MWONGOZO WA MKUFUNZI WA MFUMO WA UJIFUNZAJI

2y ago
645 Views
24 Downloads
916.46 KB
13 Pages
Last View : 2d ago
Last Download : 1m ago
Upload by : Callan Shouse
Transcription

CHUO CHA SERIKALI ZA MITAAMWONGOZO WA MKUFUNZI WAMFUMO WA UJIFUNZAJI WA KIELETRONIKI (MUKI)Agosti 2019Mwongozo huu wa Mkufunzi umetayarishwa kwa ushirikiano baina ya Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali zaMitaa (OR-TAMISEMI), Chuo cha Serikali za Mitaa Dodoma, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na Mradi wa UimarishajiMifumo ya Sekta za Umma (PS3) unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID), uliopo Dares Salaam, Tanzania Chini ya mkataba AID-621-C-15-00003

USAID/Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma Tanzania (PS3)Lengo kuu la Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) kupitia ufadhili wa Shirika la Maendeleo yaKimataifa la Marekani (USAID), ni kusaidia Serikali ya Tanzania katika uimarishaji wa mifumo ya umma ili kufanikishautoaji wa huduma bora na hasa kwa wananchi walioko maeneo ya pembezoni. PS3 inaongozwa na kampuni ya AbtAssociates kwa ushirikiano na Benjamin William Mkapa Foundation (BMF), Broad Branch Associates, IntraHealthInternational, Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo (LGTI), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Urban Institutena Tanzania Mentors Association (TMA)Agosti 2019Namba ya Mkataba: AID-621-C-15-00003Mwongozo Wa Mkufunzi Wa Mfumo Wa Ujifunzaji Wa Kieletroniki (MUKI) Agosti, 2019.KANUSHOChuo cha Serikali za Mitaa (Hombolo) ndicho kitawajibika na matokeo ya kazi hii. Mwongozo Wa Mkufunzi WaMfumo Wa Ujifunzaji Wa Kieletroniki (MUKI) ni maoni ya Chuo cha Serikali za Mitaa (Hombolo), na si lazimakiwakilishe maoni ya Serikali ya Marekani au USAID.i

MWONGOZO WA MKUFUNZI WAMFUMO WA UJIFUNZAJI WA KIELETRONIKI (MUKI) Chuo cha Serikali za Mitaa, 2019Toleo la Kwanza (Elimu Masafa), Agosti 2019. Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kuiga, kunakili au kutoakwa njia yoyote ile bila idhini ya maandishi ya Chuo cha Serikali za Mitaaii

YALIYOMOYaliyomo . 11.utangulizi . 22.Mahitaji Muhimu Katika Kutumia Mfumo . 23.Jinsi ya Kuingia Kwenye Mfumo . 24.Muhtasari wa Mfumo. 35.Kutoka Nje ya Mfumo . 46.Jinsi ya Kuendesha Mafunzo. 56.1.6.2.6.3.6.4.6.5.Kufikia kozi . 5Mwonekano wa Kozi . 5Kuhariri Mipangilio ya Kozi . 6Kuingiza na kuhariri Maudhui . 6Uwezeshaji wa kozi . 7Orodha ya Jedwali na MichoroKielelezo 1: Ukurasa wa mwanzo . 3Kielelezo 2: Menyu ya kuhakiki wasifu . 3Kielelezo 3: Menyu ya awali . 4Kielelezo 4: Menyu ya miongozo na msaada . 4Kielelezo 5: Orodha ya kozi . 5Kielelezo 6: Safu za mwonekano wa kozi . 5Kielelezo 7: Menyu ya mipangilio ya kozi. 6Kielelezo 8: Kitufe cha kuweka rasilimali za ujifunzaji . 6Kielelezo 9: Orodha ya rasilimali ujifunzaji . 7Kielelezo 10: Mwonekano wa uwekaji jukwaa la mjadala . 7Kielelezo 11: Mwonekano wa uwekaji kazi . 8Kielelezo 12: Menyu yenye kitufe cha washiriki . 8Kielelezo 13: Menyu ya washiriki . 9Kielelezo 14: Menyu ya kuandikisha watumishi. 91

