Kwa Watetezi Wa Haki Za BinadaMU - Protection International

1y ago
17 Views
2 Downloads
4.80 MB
220 Pages
Last View : 16d ago
Last Download : 3m ago
Upload by : Rafael Ruffin
Transcription

Mwongozo Mpya Wa UlinzikwaWatetezi Wa Haki Za BinadamuUmetafitiwana kuandikwa naEnrique Eguren na Marie Caraj

Mwongozo Mpya Wa UlinzikwaWatetezi Wa Haki Za BinadamuUmetafitiwa na kuandikwa na Enrique EgurenMarie Caraj, Protection International (PI)naUmechapishwanaProtection International1

Kimechapishwa na Protection International 2012Rue de la Linière, 11B-1060 Brussels, Belgium.Aliyetafsiri: Kimani NjoguToleo la TatuHaki ya kunakili 2008 ni ya Protection International. Mwongozo huuumetolewa kwa manufaa ya wateteaji wa haki za binadamu na unawezakunukuliwa kwa matumizi yasiyokuwa ya kibiashara mradi tu shukuranizitolewe kwa chanzo na waandishi. Tafadhali omba ruhusa ili kuingizamwongozo huu kwenye machapisho mengine au kwa matumizi mengine.Nakala za Mwongozo Mpya kutoka kwa:Protection InternationalRue de la Linière, 11.B-1060 Brussels, BelgiumSimu: 32(0)2 609 44 05 / 32(0)2 609 44 07Faksi: 32(0)2 609 44 07Barua pepe: pi@protectioninternational.orgNakala hii inaweza kupakuliwa bila malipo kutoka www.protectionline.orgNakala hii mpya inapatikana kwa Kiingereza, Kifaransa, Kihispania naKiswahili (pia inatafsiriwa kwa lugha nyingine na Protection International)ISBN: 978-2-930539-25-62

Katika kazi yangu kama Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuukuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu nimegundua kwa masikitikomakubwa ongezeko la idadi ya ripoti zinazohusu dhuluma za haki zabinadamu dhidi ya watetezi na namna wanavyolengwa kuanzia hali yachini kama vile kudhalilishwa na kunyanyaswa hadi ukiukaji mkubwa kamavile kushambuliwa na kutishiwa haki zao za kuishi na wengine. Katikamwaka wa 2004, tulishughulikia ripoti za angalau watetezi 47 waliokuwawameuawa kutokana na kazi yao.Ni dhahiri kwamba wajibu wa kimsingi wa kuwalinda wateteziwa haki za binadamu ni wa serikali, kama inavyodhihirishwa katika AzimioLa Umoja wa Mataifa kuhusu watetezi wa haki za Binadamu1. Ni lazimatuendelee kuhakikisha kwamba serikali zote zinachukulia uzito majukumuyake kuhusu suala hili na kuchukua hatua madhubuti za kuhakikishakwamba watetezi wa haki za binadamu wanalindwa.Hata hivyo, kiwango cha hatari wanazokabiliana nazo watetezihawa kila siku ni cha juu hivi kwamba ni muhimu pia kutafuta mbinunyinginezo za kuimarisha ulinzi wao. Kwa hali hii,ninatumai kwambaMwongozo huu wa Ulinzi utawapa watetezi wa haki za binadamu usaidiziwa kuendeleza mipango yao ya usalama na mikakati ya kujilinda. Wateteziwengi wa haki za binadamu wanajihusisha sana na kazi yao ya kuwalindawengine kiasi kwamba hawaupi uzito ufaao usalama wao. Ni muhimukwamba sote tushughulike na haki za binadamu ili tuwe makini kwausalama wetu na ule wa watu tunaofanya nao au kuwafanyia kazi.Hina Jilani Mwakilishi maalum wa zamani wa Katibu Mkuu wa Umoja waMataifa kuhusu watetezi wa haki za Binadamu1 Azimio la Haki na Jukumu la Watu, Makundi, na Mashirika ya Kijamii ili Kudumisha na KuheshimuHaki za Binadamu na Uhuru wa Msingi Kama Ilivyotambuliwa Kimatifa.3Mwongozo Mpya wa Ulinzi kwa Watetezi wa haki za BinadamuUtangulizi kwa toleo la kwanza na Hina Jilani

