MTIHANI WA PAMOJA MECS 2021 - Elimucentre.co.ke

1y ago
14 Views
2 Downloads
1.10 MB
15 Pages
Last View : 15d ago
Last Download : 3m ago
Upload by : Genevieve Webb
Transcription

MTIHANI WA PAMOJA - MECS 2021Jina:Nambari ya mtahiniwa: Darasa: Tarehe: Sahihi:102/2KiswahiliKaratasi ya 2Muhula wa Pili - 2021Muda: Saa 2½MAAGIZO(i)Andika jina lako na nambari yako ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.(ii)Tia sahihi yako kisha uandike tarehe ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.(iii)Jibu maswali yote.(iv)Majibu yote yaandikwe katika nafasi ulizoachiwa katika kijitabu hiki cha maswali.(v)Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.KWA MATUMIZI YA MTAHINISWALIUPEO115215340410JUMLA80ALAMAPage 1 of 15https://elimuspace.co.ke/- 0705738367 MECS 2020

1. UFAHAMU : (Alama 15)Soma kifungu kifuatacho kasha ujibu maswali.Nchi nyingi duniani zimetia sahihi mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watoto. Haki hizi nipamoja na uhai, lishe bora inayotosha na makazi bora yaliyo salama. Hali kadhalika, kila mtoto ana hakiya kupata elimu. Elimu inastahili kutolewa bure, iwe inafaa na inayopatikana kwa urahisi. Isitoshe ,mtoto hastahili kupigwa, kudunishwa, wala kubaguliwa kwa namna yoyote ile: iwe kitabaka, kirangi,kijinsia au vinginevyo.Mtoto hapaswi kufanya kazi za kitumwa, nzito na za kushurutishwa. Vile vile ,mtoto anastahili kushirikishwa katika kufanya maamuzi yanayoweza kumwathiri maishani. Pia mtotoana haki ya kupata huduma za afya, mahitaji maalum na habari kuhusu masuala mbalimbali. Pamoja nahayo anastahili kupendwa na kuheshimiwa kimawazo na kihisia.Haki za watoto zinatakiwa kulindwa na kila mwanajamii, serikali na wazazi wakiwa katika mstari wambele. Hii ndiyo sababu serikali za mataifa mengi zimeshirikisha haki hizi katika katiba na sheria zanchi husika.Yeyote anayezikiuka anapasa kuadhibiwa kwa mujibu wa sheria .Walakini , haki hizi badozinakiukwa. Watoto wengi kote duniani bado wananyimwa haki zao. Kuna watoto ambao hawajawahihata kupata kibanda cha kuweka ubavu. Wengi wa hawa wamejipata wakiselela kwenye mitaa na hatamajaa ya mji na vijiji ambako hulazimika kupitisha usiku hata katika majira ya kipupwe na masika!Wengine hawapati chakula: licha ya kuwa wanatakiwa kupata chakula chenye lishe bora. Kwaokutarajia mlo awamu tatu kwa siku ni njozi: kwani hata awamu moja ni adimu kupata! La kusitikisha nikwamba wale wanaotarajiwa kuwa vigogo wa kuzilinda haki hizi ndio wanaoongoza katika kupaliliaukiukaji wazo. Kila siku tunasikia na kushuhudia visa vya watoto kupigwa, kushinikizwa kufanya kaziza sulubu kipunda, kunyanyaswa kinjinsia, kuishi katika mazingira hatari na hata kuuawa. Baadhi yawanaohusika na vitendo hivi hasi huwa wazazi au jamaa wa karibu kama vile mjomba, shangazi auwahudumu wa nyumbani.Madhila yanayowapata watoto hayatokei tu katika mazingira ya nyumbani. Mateso huvuka mipaka nakufikia ngazi ya kimataifa. Watoto wengi katika mataifa yenye fujo na ghasia hutekwa na kutumikishwavitani. Linalokata maini ni kwamba baadhi ya viongozi katika mataifa haya hawafanyi lolotekuwanusuru. Lao huwa kuwatazama watoto wanaotakiwa kuwalinda wakigeuzwa kuwa mababe wakuua na kuuana.Watoto hawa huvishwa magwanda ambayo miili yao minyonge haiwezi kuyahimili. Piahulazimika kuvaa mabuti ya kijeshi ambayo huwa nanga kwao kubeba, licha ya bunduki zinazokaribiakuwazidi uzani.Mojawapo ya mambo ambayo viongozi nchini humu walilenga shabaha kuyafikia baada ya kijinyakuliauhuru ni elimu kwa wote. Hata hivyo, hii imekuwa kama ndoto isiyotabirika katika baadhi ya janibu. Nikweli kwamba sera ya elimu bila malipo katika shule za msingi nchini humu inaendelea kutekelezwa.Hata hivyo, asilimia ya watoto na hata watu wazima wasiojua kusoma na kuandika ingali kubwa.Jukwaa la vijiji nchini humu na hata katika mataifa mengine ya ulimwengu wa tatu limesheheni idadikubwa ya watoto wasioenda shuleni. Kichocheo kikuu cha hali hii ni kwamba wazazi na waleziwamejipata katika lindi la ufukara uliokithiri. Hata wanapojitahidi kujinyanyua na kujikuna wapatapoPage 2 of 15https://elimuspace.co.ke/- 0705738367 MECS 2020

