MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU YA

2y ago
477 Views
6 Downloads
3.69 MB
60 Pages
Last View : 13d ago
Last Download : 3m ago
Upload by : Annika Witter
Transcription

MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NAELIMU YA SEKONDARI (MUES)Kitabu cha MwanafunziMsichana Timiza Ndoto Yako!

Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwanafunzi - Msichana Timiza Ndoto Yako!

MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGANA ELIMU YA SEKONDARI (MUES)EQUIP-TanzaniaJamhuri ya Muungano wa TanzaniaOfisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR-TAMISEMI)Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.Imefadhiliwa na Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DFID)Agosti, 2017Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwanafunzi - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwanafunzi - Msichana Timiza Ndoto Yako!

YALIYOMOUTANGULIZI . 2MADA YA KWANZA: JINSIA NA MAENDELEO YA KITAALUMA/ KAZI . 3Sehemu ya kwanza: Tafsiri ya dhana .3Sehemu ya Pili: Majukumu ya Kijinsi na Kijinsia.6Sehemu ya Tatu: Maendeleo ya Kitaaluma na Jinsia.7MADA YA PILI: MIMI NA MALENGO YANGU . 11Sehemu ya kwanza: Mimi ni nani? .11Sehemu ya pili: Maana, Sababu na Hatua za kuweka malengo .13Sababu na Hatua za kuweka malengo .14Sehemu ya Tatu: Mikakati na mahitaji ili kufikia lengo .15Sehemu ya nne: Kupanga na kufikia malengo.15MADA YA TATU: KUFANYA MAAMUZI NA KUTATUA MIGOGORO NA CHANGAMOTO . 17Sehemu ya kwanza: Kufanya Maamuzi .17Hatua za kufanya maamuzi .19Sehemu ya pili: Utatuzi wa Migogoro .19Sehemu ya tatu: Mawasiliano .21MADA YA NNE: MSUKUMO WA KUNDI RIKA . 25Sehemu ya Kwanza: Tafsiri ya dhana .25Sehemu ya pili: Athari za misukumo rika .27Sehemu ya tatu: Matamanio na Mahitaji .27Sehemu ya nne: Kukabiliana na Misukumo Rika Hasi na Kukuza Misukumo Rika Chanya .28Sehemu ya tano: Hitimisho la mada.28MADA YA TANO: UBUNIFU WA VYANZO VYA MAPATO . 29Sehemu ya kwanza: Vyanzo sahihi vya ufadhili .29FOMU YA UFADHILI KWA AJILI YA KUJIUNGA NA ELIMU YA SEKONDARI . 31Sehemu ya pili: Njia za kufanya kazi za ubunifu kujipatia kipato .33Sehemu ya tatu: Stadi sahihi za kutumia na kuweka akiba .34MADA YA SITA: JINSI YA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA MWILI KWA WASICHANA . 37Sehemu ya kwanza: Tafsiri ya dhana .37Sehemu ya pili: Mzunguko wa hedhi .39Sehemu ya tatu: Usafi wakati hedhi .41Sehemu ya nne: Jinsi ya kutengeneza pedi zinazoweza kutumika tena .42MADA YA SABA: UKATILI WA KIJINSIA . 43Sehemu ya Kwanza: Maana ya ukatili wa kijinsia .43Sehemu ya Pili: Ukatili dhidi ya Wasichana/Wanawake .43Sehemu ya Tatu: Ubakaji na rushwa ya ngono .44Sehemu ya Nne: Mazingira hatarishi yanayopelekea kufanyiwa vitendo vya ukatili .47Sehemu ya Tano: Ndoa na Mimba za Utotoni .47Sehemu ya sita: Mimba za Utotoni na Madhara ya Mimba za Utotoni .48MADA YA NANE: MAAMBUKIZI YA MAGONJWA YA NGONO NA KUACHA KUFANYA NGONO . 51Sehemu ya Kwanza: Magonjwa ya ngono .51Sehemu ya pili: Kudhibiti mihemko na kuepuka ngono .52Sehemu ya tatu: Mbinu za Kuepuka Mihemko ya Kingono na Ngono .53Sehemu ya nne: Tabia Hatarishi.54Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwanafunzi - Msichana Timiza Ndoto Yako!1

