Le Bureau Du Procureur The Office Of The Prosecutor Sera Ya .

3y ago
118 Views
2 Downloads
3.93 MB
50 Pages
Last View : 13d ago
Last Download : 3m ago
Upload by : Philip Renner
Transcription

ICC POLICY COVER swahili.pdf22016-11-069:57 PMLe Bureau du ProcureurThe Office of the ProsecutorSera ya WatotoNOVEMBA 2016CMYCMMYCYCMYK

Sera ya WatotoNovemba 2016

Novemba 2016Sera ya WatotoYaliyomoUfupishoI.UtanguliziII.Sera ya UjumlaIII.Mfumo wa Kisheria(a)Kuingiza kwa nguvu, kuandikisha na kutumia kikamilifu kwenye uhasama watoto wenyeumri wa chini ya miaka kumi na tano(b)Kuhamisha watoto kwa nguvu na kuzuia uzazi(c)Kuchuuza watoto kama aina ya utumwa(d)Mashambulizi dhidi ya majengo ya elimu na ya afya(e)Mateso na makosa ya jinai yanayohusiana nayo(f)Utesaji(g)Makosa ya jinai ya kingono na ya kijinsiaIV.Uchunguzi wa AwaliV.Upelelezi(a)Mawasiliano ya awali na mahojiano na watoto(b)Tathmini ya kisaikolojia na kijamii(c)Hatua za ulinziVI.Mashtaka(a)Kuchagua mashtaka(b)Maongezi na watoto(i)Kabla ya ushuhuda(ii)Hatua za mahakamani(iii)Ufuatiliaji na mawasiliano baada ya ushuhuda(c)Ushahidi(d)Utoaji wa adhabu(e)FidiaVII.Ushirikiano na Mahusiano ya NjeVIII.Maendeleo ya KitaasisiIX.Utekelezaji wa Sera hii1

Novemba 2016Sera ya WatotoUfupishoMamilioni ya watoto, wanawake na wanaume wamekuwa, na wanaendelea kuwawahanga wa mauaji yasiyoweza kufikiriwa na yanayoshtua kwa undani dhamiriya kibinadamu. Baada ya kutambua jambo hili, Nchi ambazo zilihudhuriaMkutano wa Roma ziliamua kuunda Mahakama ya Kimataifa ya Jinai “kwa ajili yakizazi cha sasa na vizazi vijavyo”. Vifungu mbalimbali vya Mkataba wa Roma,Kanuni ya Utaratibu na Ushahidi na Vipengele vya Makosa ya Jinai huonyeshaumuhimu wa uchunguzi wa kina na uendeshaji wa mashtaka ya makosa ya jinaidhidi ya watoto au yanayoathiri watoto; pamoja na kutetea haki na maslahi yawatoto. Vifungu hivi huorodhesha, kwa upande mmoja, makosa ya jinaiyanayoathiri hasa watoto, kama vile makosa ya jinai ya kivita ya kuandikisha,kuingiza kwa nguvu na kutumia watoto wenye umri wa miaka chini ya 15 katikauhasama; na kwa upande mwingine, makosa ya jinai yanayowaathiri watotokuliko watu wengine, kama vile kosa la jinai la mashambulizi dhidi ya majengo yaelimu na ya afya.Ikizingatia madhumuni ya Mkataba, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka iliinua sualahili na kuliweka katika malengo sita ya kimkakati katika Mpango Mkakati wa2012-2015, na kuahidi “kuwa makini sana kuhusu suala la makosa ya jinai yakingono na kijinsia na jinai dhidi ya watoto”. Ahadi hii ilithibitishwa katikaMpango Mkakati wa 2016-2018. Sera ya Watoto inaenda sambamba na MpangoMkakati na itachangia katika kufikia malengo ya kimkakati.Ofisi huchukulia “watoto” kama watu ambao hawajafikia umri wa miaka kumi nanane. Kwa ujumla, makosa ya jinai dhidi ya watoto au yanayoathiri watotohuonekana kama makubwa haswa panapozingatiwa dhamira iliyotolewa kwawatoto katika Mkataba na ukweli kwamba sheria za kimataifa huwatambuawatoto na kuwapatia ulinzi maalumu.Ofisi inatambua kwamba makosa ya jinai mengi yanayotajwa katika Mkatabahuwaathiri watoto kwa njia mbalimbali na kwamba wakati mwingine watotohulengwa haswa. Ofisi itatumia kikamilifu mfumo wa kisheria kwa ajili yakushughulikia njia mbalimbali ambamo makosa ya jinai ya aina hiyo huwaathiriwatoto. Kila wakati ushuhuda utakuwepo, Ofisi itajitahidi kuleta mashtaka yamakosa ya jinai yanayoathiri hasa watoto, pamoja na makosa ya jinai ambayo2

