Serikali Ya Mapinduzi Ya Zanzibar

1y ago
13 Views
2 Downloads
585.98 KB
75 Pages
Last View : 5d ago
Last Download : 3m ago
Upload by : Averie Goad
Transcription

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAROFISI YA RAIS NA MWENYEKITI WABARAZA LA MAPINDUZIHOTUBA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YARAIS NA MWENYEKITI WA BARAZA LAMAPINDUZIMHESHIMIWA ISSA HAJI USSI GAVUKUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NAMATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKAWA FEDHA2018/2019MEI, 2018

ORMBLMZANZIBARYALIYOMOYALIYOMOORODHA YA VIAMBATISHOVIFUPISHO VYA MANENO1.UTANGULIZI2.UTEKELEZAJI WA PROGRAMU ZA OFISI YARAIS NA MWENYEKITI WA BARAZA LAMAPINDUZI KWA KIPINDI CHA JULAI – MACHI2017/20182.1 UPATIKANAJI WA FEDHA3.MAFANIKIO YA PROGRAMU ZA OFISI YARAIS NA MWENYEKITI WA BARAZA LAMAPINDUZI KWA KIPINDI CHA JULAI – MACHI,2017/20184.MWELEKEO WA BAJETI YA OFISI YA RAIS NAMWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZIKWA MWAKA WA FEDHA 2018/20195.PROGRAMU KUBWA NA NDOGO NA MAKISIOYA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2018/20196.MAOMBI YA FEDHA KWA KAZI ZILIZOPANGWAKUTEKELEZWA KATIKA MWAKA WA FEDHA2018/20196.1 MATUMIZI YA KAWAIDA NA MRADI WAMAENDELEO6.2 MAOMBI YA FEDHA 2018/20197.MWISHOiiiiiiiiv1457373949494950

ORMBLMZANZIBARORODHA YA VIAMBATISHOKIAMBATISHO 1: RATIBA YA ZIARA YA RAIS UAE52KIAMBATISHO 2: ORODHA YA WAGENI WALIOFIKAIKULU NA KUONANA NA MHESHIMIWA RAIS KUANZIAAGOSTI 2017 HADI APRILI, 201855KIAMBATISHO 3: VIPINDI VILIVYORUSHWA HEWANINA IDARA YA MAWASILIANO NA HABARIIKULU-ZANZIBAR 2017-201859KIAMBATISHO 4: WAFANYAKAZI WALIOPATIWAMAFUNZO KWA MWAKA 2017/201861KIAMBATISHO 5: IDADI YA WATUMISHIWALIOKWENDA LIKIZO63KIAMBATISHO 6: ORODHA YA TAASISI ZILIZOFANYIWAUPEKUZI64KIAMBATISHO 7: IDADI YA WATUMISHI WALIOPEWAMAFUNZO YA UDHIBITI NA UTUNZAJI SIRI NA TAASISIWANAZOTOKA65KIAMBATISHO 8: ORODHA YA NYARAKA ZA SERA NASHERIA ZILIZOJADILIWA NA BARAZA LA MAPINDUZIKWA KIPINDI CHA JULAI – MACHI 2017/201866KIAMBATISHO 9: MAPITIO YA UPATIKANAJI WAFEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2017/201867KIAMBATISHO 10: MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZIYA BAJETI KWA MWAKA WA FEDHA 2018/201969iii

ORMBLMZANZIBARVIFUPISHO VYA ECOZRBZURAUmoja wa AfrikaBaraza la WawakilishiChama Cha MapinduziSoko la pamoja la Nchi za Mashariki na Kusinimwa AfrikaJumuiya ya Afrika MasharikiOfisi ya Usalama wa SerikaliJumuiya ya Nchi zilizopakana na Bahari yaHindiKikosi Maalum cha Kuzuia MagendoMkakati wa Kukuza Uchumi na KupunguzaUmasikini ZanzibarOfisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza laMapinduziOfisi ya Makamu wa Pili wa RaisOfisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZKamati ya Kusimamia Hesabu za Mashirika yaUmmaJumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwaAfrikaChuo Kikuu cha Taifa cha ZanzibarShilingi ya TanzaniaUmoja wa Falme za KiarabuUkosefu wa Kinga MwiliniWizara ya Biashara na ViwandaWizara ya Elimu na Mafunzo ya AmaliWakala wa Serikali wa UchapajiShirika la Utangazaji ZanzibarTaasisi ya Viwango ZanzibarShirika la Umeme ZanzibarBodi ya Mapato ZanzibarMamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji naNishati Zanzibariv

kutoahojakwamba Baraza lako tukufu, likae kama Kamatikwa madhumuni ya kupokea, kujadili, kuzingatiana hatimae kuidhinisha Makadirio ya Mapato naMatumizi ya Fedha ya Ofisi ya Rais na Mwenyekitiwa Baraza la Mapinduzi kwa mwaka wa fedha2018/2019.2.Mheshimiwa Spika, awali ya yote, sina budikumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu, muumbawa mbingu na ardhi kwa kutujaalia kufika hapatukiwa katika afya njema na furaha. NamuombaMwenyezi Mungu aendelee kutudumisha katikaamani na utulivu nchini petu. Atuzidishie imanithabiti ya kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduziya mwaka 2015- 2020 katika kuwatumikia wananchiwetu kufikia maendeleo tuliokusudia.3.Mheshimiwa Spika, naomba kumpongeza kwadhati kabisa Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza laMapinduzi kwa umahiri wake wa kuiongoza nchi yetuna kusimamia ipasavyo utekelezaji wa majukumuya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kufuataIlani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 20152020 na Mipango Mikuu ya Kitaifa.4.Mheshimiwa Spika, tabia ya uwazi na uadilifuya Mheshimiwa Dk. Shein katika uongozi wake nimiongoni mwa mambo yanayoimarisha uwajibikaji1