1. UTANGULIZIMfumo wa Ujifunzaji Kielektroniki (MUKI) umetengenezwa maalumu kwa ajili ya kijifunzia nakufundishia. Kila mtumishi mpya anapaswa kujiunga na mfumo huu na kushiriki katika mafunzo ya awaliili kukidhi vigezo vya ajira katika utumishi wa umma. Mwongozo huu unalenga kumpatia mkufunzimaelekezo ya jinsi ya kutumia mfumo huu kwa kufundishia.2. MAHITAJI MUHIMU KATIKA KUTUMIA MFUMOIli kuweza kutumia mfumo wa MUKI unahitaji kuwa na baadhi ya vifaa, vivinjari, na programukama zilivyoainishwa hapo chini.Mfumo unaweza kupatikana kwa kutumia moja ya vifaa vifuatavyoa) Kompyuta ya mezani/mpakatob) Tabiti (tablet)c) Simu janja (smartphone)Kabla ya kuingia kwenye MUKI, utahitji kuhakikisha kwamba una moja kati ya vivinjarivilivyopendekezwa.a) Google Chromeb) Firefoxc) Internet explorerd) Microsoft EdgeIli kutazama baadhi ya mafaili, media au vitu vingine vinavyoweza kupatikana katika mfumohuu, utahitaji programu zifuatazo:a)b)c)d)Adobe FlashMicrosoft OfficeWindows Media PlayerAdobe Reader3. JINSI YA KUINGIA KWENYE MFUMOMfumo wa MUKI unapatikana katika anuani http://muki.lgti.ac.tz. Ili uweze kuingia katikamfumo andika anuani hiyo katika eneo la anuani kwenye kivinjari chako, kwenye ukurasautakaofunguka andika jina la mtumiaji (username) pamoja na nywila (password) yako kamainavyoonekana kwenye kielelezo namba 1.2

Kielelezo 1: Ukurasa wa mwanzo4. MUHTASARI WA MFUMOBaada ya kufanikiwa kuingia katika mfumo wa MUKI ukurasa wa kwanza utaweza kufanya mamboyafuatayo.a) Kubadili nywila (password)Unashauriwa kubadili nywila (password) kwa sababu za kiusalama.b) Hakiki/hariri taarifa binafsi. Katika kona ya juu Zaidi ya kulia bofya kwenye jina lako, kishamenyu ya wasifu itafunguka. katika eneo linaloonekana kwenye kielelezo namba 2.Kielelezo 2: Menyu ya kuhakiki wasifuc) Upande wa kushoto wa ukurasa wa mwanzo utaona orodha yenye vipengee mbalimbalikama inavyoonekana kwenye kielelezo namba 3.3

Dashibodi: Huu ni Huu ni ukurasa unaoonesha taarifa za kozi ambazomwanafunzi amesajiliwa. Kalenda: Inaonesha tarehe za matukio mbalimbali yanayohusiana na kozi.Mfano tarehe ya mwisho ya kuwasilisha kazi/zoezi. Mafaili binafsi: Inaonesha orodha ya mafaili binafsi ya binafsi. Kozi zangu: Inaonesha orodha ya kozi ambazo mwanafunzi amesajiliwa.Kielelezo 3: Menyu ya awalid) Katika ukurasa wa mwanzo utaona menyu yenye maelezo kama inavyoonekana katikakielelezo namba 4.Kielelezo 4: Menyu ya miongozo na msaada Miongozo: utakutana na miongozo mbalimbali ya namna ya kutumia mfumo wa MUKI. Chaguamuongozo kulingana na kozi unayoshiriki. Msaada: kitakuwezesha kusoma waraka wenye maelekezo ya mfumo au kuangalia video inayooneshanamna ya kutumia mfumo. Dawati la msaada: kitakuwezesha kuwasiliana na mwalimu au afisa TEHAMA ikiwa utahitaji msaadaunaohusiana na kozi yako au matumizi ya mfumo. Kiswahili (sw)/English (en): kitakuwezesha kubadilisha lugha kutoka kwenye Kiswahili kwenda lugha yaKielelezo 1: Menyu ya miongozo na msaadaKiingereza.5. KUTOKA NJE YA MFUMOUnashauriwa kutoka nje ya mfumo baada ya kumaliza kutumia mfumo. Kutoka nje ya mfumo bofya“toka nje ya mfumo” kama inavyoonekana kwenye kielelezo namba 2.4

6. JINSI YA KUENDESHA MAFUNZOIli kushiriki mafunzo ni lazima mkufunzi awe awe amesajiliwa katika mfumo na kozi husika.6.1. Kufikia koziIli kufikia maudhui ya kozi husika, bofya kitufe chanye msimbo wa kozi (course code) husika kamainavyoonekana kwenye kielelezo namba 5.Chagua kozihusikaKielelezo 5: Orodha ya kozi6.2. Mwonekano wa KoziKozi yako katika MUKI itaonekana katika mtazamo wa safu tatu (3), kama inavyoonekana kwenyekielelezo namba 6.Safu yakushotoSafu yakatikatiSafu yakuliaKielelezo 6: Safu za mwonekano wa kozia) Safu ya kushoto: hii inaonesha washirika, alama, na mtiririko wa mada.b) Safu ya katikati: ni mahali ambapo pamebeba maudhui ya kozi mfano matini ya mada, soga,mjadala, na kazi mbalimbali za kujipima.c) Safu ya kulia: ni mahali ambapo matangazo na matukio yanayoendelea yanapatikana.5

