AAP 64 (2000): Swahili Forum VII 145-152 NAFASI YA .

2y ago
40 Views
2 Downloads
567.25 KB
8 Pages
Last View : 26d ago
Last Download : 3m ago
Upload by : Elise Ammons
Transcription

AAP 64 (2000): Swahili Forum VII 145-152NAFASI YA MUZIKI ULIOPENDWA KATIKA FASIID YA KISWAHILIPAMELA M. Y NGUGIInkisiriNyimbo, kama tanzu ya fasihi yeyote ile zina majukumu mbalimbali ambayo hutekeleza katikajamii. Lengo kuu la fasihi ni lile la kuielimisha na hata kuiburudisha jamii. Ndivyo ilivyo katikanyimbo kwa sababu kupitia kwazo wanajamii huburudika na kuelimishwa . Ni kwa sababu hiyondipo makala hii inalenga kuangalia nafasi ya nyimbo zinazopendwa katika fasihi ya Kiswahili.Huu ni utanzu ambao huwafikia watu wengi katika jamii. Kutokana na kutumia lugha yaKiswahili, utanzu huu unaweza kueleweka na Wakenya wingi. Nchini Kenya, vyombo vya habarivimeipa fasihi hii nafasi kubwa sana na hivyo basi kuipanua hadhira yake. Hii ni kutokana nasababu kuwa fasihi hii inathaminiwa sana na wengi na ipewe nafasi kubwa katika vyombo vyahabari hasa katika redio kwa muda mrefu. Ni kutokana na sababu hii ndipo tunajaribu kuonyeshanafasi yake katika fasihi ya Kiswahili .MakalaMahusiano ya kijamii hujengwa kutokana na historia, mazingim na shughuli za watu za kila sikuna imani yao pia . Watu wa jamii moja mara nyingi husikilizana kwa lugha, mila na desturi.Misingi hiyo ya utamadununi na utamaduni wenyewe huwa ni vigezo maalum vya kumfanya mtuaitambue nafasi yake katika jamii na vile vile kutambua wajibu wake na majukumu yake, Mazrui(1986).Tanzu mojawapo inayodhihirisha utamaduni wa jamii ni muziki wake . Wasanii hawa, hasawaimbaji wanaoimba kwa lugha ya Kiswahili nyimbo ambazo twaweza kuziita nyimbo-pendwawamechukua nafasi kubwa katika kukuza lugha hii, utamaduni na mawasiliano .

146PAMELA M. Y NGUGIMuziki umekuwa chombo ambacho kimewavutia wanadamu. Jambo hili limewafanya watu wamatabaka mbalimbali wakiwemo wanafalsafa na watu wa kawaida kujru:ibu kuelewa muziki lakini hakuna fasili ambayo imeweza kueleza muziki ni nini hasa: Uasili wake haujulikani, kamaanavyodai Schumann katika kofia (1994) kuwa:"Sayansi hutumia hisibati na umantiki, ushaiii nao hutumia maneno teule. . muziki niyatima ambaye babake na mamake hawajulikani kamwe . Hata hivyo, ni huu utata wauasili wake ambao umefanya muziki uonekane kuwa kitu bora zaidi katika jamii"(Tafsiii yangu).Katika kutumia nyimbo, waimbaji hawa wameweza kuhifadhi historia na utamaduni wa jamiizao . Hata hivyo, hivi sasa utaona kuwa maendeleo ya kisayansi na teknolojia yameanza kuiingizajamii nyingi katika fasihi ya televisheni na video na hivyo kuonekana kama kwamba jambo hililinafifisha stru:ehe inayopitikana katika nyimbo (Mlacha, 1998}.Dhru:nlla kuu ya makala haya ni kuangalia nafasi ya nyimbo-pendwa katika fasihi ya Kiswahili.Mabadiliko katika jamii yamesababisha mabadiliko katika nyimbo na hivyo basi nyimbozimekuwa na maudhui na fani tofauti kutegemea namnajamii ilivyobadilika.Uchunguzi uliofanywa juu ya nyimbo umeonyesha kuwa nyimbo ni kipengele muhimu sanakatika jamii zote ulimwenguni. Nyimbo ni utanzu uliothaminiwa sana, na zilitawala katikamifumo yote yajamii, Brandel (1959). Akuno (1999) anasema kuwa muziki ni zaidi ya sauti tuambazo huimbwa na kuchezwa. Muziki sio wazo la dhana fulani bali ni tajriba, ni tukio ambalohuwasilisha mambo mbalimbali yenye umuhimu katika jamii husikaAkuno anaonanyimbo/muziki ukiwa na uamali wa kiujozi: Kwanza ni kama kiburudisho, muziki huendelezauhusiano wa mtu binafsi, humstru:·ehesha na kumwezesha mtu huyu kuwasilisha hisia zake Nakama tambiko, muziki huendeleza uhusiano wa kimazingiia - kwa kuwahusisha wanadamu naviumbe vingine vinavyopatikana katika mazingiia hayo.Katika kuangalia upande wa kijru:nii, Akuno anaona muziki kama chombo ambacho hutumiwakuelezea histmia ya jamii, hutumiwa kupasha 11iumbe maalum kwa wanajru:nii hasa kutoka kizazikimoja hadi kingine na hutumiwa hasa kuelezea histmia, imani, itikadi na kaida zajamii. Nyimboni zao la mazingiia ya jamii. Zinaweza kufananishwa na mtoto ambaye hufinyangwa na mambo