Protection International -PI-Wanachama wa PI wana uzoefu wa zaidi ya miaka 25 katika kuwalinda watetezi wa hakiza binadamu na makundi mengineyo dhaifu1.PI inalenga kuchangia katika kuyatimiza majukumu ya kitaifa na kimataifa ya kuwalindawatetezi hao. Tayari mashirika mengi yasiyo ya kiserikali pamoja na taasisi mbalimbalizinayashughulikia masuala ya haki za binadamu pamoja na watetezi wazo.Mikakati ya kilimwengu ya PI ya kuwalinda watetezi ni kama vile:Kujenga uwezo na mafunzo ili kuimarisha ulinzi na usalama Tathmini ya Hatari, hifadhi ya ulinzi/ usalama. Uhamisho wa maarifa na vifaa. Uchapishaji wa miongozo, miongoni mwayo ni huu mpya (pamoja na toleo lake lahapo awali2). Mafunzo: kati ya 2004 – 2008, zaidi ya watetezi 1700 wameshiriki katika ujenziwa uwezo na warsha za usalama huku wakiimarisha uwezo wa kuulinda usalamawao binafsi na ule wa watu wengine.Utafiti wa ulinzi Mafunzo na uwekaji wazi wa zana tendaji za ulinzi/usalama Uchapishaji wa habari kutokana na yale waliojifunza pamoja na matendo bora.Mwongozo Mpya wa Ulinzi kwa Watetezi wa haki za BinadamuUtetezi wa ulinzi Usambazaji wa habari kuhusu ulinzi miongoni mwa taasisi za HRD, IDP, EU nawanachama wa Umoja wa Nchi za Ulaya kwa njia za mapendekezo, ripoti na taarifakwa waandishi wa habari na pia habari halisi za matukio au watu fulani. Kuzikumbusha mamlaka za kitaifa na kimataifa kuhusu wajibu wao wa kimataifa wakulinda watetezi wa haki za binadamu, wakimbizi wa ndani kwa ndani, wakimbizikutoka nje na wahudumu wengine wa jamii. Kuendeleza mijadala na hatua za kulinda watetezi hao, uhusishaji wa bunge, vyamavya wafanyikazi na vyombo vya habari. Juhudi za kupinga uhuru wa kutumia mamlaka vibaya dhidi ya watetezi kupitiaushahidi wa kimahakama na rufaa dhidi yake.1 Kufikia tarehe 25 Oktoba 2007, kupitia kwa agizo la kifalme la Federal Public Justice Service, shirikala European Bureau of peace Brigades International, kupitia kwa marekebisho ya makala yakeyaliyochapishwa katika Jarida rasmi la Ubelgiji, lilikuwa “Protection International” muungano wakimataifa usio wa kutengeneza faida.2 Lilichapishwa mwaka 2005 kwa usaidizi wa kifedha wa Front Line na Development Co-operationof Ireland.4PANTONE 144

Picha za watetezi wa haki za binadamu.Dawati la Ulinzi Kwa ushirikiano na miungano iliyopo ya watetezi wa haki za binadamu, dawati zaulinzi huwekwa katika sehemu za kitaifa na kimaeneo kwa ajili ya ulinzi na usalama. Ukabidhi endelevu wa mchakato mzima wa usalama/ulinzi kwa PD (umilikaji nisehemu ya mchakato).Ulinzi kwa tovuti www.protectionline.org ni tovuti tosha inayoweza kutumiwa na au kwa ajili yaWatetezi wa Haki za binadamu na wale wanaotaka kuchangia kwa ulinzi wawatetezi hao. Kujenga upya habari,nyaraka,machapisho,ushuhuda, hatua za dharura na zana zakuendeleza ulinzi wa watetezi.Mfumo sanifuPI inafuata kanuni zote za kimataifa katika sheria ya kimataifa kuhusu haki za binadamu. PIitatumia hususan miongozo iliyotolewa na Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu watetezi hakiza binadamu (1998), miongozo ya Umoja wa Nchi za Ulaya ya HRD (2004), na pia maazimiokuhusu watetezi waliopandishwa cheo na PI na kuidhinishwa na nchi wanachama wa Umojawa Nchi za Ulaya kule Uhispania, Ubelgiji na Ujerumani.Warsha Za Protection International (pi)Za Kujenga Uwezo Na UsalamaKuanzia mwaka 2004 hadi 2007, jumla ya watetezi 1747 wa haki za binadamuwameshiriki katika warsha za PI za kujenga uwezo na usalama. Katika Amerika ya Kati na Kusini: watetezi 558(Bolivia, Brazil, Colombia, Guatemala, Honduras, México, Peru) Katika Asia: watetezi 650(Burma, Indonesia, Nepal, Thailand) Katika Afrika: watetezi 441(Kenya, Uganda, Democratic Republic of Congo) Katika Ulaya: watetezi 98(Germany, Belgium, Ireland, Serbia, Republic of Ingushetia)Watetezi wa haki za binadamu aghalabu huwatetea watu wengine hukuwakipuuza usalama wao kutokana na sababu kadhaa. Mafunzo ya PI ya usalamana ulinzi huzishughulikia sababu hizi na kisha hutenga muda wa kutafakari juuya hatari na vitisho ambavyo walengwa wakuu huwa ni watetezi hawa. Mafunzoya PI hupelekea kuwepo kwa mchanganuo wa kina wa matishio na pia ufahamuna mantiki inayohitajika kuhusisha usalama katika ratiba za kazi za watetezi wahaki za binadamu. Katika mafunzo haya, mada ya usalama huainishwa katikavipengele mbalimbali ili kuweza kuvichambua, kutafakari juu ya uwezekano wakuwepo nadharia fulani, hali na matokeo ya machaguo maalum yanayowezakupatikana na kisha kuchukua chaguo ambalo watetezi hao wanaamini kwambawanaweza kumudu matokeo yake, wakifahamu fika kwamba hawawezi kuwa nauhakika wa matokeo maalum.Katika hali yoyote ile hakuna jawabu la kimiujiza linaloweza kufaa kila wakati;mafunzo haya yanakusudiwa kuhakikisha kwamba watetezi wanapata maarifayanayohitajika kwa ajili ya usalama wao: uchanganuzi, matokeo, usimamizi naujengaji upya wa mchakato huo mzima. Wanapaswa kufanya hivi kwa kiwango chamtu binafsi, cha shirika au baina ya mashirika kukitiliwa maanani kwamba wanafaakuwa na ufahamu wa kiasi wa masuala ya kisiasa, jamii-nafsia na ufahamu wa nje.5Mwongozo Mpya wa Ulinzi kwa Watetezi wa haki za BinadamuUlinzi kwa video (Utetezi wa video)

