Migororo Katika Jamii: Kusuluhisha Migogoro Katika

2y ago
173 Views
4 Downloads
256.20 KB
24 Pages
Last View : 9d ago
Last Download : 3m ago
Upload by : Vicente Bone
Transcription

5Sura yaMigororo katika jamii: kusuluhishamigogoro katika maeneo yenyemifugo, kilimo na wanyamapori

5UtanguliziHADITHI YA VIJIJI VIWILIMwaka 2006, mkulima kutoka NarakauwoWilayani Simanjiro alianza kupanda mazao nakujenga majumba kwenye eneo lake lenye ekari60. Punde mkulima kutoka kijiji cha jirani chaLoiborsiret naye aliamua kuliendeleza eneolake. Lakini aligundua kwamba sehemu ya eneohilo lilikuwa limeshaendelezwa na mtu kutokaNarakauwo.Wakulima hao wawili wakazungumza. Kilammoja akatoa cheti cha umiliki alichopewa naViongozi wa Kijiji. Vijiji vyote viwili vilionekanavimo katika ramani, vimeshapimwa na kusajiliwamwaka 1978.Mkulima wa Loiborsiret hakuwa radhi kupoteza hakiyake hivyo alianza kusafisha eneo la ardhi lililokondani ya eneo lenye mgogoro. Punde ndugu,marafiki na viongozi wa vijiji vya pande zote mbiliwalijihusisha katika hayo majadiliano ambayoyaligeuka kuwa mgogoro wa mipaka ya vijiji.Viongozi wa Loiborsiret waliitisha mkutanona wakaamua kwamba, kulingana na ramaniiliyokuwa imesajiliwa, mkulima wao ndiyemmiliki halali wa eneo la ardhi lenye mgogoro.Baada ya hapo wakawafuata viongozi waNarakauwo na kufanya mkutano wa pamojauliohusisha wakazi wote.Utafutaji wa taarifa kuhusu ukweli wasuala hiloKulifuatia mikutano kadhaa ya majadiliano yaliyohusishakamati za vijiji kutoka pande zote mbili pamoja na wazee,viongozi wa kimila na wawakilishi kutoka kwenye Asasiisiyo ya Kiserikali inayofanya kazi kwenye hilo eneo.Majadiliano hayo yalilenga kwenye utafutaji wataarifa: Kulikuwa na hasara au uharibifu gani? Nini chanzo cha mgogoro huo? Historia yake ikoje? Nani mwenye haki juu ya ardhi hiyo, kwa kuwawote wana hati? Eneo hilo ni la kijiji kipi kwa kufuata ramani ipi yampaka wa kijiji?Ramani ziliangaliwa lakini kila upande ulimlaumumwenzake kwa kushindwa kuzisoma hizo ramani vizuri.Migororo katika jamii: kusuluhisha migogoro katika maeneo yenye mifugo, kilimo na wanyamaporiSura ya1