UTANGULIZIKitabu hiki kimeandaliwa na Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania) kwakushirikiana na Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wizara ya Elimu, Sayansi naTeknolojia (WyEST), Taasisi ya Elimu Tanzania, CAMFED-Tanzania na TGNP Mtandao.Kitabu hiki kinakusudiwa kutumika na mwanafunzi muda wote wa utekelezaji wa Mpango wa utayari wakujiunga na Elimu ya Sekondari, (MUES) unaolenga kuwapatia wasichana stadi za msingi za maisha ilikuweza kujiunga na kumaliza kwa ufanisi elimu ya sekondari.Vijana wakiwemo wasichana wanapambana na changamoto nyingi ikiwemo: Kuongezeka kwa idadi yamimba na ndoa za utotoni; Kuacha shule; kutumia madawa ya kulevya; matatizo ya kujamiiana na afyaya uzazi kama vile ubakaji maambukizo ya magonjwa yatokanayo na kujamiaina (STIs ) nk. Hivyo kitabuhiki kimesheni mada mbali mbali zitakazomsaidia kijana haswa wa kike kuweza: Kutambua umuhimuwa kutii maadili; Kujifunza kuhusu mabadiliko ya mwili; Kushughulikia hisia na tabia, na njia za kuepukana kutataua migogoro inayoweza kuathiri maisha yao; Na zaidi kujua jinsi ya kupanga kuhusu maishayao ya baadaye (kujijua yeye ni nani sasa, anaelekea wapi, anatarajia kuwa nani, na namna ya kufika kuleanakotaka kuwa ili kuweza kutizmia ndoto yake hapo baadaye)Kitabu kina jumla ya mada kuu nane zenye vipengele mbalimbali ambazo zitafundishwa wa mudawa wiki nane. Kitabu ina kazi nyingi za kuvutia, mazoezi na taarifa za uhakika za kumsaidia msichanakwenye safari yake ya kufikia ndoto zake za maisha. Mwanafunzi ana wajibu wa kukitunza na kuwanacho muda wote anaposhiriki kwenye mpango wa MUES.2Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwanafunzi - Msichana Timiza Ndoto Yako!

MADA YA KWANZA: JINSIA NA MAENDELEO YAKITAALUMA/ KAZISEHEMU YA KWANZA: TAFSIRI YA DHANAJinsiNi maumbile ya kibaiolojia yanayotofautisha viumbe kuwa mwanamke au mwanaume kutokana natofauti iliyopo ya viungo vya uzazi.Mfano:Binadamu:Wanyama:kati ya mwanamke na mwanaume.kati ya mbuzi jike na mbuzi dume.Zoezi la KwanzaKatika makundi ya watano watano kamilisheni kuchora maumbile ya binadamu yanayotofautisha jinsimbili (mwanamke na mwanaume).Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwanafunzi - Msichana Timiza Ndoto Yako!3

