KISWAHILI - Rwanda Education Board

1y ago
18 Views
2 Downloads
5.62 MB
179 Pages
Last View : 13d ago
Last Download : 3m ago
Upload by : Jerry Bolanos
Transcription

KISWAHILIKWA SHULE ZA RWANDAMichepuo MingineKitabu cha MwanafunziKidato cha 4

Hati milki 2019 Bodi ya Elimu RwandaKitabu hiki ni mali ya Bodi ya Elimu Rwanda. Haki zote zimehifadhiwa. Kimetayarishwana Bodi ya Elimu Rwanda kwa idhini ya Wizara ya Elimu.Chapa ya Kwanza 2019

DIBAJIMwanafunzi MpendwaBodi ya Elimu Rwanda inayo heshima kwa kutoa kitabu hiki cha Somo la KiswahiliMichepuo mingine kidato cha nne kitabu cha mwanafunzi .Kitabu hiki kitakuwawaraka rasmi utakaoongoza ufundishaji na ujifunzaji kuendana na mtaalauegemeao katika uwezo .Falsafa ya Elimu Rwanda inalenga katika kumpatia mlengwa uwezo katika kilangazi ya Elimu kuweza kumudu vizuri katika jamii na kumpa fursa ya kujipatiaajira .Ili kwenda sambamba na juhudi za kuboresha ubora wa Elimu Serikali ya Rwandainasisitiza umuhimu wa kufungamanisha ujifunzaji na ufundishaji na zana pamojana mitaala ili kuwezesha mchakato wa wa ujifunzaji . Mambo mengi yanayoathiriyale ambayo wanafunzi wanafundishwa , namna nzuri ya kujifunza na uwezowaupatao . Mambo hayo ni pamoja na umuhimu mahsusi wa yaliyomo,uborawa walimu , mbinu za ufundishaji na ujifunzaji, mikakati ya upimaji na vifaa vyakufundishia vilivyopo . Tumezingatia umuhimu wa mbinu zenye mchakato wakujifunza ambao unakuwezesha kuendeleza mawazo yako na kufanya ugunduzimpya wakati wa mazoezi thabiti yawe ya binafsi au katika makundi ,kwa msaada wawalimu ambao majukumu yao ni kufanikisha ufundishaji.Utapata stadi zinazofaakukuwezesha kutumia yale uliyojifunza katika miktadha ya maisha halisi.Kwakufanya hivyo , utaonyesha tofauti siyo tu katika maisha yako bali hata kwa Taifa .Hii inatofautiana na mfumo wa zamani kuhusu nadharia ya ujifunzaji,iliyosisitizamchakato wa kujifunza kama upataji wa maarifa kutoka yule aliyemzidi maarifana hasa akiwa ni mwalimu.Katika mtaala uegemeao katika uwezo , ujifunzaji unachukuliwa kama mchakatowa kazi ya kujenga na kuendeleza maarifa na ufahamu, stadi na maadili namweneno mwema kutoka kwa mwanafunzi ambapo dhana aghalabu huanzishwakwa mazoezi , hali na mazingira yanayomsaidia mwanafunzi kujenga maarifa ,kuendeleza stadi na upatikanaji chanya wa maadili na mwenendo mwema .Aidha kazi ya kujifunza hujishughulisha na wanafunzi kwa kufanya mambo nakufikiri kuhusu yale wanayoyafanya na wanafarijika kuonyesha uzoefu wao halisina maarifa katika mchakato wa ujifunzaji .Kiswahili Kidato cha 4 Kitabu cha Mwanafunziiii

