TAASISI YA ELIMU TANzANIA MPANgo WA UTAYARI WA KUMUANDAA .

3y ago
290 Views
7 Downloads
8.26 MB
68 Pages
Last View : Today
Last Download : 3m ago
Upload by : Harley Spears
Transcription

TAASISI YA ELIMU TANzANIAMPANgo WA UTAYARI WA KUMUANDAAMToTo KUANzA SHULEMAfUNzo ELEKEzI KWA WALIMU WASAIDIzI WA JAMIIMWoNgozo WA MWEzESHAJI WA MAfUNzo2015

SHUKURANIMwongozo huu umeandaliwa kwa ushirikiano wa Taasisi ya Elimu Tanzani (TET),EQUIP-T, na Aga-Khan Foundation (AKF). TET inawashukuru EQUIP-T kwakugharamia warsha ya kuandika mwongozo huu. Aidha TET inawashukuru wotewalioshiriki kwa namna moja au nyingine katika kuandika mwongozo huu.Shukurani za pekee ziwaendee wafuatao:WaandishiVida Ngowi – Taasisi ya Elimu Tanzania (TET)Sharifa Majid – Aga Khan Foundation (AKF)Rose Chipindula – Taasisi ya Elimu Tanzania (TET)Laurence Kunambi – Taasisi ya Elimu Tanzania (TET)ViongoziDr. Wilberforce Meena – Mkurugenzi Idara ya Ubunifu na Uboreshaji wa Mitaala .Ni matumaini yetu kuwa mwongozo huu utakuwa na manufaa kwa WalimuWasaidizi wa Jamii wanaofundisha katika Mpango wa Utayari wa Kuanza Shule.PichasAKDN / Lucas Cuervo MouraAKDN / Jean-Luc RayAKDN / Zul MukhidaDr. Leonard AkwilapoKAIMU MKURUGENZI MKUUTAASISI YA ELIMU TANZANIAMpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania Uongozi na Usimamizi wa Shule

VifupishoAKF: Aga Khan FoundationEQUIP-Tz: Education Quality Improvement Programme – TanzaniaMMJ: Mwalimu Msaidizi wa JamiiWWJ: Walimu Jamii WasaidiziTET: Taasisi ya Elimu TanzaniaMpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania Uongozi na Usimamizi wa Shule

YALIYOMOUtangulizi1Malengo ya Mwongozo:1Walengwa wa Mwongozo:1Muundo wa Muongozo1Muda wa Mafunzo1Mbinu za Ufundishaji1Vifaa/Zana2Umuhimu wa Muongozo2Muongozo wa Utekelezaji wa Mpango wa Utayari wa kuanza Shule3Majukumu ya Mwalimu Msaidizi wa Jamii4Maeneo ya Umahiri4Matumizi ya Vitabu vya Hadithi10Maendeleo ya Mtoto10Hatua za Makuzi na Maendeleo ya Mtoto10Mpango wa Shughuli kwa Wiki12Mpangilio wa Hadithi12Maelekezo ya ufundishaji wa Hadithi13Ratiba ya Siku16Utekelezaji wa Ratiba ya Siku17Ufundishaji na Ujifunzaji wa Hadithi20Wiki ya Kwanza - Hadithi ya Nyumbani Kwetu20Wiki ya Pili - Hadithi ya Upendo30Wiki ya Tatu - Hadithi ya Nyoka Mkubwa39Wiki ya Nne - Hadithi ya Ninapenda kwenda Shule48Siku ya Tano ya Mafunzo56

