WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA TAASISI YA

2y ago
301 Views
4 Downloads
1.17 MB
67 Pages
Last View : Today
Last Download : 3m ago
Upload by : Francisco Tran
Transcription

WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIATAASISI YA ELIMU TANZANIAMTAALA WA MAFUNZO YA ASTASHAHADAYA UALIMU ELIMU MAALUMU TANZANIAi

Taasisi ya Elimu Tanzania, 2019Toleo la kwanza 2019ISBN: 978-9976-61-832-7Taasisi ya Elimu TanzaniaS.L.P 35094Dar es SalaamSimu: 255222773005Faksi: 2552227744420Baruapepe: la huu urejelewe kama: Taasisi ya Elimu Tanzania. (2019). Mtaala wa Mafunzo yaAstashahada ya Ualimu Elimu Maalumu. Dar es Salaam:Taasisi ya Elimu Tanzania.Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kunakili, kurudufu, kuchapisha wala kufasiriandiko hili kwa namna yoyote ile bila idhini ya maandishi kutoka Taasisi ya ElimuTanzania.ii

IdhiniMtaala ni nyenzo muhimu ya ufundishaji na ujifunzaji katika ngazi yoyote ya elimu nahuakisi ubora wa elimu inayotolewa. Lengo la mtaala huu wa Astashahada ya UalimuElimu Maalumu ni kumsaidia mkufunzi na wadau wa elimu maalumu nchini Tanzaniakutoa elimu na malezi yenye viwango vya ubora vinavyokubalika kitaifa na kimataifa.Mtaala huu umeandaliwa ili kujenga umahiri kwa mwalimu tarajali utakaomwezeshakumudu ufundishaji na ujifunzaji katika shule za msingi. Mkufunzi hana budi kuupitiamtaala kwa umakini ili aweze kuwa na mtazamo mpana kuhusu kile anachotakiwakukifundisha.Ni matarajio yangu kuwa watekelezaji wa mtaala huu watamwezesha mwalimu tarajalikujenga umahiri uliokusudiwa kama ulivyoelekezwa katika mtaala huu.Kaimu Kamishna wa ElimuWizara ya Elimu, Sayansi na TeknolojiaS.L.P. 10DodomaSimu: 255 26 296 3533Baruapepe: info@moe.go.tzTovuti:www.moe.go.tziii

DibajiMtaala wa Mafunzo ya Astashahada ya Ualimu Elimu Maalumu umeandaliwa ilikukidhi mahitaji ya upatikanaji wa walimu wa kufundisha wanafunzi wenye mahitajimaalumu katika ngazi ya shule za msingi. Mtaala huu utawawezesha wakufunzi nawadau wengine wa elimu kufanikisha mafunzo ya ualimu ngazi ya Astashahada yaUalimu Elimu Maalumu.Mtaala huu una vipengele vikuu tisa ambavyo ni: utangulizi, muktadha wa sasa wamtaala wa mafunzo ya Astashahada ya Ualimu Elimu Maalumu unaozingatia mahitajiya kijamii na kiuchumi, dira, dhamira, malengo na ujuzi wa jumla wa Mtaala, mudawa mafunzo, muundo wa maudhui, maeneo ya kujifunza na viwango vya rasilimalikatika utekelezaji wa Mtaala. Vipengele vingine ni: njia za kufundishia na kujifunzia,upimaji wa maendeleo ya mwalimu tarajali, ufuatiliaji na tathmini ya Mtaala.Mtaala unaelezea mazingira halisi ya sasa ya kijamii na kiuchumi ambapo utatekelezana kubainisha malengo makuu ya elimu, Elimu ya Ualimu na Elimu ya UalimuElimu Maalumu. Pia, Mtaala umebainisha wazi umahiri ambao mwalimu tarajalianatakiwa kuujenga. Aidha, katika masomo, maeneo ya kujifunza na mgawanyo wakeumeoneshwa wazi katika masomo ya fani, ualimu na yale ya ufundishaji ili kutoamwongozo katika ufundishaji na ujifunzaji wa wanafunzi wenye mahitaji maalumu.Vilevile, Mtaala unaeleza sifa anazopaswa kuwa nazo mkufunzi na kiongozi wa chuopamoja na mahitaji ya rasilimali watu na vitu vinavyotakiwa chuoni. Muundo waupimaji wa walimu tarajali katika mafunzo kwa vitendo umeoneshwa kwa ajili yakuwawezesha kupata umahiri wa ufundishaji na ujifunzaji.Mwisho, Mtaala unaeleza njia za ufuatiliaji na tathmini ya Mtaala ambazo zinatakiwakutumika wakati Mtaala unatekelezwa na baada ya utekelezaji wake. Kwa ujumla,Mtaala umelenga kuwa mwongozo kwa wadau wote wa Elimu katika kuwezeshautekelezaji wenye ufanisi.Dkt. Aneth A. KombaMkurugenzi MkuuTaasisi ya Elimu Tanzaniaiv

