Kuchunguza Tamathali Za Usemi Katika Mashairi Ya Magazetini: Uchunguzi .

1y ago
8 Views
1 Downloads
560.04 KB
128 Pages
Last View : 11d ago
Last Download : 3m ago
Upload by : Brady Himes
Transcription

KUCHUNGUZA TAMATHALI ZA USEMI KATIKA MASHAIRI YAMAGAZETINI: UCHUNGUZI KIFANI WA MASHAIRI YA UKIMWIKATIKA MAGAZETI YA KISWAHILIOMARI MTUNGUJA KOMBOTASINIFU ILIYOWASILISHWA KWA AJILI YA KUTIMIZA SHARTIPEKEE LA KUTUNUKIWA DIGRII YA UZAMILI (M.A KISWAHILI) YACHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA2014

iiUTHIBITISHIMimi Profesa T.S.Y.M. Sengo ninathibitisha kuwa nimesoma tasinifu hii iitwayoKuchunguza Tamathali za Usemi katika Mashairi ya Magazetini: Uchunguzikifani wa Mashairi ya UKIMWI katika Magazeti ya Kiswahili na ninapendekezaikubaliwe na Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania kwa ajili ya kukamilisha masharti yaDigrii ya M.A. Kiswahili ya Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania.Sheikh, Daktari, Professa T.S.Y. SENGO(Msimamizi)Tarehe

iiiHAKIMILIKIHairuhusiwi kuiga au kunakili kwa namna yoyote sehemu yoyote ile ya tasinifu hiikwa njia yoyote kama vile, kielektroniki, kurudufu nakala, kurekodi au njia yoyotenyingine bila ya idhini ya mwandishi au Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kwa niaba.

ivTAMKOMimi Omari Mtunguja Kombo, ninathibitisha kuwa tasinifu hii ni kazi yangu halisina haijawahi kuwasilishwa katika Chuo Kikuu kingine chochote kwa ajili yakutunukiwa shahada kama hii au nyingine yoyote. .Sahihi .Tarehe

vTABARUKUNinapenda kuitabaruku kazi hii kwa wazazi kwa wazazi wangu, wake zangu nawatoto wetu wapendwa.

viSHUKURANIKazi hii ya utafiti ni matokeo ya mchango na ushirikiano kati yangu na watuwengine wakiwemo walimu wangu. Kwa kuwa sio rahisi kuandika kwa kinamchango wa kila aliyenisaidia kukamilisha kazi hii, wafuatao wanastahili shukraniza kipekee. Kwanza napenda kumshukuru Mungu kwa kunijalia nguvu na uelewakipindi chote cha masomo yangu hata kukamilika kwa kazi hii.Pia napenda kutoa shukurani zangu za pekee kwa msimamizi wangu wa tasinifu hii,sheikh, daktari, professa, T.S.Y. Sengo kwa kuniongoza vyema katika kila hatua yautafiti huu. Hakusita wala kuchoka kunishauri na kuirekebisha kazi hii katika hatua zotempaka ilipokamilika. Usaidizi wake hauwezi kukisiwa wala kulipwa. Ninachowezakusema ni asante sana professa, Mungu akubariki na kukujalia afya njema na maishamarefu.Napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa familia yangu nikianza na wake zanguTatu Mwokeachao Omar na Mariamu Mwiduchi Omar. Ninawashukuru sana kwauvumilivu wenu hasa katika kipindi ambacho nilikuwa mbali na nyumbani nikikazanakatika kufanikisha utafiti huu.Pia, ninapenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa Bwana Nyuni Ndaro ambayeamekuwa bega kwa bega na mimi katika hatua zote muhimu za utafiti huu. Kila maraalinitia moyo kwamba nikazane na Mwenyezi Mungu ataniwezesha kumaliza masomoyangu. Mwisho ninapenda kumshukuru Mwalimu Mohamed Omary kwa kuisoma kazihii mara kadhaa na kunipatia maoni yaliyonifungulia njia ya kukamilisha kazi hii.