5Migororo katika jamii: kusuluhisha migogoro katika maeneo yenye mifugo, kilimo na wanyamaporiSura yaUtanguliziKualika taasisi au watu walio nje yamgogoroHatimaye wanakijiji walikubali kwamba hizo ramanihazingewasaidia. Wakaamua kuihusisha taasisi nyingine- Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro - ambayo ilipelekawataalamu ambao waliahidi kutopendelea upande wowote.Baada ya kuzisoma zile ramani za vijiji kwa kutumia GPS- njia inayotumia kompyuta kupima kwa uhakika maeneo- hiyo timu ya wataalamu ilisema kwamba mamlaka zaNarakauwo ndizo zilizopanua mpaka lakini hawakupanuampaka wa ramani kwenda Loiborsiret kwa makusudi.Kwa hiyo Kijiji cha Loiborsiret kilishinda mgogorohuo wa ardhi. Vijiji hivyo vilikubaliana: kutengua zile hati mbili za wamiliki ardhi zakwanza na kutoa hati mpya za umiliki; kumhamisha mkulima wa Narakauwo aliyekuwawa kwanza kuiendeleza ile ardhi ili awe mwanakijijiwa kijiji cha Loiborsiret; kumuomba huyo mkulima kusalimisha nusu yaardhi yake ya awali kwa mkulima wa pili (ingawaalifidiwa ardhi mahali pengine); na kuweka mawe ya mipaka ili kuepuka migogorosiku za usoni.Tunachojifunza Usuluhishi wa mgogoro ulitegemea utafutaji wataarifa wa pamoja. Wadau walifanya maamuzikulingana na taarifa hizo. Inaweza kusaidia kuhusisha taasisi au watuwalionje ya mgogoro, kutoka ndani au nje yajamii. Wanaweza kusaidia kufanya utafiti wa kesipamoja na kuwezesha mazungumzo yenye amani. Lengo kuu lilikuwa ni kuendeleza uhusiano uliopo,Wakulima wawili wakibishana juu ya mpaka wa ardhi2Wanaogombea ardhi wakisoma ramani, akiwepo mtu mwingineasiyehusika na mgogoro huokwa hiyo vijiji vililenga katika ushirikiano-suluhishoambalo kila mmoja atanufaika na atakubali, kulikokujaribu kuthibitisha kwamba mmoja wao ndiyealiyekosea. Uaminifu na kusema ukweli ndio ilikuwa muhimukatika kuamua mmiliki halali wa ardhi bilakuharibu uhusiano.Umuhimu wa sura hiiHata tujaribu vipi, hakuna hata mmoja wetu ambayeanaweza kuepuka mgogoro. Iwe mgogoro juu yamipaka, au baina ya watu na wanyamapori; ndani aubaina ya wanafamilia; miongoni mwa vijiji; baina yabiashara au vitengo vya serikali - hata kwa mtu binafsi- mgogoro hauepukiki.Ingawa inaweza kuwa inaumiza, mwishoni mgogorounaweza ukasaidia. Mgogoro uliodhibitiwa vizuri kwakuhusisha kwenye utatuzi wa mgogoro pande zotezinazohusika unaweza: kusaidia watu kuelewa maslahi na mahitaji yawengine; kurekebisha au kuimarisha uhusiano kupitiakuelewana na mawasiliano bora na ya mpangilio; kusukuma watu kuwaza njia mbalimbali ambazowasingeweza kuzifikiria; na kuleta suluhisho ambapo pande zote mbilizinanufaika - inajulikana kama suluhisho la “woteni ushindi”.Migogoro mingi inayohusisha watu, mifugo nawanyamapori inatokana na uhaba wa rasilimali ambayo ni changamoto ya kweli na ngumu. Lakinimvutano mara nyingi hukua kwa sababu watu wanamwelekeo na maadili tofauti, na kushindwa kuelewamtazamo wa mwenzake. Migogoro mingi inasababishwa