Katika ufahamu huu , ufanisi mzuri kwa kutumia kitabu hiki, jukumu lako litakuwa : Kuendeleza maarifa na stadi kwa kufanya kazi,mazoezi yanayolengakwenye mada . Kuwasiliana na kupeana taarifa sahihi pamoja nawanafunzi wengine kwa kupitia wasilisho , mijadala , kazi katikamakundi na mbinu nyingine za ufundishaji kama : michezo ya kuigiza,utafiti, uchunguzi na utafiti katika maktaba , katika mitandao na nje yashule . Kushiriki na kuwajibika kuhusu ujifunzaji wako na Kufanya utafiti,uchunguzi kwenye maandishi yaliyochapishwa /mtandaoni,wataalam nakuwasilisha matokeo ya utafiti. Kuhakikisha ufanisi mzuri wa mchango wa kila mwanakundi katikakazi sahihi uliyopewa kupitia maelezo na majadiliano unapoongeahadharani. Kutoa hitimisho sahihi kuhusu matokeo ya utafiti uliotokana na mazoeziya ujifunzaji.Napenda kutoa shukrani kwa wale wote walioshiriki kutoa mchango wakuboresha kitabu hiki, na hasa wafanyakazi wa Bodi ya Elimu Rwanda (CTLR-REB)walioandaa mchakato wa kazi hii tokea ilipoanza .Pongezi muhimu ziwaendee walimu chuo Kikuu cha Rwanda kwa msaada wao wakutoa wataalamu ambao ni ,wahadhiri walimu wachoraji waliosaidia kusimamia,kuendeleza na kufanikisha uboreshaji wa kazi hii kuhusu picha na michoro sahihi.Maoni au mawazo yoyote yanakaribishwa kwa ajili ya uboreshaji wa kitabu hikikwa matoleo yatakayofuata .Dr Ndayambaje IrénéeMkurugenzi Mkuu Bodi ya Elimu RwandaivKiswahili Kidato cha 4 Kitabu cha Mwanafunzi

SHUKRANINapenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa wale wote walioshiriki kwa hali namali katika kukiandaa na kukifanikisha kitabu hiki. Kitabu hiki kisingeliwezekanakufanikiwa bila kuwepo wadau mbalimbali walioshiriki , jambo ambalo limenifanyanitoe shukrani zangu za dhati .Shukrani zangu ziwaendee vyuo vikuu na shule mbalimbali walioruhusuwafanyakazi wao kufanya kazi na Bodi ya Elimu katika mradi wa utoaji wa kitabuhiki. Napenda kutoa shukrani zaidi kwa Wahadhiri na walimu ambao juhudi zao nauandikikaji wa kitabu hiki ulivyo kuwa wa thamani.Natoa shukrani zangu kwa shule mbalimbali Rwanda zilizoweza kuwaruhusuwalimu na wahadhiri katika kuandaa kitabu hiki hadi kuhaririwa kwake.Shukrani zaidi ziwaendee vyuo vikuu na shule mbalimbali walioruhusu wafanyakaziwao kufanya kazi na Bodi ya Elimu katika mradi wa utoaji wa kitabu hiki.Napendakutoa shukrani zaidi kwa Wahadhiri na walimu ambao juhudi zao na uandikikaji wakitabu hiki ulivyokuwa wa thamani.Mwishowe neno la mwisho la shukrani liwaendee wafanyakazi wote wa Bodi yaElimu Rwanda (CTLR-REB) walioshiriki katika mchakato wa kufanikisha uandikajiwa kitabu hiki.Joan MurungiMkuu wa idara ya Mitaala, Ufundishaji, Ujifunzaji na Zana ( CTLR)Kiswahili Kidato cha 4 Kitabu cha Mwanafunziv