Novemba 2016Sera ya Watotohuwaathiri watoto vibaya sana na kuliko watu wengine. Ofisi itazingatia kwambawatoto huathiriwa tofauti na makosa ya jinai kufuatana na jinsia, mwelekeo wakijinsia au hadhi au utambulisho nyingine. Ili kuonyesha kikamilifu kiwango chamadhara yaliyofanyika, Ofisi itajitahidi kusisitizia athari mbalimbali za makosa yajinai kwa watoto, katika hatua zote za kazi yake.Ofisi hujihusisha na watoto katika mazingira mbalimbali, hasa watoto ambao nimashahidi na wale ambao wazazi wao au walezi wao wamekubali kutoaushuhuda mbele ya Mahakama. Katika miingiliano hii, Ofisi itazingatia maslahi,haki na ustawi wa watoto ambao wataathiriwa moja kwa moja na shughuli zake.Ofisi itajitahidi kuhakikisha kwamba shughuli zake haziwadhuru watoto ambaoitahusiana nao.Ofisi itatumia mbinu nyeti kuhusu watoto katika nyanja zote za kazi zakezinazohusisha watoto. Mbinu hii huchukulia mtoto kama mtu binafsi na hutambuakwamba, katika mazingira fulani, mtoto anaweza kuwa katika mazingiramagumu, kuwa na uwezo au hali zote mbili. Mbinu hii ina msingi juu ya heshimaya haki za watoto na inaongozwa na kanuni za ujumla za Azimio la Haki za Mtotola mwaka wa 1989: kutobaguliwa, maslahi ya mtoto, haki ya kuishi, maisha namaendeleo, na haki ya mtu kutoa maoni yake na maoni hayo kuzingatiwa.Ofisi hutambua haki mbalimbali za watoto chini ya sheria za kimataifa naitazingatia kwamba watoto wengi hukabiliana na changamoto katika utekelezajiwa haki zao kutokana na umri wao na hadhi yao katika jamii.Katika mazingira ya mamlaka yake, Ofisi itachukulia maanani maslahi ya mtotokama suala la msingi. Uchunguzi wa maslahi unahusisha mchakato wa hatuambili. Kwanza, Ofisi itatathmini maslahi ya mtoto, baada ya kuzingatia halimaalumu ya mtoto, maoni ya mtoto na yale ya wahusika wengine, pamoja na hakihusika za mtoto. Pili, Ofisi itaangalia kama kuna sababu nyingine, ikiwa ni pamojana sababu za kisheria na za uendeshaji, ambazo zinalazimisha kusawazishamaslahi mbalimbali kwa umakini. Ofisi itatatua migogoro itakayojitokeza kwamsingi wa kesi kwa kesi, katika jitihada ya kufikia maelewano mwafaka. Pia Ofisiitazingatia uwezo endelevu wa mtoto.Wakati wa uchunguzi wa awali wa hali fulani, Ofisi inachunguza mazingira ya3