5Utangulizina vyanzo vya undani sana kuliko vile vinavyoonekanadhahiri, na vinafanywa kuwa vigumu zaidi kwa sababuya hisia za kimaslahi, woga na mahitaji pamoja namaslahi na matakwa ya mtu (kisanduku namba 1).Kwa kuongezea, majungu au kukosekana kwamawasiliano kunaweza kuchochea migogoro nakuharibu hata ule uhusiano wa karibu.Sura hii inaelezea . Mbinu za kawaida za kufanyia kazi migogoro Mifumo mikuu ya kitaasisi iliyopo kusaidia jamiikutatua matatizo magumu Hatua muhimu za kufikia katika suluhisho la“wote kushinda”, ama kwa mazungumzo ya mojakwa moja au kwa kutumia mbinu nyingine. Hatuahizi zinajumuisha jinsi ya kuchanganua mgogoro,kujadiliana, kuongeza uwezekano, kutengenezamakubaliano yenye nguvu na ufuatiliaji.MBINU ZA KAWAIDA ZAKUSIMAMIA NA KUDHIBITIMIGOGOROKila mtu ana mbinu au namna yake mwenyeweanayopendelea kushughulikia migogoro. Lakini watuna jamii wanaweza kuchagua mbinu ipi watumie, nambinu nyingine zinaweza kuleta suluhisho za kudumukuliko zingine.Hapo chini kuna maelezo mafupi kuhusu mbinumuhimu tano za udhibiti wa migogoro, inayoelezewakwa mtindo wa hadithi.Mbinu kuu tanoUepukaji ni kuepuka matatizo na pengine hata kuwaepukawatu wanaohusika na mgogoro. Kwa kawaida, watuhutumia mbinu ya kuepuka pale ambapo mgogorounaleta usumbufu au unaonekana kuwa hauna maana.Hii inaweza kufanya kazi ijapokuwa kwa muda, kwenyemigogoro midogo. Lakini mbinu ya kuepuka inawezaKisanduku namba 1: Sababu za migogoro kwenye eneo la mradiKatika vijiji vya Kaskazini mwa Tanzania karibu na Hifadhiya Tarangire, ongezeko la idadi ya watu na uhamiaji wawatu kutoka wilaya nyingine imeongeza uhaba wa ardhina mabadiliko ya matumizi ya ardhi kutoka ardhi yamalisho na kuwa ardhi ya kilimo. Migogoro ya ardhi, majina rasilimali nyingine, baina ya wanyamapori, wafugajina wakulima inaibuka. Migogoro hii inachochewa nauharibifu wa mazingira na upotevu wa uwezo wa ardhi wakuzalisha, kuzuiwa kwa njia kuu wanazopita wanyamaporiwanapohama na maeneo ya malisho, na ongezeko la ukamena mafuriko kutokana na mabadiliko ya tabianchi.Sababu za migogoro1. Kupanua mashamba na makazi. Kilimo cha kujikimuna kilimo cha biashara pamoja na maeneo ya biasharayanasogea kwenye maeneo ambayo kwa kawaidayalikuwa ni maeneo ya wafugaji na wanyamapori.Mabadiliko haya yameleta: kiwango kikubwa cha ufyekaji wa msitu na vichaka,yote kwa ajili ya mashamba na mkaa; moto kichaa; uwindaji haramu, kwa ajili ya kujikumu na biashara; kupunguza na kugawa ardhi ya mifugo na makazi yawanyamapori; na upoteaji wa vyanzo vya kudumu vya maji, mmomonyokowa udongo, na uharibifu mwingine wa mazingira.2. Wanyamapori kuvamia mazao na mifugo. Asilimia 70 yawanyamapori wa Tarangire wanakwenda nje ya mipakaya hifadhi wakati wa masika. Wanyamapori walaomajani wanavamia mazao yaliyolimwa na wanyamaporiwengine wanaua ng’ombe, mbuzi na kondoo.3. Sera na Sheria za rasilimali za ardhi zinazokinzana.Kwa mfano, sera inayoruhusu Jumuiya ya Hifadhi yaWanyamapori inasema jamii ilipwe moja kwa moja nabiashara zinazotumia ardhi zao. Lakini mwaka 2007tangazo la Serikali liliagiza kwamba malipo yafanywekwa Serikali Kuu, ambayo itarudisha kiasi kwa jamii. Kwakuongeza, wakati Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamaporiinakusudia kuruhusu jamii kusimamia rasilimali zaowenyewe, mwanzoni mwa mwaka 2009, vibali vyauwindaji vilivyopitishwa na Serikali Kuu viliruhusiwakwa kiasi kikubwa kuondoa maslahi mengine ambayojamii ingekuwa nayo kama vile utalii wa kupiga picha.4. Kukosekana kwa uwazi na usawa. Kutokuwa na uwazikwenye kipato, mapato na ufanyaji maamuzi kuhusianana faida kutokana na rasilimali inaleta migogorobaina ya wawekezaji, serikali, na jamii, na baina yaviongozi katika jamii na wajumbe. Zaidi ya hayo, walewanaonufaika kutokana na wanyamapori na rasilimali. nyingine mara nyingi si kati ya hao wanaodhurika namigogoro kati ya watu na wanyamapori.Migororo katika jamii: kusuluhisha migogoro katika maeneo yenye mifugo, kilimo na wanyamaporiSura ya3