UtanguliziMwongozo huu wa mafunzo umeandaliwa kwa kufuata nadharia ya utekelezaji wa mpango waUtayari wa Kuanza Shule. Mwongozo unatoa maelekezo ya namna ya kumjengea mtoto umahiriufuatao: kuwasiliana kwa lugha ya Kiswahili, utambuzi, kuhusiana, kujenga mwili na kuthaminimazingira. Aidha mwongozo huu unatoa maelekezo ya kutumia hadithi 12 zilizoandaliwa ili kufikiaumahiri uliobainishwa katika nadharia. Mwongozo huu unazingatia mbinu shirikishi zitakakazotoafursa kwa mtoto kuweza kujifunza kwa urahisi. Mwongozo huu pia unapendekeza shughuli, vifaa/zanaambazo mwezeshaji anaweza kuzitumia wakati wa mafunzo. Vilevile mwongozo unapendekeza mbinuzitakazotumika ili kupima ufanisi wa ujifunzaji wa mtoto.Malengo ya Mwongozo:Malengo ya mwongozo huu ni: Kumuongoza mwezeshaji namna ya kuwawezesha Walimu Jamii Wasaidizi kutekeleza mpangowa kumuandaa mtoto kuwa tayari kuanza shule. Kumwongezea mwezeshaji stadi mbali mbali zitakazomsaidia kumuongoza. Mwalimu Msaidiziwa Jamii kuweza kutumia hadithi 12 katika kumjengea mtoto umahiri uliokusudiwa. Kumjengea Mwalimu Msaidizi wa Jamii umahiri wa kutekeleza mpango wa kumuandaa mtotokuwa tayari kuanza shule.Walengwa wa Mwongozo:Walengwa wa mwongozo huu ni hawa wafuatao: Wawezeshaji wa Walimu Wasaidizi wa Jamii. Walimu Wasaidizi wa Jamii. Wathibiti wa ubora wa elimu. Waratibu Elimu Kata. Walimu wakuu. Walimu wa darasa la kwanza.Muundo wa MuongozoMuongozo huu umegawanyika katika sehemu kuu tatu, sehemu ya kwanza ni utangulizi ambaounajumuisha maelezo mafupi kuhusu mwongozo wa mafunzo, sehemu ya pili ni muongozo wautekelezaji wa programu na sehemu ya tatu ni utekelezaji wa programu ya Utayari wa kuanza Shule.Muda wa MafunzoMuda wa mafunzo utakaotumika kutekeleza mpango huu umegawanyika katika awamu mbili.Awamu ya kwanza ya mafunzo itakuwa ni ya wiki nne ambapo muongozo huu umebainishashughuli zitakazofanyika kwa kipindi hiki kwa ajili ya kumjengea mtoto umahiri tarajiwa. Awamu yapili itakuwa ya wiki nane ambayo itaandaliwa baada ya kufanya tathimini ya wiki nne za mwanzo.Mbinu za Kumwezesha MMJ Kufundisha.Wawezeshaji wanashauriwa kutumia mbinu shirikishi katika kuwezesha ili kumsaidia MMJ kuzitumiambinu hizi katika kufundisha watoto. Baadhi ya mbinu hizo ni hadithi, igizo dhima, michezo,nyimbo, ziara, kumualika mgeni, matembezi ya galari, changanya kete, majadiliano ya vikundi,fikiri- jozisha-shirikisha, maswali na majibu.Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania Uongozi na Usimamizi wa Shule1

