Zana Ya Elimu Ya Dijitali - CORE

2y ago
239 Views
2 Downloads
1.80 MB
28 Pages
Last View : 14d ago
Last Download : 3m ago
Upload by : Bria Koontz
Transcription

Zana ya Elimu ya DijitaliSehemu ya 1: Maarifa ya Jumla ya Elimu ya DijitaliSehemu ya 2: Programu za LughaSehemu ya 3: Programu za AjiraSehemu ya 4: Programu za Elimu

Utangulizi wa Economic Integration SuiteEconomic Integration Suite (EIS) imegawanywa katika sehemu 4: Sehemu ya kwanza niMuhtasari wa mada saba za Elimu ya Dijitali. Sehemu 3 zifuatazo zinahusiana na programuna zinakagua njia 3 za masomo ya dijitali, ikiwemo Masomo ya Lugha ya Kiingereza, Ajirana Elimu. Fomu zote 24 za maelezo zimeundwa ili kuongeza stadi zako za dijitali na ujasiriwa kuendelea kuwa mshindani katika uchumi wa dijitali.JEDWALI LA YALIYOMO LA EISSehemu ya 1: Muhtasari1.1 App Stores1.2 Kufuatilia Matumizi ya Data1.3 Kuepuka Ulaghai1.4 Ufuatiliaji Watoto1.5 Kudhibiti Historia yako ya Dijitali1.6 Programu Hasidi, Virusi, Ulinzi dhidi ya Virusi na Kinga Mtandao1.7 Taarifa za KupotoshaSehemu ya 2: Lugha2.1 Rosetta Stone2.2 Lingokids2.3 Duolingo2.4 Tarjimly2.5 Google TranslateSehemu ya 3: Ajira3.1Google lassdoor3.7Zoom3.8 CreditWiseSehemu ya 4: Elimu4.1 Huduma za Elimu Duniani (World Education Services)4.2 SettleIn4.3 Coursera4.4 Google Hangouts

Watu MaarufuKwa kila fomu ya maelezo kuhusu programu, mtu maarufu anatoa taarifa kuhusumipangilio ya lugha, ufikiaji wa mifumo yote ya dijitali, matumizi ya datayanayotarajiwa na gharama. Pia, kuwa makini kuhusu alama za JILINDE au FAHAMUzilizo chini ya kila fomu ya maelezo.Mipangilio ya LughaProgramu inapatikana katika zaidi ya lugha 2Programu inapatikana katika lugha 1-2Ufikiaji wa Mifumo Yote ya DijitaliInapatikana kama programu ya wavuti na yacha mkononi na ufikiaji kwenye vifaa vyoteInapatikana tu kama programu ya mkononi nainafikiwa kwenye simu za mkononi na tabletiMatumizi ya Data YanayotarajiwaProgramu hutuma na kupokea taarifa mara kwamara kutoka kwenye minara ya simu za mkononiWakati imeunganishwa kwenye Wi-Fi, taarifainaweza kupakuliwa kwa matumizi ya nje yamtandaoTaarifa nyingi zinahifadhiwa kwenye programuna kupatikana kwa matumizi ya nje ya mtandaoGharama InayotarajiwaMatumizi ya Bila MalipoGharama inatofautiana kulingana na usajili,lakini programu inaweza kuwa na toleo la bilamalipo lenye vipengele vichacheAlama ya JILINDE inaonyesha ujumbe muhimuwa usalama kwa watumiaji wa programuAlama ya FAHAMU inaonyesha maelezomuhimu ya kujua unapotumia programu.