ORMBLMZANZIBARna kuharakisha maendeleo kwa wananchi wavisiwa vyetu vya Unguja na Pemba siku hadi siku.Namuomba Mwenyezi Mungu amzidishie hekima nabusara katika kuwatumikia wananchi, ili tuendeleekufaidika na uongozi wake ongeza wewe binafsi, naibu wako MheshimiwaMgeni Hassan Juma na Wenyeviti wa Barazalako Tukufu, Mheshimiwa Mwanaasha KhamisJuma na Mheshimiwa Shehe Hamadi Mattar kwakuliongoza vyema Baraza hili. Katika uongozi wakotumeshuhudia uendeshaji wa mijadala iliyo wazikatika nidhamu ya hali ya juu ya WaheshimiwaWajumbe wa Baraza lako.6.Mheshimiwa Spika, shukrani maalum ziendekwa Kamati ya Kudumu ya Baraza la Wawakilishiya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifainayoongozwa na Mwenyekiti; Mheshimiwa OmarSeif Abeid, Mwakilishi wa Wananchi wa Jimbo laKonde. Kamati hii, kwa kipindi chote ambachotumefanya kazi nayo, imekuwa ikishirikiana nasipamoja na ushauri ambao uliiwezesha Ofisi ya Raisna Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kutekelezamajukumu yake kwa ufanisi zaidi.7.Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Kamati za Kudumuza Baraza la Wawakilishi zimefikia ukomo kwa mujibuwa kanuni zetu, nachukua fursa hii, kabla ya kuziundaupya Kamati hizi, kuwashukuru sana Wajumbe waKamati hii kwa uweledi wao waliotuonesha wakati2

ORMBLMZANZIBARwakifanya kazi nasi. Nawatakia kila la kheri nakuwaahidi kuwa tutakuwa nao pamoja katika kazizetu na tutaendelea kusikiliza ushauri wao.8.Mheshimiwa Spika, sambamba na hilo, natoashukurani zangu za dhati kwa Kamati nyengine zaKudumu za Baraza la Wawakilishi zinazofanyakazikwa karibu na Ofisi ya Rais na Mwenyekiti waBaraza la Mapinduzi ambazo ni Kamati ya Bajetiinayoongozwa na Mheshimiwa Mohamed SaidMohamed (Dimwa), Mwakilishi wa wananchi waJimbo la Mpendae na Kamati ya Kudumu ya Barazala Wawakilishi ya Hesabu za Mashirika ya Umma(PAC) inayoongozwa na Mheshimiwa Miraji KhamisMussa (Kwaza), Mwakilishi wa wananchi wa Jimbola Chumbuni.9.Mheshimiwa Spika, mabadiliko ya tabia nchiyamesababisha kuwa na misimu ya mvuaisiyotabirika. Mvua za masika zilianza vizuri katikawiki ya kwanza kwa kunyesha kwa wastani nahazikuleta athari kubwa kwa wananchi. Hata hivyo,katika wiki ya pili mvua kubwa zilishuhudiwa katikamwambao mzima wa pwani ya Afrika Masharikiambazo zilileta maafa kwa baadhi ya wananchiwetu. Nawapa pole wale wote walioathirika namvua hizi kwa namna moja au nyengine.10. Mheshimiwa Spika, taarifa ya Mamlaka ya Haliya Hewa nchini Tanzania imetabiri kuwapo kwamvua kubwa katika msimu huu wa masika kwenyemaeneo yote ya Unguja na Pemba na mwambao3

ORMBLMZANZIBARmzima wa Afrika Mashariki. Kutokana na utabirihuo, nawaomba wananchi wachukue tahadhari yahali ya juu kujiepusha na madhara yanayowezakusababishwa na mvua hizo. Hata hivyo, ni muhimupia kuzitumia mvua hizo vizuri kadri inavyowezekanakatika kuimarisha shughuli za kilimo.11. Mheshimiwa Spika, namalizia utangulizi wangukwa kutoa shukurani zangu maalum kwa Wananchiwote wa Zanzibar kwa umoja na mshikamano waona kudumisha amani na utulivu. Aidha, kwa heshimakubwa nawapongeza wananchi kwa kuendeleakuunga mkono Serikali yao inayoongozwa naChama cha Mapinduzi katika jitihada zake zakuwaletea maendeleo. Natoa wito kwa wananchiwote tuendelee kutunza amani yetu tukizingatiakwamba pasipo amani na utulivu hukosekana;na panapokosekana utulivu maendeleo hayawezikupatikana.12. Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo yautangulizi, sasa naomba uniruhusu niwasilishe kwaufupi Utekelezaji wa Programu za Ofisi ya Rais naMwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kipindi chaJulai – Machi 2017/2018.2. UTEKELEZAJI WA PROGRAMU ZA OFISI YA RAISNA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI KWAKIPINDI CHA JULAI – MACHI 2017/201813. Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Rais na Mwenyekitiwa Baraza la Mapinduzi kwa mwaka wa fedha4