Vifaa/Zana Zitakazotumika katika UwezeshajiMwanasesere, picha, vitabu vya hadithi, chati, kadi, vifaa vya TEHAMA, vitu halisi vinavopatikanakutoka katika mazingira yao na miongozo ya kufundishia.Umuhimu wa MwongozoMatumizi bora ya Mwongozo huu yatampa Mwalimu Msaidizi wa Jamii: Uwezo wa kufundisha na kujifunza kwa udadisi na ufasini kwa watoto katika kutumia mwongozohuu Mwalimu Msaidizi wa Jamii atawawezesha kujenga stadi na ujuzi wa kujitegemea.Uwezo wa kushirikiana na watoto katika ufundishaji bora unaolenga katika kumjengea mtotoumahiri unaotarajiwa.Aidha kwa kutumia mwongozo huu vilevile utamuwezesha Mwalimu Msaidizi wa Jamii kufikiri nakubuni mikakati itakayoboresha ufundishaji wake wa kila siku darasani kwa kutumia hadithi nne(4) katika majuma manne ya mpango wa utayari wa kuanza shule.Mwongozo huu pia umezingatia ufanisi wa ufundishaji wa hadithi nne katika maeneo ya: Malengo mahususi yanayobainisha umahiri kwa kila hadithi.Njia na mbinu shirikishi za kufundishia na kujifunzia.Matokeo ya mafunzo.Upimaji na tathmini na ufuatiliaji wa uhawilishaji wa maarifa ya watoto nyumbani wanakoishi.Matumizi ya Mwongozo:Mwongozo huu utamsaidia Mwalimu Msaidizi wa Jamii katika: 2Kuchambua nadharia ya mpango wa utayari wa kuanza shule.Kuandaa azimio la kazi la wiki nne (4) na andalio la somo lenye mwelekeo wa kumjengea mtotoumahiri tarajiwa.Kuweka mikakati ya ufundishaji wa wiki nne(4) kwa ufanisi.Kufanya upimaji na tathmini ya maendeleo ya watoto kwa kutumia mbinu zilizopendekezwakatika mwongozo.Mwalimu Msaidizi wa Jamii kujipima mwenyewe.Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania Uongozi na Usimamizi wa Shule

MUONGOZO WA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA UTAYARI WAKUANZA SHULEMwezeshaji awakaribishe washiriki katika mafunzo kwa namna inayofaa. Kisha atoe fursa kwawashiriki kufahamiana. Haya yanaweza kufanyika kwa kutumia njia ya mchezo. Kwa mfano;TANBINGO: Huu ni mchezo unaotoa fursa kwa washiriki kufahamiana na kujifunza kutoka kwa kilammoja. Unaweza kufuata maelekezo yafuatayo:i.Washiriki wakae wawili wawili.ii.Wape maswali ya muongozo ya utambulisho binafsi kwa mfano; Jina Shughuli anazofanya Michezo anayopenda Matarajio yake baada ya mafunzoiii.Washriki wakumbuke majibu waliyoyapata, kisha washirikishaneiv.Waulize washiriki wamejifunza nini kwa kufanya shughuli hii?JielezeKuimba wimboWOTE: Jieleze, jieleze, jieleze, jieleze, jieleze, jieleze shajieleza mamaMMOJA: Mimi hapa ni Tatu, baba yangu ni Khamis, nakaa Bububu, nishajieleza mama.WOTE: Jieleze, jieleze, jieleze, jieleze, jieleze, jieleze shajieleza mamaMMOJA: Mimi hapa Maimuna baba yangu ni Mzee, Mama yangu ni Hadia, nishajieleza mama.WOTE: Jieleze, jieleze, jieleze, jieleze, jieleze, jieleze shajieleza mamaMwezeshaji awaulize washiriki je kuimba wimbo husaidia nini katika ujifunzaji?Kuimba wimbo husaidia kujifunza msamiati mpya, kukumbuka sentensi fupi, kuimarisha mfumo waupumuaji na kuvuta oksijeni zaidi kwenye ubongo, pamoja na kukuza ushirikiano.Mwalimu Msaidizi wa JamiiMwezeshaji awaongoze washiriki ili waweze kutambua majukumu ya MMJ. Pamoja na maelezowatakayotoa mwalimu msaidizi wa jamii ni mtekelezaji mkuu wa mpango wa kumuandaa mtotokuwa tayari kuanza shule. Mwalimu huyu anachaguliwa kwa kushirikisha wadau muhimu katikajamii husika.Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania Uongozi na Usimamizi wa Shule3