MUZIKI ULIOPENDWA KATIKA FASIHI YA KISWAHILI147mengi katika historia ya jamii yake . Hii inamaanisha kwamba muziki hauibuki katika ombwetupu na hauwezi vilevile kujiundia mazingira yazo yenyewe. Mabadiliko na maendeleo ya muzikiyamekuwa yakifuatana na historia ya watu wenyewe. Nyimbo huathiriwa sana na mamboyanayotendeka ulimwenguni .Umuhimu wa muziki unadhihirika katika matumizi ya nyimbo katika wakati maalum kama njiamojawapo ya kuanzisha mabadiliko katika tabia za jamii au mtu binafsi, (McAI!ester 1971).Muziki umetumika kama njia mojawapo ya kujifundisha utamaduni na aghalabu hutumiwa katikakuelezea mtu mazingira yake na jinsi anavyoweza kuyatumia na kuyatunza vilivyoNyirnbo vi1evile zimekuja kuchukuliwa kama chanzo cha elimu na jinsi ya kujieleza katika jamiina hasa katika sana ya ma.zllngumzo Nyimbo humfanya mtu jenge kumbukumbu ya vitu autukio kwa urahisi na kumbukumbu hiyo huweza kudumu kwa muda mrefu sana . Kwa mfano,masomo shuleni hufanikishwa kupitia nyimboMuziki ulioimbwa kwa Kiswahili ni sehemu muhimu sana zirrazojenga utamaduni wa Wakenya.Kwa Wakenya wengi muziki ni neno lirraloeleweka kwa wananchi wengi kwa sababu watu haohuwa na upenzi wa muziki Kuhusu muziki ni nini, tunaweza kusema ni taaluma maalum ya sautiinayochanganya kwa usahihi sanaa na sayansi. Muziki ni sanaa katika matokeo na utendaji wakena ni sayansi katika maandalizi yake na utendaji, (Sekella, 1995).Wanamuziki wa Kenya wamegawanyika katika makundi mbalirnbali:- Watendaji wa muziki wabendi, kwaya, taarabu na watendaji wa muziki wa kiasili . Karibu kila kundi hutumia lugha yaKiswahili linapokuwa na ujumbe maalum kwa wananchi. Muziki wa kiasili nao huwezakugeuzwa maneno ya lugha ya kiasili ya wimbo unaohusika hadi katika lugha ya kiswahili iliujumbe wake uweze kueleweka kwa wasikilizaji wengi.Kenya irnepitia hatua mbalirnbali ya mabadiliko . Hatua hizi zirneathiri nyimbo kwa njia tofautitofimti. Tunacho kipindi kabla ya wageni au wakoloni. Huu ndio wakati ambapo nyimbozilizoimbwa zilikuwa nyimbo za kikabila Wanajarnii, kulingana na lugha zao za mama walibuninyimbo zao . Kipindi cha pili ni cha maajilio ya wazungu . Hiki ni kipindi ambacho mwafrikaalidhalalishwa na mzungu. Hii ilikuwa dhuluma ambayo ilivuka mipaka ya uchumi na siasa