DibajiBaada ya zaidi ya mwongo mmoja wa mafunzo, utafiti na mikutano na watetezi wa hakiza binadamu na washikadau wengineo wanaohusika na ulinzi wa watetezi wa haki zabinadamu, sisi katika Protection International tumeamua kuwashukuru upya watetezina tena kuihusisha michango yao katika mwongozo huu mpya wa ulinzi ulioandikwapamoja na, kutoka kwa, na kwa ajili ya watetezi wote wa haki za binadamu.Kwa miaka mitatu ya nyuma iliyopita, Protection International imepiga hatua zaidikatika mafunzo na utafiti wake, huku ikipata uzoefu wa nyanjani na maoni rejea kutokakwa watetezi wa haki za binadamu.Katika mwongozo huu mpya, PI inapendekeza mantiki ya usimamizi inayowezakuhusishwa katika miundo na mazingira ya kiuendeshaji huku ikifikia matokeo yaliyosawa: kuhusisha mpango wa usalama katika utaratibu wa kazi. Hakuna jibu la kimiujiza,bali ni hali ya kumudu machaguo na matokeo tu. Haya yanaweza kufanikishwa kupitiauchangizi wa pamoja wa mawazo, kuuliza maswali halisi, kufanya tathmini ya usalama wakiuendeshaji pamoja na hatari, kuandika mipango na michakato jumuishi .Hivyo basi, mwongozo huu mpya unalenga kuwafanya watetezi wa haki za binadamuwaimiliki harakati nzima ya usalama na ulinzi.Mwongozo Mpya wa Ulinzi kwa Watetezi wa haki za BinadamuUmilikaji ni kipengele cha usalama wenyewe. Mwongozo huu mpya unachangia katikakujenga uhuru na uendelezaji wa usalama na ulinzi wa watetezi wa haki za binadamu.Ijapokuwa hakuna mpango wa usalama wa kijumla,mwongozo huu unavuka mipaka yatofauti za kitamaduni,kijamii,kidini,mazingira na miundo ya kishirika. Mwongozo huuwaweza kutumika na watetezi wa haki za binadamu kuuimarisha usalama na ulinzi waokama tunavyojua kwamba wanazo mbinu zifaazo za kufanya hivyo:maarifa na uzoefu wahali zao binafsi.Protection International hutofautisha baina ya usalama wa watetezi wa haki za binadamuwa kwake (mtetezi) binafsi- na ule unaotoka kwa washikadau wengineo hadi kwa mtetezi.ShukraniToleo jipya la mwongozo lilioendelezwa na kuandaliwa kisasa ni matokeo ya mchango wa: Watetezi wote wa haki za binadamu ambao wamehudhuria mafunzo yaProtection International kuhusu hifadhi ya usalama na ulinzi. Haiwezekanikuwaorodhesha wote hapa. Wanapatikana Bolivia, Brazil, Burma, Colombia,Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Guatemala, Honduras, Indonesia,Ingushetia, Kenya, Mexico, Nepal, Peru, Serbia, Sri Lanka, Thailand, Uganda. Wanachama wa PI wa sasa na wa awali: Pascal Boosten, Soledad Briones,Shaun Kirven, Christor Klotz, Rainer Mueller, Michael Schools. Washiriki wa PI ni Ana Cornida, Eric Juzen, Maria Martin, Thomas Noirfalisse,Sheila Pais, Flora Petrucci, Sophie Roudil, Catherine Wielant, Jabier Zabala.6