kuyakidhi mahitaji ya kielimu ya wanao, wao hujipata wakitapatapa katika kinamasi hicho hicho chaulitima. Matokeo ni kwamba watoto wa matajiri wanaendelea kuelimika huku wa maskini wakibakiakwenye kiza cha ujinga. Wanaong’ang’ania kuwepo kwa elimu bila malipo ni kama kwamba niwaota ndoto za mchana.Hali ilivyo sasa hivi inadai kuwa mimi na wewe ttufanye hima tuungane mikono na kutafuta suluhishola kudumu kuhusu utekelezaji wa haki za watoto. Twapaswa kuhimiza serikali zetu kufanya kilaziwezavyo kuhakikisha kuwa watoto wote wako shuleni. Nasi tushirikiane kutoa huduma kwa watoto nakukomesha dhuluma , mateso na dhiki kwao. Haitoshi kupeleka miswada bungeni kuhusu haki zawatoto na kuipitisha kuwa sheria. Twastahili kubadilisha misimamo yetu kuhusu haki hizi na kuzilindakwa dhati.(a) Huku ukitoa mifano minne, eleza hali ya kinyume inayojitokeza katika aya ya pili.(alama 4) (b) Eleza namna hali ya usalama inavyoathiri utekelezaji wa haki za watoto kwa mujibu wa kifungu.(alama 3)Page 3 of 15https://elimuspace.co.ke/- 0705738367 MECS 2020

(c) Kwa kurejelea aya ya nne , onyesha mchango wa serikali katika kuwajibikia haki za watoto.(alama 3) (d) “Wanaong‟ang‟ania kuwepo kwa elimu bila malipo ni kana kwamba ni waota ndoto mchana.”Thibitisha kauli hii kwa kurejelea kifungu.(alama 2) (e) Eleza maana ya msamiati ufuatayo kama ulivyotumika katika taarifa.(alama 3)(i)Vigogo (ii)Huwa nanga kwao (iii)Kujikuna wajipatapo 2. MUHTASARI (Alama 15)Page 4 of 15https://elimuspace.co.ke/- 0705738367 MECS 2020