Novemba 2016Sera ya Watotoujumla ambamo makosa ya jinai yanayodaiwa kufanywa dhidi ya watoto auyanayoathiri watoto yalitokea. Pia, Ofisi itatathmini kuwepo kwa taasisi nautaalamu vya wenyeji, mashirika ya kimataifa, mashirika yasiyo ya kiserikali nataasisi nyingine kama vyanzo vya habari na/ama usaidizi. Ofisi itahakikishakwamba tathmini ya athari za makosa ya jinai yanayodaiwa kufanywa dhidi yawatoto unaingizwa katika uchambuzi wa uzito wa kesi zenye uwezekano wakuanzishwa.Upelelezi wa uhalifu wa kimataifa unazo changamoto mbalimbali. Changamotohizo ni pamoja na kuwatafuta watu kwa ajili ya kushirikiana na Ofisi, kuwalindiausalama wa kimwili, ustawi wa kisaikolojia, heshima na faragha. Ikiwa upeleleziunahusu watoto, maswala haya huwa magumu zaidi. Ofisi itatafuta njia maalumuza kushughulikia masuala hayo ikizingatia kila wakati maslahi ya mtoto.Ofisi inatambua kwamba watoto wanaweza kutoa ushahidi wa kuaminika. Katikamaamuzi yake kuhusu kuhoji mtoto au kuchukua ushuhuda wake, Ofisi inatakiwakutilia maanani umri wa mtoto, maendeleo yake, kiwango cha ukomavu, uwezona udhaifu wake, pamoja na upatikanaji wa ushahidi kwa njia nyingine.Katika maoni yake kuhusu utoaji wa adhabu, Ofisi itaomba adhabu inayolinganana uzito wa jinai dhidi ya watoto, ikiwa ni pamoja na madhara yanayoonekanamoja kwa moja na madhara ya muda mrefu yaliyofanyiwa watoto, familia zao najamii zao.Ofisi inaunga mkono utaratibu wa fidia unaompatia mtoto nafasi nyeti,ikizingatia kwamba wavulana na wasichana huwa na madhara na atharimbalimbali kutokana na jinai zilizofanywa na mtu aliyepatikana na hatia;utaratibu huu ni pamoja na haki ya watoto waathirika kuunganishwa tena najamii zao.Ofisi itaendelea kujitahidi kuimarisha ushirikiano na uungaji mkono washughuli zake, hasa kuhusu watoto na kuupigia debe utaratibu unaompatiamtoto nafasi nyeti katika mfumo wa sheria za kimataifa za jinai. Juhudi zapamoja zitafanyika ili kuhakikisha ushirikiano wa maana na Nchi, mashirikaya kimataifa na vyombo husika kwa ajili ya kutafutia msaada kazi ya Ofisikuhusu watoto, hasa katika nchi ambapo Ofisi inaendesha shughuli zake.4

Novemba 2016Sera ya WatotoKulingana na kanuni ya kusaidiana vyema na katika jitihada za kuziba pengokatika hali ya kutoadhibiwa, Ofisi itaendelea kutia moyo na kuunga mkono juhudiza kitaifa za kuwajibisha watuhumiwa wa makosa ya jinai dhidi ya watoto auyanayoathiri watoto.Katika shughuli zake za kutoa taarifa kwa umma, Ofisi itatilia mkazo haki zawatoto na maslahi yao katika mazingira ya makosa ya jinai ya kimataifa, kamaifaavyo. Ofisi itachukua hatua kwa ajili ya kusambaza taarifa kwa watoto kuhusukazi zake, ikiwa ni pamoja na Sera hii, kwa namna ambayo watoto wanawezakuelewa.Ofisi itajitahidi kuhakikisha kwamba inao uwezo wa kitaasisi ambao ni muhimukwa ajili ya kuendesha kwa ufanisi zaidi shughuli za uchunguzi wa awali,upelelezi na mashtaka ya makosa ya jinai dhidi ya watoto au yanayoathiri watoto,na kwamba miingiliano yake na watoto hao inaheshimu haki zao na maslahi yao.Ofisi itafuatilia utekelezaji wa Sera hii.Sera hii inapatikana kwa URL ya kudumu: [Insert link to Swahili version]5

