JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA

2y ago
335 Views
10 Downloads
899.46 KB
36 Pages
Last View : 10d ago
Last Download : 3m ago
Upload by : Angela Sonnier
Transcription

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAWIZARA YA ELIMU,SAYANSI NA TEKNOLOJIABARAZA LA MITIHANI LA TANZANIAFOMATI YA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGIIMETOLEWA NA:BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIAS.L.P 2624DAR ES SALAAMTANZANIAImerekebishwaJULAI, 2020

FOMATI YA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGIIMETOLEWA NA:BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIAS.L.P 2624DAR ES SALAAMTANZANIAImerekebishwaJULAI, 2020

Imechapishwa na:Baraza la Mitihani la Tanzania,S.L.P. 2624,Dar es Salaam. Baraza la Mitihani la Tanzania, 2020Haki zote zimehifadhiwa.

YALIYOMODIBAJI . iii01 KISWAHILI . 102 ENGLISH LANGUAGE . 403 MAARIFA YA JAMII NA STADI ZA KAZI . 704 HISABATI . 1005 SAYANSI NA TEKNOLOJIA . 1306 URAIA NA MAADILI . 16VIAMBATANISHO (FOMU ZA OMR) . 19ii

DIBAJIKitabu cha fomati ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi kimeandaliwa na Baraza laMitihani la Tanzania kwa kuzingatia matakwa ya Mtaala wa Elimu ya Msingi wamwaka 2015. Fomati hii itaanza kutumika kwa watahiniwa wa Mtihani wa KumalizaElimu ya Msingi 2021.Mtaala mpya umebainisha masomo ya lazima yatakayofundishwa Darasa la III hadi laVII. Masomo hayo ni Kiswahili, English Language, Hisabati, Sayansi naTeknolojia, Uraia na Maadili, Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi.Mabadiliko katika mtaala, yalisababisha maboresho ya mihtasari ya masomo yaDarasa la III hadi la VII. Hivyo, Baraza la Mitihani litapima masomo sita (6) ambayo niKiswahili, English Language, Hisabati, Sayansi na Teknolojia, Uraia na Maadilina Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi.Hata hivyo, katika fomati hii hakuna mabadiliko yaliyofanyika katika muundo wamtihani wa masomo yote yanayotahiniwa katika ngazi hii ya elimu. Muundo wa Mtihaniwa Kumaliza Elimu ya Msingi utaendelea kuwa na maswali 40 ya kuchagua jibu sahihina yataendelea kujibiwa katika fomu za Optical Mark Reader (OMR). Aidha, maswalimatano (5) yatajibiwa upande wa pili wa fomu ya OMR (Tafadhali ona Viambatanisho).Fomati hii imeandaliwa kwa kufuata muundo wa aya tano ambazo ni Utangulizi,Malengo ya Jumla, Ujuzi wa Jumla, Muundo wa Mtihani na Umahiri utakaopimwa kwakila somo. Aidha, Jedwali la utahini limewekwa mwishoni mwa fomati ya kila somo nalinaonesha mahiri zitakazopimwa, nyanja za utambuzi, idadi ya maswali na asilimia yauzito kwa kila mahiri.Kwa ujumla, fomati inatoa mwongozo kwa watunzi wa mitihani, warekebishaji wamaswali ya mtihani na walimu katika kuandaa mitihani inayozingatia haki, uhalali nayenye kuaminika. Baraza linasisitiza mahiri zote katika masomo yote yanayofundishwakatika ngazi ya elimu ya msingi zifundishwe kwa kuzingatia mihtasari ya masomohusika. Fomati hii ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi isitumike kama mbadalawa mihtasari.Baraza la Mitihani linatambua na kuthamini mchango wa wote walioshiriki katikakufanya maboresho ya kitabu hiki cha fomati.Dkt. Charles E. MsondeKATIBU MTENDAJIiii