YALIYOMODIBAJI. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ivSHUKRANI. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . viUTANGULIZI . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . xMADA KUU YA 1: MATUMIZI YA LUGHA KATIKA MAZINGIRA MBALIMBALI . . . . . . . . . . . . 14MADA NDOGO: MSAMIATI KATIKA MAZINGIRA YA HOSPITALI. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 14SOMO LA 1: MAZUNGUMZO HOSPITALINI . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 151.1. Kusoma na Ufahamu: Mazungumzo Hospitalini. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 151.2. Msamiati Kuhusu Mazingira ya Hospitali. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 191.3. Sarufi: Matumizi ya Kiambishi -nge- . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 201.4. Matumizi ya lugha: Vifaa vya Hospitalini. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 221.5. Kusikiliza na kuzungumza. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 231.6. Kuandika. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 23SOMO LA 2: USAFI WA MAZINGIRA YA HOSPITAL. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 242.1. Kusoma na Ufahamu: Umuhimu wa Usafi wa Mazingira Hospitalini. . . . . . . . 242.2. Msamiati kuhusu Usafi Hospitalini. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 262.3. Sarufi: Matumizi ya Kiambishi -ngeli- . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 282.4. Matumizi ya Lugha. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 302.5. Kusikiliza na Kuzungumza: Majadiliano na Mawasilisho . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 312.6. Kuandika: Utungaji wa Kifungu. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 31SOMO LA 3 : ADABU HOSPITALINI . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 323.1. Kusoma na Ufahamu: Maelekezo na Kanuni Hospitalini . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 323.2. Msamiati kuhusu Adabu Hospitalini. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 343.3. Sarufi: Matumizi ya Kiambishi chenye Dhana ya Masharti -ngali-. . . . . . . . . . . 363.4. Matumizi ya Lugha: Msamiati wa Adabu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 373.5. Kusikiliza na Kuzungumza: Majadiliano. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 383.6. Kuandika: Sifa za Aya katika Uandishi. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 38MADA KUU YA 2: MATUMIZI YA LUGHA KATIKA MAZINGIRA MBALIMBALI. . . . . . . . . . . . . 42MADA NDOGO: MSAMIATI KATIKA MICHEZO. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 42SOMO LA 4: MICHEZO SHULENI . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 434.1. Kusoma na Ufahamu: Timu Hodari. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 434.2. Msamiati kuhusu Michezo Shuleni. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 464.3. Sarufi: Matumizi ya majina ya ngeli ya LI-YA. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 474.5. Kusikiliza na Kuzungumza: Zoezi la Kutangaza Mpira wa Miguu Redioni . . . 49viKiswahili Kidato cha 4 Kitabu cha Mwanafunzi

4.6. Kuandika: Utungaji . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 49SOMO LA 5: FAIDA ZA MICHEZO. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 505.1. Kusoma na Ufahamu: Faida za Michezo. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 505.2. Msamiati kuhusu Faida za Michezo. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 525.4. Matumizi ya Lugha: Utambuzi wa Maana za maneno. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 562.5. Kusikiliza na Kuzungumza: Majadiliano. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 572.6. Kuandika: Utungaji wa Kifungu cha Habari. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 57SOMO LA 6: MASHINDANO KATIKA MICHEZO . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 586.1. Kusoma na Ufahamu: Mchezo wa Kandanda. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 586.2. Msamiati kuhusu Mchezo wa Kandanda. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 616.3. Sarufi: Matumizi ya Vivumishi vya Kuuliza, vya Idadi na vya Sifa. . . . . . . . . . . . 626.4. Matumizi ya Lugha: Upangaji wa Maneno katika Sentensi na Miktadha yaMatumizi. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 646.5. Kusikiliza na Kuzungumza: Majadiliano. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 646.6. Kuandika: Utungaji wa Kifungu kuhusu Matukio ya Mchezo. . . . . . . . . . . . . . . 64MAADA KUU YA 3: UHAKIKI WA HADITHI ZA MASIMULIZI KATIKA KISWAHILI. . . . . . . . . . 68MADA NDOGO: MUHTASARI, FANI NA MAUDHUI. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 68SOMO LA 7: MUHTASARI. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 697.1. Kusoma na Ufahamu: Mhunzi Tulia. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 697.2. Msamiati Kuhusu Kifungu. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 717.3. Sarufi: Majina ya Ngeli ya Pa- na vivumishi vyake. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 727.4. Matumizi ya Lugha: Sifa za Muhtasari. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 757.5. Kusikiliza na kuzungumza: Majadiliano. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 777.6. Kuandika: Uandishi wa Muhtasari. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 77SOMO LA 8: FANI KATIKA HADITHI SIMULIZI . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 788.1. Kusoma na Ufahamu: Kobe na Nyani . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 788.2. Msamiati kuhusu kifungu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 818.3. Sarufi: Matumizi ya Majina ya Ngeli ya M- na Vivumishi Ambatana. . . . . . . . . 828.4. Matumizi ya Lugha: Fasihi. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 858.5. Kusikiliza na Kuzungumza: Majadiliano. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 888.6. Kuandika: Utungaji wa Hadithi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 88SOMO LA 9: MAUDHUI KATIKA HADITHI SIMULIZI . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 899.1. Kusoma na Ufahamu: Wafalme Wawili. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 899.2. Msamiati kuhusu Wafalme Wawili. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 929.3. Sarufi: Matumizi ya Majina ya Ngeli ya Ku- na Viumishi Ambatana. . . . . . . . . 93Kiswahili Kidato cha 4 Kitabu cha Mwanafunzivii