Novemba 2016I.Sera ya WatotoUtangulizi1.Mamilioni ya watoto, wanawake na wanaume wamekuwa, na wanaendeleakuwa wahanga 1 wa mauaji yasiyoweza kufikiriwa na yanayoshtua kwaundani dhamiri ya kibinadamu. Zikitambua jambo hili, Nchi zilizohudhuriaMkutano wa Roma ziliamua kuunda Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (”ICC”au “Mahakama”) “kwa ajili ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo”.2 Vifungumbalimbali vya Mkataba wa Roma (“Mkataba”), Kanuni ya Utaratibu naUshahidi (“Kanuni”) na Vipengele vya Makosa ya Jinai (“Vipengele”)huonyesha umuhimu wa uchunguzi wa kina na uendeshaji wa mashtaka yamakosa ya jinai dhidi ya watoto au yanayoathiri watoto; pamoja na kuteteahaki na maslahi ya watoto.2.Dhamira ya kushughulikia makosa ya jinai dhidi ya watoto au yanayoathiriwatoto inapatikana katika vifungu mbalimbali vya Mkataba, ikiwa ni pamojana orodha ya jinai dhidi ya watoto peke yake, kama vile kuandikisha,kuingiza kwa nguvu kwenye jeshi na kutumia watoto wenye umri wa chiniya miaka kumi na tano katika uhasama (“kuandikisha au kutumia watoto”),uhamishaji wa watoto kwa nguvu na kuchuuza watoto,3 na makosa ya jinaiyanayowaathiri watoto kuliko watu wengine, kama vile mashambulizi dhidiya majengo ya elimu.4 Pia watoto hukumbwa sana na makosa ya jinai yakingono na kijinsia, ambazo zimepigwa marufuku na Mkataba, jamboambalo limewekwa wazi katika Vipengele.5Ofisi ya Mwendesha Mashtaka (“Ofisi”) inatambua kwamba waathirika wengi wa makosa ya jinaiambayo yako chini ya mamlaka ya Mahakama ni watu walionusurika pia. Matumizi ya neno“waathirika” peke yake huenda sambamba na Mkataba wa Roma.2 Dibaji ya Mkataba, aya. 9. Angalia Mfuko wa Kimataifa wa Watoto (UNICEF), Children andemergencies in 2014 Facts & Figures (Watoto na dharura katika 2014 Ukweli na Takwimu), ambapoinakadiriwa kwamba watoto miliyoni 230 wanaishi katika nchi na maeneo yaathiriwayo na vita.3 Vifungu vya 8(2)(b)(xxvi) na 8(2)(e)(vii), 6(e), 7(1)(c) na 7(2)(c) vya Mkataba.4 Vifungu vya 8(2)(b)(ix) na 8(2)(e)(iv) vya Mkataba hupiga marufuku makosa ya jinai ya kivita, katikavita vya kimataifa na visivyo vya kimataifa, “kushambulia kwa makusudi majengo yanayotumiwa kwaajili ya shughuli za kidini, elimu, sanaa, sayansi, madhumuni ya hisani, makumbusho ya kihistoria,hospitali na mahali ambapo wagonjwa na majeruhi wamekusanywa, sharti majengo hayo si malengo yakijeshi”.5 Katika Vipengele, “kuchuuza watu, hasa wanawake na watoto” katika mazingira ya utumwa wangono, umetajwa kwa namna maalumu kama kosa la jinai dhidi ya binadamu na kosa la jinai ya kivita11