6.3. Kuhariri Mipangilio ya KoziMkufunzi amepewa idhini ya kubadili mipangilio ya kozi pale inapobidi, mfano kubadili jina la kozi,msimbo (course code), tarehe ya kuanza na kumaliza kozi. Ili kuhariri mipangilio ya kozi, mkufunzianapaswa kubofya ikoni ya mipangilio, kisha achague na kubofya kipengee cha “Hariri Mpangilio”kama inavyoonekana kwenye kielezo namba 7.Ikoni yamipangilioHaririmpangiliouhaririKielelezo 7: Menyu ya mipangilio ya kozi6.4. Kuingiza na kuhariri MaudhuiNi wajibu wa mkufunzi kuhakikisha maudhui ya kozi yameandaliwa na yamehaririwa kikamilifu nakuingizwa kwenye mfumo. Ili kuingiza maudhui kwenye mfumo, mkufunzi anapaswa kubofya ikoni yamipangilio, kisha achague na kubofya kipengee cha “Ruhusu uhariri” kama inavyoonekana kwenyekielezo namba 7.Kuingiza Rasilimali za UjifunzajiMkufunzi atapaswa kuingiza rasilimali za kujifunzia, ili kumwezesha mwanafunzi kujifunza kupitia ainambalimbali za rasilimali. Rasilimali hizi ni kama zifuatazo; kurasa, faili, foda, kazi, zoezi, wavuti, tathmini,soga, jukwaa la mjadala, wiki, na faharasa. Ili kuingiza rasilimali za kujifunzia mkufunzi atabofya kitufecha “Weka kazi au rasilimali ujifunzaji”, kisha chagua na weka rasilimali inayofaa kwa wakati huo kamainavyoonekana kwenye kielelezo namba 8 na namba 9.Bofya hapa kuwekarasilimali ujifunzajiKielelezo 8: Kitufe cha kuweka rasilimali za ujifunzaji6

Chagua rasilimaliujifunzajiBofya wekakuingizarasilimali husikaKielelezo 9: Orodha ya rasilimali ujifunzaji6.5. Uwezeshaji wa koziMkufunzi anawajibika kuwaongoza watumishi wapya katika kozi ili kuhakikisha wanapata uelewakulingana na mahitaji ya kozi. Majukumu ya mkufunzi yamegawanyika katika sehemu zifuatazo.Kuwezesha mijadalaIli kuboresha ufundishaji kwa njia ya masafa, mkufunzi atatakiwa kuanzisha mijadala na kuchocheaushiriki wa watumishi wapya katika kuchangia mada husika. Ili kuanzisha mjadala mkufunzi atabofyakitufe cha “Jukwaa la mjadala” kama inavyoonekana kwenye kielelezo namba 9, kisha atabofyakitufe cha “Weka”. Mkufunzi atapaswa kuandika jina la mjadala huo na kuweka maelezo/mada yamjadala kama inavyoonekana kwenye kielelzo namba 10.Kielelezo 10: Mwonekano wa uwekaji jukwaa la mjadalaKutunga, kusahihisha na kutoa alama kwa kazi na mazoezi mbalimbaliMkufunzi anawajibu wa kuandaa maswali ya kupima uelewa pamoja na kutoa alama kwa watumishikatika kozi husika. Pia, mkufunzi anapaswa kutoa mrejesho wa alama kulingana na uelewa wa watumishi.7

Ili kuandaa kazi na zoezi mkufunzi atapaswa kubofya kitufe cha “Kazi” kuweka kazi (assignment) nakitufe cha “Zoezi” kuweka zoezi (quiz) kama inavyoonekana kwenye kielelezo namba 9, kisha atabofyakitufe cha “Weka”. Mkufunzi atapaswa kuandika jina la kazi hiyo na kuweka maelezo/swali la kazi kamainavyoonekana kwenye kielelezo namba 11.Jina la kaziSwali/maelezoKielelezo 11: Mwonekano wa uwekaji kaziKusajili WatumishiMkufunzi anaweza kumsajili mtumishi mpya kwenye kozi husika kwa kubofya kitufe cha “Washiriki”kama inavyoonekana kwenye kielelezo namba 12, kisha kubofya kitufe cha “Andikishawatumiaji” kama inavyoonekana kwenye kielelezo namba 13, andika jina la mtumishi na bofyakitufe cha “Andikisha mtumiaji” kama inavyoonekana kwenye kielelezo namba 14. Mtumishianayeweza kusajiliwa kwenye kozi ni yule ambaye amekwishasajiliwa kwenye mfumo.Kielelezo 12: Menyu yenye kitufe cha washiriki8

