Uboreshaji Huduma Za Lishe Katika Kuimarisha Afya Ya Uzazi .

2y ago
190 Views
4 Downloads
1.24 MB
7 Pages
Last View : 15d ago
Last Download : 3m ago
Upload by : Dani Mulvey
Transcription

Jenga familiainayozingatia lishe na afya bora!UboreshajiHuduma za Lishekatika KuimarishaAfya yaUzazi kwaMama naMtoto Singidana Shinyanga( ENRICH)

Kutoka kwa Mkurugenzi wa MiradiHuu ni mwendelezo wa nia yetu ya dhati katika kuboreshaafya na lishe ya mama na mtoto ili kupunguza vifo vyawatoto chini ya miaka mitano na vifo vya uzazi nchiniTanzania.Kutoka kwa Mkurugenzi wa Miradi. 1Kuhusu Mradi na Mafanikio. 2World Vision Tanzania tunaamini kuwa afya njema ni msingiwa maisha ya mtoto. Hivyo ni azma yetu kuhakikishamama na mtoto wanapata lishe bora, wanalindwa dhidi yamagonjwa na wanapata huduma za afya za msingi. KupitiaMradi wa ENRICH tunakabiliana na utapiamlo ndani ya siku1000 za mtoto. Huu ni muda muhimu kwa mtoto kupatalishe bora.Vikundi Lishe: Kuhamasisha Matumizi ya Chakula Bora kwaAfya ya Mama na Mtoto. 3Wahudumu wa Afya ya Jamii: Washauri Muhimu wa Kaya Juu yaAfya na Lishe ya Mama na Mtoto. 4Matumizi ya mazao yaliorutubishwa kibaiolojia katika kukabilianana upungufu wa virutubishi. 6Ndugu Msomaji,Uelewa wa Sera: Kichocheo cha Huduma Bora za Afya na Lishe. 7Kuna wakati unatembelea jamiii ambayo ina wingi wachakula lakini unajiuliza kwanini kuna watoto wenyeutapiamlo. Kadhalika unajiuliza kwanini kuna vifo vya uzazi.Hakika kuna sababu nyingi zinazosababisha dhahama hiyolakini ukweli ni kuwa vifo hivyo vinaweza uzuilika.Ushindi dhidi ya vikwazo vya kitamaduni kwa kuhusishawanaume katika masuala ya lishe na afya ya mama na mtoto.Timu ya Uhariri:Melkizedeck Karol - Meneja Mawasiliano, World Vision TanzaniaAgness John - Afisa Mawasiliano, Mradi wa ENRICHTimu ya WataalamuMwivano Malimbwi - Meneja Mradi - ENRICHRester Boniface - Mratibu Mradi Mkoa - ENRICHWorld Vision Tanzania March 2018World Vision TanzaniaMradi wa ENRICHOfisi ya Mkuu wa Mkoa SingidaS.L.P 1573SingidaMakao MakuuBarabara ya Radio TanzaniaKutokea barabara ya NjiroNyumba Na. C, kitalu. 181 NjiroS.L.P 6070Arusha TanzaniaSimu: 255 27 254 9252 / 253/2549Ingawaje ni mwaka mmoja sasa tangu kuanza kwa mradi,tumeshuhudia mabadiliko na maendeleo makubwa kuelekeamatarajio yetu juu ya wanawake na watoto. Kupitia kufanyakazi na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee naWatoto, jamii, serikali za mitaa, timu za usimamizi wa afyangazi za mkoa na wilaya pamoja na watoa huduma za afya,Mradi wa ENRICH umenufaisha vijiji 50 na vituo vya afya 58.Hili nina mchango madhubuti katika ubora wa upatikanajiwa huduma za lishe kwa watoto, wanawake wajawazito,wanawake wanaonyonyesha na jamii kwa ujumla.Kwa miaka kadhaa ya hivi karibuni, Tanzania imekuwainafanya jitihada kubwa ili kuzuia vifo vyote vya uzazi, watotowachanga na watoto wadogo. Katika kuunga mkono jitihadahizo na kama ilivyoelezwa na moja ya matarajio yetu juu yaustawi wa watoto “watoto wafurahie afya njema”, WorldVision Tanzania inatekeleza mradi wa ENRICH.World Vision Tanzania tunawapongeza wanajamii, Serikaliya Kanada, World Vision Kanada, wadau wa utekelezaji wamradi, serikali za mitaa katika ngazi zote na wafanyakazi waWorld Vision Tanzania hususani wafanyakazi wa mradi waENRICH. Tunatoa wito wa kuendelea kutoa ushirikiano nakujitolea zaidi kwa kazi hii muhimu kwa watoto.Mradi wa Uboreshaji Huduma za Lishe katika KuimarishaAfya ya Uzazi kwa Mama na Mtoto (ENRICH)una lengokuu la kuchangia kupunguza maradhi na vifo vya uzazi kwamama na mtoto vinavyosababishwa na sababu za kilishekatika mikoa ya Shinyanga na Singida. Hii ni kwa njia yautekelezaji wa hatua za gharama nafuu za lishe bora ambazoni pamoja na: kuimarisha mfumo wa afya,kuendelezamazao yaliyorutubishwa kibaiolojia, kuhamasisha ushirikiwa wanaume, na kushughulikia moja kwa moja utapiamlondani ya siku 1000 za kwanza za maisha ya mtoto.Furahia usomaji wako!Devocatus Kamara1