Majukumu ya Mwalimu Msaidizi wa Jamiii.Anatarajiwa kushiriki katika shughuli zote zitakazofanyika wakati wa mafunzo.ii.Kupata mafunzo ili aweze kutekeleza mpango wa wiki 12 za utayari wa kuanza shule.iii.Kukakimilisha shajala inayoonesha ufupisho wa shughuli zote zinazotekelezwa kwakipindi chote.iv.Kuweka kumbukumbu ya maendeleo ya watoto katika shajala.v.Kushirikiana kwa karibu na kufanya kazi na mwalimu wa darasa la kwanza katika kipindi champito katika shule ya msingi.vi.Kuunganisha familia, jamii na shule iliyo karibu kwa kutumia lugha ya Kiswahili.Maeneo ya Kutilia msisitizoMwezeshaji awapitishe washiriki katika maeneo ya kutilia msisitizo kwa kuwagawa wanafunzi katikamakundi matano kulingana na uchanganuzi wa maeneo hayo kama yalivyobainishwa kwenyeJedwali lifuatalo;Uchanganuzi wa Maeneo MuhimuMaeneo muhimuZaidiKuwasiliana KwaLugha ya KiswahiliUmahiri MahususiShughuli za kutendamwanafunziKukuza lugha yamazungumzoUsalimiaji umefanyika kwa usahihi kwakuzingatia umri, rika nautamaduni wa mtotoUtambulishajiumefanyika kwausahihiUkaribishaji nauagaji umefanyikakwa usahihiKuuliza, kuombaKuuliza, kuomba nakushukuru anapopewa na kushukuru kumefanyika kwa usahihikitu.Ufuataji wa maelekezoKufuata maelekezoanayopewa umefananayopewa na watuyika kwa usahihiwengine.Kuhesabu idadi ya vitu Uhesabuji wa vituvinavyopatikana katika umefanyika kwa ufanisimazingira ya shule nanyumbani.Kutambua mlinganoutambuaji warahisimilingano umefanyikakwa usahihiKuhesabu4Vigezo vya UpimajiKusalimiana kwakuzingatia umri, rika(kutokana nautamaduni)Kujitambulisha nakuwatambulishawengine.Kukaribisha na kuaganaMpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania Uongozi na Usimamizi wa Shule

Maeneo muhimuZaidiUtambuziUmahiri MahususiShughuli za kutendamwanafunziVigezo vya Upimajimaumbo rahisi (mraba. Ubainishaji waMduara, pembe tatu)maumbo rahisi umefanyika kwa usahihiKusoma vitabu vyaUsomaji vitabu vyaKuelezea hisiapichapicha umefanyika(anachopenda,kwa usahihiasichopenda,furaha, huzuni, hasira, Kusimulia hadithi kwa Usimuliaji wa hadithikuchanganyikiwa)kuonesha hisiakwa kuonesha hisiaumefanyika kwausahihiUchoraji wa pichaKuchora picha naumefanyika kwakujieleza kwa njia yausahihipichaKuuliza na kujibuKusoma picha naUsomaji picha namaswalikujibu maswaliujibuji wa maswaliumefanyika kwausahihiZiara ya kutembeleaZiara ya kutembeleamaeneo ya historia namaeneo ya historiashamba la mifugo imau kwenye shamba laefanyika kwa usahihimifugoKuchunguza mazingira Kuuliza na kujibuUulizaji na ujibuji wamaswalimaswali umefanyikakwa usahihiKuchunguza vitu ndani Uchunguzaji wa vituya darasa na kuvitajandani na nje ya darasaumefanyika kwausahihiKuchunguza vitu nje ya Uelezeaji wa vitudarasa na kuvielezeavilivyochunguzwa njeya darasa umefanyikakwa usahihi.Kuchunguza na kubuni Kuotesha mbegu zaUoteshaji wa mbegu zanafakanafaka umefanyika kwausahihiKuunda vituUundaji wa vitu umembalimbali.fanyika kwa usahihiUchunguzi kutokanaKutembelea maeneoya kihistoria, shamba la na eneo liliokusudiwaumefanyika kwamifugo/kilimousahihiMpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania Uongozi na Usimamizi wa Shule5

