ATHARI ZA KIISIMU ZA LAHAJA YA KITUMBATU KATIKA

2y ago
305 Views
2 Downloads
877.27 KB
106 Pages
Last View : 14d ago
Last Download : 3m ago
Upload by : Jayda Dunning
Transcription

ATHARI ZA KIISIMU ZA LAHAJA YA KITUMBATU KATIKAKISWAHILI SANIFU KINACHOTUMIKA KATIKA SHULE ZA TUMBATUZANZIBARPANDU MACHANO AMETASNIFU ILIYOWASILISHWA IKIWA NI SEHEMU YA MASHARTI YAKUPATIWA SHAHADA YA UZAMILI (M.A. KISWAHILI - ISIMU) YACHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA2017

iiUTHIBITISHOAliyetia saini hapo chini anathibitisha kuwa amesoma na anapendekeza tasnifu hiiinayohusu athari za kiisimu za lahaja ya Kitumbatu katika Kiswahili Sanifukinachotumika katika shule za Tumbatu Zanzibar, ipokelewe na ikubaliwe na ChuoKikuu Huria cha Tanzania kwa ajili ya kukamilisha matakwa ya kuhitimu shahada yauzamili wa Kiswahili ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. . Dkt. Anna Kishe( Msimamizi) .Tarehe

iiiHAKIMILIKIHairuhusiwi kuiga au kunakili kwa namna yoyote, sehemu yoyote ya tasnifu hii kwanjia yoyote kama vile kielektroniki, kurudufu nakala, kurekodi au njia yoyotenyingine bila ya ruhusa ya mwandishi au Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kwa niaba.

ivTAMKOMimi,Pandu Machano Ame,natamka kuwa kazi hii yenye jina “Athari za kiisimu zalahaja ya Kitumbatu katika Kiswahili Sanifu kinachotumika katika shule za TumbatuZanzibar”ni yangu mwenyewe, haijawahi kuwasilishwa popote kwa lengo la kufaulushahada kama hii. .Sahihi .Tarehe

vTABARUKUTasnifu hii ninaitabaruku kwa wazazi wangu wapendwa, marehemu Machano AmeJuma na Fatuma Moh‟d Yussufu kwa kunilea katika malezi bora na katika misingibora ya kitaaluma ya kidini na kidunia. Pia ninaitabaruku kwaMke wangu MariamuHabibu Bakari kwa kunipa ushirikiano mzuri katika maisha yanguna katika kipindicha masomo.

viSHUKURANIWatu waliotoa michango yao hadi kumalizika kwa kazi hii ni wengi sana na nivigumu kuwataja wote, ila ninawaomba waamini kuwa michango yao imepokelewakwa moyo mkunjufu na imesaidia kufanikisha kazi hii. Ninawaomba radhi sana kwakutowataja ila Mungu awajaze imani na Baraka katika misha yao. Hata hivyoninapenda kuwataja wachache kwa niaba yao.Kwanza kabisa ninatoa shukrani za dhati kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu aliyenipauhai, nguvu, fikra na uwezo wa kuandika na kukamilisha kazi hii.Pili, ninatoa shukrani za pekee kwa msimamizi wangu wa utafiti huu Dkt, AnnaKishe kwa kukubali kubeba jukumu la kusimamia kazi hii, ninamshukuru kwaujasiri, upendo na uvumilivu wake mkubwa tokea hatua ya kuandika pendekezo lautafiti hadi kumalizika kwa kazi hii. Ni imani yangu kwamba amevumilia sanakutokana na udhaifu wangu wa kibinaadamu na uanafunzi. Mafanikio ya tasnifu najuhudi yake kubwa ya kusoma, kukosoa, kurekebisha, kuelekeza na kushauri yaleyote yanayofaa kuzingatiwa katika utafiti huu. Pamoja na majukumu mengialiyonayo, hakusita hata mara moja kusoma kazi yangu kwa umakini mkubwa. Kwakweli sina kitu cha kumlipa ila ninamuombea dua kwa Mwenyezi Mungu amzidishieupendo, ampe afya njema, ampe maisha marefu yenye kheri ili aweze kutoamchango kwa wanataaluma na taifa kwa ujumla.Tatu, ninapenda kuushukuru uongozi wa chuo Kikuu Huria cha Tanzania pamoja naidara ya isimu na taaluma za fasihi kwa kuanzisha shahada ya uzamili ya Kiswahilina kunichagua mimi kuwa ni mmoja kati ya wanafunzi wa isimu waliochaguliwa