1.1 ELIMU YA DIJITALI I MuhtasariApp StoresProgramu ni zana za dijitali zinazotumiwa kutekeleza majukumu kwa mambo ya binafsi na kazi. Programu zawavuti zimeundwa kwa matumizi kwenye kompyuta, huku programu za mkononi zikiwa zimeundwa kwamatumizi ya simu za mkononi. Nyingi ya programu hizi huhitaji watumiaji kupakua programu moja kwamoja hadi kwenye vifaa vyao. Hata hivyo, baadhi ya programu za wavuti zinahitaji mtandao na hakunakupakua. Baadhi ya programu kama vile Microsoft Word, programu unayoweza kutumia kuandikawasifukazi na barua za maelezo mafupi, zinapatikana katika miundo yote miwili, lakini nyinginezinapatikana tu katika muundo mmoja. Unaweza kupakua na kusakinisha baadhi ya programu bila malipo.Programu nyingi zinaweza kununuliwa, kupakuliwa na kusakinishwa kupitia tovuti ya msanidi programuau kupitia mfumo wa kusakinisha programu.Mifumo ya Usakinishaji wa ProgramuMisimbo ya QRApp store unayotumia hutegemea kifaa unachomiliki. Ikiwa unaiPhone, tumia App Store. Ikiwa una kifaa cha Android, tumia GooglePlay Store na ikiwa una kifaa cha Samsung, tumia Galaxy Store.Misimbo ya QR, au Jibu la Haraka, nimisimbopau inayohifadhi data. Data hiiinaweza kujumuisha viungo vya wavuti,viungo vya kupakua programu, tiketi, autaarifa nyingine zinazoweza kuletwa nakuchanganua msimbo. Ingawa iPhonezinazotumia iOS 11 au toleo la juu na simu zamkononi za Android Pixel zinawezakuchanganua misimbo ya QR kiotomatiki,simu nyingi mahiri hutumia programuzinazoweza kupakulika kama vile GoogleLens na Kisomaji cha Msimbo wa QR ilikufanya hivyo.App StoreMfumo huu wa kusakinisha programu unafikiwa kiotomatikikwenye kifaa chochote cha Apple kinachotumika kwenye Mfumowa Uendeshaji wa Apple (iOS). App Store inatoa programuzilizoundwa na Apple na wasanidi programu wa nje.Google PlayMfumo huu wa kusakinisha programu unafikiwa kiotomatikikwenye kifaa chochote kinachotumika kwenye mifumo yauendeshaji ya Android. Mfumo huu una programu zilizosanidiwa naGoogle na wasanidi programu wa nje.Galaxy StoreMfumo huu wa kusakinisha programu unafikiwa kiotomatiki kwenyekifaa chochote kinachotumika kwenye mfumo wa uendeshaji waSamsung. Mfumo huu mara nyingi huwa na programu zilizosanidiwahaswa na, au kwa ajili ya mfumo wa uendeshaji wa Samsung.Hebu ijaribu sasa! Pata na upakuekichanganuzi cha QR cha bila malipokutoka App store yako. Kisha, jaribukuchanganua Msimbo wa QR uliohapa chini ili kufikia CORE Nav!CORE Nav hukupa taarifa kuhusu mada nyingikuhusu maisha nchini Marekani. Madanyingine zinajumuisha kujifunza Kiingereza,ajira, udhibiti wa pesa na elimu.