Novemba 20163.Sera ya WatotoMkataba hutambua watoto kama watu wenye haki za mtu binafsi, kamawanafamilia na kama wanajumuia wa jamii zenye vizazi mbalimbali. 6Utambuzi huu huenda sambamba na uelewa wa kimataifa unaoelezwa naAzimio la Haki za Mtoto la mwaka wa 19897 (“CRC”) na vyombo vinginevingi vya kimataifa, ya kwamba watoto ni watu wanyonge wenye haki yakupewa matunzo na ulinzi za kipekee,8 na kwamba maslahi yao, haki zao namazingira yao ya kibinafsi zizingatiwe ipasavyo.9iwe katika vita vya kimataifa au visivyo vya kimataifa, chini ya vifungu vya 7(1)(g), 8(2)(b)(xxii),8(2)(e)(vi) vya Mkataba.6 Kwa mfano, kifungu cha 84(1) kinatoa uwezekano wa kwamba, mtu aliyetiwa hatiani akifariki, watotowake wanaweze kuomba kurudiwa kwa hukumu yake ya mwisho iliyomtia hatiani au hukumu yaadhabu; na vifungu vya 6(d) na 7(1)(g) huvifanya kama makosa ya jinai vitendo vya utumiaji wa nguvukwa ajili ya kumkataza mtu kuzaa au kutia mimba kwa nguvu. Watu wengine wanaoathiriwa kwa namnainayogusa vizazi mbalimbali ni watoto wanaozaliwa wakati wa mgogoro au kwenye mazingira mengineyaliyopo chini ya mamlaka ya Mahakama, hasa waliozaliwa na wasichana waliokuwa na uhusiano navikundi vyenye silaha. Angalia Principles and Guidelines on Children Associated with Armed Forces orArmed Groups (Kanuni na Miongozo juu ya Watoto Waliohusika katika Vikosi vya Jeshi au Vikundivyenye Silaha) (“Kanuni za Paris”), Februari 2007, Kanuni 3.2.7 Azimio la Haki za Mtoto, Convention on the Rights of the Child (Mkataba wa Haki za Mtoto)(“CRC”), ulipitishwa kwa kauli moja na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika mwaka 1989.CRC umetiwa mkono na karibia nchi zote, isipokuwa nchi moja, na inachukuliwa kuwa kanuni zakenyingi zinaakisi sheria ya kimataifa ya kimila.8 Angalia, kwa mfano, kifungu cha 25 cha Azimio la Haki za Binadamu, Universal Declaration of HumanRights (Azimio la Haki za Binadamu), lililopitishwa na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa katikamwaka wa 1948; kanuni 2 ya Declaration of the Rights of the Child (Azimio la Haki za Mtoto),lililopitishwa na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika mwaka wa 1959; kifungu cha 10(3) chaInternational Covenant on Economic, Social and Cultural Rights (Mkataba wa Kimataifa wa Haki zaUchumi, Jamii na Utamaduni); 1966, kifungu cha 24 cha International Covenant on Civil and PoliticalRights (Makubaliano ya Kimataifa kuhusu Haki za Kiraia na za Kisiasa), 1966; vifungu vya 14, 17, 23, 24,38, 50, 51, 68, 76, 82, 89, 94 na 132 cha Geneva Convention (IV) relative to the Protection of Civilian Personsin Time of War (Mkataba wa Geneva (IV) kuhusu Ulinzi wa Raia Wakati wa Vita) 1949 (“Mkataba waGeneva IV”), ulioridhiwa na kila nchi duniani; vifungu vya 8, 70(1), 77 na 78 vya Protocol Additional tothe Geneva Conventions of 12 August 1949, and relating to the Protection of Victims of InternationalArmed Conflicts (Itifaki ya ziada ya Mikataba ya Geneva ya 12 Agosti 1949 kuhusu Ulinzi wa Waathirikawa Vita vya Kimataifa) 1977 (“API”); vifungu vya 4(3) na 6(4) vya Protocol Additional to the GenevaConventions of 12 August 1949, and relating to the Protection of Victims of Non-International ArmedConflicts (Itifaki ya Ziada ya Mikataba ya Geneva ya 12 Agosti 1949 kuhusu Ulinzi wa Waathirika wa Vitavisivyo vya Kimataifa) 1977 (“APII”); na kifungu cha 3(2) cha CRC.9 Angalia, kwa mfano, kifungu cha 3(1) cha CRC.2

Novemba 2016Sera ya Watoto4.Dhamira iliyopewa watoto katika Mkataba ni dhahiri vivyo hivyo katika sifazinazohitajika kwa majaji na washauri, 10 katika mamlaka ya ulinzi wawaathirika na mashahidi,11 na kwa kutokufunguliwa mashtaka ICC dhidi yawatu wenye umri wa chini ya miaka kumi na nane.12 Kanuni huimarishaulinzi wa kiutaratibu unaopewa watoto ambao ni mashahidi na waathirika.135.Ikizingatia madhumuni ya Mkataba, mnamo mwaka wa 2003, Ofisi yaMwendesha Mashtaka (“Ofisi”), iliunda Kitengo cha Jinsia na Watoto(“GCU”) chenye wafanyakazi wenye uzoefu wa kisheria, kisaikolojia nakijamii. Katika kazi yake kwa ajili ya waathirika na mashahidi, GCU husaidiatimu zote za Ofisi na kushauri Ofisi katika hatua zote za operesheni juu yamasuala yote kuhusu watoto.6.Aidha, katika nyaraka za mkakati wa awali, Ofisi ilitoa ahadi ya kuimarishaupelelezi na mashtaka ya makosa ya jinai dhidi ya watoto au yanayoathiriwatoto.14 Kesi ya kwanza kabisa ya ICC iliishia na mtuhumiwa kupatikanana hatia kwa makosa ya jinai ya kivita ya kuandikisha au kutumia watoto.15Kifungu cha 36(8)(b) cha Mkataba kinasema kwamba Nchi Wanachama zina wajibu wa kuzingatiahaja ya kuteua majaji wenye utaalamu wa kisheria katika masuala fulani, ikiwa ni pamoja na vitendovya vurugu dhidi ya watoto; na kwa mujibu wa kifungu cha 42(9) Mwendesha Mashtaka anatakiwakuteua washauri wenye utaalamu wa kisheria kuhusu masuala fulani, kama vile vitendo vya vurugudhidi ya watoto.11 Kifungu cha 54(1)(b) cha Mkataba humtaka Mwendesha Mashtaka, anapofanya upelelezi nakuendesha mashtaka, kuheshimu maslahi na mazingira binafsi ya waathirika na mashahidi, ikiwa nipamoja na umri, aina ya kosa la jinai, hasa pale ambapo kosa hilo ni kuhusu ukatili wa ngono, ukatiliwa kijinsia au ukatili dhidi ya watoto. Aidha, kifungu cha 68(1) hulazimisha Mahakama kwa ujumla, napia Mwendesha Mashtaka kwa namna maalumu, kuwa na wajibu wa kuchukua hatua mwafaka zakulinda usalama, ustawi wa kimwili na wa kisaikolojia, heshima na faragha ya waathirika namashahidi, huku ikizingatia sababu zote, ikiwa ni pamoja na umri na aina ya kosa la jinai, hasa paleambapo kosa hilo ni kuhusu ukatili wa ngono, ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto.12 Kwa mujibu wa kifungu cha 26 cha Mkataba, Mahakama haina mamlaka juu ya mtu yeyote ambayealikuwa na umri wa chini ya miaka kumi na nane wakati kosa la jinai linalodaiwa lilifanyika.13 Angalia, kwa mfano, kanuni 17(3), 19(f), 66(2), 86, 88(1), 89(3) na 112(4) za Kanuni.14 Report on Prosecutorial Strategy (Ripoti juu ya Mkakati wa Kuendesha mashtaka) (ICC-OTP 2006),uk. 7; Prosecutorial Strategy: 2009-2012 (Mkakati wa Kuendesha mashtaka: 2009-2012) (ICC-OTP 2010),uk. 8, 14, 16-18.15 Mwendesha Mashtaka dhidi ya Lubanga, “Hukumu kwa mujibu wa kifungu cha 74 cha Mkataba”,103