katika kusuka na kuandaa matoleo ya awali na ya sasa ya miongozo. ThomasNoirfalisse alichangia kwa usanifu wake wa nembo ya PI na mawazo ya jinsi yakulisanifu jalada. Wazo kunjufu kwa Brigitte Scherer.Tunatoa shukrani kwa usaidizi wa Bundeministerion fur wirtshchaftliche Zusammenarbeitund Entwicklung (Wizara ya Ujerumani ya maendeleo na Ushirikiano, na Service publicfederal Affaires Etrangeres Belgique (Huduma ya Umma na Mambo ya Nchi za kigeniya Ubelgiji).Mwongozo Mpya wa Ulinzi wa watetezi wa haki za binadamu unatia usasa na kuuendelezamwongozo wa kwanza wa ulinzi wa watetezi wa haki za binadamu (Mwandishi: LuisEnrique Eguren 2005 PI) ambao ulichapishwa kwa msaada wa kifedha wa Front Linena wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Ireland.Muswada wa mwongozo cha kwanza ulitolewa maoni na Arnold Tsunga (Zimbabwe,Lawyers for Human Rights), Sihem Bensedrine (Tunis, Conseil National pour les libertes enTunisie), Father Bendan Forde (Colombia, Itinerant Franciscans), Indai Sajor (Philippines,Mkurugenzi wa zamani wa Asia centre for human rights), James Cavallaro (Brazil, mshirikiwa haki za binadamu-Chuo cha Sheria cha Havard), Nadejda Marques (Brazil, mshauri namtafiti-Global Justice) na Marie Caraj (PI former PBIBEO).Washiriki wengine wamechangia kwa kazi zao binafsi: Jose Cruz na Iduvina kutoka SEDEM(Guatemala), Jaime Prieto (Colombia), Emma Eastwood (Uingereza) na Cintia Lavanderaakiwa Human Rights Defenders Program from Amnesty International kule London.Mpango wa Utetezi wa Haki za Binadamu kutoka shirika la kimataifa la AmnestyInternational kule London (The Human Rights Defenders Program from AmnestyInternational in London) pamoja na mradi wa Indonesia wa PBI (the Indonesia Project ofPBI) ilitoa pesa za kugharamia tafsiri za toleo la kwanza la Mwongozo hadi katika lughaya Kireno na Kiindonesia mtawalio. Tume ya Kimataifa ya Wanasheria (The InternationalCommission of Jurists) ilitafsiri toleo hilo hadi katika lugha ya Kithai, na PBI hadi katikalugha ya Kinepali.Sura ya 2.11 inatokana na kazi ya Robert Guerra, Katitza Rodriguez na Caryn Maddenkutoka Privaterra (Canada).Shukrani kutoka kwa mwandishi: Luis Enrique EgurenPia watu wengi wengineo wamechangia katika ukusanyaji wa maelezo ya asiliayaliyohitajika kuuandika Mwongozo huu,hivi kwamba ni vigumu kuwaorodheshahapa wote. Ningependa kutaja majina ya wachache wao:To Kwa watu wote wa PBI na hasa kwa washiriki wenzangu wa karibu wa hapoawali kwenye mradi wa Colombia ambao walikuwa Marga, Elena, Francesc, Emma,Tomas, Juan, Mikel, Solveig, Mirjam, Jacob na wengi wengineo.Kwa Danilo, Clemencia na abilio na washiriki wenzao kutoka Comision Interedesialde Justicia Paz kule Colombia. Walinifunza jinsi ya kuishi na kupendwa na watu.Kwa watu wa Santa Marta, kule El Salvador, na wale wa Cacarica, Jiguamiando naSan Jose de Apartado kule Colombia. Wao miongoni mwa wengine walinifunza jinsiwatu wa mashambani wanaishi kwa heshima.Kwa Irma Ortiz, mkufunzi-mwenza katika warsha nyingi na washiriki wenzanguwengine katika Pensamiento Accion Social (PAS) kule Colombia.7Mwongozo Mpya wa Ulinzi kwa Watetezi wa haki za Binadamu Carmen Díez and Montserrat Muñoz ambao wote walishughulika pakubwa

Kwa ushauri na maarifa ya awali yaliyotolewa na REDR (London) na Koenraad VanBrabant (Ubelgiji).Na kwa watetezi wengi waliokutana El Salvador, Guatemala, Colombia, Mexico, Peru,Bolivia, Burma, Sri Lanka, Croatia, Serbia, Kosovo, Rwanda, Jamhuri ya kidemokrasiaya Kongo, Ingushetia na kadhalika. Mazungumzo mengi,vilio, tabasamu, kujifunza nahata kujitolea .Mwisho, hakuna ambacho kingewezekana bila ya mapenzi na kujitolea na usaidiziwa Grisela na Iker na wazazi wangu. Pendo langu lote liwaendee.Shukrani kutoka kwa mwandishi-mwenza: Marie CarajNinahisi upendo, heshima, mshikamano, huruma na shukrani kwa mtetezi yeyote wahaki za binadamu niliyekutana naye. Wameyabadilisha maisha yangu. Siku tulizokuwanao pamoja zimepelekea kuwepo kwa mshikamano thabiti baina yetu.Nina ghadhabu kubwa kwa wakiukaji wa haki za kibinadamu na ninatarajia kuwa sikumoja wakiukaji hao watakuja kutambua kuwa katu hawabaguliwi na watetezi wa hakiza kibinadamu na hivyo watajiunga na vuguvugu hilo wakati ambapo haki zote zakibinadamu zitaheshimiwa na watetezi wazo kufurahia maisha ya kawaida.Kwa Leze Gegaj, mamangu,ambaye ndiye mtetezi wa haki za kibinadamu wa kwanzamwanamke niliyekutana naye.Mwongozo Mpya wa Ulinzi kwa Watetezi wa haki za BinadamuKwa rafiki na washiriki wenzangu wote kwa msaada wao usiosemeka. Wengi waowamewasimulia wenzao yale yote niliyorejea nayo na wamenisaidia kuzichocheahamasa zangu.Tunawashukuru wote tuliowataja hapa na watetezi wengi wa haki za binadamuambao tumefanya nao kazi na tuliosoma kutoka kwao kwa msaada wao. Makosayoyote yaliyosalia katika Mwongozo huu mpya (ingawa tumejitahidi kuyaondoa yote)yanatokana kikamilifu na sisi katika uhariri wa nakala ya muswada. Tunatarajiakwamba mwongozo huu mpya utakuwa kifaa muhimu katika uimarishaji wa ulinzina usalama wa watetezi wa haki za kibinadamu, ingawa tunagundua kwamba hakitoidhamana yoyote na kwa vyovyote vile kila mmoja anapaswa kujiwajibikia kuhusumasuala haya. Tunayatarajia maoni yako.Protection InternationalApril 2009Hati ya kukanaYale yote yanayopatikana katika mwongozo huu hayawakilishi kwa vyovyote vilemsimamo wa Protection International.Waandishi na wachapishaji hawawezi kuhalalisha kwamba habari inayopatikana katikachapisho hili ni kamilifu na sahihi na hawatawajibikia kasoro zozote zitakazopatikanakatika harakati ya kulitumia. Sehemu yoyote ya mwongozo huu haiwezi kutumika kamakanuni au dhamana au kutumika kwa njia isiyofaa kutathmini hatari na matatizo yausalama anayoweza kukabiliana nayo mtetezi.8