YALIYOMOIdhini .iiiDibaji .ivOrodha ya Majedwali.viiVifupisho .1.0Utangulizi .1.1Sababu za Kuandaa Mtaala .1.2Muundo wa Mtaala wa Astashahada ya Ualimu ElimuMaalumu .2.0Muktadha wa Sasa wa Mtaala wa Mafunzo ya Astashahada yaUalimu Elimu Maalumu .2.1Mahitaji ya Kijamii .2.2Mahitaji ya Kiuchumi .2.3Matamko ya Sera .3.0Dira, Dhamira, Malengo na Ujuzi wa Jumla wa Mafunzo yaAstashahada ya Ualimu Elimu Maalumu .3.1Dira .3.2Dhamira .3.3Malengo ya Jumla ya Elimu, Mafunzo ya Astashahada yaUalimu na Ualimu Elimu Maalumu .4.0Muda wa Mafunzo ya Astashahada ya Ualimu Elimu Maalumu .4.1Miaka ya Mafunzo .4.2Muda wa Masoma .4.3Mihula ya Masomo .5.0Muundo wa Maudhui, Maeneo na Masomo ya Kujifunza .5.1Masomo ya Fani za Ualimu Elimu Maalumu .5.2Masomo ya Ufundishaji .6.0Viwango vya Rasilimali Katika Utekelezaji wa Mtaala .6.1Sifa ya Kujiunga na Mafunzo .6.2Sifa za Mkufunzi.6.3Sifa za Kiongozi wa Chuo.6.4Rasilimali vitu.7.0Njia za Kufundishia na Kujifunzia .viii11v12333777710101011111213383838383941

8.0Upimaji wa Maendeleo ya Mwalimu Tarajali .8.1Upimaji Endelevu .8.2Utahini wa Mafunzo kwa Vitendo .8.3Upimaji Tamati .8.4Mtihani wa Mwisho .9.0Ufuatiliaji na Tathmini ya Mtaala .9.1Ufuatiliaji wa Mtaala .9.2Tathmini ya Mtaala .Rejea .vi424242435556565759

Orodha ya MajedwaliJedwali la 1: Mchanganuo wa Vipindi kwa Wiki kwa Fani na Mchepuo.Jedwali la 2: Masomo katika Fani ya Ualimu Elimu Maalumu .Jedwali la 3: Michepuo na Masomo ya Ufundishaji katika Mafunzo yaAstashahada ya Ualimu Elimu Maalumu .Jedwali la 4: Umahiri Mkuu wa Masomo ya Fani kwa Mwalimu Tarajali .Jedwali la 5: Umahiri wa Jumla wa Somo na Umahiri Mkuu wa kila Fanikwa Masomo ya Ufundishaji kwa Mwalimu Tarajali .Jedwali la 6: Umahiri Mkuu wa Somo la Ualimu na Somo la Elimu1212Jumuishi.Jedwali la 7: Mpangilio wa Muda wa Mafunzo kwa Saa .Jedwali la 8: Upimaji wa Masomo ya Fani ya Astashahada ya Ualimu waElimu Maalumu .Jedwali la 9: Upimaji wa Masomo ya Mbinu za Kufundishia Masomo yaElimu ya Msingi .Jedwali la 10: Ufuatiliaji wa Mtaala.Jedwali la 11: Tathmini Endelevu .3537vii14151944535758