5Migororo katika jamii: kusuluhisha migogoro katika maeneo yenye mifugo, kilimo na wanyamaporiSura yaUtangulizikudhuru uhusiano pale watu wanapojitenga na wenzaona pengine kuunda makundi kuwazunguka marafiki zao.Hii inaweza kuongeza mgogoro pale ambapo sababu zamgogoro zinabaki bila kutatuliwa (Jedwali namba 1).Mfano: Tuseme mtu ananunua ng’ombe kutokakwa jirani yake. Ndani ya wiki moja huyong’ombe anaugua. Mnunuzi ana matumaini yakwamba ng’ombe atapona. Hata hivyo, mnunuzianahisi kwamba ngo’mbe alikuwa mgonjwa tangualiponunuliwa. Hajadiliani kuhusu hili suala namuuzaji, na anakaa mbali na maeneo ambayowanaweza kukutana.Kuchukuliana ambako kunaweza kuwa hali ya“kukubali kushindwa” kwa ajili ya kuleta amani (yamuda mfupi). Hii pia inajulikana kama shindwa/shinda(“mimi ninashindwa, wewe unashinda”). Kutoa mhangamaslahi yetu kwa ajili ya maslahi ya wengine maranyingi inasifiwa. Lakini, kwa mtazamo wa muda mrefu,kama suala hilo ni muhimu, kutoridhika kunawezakujengeka, na kuathiri uhusiano.Rafiki wa mnunuzi na familia walimwambiakwamba aachane na suala hilo na kwa sasaamtibu ng’ombe tu, kwa kuwa muuzaji anawezakukasirishwa na shutuma yoyote inayohusumauzo ya mifugo isiyo na afya. Halafu ng’ombeanakufa.Ushindani au ushambulizi unatokea watu wanapojiwekawenyewe mbele na wanalenga matokeo ya “waokushinda/na wengine kushindwa”. Mbinu ya ushindaniinaweza kugeuka kuwa kushindania mamlaka, ambayohuenda mbali zaidi ya mgogoro asilia. Watu waliokwenye mgogoro wanaweza kuamua kuanza vitishoau uhasama ili kulazimisha matakwa yao. Mbinu hii yaushindani haileti uhusiano mzuri.Kwa hasira ya kupoteza ng’ombe na kuhisikudhalilika kwa kutofanya kitu chochote,mnunuzi aliiba ndama kutoka kwa muuzajiwakati wa usiku.Muuzaji naye akatishia kuchoma moto nyumba yamnunuzi. Walipokutana sokoni, walishutumianakwa kuwa na mifugo isiyo na afya, na kupigizanakelele kuhusu ugomvi uliotokea hapo zamani.Wakaanza kupigana lakini wakatenganishwa namarafiki ili wasiendelee