1.2 ELIMU YA DIJITALI I MuhtasariKufuatilia Matumizi ya DataIngawa kompyuta, simu za mkononi na vifaa vingine vya elektroniki vyenye intaneti vimeletanafasi nyingi za ajira, pia vimeleta changamoto na hatari nyingi. Kutozwa kwa ajili ya data zaidi nakuwa mateka wa uhalifu wa mtandaoni ni vitu viwili maarufu. Masuala haya mengi hutokana namatumizi ya moja kwa moja ya huduma ya intaneti yasiyo ya busara wala uangalifu. Yeyoteanayetumia kifaa kinachounganisha kwenye intaneti anapaswa kuelewa data ya mtandao wasimu na Wi-Fi, jinsi zinavyolipiwa na jinsi ya kuzitumia kwa usalama na kwa bei nafuu.Data ya Mtandao wa SimuWi-FiUnapotumia data ya mtandao wa simu, kifaa chakokinaunganisha kwenye intaneti kwa kutuma na kupokeataarifa moja kwa moja kwenye na kutoka minara ya simuya mkononi, inayodumishwa na Watoa Huduma.Unapotumia Wi-Fi, kifaa kinaunganisha kwenye intanetikwa kutuma na kupokea taarifa kupitia kisambaza data chakaribu. Kisambaza data ni kifaa kinachochomekwa kwenyekebo, kebo za mtandao, au mtandao wa Digital SubscriberLine (DSL) na pia inatoa huduma ya intaneti pasiwayakwenye vifaa ndani ya nusu kipenyo iliyowekwa.Watoa Huduma wa Simu za Mkononi hutoa mipango yadata ambayo huwaruhusu wateja kulipa ada mojainayofidia kiasi cha matumizi ya data kwa kipindikilichowekwa, au ada moja kwa matumizi ya data bilaukomo. Unapotafuta mipango ya data, unaweza kuonaofa kama vile ifuatayo: Jigabaiti mbili (GB) za fidia ya 34.99 kwa mwezi. Katika mipango hii, wakati mtumiajianazidisha kikomo cha data yake ya kila mwezi, anatozwakwa data ya ziada kwa kiwango cha juu kwa GB. Mtejaanaweza pia kutarajia kulipa ada za ziada zaidi kwakuzidisha kikomo chake cha data.Kwa jumla, kipimo data cha Wi-Fi kinatozwa bei moja.Unalipia jumla na unaweza kuitumia mara kwa mara aukidogo unavyohitaji. Hakuna tunu kwenye matumizi yako.Ili kuweka mtandao wa Wi-Fi wa faragha nyumbanimwako, utahitaji kununua au kukodisha kisambaza datakutoka kwa Mtoa Huduma za Intaneti. Kuna WatoaHuduma Wengi wa Intaneti wa kuchagua. Hakikisha kuwaumefanya utafiti na kulinganisha kampuni ili upate beinzuri! Mwulize Msimamizi wako wa Huduma ikiwa kunamapunguzo ya Wi-Fi kwa familia za mapato ya chiniunayoweza kutuma ombi.Kwenye simu na tableti nyingi, mipangilio ya Wi-Fi na simu yamkononi inafikiwa kwa urahisi. Ili kufuatilia matumizi ya datayako, zima data ya mtandao wa simu yako ukiwa eneo lenyeWi-Fi. Pia unaweza kuchagua kuzima data ya mtandao wa simukwa programu mahususi. Ukichagua kufanya hili, inaamishautaweza tu kufikia programu hizi wakati kifaa chakokimeunganishwa kwenye Wi-Fi.Biashara nyingi hutoa Wi-Fi bila malipo kwa wateja wanaolipa.Kuunganisha kwenye Wi-Fi ya umma bila malipo hukuruhusukufikia intaneti bila kuhitaji kutumia data ya mtandao wa simuambayo ni ghali, lakini si salama sana! Wadukuzi na wahalifu wamitandao wanaotumia mtandao uo huo wa Wi-Fi bila malipowanaweza kujaribu kufikia manenosiri, majina ya watumiaji,taarifa za benki na barua pepe zako. Wakati usalama unahusika,unganisha ukitumia data yako ya simu ya mkononi!

1.3 ELIMU YA DIJITALI IMuhtasariKuepuka UlaghaiUlaghai ni jaribio la uongo la kumhadaa mtu kwa njia ambayo inamnufaisha kifedha mtuanayehadaa, kwa hasara ya mtu anayehadaiwa. Ni muhimu kuelewa aina chache maarufu zaulaghai na kujua jinsi ya kuzitambua.Ulaghai MaarufuHapa chini pana mifano minne ya ulaghai maarufu. Kuna mamiazaidi. Kwa jumla, tahadhari kuhusu simu, barua pepe, au ujumbe wamaandishi unaotoa ofa ambazo ni za kutilia shaka, zinatoa vitisho aushtuma, zimejaa makosa ya hijai na sarufi, au kuomba TaarifaZinazotambulisha Binafsi (PII).Fedha za Ushindi ZisizotarajiwaKatika ulaghai huu, mtu anayehadaiwa anatumiwa mawasilianona kuambiwa kuwa ameshinda pesa, bidhaa, au huduma katikashindano ambalo hakushiriki. Anaombwa atume pesa au PII ilikudai fedha za ushindi. Fedha hizi za ushindi huwa hazitumwi.Ukiwa na PII yako, mtu anayehadaa anaweza kufikia akaunti yakoya benki na kuhamisha akiba yako hadi kwenye akaunti yakebinafsi.Mashirika ya Hisani ya UongoKatika ulaghai huu, mtu anayehadaiwa anatumiwa mawasilianona mtu anayejifanya kuwa mwakilishi wa shirika la hisani, ambayebaadaye anaomba pesa. Tafuta mashirika ya hisani mtandaoni iliuthibitishe uhalali wayo na utumie tu vituo salama vya mchangokutoa mchango wa pesa.Kodi UnazodaiwaKatika ulaghai huu, mtu anayehadaiwa anapigiwa simu na mtuanayedai kuwa mwakilishi wa Huduma ya Mapato ya Ndani(Internal Revenue Service, IRS) au tawi jingine la serikali, akitishakukamatwa au kufukuzwa nchini isipokuwa alipe ada fulani. IRShaitawahi kuomba PII, hivyo usitoe zako! Ukipigiwa simu ya ainahii, angalia nambari ya simu ya anayepiga katika kivinjari chako.Hii itakusaidia kujua ikiwa nambari iliripotiwa awali kuwa yaulaghai. Ikiwa una wasiwasi, ripoti tukio kwa Msimamizi wako waHuduma.Ofa za Kazi Bila KuzionaKatika ulaghai huu, mtu anayehadaiwa anatumiwa mawasilianona kampuni bandia inayompa kazi kabla hajahojiwa ana kwa anawala kutuma ombi rasmi. Usiwahi kumpa mwajiri mtarajiwa PIIyako bila kuthibitisha uhalali wao.Je, Taarifa ya KutambulishaBinafsi ni Nini?Taarifa ya Kutambulisha Binafsi (PII) ni taarifayoyote ambayo inayoweza kukutambulishabinafsi. Inajumuisha, lakini si tu yafuatayo: Nambari za Ruzuku ya SerikaliMajina KamiliTarehe za KuzaliwaAnwaniNambari za Akaunti ya BenkiJe, ni dalili ganizinazoonyesha kuwaujumbe huu ni wa ulaghai?Hujambo Bi. Sanchez,Ujumbe huu unatoka Cleveland Police.Unadaiwa 2000 za kodi za jiji. Usipolipapesa hizi kufikia mwisho wa mwezi,UTAKAMATWA!Afisa ametumwa nyumbani kwako.Anapowasili MUDA UTAKUWA UMEISHA!Kwa sababu malipo yamechelewa,utahitaji kulipa kwa njia ya kadi ya malipoya kulipa mapema. Sauti isiyo rasmiOmbi la kadi ya kulipia mapemaJe, nini kingine?

