kumshurutisha kwa njia ya kumtia machungu makali iliaikubali Imani hiyo.Kinyume kabisa cha kuchangia katika ukuwajiwa Imani hiyo, kitendo hicho kitawapatia wapinzani fursa ya kuitoamakosa. Matokeo ya mwisho ya kanuni hii ni kwamba nyoyozitakuwa zimehamwa na ile sifa ya huruma ya kibinadamu nakwamba amani na haki ambazo ni sifa kuu za maadili yakibinadamu zinamhama mtu kabla na badala yake chuki na uaduivinaelekea kuota mizizi; zinazosalia nyuma ni silika za kinyamatu zikiendelea kufutilia mbali maadili yote mema. Lakiniitatambulika kwamba fundisho kama hilo halitakuwa limetoka kwaMwenyezi Munngu, ambaye hashushi adhabu Yake isipokuwa tubaada ya kukamilisha hoja Zake.Kwa hiyo jambo hili ni lazima lifikiriwe kwa makini: Kwambaiwapo kuna ambaye haikubali Imani ya kweli kwa sababu badoyungali mjinga na hajui ukweli wake, hajui mafundisho yake nahajui uzuri wake, je, itakuwa jambo la busara kumwua mtu wanamna hiyo mara moja? Sivyo, mtu huyu anastahili kuhurumiwa;anastahili kufundishwa polepole kwa heshima kuhusu ukweli,uzuri na faida za kiroho za imani ile; siyo akikataa basi kukataakwake kujibiwe kwa upanga au bunduki.Kwa hiyo, itikadi ya Jihadi inayopendekezwa na firqa hizi napia ile imani kwamba wakati umekaribia ambapo patatokea Mahdimwenye kumwaga damu ambaye jina lake litakuwa ImamMuhammad, na kwamba Masihi atateremka kutoka mbinguni ilikuja kumsaidia, na kwamba hao wawili kwa pamoja watawauawatu wote wasiokuwa Waislamu iwapo wataukataa Uislam, yotehaya ni kinyume kabisa na maadili ya kiakili. Je imani hii siyo ileimani ambayo inaua sifa zote nzuri na maadili mema ya binadamuna kutilia nguvu sifa za maisha ya porini? Wale wanaoshikiliaimani kama hizi wanaishi maisha ya kinafiki kwa kulinganishwana watu wengine, kwa kiasi hiki kwamba hawawezi kuonyeshautii wa kweli kwa viongozi wa serikali wa Imani nyingine, wanaapakiudanganyifu kuwa watiifu kwa viongozi hao, ambalo ni kosa.12

Hii ndiyo sababu baadhi ya firqa za Ahli-Hadithi nilizozitaja hivipunde zinaishi maisha ya namna mbili chini ya serikali yaKiingereza katika India inayotawaliwa na Uingereza. Kisirisiriwanawapa matumaini watu wa kawaida kuhusu ujaji wa siku zaumwagaji damu za Mahdi mwenye kumwaga damu nakuwafundisha jinsi watakiwavyo kufanya wakati huo, lakiniwanapokwenda kwa viongozi wa serikali wanawasifu kwa sifaza uwongo na kuwahakikishia kwamba wao hawaungi mkonomawazo ya namna hiyo. Lakini kama ni kweli kwamba waohawaungi mkono mawazo ya namna hiyo, kwa nini hawatangazimsimamo wao huo kimaandishi na kwa nini wao waendeleekusubiri ujaji wa yule Mahdi na Masihi ambao kama isemwavyowako kwenye kizingiti cha mlango tu, wakiwa tayari kuja kuungananao katika kampeni zao?Kwa kifupi imani kama hizo zimeharibu kwa kiwango kikubwasana tabia za Mashekhe hawa; hawana uwezo wa kuwafundishawatu adabu wala amani. Kwa upande mwingine, kuwaua watuwengine bila sababu ya msingi, kwao ni wajibu mkubwa wa kidini.Ningefurahi sana kama firqa yo yote ya Ahli-Hadithi ingezipingaimani hizi, lakini kwa masikitiko makubwa siwezi kujizuia kusemakwamba miongoni mwa hizi firqa za Ahli-Hadithi(1) wako waleambao kwa sirisiri wanaamini kufika kwa Mahdi mwenyekumwaga damu na dhana zilizoenea kuhusu Jihadi. Hawazikubalifikra sahihi na wanakihesabu kitendo cha kuua kwamba ni chenyekustahili pale wapatapo fursa ya kuwaua watu wanaoungamaimani zingine, wakati ambapo hizi imani za kuwaua watu wenginekwa jina la Islam, au kuziamini tabiri kama huu utabiri wa kujaMasihi mwenye kumwaga damu na kutaka kuiendeleza silsila ya(1) Baadhi ya Ahli-Hadithi wanasema isivyopasa na bila haki yo yote katikavitabu vyao kwamba kufika kwa Mahdi kumekaribia sana: Kwamba atawatiagerezani watawala wa Kiingereza wa India na kwamba mfalme wa Kikristoatakamatwa na kuletwa mbele yake. Vitabu kama hivyo bado vinawezakupatikana katika nyumba za hawa Ahli-Hadithi, kimojawapo kikiwa IqtarabusSa'at cha Ahli-Hadithi aliye mashuhrui sana, ambamo katika ukurasa wa 64taarifa kama hiyo inaweza kuonekana.13