viiIKISIRIUtafiti huu umeshughulikia matumizi ya lugha ya tamathali za usemi katika mashairiya magazetini. Ili kukamilisha lengo hili kuu madhumuni mahususi matatuyalitimizwa. Madhumuni hayo yalihusu kubainisha tamathali za usemi, dhamira nadhima za tamathali za usemi katika kujenga dhamira mbalimbali katika mashairi yamagazetini. Mtafiti ametumia mbinu za uchambuzi wa kimaudhui, usaili na upitiajiwa nyaraka katika kukusanya data za utafiti. Mikabala ya kifasihi na ule wakimaelezo ndio iliyotumika katika kuchambua data za utafiti wetu.Kwa ujumla utafiti umeweza kukusanya data ambazo zimeweza kujibu maswali yautafiti wetu ambapo imethihirika kwamba, mashairi ya magazetini yameshehenimatumizi ya tamathali mbalimbali za usemi. Pia imebainika kwamba tamathali hizoza usemi zinatumika kujenga dhamira mbalimbali na mwisho tamathali za usemizimebainika kuwa na dhima mbalimbali za kifani na kimaudhui katika kujenga nakuwasilisha dhamira mbalimbali kuhusiana na masuala ya UKIMWI kwa jamii yaKitanzania.Mwishoni mwa utafiti kumetolewa mapendekezo kwa wadau mbalimbali wamashairi ya magazetini kuhusiana na namna bora za kuimarisha mashairi hayo iliyaendelee kutekeleza wajibu wake kwa jamii. Pia, tumetoa mapendekezo kwa ajili yatafiti za baadaye katika uwanja wa mashairi ya magazetini.

viiiYALIYOMOUthibitishi . iiHakimiliki. . iiiTamko . . ivTabaruku . . vShukurani. . viIkisiri . . viiYaliyomo. . viiiSURA YA KWANZA: UTANGULIZI . 11.1Usuli wa Tatizo la Utafiti . 11.2Tamko la Tatizo la Utafiti . 51.3Malengo ya Utafiti . 61.3.1Lengo Kuu la Utafiti . 61.3.2Malengo Mahususi . 61.3.3Maswali ya Utafiti. 71.4Umuhimu wa Utafiti . 71.5Mipaka ya Utafiti . 91.6Vikwazo vya Utafiti na Utatuzi wake . 91.7Mpango wa Tasinifu . 10SURA YA PILI: UTALII WA KAZI TANGULIZI NA MKABALAWA KINADHARIA . 122.1Utangulizi . 122.2Ufafanuzi wa Dhana Mbalimbali . 12

ix2.2.1Dhana ya Ushairi . 122.2.2Ushairi wa Kiswahili. 132.2.3Dhana ya Shairi . 142.2.4Tamathali za Usemi . 152.2.4.1Sitiari . 152.2.4.2Ishara . 152.2.4.3Taswira . 162.3Utalii wa Kazi Tangulizi . 162.3.1Ushairi kwa Ujumla . 162.3.1.1Dhamira katika Mashairi . 162.3.1.2Fani katika Mashairi . 232.4Mashairi ya Magazetini. 262.5Hitimishi . 292.6Mkabala wa Kinadharia . 302.6.1Nadharia ya Mwitiko wa Msomaji . 302.6.2Nadharia ya Ufeministi . 322.6.3Nadharia ya Simiotiki . 372.7Hitimishi . 38SURA YA TATU : MBINU ZA UTAFITI . 393.1Utangulizi . 393.2Eneo la Utafiti . 393.3Umbo la Utafiti . 393.4Watafitiwa . 40

x3.4.1Uteuzi wa Watafitiwa. 413.5Vyanzo vya Data . 423.5.1Data za Msingi . 423.5.2Data za Upili . 423.6Mbinu ya Ukusanyaji wa Data . 423.6.1Uchambuzi wa Kimaudhui . 433.6.2Usaili . 433.7Uchambuzi wa Data . 443.8Usahihi wa Mbinu za Utafiti . 453.8.1Kuaminika kwa Matokeo ya Utafiti . 453.9Maadili ya Utafiti . 463.10Hitimishi . 46SURA YA NNE: UWASILISHAJI, UCHAMBUZI NA MJADALA WADATA ZA UTAFITI . 484.1Utangulizi . 484.2Tamathali za Usemi katika Mashairi ya Magazetini . 484.2.1Taswira . 484.2.2Sitiari . 554.2.3Takriri . 614.2.4Tafsida. 674.2.5Tashibiha . 704.2.6Ishara . 754.3Dhamira katika Mashairi ya Magazetini . 79