Novemba 2016Sera ya Watoto7.Katika Mpango Mkakati 2012-2015, Ofisi iliinua suala hili na kuliweka katikamalengo sita ya kimkakati, huku ikiahidi “kuwa makini kuhusu makosa yajinai ya kingono na kijinsia na makosa ya jinai dhidi ya watoto”.16 Ahadi hiiilithibitishwa katika Mpango Mkakati 2016-2018, ambao ulikuwa na malengomengi ikiwemo “kuendelea kuingiza mtazamo wa kijinsia katika maeneoyote ya kazi ya Ofisi na kuwa makini kuhusu makosa ya jinai ya kingono nakijinsia na makosa ya jinai dhidi ya watoto na yanayoathiri watoto, kulinganana sera za Ofisi.”178.Sera hii inaenda sambamba na Mpango Mkakati na itachangia katika kufikiamalengo ya kimkakati. Inatilia mkazo makosa ya jinai dhidi ya watoto auyanayoathiri watoto zinazofanywa wakati wa vita na katika mazingiramengine yaliyo chini ya mamlaka ya Mahakama.9.Sera hii ina malengo yafuatayo: Kuthibitisha ahadi ya Ofisi ya kuwa makini kuhusu makosa ya jinaidhidi ya watoto au yanayoathiri watoto; Kutoa ufafanuzi na mwelekeo kwa wafanyakazi katika fasiri namatumizi ya Mkataba na Kanuni, katika hatua zote za kazi ya Ofisi, ilikushughulikia kwa ufanisi makosa ya jinai dhidi ya watoto auyanayoathiri watoto; Kuhakikisha kwamba uhusiano kati ya wafanyakazi na watotounafanyika kwa makini na heshima inayofaa kwa maslahi yao na hakizao chini ya sheria za kimataifa;18 Kukuza na kuendeleza utamaduni wa utendaji bora kuhusu kutetea hakiza watoto, ikiwa ndani ya Ofisi au kwa ujumla; naICC-01/04-01/06-2842, 14 Machi 2012 (“Hukumu ya Lubanga”).16 Mpango Mkakati, Juni 2012-2015 (ICC-OTP 2013), uk. 27.17 Mpango Mkakati 2016-2018 (ICC-OTP 2015), uk. 19.18 Sura 2, Sehemu 3 ya Kanuni za Maadili za Ofisi ya Mwendesha Mashtaka.4