Mwongozo Mpya wa Usalamana Ulinzi kwa Watetezi waHaki za BinadamuHaki za watetezi wa haki za binadamu ziko hataraniHaki za binadamu zinapewa dhamana chini ya sheria ya kimataifa lakini kufanyajuhudi ya kuhakikisha kwamba zinafanikishwa na kuziwasilisha kesi za wale ambaohaki zao zimekiukwa,linaweza kuwa jambo hatari katika nchi zote za ulimwengu.Watetezi wa haki za binadamu aghalabu huwa nguzo ya pekee baina ya watu wakawaida na mamlaka yasiyozuilika ya nchi. Wao ni muhimu kwa maendeleo yaharakati za kidemokrasia na taasisi, na hujitahidi kukomesha utekelezaji wa maovubila kuadhibiwa pamoja na kuendeleza na kuzilinda haki za binadamu.Watetezi wa haki za Binadamu aghalabu hukumbana na unyanyasaji, kuzuiliwa,mateso, kuharibiwa sifa, kusimamishwa kazi kwa muda, kunyimwa uhuru wakutembea na hata miungano yao kupata ugumu wa kutambulika kisheria. Katikanchi nyinginezo, wao huuawa, wakatekwa nyara au “wakapotea”.Kwa miaka michache iliyopita, ufahamu wa kijumla umeongezea hatari kubwawanayokumbana nayo watetezi wa haki za binadamu wakiwa kazini. Hatari hiyoinaweza kutambulika kwa haraka watetezi hao wanapofanya kazi katika mazingiraya uhasama, kwa mfano, ikiwa sheria za nchi zinaadhibu watu wanaoshughulikia hakifulani za binadamu. Watetezi pia wanakabiliwa na hatari ikiwa sheria kwa upandemmoja, itaiwekea vikwazo kazi ya utetezi wa haki za binadamu, na kwa upandemwingine ipuuze kuwaadhibu wale wanaowatishia au wanaowashambulia watetezihao.Katika hali za mapigano ya kijeshi, hatari hizo huwa katika upeo wa juu.Isipokuwa kwa hali chache za machafuko ambapo maisha ya mtetezi wa haki zabinadamu yanaweza kuwa mikononi mwa wanajeshi kwenye kituo cha ukaguzi,uhasama wanaotendewa watetezi hauwezi kutambulika kama usio wa mpango.Katika hali nyingi, mashambulizi ya kihasama huwa mwitiko wa kimakusudina vilevile uliopangwa vizuri dhidi ya kazi ya watetezi, na aghalabu huwayanahusishwa (mashambulizi hayo) na ajenda wazi ya kisiasa au kijeshi.Changamoto hizi zinawahitaji watetezi wa haki za binadamu kuitekeleza mikakati yausalama iliyo thabiti na yenye nguvu katika kazi zao za kila siku. Kuwapa watetezihawa nasaha nzuri au kuwashauri ‘wawe waangalifu’ hakutoshi. Ulinzi bora wausalama ni muhimu. Mwongozo huu hautoi suluhisho zifaazo zinazoweza kutumiwakatika mazingira ya aina yoyote. Hata hivyo, unajaribu kutoa mikakati kadhaainayodhamiriwa kuimarisha hali ya usalama ya watetezi wa haki za binadamu.9Mwongozo Mpya wa Ulinzi kwa Watetezi wa haki za BinadamuUtangulizi