Jamii ya leo inatawaliwa na kuendeshwa na kanuni ya maarifa. Inawezekana kusema kuwauchumi wa jamii za leo na zijazo utategemea maarifa zaidi kuliko utakavyotegemea wenzowowote mwingine. Utambuzi wa uwezo mkubwa wa maarifa katika maisha ya binadamu ndiomsingi wa watu kusema „maarifa ni wezowa:kuyadhibiti,kuyaendesha,kuyatawala na kuyaongoza maisha ya binadamu popote pale walipo.Mtu ambaye ameyakosa maarifa Fulani huwa ameikosa nguvu hiyo muhimu na maisha yakehuadhirika pakubwa. Kwa msingi huu, maarifa yanaweza kuangaliwa kama utajiri mkubwaambao binadamu anaweza kuutumia kwa faida yake au kwa faida ya wanajamii wenzake.Ukweli huu ndio unaoelezwana methali ya Kiswahili: „Elimu ni mali.‟ Elimu ni chimbuko lamaarifa muhimu maishani.Msingi wa utajiri na maendeleo ya binadamu popote alipo basi ni maarifa. Je, maarifakwa upande wake yana sifa gani? Maarifa yenyewe hayana upizani. Maarifa uliyo nayo huwezakuwa na watuwengine wengi pasiwe na upizani baina yenu kwa kuwa kila mmoja ana maarifasawa.kila mmoja ana uhuru wa kuyatumia maarifa hayo kama chanzo cha kuyazalisha maarifamengine. Utumiaji wa maarifa yenyewe hauyamalizi maarifa hayo. Maarifa hayawezi kugusikaingawa mtu anaweza kuyanyumbua maarifa yenyewe kwa kuyatumia kwa namna tofauti.Maarifa huingiliana na maarifa mengine. Maarifa aliyo nayo mtu mmoja huwezakuhusishwa na maarifa aliyo nayo mtu mwingine ili kuvyaza au kuzuka na maarifa tofauti.Maarifa yanaweza kuchukuliwa kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa namna ambavyo mtuhawezi kufanya bidhaa nyingine ile. Kwa mfano, ni muhali mtu kulalamika kuwa hawezikutembea kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa sababu ana mzigo mzito wa maarifa kichwaniSifa nyingine muhimu ya maarifa ni kuwa yanaweza kuwasilishwa kwa njia ya ishara aumitindo mingine ya kidhahania. Ikiwa unataka kukihamisha chombo Fulani kutoka sehemu mojahadi nyingine, lazima uwazie ukubwa wake, uzito wake na labda hata umbali wa panapohusika.Maarifa huweza kubadilishwa au kugeuzwa na kuwa ishara ambazo huyafanya kuwasilishwakwa njia nyepesi kuliko kwa mfano ikiwa mtu atayawasilisha katika muundo wa, kwa mfanokitabu.Maarifa yana sifa ya uhusianaji. Kipengele Fulani cha maarifa huwa na maanakinapowekwa sambamba au kugotanishwa na kipengele kingine cha maarifa. Huo huwamuktadha mzuri wa kueleweka au kuwa na maana. Kwa mfano , neno „mwerevu „huweza kuwana maana kwa kuweka katika muktadha wa „mjinga‟, „mjanja‟, „hodari‟, na kadhalika.Maarifa huweza kuhifadhiwa katika nafasi ndogo sana. Suala hili linaeleweka kwa njianyepesi tunapoangalia maarifa katika muktadha wa teknologia. Data zinazowahusu mamilioni yaPage 5 of 15https://elimuspace.co.ke/- 0705738367 MECS 2020

watu, ambazo zingehitaji maelfu ya maktaba na lukuki ya vitabu, huweza kuhifadhiwa kwenyekifaa kidogo kianachoweza kutiwa mfukoni.Maarifa hayawezi kudhibitiwa au kuzuiliwa mahali Fulani yasisambae. Maarifa hueneaharaka sana. Maarifa ni kitu kinachoepuka pingu za watu wanopenda kuwadhibiti binadamuwenzao. Hata pale ambapo mfumo wa kijamii au wa kisiasa unafanya juu chini kuwadhibiti raiaau watu wenyewe, ni muhali kuyadhibiti maarifa yenyewe. Inawezekana kuzidhibiti njia Fulaniza ueneaji wa maarifa lakini maarifa hayo yatapata upenyu wa kusambaa. Ni kweli kuwa maarifani nguvu inayozishinda nguvu zote.(a) Fupisha aya ya pili na ya tatu. (maneno 55-60)(alama 5, 1 ya utiririko)Matayarisho .Nakala safiPage 6 of 15https://elimuspace.co.ke/- 0705738367 MECS 2020

(b) Eleza sifa kuu za maarifa kama zinavyojitokeza kuanzia aya ya nne hadi aya ya nane.(maneno 100-110)(alama 10, 2 za utirriko)Matayarisho Page 7 of 15https://elimuspace.co.ke/- 0705738367 MECS 2020

.Nakala safi 3. MATUMIZI YA LUGHA(a) Tofautisha sauti zifuatazo.(i)/t/(ALAMA 40)(alama 2)/s/Page 8 of 15https://elimuspace.co.ke/- 0705738367 MECS 2020