JinsiaMahusiano yaliyojengeka baina ya makundi mbalimbali katika jamii yanayohusisha wanawake nawanaume ambayo huweza kubadilika wakati wowote kulingana na nyakati, mazingira, hali yauchumi, mila na desturi katika jamii husika. Mahusiano haya huweza kutofautiana baina ya jamii mojana nyingine.Jinsia inachangia kuwepo kwa tofauti kati ya mwanamke na mwanaume katika mgawanyo wamajukumu, rasilimali, mamlaka na nafasi za maamuzi. Hali hii husababisha jamii kuwapa wanawake nawanaume hadhi, majukumu na kazi tofauti.Jinsia haitegemei maumbile ya kibaiolojia, bali imejengwa kutokana na mila na desturi za jamii husikana pia hutofautiana kutoka jamii moja hadi nyingine. Mfano, katika jamii nyingi ni jambo la kawaidakabisa kwa mwanamke kupika, kufua, kuosha vyombo na kazi nyingne za nyumbani. Endapo kazi hizozitafanywa na mwanaume huonekana kuwa ni jambo geni.Zoezi la PiliJadilianeni katika vikundi na kuwasilisha majibu.1.2.3.4.Taja kazi zinazofanywa na wanawake tu katika jamii yakoTaja kazi zinazofanywa na wanaume tu katika jamii yakoNani aliefanya maamuzi ya mgawanyo wa kazi hiziUna maoni gani juu ya mgawanyo huu wa kazi na unakuathiri vipi?Mfumo dumeHuu ni utaratibu uliojengeka katika maisha ya jamii unaowapa wanaume mamlaka ya umiliki warasilimali, kutoa maamuzi na kauli ya mwisho hivyo kumfanya mwanamke aonekane duni, dhaifu nahana thamani. Mfumo dume unachukulia kuwa mwanaume ni kipimo cha uwezo, mamlaka na umilikiUmejengeka katika ngazi zote kuanzia kaya, jamii, kitaifa hadi kimataifaUnaendelezwa na sera, sheria, michakato na mikakati ya maendeleoKwa kiasi kikubwa mfumo dume husimamiwa na wanaumeMfano, katika familia nyingi wasichana hupangiwa kazi za nyumbani kama vile kupika, kulea, usafi na kazinyingine wakati wavulana huhimizwa kujisomea na kusikiliza taarifa katika vyombo vya habari, kuchezana kufanya mazoezi na masomo ya shuleni.Vyanzo vinavyokuza na kuendeleza mfumo dume ni pamoja na: 4malezi na makuzimifumo ya ukolonimila na desturiutandawaziMpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwanafunzi - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Zoezi la TatuFanyeni kazi ifuatayo katika makundi ya watano watano na kuwasilisha.a. Wanafunzi kwa ubunifu wao wafanye igizo dhima linaloonesha dhana ya mfumo dume.b. Wanafunzi waainishe kazi tofauti zinazofanywa na wasichana na wavulana kuanzia asubuhi hadi usiku.c. Nini kifanyike kuleta usawa katika mgawanyo wa kazi.Mawazo mgando ya kijinsiaZoezi la NneAngalia mfano wa katuni hapo chini, fikiria kisha utaje dhana, fikra, mitazamo na tabia zilizopo juu yawasichana na wavulana. Ziweke katika makundi ya Ke au Me katika jedwali linalofuata.Kha! We kilaza kweliwa HisabatiKha! Nyie wasichanani vilaza kweli waHisabatiMpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwanafunzi - Msichana Timiza Ndoto Yako!5

Mitazamo au dhana juu ya Wanawake (Ke)a)b)c)d)Mitazamo au dhana juu ya Wanaume (Me)Je, ni kweli mitazamo au dhana tajwa hapo juu zinawahusu wanawake au wanaume? Jadili.Je, kuna mitazamo au dhana ambazo umeorodhesha kwa wanawake ziko kwa wanaume na kwawanaume ziko kwa wanawake?Chukua mfano wa mtazamo au dhana moja iliyotajwa hapo juu jadili. Je, ni wanawake wote au niwanaume wote wako hivyo?Kwa majibu uliyotoa hapo juu andika maana ya neno mawazo mgando ya kijinsia kwa manenoyako.SEHEMU YA PILI: MAJUKUMU YA KIJINSI NA KIJINSIAZoezi la KwanzaAngalia kazi zilizoorodheshwa kwenye jedwali hapo chini kisha ainisha kazi zinazofanywa na wanaumeau wanawake kwa sababu ya maumbile yao ya kibaiolojia (majukumu ya jinsi). Je ni kazi zipi zinafanywana wanawake au wanaume kwa sababu ya mfumo na taratibu za kijamii (majukumu ya jinsia).kubeba ujauzito; kutungisha mimba; kunyonyesha; kukata kuni; kupika; kupata hedhi; kupatandoto nyevu; kuchota maji; kufanya kazi za matengenezo; kuhudumia watoto nyumbani.Ainisha kazi tajwa hapo juu katika jedwali lifuatalo:Majukumu ya Jinsi6Majukumu ya JinsiaMpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwanafunzi - Msichana Timiza Ndoto Yako!

SEHEMU YA TATU: MAENDELEO YA KITAALUMA NA JINSIAZoezi la KwanzaOrodhesha aina mbalimbali za kazi au ujuzi kufuatana na mwanzo wa herufi katika alfabeti.A: G:M: T:B: H:N: U:C: I:O: V:D: J:P: W:E: K:R: Y:F: L:S: Z:Zoezi la PiliChora picha ya ndoto yako kuonesha unavyotaka kuwa siku za usoni.Mimi nataka kuwa nani?Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwanafunzi - Msichana Timiza Ndoto Yako!7