1.4 ELIMU YA DIJITALI I MuhtasariKuwafuatilia WatotoKama mzazi katika kipindi cha dijitali, kufuatilia shughuli za mtoto wako mtandaoni kunaweza kuwakugumu. Ni muhimu kuwafunza watoto kuhusu intaneti, ambayo itakuwa sehemu ya maisha yao ya jamii,elimu na taaluma. Wakati uo huo, ni muhimu kulinda watoto dhidi ya vipengee vyenye madhara kuhusuintaneti, ikijumuisha unyanyasaji mtandaoni, maudhui yasiyofaa, unyanyasaji kifedha na wawindanjiwatoto mtandaoni. Udhibiti wa mzazi na zana za kufuatilia ni muhimu kwa kuwalinda watoto wenu.Misamiati MuhimuKitu cha KuangaziaProgramu mpya ya Android na iOS (Apple) inajumuishaudhibiti wa mzazi uliojengewa ndani. Programu za ziada zaudhibiti wa mzazi zinapatikana bila malipo, au nunuakwenye mifumo ya kusakinisha programu (kwa maelezozaidi kuhusu app stores, kagua 1.1).Kuna njia nyingi ambazo watoto na vijanawanaweza kutumia kwenye intaneti. Kama wazazi,kuelewa unyanyasaji mtandaoni na wawindajiwatoto mtandaoni kunaweza kukusaidia kuzuia.Unyanyasaji mtandaoniUnyanyasaji mtandaoni ni kutuma, kuchapisha, aukushiriki maudhui hasi, yanayodhuru au ya uongokumhusu mtu kwenye ujumbe wa maandishi,programu, mitandao ya jamii, mijadala, au michezo yavideo ambapo watu wanaweza kutazama, au kushirikimaudhui na wengine.Wawindaji Watoto MtandaoniWawindaji watoto mtandaoni ni watumiaji wamtandaoni ambao ni watu wazima wanaowatumiavibaya watoto kwa kutumia teknolojia ya dijitalikutafuta na kuwalenga watoto.Vichujio vya maudhuiZana hizi huzuia watoto kufikia maudhui yasiyofaa kwaumri. Vichujio vya maudhui vinapatikana kwenyeprogramu, vifaa na vivinjari vingi.Vidhibiti vya MatumiziVidhibiti hivi huzuia muda ambao watoto wanafikiaprogramu fulani, saa ambazo wanatumia programufulani na ikiwa wanaweza au hawawezi kufikiaprogramu kabisa.Zana za UfuatiliajiZana hizi huwaruhusu wazazi kufuatilia eneo la vifaa,kuona kile ambacho watoto wanafanyia vifaa vyao nakujifunza kuhusu vipengee vingine vya matumizi yao.Programu na michezo mingi huonekana kwenyeununuzi ndani ya programu. Hizi huwaruhusuwatoto kufanya ununuzi halisi wa fedha.Inapowezekana, zuia ununuzi wa ndani ya programukwa kusasisha mipangilio ya udhibiti wa mzazi nakuepuka kuunganisha taarifa yako ya benki kwenyeduka la programu.Maudhui ya vurugu, ngono, au yasiyofaayanapatikana kila mahali kwenye intaneti.Mwepushie mtoto wako hatari kwa kukagua tovuti,michezo na programu kabla ya kuwaruhusu watotowako kuzitumia.Inawezekana kumwepushia mtoto wako hatari yamaudhui yanayodhuru, lakini si kuyazuia kikamilifu.Hakikisha kuwa umejadili usalama wa intaneti nawatoto wako moja kwa moja. Stadi hizi nyingizitakuwa muhimu katika vipengee vingine vyamaisha yao.