ORMBLMZANZIBAR2017/2018 ilitekeleza Programu kuu tano na ndogo11 chini ya Mafungu mawili ambayo ni A01 na A02.Programu Kuu hizo ni kama zifuatazo:-i. Programu ya Kusimamia Huduma na Shughuliza Mheshimiwa Rais na Kuimarisha MawasilianoIkulu;ii. Programu ya Kuratibu Ushirikiano wa Kikanda,Mashirika ya Kimataifa na Wazanzibari WanaoishiNje ya Nchi;iii. Programu ya Utawala na Uendeshaji wa Ofisi yaRais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi;iv. Programu ya Usimamizi wa Majukumu yaKikatiba na Kisheria ya Baraza la Mapinduzi naKamati ya Makatibu Wakuu; nav. Programu ya Utumishi na Uendeshaji wa Ofisiya Baraza la Mapinduzi.14. Mheshimiwa Spika, Utekelezaji wa Programuhizi, ulizingatia Mipango Mikuu ya Kitaifa ikiwemoIlani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015 2020, MKUZA, pamoja na Mpango Mkakati wa Ofisiya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.2.1 UPATIKANAJI WA FEDHA15. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha2017/2018, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Barazala Mapinduzi ilitengewa jumla ya TZS. milioni8,342.6 kwa mafungu yake mawili. Fungu A01lilitengewa jumla ya TZS. milioni 6,634.7. Katiya hizo TZS. milioni 730.0 kwa ajili ya mradi wa5

ORMBLMZANZIBARmaendeleo na TZS. milioni 5,904.7 kwa ajili yakazi za kawaida. Fungu A02 lilitengewa jumla yaTZS. milioni 1,707.9. Hadi kufikia mwezi Machi,2018 Fungu A01 liliingiziwa jumla ya TZS. milioni4,605.0 sawa na asilimia 78 kwa ajili ya matumiziya kawaida na TZS. milioni 730.0 sawa na asilimia100.0 kwa ajili ya mradi wa maendeleo. Aidha,fungu A02 liliingiziwa TZS. milioni 1,263.0 sawa naasilimia 74.0.16. Mheshimiwa Spika, kupitia Programu zake, Ofisiilitekeleza bajeti yake ya 2017/2018 na kuwekavipaumbele katika maeneo yafuatayo:-i. Kusimamia utekelezaji wa majukumu ya Kikatibana Kisheria ya Rais, Baraza la Mapinduzi na Kamatizake;ii. Kusimamia utekelezaji wa kazi za Baraza laMapinduzi, Kamati zake na Kamati ya MakatibuWakuu kwa kuzingatia Katiba na Sheria za Nchi;iii. Kuwahudumia Wananchi kwa kuzitekeleza ahadiza Mheshimiwa Rais pamoja na kuwapatia taarifaza shughuli za Serikali na maendeleo ambayo nihaki yao ya Kikatiba;iv. Kusimamia utendaji na ufanisi wa kazi katikaORMBLM;v. Kuendeleza ujenzi na kuimarisha usalama wanyumba za Ikulu; navi. Kusimamia maendeleo ya wafanyakazi wa ORMBLMkatika kutekeleza wajibu wao, uendelezaji wamaslahi yao zikiwemo stahiki na haki zao, iliwaweze kutoa huduma kwa wananchi ipasavyo.6

ORMBLMZANZIBAR3. MAFANIKIO YA PROGRAMU ZA OFISI YA RAISNA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI KWAKIPINDI CHA JULAI – MACHI, 2017/201817. Mheshimiwa Spika, naomba kulithibitishia Barazalako Tukufu kwamba Ofisi ya Rais na Mwenyekitiwa Baraza la Mapinduzi kwa mwaka wa fedha2017/2018 ilitekeleza bajeti yake kwa mafanikiomakubwa kupitia Programu zake zote.Programu ya Kusimamia Huduma na Shughuli zaMheshimiwa Rais na Kuimarisha Mawasiliano Ikulu18. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha2017/2018, Programu hii iliidhinishiwa TZS. milioni3,664.1 kwa matumizi ya kawaida na maendeleo.Hadi kufikia mwezi Machi, 2018 iliingiziwa TZS.milioni 2,379.8 sawa na asilimia 81 kwa kazi zakawaida na TZS. milioni 730.0 sawa na asilimia 100kwa kazi za maendeleo.19. MheshimiwaSpika,mafanikiomakubwayamepatikana kupitia Programu hii ambaposhughuli za Mheshimiwa Rais zimefanyika vizuri nawananchi wameeleweshwa juu ya shughuli kadhaaza Serikali zikiwemo maendeleo ya kiuchumi nakijamii. Jarida la Ikulu pamoja na vipindi mbalimbali vya Redio na Televisheni vilitayarishwa nakurushwa hewani. Kadhalika, mitandao ya kijamiina magazeti yalitumika katika kuwapatia taarifawananchi na watu mbali mbali.7