Mafunzo bora zaidi ya usalama hutokana na watetezi wenyewe – kutokana naharakati zao za kila siku na mbinu na mikakati wanayobuni baada ya kipindicha muda ili kuwalinda wengine pamoja na mazingira yao binafsi ya kazi. Hivyobasi, mwongozo huu unapaswa kueleweka kwamba ni kazi inayoendelea naambayo itahitaji kuongezewa mambo mengi ili ilingane na hali ya sasa, na upatekutumika huku tukiendelea kukusanya habari mbalimbali kutoka kwa wateteziwa haki za binadamu.Pia kuna mafunzo ya kupata kutoka kwa mashirika ya kibinadamu na yakimataifa yasiyo ya kiserikali ambayo hivi majuzi yameanza kubuni kanuni nataratibu zao binafsi ili kuuhifadhi usalama wa wafanyikazi wao.Ni muhimu kuwa na ufahamu kwamba hatari kuu inayowakabili watetezi wa hakiza binadamu ni kuwa matishio dhidi yao hugeuka baadaye kuwa mashambuliziya kihakika. Washambulizi wanayo nia, mikakati na uwezo wa kutekelezamatishio pasina kuadhibiwa.Kwa hivyo njia bora ya kuwalinda watetezi hao nihatua ya kisiasa ya kulishughulikia suala moja kubwa lililosalia:haja ya serikalina mashirika ya kiraia kushinikiza na kuchukua hatua dhidi ya wale ambao kilasiku wanawatishia na kuwanyanyasa na hatimaye kuwaua watetezi wa haki zabinadamu. Ushauri unaotolewa katika mwongozo huu haukusudii kwa vyovyotevile kuchukua nafasi ya wajibu halali wa serikali zote wa kuwapa ulinzi wateteziwa haki za binadamu.Hayo yakishasemwa, watetezi wanaweza kwa njia wazi, kuimarisha usalama waokwa kuzifuata kanuni na taratibu chache zilizojaribiwa na kuthibitishwa.Mwongozo huu ni mchango mchache kwa lengo la kijumla la mashirika mengitofauti:kulinda kazi ya thamani kubwa inayofanywa na watetezi wa haki zabinadamu. Wao ndio washika dau wa kwanza na pia wahusika wakuu katikamwongozo huu.Mwongozo Mpya wa Ulinzi kwa Watetezi wa haki za BinadamuMwongozoMakusudio ya mwongozo huu ni kuwapa watetezi wa haki za binadamu nyongezaya maarifa na zana ambazo zaweza kuwa muhimu katika kuimarisha ufahamuwao kuhusu usalama na ulinzi. Inatarajiwa kwamba mwongozo huu utachangiakatika mafunzo ya usalama na ulinzi na utawasaidia watetezi kufanya makadirioya hatari zao wenyewe na vilevile kuzibainisha kanuni na taratibu za usalamazinazoambatana na hali zao mahsusi.Mwongozo huu ni tokeo la tajiriba sawia ya zaidi ya miaka 25 ya wanachama waProtection International (PI) ya kushughulikia haki za binadamu na sheriaya kibinadamu na vilevile katika kuwalinda watetezi wa haki za binadamu (HRD)na makundi mengineyo dhaifu. Tajiriba ya wanachama wa PI inatokana nakujihusisha na kushiriki kwao hapo awali katika Peace Brigades International(PBI) ziara za nyanjani na miundo.Tumepata kuwa na fursa ya kujifunza na kubadilishana tajiriba na maarifa kutokakwa mamia ya watetezi wa haki za binadamu kule nyanjani,na hata katikawarsha mbalimbali, mikutano na mijadala kuhusu usalama. Mambo mengi katikamwongozo huu yameshatekelezwa,ama katika kazi ya ulinzi au kutoa mafunzo10

Usalama na ulinzi ni masuala tata. Yana msingi katika maarifa ya kimuundo,lakini pia yanaathiriwa na mielekeo ya mtu binafsi na mienendo ya kiuendeshaji.Moja katika jumbe muhimu kwenye mwongozo huu ni kulipa suala la usalamamuda,nafasi na nguvu inayohitajika, licha ya ajenda nyingi za kazi na msongomzito wa akili na pia hofu walio nayo watetezi na mashirika yao. Hii ina maanaya kwenda zaidi ya ufahamu wa kibinafsi wa watu kuhusu usalama hadi kwenyempangilio wa kitamaduni ambao suala la usalama ni la msingi.Kuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu hali ya mgogoro na kufahamu mantikiiliyopo ya kisiasa ni muhimu pia kwa kuudhibiti ipasavyo usalama wa mtetezi.Mwongozo huu umesheheni mbinu ya kijumla na pia utaratibu wa hatua kwahatua wa kuandaa mpango (zao) wa usalama na kuudhibiti usalama wenyewe(mchakato). Unajumuisha mawazo fulani kuhusu dhana za kimsingi kama vilehatari, udhaifu na tishio, na mapendekezo machache ya namna ya kuimarishana kujenga usalama wa watetezi katika harakati zao za kila siku. Tunatarajiakwamba mada zilizoshughulikiwa humu zitaruhusu mashirika yasiyo ya kiserikalipamoja na watetezi wa haki za binadamu kulipangia na hata kulimudu ongezekola changamoto za usalama katika kazi ya haki za binadamu.Haya yote yakishasemwa, jambo la kwanza tunalopenda lizingatiwe ni kwambawatetezi wanahatarisha maendeleo yao na hata maisha yao, na hili ni jambo lisilola utani. Wakati mwingine, njia ya pekee ya kuokoa maisha ni kuingia mafichonina kisha baadaye kutoroka. Tunataka kuweka wazi kwamba mikakati namapendekezo yote katika mwongozo huu kwa vyovyote vile, siyo njia ya pekeeya kuwazia kuhusu masuala ya usalama kwa watetezi wa haki za binadamu.Mwongozo huu umeandikwa kwa nia nzuri japo kwa masikitiko makubwa hautoihakikisho la mafanikio.Tuuimarishe mwongozo huu .Hatari hubadilika. Mwongozo huu ni kazi inayoendelea na utahitaji kuendelezwa,kuimarishwa na kuboreshwa kadiri muda unavyoendelea. Maoni yako kamamtetezi kuhusu kipengele chochote cha mwongozo huu yatakuwa muhimu zaidi.Tafadhali tuma maoni na mawazo yoyote hasa kwa kurejelea uzoefu wako wakutumia mwongozo huu kazini pako. Kwa msaada wenu, tunaweza kuufanyamwongozo huu kuendelea kuwa chombo cha manufaa kwa watetezi wa haki zabinadamu kote ulimwenguni.Tuandikie barua pepe:pi@protectioninternational.orgAu tuma barua ya posta kwa PI: Protection International. Rue de la Linière, 11, 1060 Bruxelles (Belgium)Simu: 32 (0)2 609 44 05, 32 (0)2 609 44 07Faksi: 32 (0)2 609 44 06www.protectioninternational.org, www.protectionline.org11Mwongozo Mpya wa Ulinzi kwa Watetezi wa haki za Binadamukwenye warsha na watetezi hawa. Mwongozo huu ni zao la mabadilishano yotehaya na tunawapa watetezi shukrani kubwa kwa mchango wao.