148PAMELA M. Y NGUGIikafikia hadi kwenye hali ya kumteka mwafrika kimawazo asiweze kuonea nyimbo zake fahru:i.Hapa ndipo mwafiika alipojiona kwru:nba yeye hakuwa na uwezo wa kufanya chochote na hatanyimbo zake hazikuwa na maana yoyote . Kipindi hiki kilishuhudia nyimbo za kutoka nje naru:nbazo zilianza kuonewa fahru:i Watu walianza kwenda katika majumba ya stru:·ehe ili kuchezadensi. Lugha iliyopendelewa sana ilikuwa ni Kingereza . Hata hivyo nyimbo hizi hazikuwafikiawatu wengi kwa sababu idadi ya watu waliokifahru:nu Kingereza ilikuwa ndogo nmo.Hata hivyo, waimbaji wachache waliendelea kutumia lugha ya Kiswahili katika muziki wao.Waimbaji kama vile Fadhili Williru:n, Daudi Kabaka, John Mwale na wengineo ni baadhi yawanru:nuziki ru:nbao bado wanasifika sana katika kuimba kwa Kiswahili. Hawa ndio watuwaliosaidia kufanikisha lugha ya Kiswahili katika miaka ya sitini, na nyimbo zao zikajulikanakama nyimbo "zilizopendwa" hadi wa sasa. Hivi sasa kuna bendi nyingi zinazoimba kwaKiswahili, hizi ni pru:noja na "Them Mushrooms", Princess Jully", Munishi na nyingine nyingiru:nbazo zinapendwa na idadi kubwa ya watu . Wanainchi, kwa bahati nzuri hupendelea muzikiwenye ujumbe na hasa ujumbe ulio katika lugha wanayoielewa ya Kiswahili. Na nyingi ya bendihizi hutimiza wajibu huu.Sanaa ya uimbaji inaonyesha uwezo wa binadamu wa kusimulia au kupasha tajriba yake na yajru:nii ya kila siku na kujru:ibu kuleta maana katika maisha ya kila siku . Mru:nbo haya hufimyikakwa njia ya ukawaida nmo - kupitia kwenye nyimbo zilizopendwa. Nyimbo hizi huweza hatakuundwa upya na wananchi wenyewe kwa sababu mbalimbali.Kama asemavyo Cru:npbell (1976) nyimbo zimeundwa kru:na sanaa nyingine ili kunasa makiniyetu. Sanaa hii basi ina ule ukale, uleo na hata ukesho. Kupitia nyimbo zilizopendwa,wanru:nuziki wa Kiswahili wanaweza kuangalia 'usasa' au dunia ya leo hapo baadaye, usasa huuutakuwa kama ukale utakao tuelekeza kufahru:nu histmia yetu ya wakati huo. 'Usasa' huuunaweza kutusaidia katika kutab:iii ukesho na kujua nru:nna ya kukabiliana na ulimwengu ujao .Muziki umetumiwa katika kupinga ukandru:nizwaji na uonevu katikajru:nii. Hapa ni pale ru:nbapomwanru:nuziki anaangalia mru:nbo ya kisiasa. Jru:nbo hili lilidhihiiika wakati wa ukoloni ru:nbapomwafiika alitumia nyimbo kru:na silaha kupigania uhmu. Muziki ulitumiwa kuwahimiza watu