1.5 ELIMU YA DIJITALI I MuhtasariKudhibiti Historia yako ya DijitaliHistoria yako ya dijitali ni rekodi ya elektroniki ya kila kitu unachokifanya kwenye intaneti. Kila ujumbewa maandishi, barua pepe, machapisho ya mitandao ya jamii, picha, ununuzi na mambo unayotafutakwenye intaneti huhifadhiwa milele. Kuna safu mbili za historia hii ya dijitali. Safu ya kwanza ni taarifazinazoweza kufikiwa na mtumiaji yeyote wa intaneti. Ya pili, ni taarifa zinazoweza kufikiwa na MtoajiHuduma wako wa Intaneti, mashirika, serikali na wahalifu wa mtandaoni. Ni muhimu kuelewa jinsitaarifa hizi zinavyokusanywa, zinachoweza kufanyiwa na jinsi ya kuzidhibiti.Misamiati MuhimuMatangazo MaalumTovuti nyingi hutumia historia yako ya jumla ya dijitalikutangaza bidhaa kutoka kwenye tovuti ulizotembelea awali.Mtandao wa Faragha wa Dijitali (Virtual PrivateNetwork, VPN)VPN hukupa faragha mtandaoni kwa kuuunda mtandao wafaragha kutoka kwenye muunganisho wa intaneti yaumma. VPN husaidia kuzuia wahalifu wa mtandaonikuingilia data unayotuma na kupokea kutoka kwenye kifaachako. Visambaza data vingi vya intaneti vina VPN. KuwekaVPN kunaweza kugharimu ada kidogo ya kila mwezi (kwamaelezo zaidi kuhusu visambaza data, pitia 1.2).Kuvinjari kwa Faragha (Hali ya Chinichini)Unapotumia kivinjari cha intaneti, kinaweza kurekodiunachofanya, kuhifadhi manenosiri na taarifa za fedha nakupakua vidakuzi kutoka kwenye tovuti ulizotembeleaawali. Kuvinjari kwa faragha huzuia baadhi ya mambo hayana ni muhimu haswa kutumia ukiwa kwenye kompyutainayotumiwa na watu wengi.VidakuziVidakuzi ni data iliyotumwa kutoka kwenye kivinjari chaintaneti na kuhifadhiwa kwenye kompyuta yako. Hatua hiihuruhusu tovuti kukumbuka na kurekodi manenosiri nahistoria ya kuvinjari. Tovuti ikikuonya kuwa hutumiavidakuzi, kwa kutumia tovuti unaipa ruhusa kufikia historiayako ya jumla ya dijitali, hatua inayoweza kusababishakutumiwa matangazo yanayokulenga.Historia Yako Msingiya DijitaliWaajiri na wenye nyumba wanaweza kutafutakwenye akaunti ya mitandao ya jamii ya mwajiriwa aumpangaji mtarajiwa ili kupata maelezo zaidi kumhusu.Mwajiri akipata akaunti yako ya Twitter, Facebookau Instagram, atafikiria nini?Ili kudhibiti historia yako msingi ya dijitali, unawezakufanya mambo mawili. Kwanza, weka mipangilioyako ya faragha unayopendelea kwenye akaunti zakozote za mitandao ya jamii. Pili, chapisha tu kitu ikiwahuna tatizo kila mtu akikiona. Kuna uwezekano wawao kukiona wakati wowote!Historia Yako ya Jumlaya DijitaliSi tu kile unachokusudia kuweka hadharanikinachobadilisha historia yako ya dijitali. Mashirika,mamlaka ya kutekeleza sheria, serikali na wahalifuwa mtandaoni hukusanya taarifa kutoka kwawatumiaji wa intaneti. Taarifa zako zinawezakutumiwa kwa njia nyingi, kuanzia kuundamatangazo yanayokulenga hadi kuiba kitambulishochako.Ni wakati gani ambapo shirika linaweza kutoataarifa zilizo kwenye historia yako ya dijitali kwamamlaka ya kutekeleza sheria? Je, ni halali?Ingawa ni halali kwa mashirika kushiriki historia yakoya dijitali, baadhi ya kampuni zina sera zinazopingahatua hiyo. Unaweza kulinda historia yako ya dijitalikwa kutumia huduma ya VPN kuficha uwepo wakomtandaoni, kuvinjari katika hali ya faragha ili kuzuiavidakuzi na kuwa mwangalifu kwakile unachokifanya mtandaoni!