Utangulizi Mfupi Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu“Mtetezi wa haki za binadamu” ni neno linalotumiwa kufafanua watu ambao, akiwayeye binafsi au pamoja na wengine, huchukua hatua ya kustawisha au kuzilindahaki za binadamu. Watetezi wa haki za binadamu wanatambuliwa pakubwazaidi kutokana na yale wafanyayo, na hivyo basi neno hili (mtetezi wa haki zabinadamu) linaweza kufafanuliwa vizuri zaidi kwa kuyabainisha matendo yao nabaadhi ya maeneo wanayofanyia kazi.Kazi ya watetezi wa haki za binadamu ni halali na imehalalishwa na mashirika yakiraia ambayo watetezi hao wanayawakilisha.Mamia ya watetezi wa haki za binadamu hukumbana na machafuko ya kisiasakila siku ulimwenguni, kwa sababu ya kutetea haki za watu wengine. Hujitahidikukomesha hali ya kutekeleza maovu bila kuadhibiwa na pia kuendeleleza hakina amani katika jamii,na katika harakati hiyo huhatarisha uzima wao wa kimwilina kiakili.Mwongozo Mpya wa Ulinzi kwa Watetezi wa haki za BinadamuKatika mwaka wa 1988, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa liliidhinisha “Azimiola Haki na Uwajibikaji wa Watu binafsi, makundi na Mashirika ya Kiraia" katikakustawisha na kulinda haki za binadamu zinazotambuliwa ulimwenguni kote napia Uhuru wa kimsingi. (Baadaye likaitwa “Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusuWatetezi wa Haki za Binadamu’) hii ina maana kwamba, miaka hamsini baadaya Azimio la Kilimwengu la haki za binadamu, na baada ya miaka ishirini yamajadiliano kuhusu maamuzi ya muswada wa watetezi wa haki za binadamu,hatimaye Umoja wa mataifa ulitambua uhakika wa mambo kwamba maelfu yawatu walikuwa wanastawisha na kuchangia katika kuzilinda haki za binadamukatika ulimwengu mzima. Hili ni Azimio jumuishi linaloheshimu idadi na wingi wawatu wanaojihusisha katika uendelezaji na ulinzi wa haki za binadamu.Kiasili, nafasi ya Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusuwatetezi wa haki za binadamu ilibuniwa “kutafuta, kupokea, kutathmini na kutoamajibu kwa habari kuhusu hali na haki za mtu yeyote, akiwa pekee yake aumiongoni mwa watu wengine, kustawisha na kuzilinda haki za binadamu na uhuruwa kimsingi”. Katika mwaka wa 2008 nafasi hiyo ilichukuliwa na ile ya MsemajiMaalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu.Miongozo ya Umoja wa Nchi za Ulaya – EU – kuhusu watetezi wa Haki za Binadamuhaijafungamanisha tu Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu, balipia imetoa mapendekezo mahsusi kwa Nchi wanachama wa Umoja wa Nchi zaUlaya – MS –Watetezi wa Haki za Binadamu ni halali na wameidhinishwa na jumuiya za kitaifana kimataifa. PI inakubaliana na ufafanuzi wa maana ya mtetezi wa haki zabinadamu ambayo ilitolewa na Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu Watetezi waHaki za Binadamu na iliyotiliwa mkazo na Miongozo ya Umoja wa Nchi za Ulayakuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu:“Mtetezi wa haki za binadamu” ni kauli inayotumika kuelezamtu ambaye, yeye binafsi au pamoja na wengine, anajitahidikuendeleza na kuzilinda haki za binadamu. Watetezi wa Haki za12