viikujiunga na Chuo hiki.shukurani za dhati ziwafikie wahadhiri wote ambao waliwezakuacha familia zao na kusafiri hadi hapa Zanzibar ili kutupatia taaluma ya kozi hii.Namuomba Mwenyezi Mungu awazidishie moyo wa upendo, awape afya njema namaisha marefu ili waendelee kutoa mchango wa kitaaluma katika taifa letu.Nne, ninatoa shukurani kwa wanafunzi wenzangu wote wa shahada ya uzamili waKiswahili wa mwaka wa masomo 2015/ 2016 kutokana na mashirikiano yao ya dhatikatika masuala ya kitaaluma kwa kipindi chote cha masomo.Tano, ninatoa shukurani kwa viongozi wa taasisi mbalimbali za serikali kwakuniruhusu kutumia maktaba zao katika kujipatia taaluma iliyojisaidia kukamilishakazi hii. Pia ninawashukuru sana viongozi wa shule za Tumbatu, walimu nawanafunzi wao wote kwa mchango wao mkubwa walionipatia hasa kwa kukubalikuwa watafitiwa na kuweza kunipatia taarifa zilizoweza kunisaidia kukamilisha kazihii.Mwisho, ninatoa shukrani za dhati kwa mama mzazi kwa malezi yake mazuri, piamke wangu na watoto wangu kutokana na uvumilivu mkubwa waliouonesha katikakipindi changu chote cha masomo hasa wakati ambapo nililazimika kuwa mbali nao.Vile vile ninawashukuru sana kaka zangu na dada zangu kwa kunitaka kuwa na subrana kuzidisha bidii katika masomo hayo. Wote hao ninawaambia ahsante sana.

viiiIKISIRIUtafiti huuumejadili “Athari za Kiisimu za Lahaja za Kitumbatu katika KiswahiliSanifu Kinachotumika Katika Shule za Tumbatu Zanzibar”.Utafiti ulifanyika Wilayaya Kaskazini “A” Unguja na uliongozwa na Nadharia Kidhi ya Mawasiliano.Nadharia hiyo ilianzishwa na Howard (1973) ambayo lengo lake kuu ni kuelezasababu za kubadili mtindo wa matamshi wakati wa mawasiliano wa kijamii nakuangalia athari zake katika jamii. Katika utafiti huu, data zilikusanywa kwa kutumiambinu ya hojaji, usaili na uchunguzi shirikishi. Jumla ya watafitiwa walikuwa 68.Miongoni mwao walimu walikuwa 29, na wanafunzi walikuwa 39. Vilevile utafitihuu umeonesha matokeo. Miongoni mwa matokeo hayo ni kwamba lahaja yaKitumbatu baadhi ya wakati maumbo ya maneno hutumia ulahaja. Pia, lahaja yaKitumbatu hudondosha viambishi katika maneno.Mwisho, sura imehitimisha kwakutoa mapendekezo ambayo yatasaidia wanajamii kufanya tafiti kwa za lahajambalimbali kwa lengo la kuweka kumbukumbu kwa vizazi vya baadaye.

ixYALIYOMOUTHIBITISHO. iiHAKIMILIKI . iiiTAMKO . ivTABARUKU . vSHUKURANI . viIKISIRI . viiiORODHA YA MAJEDWALI . xiiiORODHA YA VIAMBATANISHO . xivSURA YA KWANZA . 1UTANGULIZI . 11.1Utangulizi kwa Jumla. 11.2Usuli waTatizo . 21.3Tatizo la Utafiti . 41.4Malengo ya Utafiti . 51.4.1Lengo Kuu. 51.4.2MalengoMahususi . 51.5Maswali ya Utafiti . 51.6Umuhimu wa Utafiti . 61.7Mipaka ya Utafiti . 61.8Maadili ya utafiti . 61.9Hitimisho . 7