MUZIKI ULIOPENDWA KATIKA FASIHI YA KISWAHILI149wapinge tamaduni za wakandamizaji. Waafrika walifanya hivi kwa kuchukuwa nyimbo zakisiasa na kuzipa mahadhi ya kidini ambapo kwa hakika maana ilikuwa tofauti na ile ya kidiniHivi sasa wanamuziki wa nyimbo zilizopendwa wanaimba nyimbo zinazowaelimisha nakuwahamasisha watu ili watekeleze kwa ufanisi sera na maagizo mbalimbali ya chamakinachotawala na serikali kwa jumla. Nyimbo nyingi zinazosikika redioni zinahusu kuwahimizawatu kuwa na uwajibikaji, kilimo cha kisasa, uzazi wa mpango, vita dhidi ya Ukimwi, kuchaguaviongozi bora na kufanya kazi kwa bidii . Lugha ya Kiswahili imetumika kuimba nyimbo zenyeushaUii kuhusu maisha, mapenzi, tabia i na mbaya, ukulima bora na kadhalika .Muziki hasa muziki wa 'zilizopendwa' ni sanaa ambayo huwaflkia watu wengi kupitia vyombovya habari hasa redio na hata televisheni. Kwa hivyo hii ni sanaa ambayo haiwezi kupuuzwakutokana na majukumu mbalimbali inayotekeleza. Vyombo vya habari virnetenga masaa kadhaaya kuwabUiudisha watu kwa kuturnia nyimbo mbalimbali. Balisidya (1987) anakubali kuwasanaa hii ni sehernu mojawapo ya fasihi ya Kiswahili na inahitaji kufanyiwa uchunguza zaidi,kwa jinsi ambavyo watu wengi wanaweza kuipata .Nyimbo za kisasa zinaweza kutupa rnwangaza kuhusu maisha ya watu duniani. Finnegan (1970),anaserna kuwa nyirnbo-pendwa zina majukumu mbalimbali ya kutekeleza hasa katika kuangaliamitazamo ya jamii kiulimwengtl, na nyirnbo hizi hutekeleza majukumu haya kama zilivyonyimbo za kijadi Mtazamo huu umeungwa rnkono na watu kama vile Kabira na Mutahi (1988),Agovi (1989), na wengine wengi ambao wanaona rnuziki kuwa utanzu teule inayodhihi!ikakatika jamii hii inayobadilika. Nyimbo pendwa zimechukuliwa na wasomi wengi kuwa kamamuingiliano wa masimulizi jadi na ukweli wa maisha ya hivi sasa, Nyimbo hizi amaishani,unyimwajiwahakinaumaskini/ubinafsi. Mambo haya ni mambo ya kisasa na huathi!i wanajamii kwa njia mbalimbali.Wairnbaji wa nyimbo zilizopendwa hushughulikia nyanja tofauti za maisha ya jarnii kama viledini, uchurni na siasa. Kwa mfano, wao wanashughulikia ndoa na mapenzi kwa kuonyesharnahusiano ya Iqjamii na migongano ya kirnawazo baina ya wazee na vijana au baina ya rnke namurne . Katika nyakati hizi za mabadiliko katika uchumi na siasa waimbaji wamekuwa wakitunganyimbo kwa kutuchorea picha ya jinsi mambo yalivyo. Wamekuwa katika mstaii wa rnbele