xi5.3.1UKIMWI na Umalaya . 795.3.2Chanzo Cha UKIMWI . 824.3.3Unyanyapaa . 834.3.4Kinga ya UKIMWI . 864.3.5Hitimishi . 884.4Dhima ya Tamathali za Usemi katika Kujenga Dhamira . 884.4.1Dhima za Kimaudhui . 884.4.1.1Kumfikirisha Msomaji . 894.4.1.2Kuhamasisha Jamii . 914.4.1.3Kufafanua Jambo . 934.5Dhima za Tamathali za Usemi Kifani . 974.5.1Kupamba Lugha . 974.5 2Tamathali za Usemi na Vipengele Vingine vya Kifani . 984.5.3Hitimishi . 99SURA YA TANO: MUHTASARI, HITIMISHI NA MAPENDEKEZO . 1015.1Utangulizi . 1015.2Muhtasari wa Tasinifu . 1015.3Hitimishi . 1035.4Mapendekezo . 1065.4.1Mapendekezo kwa Watunzi wa Mashairi . 1065.4.2Mapendekezo kwa Wachapaji . 1075.4.3Mapendekezo kwa Tafiti za Baadaye . 107MAREJELEO . . 108VIAMBATANISHO . 116

1SURA YA KWANZAUTANGULIZI1.1Usuli wa Tatizo la UtafitiUshairi wa Kiswahili ni miongoni mwa tanzu za fasihi ambazo zina historia ndefukatika kuwako kwake Uswahilini. Kimani (1983) anaeleza kwamba, Utenzi waTambuka au kwa jina lake la pili, Chuo cha Herekali ni utenzi maarufu sana katikahistoria ya ushairi wa Kiswahili. Utenzi huu ni wa kwanza kuandikwa kwa lugha yaKiswahili, ingawa inaaminika kwamba kabla ya utenzi huu kuandikwa na Mwegobin Athumani katika 1728, kulikuwa kuna mashairi mengi mengine ya Kiswahili.Katika kufanya hivi, bwana Mwego, aliyeishi Pate Kisiwani, akawa ametufunguliahistoria ya ushairi wa Kiswahili. Utenzi huu unasimulia habari za Fumo LaitiNabahani, Sultani wa Pate wa wakati huo. Pia utenzi huu unahusisha vita vya mieziminane iliyotokea Syria kati ya Waarabu na wenyeji wa Byazantine kwa ajili ya diniya Kiislamu.Kama inanavyosadikiwa, mashairi yalikuwa mengi sana kabla ya utenzi huukuandikwa. Kasoro ni kwamba washairi wa siku hizo hawakuyahifadhi mashairi yaokatika maandishi. Ilikuwa bado ni jadi ya Waswahili kuhifadhi tungo zao vichwanikutokana na uwezo wao wa kuhifadhi Quraani. Waislamu walipofika, waliwakutawenyeji wakiwa na utamaduni wao, wakawafunza kuandika kwa hati za Kiarabuambazo wenyeji waliziongezea herufi na kuzifanya hati za Kiswahili. Wenyejiwakaanza kuandika na kuhifadhi utamaduni wao kwa njia hii, ndipo akazuka Mwegobin Athumani na kuandika utenzi wake.Maelezo haya juu ya historia ya ushairi wa Kiswahili, yanaonesha kwamba ushairiwa Kiswahili wa hapo kale haukuandikwa na kuhifadhiwa katika maandishi kwa