VifupishoKKKMKUKUTATEHAMATETUKIMWIVVUWyESTKusoma, Kuandika na KuhesabuMkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini TanzaniaTeknolojia ya Habari na MawasilianoTaasisi ya Elimu TanzaniaUpungufu wa Kinga MwiliniVirusi vya UKIMWIWizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojiaviii

1.0UtanguliziMtaala ni mwongozo mpana unaoweka viwango vya utoaji wa elimu kwakuzingatia maudhui na ujuzi watakaojifunza walimu tarajali kama vile maarifa,stadi na mwelekeo, njia za kufundishia na kujifunzia zitakazotumika katikautekelezaji wa Mtaala, vifaa vya kufundishia na kujifunzia vinavyohitajika,sifa za kitaaluma na kitaalamu za mkufunzi atakayeuwezesha mtaala,miundombinu wezeshi katika utekelezaji wa Mtaala, muda utakaotumikakatika ufundishaji na ujifunzaji, upimaji, ufuatiliaji na tathmini ya Mtaala.Kwa hiyo, Mtaala wa Mafunzo ya Astashahada ya Ualimu Elimu Maalumuuna mtazamo wa kisasa unaoonekana kama ni kioo kinachoakisi falsafa nautamaduni wa jamii, vikiwamo vyanzo vya maarifa na malengo ya elimuya nchi. Kioo hiki huonesha pia maarifa, stadi na mwelekeo unaotarajiwakumjenga mlengwa kumudu kufundisha masomo ya elimu ya msingi kwakuonesha njia za utahini, ufuatiliaji na tathmini.1.1Sababu za Kuandaa MtaalaMtaala huu wa Astashaada ya Ualimu Elimu Maalumu umeandaliwa kwakuzingatia Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014, Dira ya Maendeleoya Tanzania 2025, Malengo ya Maendeleo Endelevu 2015-2030, Mkakati waKukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA), Mkakatiwa Taifa wa Elimu Jumuishi wa mwaka 2009-2017 na Mkakati wa Taifa waElimu Jumuishi wa mwaka 2018-2021. Vilevile, Mtaala huu umezingatiamapendekezo ya tafiti anuwai za kielimu, hususani “Ripoti ya utafiti wakuboresha Elimu ya Msingi Tanzania Bara” ya Agosti, 2004 na “Ripoti yautafiti na maoni ya kuboresha Mtaala wa Mafunzo ya Ualimu Tarajali ngaziya Astashahada” ya mwaka 2018. Matokeo ya utafiti na maoni ya wadauyalidhihirisha umuhimu wa kuboresha Mtaala uliokuwa ukitumika kuandaawalimu kwa njia ya mafunzo kazini katika fani za Ualimu Elimu Maalumuwa mwaka 2012 ili kuandaa Mtaala wa Ualimu Elimu Maalumu ngazi yaAstashahada.1.2Muundo wa Mtaala wa Astashahada ya Ualimu Elimu MaalumuMtaala huu una sehemu tisa. Sehemu ya kwanza inahusu utangulizi wa mtaala.1