xSURA YA PILI . 8MAPITIO YA KAZI Tangulizi na mkabala wa Nadharia . 82.1Utangulizi . 82.2Maandiko kuhusu Kiswahili Sanifu . 82.3Tafiti Zinazozungumzia Athari za Lahaja katika Kiswahili . 92.4Kazi Tangulizi Kuhusu Kitumbatu . 112.5Pengo la Utafiti . 172.6Mkabala wa Nadharia . 182.7Hitimisho . 20SURA YA TATU . 21MBINU ZA UTAFITI . 213.1Utangulizi . 213.2Eneo la Utafiti . 213.3Kundi Lengwa . 213.4Sampuli na Usampulishaji . 223.4.1Sampuli. . 223.4.2Mchakato wa Usamplishaji . 223.5Mbinu za Utafiti . 233.5.1Data ya Upili . 233.5.2Data za Msingi . 243.5.2.1 Mbinu ya Usaili. 243.5.2.2 Mbinu ya Hojaji . 253.5.2.3 Mbinu ya Uchunguzishirikishi . 25

xi3.6Zana za Utafiti. 253.7Hitimisho. 26SURA YA NNE . 27UWASILISHAJI NA UCHANGANUZI WA DATA . 274.1Utangulizi . 274.2Mifanyiko ya Kifonolojia na Kimofolojia Inayotokana na Lahaja yaKitumbatu Iliyoathiri Kiswahili Sanifu . 284.2.1Sauti za Kitumbatu . 284.2.2Mfumo wa Irabu katika Kitumbatu . 284.2.2Mfumo wa Konsonanti. 304.3Maumbo ya Maneno ya Kitumbatu. 354.3.1Maumbo ya Kitumbatu na Viambishi Vya Nafsi . 354.3.2Maumbo ya Maneno na Njeo . 374.3.3Maumbo ya Maneno ya Umilikishi . 394.3.4Maumbo ya Maneno na Udondoshaji . 404.3.5Maumbo ya Maneno Katika Uyakinishi na Ukanushi . 414.3.6Maumbo ya Maneno na Mnyambuliko . 424.3.7Maumbo ya Ngeli za Nomino za Kitumbatu . 444.4Tungo za Kitumbatu. 474.4.1Tungo katika Hali ya Kiima na Kiarifu . 474.4.2Tungo za Kitumbatu na Upatanishi wa Kisarufi . 484.5Matumizi ya Lahaja ya Kitumbatu Darasani . 494.5.1Matini za Walimu. 49

xii4.5.2Utungaji wa Insha . 504.6Athari za lahaja ya Kitumbatu katika Kiswahili Sanifu . 534.6.1Athari za kiisimu . 534.6.1.1 Athari Katika Sauti . 544.6.1.2 Athari katika maneno . 564.6.1.3 Athari katika Tungo . 604.6.1.3.1 Tungo Kirai . 604.6.1.3.2 Tungo Kishazi . 614.6.1.3.3 Tungo Sentensi . 624.6.2Athari Katika Masomo Yanayofundishwa Shuleni . 644.6.3Athari Katika Ujifunzaji . 654.6.4Athari katika Ufundishaji . 664.7Sababu zilizosababisha Athari Hizo katika Kiswahili Sanifu. 674.8Hitimisho. 68SURA YA TANO . 69MUHUTASARI, HITIMISHO NA MAPENDEKEZO . 695.1Utangulizi . 695.2Muhtasari wa Utafiti . 695.3Matokeo ya Utafiti . 705.4Mapendekezo ya Utafiti . 735.5Hitimisho . 74MAREJELEO . 75VIAMBATANISHO. 79

xiiiORODHA YA MAJEDWALIJedwali Na 3.1: Idadi ya Sampuli ya Watafitiwa . 22Jedwali Na. 4.1: Mfumo wa Irabu za Kitumbatu . 29Jedwali Na. 4.2: Konsonanti za Kitumbatu. 30Jedwali Na 4.3: Athari za sauti katika Kitumbatu. 54Jedwali Na 4.4: Athari za maneno katika Kitumbatu . 56

xivORODHA YA VIAMBATANISHOKiambatanisho 1: Maswali ya Mtafiti kwa Walimu wa Somo la Kiswahili . 79Kiambatanisho 2: Maswali ya Mtafiti kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi naSekondari . 84Kiambatanisho 3: Matini ya mwalimu wa somo la Kiswahili . 89Kiambatanisho 4: Utungaji wa Insha kwa Wanafunzi wa Shule za Msingina Sekomdari . 90Kiambatanisho 5: Maswali ya Mahojiano. 91