01 KISWAHILI1.0UTANGULIZIFomati ya Mtihani wa Kiswahili imeandaliwa kwa kuzingatia muhtasari wa somola Kiswahili wa mwaka 2016 ulioanza kutumika 2017. Muhtasari huo unabainishaUmahiri Mkuu na Umahiri Mahsusi. Hivyo, mtihani wa somo la Kiswahiliunalenga kupima utendaji wa mtahiniwa kutokana na umahiri aliokuwa naokuanzia Darasa la III hadi VII.2.0MALENGO YA JUMLAMtihani wa somo la Kiswahili utapima ni kwa kiwango gani mtahiniwa anaweza:2.1kusoma na kuandika kwa kutumia lugha ya Kiswahili;2.2kutumia Kiswahili fasaha katika miktadha mbalimbali;2.3kutumia Kiswahili kupata maarifa, stadi na mwelekeo wa kijamii,kiutamaduni, kiteknolojia na kitaaluma kutoka ndani na nje ya nchi;2.4kukuza stadi za mawasiliano ili kumwezesha mwanafunzi kumudu maishayake;2.5kujenga msingi bora na imara wa kujifunza kwa ajili ya elimu ya juu nakujiendeleza binafsi kwa kutumia lugha ya Kiswahili; na2.63.0kuifahamu na kuitumia lugha ya Taifa.UJUZI WA JUMLAMtihani utapima ujuzi na utendaji wa mtahiniwa katika:3.1kukuza stadi ya kusoma, kuandika na kuwasiliana;3.2kukuza uwezo wa mwanafunzi kufikiri, kubuni na kutatua matatizo;3.3kuifahamu na kuitumia Lugha ya Kiswahili;3.4kutathmini utamaduni wa Kitanzania na wa jamii nyingine; na3.5kujiandaa kwa ngazi nyingine ya elimu pamoja na kujifunza kusiko nakikomo.1

4.0MUUNDO WA MTIHANIMtihani wa somo la Kiswahili utafanyika kwa saa 1:40 kwa watahiniwa wenyeuoni na muda wa saa 1:55 kwa watahiniwa wasioona. Mtihani utakuwa nasehemu A, B na C zenye jumla ya maswali 45. Maswali ya sehemu A na B (1 –40) yatajibiwa katika fomu ya OMR kwa kutumia kalamu ya penseli ya HB. Aidha,kuanzia swali la 41 – 45 yatajibiwa katika fomu ya OMR kwa kutumia kalamu yawino wa bluu au mweusi. Mtahiniwa atatakiwa kujibu maswali yote yenye jumlaya alama 50.Sehemu A itakuwa na maswali 35 ya kuchagua jibu sahihi. Miongoni mwamaswali 35, matano (05) yatatokana na kifungu cha maneno/hadithiitakayosomwa na Msimamizi ambapo mtahiniwa atatakiwa kusikiliza kwa makinikisha kujibu maswali hayo. Kila swali litakuwa na alama moja (1) na kufanyajumla ya alama 35.Sehemu B itakuwa na maswali matano (5) ambapo mtahiniwa atapewa sentensitano (5) zilizochanganywa na atatakiwa kuzipanga katika mtiririko unaoletamaana au kukamilisha utungaji kwa kuchagua herufi inayowakilisha jibu sahihi.Kila swali litakuwa na alama moja (1) na kufanya jumla ya alama tano (5).Sehemu C itakuwa na maswali matano (5) ya majibu mafupi kutoka katikakifungu cha maneno habari, hadithi au shairi. Kila swali litakuwa na alama mbili(2) hivyo kufanya jumla ya alama 10.5.0 UMAHIRI UTAKAOTAHINIWAUmahiri utakaotahiniwa katika mtihani wa Kiswahili ni kama ifuatavyo:5.1Kuanzisha na kuendeleza mazungumzo katika miktadha mbalimbali.5.2Kutumia msamiati katika kuzungumza kwa kuwasilisha hoja kulingana namiktadha mbalimbali.5.3Kutumia maandishi katika mawasiliano kulingana na miktadha mbalimbali.5.4Kusikiliza na kuonesha uelewa wa jambo alilolisikiliza.5.5Kusoma kwa ufasaha na kuonesha uelewa wa matini ilishwa katika matini mbalimbali.2nakuchanganuamawazo

Kuanzisha na kuendelezamazungumzo katika kwakuwasilisha2.hoja kulingana na miktadhambalimbali.Kutumia maandishi katika3.mawasiliano kulingana namiktadha mbalimbali.Kusikiliza na kuonesha uelewa4.wa jambo alilolisikiliza.Kusoma kwa ufasaha na5.kuonesha uelewa wa anganua6.mawazoyaliyowasilishwakatika matini mbalimbali.Idadi ya Maswali1.Idadi ya hiri 7.0613.3715.5715.5817.7511.045Asilimia ya Uzito wa Maswali3Asilimia ya uzitokwa kila mahiriJedwali la Utahini Somo la 01 Kiswahili100