Sehemu nane zinazofuatia katika Mtaala huu zinaelezea muktadha wa Mtaalawa Mafunzo ya Ualimu Elimu Maalumu unaozingatia mahitaji ya kijamii nakiuchumi, dira, dhamira, malengo na ujuzi wa jumla wa Mtaala, muda wamafunzo, muundo wa maudhui, maeneo na masomo ya kujifunza, viwangovya rasilimali katika utekelezaji wa Mtaala, njia za kufundishia na kujifunzia,upimaji wa maendeleo ya mwalimu tarajali na ufuatiliaji na tathmini yaMtaala.Mtaala wa Mafunzo ya Astashahada ya Ualimu Elimu Maalumu utatekelezwakwa ufanisi kwa kufuata mwongozo unaobainisha masuala muhimu yaelimu, ikiwa ni pamoja na matamko ya Sera ya Elimu (2014) inayoelezamalengo ya elimu Tanzania. Ieleweke wazi kuwa kuna malengo makuu yakitaifa yanayotazamiwa kufikiwa pamoja na ujuzi wa jumla unaokusudiwakujengwa kwa mwalimu tarajali katika Mafunzo ya Astashahada ya UalimuElimu Maalumu. Katika Mtaala huu, mambo yafuatayo yameainishwa:Muda wa mafunzo, maudhui, masomo na maeneo ya kujifunza, viwango vyarasilimali vinavyohitajika katika utekelezaji wa Mtaala, njia za kufundishia nakujifunzia, taratibu za upimaji wa mwalimu tarajali na ufuatiliaji na tathminiya Mtaala.2.0Muktadha wa Mtaala wa Mafunzo ya Astashahada ya UalimuElimu MaalumuMadhumuni ya Elimu ya Ualimu Elimu Maalumu ni kujenga misingi yakielimu, kijamii na kiutamaduni kwa mwalimu tarajali katika kuwezeshaujifunzaji wa wanafunzi wenye mahitaji maalumu. Elimu hii inakusudiwakumwezesha kila mwalimu tarajali kupata maarifa, mwelekeo, ujuzi nastadi za msingi za ufundishaji na ujifunzaji, ujasiriamali pamoja na misingiya uongozi ili kukabiliana na changamoto mbalimbali katika mazingira yaufundishaji na ujifunzaji wa wanafunzi wenye mahitaji maalumu. Maendeleomakubwa na ya haraka katika sayansi na teknologia na hasa teknolojia yakupashana habari, yamesababisha mabadiliko makubwa ya uendeshaji washughuli za kiuchumi na kijamii katika kila nchi ikiwa ni pamoja na utoajiwa elimu kwa watu wenye mahitaji maalumu. Hivyo, Mtaala wa Mafunzoya Astashahada ya Elimu ya Ualimu Elimu Maalumu umezingatia mahitajihayo.2