1SURA YA KWANZAUTANGULIZI1.1Utangulizikwa JumlaSura hii imezungumzia historia fupi ya Tumbatu, usuli wa tatizo, tatizo la utafiti,malengo ya utafiti, maswali ya utafiti, umuhimu wa utafiti, mipaka ya utafiti namaadili ya utafiti.Tumbatu ni miongoni mwa visiwa vichache vinavyokaliwa na watu waZanzibar. Kisiwa hiki kipo Kaskazini Unguja kilomita 48 kutoka mjini ungujana kilomita 3 kutoka mkototoni. Kisiwa hiki kina urefu wa kilomita 15.5 naupana wa kilomita 2.5.Wakaazi wa kisiwa cha Tumbatu wamegawika katikasehemu kuu mbili. Nao ni wale Wanaoishi Jongowe ambao wako kusini yakisiwa hicho na wale wanaoishi Gomani ambao wako kaskazini kwa kisiwahicho. Wenyeji wa kisiwa hicho hujuilikana kwa jina la watumbatu.Vilevile kisiwa cha Tumbatu kiko kaskazini “A” Unguja ambacho hivi sasahuitwa wilaya ndogo ya Tumbatu. Wazungumzajiwakubwa wa kitumbatu niwatumbatu wenyewe. Wakaazi wa kisiwahiki wanakadiriwa kuwa ni watu370,000 ambao hujishughulisha zaidi na uvuvi, biashara, kilimo, ufugaji nk.Kwa upande wa lugha, lugha moja hutofautiana na lugha nyengine na ndipohujitokeza lahaja. TUKI ( 2004 - 2005 ) amesema kuwa “ lahaja ni tofauti yamatamshi, maumbo na matumizi ya maneno mbalimbali kwa lugha yenye asilimoja.”

21.2Usuli waTatizoTafiti kuhusu lahaja za Kiswahili zilianza kujitokeza siku nyingi.Miongoni mwa kaziza mwanzo ni ile ya Stigand (1915) anayeleza kuwa lengo lake lilikuwa nikusambazamaneno mengi ya lahaja kutokana na hofu kwamba mabadilikomakubwa yaliyokuwa yakitokea yangeweza kusababisha kupotea kwake. Hivyokimsingi kazi yake ilijihusisha zaidi na orodha ya maneno ya lahaja kwa nia yakuyahifadhi kimaandishi.Vilevile, Stigand (ameshatajwa) amebainisha lahaja 15 zaKiswahili ambazo kwa wakati huo bado ubainishaji wakehaukufanyikakwamisingi ya kitaaluma.Mbaabu (1991) aneleza changamoto zilizokuwepo mwishoni mwa karne ya 19katika harakati ya kuichagua lahaja moja ya kuisanifisha. Pamoja na changamotozilizokuwepo, mwisho, lahaja yaKiunguja Mjini ilisanifiwa.Jambo hilo lilisababishakuibuka kwa lahaja ya Kiswahili sanifu iliyopewa hadhi ya kutumika katikasehemu za kazi, kwenye vyombo vya kutunga sheria, na maandishi yake kutawalakwenye vitabu kadhaa vya kitaaluma.Kamati na mabaraza mbalimbali yaliundwakwa lengo lakukitetea Kiswahili Sanifu. (Maganga 1997) Kamati na mabarazahayo yalifanya kazi yake na hatimaye kukubaliana kwamba lahaja ya KiungujaMjinindio isanifishwe na kuwa Kiswahili Sanifu. Hatahivyonijambolisilopingika kwamba, wengi kati ya wanakamati hao walikuwa ni Wazungumzajiambao hakuwa na ujuzi wa kutosha katika taaluma ya lugha hususani lugha yaKiswahili na lahaja zake.Kutokana na ukweli huu kulikuwa na makosa mengi katikausanifishaji wa lugha ya Kiswahili uliofanywa na watu hao (Maganga 1997). Pamojana makosa hayo, kuwepo Kiswahili Sanifu kilichofanywa na watu hao ndicho