Kielelezo 13: Menyu ya washirikiKielelezo 14: Menyu ya kuandikisha watumishi9

MWONGOZO WA MKUFUNZI WAMFUMO WA UJIFUNZAJI WA KIELETRONIKI(MUKI)10

Namba ya Mkataba: AID-621-C-15-00003 Mwongozo Wa Mkufunzi Wa Mfumo Wa Ujifunzaji Wa Kieletroniki (MUKI) Agosti, 2019. KANUSHO Chuo cha Serikali za Mitaa (Hombolo) ndicho kitawajibika na matokeo ya kazi hii. Mwongozo Wa Mkufunzi Wa Mfumo Wa Ujifunzaji Wa Kieletroniki (MUKI) ni maoni ya

Related Documents:

Amemaliza elimu ya sekondari Mtoa huduma ya afya Awe ana ari ya kujifunza KUENDEDSHA MAFUNZO Mafunzo haya yataendeshwa kwa siku 4; kila siku muda wa saa 8. Kila siku asubuhi kutakuwa na muhtasari wa masomo yaliyofundishwa siku iliyotangulia. Mkufunzi ataeleza malengo ya

Sehemu ya 3: Hutoa mwongozo au maelekezo ya ufundishaji kwa kila dha-na iliyotolewa ndani ya kitabu . Ingawa mwongozo huu wa mwalimu una majibu kwa kila kazi zote zilizotolewa katika kitabu cha mwanafunzi, unaombwa kupitia kila swali na kazi kabla ya ku-tathmini matokeo ya utafiti.

sayansi na hapo mmjoa wa watafiti mashuhuri na mtetezi wa mbinu hii akiwa ni Nor-man Uphoff, profesa katika chuo kikuu cha Cornell huko Marekani. Kupitia juhudi zake na za wanasayansi wengine na hata wakulima walioshiriki kwa hiari yao, mfumo wa ‘SRI’ sasa umeweza kutumika k

i) Rais wa awamu ya saba wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni Dr. Ali Mohammed Shein. _ ii) Shehia inaundwa kwa kuunganishwa vijiji kumi. _ iii) Wimbo wa taifa huimbwa wakati bendera ya skuli inapopandishwa. _ iv) Mfumo wa chama kimoja cha siasa hauna gharama ukilinganisha na mfumo wa vyama vingi vya siasa.

FASIHI MWONGOZO WA KUSAHIHISHIA FASIHI TATHMINI YA PAMOJA MACHI/APRILI 2017 SEHEMU YA A: FASIHI SIMULIZI (a)i Utungo wa kishairi ambao hutungolewa kwa kutumia sauti iliyo kati ya uimbaji na uzungumzaji (kalima) 1 x 2 alama 2 (ii) Sifa za maghani (i) Yana muundo wa kishairi. (ii) Tamathali za semi hutumika kwa wingi.

Ms. Fika Mwakabungu - Mkurugenzi Idara ya Mafunzo na Mitaala . kuwasiliana kwa lugha ya Kiswahili, Utambuzi, Kuhusiana, Kujenga Mwili na Kuthamini Mazingira. Aidha mwongozo huu unatoa maelekezo ya kutumia . Kufanya upimaji na tathmini ya maendeleo ya watoto kwa kutumia mbinu zilizopendekezwa katika mwongozo.

Sheria ya Elimu Na. 25 ya mwaka 1978 na Rekebisho Na. 10 la mwaka 1995 ikisomwa pamoja na Waraka wa Elimu Na. 4 wa mwaka 2016 unaohusu mwongozo wa uundaji wa Kamati ya Shule. Ibara ya 3 kifungu cha 39 cha Sheria ya Elimu Na. 25 ya mwaka 1978, inazitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa kuunda Kamati ya

2. IDC, “Emerging Tech and Modern IT: The Key to Unlocking your Data Capital,” 2018 – Document #US44402518 3. Based on ESG Research Insight Paper commissioned by Dell EMC and Intel, “How Organizations Unlock Their Data Capital with Artificial Intelligence” November 2019. Results based on a survey of 750 global IT decision makers.