Novemba 2016 Sera ya WatotoKuchangia, kwa njia ya utekelezaji wa Sera hii, maendeleo endelevu yasheria za kimataifa kuhusu makosa ya jinai dhidi ya watoto auyanayoathiri watoto.10.Ofisi huchapisha sera zake kwa maslahi ya kukuza uwazi, ufafanuzi nauhakika katika utekelezaji wa mfumo wa kisheria. Uchapishaji, usambazajina utekelezaji wa Sera hii huweza kuimarisha ushirikiano na kusaidianamiongoni mwa watendaji (kwa mfano, Nchi, ikiwa ni pamoja na mamlaka yakitaifa ya kutekeleza sheria na mamlaka ya kisheria, taasisi za kimataifa,mameneja wa migogoro na wapatanishi, mashirika yasiyo ya kiserikali navikundi vya utetezi) kuhusu masuala yanayowahusu watoto. Sera hii hukuzaheshima ya haki za watoto, na hutafuta kuimarisha uwajibikaji kwa, nakuzuia, makosa ya jinai dhidi ya watoto au yanayoathiri watoto.11.Misingi ya Sera hii ni Mkataba, Kanuni, Taratibu za Mahakama na Taratibuza Ofisi, na inaenda sambamba na nyaraka nyingine za sera. Pale ambapoinafaa, inayo pia misingi katika mikataba husika ya kimataifa, hasa mkatabakuhusu haki za watoto (CRC) na kanuni na vifungu v

Ufupisho I. Utangulizi II. Sera ya Ujumla III. Mfumo wa Kisheria . Ofisi itatumia mbinu nyeti kuhusu watoto katika nyanja zote za kazi zake zinazohusisha watoto. Mbinu hii huchukulia mtoto kama mtu binafsi na hutambua . waathirika peke yake huenda sambamba na Mkataba wa Roma. 2 Dibaji ya Mkataba, aya. 9. Angalia Mfuko wa Kimataifa wa Watoto .

Related Documents:

May 02, 2018 · D. Program Evaluation ͟The organization has provided a description of the framework for how each program will be evaluated. The framework should include all the elements below: ͟The evaluation methods are cost-effective for the organization ͟Quantitative and qualitative data is being collected (at Basics tier, data collection must have begun)

Silat is a combative art of self-defense and survival rooted from Matay archipelago. It was traced at thé early of Langkasuka Kingdom (2nd century CE) till thé reign of Melaka (Malaysia) Sultanate era (13th century). Silat has now evolved to become part of social culture and tradition with thé appearance of a fine physical and spiritual .

Bulletin d’information hebdomadaire du Bureau du Procureur 27 Le Bureau publie sa décision au sujet de l’examen préliminaire de la situation en Palestine 3 avril ‐ Le Bureau du Procureur a publié sa décision au sujet de l’examen préliminaire qu’elle mène sur la situation en Palestine.

On an exceptional basis, Member States may request UNESCO to provide thé candidates with access to thé platform so they can complète thé form by themselves. Thèse requests must be addressed to esd rize unesco. or by 15 A ril 2021 UNESCO will provide thé nomineewith accessto thé platform via their émail address.

̶The leading indicator of employee engagement is based on the quality of the relationship between employee and supervisor Empower your managers! ̶Help them understand the impact on the organization ̶Share important changes, plan options, tasks, and deadlines ̶Provide key messages and talking points ̶Prepare them to answer employee questions

Dr. Sunita Bharatwal** Dr. Pawan Garga*** Abstract Customer satisfaction is derived from thè functionalities and values, a product or Service can provide. The current study aims to segregate thè dimensions of ordine Service quality and gather insights on its impact on web shopping. The trends of purchases have

Chính Văn.- Còn đức Thế tôn thì tuệ giác cực kỳ trong sạch 8: hiện hành bất nhị 9, đạt đến vô tướng 10, đứng vào chỗ đứng của các đức Thế tôn 11, thể hiện tính bình đẳng của các Ngài, đến chỗ không còn chướng ngại 12, giáo pháp không thể khuynh đảo, tâm thức không bị cản trở, cái được

Le genou de Lucy. Odile Jacob. 1999. Coppens Y. Pré-textes. L’homme préhistorique en morceaux. Eds Odile Jacob. 2011. Costentin J., Delaveau P. Café, thé, chocolat, les bons effets sur le cerveau et pour le corps. Editions Odile Jacob. 2010. Crawford M., Marsh D. The driving force : food in human evolution and the future.