(Tazama kwenye kiambatisho mwishoni mwa mwongozo huu kwa maelezo zaidikuhusu Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu na kwaMiongozo ya Umoja wa Nchi za Ulaya kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu).Ni nani anayewajibika kuwalinda watetezi wa Haki za Binadamu?Azimio la Watetezi wa Haki za Binadamu linasisitiza kwamba nchi ndiyo yakwanza katika kuwalinda watetezi wa Haki za Binadamu. Linatambua pia “kazimuhimu ya watu binafsi, makundi na miungano inayochangia katika kukomeshaukiukaji wa haki za binadamu na uhuru wa kimsingi.”Lakini kulingana na Hina Jilani2, Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifakuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu, “ukiukaji wa haki za binadamu wa wazina utafutaji wa suluhu yazo unategemea zaidi kiwango cha usalama walio naowatetezi wa haki za binadamu.3” Kutazama ripoti yoyote inayohusu watetezi wahaki za binadamu katika ulimwengu mzima kunaonyesha visa vingi vya mateso,utorokaji, mauaji, vitisho, unyang’anyi, uvamizi afisini, unyanyasaji, kuzuiwakusiko kwa haki, kufanyiwa upelelezi na ujasusi na kadhalika. Kwa bahatimbaya, hii ndiyo sheria wala si kitu kinachoweza kuepukwa na watetezi.Usomaji wa ziada uliopendekezwaKuyapata mengi kuhusu watetezi wa haki za binadamu, zuru: www.unhchr.ch/defender/about1.htm (The UN High Commissioner onHuman Rights) www.protectionline.org (Protection International). The observatory of the Protection of Human Rights Defenders, ulioundwana International Federation on Human Rights (FIDH; www.fidh.org) naWorld Organization Against Torture (OMC T; www.omct.org). Amnesty International: www.amnesty.org na http://web.amnesty.org/pages/hrd-index-eng www.ishr.ch, tazama chini “HRDO” (The HRD Office of the InternationalService for Human Rights in Geneva). www.frontlinedefenders.org (Front Line, The International Foundation forHuman Rights Defenders).1 Watetezi wa Haki za Binadamu: Kuhifadhi Haki ya Kuzitetea Haki za Binadamu. Fact Sheet No.29 www.unhchr.ch2 Margaret Sekaggya (Uganda) alichukua nafasi ya Hina Jilani, mwaka wa 2008, kama Ripotamaalum kuhusu hali za watetezi wa haki za binadamu ambaye aliteuliwa na Baraza la Umoja waMataifa la Haki za Binadamu.3 Ripoti kuhusu watetezi wa Haki za Binadamu, 10 Septemba 2001 (A/56/341).13Mwongozo Mpya wa Ulinzi kwa Watetezi wa haki za BinadamuBinadamu wanatambulika pakubwa zaidi kwa yale wanayoyafanyana ni kupitia kwa kuyafafanua matendo yao na kati

uchangizi wa pamoja wa mawazo, kuuliza maswali halisi, kufanya tathmini ya usalama wa kiuendeshaji pamoja na hatari, kuandika mipango na michakato jumuishi . Hivyo basi, mwongozo huu mpya unalenga kuwafanya watetezi wa haki za binadamu waimiliki harakati nzima ya usalama na ulinzi. Umilikaji ni kipengele cha usalama wenyewe.

Related Documents:

Utekelezaji wa haki ya kupiga kura na kugombania nafasi za uongozi wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020. Matukio ya ukatili wa kingono dhidi ya watoto kuongezeka, hasa ubakaji na ulawiti. Kupungua kwa kiasi kikubwa kwa wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kifo baada ya Mh. Rais Magufuli kuwapu

7. Onyesha kwa vitendo maisha yako mapya kwa kuonyesha upendo na shauku ya kuwajali wengine. Maisha inayotawaliwa na Kristo Maisha ya Mkristo yanaweza kuwakilishwa na picha ya msalaba. Kristo ndiye kiini cha maisha yetu mapya. Tunaishi kwa kujisalimi-sha kwake.Mstari ulio wima, unawakilisha ushirika wetu pamoja na Mungu kwa maombi na kwa kusoma .

KI 214 UFUNDISHAJI KISWAHILI KWA WAGENI MBINU ZA UFUNDISHAJI KISWAHILI KWA WAGENI I. Malengo ya ufundishaji lugha kwa wageni Lengo kubwa ni kwamba ili mwanafunzi aweze kujua lugha hiyo kwa stadi zote za lugha ile. Stadi za lugha ni 1. Kusikiliza 2.kuzungumza

Kwa nini tunakosa kui mwito wa Mungu kuwa mawakili wema. 1. Mtazamo wetu potovu kuhusu fedha. Kwanza tunaona kuwa mali ni yetu na sio ya Mungu. Pili twafikiri kutoa kwetu ni kitendo cha huruma kwa kazi ya Mungu wala sio amri. na Si amri. Tatu ,twafikiri kwa kufanya huvyo twamfanyia Mungu huruma kwa kupeana kwa Kanisa lake. 2.

Yesu aliwaacha waamini na utume mkuu wa kuufikia ulimwengu kwa Injili ya Ufalme. Kazi hii haitakamilishwa kwa maneno pekee. Kama katika kanisa la kwanza, lazima pia kuwe na . Hizi zote ni nguvu kubwa zinazofanya kazi katika ulimwengu wetu wa leo. Lakini mwito kutoka kwa Yesu sio kwa mamlaka ya kidunia. Ni kwa nguvu za kiroho. Ni nguvu ambayo .

Going to school ATD Dunia ya Nne katika Tanzania ATD Fourth World in Tanzania. 1989 - 2009 : Maadhimisho ya miaka 20 ya mabadiliko ya sheria za haki za watoto Rejea Kifungu no 28 1. Kinachoelezea sehemu zinazothamini haki ya elimu kwa mtoto, pamoja na mtazamo wa kufikia malengoendelevu ya fursa sawa

(1990s). Toleo hilo la Ghana lilitayarishwa kutokana na mitaala ya mafunzo mingine mbalimbali ya PATH, ikiwemo Kuelekea kwenye Utokomezaji wa Ukeketaji: Mawasiliano kwa Ajili ya Mabadiliko – Mtaala kwa ajili ya Wakufunzi wa Wafanyakazi wa Afya ya Jamii, Watayarishaji wa Afya ya Jamii, Watetezi wa Vijana, na Waalimu (PATH:2001).

Artificial Intelligence – A European approach to excellence and trust. It outlines the main principles of a future EU regulatory framework for AI in Europe. The White Paper notes that it is vital that such a framework is grounded in the EU’s fundamental values, including respect for human rights – Article 2 of the Treaty on European Union (TEU). This report supports that goal by .