Zoezi la TatuSoma hadithi zifuatazo kisha jibu maswali yanayofuata.Hadithi ya KwanzaPalikuwa na baba mmoja alikuwa akisafiri safari ya mbali. Kwenye safari hiyo alikuwa pamoja na mwanaewa kiume na pia walisafiri kwa gari yao binafsi.Njiani waliona vitu vizuri vinavyovutia sana vikiwemo wanyama, miti mbalimbali pamoja na mauamazuri. Wote walijawa na furaha katika safari yao na walikuwa na mategemeo kuwa wangefika sikuhiyo jioni sana. Baba huyu alimpenda sana mtoto wake na alitamani aje amuone akiwa ni mtotomwenye mafanikio.Baada ya muda mrefu kuwa barabarani ambapo baba ndio alikuwa akiendesha gari hilo, kwa bahatimbaya walipishana na lori kubwa sana lililokuwa likiendeshwa kwa kasi na wakapata ajali mbaya sanakwa kuwa gari lao liligongana uso kwa uso na lori lile.Watu walikimbilia eneo la tukio kwenda kutoa msaada, kwa bahati mbaya Baba yule alikuwa amepotezauhai wake palepale. Hali ya mtoto wake ilikuwa ni mbaya sana, kwa bahati nzuri alikimbizwa hospitalikwa ajili ya matibabu. Alipofika hospitali kijana huyo aliingizwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi. Baada ya uchunguzi wa haraka ilionekana kuwa mtoto huyo anahitaji upasuaji wa haraka ili kuwezakuokoa maisha yake. Daktari aliyekuwa zamu alipewa taarifa kuwa anahitajika ili aweze kutoa hudumaya upasuaji kwa mtoto huyo aliyekuwa mahututi. Mara Daktari alipoingia kwenye chumba cha upasuaji,alifadhaika na kukosa furaha. Kisha alisema kwa uchungu sana “Huyu ni mwanangu, ni mtoto wangusitaweza kumpatia huduma ya upasuaji”. Daktari yule alitoka kwenye chumba cha upasuaji akiwa analia.Ilibidi hospitali ifanye utaratibu wa kumpata daktari mwingine ili mtoto yule apatiwe matibabu.Fikiri na jibu maswali yafuatayo:1. Je, unafikiri daktari aliyeshindwa kutoa huduma ya upasuaji alikuwa ni mzazi wa mtoto huyo?Toa jibu lako na ueleze sababu.2. Je, ni kazi au fani gani nyingine ambazo watu hufikiri ni kwa ajili ya wanawake tu au wanaumetu? Je ni sawa? Kwanini?Hadithi ya PiliAmina na Maria ni wasichana wenye umri wa miaka ishirini. Wasichana hawa walikuwa ni marafiki sana.Walipomaliza darasa la saba walifaulu vizuri sana masomo ya sayansi, baadaye walijiunga na elimu yaSekondari na hatimaye Chuo Kikuu. Huko walisomea fani ya ufundi-magari. Baada ya kuhitimu chuokikuu walipata kazi katika gereji nzuri na ya kisasa iliyomilikiwa na mjomba wake Maria. Walifanya kazikatika gereji hiyo kwa muda wa miaka mitano, wakati huo walipata ujuzi na uzoefu wa kutosha na hivyoiliwasababisha kuwa na ndoto ya kumiliki gereji ili waweze kujiajiri wenyewe na kuajiri wafanyakaziwengine. Pia walikuwa wamejizolea sifa za ufundi ulio mahiri. Mabinti hawa wawili walishakuwawameweka akiba ya fedha za kutosha ambazo zingewawezesha kufungua gereji yao, ambayowangependa iitwe “A&M” gereji.8Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MUES) - Kitabu cha Mwanafunzi - Msichana Timiza Ndoto Yako!