02 ENGLISH LANGUAGE1.0 INTRODUCTIONThis revised format is based on the 2016 version of the English LanguageSyllabus used in teaching standards III - VII with effect from 2017. The formathas been prepared to accommodate some improvements made in the syllabus,specifically the competence-based assessment. Thus, the English Languageexamination will assess the candidate’s competencies acquired from standard IIIto VII.2.0 GENERAL OBJECTIVESThe English Language examination aims to test the candidate’s ability to:2.1 express him/herself appropriately in a given situation;2.2 use basic skills in listening, reading, and writing in English;2.3 use vocabulary through listening, reading, and writing;2.4 apply correct English grammar; and2.5 use the English Language in acquiring higher education and for personaladvancement.3.0 GENERAL COMPETENCIESThe examination will measure the candidate’s competencies on how to:3.1 Comprehend oral and written information;3.2 communicate through writing; and3.3 use vocabulary through listening, reading and writing.4.0 EXAMINATION RUBRICThe examination will consist of one (1) paper of 1:40 hours. The paper forvisually-impaired candidates will last for 1:55 hours. The paper will comprisethree sections A, B and C with a total of 45 questions. Candidates will berequired to answer all the questions, weighing 50 marks. Candidates will berequired to provide their answers for sections A and B by shading the letter of thecorrect answer on the OMR forms using the HB pencil. However, for section C,4

candidates will write their answers in the spaces provided on the other side of theOMR form.Section A will consist of 35 multiple-choice questions. Out of 35 questions, five(5) will be from the passage/story read by the invigilator. A candidate will berequired to listen attentively to the passage and respond to the questions. Eachitem will carry one (1) mark. This section will weigh a total of 35 marks.Section B will consist of five (5) questions. The questions will be either onarranging the jumbled sentences chronologically or completing the compositionby choosing the letter of the correct answer. Each question will carry one (1)mark. The section will weigh a total of five (5) marks.Section C will consist of a short passage/poem followed by five (5) short answerquestions. Each question will carry two (2) marks. The section will weigh 10marks.5.0 EXAMINATION CONTENTThe following competencies will be assessed:5.1 Listening and comprehending information presented orally.5.2 Developing and using vocabulary appropriately through listening, writingand reading.5.3 Communicating simple ideas through writing.5.4 Reading and comprehending written information.5

02 English Language Table of geWeightingper CompetenceListeningandcomprehendinginformation presented orally.2.Developing and using vocabularyappropriatelythroughlistening,writing and reading.3.Communicating simple ideas throughwriting.4.Reading and comprehending writteninformation.Total Number of ItemsTotal Percentage WeightNumber of Items1.ApplyingRememberingSpecific CompetenciesUnderstandingCognitive Levels to beTestedS/N715.61533.31635.5715.645100

03 MAARIFA YA JAMII NA STADI ZA KAZI1.0 UTANGULIZIFomati ya mtihani wa Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi iliyoboreshwa inatokanana mihtasari mipya ya masomo ya Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi ya mwaka2016 iliyoanza kutumika mwaka 2017. Mihtasari hiyo inabainisha Umahiri Mkuuna Umahiri Mahsusi. Maboresho ya fomati yaliyofanyika yamelenga kutathminiumahiri unaozingatia viwango vya utendaji wa watahiniwa katika mambowaliyojifunza kuanzia Darasa la III hadi la VII kupitia mihtasari hii.2.0 MALENGO YA JUMLAMtihani wa Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi unalenga kupima ni kwa kiwangogani mtahiniwa anaweza:2.1kuthamini na kulinda mazingira na rasilimali za taifa;2.2kuthamini uhusiano wa watu na mazingira katika jamii;2.3kutambua na kutumia fursa zilizopo katika mazingira yake;2.4kutambua asili ya jamii za taifa letu;2.5kujenga misingi ya kujitegemea;2.6kuwa mbunifu; na2.7kutambua fursa katika mazingira yake.3.0 UJUZI WA JUMLAMtihani utapima ujuzi na utendaji wa mtahiniwa katika:3.1kuthamini utamaduni wa kitanzania na jamii nyingine;3.2kukuza uwezo wa kufikiri, kubuni na kutatua matatizo;3.3kujiheshimu na kuheshimu wengine;3.4kutenda matendo ya kizalendo; na3.5kushiriki katika kazi zinazokuza uwezo wake wa kufikiri kimantiki nakiyakinifu.7