Islam kwa umwagaji damu au kwa vitisho, ziko kinyume kabisana Qur an Tukufu na Hadithi zenye kuaminika. Mtume wetuMtukufu (amani na rehema za Mwenyezi Mungu juu yake) alipatamateso makali sana mikononi mwa makafiri akiwa Makka na piabaadaye. Miaka kumi na mitatu aliyokaa Makka ilikuwa miaka yausumbufu na mateso ya kila aina - kuifikiria miaka hiyokunasababisha machozi yatiririke katika macho ya mtu. Lakiniyeye hakuinua upanga dhidi ya maadui zake, wala hakuujibuuchokozi wao mpaka wengi miongoni mwa masahaba zake narafiki zake wapenzi walipouawa kinyama; na mpaka yeyemwenyewe alipotiwa katika mateso ya kila namna kama vilekutiliwa sumu mara nyingi; na mpaka majaribio mengi ya kutakakumwua yalipofanywa. Lakini ulipizaji wa Mwenyezi Munguulipowadia, ikatokea kwamba wazee wa Makka na machifu wamakabila mbalimbali kwa pamoja waliamua kwamba kwa vyovyote vile mtu huyu ni lazima auawe. Wakati ule ule, MwenyeziMungu ambaye Ndiye Msaidizi wa wapendwa Wake na Msaidiziwa wakweli na wachamungu, Alimjulisha yeye kwamba hakunakilichosalia katika mji ule isipokuwa ouvu, na kwamba watu wamji ule walikuwa wamejiandaa kumwua na kwamba ni lazimaauhame mara moja. Kisha kulingana na amri ya kimbingu alihamiaMadina, lakini pamoja na hatua zote hizo maadui zakehawakumwachilia; wakamfuata kule na wakataka kuuteketezaUislam kwa njia yo yote ile. Wakati urukaji wao mipaka ulipofikiakikomo, na walipokuwa wao wenyewe wamejihalalishia adhabukwa kuwaua watu wengi wasiokuwa na hatia, ambao waliwauasiyo katika ugomvi au vita bali hivi hivi tu, kutokana na utunduwao wa kuleta madhara, na ambao waliwanyang anya mali zao.Lakini, licha ya yote haya, wakati Makka ilipotekwa Mtume wetuMtukufu (amani na rehema za Mwenyezi Mungu juu yake)aliwasamehe wote hao. Kwa hiyo ni makosa makubwa na sijambo la haki kudhani kwamba Mtukufu Mtume (amani na rehemaza Mwenyezi Mungu juu yake) au Masahaba zake waliwahikupigana kwa nia ya kueneza Imani, au kwamba waliwahikumlazimisha mtu ye yote kujiunga na silsila ya Islam.14