9.4. Matumizi ya Lugha: Maudhui katika Fasihi. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 959.5. Kusikiliza na Kuzungumza: Majadiliano. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 979.6. Kuandika: Utungaji wa Hadithi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 97MADA KUU YA 4: UKUZAJI WA MATUMIZI YA LUGHA KIMAZUNGUMZO. . . . . . . . . . . . . . 102MADA NDOGO: MIDAHALO NA MIJADALA. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 102SOMO LA 10: MDAHALO. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 10310.1. Kusoma na Ufahamu: Mazungumzo Baina ya Wanafunzi. . . . . . . . . . . . . . . . 10310.2. Msamiati kuhusu Maana ya Mdahalo. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 10610.3. Sarufi: Matumizi ya Hali ya Kushurutisha kwa Vitenzi. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 10710.4. Matumizi ya Lugha: Maana ya Mdahalo. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 10910.5. Kusikiliza na Kuzungumza . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 11010.6. Utungaji. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 110SOMO LA 11:MAANDALIZI NA UTEKELEZAJI WA MDAHALO. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 11111.1 Mdahalo : Dawa za Kulevya Ndilo Tatizo Linaloathiri Maendeleo ya Vijana. . .11.2 Msamiati kuhusu “Mdahalo”. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 11911.3 Sarufi: Matumizi ya Vitenzi vya Silabi Moja . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 12011.4. Matumizi ya lugha: Maandalizi na Utekelezaji wa Mdahalo. . . . . . . . . . . . . . 12211.5. Kusikiliza na Kuzungumza: Mdahalo. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 12411.6. Kuandika: Uandishi wa Mdahalo . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 124SOMO LA 12: MJADALA. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 12512.1. Kusoma na Ufahamu : Maana ya Mjadala. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 12512.2. Msamiati kuhusu Maana ya Mjadala. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 12712.3. Sarufi: Hali Shurutishi ya Vitenzi. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 12912.4. Matumizi ya Lugha: Maana ya Mjadala . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 13112.5. Kusikiliza na Kuzungumza . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 13212.6. Utungaji. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 132SOMO LA 13: MAANDALIZI NA UTEKELEZAJI WA MJADALA . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 13313.1. Mjadala kuhusu: “Mchango wa Wazazi katika Malezi ya Watoto Wao”. . . . 13313.2. Msamiati kuhusu “Andalio la Mjadala”. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 13813.3. Sarufi: Matumizi ya Hali ya Vitenzi. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 13913.4. Matumizi ya lugha: Maandalizi na Utekelezaji wa Mjadala. . . . . . . . . . . . . . . 14113.5. Kusikiliza na Kuzungumza . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 14213.6. Utungaji. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 143MADA KUU: UTUNGAJI . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 146viiiKiswahili Kidato cha 4 Kitabu cha Mwanafunzi