3kilichokubalika na serikali na kutumika katika shughuli rasmi kama vileelimu,utawala, mahakama na katika mikutano ya hadhara.Mbaabu (2003) anaeleza kwamba, lugha ya Kiswahili ina lahaja nyingi kiasikwamba zile zinazofahamika kwa wataalamu wa lugha ya Kiswahili ni chache tukutokananakutozitafitivya kutosha. Anaendelea kuelezakwamba, jambolililowafanya wataalamu hao wa Kiswahili kutoitafiti lugha hii kwa upanaunaostahiki ni dhana kwamba Kiswahili Sanifu ndiyo hasa Kiswahili chenyewena hivyo kupuuza lahaja mbalimbali. Masebo na Nyangwine (2006,2007, 2008)katika ufafanuzi wao juu ya maana ya lahaja katika lugha ya Kiswahili pamoja namambo mengine wanakiri kwamba kuna tofauti mbalimbali zinazojitokeza kutokalahaja moja na nyingine.Miongoni mwa mambo yanayotofautisha lahaja hizo ni lafudhi, fonolojia namsamiati.Maelezo haya yanatoa ufahamu kwamba kama kuna tofauti zakifononolojia, msamiati na lafudhikati ya lahaja moja na nyingine ni wazi kwambakuathiriana kwa lahaja hizo katika vipengele hivyo ni jambo lisilopingika.Tunasemahivi kwa sababu jamii ya Watumbatu kwa mfano, huzungumza Kitumbatu katikashughuli na mawasiliano katika sehemu kubwa ya maisha yao ya kila siku.Kwamsingi huu,wanapokuwa katika shughuli rasmi ambapo wanalazimika kuzungumzaKiswahili Sanifu ni wazi kwamba athari za lahaja ya Kitumbatu zimejitokezakatika Kiswahili Sanifu bilahata ya wao kutarajia. Msanjila (2006) anaelezakwamba ni vigumu sana kuitenganisha jamii na lugha yake kwa kuwa lugha na jamiini kama pande mbili za sarafu moja.

4Kitala (2006) anaeleza kwamba, utamaduni uliopo ndani ya lugha ya Kiswahilihubainika katika lahaja zake. Anaendelea kueleza kwamba ukitaka kuufahamu vizuriutamaduni wa lugha ya Kiswahili basi pitia lahaja zake mbalimbali ndipo utaonautajiri wa utamaduni upatikanao katika ugha ya Kiswahili. Suala kwamba katikalugha kumesheheni utamaduni wa jamii husika ni jambo lisilopingika kwa namnayoyote ile kwa kuwa ni jambo la kweli ambalo limethibitishwa na tafiti mbalimbaliambazo zimeshafanyika.Maelezo haya yanasisitiza uelewa wetu kwamba Kamakatika ama lahaja nyingine tofauti na ile ya kweli. Kitumbatukina utamaduni wakekama zilivyo lugha ama lahaja nyengine za lugha ya Kiswahili jambo tamadunihuopaleanapozungumza KiswahiliSanifu.Katika kudhihirisha utamadunihuo ndipoathari zaKitumbatu katika Kiswahili Sanifu huonekana.Hivyo basi wanafunzi na walimu wao wanapokuwa shuleni husisitizwa kutumiaKiswahili Sanifu katika mawasiliano mbalimbali baina yao. Hata hivyo pamoja namsisitizo huo bado hujitokeza athari mbali mbali zikiwemo za kiisimu na lahajaya Kitumbatu katika Kiswahili Sanifu kinachotumika shuleni. Kwa msingi huobasi, utafiti huu umefanywa ili kuchunguza „athari za kiisimu za lahaja ya Kitumbatukatika Kiswahili Sanifu kinachotumika katika shule za Tumbatu Zanzibar.”1.3Tatizo la UtafitiKutokana na kukua na kupanuka kwa matumizi ya Kiswahili Sanifu katika mazingirarasmi, kumekuwa na mijadala mingi kuhusu athari ya lugha hii kwa lugha nyingineza kijamii (taz. K.m. Mochiwa, 1979).Pia imewahi kuchunguzwa jinsi lugha hizi zakijamii zinavyoathiri matumizi ya Kiswahili hasa katika mazungumzo pale matamshi