SHINYANGAKuhusu Mradi na Mafanikio YakeNchini Tanzania, lishe duni huchangia zaidi ya theluthi mojaya vifo vyote vya watoto wa umri kati ya miezi 0 hadi miezi5.9 na utapiamlo huongeza hatari ya mtoto kufa kutokanana magonjwa mengi, mara nyingi zaidi ugonjwa wa surua,kuhara na nimonia.Mradi wa ENRICH utatumia njia mbilimahsusi;Kuimarisha mifumo ya afya: Hii ni kupitia mafunzona uwezeshaji wawatoa huduma za afya ya jamii pamojanaTimu za Usimamizi wa Afya ngazi za mkoa na wilaya(RHMT na CHMT) ili kukuza na kutoa huduma za msingiza lishe, na pia kutoa taarifa na kuongeza ushiriki wa jamiikatika mazungumzo na serikali juu ya sera za masuala yaafya na lishe ya uzazi, watoto wachanga na watoto wadogo.Hili linafikiwa kupitia sauti ya umma na uwajibikaji.Uboreshaji Huduma za Lishe katika Kuimarisha Afya yaUzazi kwa Mama na Mtoto (ENRICH) ni mradi wa miakamitano (2016-2020) unaofadhiliwa na serikali ya Kanadana kutekelezwa na shirika la World Vision Tanzania pamojana wadau wengine. Mradi huo uko sambamba na mkakatiwa kitaifa wa kuboresha afya ya uzazi, watoto wachangana watoto wadogo kwa nia yakukabiliana moja kwa mojana utapiamlo ndani ya siku 1000 za kwanza za maisha yamtoto. Lengo kuu la mradi ni kupunguza maradhi na vifo vyauzazi vya mama na mtoto vinavyosababishwa na sababu zalishe. Hii ni kwa kushughulikia maswala muhimu kwa afya yamama, watoto wachanga na watoto chini ya miaka miwili.Kuboresha huduma za lishe: Kwa kuongeza ufahamuna kukuza ujuzi juu ya lishe iliyopendekezwa kwa mama,watoto wachanga na watoto chini ya miaka miwili ikiwa nipamoja na ulaji wa virutubisho, mbinu bora za ulishaji naulaji wa vyakula vyenye wingi wa virutubisho kwa watotowachanga na watoto wadogo. Vilevile kutoa mafunzo nakuwezesha utengenezaji wa bustani za nyumbani na kukuzamazao yaliyorutubishwa kibaiolojia. Haya yote ni kupitiamafunzo yanayotolewa kwa vikundi vya lishe, vikundi vyawakulima, wahudumu wa afya ya jamii, kamati za hudumaza jamii, vongozi wa jamii, viongozi wa dini, wanaume kwawanawake.Kupitia ufadhili wa serikali ya Kanada na World VisionKanada, mradi unatekelezwa kwa ushirikiano wa serikaliya Tanzania, Nutrition International (NI), Harvest Plus(H ), Canadian Society for International Health (CSHI) naChuo Kikuu cha Toronto (UofT). Mradi huu unatekelezwakatika mikoa ya Singida (halmashauri ya wilaya ya Ikungina Manyoni) na Shinyanga (halmashauri ya mji Kahama,halmashauri ya wilaya ya Kishapu na Shinyanga) kutokaMachi 2016 mpaka Septemba 2020.Kiwango cha vifo vya uzazi ni556100000kati ya vizazi haiSINGIDA28%29%3.3%4.3%12.3%11.7%71%37%Kiwango cha udumavuKiwango cha udumavuKiwango cha uzitopungufuKiwango chaupungufu wa damuChanzo cha Takwimu: Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria Tanzania 2015-16Mafanikio ya Awali ya MradiKiwango cha vifo vyawatoto wachanga niKiwango cha vifo vyawatoto chini ya miakamitano nikati ya watoto haikati ya watoto hai4310002671000.ViashiriaTakwimu za awali (2016)Ufuatiliaji wa Matokeo ya Mwaka (2017)Upatikanaji wa huduma kwa Wajawazito45.0%48.4%Uzazi uliofanywa na mhudumu mwenye ujuzi74%85.7%Upatikanaji wa huduma baada ya mtoto kuzaliwa 54.4%72.4%Unyonyeshaji wa maziwa pekee ya mama69.3%59.0%Kiwango cha chini cha lishe kinachokubalika16.7%33.3%Ulimaji mazao yaliyorutubishwa kibaiolojia0%10.5%3