2kuwa utaalamu wa kusoma na kuandika haukuwepo katika jamii ya wakati huo. Kwahivyo, ushairi uliokuwapo ni ushairi simulizi, hasa nyimbo. Hata hivyo, ushairisimulizi ndiyo uliozusha ushairi andishi wa Kiswahili mara baada ya utaalamu wakuandika na kusoma ulipoletwa na Waislamu wa tapo la Mtume Muhammad (SAW).Jambo hili laonesha kwamba, ushairi andishi wa Kiswahili una sifa nyingi za ushairisimulizi kwa sababu ndicho chanzo chake.Kimsingi, Waarabu waliukuta Ushairi wa Kiswahili wakautumia kwa kuandika tenzi,mashairi, kasida na duwa kwa lugha ya Kiswahili baada ya wao kujifunza Kiswahilina hati za Kiswahili zilizofanana na za Kiarabu (Mansour, 2013; Omary, 2011).Hivyo ni kusema kwamba, mashairi ya Kiswahili ya zamani yalihifadhiwa vichwanina kutongolewa kwa midomo kila ilipohitajika. Dhima mojawapo kuu ya Ushairi waKiswahili ni kuimbika ili uelimishe na huku ukiburudisha. Hii ndiyo kanuni yakwanza na iliyo muhimu sana katika Ushairi wa Kiswahili (Kimani, 1983;Massamba, 1983).Maelezo hayo yanatuonesha kwamba Ushairi wa Kiswahili ulianza na nyimbo zaWaswahili ambazo wamekuwa wakiziimba karne na karne. Kauli kwamba asili yaushairi wa Kiswahili ni fasihi ya Kiarabu na Dini ya Kiislamu zinatokana na chuki zaKikoloni, za Kidini na kibinafsi. Chuki si tabia ya Wasomi. Ushairi wa Kiswahili unakwao (Sengo, 2009). Hii inadhibitishwa na utafiti uliofanywa na Mulokozi na Sengo(1995) ambao nao walihitimisha kwamba, Ushairi wa Kiswahili unatokana nanyimbo za Kiafrika ingawa na wao wanakiri kuwa fasihi ya Kiarabu na Dini yaKiislamu zimetoa mchango mkubwa katika kuathiriana na fasihi ya Kiswahili.Waislamu wageni walipokuja Pwani ya Afrika ya Mashariki, walifundisha Dini ya

3Kiislamu na ustaarabu wake ambao ulifuatwa na Waswahili wengi na kuwa sehemumuhimu ya utamaduni wao. Kwa hali hiyo, ikawa ni jambo la kawaida kwa ushairina aina nyingine ya fasihi ya Waswahili iliyokuwapo wakati huo kusawiri utamaduniwa Uswahilini. Waswahili walikuwa na ushairi wao ambao uliimbwa katika hadharakulingana na matukio maalumu. Kimani (1983:131) anasema:Tungo za zamani na za siku hizi zinatungwa kufuatana na matukioau majira: mvua au ukame, njaa au shibe, au nyakati Kama vile zavita, amani, mabadiliko ya siasa (na kwa hivyo kufunza siasa mpyaya nchi) na hata kuwashutumu au kuwasifu viongozi. Tungo nyinginezinatungwa kwa nia ya kuwavunja moyo maadui walio tayarikushambulia. Mfano mzuri wa tungo za aina hiyo ni zilezilizotungwa na Muyaka bin Haji-Al Ghassani.Kwa mantiki hii ushairi wa Kiswahili unaonekana kuanza tangu pale mwanadamualipoanza kuwasiliana kwa kutumia lugha. Hii inaonekana katika nukuu hapo juuambapo tunaelezwa kwamba ushairi wa Kiswahili uliimbwa kwa lengo la kuelezajuu ya masuala mbalimbali ambayo yanaonekana kutokea mara kwa mara katikajamii za zamani na jamii za siku hizi.Ushairi wa Kiswahili uliendelea kutekeleza dhima zake katika vipindi tafautitafautivya maisha ya jamii ya Waswahili. Kwa mfano, Mulokozi (1982) anaeleza kwamba,Ushairi wa Kiswahili ulitumika kama silaha muhimu ya kupinga utawala waKikoloni kwa kuelezea madhila yanayofanywa na Wakoloni dhidi ya wananchi. Kwakufanya hivyo, washairi waliwataka wakoloni kuondoka nchini na kuwaachiawananchi nchi huru ili wajitawale wenyewe. Mfano mzuri ni ule wa kipindi chautawala wa Wareno ambapo utawala huo ulipewa onyo kali na washairi la kutakiwakuondoka nchini. Shairi la Mzungu Migeli ndilo linalothibitisha hoja hii kwamba:

4Mzungu MigeliMzungu Migeli UmuongoMato yako yana tongoKwani kuata mpangoKwenda Kibanga uani(Kitogo, 2002).Hiki ni kipande cha ubeti wa shairi ambalo halijulikani lilitungwa na nani lakinililiimbwa na wananchi katika kipindi cha utawala wa Wareno kwa nia yakuwakumbusha kuwa wanatakiwa kuondoka nchini na kuwaachia wananchi nchi yaowaiongoze wao wenyewe. Kipande hiki cha shairi ni sehemu ya ushairi simuliziambacho hakikuwahi kuandikwa katika kipindi hicho, ndiyo maana mtunzi wakehakupata kutambulikana. Mashairi ya wakati wote huo yalitungwa kwa namnaambayo itaweza kuimbika kwa sababu hakukuwa na maandishi na hivyo kuliimbashairi ni kulihifadhi. Shairi linapoimbwa mara kwa mara hukaa kichwani kwamwimbaji au waimbaji na hivyo kuzoeleka katika jamii. Kwa hivyo, ili shairi liwezekukaa kichwani kwa msomaji kwa harakaharaka ni lazima liwe na mapigo ya vina naurari wa mizani (Omari, 2009; Omary, 2011).Mashairi ya Kiswahili yaliendelea kufanya kazi ya kuelimisha na kuburudisha jamiikatika vipindi mbalimbali ambapo mashairi mengi yaliandikwa katika magazetikama vile Baragumu, Mambo Leo, Uhuru, Mzalendo na kadhalika. Mutembei (2009)anaeleza kwamba, mashairi yanayoandikwa magazetini yana nafasi kubwa katikakuelimisha jamii juu ya mambo yanayotokea katika jamii yao na namna yakukabiliana nayo. Kwa mfano, anaeleza kwamba ugonjwa hatari wa UKIMWIulipoingia nchini na kusababisha vifo vya wananchi wengi, washairi walitumiakalamu zao kutungia mashairi katika magazeti kwa nia ya kuihamasisha jamii

5kuufahamu ugonjwa huo ili wachukue hatua stahiki za kukabiliana nao. Vilevile,anaendelea kueleza kwamba, mashairi yanayoandikwa katika magazeti yana nguvukubwa ya kuleta mabadiliko katika jamii.Mashairi ya magazetini yana mchango mkubwa katika kujenga na kuimarishautamaduni wa jamii. Hata hivyo, hakuna utafiti wa kina ambao tayariumekwishafanyika kwa nia ya kuonesha ushairi huo unatumia lugha ya aina gani nalugha hiyo, ina dhima gani katika kuwasilisha ujumbe kwa jamii iliyokusudiwa.Utafiti wetu umefanywa ili kuchambua matumizi ya lugha hasa ile ya kitamathalikatika mashairi ya magazetini na kisha kuchunguza dhima ya tamathali hizo kwajamii inayohusikahusika, hivyo, kuziba pengo la utafiti1.2Tamko la Tatizo la UtafitiMashairi ya magazetini kwa taarifa tulizozipata yalianza kuandikwa tangu palemagazeti hayo yalipoanza kutolewa katika kipindi cha ukoloni wa Waingereza nakuendelea (Khalifan, 2013). Hata hivyo, katika kipindi hicho, magazeti mengihayakutoa fursa kwa watunzi wa mashairi ya Kiswahili kuchapishiwa mashairi yaoyaliyoikosoa serikali ya kikoloni na badala yake washairi walitakiwa kuandikamashairi ambayo yaliisifu serikali ya kikoloni (Kitogo, 2002). Kasi ya kutunga nakuchapisha mashairi katika magazeti iliongezeka mara tu ulipopatikana uhuru waTanganyika mnamo mwaka 1961, ambapo, washairi kama Saadan Kandoro, MzeeWaziri Kijana, Komba, Sudi Andanenga na wengine wengi waliandika mashairiyaliyojaa dhamira mbalimbali. Miongoni mwa dhamira zilizotia fora katika mashairihayo ni zile zilizohusu ujenzi wa jamii mpya pamoja na siasa za ujamaa nakujitengemea (Khatibu, 1987).

6Ingawa, mpaka kufikia sasa, mashairi ya magazetini yanaendelea kuchapishwa, niutafiti mchache mno ambao umekwishafanyika kwa nia ya kuyachunguza mashairihayo. Miongoni mwa uchachefu huo ni kazi ya Mutembei (2009), ya Chaligha(2011) na ya Khatibu (1987). Hata hivyo, watafiti hawa hawakuwa na lengo lakuchunguza matumizi ya lugha ya kitamathali katika mashairi ya magazetini, jamboambalo linaonesha kuwapo kwa pengo la kiutafiti linalohitaji kushughulikiwa.Katika kushughulikia pengo hili la kiutafiti, utafiti huu umefanywa kwa kuchunguzamatumizi ya lugha ya kitamathali katika mashairi ya magazetini kupitia magazetiyaliyoteuliwa.1.3Malengo ya UtafitiUtafiti huu una lengo kuu moja, na madhumuni mahususi matatu ambayo kukamilikakwake ndio kukamilika kwa utafiti wetu.1.3.1Lengo Kuu la UtafitiLengo kuu la utafiti huu, ni kuchunguza matumizi ya lugha ya kitamathali katikamashairi ya magazetini ya Mzalendo, Nipashe, Majira, Uhuru na Mtanzaniayanayozungumzia ugonjwa wa UKIMWI.1.3.2Malengo MahususiUtafiti huu umekamilika baada ya kutimizwa kwa malengo mahususi yafuatayo:(a)Kuainisha tamathali za usemi zinazojitokeza katika mashairi ya UKIMWIya magazetini kupitia magazeti yaliyoteuliwa.(b)Kubainisha dhamira mbalimbali zinazowasilishwa na lugha ya kitamathalikatika mashairi ya UKIMWI ya magazetini kupitia magazeti yaliyoteuliwa.