Ni jambo la kuzingatiwa pia kwamba kwa kuwa wakati ulewatu wote walikuwa na chuki dhidi ya Islam, na kwa kuwawapinzani walikuwa wanafanya mpango wa kuuteketeza Uislamambao waliudhania kuwa ni dini mpya ambayo wafuasi wake nijumuiya ndogo tu, na kwamba kila mtu alikuwa na shauku yakuona Waislamu wakiteketezwa mapema au kusambaratishwaili pasiachwe hofu ya hao kuongezeka zaidi na kujiendeleza,Waislamu wa wakati ule waliwekewa vipingamizi hata katikamambo madogo sana, na mtu ye yote kutoka katika kabila lo lotealiyeupokea Uislam na akawa Mwislamu, imma aliuawa maramoja na watu wa kabila lake au aliishi katika hatari ya kudumu.Katika wakati kama huu, Mwenyezi Mungu, Akiwahurumia walewaliojiunga na Islam, Aliwatwisha adhabu watawala wadhalimu,yaani wawe wasaidizi kwa Islam na hivyo kufungua milango yauhuru wa Islam. Hii ilikuwa na shabaha ya kuondoa vipingamizikatika njia ya wale waliotaka kuikubali Imani hii; ilikuwa ni hurumaya Mwenyezi Mungu kwa ulimwengu na haikumdhuru mtu ye yote.Lakini ni jambo lililo bayana kwamba watawala wasiokuwaWaislamu wa siku hizi hawajiingizi katika masuala ya Islam;hawapigi marufuku sunna muhimu za Kiislam. HawawauiWaislamu wapya; hawawatii gerezani au kuwatesa; kwa nini basiIslam iinue upanga wake dhidi ya watu hawa? Ni dhahiri kwambaIslam haijawahi kushabikia ulazimishaji. Iwapo Qur an Tukufu,vitabu vya Hadithi na kumbukumbu za historia vitachunguzwakwa uangalifu na pale inapowezekana iwapo vitasomwa aukusikilizwa kwa makini, itafahamika kwa yakini madai kwambaIslam ilitumia upanga ili kueneza Imani hiyo kwa nguvu ni madaiya aibu na yasiyokuwa na msingi dhidi ya Islam.Dai kama hilo dhidi ya Islam linafanywa na watu ambao badohawajaisoma Qur an, Hadithi na taarikhi za kuaminika za Islamkatika hali ya kujitegemea wao wenyewe, bali wameutegemeasana uwongo na kwa hiyo wakaleta madai yenye makosa dhidiya Islam. Lakini najua kwamba wakati umeisha karibia ambapowale wenye njaa na kiu ya kutafuta ukweli watatiwa nuru ya kujuaiwapo kuna ukweli wo wote katika madai haya. Je tunaweza15

kuielezea Imani hii kuwa ni imani ya kutumia nguvu wakati kitabukitakatifu Qur an, kinaelekeza wazi kwamba hakuna ushurutishajikatika mambo ya dini na kwamba hairuhusiwi kutumia shuruti aunguvu katika kumfanya mtu ajiunge na Islam? Je tunawezakumshitaki Mtume yule Mkuu kwamba alitumia mabavu dhidi yawatu wengine, ambaye usiku na mchana kwa miaka kumi namitatu aliwahimiza Masahaba zake wote mjini Makka wasirejesheuovu waliotendewa na maadui, bali wavumilie na kusamehe?Lakini wakati fujo ya maadui ilipopita kiasi na wakati kila mtualipokuwa anajitahidi kuufutilia mbali Uislam, Mwenyezi Mungumwenye ghera Aliamua kwamba ulikuwa ni wakati muafaka walewatu waliopigana kwa upanga lazima wateketezwe kwa upanga.Waila Qur an Tukufu haijaidhinisha kulazimisha. Kamakulazimisha kungeidhinishwa na Islam, Masahaba wa Mtumewetu Mtukufu (amani na rehema za Mwenyezi Mungu juu yake)wasingeonyesha tabia ya watu wakweli na wanyoofu, wakati wamajaribu. Lakini utiifu na uaminifu wa masahaba wa Bwana wetuMtukufu Mtume (amani na rehema za Mwenyezi Mungu juu yake)ni jambo ambalo sina haja ya kulitaja. Si jambo la siri kwambamiongoni mwao kuna mifano ya msimamo imara ambao ni vigumukupata cha kuwalinganisha nao katika taarikhi za mataifa mengine;kundi la waaminio halikutetereka katika utiifu na msimamo waoimara hata walipokuwa chini ya kivuli cha upanga. Bali wakiwapamoja na Mtume wao Mkuu na Mtukufu walitoa uthibitisho waule msimamo imara ambao hakuna mtu awezaye kwa vyo vyotevile kuuonyesha mpaka moyo wake na kifua chake viwe vimetiwanuru ya imani ya kweli. Kwa kifupi hakuna kulazimisha katikaIslam. Vita katika Islam ni vya aina tatu: (1) vita ya kujihami, yaanivita kwa sababu ya kujilinda; (2) vita ya kuadhibu, yaani damukwa damu; (3) vita ya kupata uhuru, yaani vita ya kuvunja nguvuya wale wanaowaua wale wanaojiunga na Islam.Kwa hiyo kwa kuwa hakuna maelekezo katika Islam kwambakila mtu aingizwe huku kwa kulazimishwa au kwa kutishiwakuuawa, ni jambo la upuuzi mtupu kusubiri kutokea kwa Mahdiau Masihi ye yote mwenye kumwaga damu. Haiwezi kutokea16