2.1Mahitaji ya KijamiiTanzania ina jamii za watu wanaotoka katika makabila mbalimbali ambaowameunda Taifa moja linalotumia Kiswahili kama lugha ya mawasiliano.Lugha hiyo inawaunganisha watu hao katika shughuli zao za kila siku zamaendeleo. Mtaala wa Mafunzo ya Astashahada ya Ualimu Elimu Maalumuumezingatia mahitaji ya kijamii kwa kutumia lugha ya Kiswahili inayoelewekana inayotumiwa na watu walio wengi. Aidha, Mtaala umehusisha masualamtambuka yanayohusu utandawazi, teknolojia ya habari na mawasiliano(TEHAMA), elimu ya jinsia na utawala bora. Pia, yanayohusu stadi zamaisha, ujasiriamali, elimu jumuishi, maadili, ushauri na unasihi pamoja nahuduma za faraja kwa wanaoishi na virusi vya UKIMWI.2.2Mahitaji ya KiuchumiTanzania ni nchi ambayo ina raslimali nyingi kama gesi asili, madini ya ainambalimbali na mbuga za wanyama ambazo zinavutia watalii wanaotuleteafedha za kigeni. Hata hivyo, kutokana na maendeleo duni ya sayansina teknolojia pamoja na kutokuwepo kwa usawa katika soko la duniakumesababisha pato la nchi kuwa dogo na kufanya vyuo vya elimu ya ualimukutovutia wanafunzi wengi wa ualimu kujiunga navyo. Jitihada za makusudizinahitajika ili kufanya kada ya ualimu kuwa kivutio kwa Watanzania. Kwamantiki hiyo, Mtaala wa Mafunzo ya Astashahada ya Ualimu Elimu Maalumuumehusisha masuala ya ujasiriamali, stadi za kazi, michezo pamoja na sayansina teknolojia ili kumwezesha mwalimu tarajali kujitegemea kwa kutumiaelimu atakayoipata kutambua jinsi ya kutumia rasilimali zilizopo kupatamahitaji yake ya msingi na kumfanya kuwa na maendeleo endelevu yenyeufanisi katika jamii. Aidha, elimu itakayotolewa itaunganisha nadharia navitendo ili kuleta tija kwa mwalimu tarajali na mwanafunzi atakayefundishwana mwalimu huyo baada ya kuhitimu.2.3Matamko ya SeraKatika uboreshaji wa Mtaala huu wa Mafunzo ya Astashahada ya UalimuElimu Maalumu, sera mbalimbali za kimataifa na za kitaifa zimezingatiwaili kumuandaa kikamilifu mwalimu tarajali aweze kupata elimu boraitakayomwezesha kuwa mwalimu mahiri wa Elimu Maalumu.3

2.3.1Sera za KimataifaSera za kimataifa zilizozingatiwa ni kama zifuatazo: Azimio la Umoja waMataifa la Haki za Binadamu la mwaka 1948 linalosisitiza haki ya elimu, Seraya Haki za Mtoto ya mwaka 1989 ihusuyo mataifa kutoa elimu kwa watotowote na Sera ya Elimu kwa Wote ya mwaka 1990 inayolenga utoaji wa elimubila kujali tofauti za kimaumbile. Kadhalika, Mtaala umezingatia Kanuni zaUmoja wa Mataifa za fursa sawa kwa watu wenye ulemavu za mwaka 1994zinazohimiza fursa sawa katika utoaji wa elimu ya msingi, sekondari na vyuokwa watoto, vijana na watu wazima wenye mahitaji maalumu. Aidha, Mtaalaumezingatia kuwapo kwa malengo ya Maendeleo ya Milenia ya mwaka 2000,kipengele cha 2 na 3 vinavyotoa haki ya elimu kwa watoto wote na elimuya jinsia ambayo inalenga kuendeleza na kukuza ujifunzaji unaozingatiakuimarisha ukuzaji wa uchumi, viwanda, ugunduzi, ajira na kuwa na uwianosawa katika uzalishaji.Pia, malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2015-2030, namba 4 na 5 yanasisitizakuhakikisha kunakuwapo elimu jumuishi ambayo ni bora kwa wote katikakukuza ushiriki wa wadau katika elimu. Vilevile, yanasisitiza kuimarishauwazi miongoni mwa watendaji, matumizi bora ya rasilimali, uwekaji nausimamizi wa mipango, tathmini na utekelezaji wa malengo ya sekta ndogoza elimu, ikiwemo elimu ya msingi, sekondari, ualimu na ufundi. Malengohaya endelevu yanalenga katika kuwapo kwa elimu jumuishi na yenyeuwiano kwa ngazi zote za elimu na fursa za elimu endelevu. Kati ya malengohayo 17, lengo namba nne (4) linasisitiza kuhakikisha utoaji wa elimu borana yenye usawa kwa wote na kutoa fursa kwa wote katika elimu endelevuili kukuza ujifunzaji. Hata hivyo, kati ya malengo hayo 17, saba yanajikitakatika uzingatiaji wa ujumuishi. Malengo hayo ni: Kuondoa umaskini nakuboresha kilimo, usalama wa chakula na lishe; kudumisha mifumo yamaisha ili kuimarisha afya na hali bora kwa watu wa rika zote; kuhakikishaelimu bora inatolewa kwa watu wote; kudumisha haki na usawa ndani ya nchina baina ya nchi na nchi pamoja na kuboresha makazi ya watu kuwa salama,yenye amani na yaliyo katika mifumo ya haki. Hali kadhalika, yanahimizwapia masuala ya kuhakikisha upatikanaji wa nishati salama, maji safi na salamana usafi wa mazingira kwa watu wote.4