(ii)/h//gh/ (iii)/o//u/ (iv)/b//a/ (b) (i) Mzizi ni nini?(alama 1) (ii) Toa mfano wa kitenzi chenye mzizi huru.(alama 1) (c) Tunga sentensi yenye muundo ufuatao:(alama 2)N RH t EPage 9 of 15https://elimuspace.co.ke/- 0705738367 MECS 2020

(d) Ainisha mofimu katika neno lifuatalo:(alama 2)Kiokoteni (e) Andika katika ukubwa.(alama 1)Paka hawa wamemfukuza mbwa wetu. (f) Taja matumizi mawili ya kiambishi /e/(alama2) (g) Andika upya ukifuata maagizo.(alama 3)(i) Maji ambayo wanakunywa ni hatari. (Andika katika hali ya mazoea bila kutumia amba) (ii) Watu wengi walihasirika bomu lilipolipuka katika jengo hilo. (Tumia nomino badala yavitenzi vilivyopigwa mstari.)Page 10 of 15https://elimuspace.co.ke/- 0705738367 MECS 2020

(iii) Pombe hiyo ilimfanya kuwa kipofu. (Tumia kitenzi badala ya neno lililopigiwa mstari) (h) Tunga sentensi ukitumia kishazi tegemezi kinachofanya kazi ya kielezi.(alama 2) (i) Bainisha aina ya vitenzi katika sentensi ifuatayo.(alama 3)Wao si wahalifu ingawa walikuwa msituni walipokamatwa. (j) Tunga sentensi ukitumia nomino waya pamoja na kivumishi cha pekee cha kusisitiza. (alama 2) (k) Andika katika usemi halisi.(alama 2)Hamisi alimwambia nyanya yake kuwa siku hiyo hakuwa na nafasi lakini angemtembelea sikuambayo ingefuata.Page 11 of 15https://elimuspace.co.ke/- 0705738367 MECS 2020

(l) Changanua kwa jedwali. (alama 2)Mwenye njaa hana miiko. (m) Taja matumizi mawili ya parandesi.(alama 2) (n) Ainisha sentensi ifuatayo kwa kuzingatia jukumu / dhamira yake.(alama 1)Rais amepiga marufuku ukataji miti nchini. (o) Andika katika umoja.(alama1)Hao wameharibu nyua zilizotengenezwa kwa mbao. (p) Andika katika wakati uliopita hali timilifu(alama 1)Miti katika msitu huo inakauka.Page 12 of 15https://elimuspace.co.ke/- 0705738367 MECS 2020

(q) Andika upya ukitumia visawe vya maneno yaliyopigiwa mstari.(alama 2)Nyanya alisomba taka na kuitia katika jaa lililo shambani. (r) Huku ukitoa mifano mwafaka taja miundo miwili ya nomino katika ngeli ya U/I (alama 2) (s) Tunga sentensi ukitumia na kama:(i)(alama 2)Kihusishi (ii)Kuonyesha umilikaji (t) Onyesha kiima, shamirisho na chagizo katika sentensi ifuatayo.(alama 3)Polisi ambao walikuja juzi waliwakamata majambazi wote jana jioni.Page 13 of 15https://elimuspace.co.ke/- 0705738367 MECS 2020

(u) Tunga sentensi mbili kuonyesha maana mbili za neno muhali.(alama 2) (v) Andika methali inayoafiki maelezo yafuatayo .Ni afadhali kupata matatizo madogo kwa sasa ili kuyaepuka mengi baadaye. ISIMU JAMII(ALAMA 10)(a) Eleza kwa ufupi jinsi mambo yafuatayo yanavyodhibiti mitindo ya lughaPage 14 of 15https://elimuspace.co.ke/- 0705738367 MECS 2020

(i)Mazingira(alama 2) (ii)Mada(alama 3) (iii)Hali(alama 2) (b) Fafanua sera tatu ambazo zimepitishwa na serikali zinazochangia kuimarika kwa lugha yaKiswahili.(alama 3) Page 15 of 15https://elimuspace.co.ke/- 0705738367 MECS 2020

MTIHANI WA PAMOJA -MECS 2021 Jina: _ Nambari ya mtahiniwa:_Darasa: _ Tarehe: _ Sahihi: _ 102/2 Kiswahili Karatasi ya 2 Muhula wa Pili - 2021 Muda: Saa 2½ . kweli kwamba sera ya elimu bila malipo katika shule za msingi nchini humu inaendelea kutekelezwa. Hata hivyo, asilimia ya watoto na hata watu wazima wasiojua kusoma na .