Vikundi Lishe:Kuongeza kasi ya uhamasishaji wa matumizi ya chakula bora kwa afyaya mama na mtotoWahudumu wa Afya ya Jamii:Washauri muhimu wa kaya juu ya afya na lishe ya mama na mtotoVikundi lishe vinatoa elimu na kusambaza maarifa kwajamii, lengo kuu ikiwa ni kupambana na utapiamlo katikangazi zote kutumia mkoba wa siku 1000. Mkoba wa siku1000 husaidia wanajamii kujifunza kwa urahisi juu ya afyana lishe bora kwa mama na mtoto hadi kuanzia mimbahadi mtoto anapofikisha miaka miwili.Kupitia mafunzo na vifaa walivyopatiwa,WAJA wamewezakujumuisha huduma za lishe na afya ya uzazi, watotowachanga na watoto wadogo kama sehemu ya kushauri.Kazi zao kubwa ni pamoja na kuwatambua, kuwapa rufaakwenda vituo vinavyotoa huduma ya afya na kuwasaidiawanawake wajawazito, kinamama wanaonyonyesha nawatoto wenye utapiamlo katika vijiji vyao. Pia kuhamasishajamii katika mikutano ya hadharana kuripoti shughulizilizofanywa katika mwezi husika.“Kujifunza imekuwa furaha kwa kutumia mkoba wa siku1000. Kuhamasisha na kuelimisha makundi ya wanawakekwa wanawake na wanaume kwa wanaume imekuwarahisi zaidi kwa kutumia redio na vipeperushi”. Graceanaongezea.“Baadhi ya mamboyamekuwa yakiachwa katika jamii kwakudhani kuwa sio tatizo kutokana na kuonekana kuwamadogo. Utembeleaji na ushauri katika kaya umekuwana faida nyingi maana nawapatia rufaa za kwenda vituovinavyotoa huduma za afya kwa matibabu zaidi hasawajawazito wenye dalili za hatari na watoto wenyeutapiamlo. Kizuri zaidi ni kwamba wanaendelea vizurisasa.”Boniphace Emanuel, Mhudumu wa Afya ya Jamii, kijijicha Mkwese.Mahudhurio ya wanawake na wanaume kwenye mikutanoya mkoba wa siku 1000 yamekuwa na matokeo chanya nakuna mabadiliko makubwa katika jamii kama mmoja wawanakikundianavyoeleza.“Siku hizi hata ripoti za visa vya magonjwa ya kuhara nanimoniamiongoni mwawatoto vimepungua. Pia ukosefuwa maziwa kwa wamama wanaonyonyesha umepunguakwa kiasi kikubwa”. Mama Dickson, anaeleza akitabasamu.Mtoto ambaye hapati virutubisho na chakula cha kutoshahawezi kukua vizuri, hali hii inaweza kuanzia katika tumbola mama mwenye utapiamlo. Katika kuimarisha matumiziya vyakula vyenye wingi wa virutubisho, vikundi lishevinaundwa.Wanakikundi lishe wanafundishwa kuhusumkoba wa siku 1000, masuala ya msingi ya lishe, mahitajiya lishe ya mama, wanawake wajawazito, wanawake waumri wa kuzaa watoto, watoto wachanga, na watotochini ya miaka miwili pamoja na kuandaa mlo kamili kwakutumia vyakula asilia vinavyopatikana.197918“Tumejua kuwa kuna vyakula bora vingi katika kijijichetu, jinsi ya kupanga vyakula katika sahani ili iwezekuwa na angalau makundi matatu ya vyakula na piakuhusu uzalishaji na matumizi ya vyakula vyenye wingi wavirutubisho.” Anasema, Grace Msengi, katibu wa kikundilishe kijiji cha Mkwese.483Wanaume4Wana kikundilishe wamepatiwamafunzo ya mkobawa siku 1000.435Wanawakewamepata mafunzoya lishe ya afyaya uzazi, watotowachanga nawatoto wadogo.Ukosefu wa huduma za afya pamoja na upungufu wahuduma za lishe bora kunakotokana na sababu kadhaaikiwemo ukosefu wa vituo vinavyotoa huduma za afya,umbali mrefu katika kuzifikia huduma za afya pamoja nauhaba wa wataalamu wa afya. Haya yanaathiri afya na lisheya mama na watoto. Katika kukabiliana na suala hili katikajamii zilizo katika eneo la mradi wa ENRICH, Wahudumuwa Afya ya Jamii (WAJA) wanahusishwa katika kuwezeshaupatikanaji wa huduma za afya za msingi na ushauri sahihiwa lishe katika kaya.101Wanaume596Wanawake