1.6 ELIMU YA DIJITALI I MuhtasariProgramu Hasidi, Virusi, Ulinzi dhidi ya Virusi na Kinga MtandaoKuna njia nyingi ambazo walaghai na wahalifu wa mtandaoni wanaweza kutumia kufikia taarifa zako. Pindiwanapofikia kifaa chako, au kufuatilia Taarifa Zinazokutambulisha Binafsi, wanaweza kufungua akaunti zamkopo kwa jina lako, kutoza ununuzi kwenye akaunti yako ya hundi na kuiba pesa kwenye akaunti yako yaakiba. Virusi na programu hasidi ni zana msingi zinazotumiwa kuwasaidia wahalifu katika jitihada hizi.Kilinde kifaa chako na ujilinde kwa programu za kuzuia virusi na kinga mtandao!Misamiati MuhimuProgramu HasidiProgramu hasidi ni aina yoyote ya programumbaya iliyoundwa ili kupata idhini ya kufikia, aukuharibu kifaa cha elektroniki. Mara nyingi huwaimeundwa ili kuiba pesa. Virusi vya kompyuta niaina ya programu hasidi inayoruhusu wahalifu wamtandaoni kufikia taarifa zako za benki nakuvuruga muamana wako (kwa maelezo zaidikuhusu muamana, pitia 4.1).Virusi vya KompyutaVirusi vya kompyuta ni programu hasidi, aumsimbo, unaokusudia kubadilisha jinsi kifaakinavyofanya kazi. Virusi vinaweza kusambaabaina ya vifaa vilivyounganishwa, kuibamanenosiri, kurekodi mibonyezo ya kibodi, failimbovu, wawasiliani wa barua pepe taka na hatakumiliki kifaa. Husambaa kupitia viambatisho vyabarua pepe, faili na programu zilizopakuliwa namaudhui ya mitandao ya jamii yaliyoshirikiwa.Ulinzi dhidi ya VirusiIshara za KuonyeshaKuwa Huenda UnaVirusi Jinsi ya Kuzuia Virusina Programu HasidiKampuni mbalimbali, kama vile Norton, huundaprogramu za kuzuia virusi. Vifurushi hivi vyaprogramu zinazoweza kupakuliwa hugharimu adaya kila mwezi, lakini hutoa ulinzi thabiti dhidi yaprogramu hasidi na virusi. Kinga Mtandao Kinga mtandao ni sawa na programu ya kuzuiavirusi kwa muunganisho wako wa intaneti.Hufuatilia na kudhibiti trafiki ya mtandaoinayoingia na kutoka. Pia huweka vizuizi baina yamitandao ya ndani ya kuaminika na mitandao yanje isiyoaminika.Madirisha ya kuibuka marakwa maraMabadiliko kwenye ukurasawako wa mwanzoBarua pepe zilizotumwa kutokakwenye akaunti yakoambazo hukuandikaKompyuta au programu kuachakufanya kazi mara kwa maraUtendakazi uliopunguakuliko kawaidaProgramu zisizojulikanakwenye kifaa chakoShughuli zisizo za kawaida Usibofye kwenye matangazoyanayoibukaTumia miunganisho salama yamtandao na usishiriki skrini walakuunganisha kompyuta ambazohazina ulinzi dhidi virusi.Kagua faili kila wakati kablaya kuzipakuaTumia programu unayoaminiya ulinzi dhidi ya virusi