ORMBLMZANZIBAR20. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha2017/2018 Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza laMapinduzi, alifanya ziara ya kikazi katika Umojawa Falme za Kiarabu (UAE). Ziara hio, ilianzatarehe 22 hadi 25 Januari, 2018, kufuatia mualikowa Mheshimiwa Sheikh Mohammed Bin Zayed AlNahyan, Mrithi wa Mtawala wa Abu Dhabi na NaibuAmiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya Umojawa Falme za Kiarabu. Katika ziara hio, MheshimiwaRais alifanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wakehuyo.21. Mheshimiwa Spika, Viongozi wengine ambaoMheshimiwa Rais alikutana nao katika ziara hioni Sheikh Mohammed Bin Rashid Al Makhtoum;Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wa UAE naMtawala wa Dubai, Sheikh Dk. Sultan MohammedAl Qasimi; Mtawala wa Sharjah pamoja na SheikhSaud Bin Saqr Al Qasimi; Mtawala wa Ras AlKhaimah. Kadhalika, Mheshimiwa Rais alikutanana Wakuu wa Taasisi mbali mbali wa Falme hizokutokana na ratiba aliyopangiwa. KiambatishoNamba 1 kinahusika.22. Mheshimiwa Spika, mazungumzo ya MheshimiwaDk. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar naMwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Viongozihao yalilenga katika kuendeleza uhusiano naushirikiano uliopo baina ya Falme za Kiarabu,Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar.Kadhalika, mazungumzo hayo yalitoa fursa kwa8

ORMBLMZANZIBARviongozi hao kubadilishana mawazo juu ya mamboya maendeleo ya kiuchumi na kijamii ambapoviongozi wa UAE wameelezea nia yao ya kuendeleakuiunga mkono Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniana Zanzibar katika jitihada zake za kuinua uchumina kuendeleza huduma za jamii.23. Mheshimiwa Spika, wakati akiwa katika ziaraya Umoja wa Falme za Kiarabu, Mheshimiwa Raisna ujumbe aliofuatana nao walipata fursa yakutembelea Mji wa Nishati Mbadala uliopo AbuDhabi (Masdar City) ambao umepiga hatua kubwakatika utafiti na matumizi ya nishati mbadala yajua. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeandaautaratibu wa kuwapeleka Wataalamu wake katikamji huo kwa lengo la kujifunza na kupata uzoefujuu ya nishati mbadala, ili utaalamu watakaoupatauweze kutumika Zanzibar. Kadhalika, MheshimiwaRais alikutana na kufanya mazungumzo naMkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Abu Dhabi (AbuDhabi Fund) ambapo Mfuko huo umeonesha nia yakuendelea kushirikiana na Zanzibar katika mipangoyake ya miradi ya maendeleo.24. Mheshimiwa Spika, miradi mingine iliyotembelewani shamba la kisasa la ufugaji wa ng’ombe wamaziwa liitwalo Al Rawabi. Serikali ya patiwa mafunzo katika shamba hilo hivikaribuni. Kadhalika, Mheshimiwa Rais, alitembeleaMakao Makuu ya RAK GAS; Ras Al Khaimah, nakuelezwa juu ya shughuli mbali mbali zinazofanywa9

ORMBLMZANZIBARna kampuni hio katika utafutaji wa Mafuta naGesi na hatimae Ras Al Khaimah na Zanzibarzimekubaliana kuendelea kutekeleza Maelewano yaAwali (MOU), yaliyotiwa saini tarehe 12 Novomba,2011. Vile vile, jitihada za pamoja baina ya Ras AlKhaimah na Zanzibar zitaendelezwa katika kufanyautafiti wa Mafuta na Gesi.25. Mheshimiwa Spika, kwa jumla, ziara yaMheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti waBaraza la Mapinduzi, katika Umoja wa Falme zaKiarabu, ilifanikiwa sana kuimarisha uhusianokatika maendeleo ya kiuchumi na kijamii. keza kwenye ziara hio, Mheshimiwa Raisameunda Kamati ya Ufuatiliaji ambayo tayariimeanza kazi na kuwasilisha taarifa Serikalini.26. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha wa2017/2018, Mheshimiwa Rais, alifanya ziara yandani katika Mikoa mitano ya Unguja na Pemba.Kwa upande wa Mkoa wa Kaskazini Unguja,Mheshimiwa Rais alitembelea Kiwanda cha SukariMahonda ambacho kimefungwa mashine mpyahivi karibuni.Kadhalika, alikagua mradi wauchimbaji wa visima na usambazaji maji Zanzibaruliofadhiliwa na Jamhuri ya Watu wa China. Mradihuo umekamilika na kukabidhiwa rasmi Serikalinitarehe 19 Aprili, 2018 ambapo wananchi 101,850wa Shehia 21 watafaidika.10

ORMBLMZANZIBAR27. Mheshimiwa Spika, katika ziara hizo, MheshimiwaRais alitembelea kijiji cha Mbuyumaji na Mlilile nakuagiza kujengwa Skuli ya madarasa manne, kituocha afya na barabara. Aidha, aliagiza kupelekahuduma za umeme katika vijiji hivyo. Maagizo hayoyametekelezwa ambapo ujenzi wa madarasa manneya Skuli katika kijiji cha Mbuyumaji umekamilikana ujenzi wa kituo cha afya unaendelea. Vile vile,mradi wa maji na umeme umetekelezwa kwa hatuakubwa. Katika kijiji cha Mlilile huduma za maji sasazinapatikana na barabara imetengenezwa.28. Mheshimiwa Spika, ziara za Mheshimiwa Raisziliendelea katika Mkoa wa Kusini Unguja, kwakutembelea Mradi wa Maji Mitakawani. Mradi huoumeshakamilika na kuanza kutoa huduma kwawananchi tangu tarehe 28 Oktoba, 2017. Vijijivinavyofaidika na huduma za maji za mradi huo niMitakawani, Tunduni, Uzini na Bambi ya Bondeni.Vile vile, katika ziara hio, Mheshimiwa Rais, aliagizaumeme ufikishwe katika pango la Mnywambiji, agizoambalo limeshatekelezwa. Hivi sasa, wananchi waMakunduchi na Kibuteni wanafaidika na huduma yamaji yanayotoka katika pango hilo.29. Mheshimiwa Spika, katika juhudi za Serikaliya Mapinduzi ya Zanzibar ya kuinua Michezo,Mheshimiwa Rais alikagua kiwanja cha MichezoKitogani ambacho ujenzi wake umepiga hatuakubwa na kuwataka wahusika wafanye juhudi yakuukamilisha. Vile vile, Mheshimiwa Rais alikaguanyumba za madaktari Kajengwa Makunduchi11