MADA NDOGO: INSHA ZA MASIMULIZI AU ZA KUBUNI . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 146SOMO LA 14: MAANA YA INSHA. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 14714.1. Kusoma na Ufahamu: Tarakilishi. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 14714.2 Msamiati kuhusu Kifungu cha Habari. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 14914.3. Sarufi: Usemi Halisi na Usemi wa Taarifa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 15114.4. Matumizi ya Lugha: Maana ya Insha na Sifa Zake. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 15214.5 Kusikiliza na Kuzungumza: Majadiliano . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 15314.6. Utungaji: Uandishi wa Insha. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 153SOMO LA 15: AINA ZA INSHA . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 15415.1. Kusoma na Ufahamu: Nchi Yetu. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 15415.2. Msamiati kuhusu Nchi Yetu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 15615.3. Sarufi: Usemi wa Taarifa. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 15715.4. Matumizi ya Lugha: Aina za Insha . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 15915.5. Kusikiliza na Kuzungumza: Majadiliano. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 16315.6. Utungaji: Uandishi wa Insha ya Wasifu. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 163SOMO LA 16: INSHA ZA MASIMULIZI . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 16416.1. Kusoma na Ufahamu: Siku Yangu ya Kwanza katika Shule ya SekondariKidato cha Nne. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 16416.2. Msamiati Kuhusu Insha ya Masimulizi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 16616.3. Sarufi: Usemi wa Asili na Usemi wa Taarifa. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 16816.4. Matumizi ya Lugha: Sehemu za Insha. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 17316.5. Kusikiliza na Kuzungumza . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 17516.6. Utungaji. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 175MAREJEO. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 176Kiswahili Kidato cha 4 Kitabu cha Mwanafunziix

UTANGULIZIKiswahili ni lugha ambayo imepewa kipaumbele zaidi kutokana na urahisi wakewa kutumiwa kama lugha rasmi miongoni mwa lugha nyingine zinazotumiwakatika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Nchini Rwanda, lugha ya Kiswahili hufundishwakatika shule za upili kuanzia kidato cha kwanza hadi kidato cha tatu katika ngazi yachini ya sekondari. Zaidi ya hivyo, mbali na mchepuo wa lugha ambapo Kiswahilihufundishwa katika mchepuo wa Kiingereza, Kinyarwanda na Kiswahili, lugha hiihufundishwa pia katika michepuo mingine. Kwa hivyo, lugha ya Kiswahili imepigahatua kimatumizi katika jamii mbalimbali barani Afrika na hata ulimwenguni. Nchikama vile Marekani, Ujerumani na nchi nyingi za Ulaya, hufundisha Kiswahili nakukitumia katika mazingira tofauti. ,Kitabu hiki kimeandikwa kwa kuwalenga wanafunzi wa Shule za Sekondari nchiniRwanda wanaosoma katika kidato cha nne, michepuo isiyokuwa na somo la Kiswahili.Kila mada iliyojadiliwa katika kitabu hiki, imegawanywa katika mada ndogo ndogo.Ambapo kila mada ndogo huwa na masomo mbalimbali yenye kugusia vipengelevifuatavyo: Kusoma na ufahamu Maswali ya ufahamu Matumizi ya msamiati wa msingi Sarufi Matumizi ya lugha Kusikiliza na kuzungumza Kuandika.Masomo yaliyopendekezwa katika kitabu hiki yamezingatia matakwa na mahitaji yanchi ya Rwanda. Kwani Kiswahili kinahitajika kutumika katika mawasiliano mapanakatika Jumuiya ya Afrika ya mashariki. Aidha, Mwanafunzi anatakiwa kujifunza hatuakwa hatua masomo yote yaliyopendekezwa ili aweze kujijengea na kujifunguliamilango ya kujiendeleza na kuliendeleza taifa lake kwa jumla.Uwezo utakaopatikana kupitia masomo hayo, utamwezesha mwanafunzikukabiliana na matatizo mbalimbali yanayojitokeza katika maisha yake ya kila siku:Kujilinda na magonjwa mbalimbali katika elimu ya afya ya uzazi, kutunza mazingira,elimu kuhusu uzalishaji mali au ujasiriamali, usawa wa jinsia, mafunzo kuhusu amanina maadili.xKiswahili Kidato cha 4 Kitabu cha Mwanafunzi