kupigana.4Kuafikiana, pale ambapo mtu “anashinda kidogo,anashindwa kidogo” mara nyingi inaonekana kamandiyo njia nzuri ya kusuluhisha mgogoro. Kila mmojaanapata anachotaka, lakini pia kila mmoja anakosakidogo. Maafikiano mara nyingi yanaweza kuletasuluhisho la haraka na la muda mfupi. Lakini kwasuluhisho la muda mrefu, watu wanaweza kutofurahiamatokeo kwa vile wanafikiria walichokikosa.Kwa kushinikizwa na marafiki na familia, haowawili walikaa chini na kuzungumzia tatizo lao.Mwanzoni kila mmoja alisisitiza kuwe na suluhishola mmoja ‘kushinda/na mwingine kushindwa.’Mnunuzi: “Nitakurudishia ndama wakoutakaponilipa kiasi nilicholipia ng’ombealiyekufa.”Muuzaji: “Nipe ndama wangu sasa hivi, na unipemagunia mawili ya mahindi kwa usumbufuulionisababishia.”Baada ya saa kadhaa, marafiki waliwasihi nahatimaye walifikiria kuafikiana: mnunuziatamrudisha ndama. Muuzaji atamuuzia ng’ombe,ambaye atakaguliwa na daktari wa mifugo, kwabei ya chini ya bei ya soko.Sio wote waliofurahia kabisa lakini kila mmojaanadhani “ameshinda” kitu.Ushirikiano, au utatuzi wa tatizo, unahusisha: kuchunguza sababu za ndani za mgogoro - ambazomara nyingi zinaweza kwenda nje ya wahusikakatika mgogoro; kuongeza njia zinazoweza kuleta suluhisho kwakuwa taarifa zaidi zinajulikana; na kushirikiana na kila mtu anayehusika kuletasuluhisho la muda mrefu la “wote kushinda”ambalo litaongeza uhusiano wa kikazi.Ushirikiano, au utatuzi wa mgogoro wa pamoja, maranyingi ndiyo njia bora ya kutatua mgogoro pamoja nakuendeleza uhusiano katika jamii.Ushirikiano huchukua muda, na unahitaji watu wotewajitolee katika huu mchakato. Mchakato huu maranyingi unawezeshwa na mtu kutoka nje au msuluhishi,iwe kutoka serikalini, asasi isiyo ya kiserikali au kutokakatika jamii nyingine.Kabla ya kukubaliana na mkataba, mnunuzina muuzaji walikutana na msuluhishi kutokaasasi isiyo ya kiserikali kutoka ngazi ya chini.Waliamua kupata taarifa nyingine na walianzakwa kushauriana na daktari wa mifugo kama