4.0 MUUNDO WA MTIHANIMtihani wa Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi utafanyika kwa muda wa saa 1:30kwa watahiniwa wenye uoni na saa 1:45 kwa watahiniwa wasioona. Mtihaniutakuwa na sehemu A na B zenye jumla ya maswali 45. Maswali ya sehemu A(1 – 40) yatajibiwa katika fomu ya OMR kwa kutumia kalamu ya penseli ya HB.Maswali ya sehemu B (41 – 45) yatajibiwa upande wa pili wa fomu ya OMR kwakutumia kalamu ya wino wa bluu au mweusi. Mtahiniwa atatakiwa kujibu maswaliyote yenye jumla ya alama 50.Sehemu A itakuwa na maswali 40 ya kuchagua jibu sahihi. Kila swali litakuwa naalama moja (1) hivyo kufanya jumla ya alama 40 katika sehemu hii.Sehemu B itakuwa na maswali matano (5) ya majibu mafupi. Mtahiniwaatatakiwa kujibu maswali yote. Kila swali litakuwa na alama mbili (2) na kufanyajumla ya alama 10 katika sehemu hii.5.0 UMAHIRI UTAKAOTAHINIWAUmahiri utakaotahiniwa katika mtihani wa Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi nikama ifuatavyo:5.1Kutambua matukio yanayotokea katika mazingira yanayomzunguka.5.2Kutambua misingi ya uzalendo katika jamii.5.3Kutumia ramani na elimu ya anga katika maisha ya kila siku.5.4Kufuata kanuni za kiuchumi katika shughuli za uzalishaji mali.5.5Kutumia misingi ya unadhifu.5.6Kumudu mapishi mbalimbali.5.7Kusanifu kazi za sanaa.5.8Kutumia stadi za ujasiriamali.8

Jedwali la Utahini Somo la 03 Maarifa ya Jamii na Stadi za KaziIdadi ya imwa28.92.Kutambua misingi ya uzalendokatika jamii.1226.73.Kutumia ramani na elimu yaanga katika maisha ya kilasiku.613.34.Kufuata kanuni za kiuchumikatika shughuli za uzalishajimali.920.05.Kutumia misingi ya unadhifu.24.46.Kumudu mapishi mbalimbali.12.27.Kusanifu kazi za sanaa.12.28.Kutumia stadi za ujasiriamali.12.2Idadi ya MaswaliAsilimia ya Uzito wa Maswali459Uzito (%)13KuundaKutambuamatukioyanayotokea katika mazingirayanayomzunguka.Kutathmini1.KutumiaUmahiri MahsusiKuelewaNa.100

04 HISABATI1.0 UTANGULIZIFomati hii imeandaliwa kwa kuzingatia muhtasari wa 2016 ulioanza kutumikamwaka 2017. Muhtasari huo una Umahiri Mkuu na Umahiri Mahususi na utaanzakupimwa 2021. Aidha, mtihani utakaondaliwa kwa kutumia fomati hii utalengakupima umahiri aliokuwa nao mtahiniwa kuanzia Darasa la III hadi VII katikanyanja mbalimbali za Hisabati.2.0 MALENGO YA JUMLAMtihani wa Hisabati unalenga kupima ni kwa kiwango gani mtahiniwa anaweza:2.1kujenga uwezo wa kufikiri kimantiki; na2.2kujenga udadisi na kutatua matatizo.3.0 UJUZI WA JUMLAMtihani huu utazingatia ujuzi na utendaji wa mtahiniwa katika:3.1kutumia dhana na kanuni za kihisabati katika maisha ya kila siku;3.2kutumia matendo ya kihisabati ya namba nzima, namba kamili na sehemu;na3.3kuchora, kuwasilisha na kutafsiri data, takwimu na grafu.4.0 MUUNDO WA MTIHANIMtihani wa somo la Hisabati utafanyika kwa muda wa saa 2:00 kwa watahiniwawenye uoni na saa 2:40 kwa watahiniwa wasioona. Mtihani utakuwa na sehemuA na B zenye jumla ya maswali 45. Maswali ya sehemu A (1 – 40) yatajibiwakatika fomu ya OMR kwa kutumia kalamu ya penseli ya HB. Maswali ya sehemuB (41 – 45) yatajibiwa upande wa pili wa fomu ya OMR kwa kutumia kalamu yawino wa bluu au mweusi. Mtahiniwa atatakiwa kujibu maswali yote yenye jumlaya alama 50.Sehemu A itakuwa na maswali 40 ya kukokotoa kisha kuchagua jibu sahihi. Kilaswali litakuwa na alama moja (1) hivyo kufanya jumla ya alama 40 katikasehemu hii.10