Ili kufanikisha ujifunzaji wake, ni vyema mwanafunzi ajitahidi kufanya mazoeziyaliyotolewa kwa kila somo. Vilevile, ni jambo muhimu kusoma kwa makini nakufanya uchunguzi wa mada zilizojadiliwa katika kitabu hiki. Mazoezi mengiyaliyopendekezwa yatamwezesha mwanafunzi kukuza uwezo wake katika kiwangocha utafiti, ushirikiano na utawala binafsi na stadi za maisha na kuendelezaujifunzaji wa muda mrefu. Vilevile, mazoezi ya mijadala ya kibinafsi na ya makundiyote yatasaidia kumjenga mwanafunzi kwa kumpa uwezo wa kuwasiliana na watumbalimbali kwa kutumia Kiswahili fasaha. Mazoezi ya makundi yaliyopendekezwayatamsaidia mwanafunzi kuelewa nafasi yake katika kujenga desturi ya heshima kwawengine, uvumilivu, upendo na amani, haki, umoja na mshikamano na demokrasiapia.Ili kufanikisha ujifunzaji wake, ni vyema mwanafunzi akumbuke kwamba kitabu hikikinafuata vitabu vingine vya Kiswahili ambavyo viliandaliwa wanafunzi wa awamuya kwanza ya shule za Sekondari nchini Rwanda. Kwa hivyo, mwanafunzi awe naujuzi wa awali wa kutosha ambao utamwezesha kuelewa mada zilizotolewa katikakitabu hiki kwa kuhakikisha kwamba amepata uwezo wa kutosha wa kutumia lughaya Kiswahili katika mawasiliano na shughuli mbalimbali za maisha.Kiswahili Kidato cha 4 Kitabu cha Mwanafunzixi

xiiKiswahili Kidato cha 4 Kitabu cha Mwanafunzi

MADA KUU YA 1MATUMIZI YA LUGHAKATIKA MAZINGIRAMBALIMBALI

MADA KUU YA 1: MATUMIZI YA LUGHA KATIKAMAZINGIRA MBALIMBALIMADA NDOGO: MSAMIATI KATIKA MAZINGIRA YA HOSPITALIUwezo upatikanao katika mada: Kusikiliza kwa makini, kusoma vifungu vya habarina kutumia msamiati muhimu katika mazingira ya hospitali; kuzingatia matumiziya viambishi -nge-, -ngeli- na -ngali-.Malengo ya Ujifunzaji Kutumia msamiati maalum wa mazingira ya hospitali katika mawasiliano; Kuelezea hospitali na mazingira yake kwa mtu yeyote anayehitaji habarikuhusu hospitali hiyo; Kulinganisha na kutofautisha hospitali moja na nyingine kwa kuzingatiamazingira na shughuli zinazofanyika hapo; Kuelezea uhusiano wa watu wapatikanao hospitalini; Kusikiliza kwa makini na kusoma kwa ufasaha kifungu cha habari kinachohusika; Kutunga sentensi fupi kwa kuzingatia hali ya masharti.Kazi Tangulizi1.2.3.4.5.6.14Hospitali ni nini?Taja vifaa vitano vitumiwavyo hospitalini, kisha eleza umuhimu wake.Ainisha kazi na majukumu ya wafanyakazi wapatikanao hospitalini.Ainisha kazi na majukumu ya wafanyakazi wapatikanao hospitalini. Andika aya moja kwa kuelezea umuhimu wa usafi hospitalini.Baadhi ya wagonjwa huonyesha mienendo isiyofaa hospitalini. JadiliKiswahili Kidato cha 4 Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 1: MAZUNGUMZO HOSPITALINITazameni mchoro ufuatao. Jadilini mnayoyaona kwenye mchoro husika.Zoezi la 1: Taja angalau vitu vitatu (watu, vifaa, majengo) ambavyohupatikana katika mazingira ya hospitali au zahanati.1.1. Kusoma na Ufahamu: Mazungumzo HospitaliniWanafunzi wa kidato cha nne kwenye Shule ya Sekondari ya Ntende wametembeleahospitali moja iliyoko mjini Kigali. Wameingia hospitalini na kukaribishwa na mpokeziwageni ambaye anamwita Daktari Mkuu pamoja na muuguzi wake ili wawaelezeemengi kuhusu vifaa na wafanyakazi wa hospitali yao.Daktari: Hamjambo vijana!Wanafunzi: Hatujambo Daktari!Daktari: Asante sana kwa wazo lenu la kutembelea hospitali yetu kwa ajili ya kujua kuhusuvifaa tofauti vinavyotumiwa, sehemu za hospitali, pamoja na wafanyakazi wa hospitali. Kwahiyo, karibuni nyote! Mimi ni Daktari Mkuu na huyu ni muuguzi wetu, anaitwa Veneranda. Kwahakika, tunafurahia kuwaonyesha sehemu mbalimbali za hospitali yetu kama mnavyohitaji.Kiswahili Kidato cha 4 Kitabu cha Mwanafunzi15