150PAMELAM. Y NGUGIkatika kuwatahadhruisha wanajamii kuhusu ugonjwa wa Ukimwi .Muziki uliopendwa katika Kiswahili ni sanaa isiyo kuwa na mipaka ya ukabila. Ni sanaa ambayohuwaunganisha watu wa makabila mbalimbali kwa kutmnia lugha inayoeleweka na kuzungumziatajriba sawa wanazozifahamu. Nyimbo hizi pia zimetumika kuimulika jamii kwa kuonyeshamaendeleo yaliyopatikana katika nyanja mbalimbali Anapoikosoa jamii, mwimbaji huwaanachukuwa jukumu la kuhakiki jamii na hata kuielekeza. Nyimbo hizi pia zinatmniwakuwazindua watu waweze kufahamu haki zao hasa pale wanaponyimwa, zinatmniwa kama ajentiwa ukombozi .Katika nyimbo hizi, pia kuna ufasihi hasa upande wa lugha. Sifa moja ambayo hubanisha nyimboni matmnizi yake ya lugha hasa zile tamathali za usemi kama vile tashbihi, methali, semi,jazanda taashira na majina ya majazi. Tamathali hizo zinazotumiwa na nyimbo huwa amazimebuniwa katika jamii ya mwimbaji au zimebuniwa na mwimbaji mwenyewe lakiniakazingatia kanuni za uundaji wake. Hii inafanya tanzu hii iweze kuchunguzwa kwa makinikiusomi kwa kuchanganua ufani wake kupitia lugha iliyotumika .Hata hivyo, waimbaji wa nyimbo-pendwa wamekumbana na vizingiti vingi. Kutokana na sababukuwa wao ni wahakiki wa jrunii, baadhi ya nyimbo zao zimepigwa mruufuku, (mwangi 1992) nahivyo basi haziwaflkii watu wengi waliolengwa na haziwezi kutumiwa kama njia ya kuwazinduawatu. Katika kule kuihaki jamii, wao-hulenga kuikosa, lakini mrua nyingi wao huwa hawafikianina viongozi kuhusiana na maongozi yao .HitimishoNyimbo zinazoimbwa kwa lugha ya Kiswahili huwaflkia watu wengi kutokana na sabau kuwalugha ya Kiswahili ni lugha ya walio wengi. Nyimbo zilizopendwa zitaendelea kukua kufuatanana mabadiliko ya kihistoria na kifani ambayo yanasababishwa na watu wengi. Hivyo · basi,nyimbo hizi hazina budi kuchukuliwa kama sehemu moja ya Fasihi ya Kiswahili kwa kuangaliamchango wake kimaudhui na kifani. Na zinahitaji kusambazwa ili ziwafikie wanajamii wote . Hiiina maanisha kuwa vyombo vya habrui vina majukumu ya kutekeleza katika kuhakikishakwamba watu wengi wameweza kuzipata nyimbo hizi . Kwa upande wa fasihi, haya ni mafanikio

MUZIK.IUL IOPENDWA KATIKAFA SIHIYAK.IS WAHILI151makubwa hasa kwa sababu tabia ya kupenda kusoma haijakomaa kwa wengi. Vyombo vya habmivinatumika kusainbaza fasihi hii kwa mainilioni ya watu. Hii ni kutokana na sababu kuwa kundim jatu la waimbaji linaweza kufundisha idadi kubwa ya watu kwa wakati mmoja kuputianyimbo zao .MarejeleoAbdalla, A 1975 Utanzu wa Ushaiii wa Kiswahili na Maendeleo yake. Wasilisho lililotolewakatika idma ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dm es Salaam.Agovi, K 1989. The Political Relevance of Ghanaian Highlife Songs Since 1975, Research inAftican Literature 20, 2: 194-201 .Akuno, E. A. 1999 . A conceptual Frainework for Research in Music Education within a CulturalContext Paper presented at cultural week seminm, Kenyatta University, NairobiBalisidya M 1987. Adopted or Adapted? To New Swahili Oral Literature in Kiswahi1i, Kiswahili54/LBrandel, R. 1959. The Music of Central Africa An Ethnomusicological study. London: MethuenCainpbell, CA. 1976. An Introduction to the Music ofSwahili Women, Seminm paper No 68University ofN airobi.Finnegan, R. 1970. Oral Literature in Aftica. Oxford: Oxford University Press .Kemoli, A1978. Music and the Creative Imagination of Afiica, in: Teaching of Afticanliterature in schools, Vol. L Nairobi: Kenya Literature Bureau .Kofie, N. N. 1994. Contemporary Aftican Music in World Perspective . Accra: Ghana UniversityPress.Lukas, G. 1956. Studies in European Pluralism . London: Hillway Publishing Co .Mazrui, A 1986. The Afticans, London: BBCMcAllester, D. 197L Readings in Ethnomusicology . New York: Reprint Corporation.