Maeneo muhimuZaidiUmahiri MahususiShughuli za kutendamwanafunziVigezo vya UpimajiKucheza (Michezo yaVibao)Uchambuaji wa vituumefanyika kwausahihiUtumiaji wa vifaambalimbali vyamichezo umefanyikakwa usahihiUtumiaji wa vifaa vyamichezo nje ya darasaumefanyika kwausahihiUtumiaji wa kona yanyumbani umefanyikakwa ufasahaKuchagua shughuliUchaguzi wa shughuliwanayotaka kuifanya. wanazotaka kufanyaumefanyika kwausahihiKuimba nyimbo zaUimbaji wa nyimbo zashuleshule umefanyika kwausahihiUchezaji wa pamojaKucheza michezombalimbali pamoja na katika michezo umefanyika kwa usahihiwenzieKufanya kazi katika jozi Ufanyaji wa kazi katikana kikundivikundi na jozi umefanyika kwa usahihiKutengeneza marafiki Utengenezaji wamarafiki umefanyikakwa usahihiKushiriki pamoja naUshiriki wa pamojawengine katika kazi.katika kazi umefanyikakwa usahihiKuelekezana katikaUelekezanaji katikaujifunzaji.kujifunza umefanyikakwa usahihiTendo la kuhudumiaKumuhudumiamwingine anapohitaji wengine limefanyikakwa usahihimsaada.Kubaini hisia zaUbainishaji wa hisia zawengine.wengine umefanyikakwa usahihiUchambuzi wa vitumbalimbali (sortingactivities)Kucheza na vifaambalimbali vilivyotengenezwa kwa mikono(kibao fumbo)Kutumia vifaa vyamichezo vya nje ya darasa (bembea mtelezo,kupanda ngazi n.k.)Kuwa na mtazamoKucheza katika kona yachanya katika kujifunza nyumbani.KuhusianaKushirikianaKusaidiana katika halimbalimbali6Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania Uongozi na Usimamizi wa Shule

Maeneo muhimuZaidiUmahiri MahususiShughuli za kutendamwanafunziKujitambua.Kuelewa jina na jinsiyakeKukuza haibaKujenga mwiliKukuza misuli midogomidogoVigezo vya UpimajiUtambuaji wa jina najinsi yake umefanyikakwa usahihiKutambua haki zakeUtambuaji wa hakizake umefanyika kwausahihiKutambua wajibuUtambuaji wa hakiwake.zake umefanyika kwausahihiKujiheshimu naTendo la kutumia lughakuheshimu wengine.ya upole limefanyikakwa usahihiKutumia mikaoUtumiaji wa mikaoinayokubalika na jamii. mbalimbali umefanyika kwa usahihiKuheshimu taratibu na Tendo la kuheshimutamaduni zinazokuba- taratibu na tamadunizinazokubalika limelika na jamiifanyika kwa ufanisiKuonesha uadilifuUoneshaji wakatika maisha yakeuadilifu umefanyikakwa usahihiKukata karatasi kwaUkataji wa karatasikutumia mkasikwa kutumia mkasiumefanyika kwausahihiKupaka rangi maumbo Upakaji wa rangi umebapafanyika kwa usahihiUundaji wa vitu kwaKuunda vitu kwakutumia udongo umekutumia udongo wafanyika kwa usahihimfinyanziKutengeneza shangaUtengenezaji wakwa kutumia kambashanga kwa kutumiakamba umefanyikakama inavyopaswaKufunga na kufungua Ufungaji na ufunguajivifungowa vifungo umefanyikakwa usahihiKuweka pamoja vibao Umaliziaji wa kibaofumbofumbo umefanyikakwa usahihiMpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania Uongozi na Usimamizi wa Shule7