ORMBLMZANZIBARna Muyuni. Mheshimiwa Rais aliahidi kuiezekapamoja na kuitia milango na madirisha nyumba yamadaktari ya Kajengwa. Ahadi ya Mheshimiwa Raisya kuiezeka nyumba hio ameshaitekeleza.30. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Pemba,Mheshimiwa Rais alifanya ziara ambapo alifunguamadarasa na maabara katika Skuli ya Chokochona kuagiza vifaa vya maabara katika Skuli hiovipelekwe. Vifaa hivyo pamoja na meza na vititayari vimeshapelekwa. Kwa upande wa kilimo,Mheshimiwa Rais alikagua mashamba ya mikarafuuna kutembelea kambi za karafuu na kushirikikatika uchumaji. Mheshimiwa Rais aliagiza juhudizichukuliwe kuyagundua mashamba yote ya Serikaliyaliyofichwa. Idadi ya mashamba yaliyogunduliwayamefikia 9982.31. MheshimiwaSpika,katikakusheherekeaMaadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi Matukufuya Zanzibar, Mheshimiwa Rais alifungua jengo laOfisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali na kuhimizaumuhimu wa ukusanyaji, utumiaji na uhifadhi watakwimu sahihi kwa ajili ya maendeleo. Aidha,mnamo tarehe 6 Januari, 2018, Mheshimiwa Raisalishiriki katika tukio la kihistoria la kuzindua mradiwa umeme katika Kisiwa cha Fundo, Wete, Pemba.Hatua hio, ilikuwa ni miongoni mwa utekelezajiwa ahadi alizozitoa Mheshimiwa Rais wakati waKampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 nautekelezaji wa Ilani ya CCM.12

ORMBLMZANZIBAR32. Mheshimiwa Spika, katika kuhakisha kwambawananchi wanapata habari na taarifa za Serikalina nyenginezo kwa uhakika, Mheshimiwa Dk. AliMohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekitiwa Baraza la Mapinduzi alizifungua Studio mpya zakisasa za Shirika la Utangazaji la Zanzibar (ZBC)tarehe 9 Januari, 2018. Ufunguzi wa Studio hizo,umeiwezesha Televisheni ya Zanzibar, kurejeshahadhi yake ya asili kwa kuwa na mitambo bora nawatangazaji mahiri.33. Mheshimiwa Spika, siku hio hio, MheshimiwaRais alifungua Soko la Kinyasini, Mkoa wa KaskaziniUnguja na kutoa wito kwa wakulima, wavuvi,wafugaji na wananchi wote kwa jumla kulitumiavyema Soko hilo. Shughuli nyengine alizozifanyaMheshimiwa Rais katika maadhimisho ya Shereheza miaka 54 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibarni ufunguzi wa barabara ya Jendele-UngujaUkuu Kaebona, Wilaya ya Kati Unguja ambayoimerahisisha usafiri kwa wananchi wa maeneo hayona kuwawezesha kusafirisha mazao na bidhaa zaombali mbali.34. Mheshimiwa Spika, kama ilivyo kawaida, tarehe12 Januari, 2018 Mheshimiwa Rais alijumuika naWananchi wa Zanzibar na viongozi mbali mbalikatika Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 54 yaMapinduzi ya Zanzibar katika Kiwanja cha Amaan.Kupitia hotuba yake aliyoitoa alielezea mafanikioyaliyopatikana katika sekta zote muhimu zakiuchumi, kijamii na kisiasa katika mwaka 2017.13

ORMBLMZANZIBARAlielezea juhudi, mwelekeo wa uchumi, uendelezajiwa miundombinu ya barabara, viwanja vya ndegena bandari na mchango wake katika kuendelezasekta nyengine, ikiwemo biashara na utalii.35. Mheshimiwa Spika, katika hotuba hio, MheshimiwaRais alifahamisha mafanikio yaliyopatikana katikakuendeleza sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Aliwatakawananchi kuwa imara katika kulinda hali ya amani nautulivu iliyopo ambayo ndio msingi wa mafanikio yetu.Aidha, alielezea mipango na juhudi za Serikali katikakuimarisha na kuulinda Muungano wa Tanganyika naZanzibar wa 1964 uliopelekea kuundwa kwa Jamhuriya Muungano wa Tanzania. Vile vile, alibainisha juhudina mipango ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yakuendeleza ushirikiano na mataifa mbali mbali pamojana mashirika ya Kimataifa.36. Mheshimiwa Spika, katika kuukaribisha mwezimtukufu wa Ramadhani 2017, Mheshimiwa Rais alitoarisala maalum ya kuwataka wananchi kuwa na nyoyoza upendo na huruma baina yao na wageni. Alihimizautamaduni wa kuvumiliana baina ya waumini wa dinimbali mbali katika mwezi wa Ramadhani. Kadhalika,aliwahimiza wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa zachakula kutoka nje ya nchi kuwapa unafuu wa beiwananchi hasa ikizingatiwa kwamba Serikali imetoapunguzo la ushuru wa bidhaa hizo. Aidha, aliwahimizawafanyabiashara wote kuwa waadilifu katikakuendesha shughuli zao na kujiepusha na tamaa zakupandisha bei ya bidhaa bila ya kuzingatia sheria.14