152PAMELA M. Y NGUGIMutahi, K. and Kabira, W. 1988. Gikuyu Oral Literature, Nairobi: Heinemann.Mutembei, A K. 1995 Korasi na Uhusiano wake na Sanaa za Maonyesho: Uchambuzi waKidayakronia, Kioo cha Lugha, Dares Salaam: Chuo Kikuu cha Dares Salaam.Mwangi, M. 1992. When KBC saysf No way, Daily Nation, 24th July 1992 .Ngngi wa Thiong'o . 1981.Writer in Politics, Nairobi: Heinemann .Sekella, M. 1995. Kiswahili katika Muziki wa Tanzania, katika Kiswahili na Vyombo ryaHabari . Dar es Salaam: Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar esSalaam.Yalwala PM 1991. Uhakiki wa Maudhui Katika Nyimbo za John Mwale . Unpublished M AThesis, University of Nairobi.

Kwa hivyo hii ni sanaa ambayo haiwezi kupuuzwa kutokana na majukumu mbalimbali inayotekeleza. Vyombo vya habari virnetenga masaa kadhaa ya kuwabUiudisha watu kwa kuturnia nyimbo mbalimbali. Balisidya (1987) anakubali kuwa sanaa hii ni sehernu mojawapo ya fasihi K

Related Documents:

pop marson star celus cherry gesipa ada32 aba32 ad32abs ab3-2a - a/a32d aap-32 gamd32a ada34 aba34 ad34abs ab3-4a - a/a34d aap-34 gamd34a ada41 aba41 ad41abs ab4-1a 4-1aad a/a41d aap-41 gamd41a ada42 aba42 ad42abs ab4-2a 4-2aad a/a42d aap-42 gamd42a ada43 aba43 ad43abs ab4-3a 4-3aad a/a43d aap-43 gamd43a

Teach Yourself Swahili (1996/2003) by Joan Russell, Swahili: A Foundation for Speaking, Reading, and Writing (1979/1998) by Hinnebusch and Mirza, and Let’s Speak Kiswahili: A Multidimensional Approach to the Teaching and Learning of Swahili as a Foreign Language

AFRICA’S ETHNIC GROUPS Arabs, Ashanti, Bantu, & Swahili . AFRICAN ETHNIC GROUPS AND THEIR . Swahili is a mixture of Bantu and Arab culture . While the Swahili language is considered a Bantu language, there are many Arabic words and phrasesFile Size: 1MB

ELEMENTARY SWAHILI 5 1. Introduction to Swahili Swahili or Kiswahili is a bantu language that is spoken in East Africa/Afrika Mashariki.It is both a national and official language in Kenya and Tanzania and

Mchango wa Fasihi ya Kiswahili katika Kuudumisha Utambulisho wa Kiswahili : Mifano Kutoka Kazi za Fasihi za Kiswahili Dk. Wael Nabil Ibrahim Othman* Abstract This study emphasizes that the Swahili literature has a very big role in consolidating and maintaining Swahili identity. In the field of Swahili poetry

Apprendre le Swahili Le swahili est certainement l'une des langues africaines les plus faciles à apprendre car elle ne comporte pas de sons "bizarres" imprononçables pour un français, pas de "tons" comme

A - THE SWAHILI ALPHABET : The basic principle which was retained to establish the Swahili alphabet, is that every distinct sound or phoneme should always be transcribed by the same distinct written form (either a single letter, or a cluster of letters), and con

GRAMMAR The Focus of This Boot Camp Lesson is Using Swahili Phrases to Learn More about Kenya. First Phrase: Kunradhi, Unasemaje -----kwa Kiswahili. Kunradhi ("Excuse me") SWAHILIPOD101.COM BASIC BOOTCAMP S1 #3 - USEFUL PHRASES FOR LEARNING SWAHILI 6 The rst word in this sentence means "excuse me" and has the same usage as in .