Maeneo muhimuZaidiUmahiri MahususiShughuli za kutendamwanafunziKuimarisha afya.Kukimbia kwendambeleKukimbia kurudinyumaKurusha na kudakampiraKukuza ujasiri naukakamavuKuthamini Mazinigira8Kubainisha vitumbalimbali katikamazingira ya shuleVigezo vya UpimajiUkimbiaji umefanyikakwa usahihiUkimbiaji umefanyikakwa usahihiUrushaji na udakaji wampira umefanyika kwausahihiKupanda na kushukaUpandaji na ushukajikwenye ngazikwenye ngazi umefanyika kwa usahihiKusimamia mguuKusimama kwa mguummojammoja umefanyikakwa usahihiKutembea kwa kusima- Utembeaji wamia vidole vya miguukusimamia vidole vyamguuni umefanyikakwa usahihikubembeaUbembeaji umefanyikakwa usahihiKuendesha baiskeliUendeshaji wa baiskeliumefanyika kwausahihiUfuatiliaji wa ala zaKuchezesha viungomuziki kwa kuchezeshakwa kufuatisha ala zaviungo umefanyikamuzikikwa usahihiKubainisha vitu vilivyo Ubainishaji wa vitundani na nje ya darasa. ndani na nje ya darasaumefanyika kwausahihiUbainishaji wa vituKubainisha vituhatarishi katika mazinhatarishi katika mazgira ya shule nyumbaniingira ya shule nana njiani yamefanyikanymbani namna yakwa usahihikujikingaUbainishaji wa wanKubainisha ainayama na mimea katikambalimbali zamazingira ya shule nawanyama na mimeanyumbani umefanyikakatika mazingira yakwa usahihishuleni na nyumbaniMpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania Uongozi na Usimamizi wa Shule

Maeneo muhimuZaidiUmahiri MahususiShughuli za kutendamwanafunziVigezo vya UpimajiKutumia choo kwausahihiKuomba ruhusaanapotaka kwendachooniUombaji wa ruhusaanapotaka kwendachooni umefanyikakwa usahihiMatumizi ya utumiajiwa choo umefanyikakwa usahihiUsafi wa mazingira yachoo umefanyika kwausahihiUoshaji wa mikonobaada ya kutokachooni umefanyikakwa usahihiUvukaji sahihi wabarabara umefanyikakwa usahihiUtembeaji sahihipembezoni mwabarabara umefanyikakwa usahihiUbainishaji wa maeneohatarishi umefanyikakwa usahihiKuonesha matumizisahihi ya choo.Kusafisha nakudumisha usafi wamazingira ya choo.Kuosha mikono baadaya kutoka chooni.Kutambua maeneosalama na hatarishiKuvuka barabara kwauangalifu.kutembea mkabalana magari pembezonimwa barabara.kubaini vitu na watuhatarishi katikamazingira ya shuleni,nyumbani na njiani.ShughuliMwezeshaji awaongoze washiriki kuhusisha hadithi anayosoma na umahiri aliouchagua kwakutumia igizo dhimaMpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania Uongozi na Usimamizi wa Shule9