Malengo mengine ni pamoja na kuimarisha ukuzaji wa uchumi, viwanda,ugunduzi, ajira, uwiano katika uzalishaji na matumizi na ujenzi wamiundombinu; na kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa, ukuzaji bora wamazingira, matumizi mazuri ya rasilimali za majini, mfumo wa teknolojia nakuhakikisha wanyama na mimea wanakaa pamoja kwa kutegemeana.2.3.2Sera za KitaifaElimu ya Kujitegemea ndiyo sera kuu ya kitaifa ambayo inasisitiza ugunduzina ubunifu, kujiamini, stadi za utatuzi, kuunganisha nadharia na vitendo,ujasiriamali, teknolojia na udadisi katika elimu. Falsafa hii ya elimu yakujitegemea imejitokeza katika sera mbalimbali za elimu ambazo zinatumikakatika utoaji wa elimu nchini, hususani hizi zifuatazo:2.3.2.1 Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 imesisitiza upatikanaji wa elimu namafunzo kwa watu wote bila kujali jinsia, rangi, kabila, dini, ulemavu na haliya kijamii au kipato. Pia kuwapo mfumo wa elimu na mafunzo unaozingatiamasuala mtambuka yakiwamo elimu ya mazingira na maambukizi ya Virusivya UKIMWI (VVU). Kwa mujibu wa Sera ya Elimu ya Mafunzo ya Mwaka2014, lugha rasmi ya kufundishia Elimu ya Msingi pamoja na maandalizi yawalimu tarajali wa vyuo vya ualimu ngazi ya Astashahada ni Kiswahili, nalugha ya Kiingereza itafundishwa kama somo la lazima. Sera pia imesisitizauandaaji wa walimu mahiri ili kukidhi mahitaji ya sekta ya elimu. Hivyo,Mtaala wa Mafunzo ya Astashahada ya Ualimu Elimu Maalumu umeandaliwaili kukidhi matakwa ya kisera ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014.2.3.2.2 Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025Dira ya Maendeleo ya Taifa kufikia mwaka 2025 imelenga kukuza maendeleoya jamii, hususani kutoa elimu bora kwa lengo la kuendeleza walengwakatika ubunifu, ugunduzi au uvumbuzi, maarifa na stadi mbalimbali ili kupatawataalamu wenye uwezo wa kutatua matatizo ya jamii, kukuza utumiaji wasayansi na teknolojia na utoaji wa elimu kwa vitendo katika ngazi zote.5

2.3.2.3 Mkakati wa Taifa wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini(MKUKUTA)Mtaala huu pia umezingatia malengo yaliyomo katika Mkakati wa Taifa waKukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUKUTA) ambao umelengakuwa na mfumo wa elimu utakaowapa walengwa maarifa, stadi na mielekeochanya ya kushiriki vyema katika kujiletea maendeleo yao wenyewe. Halihiyo italeta tija kwa mtu binafsi na kwa taifa kwa ujumla na hivyo kupunguzaumaskini.2.3.2.4 Sera ya Huduma na Maendeleo kwa Watu wenye Ulemavu yamwaka 2004Sera ya Huduma na Maendeleo kwa Watu wenye Ulemavu ya mwaka 2004inalenga upatikanaji wa huduma za afya, elimu, ajira, habari na uandaajiwa mazingira rafiki kwa watu wenye ulemavu. Hivyo, sera inasisitiza watuwenye ulemavu kupatiwa mafunzo ya stadi za maisha ili waweze kujitegemeana kumudu mazingira wanayoishi.2.3.2.5 Sheria ya watu wenye Ulemavu ya mwaka 2010Sheria ya watu wenye ulemavu namba 9 ya mwaka 2010 inasisitiza utoaji waelimu kwa kuzingatia mahitaji ya mwanafunzi mwenye mahitaji maalumu.2.3.2.6 Mkakati wa Taifa wa Elimu Jumuishi wa Mwaka 2018-2021Mkakati wa Taifa wa Elimu Jumuishi wa mwaka 2018-2021 unalenga katikakuhakikisha kuwa watoto wote, vijana na watu wazima wanapata elimuiliyo bora na kwa usawa katika mazingira jumuishi. Mkakati huu unasisitizaufundishaji n