ORMBLMZANZIBAR37. Mheshimiwa Spika, katika hotuba aliyoitoa kwenyeBaraza la Idd-el-Fitri mwaka 2017, MheshimiwaRais alitoa pongezi maalum kwa Waislamu kwakukamilisha Ibada ya Funga ya Mwezi Mtukufu waRamadhani na kuwataka wananchi wote kwa ujumlakuishi kwa mapenzi na kuvumiliana. Alitoa pongezimaalum kwa Taasisi zote za Serikali na Binafsi kwakutoa huduma nzuri kwa wananchi katika kipindichote cha mwezi mtukufu wa Ramadhani. Vilevile, katika hotuba hio, Mheshimiwa Rais alisisitizahaja ya kuimarisha uwajibikaji na uadilifu katikakutekeleza majukumu yetu.38. Mheshimiwa Spika, katika kuukaribisha mwakampya wa 2018, Mheshimiwa Rais aliendelea nautamuduni wake wa kuhutubia wananchi kupitiavyombo vya habari. Katika risala yake, alielezeamatukio makubwa na muhimu yaliyopita katikamwaka 2017 ambayo yalikuwa na umuhimumaalum kwa maendeleo na historia ya nchi yetu.Kupitia Risala hio, Mheshimiwa Rais alitoa salamumaalum za upendo kwa wanafamilia wa wanajeshi14 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waliofarikinchini Congo (DRC).39. Mheshimiwa Spika, shughuli nyengine ambazoMheshimiwa Rais alizifanya katika mwaka wafedha 2017/2018 ni kuufungua Mkutano wa 17 waBaraza la Mawaziri la Umoja wa Nchi za Masharikina Kusini mwa Afrika na Udhibiti wa Biashara yaFedha Haramu tarehe 8 Septemba, 2017, Unguja.Lengo la mkutano huo lilikuwa ni kuweka mikakati15

ORMBLMZANZIBARna kuongeza maarifa ya kupambana na mbinuzinazotumiwa katika kutakatisha fedha haramu.40. Mheshimiwa Spika, katika hatua nyengine,Mheshimiwa Rais alizindua Maonesho ya KilimoKizimbani yaliyofanyika tarehe 10 Oktoba, 2017 nakuhimiza umuhimu wa utumiaji wa mbinu za kisasakatika kuendeleza Kilimo, Ufugaji na Uvuvi. Vile vile,Mheshimiwa Rais alihudhuria katika Kongamanola Kiswahili lililoandaliwa na Baraza la Kiswahilila Zanzibar tarehe 21 Disemba, 2017 ambapoalisisitiza juu ya kuendeleza lugha ya Kiswahilikatika ngazi ya Kimataifa pamoja na matumizi yaKiswahili fasaha.41. Mheshimiwa Spika, akiendelea na shughuli zake,Mheshimiwa Rais alifungua mkutano mkuu waChama cha Walimu Zanzibar, tarehe 10 Februari,2018. Mheshmiwa Rais aliwanasihi walimu kupanuawigo wa shughuli zao kwa kulipatia ufumbuzi tatizola wanafunzi la kuanguka katika mitihani yao nakuutaka uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzoya Amali kuwa karibu zaidi na walimu. Aidha,aliwahimiza walimu kuwa imara katika kutekelezamaagizo ya Serikali ya kutoa elimu bure kuanziangazi ya msingi hadi sekondari.42. Mheshimiwa Spika, miongoni mwa shughulinyengine alizozifanya Mheshimiwa Rais ni kushirikikatika Maadhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar,tarehe 12 Februari, 2018. Katika wadhifa wake waMkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA),16

ORMBLMZANZIBARMheshimiwa Rais alitunuku Stashahada, Shahada,Shahada za Uzamili na Shahada za Uzamivu kwawahitimu wa Chuo hicho tarehe 13 Febuari, 2018.Aidha, Mheshimiwa Rais alizindua ukumbi mpya waChuo hicho uliopewa jina la Dk. Ali Mohamed Shein.43. Mheshimiwa Spika, kama ilivyo kawaida, tarehe01 Mei, 2018. Mheshimiwa Rais, alishiriki katikamaadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani, Wete,Pemba. Katika maadhimisho hayo, Mheshimiwa Raisalisisitiza juu ya suala la uwajibikaji, kuendelezamapambano dhidi ya rushwa na ubadhirifu wamali za Umma pamoja na kuwataka wafanyakaziwaongeze juhudi katika kazi. Vile vile, aliwatakaWaajiri na Chama Cha Wafanyakazi kushirikianana Serikali katika kukabiliana na changamotozinazojitokeza katika sehemu za kazi.44. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha,2017/2018, Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza laMapinduzi, alikutana na Viongozi wa nchi mbalimbali, wakuu wa Taasisi za Kimataifa na Mabalozi.Tarehe 8 Agosti, 2017, Mheshimiwa Rais alikutanana Rais wa Mauritius wa wakati huo, MheshimiwaAmeenah Gurib Fakim. Mazungumzo ya Viongozihao yalikwenda vizuri ambapo masuala yakushirikiana yalitiliwa mkazo. Vile vile, MheshimiwaRais alikutana na Bibi Patricia Janet Scotland,Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Ikulu Ungujaambapo Kiongozi huyo alimthibitishia Mheshimiwa17