kamwe kwamba katika ulimwengu huu atokee mtu ambayekinyume na mafundisho ya Qur an atumie upanga kuwasilimishawatu. Hili si jambo gumu kutambua wala haliko nje ya uwezo wamtu wa kufahamu. Ni watu wajinga tu walioangukia imani hiikutokana na uchoyo wao. Kwani takriban Mashekhe wetu wotewanajihangaisha na fikra zao potofu kwamba vita atakazopiganahuyu Mahdi zitawaletea utajiri mwingi sana kiasi kwambawatakuwa hawana mahali pa kuhifadhia utajiri huo, na kwa kuwatakriban Mashekhe wote wa hivi sasa ni watu walio fukara sana,wanasubiri usiku na mchana kutokea kwa huyo Mahdi ambayewanadhani atakuja kukidhi hizo tamaa zao za kiuchoyo. Kwa hiyowatu hawa humpinga kila mtu ambaye haamini kutokea kwa Mahdiwa namna hiyo; mtu wa namna hiyo atatangazwa mara mojakuwa ni Kaafir na yuko nje ya wigo wa Islam. Kwa hiyo mimi pianimekuwa Kaafir machoni pa watu hawa; na nimepewa ukafirihuo kwa misingi hiyo hiyo. Kwani, mimi siamini kutokea Mahdimwenye kumwaga damu na Masihi mwenye kumwaga damu.La, bali nayachukia mawazo ya kipuuzi ya namna hiyo nanayadharau sana. Na nimetangazwa kuwa Kaafir siyo tu kwasababu ya kukanusha kwangu kutokea kwa huyo anayesemekanakuwa Mahdi na huyo anayesemekana kuwa Masihi ambaowanaamini, bali pia nimetangaza hadharani baada ya kujulishwajambo hili na Mwenyezi Mungu kwa njia ya ufunuo kwamba MasihiAliyeahidiwa halisi na wa kweli ambaye pia ndiye Mahdi wa kweliambaye ishara za kutokea kwake zinapatikana katika Biblia naQur an na ambaye kuja kwake kumeahidiwa pia katika Hadithi, nimimi mwenyewe; lakini ni mimi ambaye sikupewa upanga wowote wala bunduki. Nimeamrishwa na Mwenyezi Mungu kuwaitawatu kwa unyenyekevu na upole kwa Mwenyezi Mungu Ambayendiye Mungu wa kweli, na milele na Asiyebadilika Ambaye anaUtakatifu uliokamilika, Ujuzi uliokamilika, Amani iliyokamilika naHaki iliyokamilika.Mimi ndiye nuru ya zama hizi za giza; yule ambaye atanifuatamimi ataokolewa katika kutumbukia ndani ya shimo lililotayarishwana Shetani kwa ajili ya wale wanaotembea katika giza.17

Nimeletwa na Mwenyezi Mungu ili kuwaongoza watu waulimwengu huu kwa Mungu wa kweli kwa njia ya amani na upolena kuzifunga upya hatamu za maadili mema katika Islam.Mwenyezi Mungu amenipatia ishara za kimbingu kwa ajili yakuwaridhisha wale wenye kutafuta haki. Amefanya mambo yaajabu katika kuniunga mkono; Amenifunulia siri za mambo yaghaibu na za mambo yajayo baadaye ambayo kulingana na vitabuvitakatifu ni ishara za mdai wa kweli wa ofisi ya kimbingu, naAkanijaalia elimu safi na takatifu. Kwa hiyo, zile nafsi ambazozinachukia ukweli na zinafurahishwa na giza zikaamua kunipinga.Lakini niliamua kuwahurumia binadamu - kwa kadiri nilivyoweza.Kwa hiyo huruma kubwa zote wawezazo kufanyiwa Wakristokatika zama hizi ni kuyaelekeza mawazo kwenye Mungu wa kweliAmbaye ameepukana na zile kasoro kama vile kuzaliwa na kufana kupata mateso; Yule Mungu ambaye aliziumba sayari zoteza awali huko mbinguni katika umbo la mviringo na katika kanuniYake ya hali ya asili aliweka kigezo hiki cha mwongozo wa kirohokwamba kama vile lilivyo umbo la mviringo, kuna Umoja ndaniYake Yeye na kwamba ndani ya Yeye hakuna welekea. Hii ndiyosababu vitu vilivyomo mbinguni havikutengenezwa kwa umbo lapembe tatu, yaani vitu ambavyo Mwenyezi Mungu aliviumba hapoawali kama vile ardhi, mbingu, jua na mwezi, nyota zote na viinivya asili vya kila kitu - vyote viko katika umbo la mviringo, ambapohali yao ya asili ya kuwa mviringo inaashiria kwenye Umoja. Kwahiyo hapawezi kuwa na kuwahurumia Wakristo zaidi kulikokwamba waelekezwe kwenye Ambaye alivyoviumbavinamtangaza Yeye kuwa ameepukana na wazo la utatu.Na huruma kubwa kuliko zote kwa Waislamu ni lazimawageuzwe kimaadili na kwamba lazima juhudi ifanywe kuondoamatumaini ya kiudanganyifu wanayoyashikilia kuhusiana nakutokea kwa Mahdi na Masihi mwenye kumwaga damu, ambayoyako kinyume kabisa na mafundisho ya Kiislamu. Na nimek