Matumizi ya mazao yaliorutubishwa kibaiolojiakatika kukabiliana na upungufu wa virutubishi mwiliniUelewa wa Sera: Kichocheo cha huduma bora zaafya na lisheinafurahia matembele kipindicha ulimaji na pia viazi lishekipindi cha uvunaji. Afya ya familia yangu imeimarika kamailivyokuwa kwa jamii yangu pia.”Mohamed Igae, Mkulimawa viazi lishe, Kijiji cha Ihanja.Pamoja na wingi wa virutubisho katika viazi lishe, WorldVision Tanzania imeona umuhimu wa kuhimiza jamii nakuiwezesha juu ya vyakula vingine vyenye virutubishokama vile mbogamboga, matunda na vyakula vyenyewingi wa protini. Kupitia Maafisa Ugani na Maafisa Mifugowa Kata, Mradi wa ENRICH umetoa elimu katika ngaziya kaya juu ya ufugaji wa kuku na ulimaji wa mboga namatunda ulioboreshwa, ili kuongeza upatikanaji na ulajiwa vyakula bora kwa wanawake wenye umri wa kuzaa,wajawazito, kinamama na watoto chini ya miaka miwili.“Mbegu za mboga na matunda nilizopata kutoka WorldVision zimeniwezesha kuanzisha bustani ya jikoni ambayonimepanda spinachi, mchicha na mapapai. Sina wasiwasitena na ulaji wa chakula kisichokuwa na virutubishi vyakutosha, ukosefu wa virutubishi katika mlo lakinipianaepuka kutumia pesa nyingi kununua mboga kwanikwa sasa vyote viko karibu na jiko langu.” Mary Jimwaga,Mnufaika, Wilaya ya Kishapu.Kwa kuelewa kuwa wanawake wengi walio wajawazitoau wanaonyonyesha pamoja na watoto wana uhitajimkubwa wa lishe bora mwilini ikilinganishwa na makundimengine, Mradi uliielimisha jamii juu ya ulimaji wa viazilishe kutokana kuwa na wingi wa virutubisho katika zaohilo. Hii ni aina ya viazi vyenye wingi wa vitamini ambayoni muhimu kwatika ukuaji pamoja na kupambana naupunguvu wa viini lishe mwilini. Wakulima walishirikimafunzo juu ya uzalishaji, ulaji na matumizi ya viazi lisheikiwa ni pamoja na kuwapa mbegu.234“Nimejifunza juu ya uzalishaji wa viazi lishe, faida zakekatika lishe na kunipatia vipando vyake. Katika kuhakikishawanakijiji wenzangu wananufaika, niligawa vipando kwakikundi lishe na timu ya Sauti ya Umma na Uwajibikaji ilikufungua bustani za mfano. Pia tuligawa kwa familia zenyewamama na wanawake wajawazito, wanawake wa umriwa kuzaa na watoto chini ya miaka miwili. Familia yangu446wamepatamafunzokuhusu njiabora zauzalishaji wamboga mbogana matundawamepatamafunzo yauzalishaji wa mazaoyaliyorutubishwakibaiolojia98Maafisa ugani namaafisa mifugowa kata 98wamefundishwakuhusu mazaoyaliyorutubishwakibaiolojia naufugaji wa kukuSauti ya umma na uwajibikaji (CVA) ni mbinu yauchechemuaji katika ngazi ya jamii inayochocheauwajibikaji kwa kuwezesha mazungumzo baina ya jamiina serikali ili kuboresha huduma za kijamii ambazozikikosekana huathiri maisha ya kila siku ya watoto nafamilia zao. Kupitia mbinu ya sauti ya umma na uwajibikaji,mradi wa ENRICH unafanya mafunzo ili kuongezauwezo wa jamii kuhusika katika usimamizi wa sera nauendeshajiwa masuala ya afya na lishe lengo likiwa nikuongeza uwajibikaji wa watoa huduma na viongozi,pamoja na uwajibikaji wa wananchi katika upatikanaji nautoaji wa huduma za msingi.“Sauti ya Umma na Uwajibikaji imetufundisha kuwachangamoto katika jamii zinaweza kutatuliwa kwamichango yetu na tutakapoanza serikali nayo itahamasikakuendeleza juhudi zetu. Kati ya suala lililoibuliwakatika jamii yetu ni uhitaji wa zahanati. Kama jamiituliafikiana kila familia kuchangia kiasi cha pesa kwa ajiliya ujenzi wa zahanati hiyo, jengo linakaribia kukamilikana tunategemea serikali kutuwezesha zana na vifaavitakavyohitajika.”Anaeleza Simon Labia, Mtendaji waKijiji cha Ulyampiti.Matokeo ya Sauti ya Umma na Uwajibikaji yanayoonekanana yanashuhudiwa katika kijiji cha Solwa, Wilaya yaShinyanga Vijijini na Kijiji cha Ulyampiti, wilayani Ikungi.Matokeo hayo chanya yanaharakisha juhudi za jamiina ushiriki wao katika shughuli za maendeleo kupitiamijadala na serikali na watoa huduma, kwa kuangaliahuduma zinazotolewa kwa kuhusianisha na viwangovinavyoelezwa katika sera ya afya. Katika kata ya Solwa,jamii iliamua kukusanya rasilimali zake kujenga wodi zakulaza wagonjwa ili kuwezesha upanuzi na uboreshajikuiwezesha zahanati hiyo kupandishwa hadhi hadi kuwakituo cha afya.223viongozi wa serikali nasiasa waliofundishwakuhusu uchechemuajiwa jamii ili kuboreshahuduma za lishe jumuishikupitia Sauti ya Umma naUwajibikaji155Wanaume768Wanawake