Related Documents:

MTIHANI WA PAMOJA WA SHULE ZA EKSIKA Hati ya kuhitimu kisomo cha sekondari Kenya(K.C.S.E) MAAGIZO: a) Jibu maswali yote. b) Andika majibu yote katika nafasi zilizoachwa. c) Karatasi hii ina alama 30. d) Hakikisha kurasa zote zimepigwa chapa. Swali Upeo Alama Ufahamu 15 Ufupisho 15 Lugha 40 Isimu Jamii 10 Jumla 80

MTIHANI WA PAMOJA WA SHULE ZA UPILI WILAYANI MAKINDU, 2014 Kenya Certificate of Secondary Education (K.C.S.E) MAAGIZO KWA MTAHINIWA . Urafiki wa namna hii ndio uletao baraka ya Mungu, kuwashukia viumbe hao kama umande wa asubuhi. Urafiki ni lazima sana katika maisha ya wanadamu. Urafiki ni mfano wa mishipa ipitishayo damu

JARIBIO LA TATHMINI YA PAMOJA MTIHANI WA CEKENAS MUHULA WA PILI MWAKA 2015 Hati ya Kuhitimu Elimu ya Sekondari KISWAHILI INSHA KARATASI YA KWANZA MUDA: SAA 1 ¾ MAAGIZO 1. Andika insha mbili. 2. Insha ya kwanza ni ya lazima. 3. Chagua insha nyingine moja kutoka hizo tatu zilizosalia. 4. Kila insha isipungue maneno 400 5. Kila insha ina alama 20.

Dr. Joseph Brink developed the rst ber bed mist eliminator for chemical and acid plant use in 1958. MECS, Inc. (MECS) continues to be the leader in mist elimination products which utilize the latest technology. MECS welcomes the opportunity to investigate and recommend solutions to any air pollution or down stream corrosion problem in your

2015 Mtihani wa Tathmini eneo la Bondo 102/1 Insha Fungua ukurasa 102/1 KISWAHILI Karatasi ya 1 Julai/Agosti - 2015 MUDA: SAA 1 ¾ MTIHANI WA KUTATHIMINI WILAYA YA BONDO - 2015 . Ardhi ndiyo chanzo cha riziki zote. Fauka ya hayo, ardhi ni dafina kubwa. . Fupisha aya ya kwanza kwa maneno 50.

4.0 KISWAHILI (102) 4.1 MATOKEO YA MTIHANI WA SOMO LA KISWAHILI Jedwali hili linaonyesha matokeo ya mtihani wa somo la Kiswahili katika muda wa miaka minne (2005 hadi 2008). Jedwali 6: Matokeo ya mtihani wa Kiswahili (2005 - 2008) Mwaka Karatasi Watahiniwa Alama ya Juu Alama ya Wastani Alama ya Tanganisho 2005 1 2 3 Jumla 259,301 40 80

3825-34, Chrysler 3 Adapter 3825-12, Ford EEC Adapter 3825-16, Ford ABS Adapter 3421-93, Kia Adapter 3825-11, MECS ABS Adapter 3825-13, Geo-Isuzu Adapter 3825-14, Mazda MECS Adapter 3825-15, Universal 9 Pin Adapter 3825-17, Toyota DCL 1/ Adapter 3825-18, Toyota DCL 2/ Adapter 3825-19, Mitsubishi/ Chrysler “Y” Adpater 3825-20, Nissan 1 Adapter

kidney (normal, mini or ultra-mini) we pass the telescope (nephroscope) through a sheath, along the track, to see the stone(s) inside the kidney (pictured). the stones are broken up using a laser, a lithoclast or an ultrasound probe and the larger fragments are removed using grasping forceps or suction when smaller nephroscopes (mini or ultra-mini) are used, the stones are .