5Sura uangalia mgogoro kama ni tatizo linalohitajikutatuliwa kwa pamoja kunaleta suluhisho lenyekunufaisha watu woteKuafikianaKushinda kitu na kupoteza kidogo ndio mkakatiwa kawaida. Kwa kuafikiana, kila mtu anawezakuridhisha maslahi yake japo kidogoUshindaniMtu mmoja ataweza ijapokuwa kwa muda kufikiamahitaji yake na kuhisi kama “mshindi” kwakutumia mamlaka au nguvu. Hii inaleta suluhishola “mmoja kushinda/na mwingine kushindwa”Kuridhisha wengine kwa kupuuza mgogoro, kwakujaribu kulinda uhusiano. Kwa kawaida inakuwa“mmoja kushindwa/na mwingine kushinda” Inachukua muda mrefu na nguvu nyingi Inahitaji uaminifu wa pande zote mbili Washirika wengine wanaweza kuchukuafursa ya uaminifu na uwazi wa mwinginekutoa maamuzi yasiyokuwa sahihi Washirika wanaweza kukosa kuona maadilimuhimu na malengo ya muda mrefu Inaweza kufanya kazi vizuri zaidi kwamuda mfupi lakini kwa muda mrefu chukiinaweza kujengeka Inaweza isifanikiwe iwapo mahitaji yamwanzo ni makuwa sana Mgogoro unaweza kukua na yeyoteatakayeshindwa atajaribu kulipa kisasi Haki inaweza kuathiriwaKuchukulianaKuepukaWatu wanaepuka migogoro kwa kujitoa, kukwepaau kuahirisha matokeo - yaani “shindwa/shindwa”au “hakuna mshindi/hakuna aliyeshindwa”yule ng’ombe alikuwa mgonjwa wakati akiuzwa.Inaoekana kwamba inawezekana kuwa ng’ombehakuwa mgonjwa wakati wa mauzo. Hatimayemuuzaji alikubali kwamba huyu ng’ombe mdogo,kama wengine hivi karibuni, hawakunyonyamaziwa ya mama zao vizuri na walikuwa wanauzito mdogo; daktari wa mifugo anakamilishakwa kusema kwamba hii inaweza kuwa sababu yakushambuliwa na maradhi kwa urahisi.Wengine katika jamii walisema kwamba ng’ombewengi wamekuwa wakiugua maradhi mbalimbali.Kwa maneno mengine, hii inaweza kuwa tatizo lajamii nzima.Wasuluhishi walimshauri daktari wa mifugo wawilaya kuhusu kinga kwa ajili ya ng’ombe wotewaliopo kijijini. Wilaya imekubali kutoa dawa yakuoshea na huduma ya chanjo kwa muda muafaka,pamoja na kutoa taarifa ya jinsi jamii inavyowezakuboresha eneo la malisho lililoharibika.Katika mchakato wa kutafuta taarifa, ugunduzi wasababu za ndani za migogoro, na kuja na suluhishombadala ambalo litaisaidia jamii nzima, mnunuzi namuuzaji wameweza kurudisha uhusiano wao. Mawazo na wasiwasi wa mmoja waohayataweza kutiliwa maanani Mtu mmoja anaweza kupoteza imani naushawishi kwa siku zijazo Maamuzi muhimu yanawezakushindikana Kuahirisha mgogoro kunawezakusababisha madhara zaidiSasa wamekubaliana kwamba wote watafaidika na fursa ya huduma bora yamatibabu ya mifugo mnunuzi atarudisha ndama muuzaji atampa mnunuzi ndama aliye na afyaatakayezaliwa karibuni, kwa kubadilisha na guniala mahindi.Wote wakasema kwamba makubaliano hayo ni yahaki na inaonekana wameridhika. Wamealika marafikiwengine na majirani ili kusherekea.Makubaliano yanaandikwa na kushuhudiwa nawasuluhishi, Ofisi ya Wilaya, na jamii.Migororo katika jamii: kusuluhisha migogoro katika maeneo yenye mifugo, kilimo na wanyamaporiJedwali NAMBA1: FAIDA NA HASARA ZA MBINU ZA KUTATUA MIGOGOROMSAADA UNAPATIKANA: MIFUMOYA KIMILA, KITAIFA NA YAKUSHIRIKIANA YA UDHIBITI WAMIGOGOROKuna mifumo mitatu mikuu ya kusaidia mtu mmojammoja na jamii kudhibiti migogoro. Kila mfumo unanguvu zake na mapungufu yake (Jedwali namba 2).Mifumo ya kimila ya kudhibiti migogoroVijiji vya Tanzania vimeendeleza mfumo wa kisheriawa kimila ambapo viongozi wa vijiji na wazee5