Ushindi dhidi ya vikwazo vya kitamaduni kwa kuhusishawanaume katika masuala ya lishe na afya ya mama na mtoto.ushiriki mdogo wa wanaume katika masuala ya lishe naafya ya uzazi na watoto.Mradi wa ENRICH unahamasisha ushirikiano wa kijinsiakatika utoaji wa huduma za afya na lishe pamoja na elimukwa umma kuhusu usawa wa kijinsia. Kama ilivyo katikamaeneo mengine nchini,wanaume hufanya maamuzi ndaniya familia juu ya matumizi ya rasilimali za familia kamavile vyakula vya lishe pamoja na uzazi salama, uhudhuriajihuduma za ujauzito,mahali pa kujifungulia na huduma zaafya za watoto. Hii ni kutokana na desturi na mila ambazozinaendeleza ukosefu wa usawa wa kijinsia na kuzidisha8Athumani, ambaye ni baba wa mtoto aliyepona utapiamloameweza kufanya tofauti na mfano wa kuigwakatika jamiiyake kwenye suala la ushiriki wa wanaume katika hudumaza lishe na afya ya uzazi, watoto wachanga na watotowadogo. Hii ni baada ya kupokea elimu juu ya lishe yamtoto na umuhimu wa ushiriki wa wanaume katika sualahilo.9