5ya lugha ya kijamii yanapojitokeza katikaKiswahili Sanifu. Hata hivyo, mijadalakama hii haijawahi kuhusisha lahaja za Kiswahili ambazo nazo ni lugha zakijamii na zenye uhusiano na lahaja na vile vile uwezekano wa kuathiri lahajasanifu.Kwa kuwa hakuna tafiti zilizofanyika kuhusu athari za lahaja mbalimbalikatikamazingira yaliyo rasmi ndipo mtafiti alipoamua kufanya utafiti ili kuchunguza“Athari za kiisimu za lahaja ya Kitumbatu katikaKiswahili Sanifu kinachotumikakatika shule Tumbatu Zanzibar.”1.4Malengo ya UtafitiMalengo ya utafiti huu ni haya yafuatayo:1.4.1Lengo KuuLengo kuu la utafiti huu nikuchunguza “athari za kiisimu za lahaja ya Kitumbatukatika Kiswahili Sanifu kinachotumika katika shule za Tumbatu Zanzibar”.1.4.2(i)MalengoMahususiKuchunguza mifanyiko ya Kifonolojia na Kimofolojia inayotokana na lugha yaKitumbatu iliyoathiri Kiswahili Sanifu.(ii)Kufafanua athari za kiisimu za lahaja ya Kitumbatu katika Kiswahili Sanifu.(iii) Kuchunguzasababu zilizosababisha athari hizo katika Kiswahili Sanifu.1.5(i)Maswaliya UtafitiNi mifanyiko ipi ya Kifonolojia na Kimofolojia inayotokana na lugha yaKitumbatu iliyoathiri Kiswahili Sanifu?

6(ii)Kuna athari gani za kiisimu za lahaja ya Kitumbatu katika Kiswahili Sanifukinachotumika katika Shule za Tumbatu Zanzibar?(iii) Ni sababu gani zilizosababisha athari hizo katika Kiswahili Sanifu?1.6Umuhimu waUtafitiUtafiti huu utawasaidia walimu na wanafunzi kuelewa athari za kiisimu za lahaja yaKitumbatu katika Kiswahili Sanifu kinachotumika katika shule za TumbatuZanzibar. Pia, utawasaidia kufahamu sababu za athari za lahaja ya Kitumbatu katikaKiswahili Sanifu kinachotumika katika shule za Tumbatu za Zanzibar ilikuziepuka.Vilevile utafiti huu utatoa mchango mkubwa katika nadharia ya Isimu.1.7Mipaka ya UtafitiUtafiti huu umejikita katika kuchunguza mifanyiko ya Kifonolojia na Kimofolojiainayotokana na lugha ya Kitumbatu katika Kiswahili Sanifu, kufafanua athari zakiisimu za lahaja ya Kitumbatu katika Kiswahili Sanifu kinachotumika katika shuleza Tumbatu Zanzibar pamoja na kuchunguza sababu zilizosababisha athari hizokatika Kiswahili Sanifu. Mtafiti ameangalia athari hizo katika kipengele chamatamshi, maumbo ya maneno na tungo tu. Mtafiti hakutembelea katika eneo lote laTumbatu bali alifanya utafiti wake katika shule za Jongowe na Tumbatu tu.1.8Maadili ya utafitiUtafiti huu umeongozwa na maadili nakanuni za kufanya utafiti. Mtafiti ameombakibali kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na katika taasisi zinazohusika ilikupataridhaayakukusanyadatakatika maeneo teule, piaamewaomba

7watafitiwa ridhaa yaushiriki waona kuahidi kutunza siri zao. Jambo lolotelinalokwenda kinyume cha maadili ya utafiti halikufanywa na mtafiti.1.9HitimishoSura hii ya Utangulizi imejadili Utangulizi wa jumla , Usuli wa tatizo, Tatizo laUtafiti. Malengo ya Utafiti, maswali ya utafiti, umuhimu wa utafiti, mipaka yautafiti, maadili ya utafiti na hitimisho.

8SURA YA PILIMAPITIO YAKAZITANGULIZINA MKABALA WA NADHARIA2.1UtanguliziMapitio ya kazi tangulizi ni maandiko yanayohusiana na mada husika ambayo tayariyameshaandikwa na watafiti wa kazi zilizotangulia. Mapitio hayo ni muhimu kwamatafiti ili kumwezesha kuelewa utafiti uliofanyika katika mada husikaa, piahumsidia kuelewa mbinu mbalimbali zilizotumiwa na watafiti waliotangulia. Vilevilehusaidia katika kuepuka kutorudia kilichoandikwa. Sura hii imejadili maandikokuhusu Kiswahili Sanifu, tafiti zinazozungumzia atahari za lahaja katika Kiswahili,kazi tangulizi kuhusu Kitumbatu, pengo la utafiti na Mkabala wa Nadharia.2.2Maandiko kuhusu Kiswahili SanifuKiswahili Sanifu ni Kiswahili kilichofanyiwa marekebisho kutoka lugha nyengine nakuingizwa kwenye lugha husika. Usanifishaji wa lugha ya Kiswahili ulianza mwaka1930 ilipoundwa kamati ya lugha ya Afrika Mashariki. Suala la msingi ilikuwa nikuteua lahaja mojawapo yalahaja za Kiswahili zisizopungua kumi na tano. Kamatihii iliamua kuisanifu lahaja ya Kiunguja mjini ambapo ilikuwa imeenea katikasehemu kubwa ya maeneo ya Bara hadi kufikia Mashariki mwa Jamhuri yaKidemokrasia ya Kongo na nchini Burundi.Kiswahili sanifu ni lugha isiyokuwa na makosa ya kisarufi. Hivyo, lugha hii huwa nasheria, kanuni, au taratibu zinazopaswa kufuatwa katika lugha fulani. Kila lughahuwa na kanuni zake lakini kwa upande wa Kiswahili Sanifu huwa tunazingatiakanuni za kisarufi kama vile sauti (utamkaji), aina za maneno, upatanisho wa