1.7 ELIMU YA DIJITALI IMuhtasariTaarifa za KupotoshaIntaneti imerahisisha kupatikana kwa taarifa. Huruhusu pia usambazaji wa taarifa kwa haraka.Leo, unaweza kupata taarifa kwa urahisi kuhusu matukio ya sasa mtandaoni, lakini si kila kituunachosoma kwenye intaneti ni cha kweli. Iwe umepata taarifa yako kwenye mitandao ya jamiiau chanzo cha habari, unapaswa kuangalia usahihi wa unachosoma mtandaoni ili kuthibitishaikiwa ni za kweli.Habari BandiaHabari bandia ni kauli ya kisasa inayoeleza taarifa zakupotosha kwenye mitandao ya jamii, kama vileFacebook na Twitter. Kauli sasa inatumiwa sana na watuna vyombo vya habari, Habari bandia inamaanisha kuwataarifa ni za uongo na hazina vyanzo, wala manukuu yakuweza kuthibitisha. Habari bandia zinaweza kumaanishakosa. Kwa mfano, ikiwa chanzo cha habari kinashirikitaarifa ambazo hazikuangaliwa usahihi, ambazokitatambua baadaye kuwa za uongo. Habari ban

1.4 ELIMU YA DIJITALI I Kuwafuatilia Watoto. Kama mzazi katika kipindi cha dijitali, kufuatilia shughuli za mtoto wako mtandaoni kunaweza kuwa kugumu. Ni muhimu kuwafunza watoto kuhusu intaneti, ambayo itakuwa sehemu ya maisha yao ya jamii, elimu na taaluma. Wakatiuo huo, ni muhimu kulinda watoto dhidi

Related Documents:

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekuwa ikiboresha Mtaala wa Elimu ya Msingi kuhakikisha kwamba elimu inayotolewa ni bora na inayomwandaa mwanafunzi kumudu maisha katika mazingira yake. Muktadha huu umeifanya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia iboreshe mchakato wa kufundisha

4.3.1 Elimu ya malezi ya awali na makuzi (ECEC), utambuzi wa mapema na afua za mapema (EIEI) . ECC Mtaala wa Msingi Uliopanuliwa ECEC Elimu ya awali ya utotoni na Uangalizi . MUHTASARI Ripoti hii ya dunia juu ya elimu jumuishi ina

Ingawa Sera ya Elimu ya Awali ipo, mafanikio ya sera hii ni madogo sana. Elimu ya Awali ilijumuishwa moja kwa moja katika elimu ya msingi (2014) lakini shule nyingi hazina madarasa mazuri ya elimu ya awali. Sekta ya shule za awali hazina walimu wenye st

Hali ya Elimu Andika idadi halisi ya huduma zilizopo kijijini. Idadi V401. Idadi ya shule za msingi za serikali V402. Idadi ya shule za msingi za binafsi V403. Idadi ya vituo vya elimu ya awali V404. Idadi ya shule za sekondari V405. Idadi ya shule za ufundi V406. Kuna kamati ya elimu na hu

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Imefadhiliwa na Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DFID) Agosti, 2017 MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU YA SEKONDARI (MUES) EQUIP-Tanzania. Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MU

wa mitaala ya elimu na mafunzo ili ikidhi mahitaji ya maendeleo ya Taifa. Aidha, Serikali itaendeleza matumizi ya lugha ya Kiswahili, Kiingereza, Alama, pamoja na lugha nyingine za kigeni katika elimu na mafunzo. Vilevile, itaendelea kuinua ubora wa mfumo wa upimaji, tathmini na utoaji vyeti katika ngazi zote.

RIPOTI YA DUNIA YA UFUATILIAJI WA ELIMU ilIcMUHTASARI Dibaji Ripoti yaDunia ya Ufuatiliaji wa Elimu ya mwaka wa 2019imeandaliwa kwa kuwashirikisha timu ya wahamiaji wa kimataifa. Wanne kati yao ni watoto wa wakimbizi. Ha

5 I. Academic Writing & Process . 2. 1 Prepare . 2. 1. 1 What is the assignment asking you to do? What kind of assignment is it? (E.g. essay, research report, case study, reflective