Matumizi ya Vitabu vya HadithiMwezeshaji awaongoze washiriki kubaini utaratibu wa matumizi ya vitabu vya Hadithi katika Mpango wa Utayari Kuanza Shule. Matumizi ya vitabu ni jambo la msingi sana katika utekelezaji wampango huu. Matumizi ya vitabu hivyo utafuata utaratibu ufuatao:1) Hadithi 12 kwa wiki 12Hadithi moja itasomwa kwa wiki, itasomwa wakati wa mduara wa asubuhi. Ni vema MMJ kubainishaumahiri uliokusudiwa baada ya kusoma hadithi kwa kutumia shughuli na mbinu mbalimbali katikaujifunzaji.2) Shughuli zitabuniwa kutokana na hadithiMwezeshaji atoe shughuli kutegemeana na hadithi ambayo itawezesha kujenga umahiriuliokusudiwa.3) UpimajiMwezeshaji awaongoze washiriki kubaini umahiri uliojengwa kwa kutumia zana mbalimbali zaupimaji kama vile; orodha hakiki, maswali na majibu na mkoba wa kazi.Maendeleo ya MtotoMwezeshaji awaongoze washiriki kubaini dhana na hatua za maendeleo na ukuaji wa mtoto.Ni muhimu washiriki kutambua kuwa watoto wote ni wa kipekee japokuwa wengi wanafuata mfumoulio sawa katika ukuaji, maendeleo na makuzi yao wakiwa wadogo kama vile kujifunza kuongea nakujifunza kutembea. Katika darasa moja unaweza kuwa na watoto wa miaka 5 ambao wana tabiakama za watoto wa miaka 4 na wengine wana tabia kama za watoto wa miaka 6. Jedwali lifuatalolinaonesha hatua za maendeleo na makuzi ya mtoto wa miaka 5 – 8.Hatua za Makuzi na Maendeleo ya MtotoUmriKipengeleYanayojitokezaMiaka 5-6Ukuaji wa MwiliMiaka 5-6Ukuaji wa Kijamii Miaka 5-610Ukuaji wa Akili(Ubongo) Kupanda na kushuka ngaziKuruka kwa kutumia miguu yoteKuongezeka kwa uwezo wa kuhimili mwendo wa misuliKuonesha kuwa anatumia mkono wa kulia au kushotoAnaonesha hisia kali kwa familia na mambo ya nyumbaniAnaonesha ukuaji na kuanza kujitegemeaAnaweza kukubali maelekezo na kufuata taratibuAnaweza kushirikiana vitu na wengine na hatakubadilishanaAnaweza kushiriki katika uzoefu wa shuleAnaonesha usikivu mkubwaAnaweza kuweka vitu katika mlolongo (kutenganisha)Kutumia lugha kwa upanaKujua majina ya vitu, rangi na maumboMpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania Uongozi na Usimamizi wa Shule

UmriMiaka 5-6KipengeleYanayojitokezaUkuaji wa Kimaadili(Kiroho) Kujua mema na mabayaKuathiriwa na tabia za watu wengineKujenga mitizamo sahihi ya kimaadili kama vile heshima,kuwa mkweli na kujenga imani au uaminifuHatua za Ukuaji kwa mtoto wa miaka 7 – 8UmriKipengeleYanayojitokezaMiaka 7-8Ukuaji wa Mwili Miaka 7-8Ukuaji wa KijamiiMiaka 7-8Ukuaji wa Kihisia Miaka 7-8Miaka 7-8Ukuaji wa Akili(Ubongo) Ukuaji wa Kimaadili (Kiroho) Anaweza kupanda juu ya mitiAnaweza kuvaa na kuvua nguo yeye mwenyeweAnaweza kushika mpira mikono yake ikiwa imesambaaAnaweza kutembea kinyumenyume na kwa kutumia nchaza vidoleAnaweza kucheza kwa ushirikiano na wezakeAnafahamu kuhusu jinsia na tofauti za rangi za watuAnafahamu miiko ya jamii ambamo anaishiAnajenga uwezo wa kujihimili zaidiAnaanza kuonesha hali ya ucheshiAnaweza kuanza kuona mtizamo wa mtu mwingine, kwakuongozwaAnaanza kuonesha uwezo wa kutatua migogoroAnakuza msamiati harakaAnaanza kutofautisha vitu kutokana na kazi zakeAnaanza kuonesha udadisi wa mambo na kuuliza “Kwanini?” nyingiAnaanza kufahamu thamani ya nambaAnafahamu vizuri matarajio ya watu wakubwa katikamazingira tofauti na anaelewa makosa yake inapotokeaameyafanyaAnafahamu kuwa matendo yanahukumiwa kwa matokeoyakeAnajua mambo ya kimaadili yanayokatazwa na jamiiambayo anaishiMwezeshaji awaongoze washiriki kuimba wimbo wa ‘Tuamkapo Asubuhi’ ili kuwajengea uwezowalimu wa kuwawezesha watoto kujenga tabia njema na msamiati kwa kutumia nyimbo.Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania Uongozi na Usimamizi wa Shule11