ORMBLMZANZIBARRais kwamba Jumuiya ya Madola inaunga mkonojuhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katikakuwaletea maendeleo wananchi wake.45. Mheshimiwa Spika, wageni wengine aliokutananao ni Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS ambaye niNaibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa BwanaMichel Sidibe. Kiongozi huyo aliahidi kushirikiana naSerikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika juhudi zakeza kupambana na maradhi ya UKIMWI. MheshimiwaRais alionana na Mheshimiwa Abdel Fatah El SisiRais wa Misri, tarehe 14 Agosti, 2017, mjini Dares Salaam ikiwa ni moja katika hatua muhimuya kuimarisha uhusiano kati ya Misri, Jamhuri yaMuungano wa Tanzania na Zanzibar kwa jumla.46. Mheshimiwa Spika, katika kipindi hicho,Mheshimiwa Rais, vile vile alikutana na Dk. JoseGraziana da Silva, Mkurugenzi wa Shirika laChakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa. Kadhalika,alikutana na Mheshimiwa Dk. Mohamed Bin HamedAl Rumi, Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman naujumbe wa UNICEF ulioongozwa na Bwana RenevanDeugen. Katika mazungumzo yake na viongozihao, Mheshimiwa Rais amesisitiza umuhimu wakuendeleza na kutekeleza diplomasia ya kiuchumipamoja na kuimarisha viwanda na uwekezajinchini. Orodha kamili ya wageni aliokutana naoMheshimiwa Rais ipo katika Kiambatisho Namba 2.47. Mheshimiwa Spika, naomba kuliarifu Baraza lakoTukufu kwamba wananchi wameendelea kupata18

ORMBLMZANZIBARtaarifa za utekelezaji wa shughuli za MheshimiwaRais kwa wakati na usahihi. Urahisi wa kupatikanahabari kwa haraka umetokana na kuongezeka kwamatumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano(ICT). Hali hii imeshuhudiwa katika ziara zaMheshimiwa Rais katika Umoja wa Nchi za Falme zaKiarabu (UAE) ambapo habari zimeweza kuwafikiawananchi kwa haraka na katika hali ya ubora.48. Mheshimiwa Spika, matoleo manne ya Jaridala Ikulu na toleo moja maalum yamechapishwaambayo yameelezea kwa kina utekelezaji washughuli za maendeleo mjini na vijijini. Jumla yaKalenda 6,300 zimechapishwa zikielezea matukioya shughuli za Mheshimiwa Rais. Katika kipindi hikijumla ya vipindi 15 vya redio na vipindi 6 maalumvya televisheni vimetayarishwa na kurushwa kupitiaZBC vikielezea utekelezaji wa ahadi za MheshimiwaRais na maoni ya wananchi kuhusu utekelezaji waIlani ya Chama cha Mapinduzi. Kiambatisho Namba3 kinatoa ufafanuzi.Programu ya Kuratibu Ushirikiano wa Kikanda,Mashirika ya Kimataifa na Wazanzibari WanaoishiNje ya Nchi49. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha2017/2018, Programu hii iliidhinishiwa jumlaya TZS. milioni 508.1 kwa matumizi ya kazi zakawaida. Hadi kufikia mwezi Machi, 2018 iliingiziwaTZS. milioni 386.6 sawa na asilimia 76 kwa kazi zakawaida.19

ORMBLMZANZIBAR50. Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa programu hiiumeiwezesha Zanzibar kuimarisha ushiriki wenyetija katika Jumuiya za Mtangamano wa Kikanda zaSADC, EAC, IORA na Jumuiya ya Utatu (EAC-SADCCOMESA). Aidha, mahusiano mazuri yameimarikazaidi baina ya Serikali na Wazanzibari wanaoishinje ya nchi yaani Diaspora. Serikali imeendelezadhamira yake ya kuwashajiisha Wanadiasporakushiriki katika kuiletea Zanzibar maendeleo yakiuchumi na kijamii kupitia Kongamano la Nne laWanadiaspora.51. Mheshimiwa Spika, Mkutano wa Kilele wa Jumuiyaya Afrika Mashariki ulifanyika jijini Kampala,Uganda tarehe 23 Februari, 2018. Mkutano huoulijadili mambo mbali mbali ya maendeleo ikiwemomaendeleo ya miundombinu na kuanzisha Taasisiya Fedha na Taasisi nyengine kwa ajili ya utekelezajiwa Itifaki ya Umoja wa Fedha ifikapo 2024.Ajenda nyengine zilizozungumzwa ni pamoja nakuharakisha utaratibu wa Nchi ya Sudan ya Kusinikushiriki kikamilifu katika shughuli za Jumuiyaya Afrika Mashariki na kushajiisha maendeleo yaviwanda vya kutengeneza gari, ili kuifanya Jumuiyakuwa na ushindani katika sekta ya viwanda hivyo.52. Mheshimiwa Spika, mikutano mingine yaWataalamu ilifanyika katika miji ya Dodoma, Dar esSalaam, Nairobi na Kampala ambayo kwa ujumlawake iliratibu utekelezaji wa kusimamia uondoshwajiwa vikwazo vya biashara visivyokuwa vya kiushuruna mapendekezo ya mapitio ya viwango vya pamoja20