Mwanafunzi wa kwanza: Asante sana kwa kutukaribisha. Jina langu ni Bella na mimi ndimikiranja wa darasa letu. Hawa ni wanafunzi wenzangu. Nasi pia tutanufaika zaidi kutokana namaelezo yenu kuhusu shughuli zinazofanywa na vifaa vinavyotumiwa hospitalini.Daktari: Asante sana! Sasa ni wakati wa kuwaelezea juu ya sehemu tofauti za hospitali.Mwanafunzi wa pili: Tafadhali Daktari! Kabla ya hayo, ningetaka kujua jina la sehemu hiiambapo tumekaribishiwa na kupata kiti.Daktari: Sehemu hii inaitwa pambajio. Ni sehemu ya kuwapokelea wagonjwa.Mwanafunzi wa tatu: Samahani Daktari! Sisi hatuko wagonjwa, najiuliza ikiwahamtatudunga sindano! Labda kwa bahati mbaya, mnaweza !Daktari: Usiwe na wasiwasi kijana! Nyie ni wageni siyo wagonjwa. Acheni tuendelee.Sehemu ya pili ni chumba cha matibabu ya dharura, yaani chumba cha kuwatibia wagonjwawanaohitaji matibabu ya haraka sana kama vile majeruhi wa ajali. Lakini, ni vyema mwelewekwamba chumba hiki ni tofauti na wodi ya matibabu maalum kwani wodi ya matibabumaalumu ni chumba cha kushughulikia maradhi ambayo si ya kawaida kama vile maradhiambayo yamezuka ghafla na bado hayaeleweki vizuri.Muuguzi: Kuna wodi nyingine ambayo ni sehemu ya kuwalaza wagonjwa wanaoendeleana matibabu.Mwanafunzi wa kwanza: Samahani Daktari! Nimesoma kwenye mlango ule nenomaabara. Kwa hiyo, ningetaka kujua maana ya neno hilo.Daktari: Asante sana! Bado ninaendelea kuwaelezea, ebu tegeni sikio! Maabara ni chumbacha kufanyia uchunguzi wa magonjwa, lakini kuna sehemu nyingine muhimu za hospitalikama vile chumba cha dawa, kungawi ambacho ni chumba cha kujifungulia kwa kina mamawajawazito, chumba cha upasuaji, chumba cha uangalizi maalumu,ambacho ni chumbacha matibabu ya kiwango cha juu sana. Hususan chumba hiki hutumiwa kwa wagonjwawalio katika hali mahututi.Muuguzi: Chumba hiki huwa na mitambo na mashine za hali ya juu sana za kumsaidiamgonjwa. Chumba cha mwisho ni ufuoni au makafani ambacho ni chumba kinachotumiwakuhifadhia maiti.Mwanafunzi wa nne: Asante sana Daktari kwa maelezo haya. Ningependa sasa utuelezeekuhusu wafanyakazi wa hospitali na vifaa muhimu wanavyotumia.Daktari: Kabla hatujatembelea vyumba vyote vyenye kuhifadhi vifaa mbalimbalitunavyotumia, chunguzeni kwenye picha hizi za vifaa vipatikanavyo hospitalini. Hapa kunaeksrei au uyoka ambayo ni mashine ya kutazamia viungo vya ndani ya mwili. Machela ni kifaakingine. Kifaa hiki ni kigari au kitanda cha kubebea wagonjwa. Maikroskopu au hadubinihutumiwa kuangalia vijidudu vidogo sana ambavyo haviwezikuonekana kwa macho.16Kiswahili Kidato cha 4 Kitabu cha Mwanafunzi