Kikristo kuhusu maisha ya mwanzoni na ya baadaye ya Yesu (amani juu yake) - mawazo potofu ambayo athari zake za hatari siyo tu zimelidhuru na kuliteketeza wazo la kuwako kwa umoja wa Mungu, bali pia ushawishi usiofaa na wenye sumu kwa muda mrefu umekuwa ukionekana katika maadili ya Waislamu wa nchi hii (India).

Related Documents:

kundi ,fanya jukumu la maana katika masomo yote.Umahiri wa maelezo maalum na wa baina ya mitaala yameshikanishwa pamoja katika muktadha wa maelezo. . baina ya mitaala katika muda wa mwaka wa shule. Kwa kufanya hivo wanaangazia kusoma kwao . na wanachukua jukumu la mchakato wao wa kimasomo. Tathmini ya kibinafsi hufanywa katika

Aya ya 15 kulingana na imani yetu katika Bwana Yesu na upendo kwa watakatifu wote; Aya ya 16 pamoja na shukrani tunatakikana kuwaombea watakatifu kwa majina! Aya ya 17 Paulo anamuomba Baba wa utukufu, Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, atupatie Roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye [Kristo], Aya ya 18 na macho ya mioyo yetu yatiwe nuru: i.

Yesu aliwaacha waamini na utume mkuu wa kuufikia ulimwengu kwa Injili ya Ufalme. Kazi hii haitakamilishwa kwa maneno pekee. Kama katika kanisa la kwanza, lazima pia kuwe na . Hizi zote ni nguvu kubwa zinazofanya kazi katika ulimwengu wetu wa leo. Lakini mwito kutoka kwa Yesu sio kwa mamlaka ya kidunia. Ni kwa nguvu za kiroho. Ni nguvu ambayo .

Data zilirekodiwa katika kinasa sauti na kunukuliwa kwa maandishi. . Tofauti za Matumizi ya Lugha katika Miktadha Mbalimbali ya Mazungumzo 13 sehemu ya pili inahusu tofauti ya matumizi ya lugha katika miktadha mbalimbali. Sehemu ya tatu inafafanua mkabala wa kinadharia uliotumika katika uch

Nyenzo za kufundisha huwa viungo muhimu wakati wa utoaji wa mafunzo. Utafiti ulichunguza matumizi ya nyenzo katika ufundishaji wa Kiswahili katika shule za msingi za umma katika Jimbo la Nyandarua, Kenya. Madhumuni ya utafiti yalikuwa: Kuainisha nyenzo zinazotumika kufundisha Kiswahili, Kutathimini kiwango cha matumizi ya

maswali yeye aliuliza ilikuwa, 'Biblia ina hadithi kuhusu mtu ambaye alimezwa na samaki mkubwa. Alikuwa nani? Asilimia themanini ya watu katika kundi hilo, kwa ushujaa wakasema, 'Pinocchio!' Marla aliniambia tukiwa bado katika ibaada kwamba swali hilo bado liliulizwa katika kanisa ambako alihundumu katika Kusini mwa California na

KITABU CHA MISINGI YA BIBLIA Carelinks, PO Box 152, Menai NSW 2234 AUSTRALIA www.carelinks.net email: info@carelinks.net . YALIYOMO 1) Biblia 2) Mungu 3) Mpango na nia ya Mungu 4) Mauti 5) Ahadi za Mungu 6) Bwana Yesu Kristo 7) Ahadi ya Mungu kwa Daudi 8) Ufufuo wa Yesu 9) Kurudi kwake Yesu Kristo .

ASTM C167 Standard test methods for thickness and density of blanket or batt thermal insulations ASTM C518 Standard test method for steady-state thermal transmission properties by means of the heat flow meter apparatus . TL-205 HOME INNOVATION RESEARCH LABS Page 6 of 6. ASTM C653 Standard guide for determination of the thermal resistance of low-density blanket-type mineral fiber insulation .