Siku moja Amina aliona gereji ambayo ilikuwa haitumiki na alipata matamanio kuifanya sehemu hiyokuanzisha biashara yao ya gereji. Mara moja alimpigia mmiliki wa gereji hiyo Ndugu Malingumu nakumuuliza kama wanaweza kukodi sehemu hiyo. Ndugu Malingumu alijibu kuwa hakuna tatizo naalimuagiza akamwambie mume wake ili aende kwa mazungumzo.Baada ya siku mbili Amina na Maria walikwenda kumuona Ndugu Malingumu ili waweze kumlipagharama zote za kukodi gereji ile. Ndugu Malingumu alimuuliza Amina “Mume wako yuko wapi?”na Amina alimjibu“ Sisi ndiyo tunaotaka kukodi gereji hii na fedha za malipo ya awali tayari tunazo”Ndugu Malingumu alicheka sana akasema “nini! Yaani nyie wasichana mnataka kukodi gereji hii?Msitake nicheke!” Amina na Maria wakamjibu “Bado hatujaolewa, sisi ni mafundi mahiri wa magari”Ndugu Malingumu akawajibu kwa kejeli “sikilizeni ninyi mabinti, siwezi kukukodisha gereji yangu,sitaki kupata hasara kwani hakuna atakae kuja kutengeneza gari yake kwenye gereji yenu, tenainayoendeshwa na wanawake! Hamtakuwa na uwezo wa kulipia kiwango cha pango kitakachobakia.”Maswalia. Una maoni gani kuhusu hadithi hiyo hapo juu?b. Ungekuwa wewe ni Amina au Maria ungejisikiaje? Kwanini?c. Je, kwa namna gani mmliki wa gereji ameonyesha ubaguzi wa kijinsia?d. Ni mawazo gani mgando ya kinjisia aliyonayo Ndugu Malingumu kuhusiana na wanawake?e. Je, ni namna gani mawazo haya mgando ya kinjisia ya Ndugu Malingumu yamewaathiri Amina naMaria?f. Je, unafikiri mawazo hayo mgando ya kinjisia yanaweza kuathiri wateja ambao wangehitaji kutengenezewa magari katika gereji hiyo? Kwanini?g. Je, ungewashauri nini Amina na Maria?h. Je, kuna mawazo

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Imefadhiliwa na Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DFID) Agosti, 2017 MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU YA SEKONDARI (MUES) EQUIP-Tanzania. Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MU

Related Documents:

Kuchambua nadharia ya mpango wa utayari wa kuanza shule. Kuandaa azimio la kazi la wiki nne (4) na andalio la somo lenye mwelekeo wa kumjengea mtoto umahiri tarajiwa. Kuweka mikakati ya ufundishaji wa wiki nne(4) kwa ufanisi. Kufanya upimaji na tathmini ya maendeleo ya watoto kwa kutumia mbinu zilizopendekezwa katika mwongozo.

“michango” – ada ya ziada kwa ajili ya gharama za uendeshaji wa shule. Awali, ada hii ya ziada ilikua kigezo cha kujiunga na elimu ya . za serikali kutoa e

za uendeshaji wa shule. Awali, ada hii ya ziada ilikua kigezo cha kujiunga na elimu ya sekondari ya kidato ch

fedha za kigeni. Hata hivyo, kutokana na maendeleo duni ya sayansi na teknolojia pamoja na kutokuwepo kwa usawa katika soko la dunia kumesababisha pato la nchi kuwa dogo na kufanya vyuo vya elimu ya ualimu kutovutia wanafunzi wengi wa ualimu kujiunga navyo. Jitihada za makusudi zinahitajika i

Ms. Fika Mwakabungu - Mkurugenzi Idara ya Mafunzo na Mitaala . kuwasiliana kwa lugha ya Kiswahili, Utambuzi, Kuhusiana, Kujenga Mwili na Kuthamini Mazingira. Aidha mwongozo huu unatoa maelekezo ya kutumia . Kufanya upimaji na tathmini ya maendeleo ya watoto kwa kutumia mbinu zilizopendekezwa katika mwongozo.

(1990s). Toleo hilo la Ghana lilitayarishwa kutokana na mitaala ya mafunzo mingine mbalimbali ya PATH, ikiwemo Kuelekea kwenye Utokomezaji wa Ukeketaji: Mawasiliano kwa Ajili ya Mabadiliko – Mtaala kwa ajili ya Wakufunzi wa Wafanyakazi wa Afya ya Jamii, Watayarishaji wa Afya ya Jamii, Watetezi wa Vijana, na Waalimu (PATH:2001).

na matokeo ya utafiti wa kufuatilia matumizi ya umma/utafiti wa viashiria vya utoajiwa huduma (Service delivery indicator survey) (public expenditure tracking survey) katika sekta ya elimu. ripoti imetolewa wakati ambapo nchi inaingia katika Mpango wa pili wa Kipindi cha Kati (Medium Term Plan—MTP)

The Asset Management Strategy supports our strategic priority to: To provide quality, well maintained homes that are fit for the future . Page 5 of 10 Asset Management Strategy 2018 The strategy supports our growth aspirations and development strategy. A key principle is that any development decision will complement and enhance our current asset portfolio. Our aim is that: We invest in our .