Sehemu B itakuwa na maswali matano (5), mtahiniwa anatakiwa kukokotoa kwakuonesha njia au kuchora. Mtahiniwa atatakiwa kujibu maswali yote. Kila swalilitakuwa na alama mbili (2) na kufanya jumla ya alama 10 katika sehemu hii.5.0 UMAHIRI UTAKAOTAHINIWAUmahiri utakaotahiniwa katika mtihani wa Hisabati ni kama ifuatavyo:5.1Kutumia dhana ya namba kuwasiliana katika mazingira tofauti.5.2Kutumia stadi za kufumbua mafumbo katika maisha ya kila siku.5.3Kutumia matendo ya namba ya kihisabati katika kutatua matatizo.5.4Kutumia stadi ya uhusiano wa namba na vitu katika miktadha mbalimbali.5.5Kutumia stadi za vipimo katika miktadha mbalimbali.5.6Kutumia stadi za maumbo katika miktadha ya Hisabati.5.7Kutumia stadi za aljebra katika maisha ya kila siku.5.8Kutumia stadi za takwimu kuwasilisha taarifa mbalimbali.Jedwali la Utahini Somo la 04 Hisabati2.3.4.11Uzito (%)Idadi ya MaswaliKuundaUtambuziKutathminiKutumia dhana ya nambakuwasilianakatikamazingira tofauti.Kutumiastadizampangiliokufumbuamafumbo katika maishaya kila siku.Kutumia matendo yanambayakihisabatikatika kutatua matatizo.KutumiastadiyaKuchambua1.KutumiaUmahiri .7511.11022.5715.5

uhusiano wa namba navitukatikamiktadhambalimbali.5.Kutumia stadi za mbo katika miktadhaya Hisabati.7.Kutumia stadi za aljebrakatika maisha ya kilasiku.8.Kutumia stadi za takwimukuwasilishataarifambalimbali.Idadi ya MaswaliAsilimia ya Uzito wa Maswali511.1613.324.424.44512Uzito (%)Idadi ya hiri MahsusiKuelewaNa.KukumbukaNyanjazaZitakazopimwa100

05 SAYANSI NA TEKNOLOJIA1.0 UTANGULIZIFomati ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi somo la Sayansi na Teknolojiaimeandaliwa kwa mujibu wa Muhtasari wa somo la Sayansi na Teknolojia wamwaka 2016 ulioanza kutumika mwaka 2017. Muhtasari huo umebainishaUmahiri Mkuu na Umahiri Mahsusi anaotakiwa kuupata mwanafunzi katika ngaziya Elimu ya Msingi Darasa la III hadi VII. Hivyo, mtihani wa somo la Sayansi naTeknolojia utakaondaliwa kwa kutumia fomati hii, utalenga kupima umahirialiokuwa nao mtahiniwa kuanzia Darasa la III hadi VII.2.0 MALENGO YA JUMLAMtihani wa Sayansi na Teknolojia unalenga kupima ni kwa kiwango ganimtahiniwa anaweza:2.1 kukuza uelewa na kutumia maarifa, stadi na kuwa na mwelekeo wakisayansi na teknolojia;2.2 kujenga uwezo wa kutumia sayansi na teknolojia katika kutatua matatizokatika maisha ya kila siku; na2.3 kukuza stadi za kutenda na kutumia vifaa mbalimbali vya teknolojia.3.0 UJUZI WA JUMLAMtihani utazingatia tathmini ya ujuzi na utendaji wa mtahiniwa katika:3.1kufanya uchunguzi na ugunduzi wa kisayansi na kiteknolojia;3.2kufahamu misingi ya sayansi na teknolojia; na3.3kutunza afya na mazingira.4.0 MUUNDO WA MTIHANIMuda wa kufanya mtihani utakuwa saa 1:30 kwa watahiniwa wenye uoni na saa1:45 kwa watahiniwa wasioona. Mtihani utakuwa na sehemu A na B zenye jumlaya maswali 45. Maswali ya sehemu A (1 – 40) yatajibiwa katika fomu ya OMRkwa kutumia kalamu ya penseli ya HB. Maswali ya sehemu B (41 – 45)yatajibiwa upande wa pili wa fomu ya OMR kwa kutumia kalamu ya wino wa bluuau mweusi. Mtahiniwa atatakiwa kujibu maswali yote yenye jumla ya alama 50.13