7(c)Kufafanua dhima ya lugha ya kitamathali ya mashairi ya magazetini katikakuibua dhamira za mashairi ya UKIMWI ya magazetini kupitia magazetiyaliyoteuliwa.1.3.3(a)Maswali ya UtafitiNi tamathali zipi za usemi zinazojitokeza katika mashairi ya UKIMWI yamagazetini kupitia mashairi yaliyoteuliwa?(b)Matumizi ya lugha ya kitamathali katika mashairi ya UKIMWI yamagazetini yanawasilisha dhamira gani kwa jamii?(c)Ni nini dhima ya lugha ya kitamathali ya mashairi ya UKIMWI yamagazetini katika kuibua dhamira za mashairi ya magazetini kupitiamagazeti yaliyoteuliwa?1.4Umuhimu wa UtafitiUtafiti huu ni wa kitaalimu na hivyo unatoa umuhimu katika maeneo ya taaluma;utafiti huu umeshakuwa rejeleo muhimu kwa wanafunzi na walimu wanaofundishafasihi ya Kiswahili. Wanafunzi, kwa sasa wanaweza kutumia utafiti huu kwa ajili yakukuzia maarifa yao ya nadharia ya Ushairi wa Kiswahili kwa kuelewa kwamba,Ushairi wa Kiswahili umeenea na kuandikwa na watu wengi waliojifunza nakuupenda; mfano hawa waliochapisha katika magazeti. Wanafunzi wa ngazi yauzamili watatumia matokeo ya utafiti huu na kuwapatia maeneo mapya ya kufanyiautafiti katika taalimu ya fasihi ya Kiswahili.Kwa upande wa walimu wa fasihi ya Kiswahili na fasihi kwa Kiswahili, watauonaumuhimu wa utafiti huu, utakapowasaidia kuandaa maalumati ya kuwafundishia

8wanafunzi wao. Pia, watautumia utafiti huu katika kuimarisha utafiti zaidi, ambaowataufanya katika tanzu za fasihi na vijitanzu vya ushairi wa Kiswahili kamanyimbo.Kwa upande wa maadili, utafiti huu unaonesha kwamba, ushairi wa Kiswahiliumepiga hatua kubwa ya maendeleo katika kufunza maadili. Hii inatokana nakutumika kwa tungo nyingi na baadhi kuimbwa na kusomwa katika magazeti nakatika shughuli za kijamii kama vile; harusi, misiba, mahafali ya kuhitimu masomo,kupongeza watumishi baada ya kupandishwa vyeo na kadhalika.Kwa upande wa utamaduni, utafiti huu una umuhimu mkubwa katika kuendeleza nakudumisha mema ya utamaduni wa Mtanzania, kwa kuwa katika ushairi wamagazetini huelezwa mambo ambayo yanatokana na utamaduni wa jamii yaWatanzania. Maadili na mafunzo mema yanayofundishwa katika mashairi yamagazetini, ni muhimu katika kuendeleza utu, heshima, adabu, ukarimu, umoja,amani na mshikamano miongoni mwa Watanzania.Kwa upande wa sera za maendeleo, utafiti huu umesaidia kuibua masuala kadhaa yakisera ambayo yanahitaji kuimarishwa kwa kutungiwa sera muafaka zitakazosaidiakuiletea jamii maendeleo. Miongoni mwa sera hizo ni kama ile ya Utamaduni naLugha ambamo ndani mwake mnazungumzwa maendeleo ya lugha ya Kiswahili.Kutokana na utafiti huu, watunga sera wameelekezewa maeneo mapya yakuimarishwa ili kuikuza lugha ya Kiswahili, fasihi yake na utamaduni wa Mtanzania.Mzee Sengo, hivi sasa yumo mbioni kutafuta fedha zake mwenyewe, kuitisha kikao