5Sura yaUtanguliziMigororo katika jamii: kusuluhisha migogoro katika maeneo yenye mifugo, kilimo na wanyamaporiJedwali namba 2: Faida na hasara za mfumo wa kusuluhisha mgogoro6MfumoFaidaHasaraMifumo ya kimila Inahimiza ushiriki wa jamii na kuheshimumaadili na tamaduni katika jamii. Ufanyaji maamuzi ni kwa ushirikiano naunaendeleza mapatano. Inasaidia jamii kujengewa uwezo. Inahusisha viongozi wa kijiji kamawasuluhishi au wazungumzaji. Inaleta hali ya umiliki wa mchakato namatokeo yake.Mfumo wa kisheria wakitaifa Inajenga utawala wa sheria, inawezeshaasasi za kiraia na kuendeleza uwajibikaji. Inahusisha wataalamu wa sheria na kiufundikatika kufanya maamuzi. Ina uwezo wa kufanya maamuzi kulinganana sifa ya kesi yenyewe, na pande zote mbilizinabaki sawa mbele ya sheria.Njia mbadala zaudhibiti wa migogoro Hazina vipingamizi katika udhibiti shirikishiwa mgogoro kama ilivyo katika njia nyingineza kibunge, kiutawala, kimahakama nakimila. Inaendeleza maslahi ya pamoja. Inajenga makubaliano na umiliki wamchakato wa suluhisho. Inasisitiza jamii kujengewa uwezo ambaoutawatayarisha watu kuwa wawezeshajiwazuri, watoa taarifa, wataalamu wamipango na wasuluhishi wa migogoro. Nafasi ya mfumo huu imechukuliwana mfumo wa mahakama na sheria zakiutawala. Inaweza isihusishe watu kwa misingi yajinsia, kundi, kabila na sababu zingine. Inaweza kuruhusu viongozi wa kijijikutumia mamlaka yao kwa manufaayao wenyewe au kwa manufaa ya kundilao la kijamii au mteja wao. Inaweza isiandike maamuzi namchakato yaliyofanywa kwa njiaya mdomo kwa ajili ya matumizi yabaadaye. Mara nyingi haiwahusishi watumaskini, wanawake, makundiyaliyotengwa na wanajamii wanaoishimbali sana kwa sababu ya gharama,umbali, matatizo ya lugha, vikwazo vyakisiasa, kutokuwa na elimu na ubaguzi. Unaruhusu ushiriki mdogo wawalalamikaji katika kufanya maamuzi. Unashindwa kufanyia kazi miundoisiyo sawa, na inaweza kuchochea aukuzidisha tofauti za kimadaraka zilizopo. Ina ugumu wa kutoweza kuwakalishawadau wote kwenye meza yamajadiliano. Unatoa maamuzi ambayo yanawezayasiwe na nguvu kisheria. Unaweza kutumia mbinu ambazozilianzishwa katika mazingira natamaduni nyingine bila ya kuzihusishana mazingira ya kwao wenyewe.wanaoheshimika wanasimamia sheria za kimila. Kwamfano, Kamati za Ardhi za Kijiji za Usuluhishi zinatumiasheria ya kimila ili kufafanua haki za ardhi. Mafanikio yamfumo huu wa sheria katika kudhibiti migogoro juu yarasilimali unategemea uhiari wa walalamikaji pamojana uwezo wa utekelezaji wa mamlaka za kimila.Mifumo mingine ya kimila hutumia usuluhishi - paleambapo taasisi au watu walio nje ya mgogoro kama vilekamati ya wazee wanawezesha majadiliano na kufanyamaamuzi kati ya walalamikaji (kisanduku namba 2). Auwanaweza kutumia njia ya usuluhishi ambapo taasisiau watu walio nje ya mgogoro, waliokubaliwa na pandezote mbili. Msuluhishi anasikiliza kila wazo na anatoamaamuzi ambayo yataleta usuluhishi.Mifumo ya kisheria ya kitaifaMfumo wa kisheria wa kitaifa unatatua migogorokupitia kesi katika mahakama za sheria: walalamikajiwanaelezea kesi yao mbele ya jaji au maofisa wengine.Walalamikaji mara nyingi wanawatumia wanasheria.Mahakama inasikiliza malalamiko na kupitia ushahidikabla ya kuamua nani mshindi - ambapo watasemakwa uhakika nani mshindi na nani ameshindwa.Mfumo wa kisheria wa kitaifa unaanzia katika kamatiza vijiji mpaka katika mahakama za kata na mahakamaza wilayani, kimkoa na katika ngazi ya kitaifa. (URT,1997). Mifumo mingine ya kitaifa pia inahusisha sheriaza kimila au maadili ya jamii (FAO, 2005).Mifumo ya kisheria pia mara nyingine inatambuausuluhishi unaotoa maamuzi ambayo ni ya lazima, paleambapo taasisi au watu walio nje ya mgogoro wanatoamamuzi ya mwisho.