fedha za kigeni. Hata hivyo, kutokana na maendeleo duni ya sayansi na teknolojia pamoja na kutokuwepo kwa usawa katika soko la dunia kumesababisha pato la nchi kuwa dogo na kufanya vyuo vya elimu ya ualimu kutovutia wanafunzi wengi wa ualimu kujiunga navyo. Jitihada za makusudi zinahitajika i

Related Documents:

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekuwa ikiboresha Mtaala wa Elimu ya Msingi kuhakikisha kwamba elimu inayotolewa ni bora na inayomwandaa mwanafunzi kumudu maisha katika mazingira yake. Muktadha huu umeifanya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia iboreshe mchakato wa kufundisha

wizara ya elimu, sayansi na teknolojia cheti cha ualimu elimu ya awali matokeo ya mtihani wa mwisho wa muhula wa ii juni 2019 wanachuo wa mwaka wa kwanza i i ja ict ja i ja ills ja u ja ct ja hili ja a ja ia ja o ja ia ja la ni ja i oni e512/283 nicodem herry swetala me 78 a 67 b 74 b 66 b 8

P a g e 1 of 6 by Mong are Teachers College, Hai Kilimanjaro,March 2020 www.mongarecollege.ac.tz for Online Downloads. WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA MONG ARE TEACHERS COLLEGE S.L.P 215 HAI, KILIMANJARO. SIMU: Mapokezi-0755 679 228 , Msajili-0

3.0 VIPAUMBELE VYA WIZARA YA ELIMU, SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UFUNDI 10. Mheshimiwa Spika, Dira ya Maendeleo ya Taifa (2 025) imelenga kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025. Katika juhudi za kufikia lengo hili, Wizara ya E

WIZARA YA ELIMU SAYANSI, TEKNOLOJIA NA MAFUNZO YA UFUNDI DARASA IV – KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA MWANAFUNZI: _ MAELEKEZO 1. Kumbuka kuandika majina yako matatu kwa usahihi. 2. Jibu maswali yoe kulingana na maelekezo. 3. Soma maswali kwa ufasaha kabla ya kuyajibu

(2019). Muhtasari wa Somo la Maarifa ya Jamii Elimu ya Msingi Darasa la III-VII. Dar es Salaam: Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kunakili, kurudufu, kuchapisha wala kufasiri andiko hili kwa namna yoyote ile bila idhini ya maandishi ya Kamishna wa Elimu,

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Imefadhiliwa na Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DFID) Agosti, 2017 MPANGO WA UTAYARI WA KUJIUNGA NA ELIMU YA SEKONDARI (MUES) EQUIP-Tanzania. Mpango wa Utayari wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari (MU

· Single-copy, protein-coding genes · DNA present in multiple copies: Sequences with known function Coding Non-coding Sequences with unknown function Repeats (dispersed or in tandem) Transposons · Spacer DNA Numerous repeats can be found in spacer DNA. They consist of the same sequence found at many locations, especially at centromeres and telomeres. Repeats vary in size, number and .