9cha Waswahili wenyewe, awakabidhi lugha yao wailee na watumiaji waendeleekuitumia vizuri bila ya kuiviza.Kwa upande wa wasanii wanaotunga mashairi yao na kuyachapisha katika magazetiwatauona utafiti huu kama changamoto ya wao kuendelea kutunga mashairi mengizaidi na kuyachapisha katika magazeti. Wasanii wataona kuwa kumbe mashairi yaoni muhimu sana katika kufunza mambo mbalimbali kwa jamii ndio maana hatawatafiti wanayashughulikia mashairi hayo.1.5Mipaka ya UtafitiUtafiti huu umeshughulikia matumizi ya lugha ya kitamathali katika mashairi yamagazetini tu. Hii inatokana na ukweli kwamba, matumizi ya lugha katika kazi zafasihi ni kipengele kipana mno ambacho hakiwezi kushughulikiwa katika utafiti wangazi wa shahada ya Uzamili na kukamilika kwa ukamilifu wake. Kwa kulifahamuhilo, ndipo kikachaguliwa kipengele cha tamathali za usemi peke yake katika ushairiwa magazetini. Magazeti yaliyohusishwa katika utafiti huu ni matano tu ambayo niMzalendo, Nipashe, Majira, Uhuru na Mtanzania.1.6Vikwazo vya Utafiti na Utatuzi wakeMtafiti wa utafiti huu amekumbana na vikwazo, kikubwa kikiwa ni kukosaushirikiano na wakuu wa kazi kuhusu muda. Mtafiti ni mtumishi wa serikali mwenyewajibati nyingi kwa mwajiri wake na hivyo kutakiwa kukamilisha kazi za mwajiriwake kwa wakati. Hali hii ilimfanya kutopata muda wa kutosha kushughulikia utafitihuu na kuumaliza kwa muda uliopangwa. Tatizo jingine ni lile linalohusiana nauhaba wa fedha za kufanyia utafiti. Mtafiti hakupata udhamini wa aina yoyote nahivyo kulazimika kutenga sehemu ya mshahara wake kwa ajili ya kujisomesha. Hili

10ni tatizo kubwa kwa watumishi wa Umma, kukosa kupangiwa taratibu zakuongezewa viwango vya visomo kwa manufaa ya maendeleo ya taifa.Ili kutatua vikwazo hivyo, mtafiti alifanya kila lililowezekana kuhakikisha kwamba,utafiti wake unakamilika kwa wakati. Hili liliwezekana baada ya yeye kutatuakikwazo cha muda kwa kutumia muda wake mwingi wa wakati wa usiku katikakuandika ripoti ya tasinifu yake. Badala ya kulala saa mbili usiku kama ilivyokuwakawaida yake alilazimika kulala saa sita ya usiku ili kuweza kufidia muda alioukosamchana kwa ajili ya kufanya kazi yake ya utafiti. Saa nne alizozimega kutoka katikausingizi zilimwezesha kupiga hatua kubwa katika uandishi wa tasinifu na kishakufanikiwa kukamilisha utafiti huu. Kuhusiana na kikwazo cha fedha, mtafitialijitahidi kutenga kiasi kikubwa katika mshahara wake kwa ajili ya kukamilishautafiti wake na hivyo kusimamisha miradi mingine ya maendeleo aliyokuwaakiifanya kupitia sehemu ya mshahara wake. Alifanya hivyo kwa sababu alifahamukwamba, elimu ndio ufunguo wa maisha kwa mwanadamu.1.7Mpango wa TasinifuTasinifu hii ina jumla ya sura tano. Sura ya kwanza inazungumzia utangulizi wajumla kuhusiana na utafiti wetu. Mambo ambayo yanazungumzwa katika sura hii niusuli wa tatizo la utafiti, tatizo la utafiti, malengo ya utafiti, madhumuni mahususi namaswali ya utafti. Mambo mengine ni mipaka ya utafiti, vikwazo na utatuzi wavikwazo. Sura ya pili inawasilisha utalii wa kazi tangulizi kulingana na mada yautafiti wetu. Kazi tangulizi zilizopitiwa ni pamoja na zile zilizotafiti ushairi waKiswahili kwa ujumla na kisha tukaeleza kazi tangulizi zilizotafiti mashairi yamagazetini. Sura ya tatu inazungumzia mbinu za utafiti zilizotumika katika

11kukusanya na kufanya uchambuzi wa data za utafiti na kuifanya tasinifu ionekanekama ilivyo. Sura ya nne inawasilisha, kuchambua na kujadili data za utafiti ilikujibu maswali ya utafiti wetu. Sura ya tano ndio inatoa muhtasari, hitimishi namapendekezo kwa ajili ya utafiti zaidi.