Dipriza hii mnayoiona ni chombo cha kuhifadhia baadhi ya dawa zinazohitajikuhifadhiwa katika baridi kali sana. Jiko lile hutumiwa kuchemshia vyombo ili kuuliavijidudu na bakteria. Hapa mnaona glovu ambayo ni kifaa chenye umbo kama lasoksi. Kifaa hiki hutengenezwa kwa mpira na huwekwa mkononi kumkinga muuguzianayekitumia dhidi ya uchafu. Kwenye mchoro huu mnaona sindano; yaani kifaacha kupenyezea dawa mwilini. Makasi haya mnayoyaona hapa hutumiwa kwakukatia. Bendeji hii mnayoiona hapa ni kitambaa cha kufungia jeraha au kidondakisiweze kuchafuliwa. Plasta ni kitambaa kigumu sana cha kufungia sehemu ya mwiliiliyovunjika. Koleo hii hapa hutumika kama kifaa cha kushikia vitu vinavyotumiwana daktari.Muuguzi: Naona daktari amewafafanulia vizuri kuhusu vifaa mbalimbali tunavyotumiahospitalini. Ningependa tutembelee sehemu ambapo tutawakuta wafanyakazi mbalimbaliili niwaelezee kazi zao. Kuhusiana na wafanyakazi wanaopatika

Kiswahili Kidato cha 4 Kitabu cha Mwanafunzi iii DIBAJI Mwanafunzi Mpendwa Bodi ya Elimu Rwanda inayo heshima kwa kutoa kitabu hiki cha Somo la Kiswahili Michepuo mingine kidato cha nne kitabu cha mwanafunzi .Kitabu hiki kitakuwa

Related Documents:

Kiswahili dialects are endangered by, among other factors, the onslaught of standard Kiswahili, English, and Sheng, and so they are likely to be dying. The paper holds the position that the Kiswahili dialects are vital for the development of standard Kiswahili and, therefore, their endangerment is the endangerment of standard Kiswahili.

Introduction to Kiswahili Poetry KSX 2102 Kiswahili Oral Literature KSX 2104 (with Mr Innocent Yerindabo) Introduction to Kiswahili Novels KSX 2202 History and Development of Kiswahili KSX 3101 Kiswahili Teaching Methods KSX 3201 Drafts Reviewed: Advanced Proficiency in Kiswahili KSX 1102 by Boaz Mutungi.

Publication August 7th, 2014: MSc Thesis: Tyre pressure and Axle load surveys of Heavy vehicles and the implications in Northern Corridor, RWANDA. Page 2 of 8 Curriculum Vitae of Jean Bosco NIZEYIMANA Post Graduate Courses Education Institution Post graduate courses Date University of Rwanda University of Rwanda University of Rwanda University of Rwanda University of Rwanda University of .

Song as an aspect of Kiswahili poetry. Origin and development of modern Kiswahili classics such as taarab. Leading founders of Kiswahili popular song in East Africa, history and development of Kiswahili solo, choral and orchestra composition. Themes, style and language use in popular Kiswahili songs.

Kiswahili) na Shahada ya Umahiri/Uzamili ya Sanaa katika Kiswahili (MA. Kiswahili – akitamilikia Fasihi) zote kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania. Chuoni anafundisha kozi za Kiswahili - Lugha, Isimu na Fasihi ikiwemo kozi ya Uandishi wa Kubuni. Pia, hufundisha Kiswahili

4.0 KISWAHILI (102) 4.1 MATOKEO YA MTIHANI WA SOMO LA KISWAHILI Jedwali hili linaonyesha matokeo ya mtihani wa somo la Kiswahili katika muda wa miaka minne (2005 hadi 2008). Jedwali 6: Matokeo ya mtihani wa Kiswahili (2005 - 2008) Mwaka Karatasi Watahiniwa Alama ya Juu Alama ya Wastani Alama ya Tanganisho 2005 1 2 3 Jumla 259,301 40 80

Rwanda, including Ministry of Health, Rwanda Biomedical Centre (), Medical Procurement RBC and Production Division (MPPD), Rwanda Food & rug Administration, Rwanda Information D Society Authority (RISA) and National Institute of Statistics Rwanda (NISR). The team visited MPPD’s warehouse, a

3 PRACTICE TEST 01 May 2004 Question 1-10 All mammals feed their young. Beluga whale mothers, for example, nurse their calves for some twenty months, until they are about to give birth again and their young are able to