Sehemu A itakuwa na maswali 40 ya kuchagua jibu moja sahihi. Kila swalilitakuwa na alama moja (1), hivyo kufanya jumla ya alama 40 katika sehemu hii.Sehemu B itakuwa na maswali matano (5) ya majibu mafupi au kukokotoa. Kilaswali litakuwa na alama mbili (2), hivyo kufanya jumla ya alama 10 katikasehemu hii.5.0 UMAHIRI UTAKAOTAHINIWAUmahiri utakaotahiniwa katika mtihani wa Sayansi na Teknolojia ni kamaifuatavyo:5.1kufanya uchunguzi wa kisayansi na teknolojia.5.2kufahamu misingi ya sayansi na teknolojia.5.3kutunza afya na mazingira.Jedwali la Utahini Somo la 05 Sayansi na anya majaribio kwausahihi.Kufuata kanuni za usafi ilikuwanaafyanamazingira bora.Kufuata kanuni za afya ilikujenga afya bora.14Uzito (%)Idadi ya MaswaliKuundaUtambuziKutathminiKuchunguza vitu vilivyopokatika mazingira.Kutambua aina anuai zanishati na matumizi yake.Kutambua nadharia zakisayansi na kiteknolojia.Kutumia TEHAMA.Kuchambua1.KutumiaUmahiri 0511.0613.3613.349.049.0511.0511.0

9.Kutambuamifumombalimbali ya mwili wabinadamu.Idadi ya MaswaliAsilimia ya Uzito wa Maswali64515Uzito (%)Idadi ya hiri 3100

06 URAIA NA MAADILI1.0 UTANGULIZIFomati ya Mtihani wa Kumaliza Eli

VII. Masomo hayo ni Kiswahili, English Language, Hisabati, Sayansi na Teknolojia, Uraia na Maadili, Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi. Mabadiliko katika mtaala, yalisababisha maboresho ya mihtasari ya masomo ya Darasa la III hadi la VII. Hiv

Related Documents:

wa aya ya 112(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Aidha, kwa mujibu wa Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama Na. 4/2011, Tume ya Utumishi wa Mahakama mbali na kuwa na majukumu mengine inalo jukumu la kuajiri watumishi wa kada mbalimbali wa Mahakama.

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA THE CONSTITUTION OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA OF 1977. CHAPTER 2 OF THE LAWS. 2005 . The following is the official Revised version in English of “KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 1977”. This revised edition of the

TARP Tanzania Agricultural Research Project TAWIRI Tanzania Wildlife Research Institute TAWLAE Tanzania Association of Women Leaders in Agriculture and Environment TBC Tanzania Broadcasting Cooperation TBS Tanzania Bureau of Standard TCC Tanzania Communications Commission TCCIA Tanzan

education in Tanzania and defines the roles of national and local education bodies. Sources: UNESCO-IBE (2010). World Data on Education VII Ed. 2010/11. United Republic of Tanzania. Geneva: UNESCO-IBE. United Republic of Tanzania (1997). National Council for Technical Education Act. Dodoma: United Republic of Tanzania.

vii MUHTASARI Tanzania inakabiliwa na changamoto ya matumizi yasiyo salama ya kemikali na usimamizi usiosalama wa

Utafiti wa THIS wa mwaka 2016-17 umeongozwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Tume ya Kuthibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) na Zanzibar (ZAC), na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee . MATOKEO YA AWALI UTAFITI WA VIASHIRIA NA MATOKEO YA UKIMWI TAN

kwa kuzingatia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977; Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025; Mpango wa Taifa wa . /12 hadi 2015/16; Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA II); Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2010 hadi 2015; Malengo ya Maendeleo ya Milenia; Sera ya Taifa

4 Shaft Capacity in Clay (Alpha Method) Soft-stiff clay Adhesion factors