ORMBLMZANZIBARvya ushuru wa forodha wa Jumuiya ya AfrikaMashariki. Aidha, Tamasha la Sanaa na Utamadunililifanyika Kampala, Uganda mwezi Septemba,2017. Maonesho ya Biashara ya Jua kali/Nguvukazi yalifanyika mwezi Disemba, 2017 Bujumbura,Burundi yakiwa na lengo la kutengeneza mazingiramazuri ya kibiashara na kutafuta fursa za masokokwa bidhaa za wajasiriamali na Wanasanaa wandani.53. Mheshimiwa Spika, naomba kuliarifu Barazalako Tukufu kuwa mwezi Agosti, 2017 mjiniPretoria, Afrika Kusini kulifanyika Mkutano waKilele wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiyaya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Miongonimwa Ajenda zilizojadiliwa ni pamoja na kuridhiwakwa Jamhuri ya Umoja wa Visiwa vya Comoro kuwamwanachama mpya wa SADC na kuifanya Jumuiyahiyo kuwa na Nchi Wanachama 16. Aidha, Mkutanowa Kilele uliagiza kukamilisha kazi ya tathmini yamaombi ya uwanachama ya Burundi na utekelezajiwa Mpango Mkakati wa Maendeleo ya Viwanda waSADC.54. Mheshimiwa Spika, kufuatia maazimio ya Mkutanowa Kilele, Baraza la Mawaziri wa Nchi za SADClilikutana mwezi Machi, 2018 mjini Pretoria. Katikamkutano huo, miongoni mwa mambo yaliojadiliwa nipamoja na utekelezaji wa

hizi, ulizingatia Mipango Mikuu ya Kitaifa ikiwemo Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015 - 2020, MKUZA, pamoja na Mpango Mkakati wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. 2.1 UPATIKANAJI WA FEDHA 15. Mheshimiwa Spika, mwaka wa fedhakwa 2017/2018, Ofisiya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ilitengewa jumla ya TZS .

Related Documents:

THE CONSTITUTION OF THE STATE OF ZANZIBAR , ¿.vVST¡ncftèrà. 1. Zanzibar subjects by birth. 2. Subjects by descent. 3. Naturalisation of aliens. 4. Registration of minors. 5. Registration of wives of Zanzibar subjects. 6. Women who have ceased to be Zanzibar subjects on marriage. 7. Deprivation of status as Zanzibar subject.

Maana ya Serikali za Mitaa na Dhana ya kupeleka Madaraka kwa Wananchi 2 Mfumo na Muundo wa Serikali za Mitaa 3 Mamlaka za Wilaya 3 Mamlaka za Miji 5 Muundo wa Serikali za Mitaa mbalimbali 6 Kitongoji 6 Mtaa 6 Kijiji 7 Kamati ya Maendeleo ya Kata 7 Mamlaka ya Mji Mdogo 8 Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Jiji (kama vile Mwanza) 8

ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2020 utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015. Vilevile, maudhui ya Ilani hii yamezingatia Mwelekeo wa Sera za Chama Cha Mapinduzi wa 2020-2030, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na Dira ya Maendeleo ya Zanzibar 2020-2050. Aidha, Ilani hii imezingatia fursa na changamoto

KATIBA YA BARAZA LA DIASPORA LA WATANZANIA DUNIANI . umoja na mshikamano, ili kushirikiana na kukuza, hamasa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambayo ni Nchi yetu. Tutazidi kuimarisha mahusiano mazuri, ushirikiano katika kukuza tamaduni, shughuli za kijamii . Halitakua na mlengo wa chama cha .

10. Mheshimiwa Spika, Katiba yetu, chini ya Kifungu cha 9, imeweka bayana kuwa mamlaka ya kuendesha nchi ni ya wananchi wenyewe. Kwamba nguvu na uwezo wa Serikali kufuatana na Katiba unatoka kwa wananchi wenyewe. Ni dhahiri kuwa, pamoja na kutoa ridhaa yao kwa Chama na viongozi wa kuwaongoza, wananchi ndio

tunakuandikia, kwa niaba ya Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kukushauri kutumia mamlaka yako chini ya ibara ya 97(2 . Kiongozi katika muundo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Katiba ya sasa ya Zanzibar imefuta nafasi hiyo na kuunda nafasi mbili

1.1 Importance of the Zanzibar Coastal Zone 1 1.2 Zanzibar s Coastal and Marine Resources 3 1.3 The Increasing Pressure on Coastal Areas and Resources 4 1.4 The need for ICAM and Government Policy Commitment 5 1.5 The Chwaka Bay-Paje Area: A Step Towards ICAM in Zanzibar 5 CHAPTER 2: THE CHWAKA BAY-PAJE AREA 9AJE AREA 2.1 Introduction 9

8 Annual Book of ASTM Standards, Vol 14.02. 9 Annual Book of ASTM Standards, Vol 03.03. 10 Annual Book of ASTM Standards, Vol 03.06. 11 Available from American National Standards Institute (ANSI), 25 W. 43rd St., 4th Floor, New York, NY 10036. 12 Available from American Society of Mechanical Engineers (ASME), ASME International Headquarters, Three Park Ave., New York, NY 10016-5990. 13 .