“Baada ya mwanangu kugundulika kuwa na utapiamloilibidi nijihusishe katika kumtunza ili kuhakikisha anapona.Mwanzoni jamii ilikuwa inanishanga nilipokuwa namlisha,nampeleka hospitali pamoja na kumuandalia chakula.kupitia elimu ya mara kwa mara na uhamasishaji sasawameanza kubadilika na kwa furaha wanaume wanaanzakujihusisha katika masuala ya afya ya mama na mtoto.”Anaeleza Athumani.wao kuhakikisha afya ya wake na watoto wao.Mradi waENRICH hutumia elimu kwa umma inayolenga kubadilitabia zisizofaa.“Siku hizi wanaume wanahitajika kuleta wake zaoila huwa furaha zaidi tunapoona wanaleta wake auwatoto wao hata wasipohitajika kwa lazima. Athumaniamekuwa mfano wa kuigwa na tunafurahi kumuhudumiamtoto wake hadi sasa ambapo uzito wa mtoto wakeumeongezeka na hivyo amehitimu kutoka lishe ya watotowenye utapiamlo.”Alisema Irene Tarimo (57), MuuguziAfya ya Umma - Hospitali ya Mkoa wa Singida.Mpango wa afya unaowahitaji wanawake wajawazitokuhudhuria kliniki kwa mara ya kwanza na wenzi waounazaa matunda zaidi kwani wanaume huona ni wajibu10

1000.kati ya watoto hai Viashiria Takwimu za awali (2016) Ufuatiliaji wa Matokeo ya Mwaka (2017) Upatikanaji wa huduma kwa Wajawazito 45.0% 48.4% Uzazi uliofanywa na mhudumu mwenye ujuzi 74% 85.7% Upatikanaji wa huduma baada ya mtoto kuzaliwa 54.4% 72.4% Unyonyes

Related Documents:

kundi ,fanya jukumu la maana katika masomo yote.Umahiri wa maelezo maalum na wa baina ya mitaala yameshikanishwa pamoja katika muktadha wa maelezo. . baina ya mitaala katika muda wa mwaka wa shule. Kwa kufanya hivo wanaangazia kusoma kwao . na wanachukua jukumu la mchakato wao wa kimasomo. Tathmini ya kibinafsi hufanywa katika

Data zilirekodiwa katika kinasa sauti na kunukuliwa kwa maandishi. . Tofauti za Matumizi ya Lugha katika Miktadha Mbalimbali ya Mazungumzo 13 sehemu ya pili inahusu tofauti ya matumizi ya lugha katika miktadha mbalimbali. Sehemu ya tatu inafafanua mkabala wa kinadharia uliotumika katika uch

Nyenzo za kufundisha huwa viungo muhimu wakati wa utoaji wa mafunzo. Utafiti ulichunguza matumizi ya nyenzo katika ufundishaji wa Kiswahili katika shule za msingi za umma katika Jimbo la Nyandarua, Kenya. Madhumuni ya utafiti yalikuwa: Kuainisha nyenzo zinazotumika kufundisha Kiswahili, Kutathimini kiwango cha matumizi ya

maswali yeye aliuliza ilikuwa, 'Biblia ina hadithi kuhusu mtu ambaye alimezwa na samaki mkubwa. Alikuwa nani? Asilimia themanini ya watu katika kundi hilo, kwa ushujaa wakasema, 'Pinocchio!' Marla aliniambia tukiwa bado katika ibaada kwamba swali hilo bado liliulizwa katika kanisa ambako alihundumu katika Kusini mwa California na

linashughulikia Misheni ya Kanisa, umoja, na asili yake ya kuwa katika maisha ya Utatu wa Mungu. Baadaye kitabu hiki kinajadili juu ya kukua kwetu katika ushirika—katika imani ya kimitume, maisha ya ekaristi takatifu, na huduma—kama ilivyo kwamba makanisa yameitwa kuishi ndani ya na kwa ajili ya dunia.

Zoezi la utambuzi wa Watoto Wanaoishi Katika Mazingira Hatarishi (WWKMH) limefanyika kwa kushirikia na Shirika la BAKAIDS. Jumla ya watoto 16010(ME 7720,KE 7,577)wametambuliwa katika mitaa 68 ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji. Watoto 253 wameunganishwa na huduma katika vituo 2 vya Compassion International vya Bangwe na .

2.0 Dhuluma dhidi ya Wanawake katika Fasihi Kama inavyodhihirika katika kazi za fasihi, wanawake wanapitia aina tofauti za dhuluma katika jamii wanamoishi. Wasomi na wahakiki wa kazi za fasihi wameshughulikia suala la dhuluma kwa wanawake na athari zake kwa muda mrefu bila kutoa suluhu.

ASP.NET MVC 4.0 IIS and ASP.NET Enabled on your machine (see top part here) Creating your first COM component for ASP.NET The first step is to create a COM object in Visual FoxPro and expose it as an MTDLL (multi-threaded STA) component. Although not really multi-threaded, STA allows COM to operate