9maneno kisarufi, muundo wa sentensi za Kiswahili na kadhalika. Kiswahili Sanifuhutumika kwamawasiliano baina ya wasemaji wa lahaja tofauti za lugha moja, piahutumika katika shughuli rasmi.2.3Tafiti Zinazozungumzia Athari za Lahaja katika KiswahiliMassamba na wenzake (2009) wameeleza historia fupi ya Kiswahili pamojanakuonesha lahaja za Kiswahili.Katika maelezo yao wamesemakuwa, yapo mambo yakimsingi yenye kutofautisha lahaja moja na nyengine. Miongonimwa mambo hayo nimatamshi, msamiati, muundo na wakati mwingine maana ya maneno.Maelezo hayayanafanana na yale yaMuhura(2009) ambaye ameorodheshaya lahaja 18 zaKiswahili na amesema kuwa miongoni mwa mambo yenye kupelekea lugha mojakuwa na lahaja tofauti ni umbali wa kijiografia, hamahama ya watu elimu na uhabawa mawasiliano kati ya jamii moja na nyengine.Mohamed (1984) alifanya utafiti unaohusiana na lahaja za Kipemba, Kiunguja Mjinipamoja na KiswahiliSanifu.Utafiti wake ukijihusisha zaidi na kueleza matamshi yalahaja ya Kipemba, pamoja na kuzungumzia jinsi ukanushi unavyojitokeza ndani yalughahizo. Katika uchambuzi wake, amedhihirisha mambo mawili makubwa.Kwanza,misamiati kadhaa ya lahaja ya Kipemba na jinsi inavyotofautiana naKiswahili Sanifu, pia ameonesha mabadiliko ya sauti mbali mbali na jinsizinavyotofautiana kutoka maeneo ya mjini hadivijijini. Aidha, ameoneshaumilikishaji wa lahaja ya Kipemba ambao kwa kiasi kikubwa hutokea ndani yanomino husika kama: nyumbayo‟ badala ya nyumba yako, pahalape‟ badala yapahala pake, na „kisungwa‟ badala ya kisu cha watu. Ni dhahiri kuwa vipengele

10hivyo vya lahaja ya Kipemba vimemsaidia mtafitikupata mwongozo wa mambo yakufanyia kazi wakati wa utafiti wake hususani wakati wa kuchunguza mifanyiko yaKifonolojia na Kimofolojia inayotokana na lugha ya Kitumbatu iliyoathiri KiswahiliSanifu.Mbaabu (1991) aliandika kitabu kinachohusu historia ya Kiswahili na usanifishajiwake. Katika kuielezea historia hiyo anaeleza kuwa ingawa kulikuwa na lahajanyingi, lakini lahaja ya kimvita na kiunguja ndio zilizokuwa katika ushindanimkubwa katika mchakato wa kuteua lahaja moja ambayo ndio itakuwa msingi waKiswahili Sanifu.Kazi ya Mbaabu ni muhimu katika utafiti huukwakuwaitamsaidia mtafiti kufahamu historia ya lugha ya Kiswahili na lahaja zakeambayo iliweza kutoa nuru kwa utafiti huu.Maganga (1991) katikatasnifu yake ya Uzamivu amezizungumzia lahaja tatu zaZanzibar. Lahaja hizo ni Kipemba, Kimakunduchi na Kitumbatu na kuzihusisha naKiswahili Sanifu. Dhamira kuu ya kazi yake ni kuchunguza mofofonolojia yalahaja za Kipemba, Kitumbatu naKimakunduchi huku akizihusisha na KiswahiliSanifu. Kazihii ni muhimu kwa utafiti huu kwasababu itamsaidia mtafiti kupatabaadhi ya misamiati ya Kitumbatu, pia kupata mwongozo wa uchambuzi wa datazake.Maganga (1997) aliongelea pia suala la lahaja.Alizitaja lahaja mbalimbali za Kusinina Kaskazini, na kueleza jinsi lahaja zinavyotofautiana kati yao. Katika kielelezocha lahajamama ya kusini, amekionesha Kimakunduchi na hivyo, itamwezeshamtafiti kuelewa