5UtanguliziKisanduku namba 2: Mgogoro kati yamkulima na mfugaji wa Afrika MagharibiMgogoro juu ya matumizi ya ardhi ni kitu cha kawaidahuko Sahel pamoja na Afrika Mas

Migororo katika jamii: kusuluhisha migogoro katika maeneo yenye mifugo, kilimo na wanyamapori 5 Sura ya Utangulizi 1 HADI

Related Documents:

inayojadiliwa hapa ni: Fasihi ni Hisi, Fasihi ni Kioo cha Jamii, Fasihi ni Mwavuli wa Jamii, na Fasihi ni Zao la Jamii husika na Mielekeo yake ya maisha. 3. Mitazamo inayofafanua Uhusiano wa Fasihi na Jamii Kama lilivyo lengo la makala haya kwamba mchango wake ni kuongeza mchango katika kufafanua uhusiano uliopo baina ya fasihi na jamii.

kuchambua maudhui yanayopatikana katika hadithi za watoto katika jamii ya wapemba mwanaika madi mzee tasnifu iliyowasilishwa kwa ajili ya kutimiza sehemu ya la pekee la kutunukiwa digrii ya uzamili (m.a. kiswahili) ya chuo kikuu huria cha tanzania 2015

"Kutathimini Mbinu za Ufutuhi Katika Kuelimisha Jamii Kuhusu Janga la Ukimwi, katika tamthiliya ya Embe Dodo ushuhuda wa mifupa nimeridhika kwamba imefikia kiwango kinachotakiwa na inafaa kuwasilishwa kwa ajili ya Utahini wa Shahada ya Uzamili ya Fasihi kwa Kiswahili ya Chuo Kikuu Huria cha . 4.2.2 Mbinu za Ufutuhi katika Ushuda wa Mifupa .

kundi ,fanya jukumu la maana katika masomo yote.Umahiri wa maelezo maalum na wa baina ya mitaala yameshikanishwa pamoja katika muktadha wa maelezo. . baina ya mitaala katika muda wa mwaka wa shule. Kwa kufanya hivo wanaangazia kusoma kwao . na wanachukua jukumu la mchakato wao wa kimasomo. Tathmini ya kibinafsi hufanywa katika

wahusika wakuu wa kazi ya fasihi na wahusika wadogo. Wahusika hao ndio wanaoipamba kazi fasihi na kuifanya iweze kuakisi mambo ya yaliyomo katika jamii (Msokile, 1992). Kwa muktadha huo tabia za wahusika wa kazi ya fasihi ndio ambao husawiri matukio na mambo mbalimbali yanayofanywa katika jamii inayohusika.

2.0 Dhuluma dhidi ya Wanawake katika Fasihi Kama inavyodhihirika katika kazi za fasihi, wanawake wanapitia aina tofauti za dhuluma katika jamii wanamoishi. Wasomi na wahakiki wa kazi za fasihi wameshughulikia suala la dhuluma kwa wanawake na athari zake kwa muda mrefu bila kutoa suluhu.

katika tamthiliya za Kinjeketile na Nyerere na Safari ya Kanaani: Utafiti linganishi. Ili kufanikisha utafiti huu, mtafiti ametumia mbinu za maktabani katika kukusanya na kuwasiilisha data kimaelezo. Pia marejeleo mbalimbali kutoka tamthiliya za Kiswahili yalipitiwa. Nadharia ya fasihi ya jamii ndiyo iliyotumika katika

273 pages Literary Criticism: An Introduction to Theory and Practice 0138974225, 9780138974220 F and S Index International 2005 Subscription , Gale Group, 2005, Business & Economics, . F& S Indexes offer you a handy compilation of company, product and industry information from financial publications, business-oriented newspapers, trade magazines and special The analysis of time series data has .