12SURA YA PILIUTA

Kikoloni, za Kidini na kibinafsi. Chuki si tabia ya Wasomi. Ushairi wa Kiswahili una kwao (Sengo, 2009). Hii inadhibitishwa na utafiti uliofanywa na Mulokozi na Sengo (1995) ambao nao walihitimisha kwamba, Ushairi wa Kiswahili unatokana na nyimbo za Kiafrika ingawa na wao wanakiri kuwa fasihi ya Kiarabu na Dini ya

Related Documents:

mawazo ya wanamsambao hususani katika ugawaji wa ngano bila kuchunguza kwa umakini sifa ya kila kundi. Propp anaamini kuwa ili kuchunguza asili ya ngano ni vema kuanza kuchunguza aina za ngano kwa kuangalia maumbo ya ngano. Hivyo mtazamo huu unaangalia asili ya ngano kwa kuchunguza maumbo ya ngano husika. Ubora wa nadhairia hii, nadharia hii inasaidia kujua aina za ngano kutokana na dhima zake .

kundi ,fanya jukumu la maana katika masomo yote.Umahiri wa maelezo maalum na wa baina ya mitaala yameshikanishwa pamoja katika muktadha wa maelezo. . baina ya mitaala katika muda wa mwaka wa shule. Kwa kufanya hivo wanaangazia kusoma kwao . na wanachukua jukumu la mchakato wao wa kimasomo. Tathmini ya kibinafsi hufanywa katika

Wapemba. Surahii pia inatoa taarifa za awali kuhusu mada ya utafiti ambapo mtafiti ataelezea kuhusu usuli wa mada,tatizo la utafiti,malengo ya utafiti yakiambatana na mswali ya utafiti ,umuhuimu wa utafiti mipaka ya utafiti hatimae hitimisho , haya yote yameelezewa juu ya kuchunguza matumizi ya tafsida katika lahaja

Data zilirekodiwa katika kinasa sauti na kunukuliwa kwa maandishi. . Tofauti za Matumizi ya Lugha katika Miktadha Mbalimbali ya Mazungumzo 13 sehemu ya pili inahusu tofauti ya matumizi ya lugha katika miktadha mbalimbali. Sehemu ya tatu inafafanua mkabala wa kinadharia uliotumika katika uch

Nyenzo za kufundisha huwa viungo muhimu wakati wa utoaji wa mafunzo. Utafiti ulichunguza matumizi ya nyenzo katika ufundishaji wa Kiswahili katika shule za msingi za umma katika Jimbo la Nyandarua, Kenya. Madhumuni ya utafiti yalikuwa: Kuainisha nyenzo zinazotumika kufundisha Kiswahili, Kutathimini kiwango cha matumizi ya

maswali yeye aliuliza ilikuwa, 'Biblia ina hadithi kuhusu mtu ambaye alimezwa na samaki mkubwa. Alikuwa nani? Asilimia themanini ya watu katika kundi hilo, kwa ushujaa wakasema, 'Pinocchio!' Marla aliniambia tukiwa bado katika ibaada kwamba swali hilo bado liliulizwa katika kanisa ambako alihundumu katika Kusini mwa California na

tamko la tatizo la utafiti, lengo kuu na madhumuni mahususi ya utafiti. Aidha maswali ya utafiti, umuhimu wa utafiti, mipaka ya utafiti na mpangilio wa tasnifu pia vimewasilishwa katika sura hii. 1.1 Usuli wa Tatizo la Utafiti Binadamu katika kuishi

The energy intensity target in China’s 11th Five-Year Plan period - Local implementation and achievements in Shanxi Province Daisheng Zhanga,*, Kristin Aunanb,a, Hans Martin Seipa,b, Haakon Vennemoc a Department of Chemistry, University of Oslo, P. O. Box 1033 Blindern, 0315 Oslo, Norway b Center for International Climate and Environmental Research — Oslo (CICERO), P.O. Box 1129 Blindern .