ii UTHIBITISHO Aliyetia saini hapo chini anathibitisha kuwa amesoma na anapendekeza tasnifu hii inayohusu athari za kiisimu za lahaja ya Kitumbatu katika Kiswahili Sanifu kinachotumika katika shule za Tumbatu Zanzibar, ipokelewe na ikubaliwe na Chuo Kikuu Huria cha Tanzani

Related Documents:

tabianchi katika maendeleo ya sasa na unatia maanani fursa za kupunguza ongezeko la hewa mkaa. Katika kutathimini athari za muda mrefu za mabadiliko ya tabianchi ya siku za baadae ,hasa maeneo ambayo yanahitaji hatua za mapema, yaani miundombinu (ya kudumu ) kwa ajili ya athari kubwa na kuc hukua hatua za kukabiliana na hali hiyo

Ikiwa una wasiwasi kuhusu dalili zozote zisizo za kawaida ambazo unaweza kuwa nazo, au una maswali kuhusu mchanganyiko wa athari kutokana na kupata chanjo zaidi ya moja kwa wakati mmoja. Ikiwa una wasiwasi kuhusu athari zako au ikiwa athari haziishi baada ya siku chache.

Wapemba. Surahii pia inatoa taarifa za awali kuhusu mada ya utafiti ambapo mtafiti ataelezea kuhusu usuli wa mada,tatizo la utafiti,malengo ya utafiti yakiambatana na mswali ya utafiti ,umuhuimu wa utafiti mipaka ya utafiti hatimae hitimisho , haya yote yameelezewa juu ya kuchunguza matumizi ya tafsida katika lahaja

mada ya utafiti: athari za lugha ya kijita katika kujifunza kiswahili mashaka wenceslaus tasnifu hii imewasilishwa kwa ajili ya kukamilisha masharti ya shahada ya uzamili m.a (kiswahili) kiti vo cha sanaa na sayansi ya jamii.chuo kikuu huria cha tanzania. novemba, 2015

karibuni, uchunguzi wa epigrafia na grafiti ulikuwepo kuanzia karne nyingi zilizopita na dhana hizo zina uhusiano wa karibu na kile kinachochunguzwa katika mandhari-lugha katika zama hizi. Baada ya michoro hiyo ya kale, dhana ya mandhari-lugha ilihusishwa na mgogoro wa kiisimu wa nchini Ubelgiji (Landry na Bourhis, 1997). Mgogoro huo

Miongoni mwao ni Mwalimu Mkuu Bw. Maurice Ogutu na manaibu wake; pamoja na walimu wengine wote. Nawashukuru sana. . Utafiti huu ni uchunguzi wa utohozi wa nomino za lahaja ya Kijaluo ya Nyanza Kusini ambazo . Kielelezo 8 Mchoro wa Uainisho wa Fonimu za Irabu Kielelezo 9 Jedwali la Ngeli za Kimofolojia za Kiswahili . viii

2.0 Dhuluma dhidi ya Wanawake katika Fasihi Kama inavyodhihirika katika kazi za fasihi, wanawake wanapitia aina tofauti za dhuluma katika jamii wanamoishi. Wasomi na wahakiki wa kazi za fasihi wameshughulikia suala la dhuluma kwa wanawake na athari zake kwa muda mrefu bila kutoa suluhu.

In Abrasive Jet Machining (AJM), abrasive particles are made to impinge on the work material at a high velocity. The jet of abrasive particles is carried by carrier gas or air. High velocity stream of abrasive is generated by converting the pressure energy of the carrier gas or air to its kinetic energy and hence high velocity jet. Nozzle directs the abrasive jet in a controlled manner onto .