Tuamkapo asubuhiTuamkapo asubuhi tuwasalimu wazazi.Shikamoo mama shikamoo baba hii ndio ndio tabia njemaTuamkapoMpango wa Shughuli kwa WikiMwezeshaji awaongoze washiriki kubaini mpango wa shughuli wa

Kuchambua nadharia ya mpango wa utayari wa kuanza shule. Kuandaa azimio la kazi la wiki nne (4) na andalio la somo lenye mwelekeo wa kumjengea mtoto umahiri tarajiwa. Kuweka mikakati ya ufundishaji wa wiki nne(4) kwa ufanisi. Kufanya upimaji na tathmini ya maendeleo ya watoto kwa kutumia mbinu zilizopendekezwa katika mwongozo.

Related Documents:

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Imefadhiliwa na Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DFID) Agosti, 2017 MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU YA SEKONDARI (MUES) EQUIP-Tanzania. Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MU

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekuwa ikiboresha Mtaala wa Elimu ya Msingi kuhakikisha kwamba elimu inayotolewa ni bora na inayomwandaa mwanafunzi kumudu maisha katika mazingira yake. Muktadha huu umeifanya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia iboreshe mchakato wa kufundisha

MUHTASARI Wafanyakazi ni wadau muhimu katika kujenga uchumi wa taifa. Kuna uhusiano wa . Chama cha wafanyakazi wa taasisi za elimu ya juu Tanzania (THTU) kimeanzishwa . yakitokea katika uendeshaji wa vyama hivi na kupelekea kupungua kwa utamaduni wa kutoaminiana uliokuwepo awali. Kutokana na mabad

Hali ya Elimu Andika idadi halisi ya huduma zilizopo kijijini. Idadi V401. Idadi ya shule za msingi za serikali V402. Idadi ya shule za msingi za binafsi V403. Idadi ya vituo vya elimu ya awali V404. Idadi ya shule za sekondari V405. Idadi ya shule za ufundi V406. Kuna kamati ya elimu na hu

Ms. Fika Mwakabungu - Mkurugenzi Idara ya Mafunzo na Mitaala . kuwasiliana kwa lugha ya Kiswahili, Utambuzi, Kuhusiana, Kujenga Mwili na Kuthamini Mazingira. Aidha mwongozo huu unatoa maelekezo ya kutumia . Kufanya upimaji na tathmini ya maendeleo ya watoto kwa kutumia mbinu zilizopendekezwa katika mwongozo.

4.3.1 Elimu ya malezi ya awali na makuzi (ECEC), utambuzi wa mapema na afua za mapema (EIEI) . ECC Mtaala wa Msingi Uliopanuliwa ECEC Elimu ya awali ya utotoni na Uangalizi . MUHTASARI Ripoti hii ya dunia juu ya elimu jumuishi ina

Ingawa Sera ya Elimu ya Awali ipo, mafanikio ya sera hii ni madogo sana. Elimu ya Awali ilijumuishwa moja kwa moja katika elimu ya msingi (2014) lakini shule nyingi hazina madarasa mazuri ya elimu ya awali. Sekta ya shule za awali hazina walimu wenye st

course. The course was advertised as a training for social and philanthropic work. Birmingham was the first UK University to give aspiring social workers full status as students. From its founding in 1900 University staff had been actively involved in social welfare and philanthropic work in the City of Birmingham. Through research into the employment and housing conditions of poor people in .