Bajeti Ya Elimu Ya Mwaka 2016/2017 - Policy Forum

2y ago
94 Views
2 Downloads
329.29 KB
8 Pages
Last View : 29d ago
Last Download : 3m ago
Upload by : Halle Mcleod
Transcription

Dondoo ya Sera 3:2016Bajeti ya Elimu ya Mwaka 2016/2017Je, ni Kweli Imeongezeka?Katika bajeti ya mwaka 2016/2017 Serikali iliidhinisha jumla ya Shilingi Bilioni4,770 kwa matumizi ya sekta ya Elimu zikiwa zimejumuisha matumizi yaWizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi. Kiasi hiki ni sawa naasilimia 22.1 ya jumla ya bajeti yote ya Taifa ambayo ni Shilingi Bilioni 29,539.6.Takwimu hizi hazijumuishi deni la taifa.Kutokana na takwimu za matumizi ya sekta ya Elimu yaliyoidhinishwa, tunawezakuona ongezeko la Shilingi Bilioni 882.3; kutoka Shilingi Bilioni 3,887 katikamwaka wa fedha wa 2015/16 hadi Shilingi Bilioni 4,769 kwa mwaka wa fedhawa 2016/17 ambalo ni sawa na ongezeko la asilimia 22.7Hivyo kwa msingi wa mgawo wa bajeti iliyoidhinishwa, kuna ongezeko katikabajeti ya sekta ya Elimu, lakini mgawo halisi unahitaji kujadiliwa. Tazama ChatiNamba1 hapa chini;Bilioni TzsChati Namba 1: Bajeti ya Sekta ya Elimu – bila Deni la TaifaChanzo: Bujeti ya Taifa 2015-16 & 2016-171

Ni muhimu kuangalia kama bajeti iliyoidhinishwa inajumuisha deni la taifa aula kwa sababu deni la taifa huwa linapunguza bajeti inayoweza kutumika. Kwamfano, kwa mujibu wa Bajeti ya Taifa Serikali imepanga kutumia Shilingi Bilioni 8,000 kulipia deni la Taifa kwa mwaka wa fedha wa 2016/17. Kiasi hikihutolewa kutoka katika bajeti kuu na hivyo kusababisha matumizi ya bajeti hiyokupungua nguvu. Kwa mfano, katika sekta ya elimu sehemu ya bajeti ya sektailiyoidhinishwa dhidi ya bajeti ya taifa bila deni la taifa ni asilimia 22.1; kiwangoambacho si cha kuaminika. Lakini tukitoa malipo ya deni la taifa, sehemu ya bajeti ya sekta ya Elimu ikilinganishwa na bajeti ya taifa inakuwa sawa na asilimia17 sawasawa kabisa na kiwango cha mwaka uliopita.Chati zifuatazo zinalinganisha sehemu ya bajeti ya sekta ya Elimu dhidi ya bajetiya taifa katika miaka miwili iliyopita kwa kuangalia matumizi yaliyoidhinishwakabla na baada ya kutoa deni la taifa.Chati Namba 2: Bajeti ya Elimu kama sehemuya Bajeti ya Taifa(Pasipokuwa na Deni la Taifa)Chati Namba 3: Bajeti ya Elimu kama sehemu yaBajeti ya Taifa(Pamoja na Deni la Taifa)Chanzo: Bujeti ya Taifa 2015-16 & 2016-17Bajeti ya sekta ya Elimu hugawanywa tena katika bajeti ya kawaida na bajetiya maendeleo. Katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2016/17 jumla ya ShilingiBilioni 3,069.5, sawa na asilimia 64.3 zilitengwa kwa matumizi ya kawaida;wakati Shilingi Bilioni 1,700.5, sawa na asilimia 35.7 ziliidhinishwa kwa ajili yamatumizi ya maendeleo.Kimsingi sehemu ya bajeti ya kawaida ikilinganishwa na bajeti ya maendeleokatika sekta ya Elimu inaonekana kuwa imeboreshwa na kukaribia uwianounaopendekezwa wa walau 60:40 (Kawaida: Maendeleo). Kutokana na uchambuziwa hapo juu uwiano wa mgawo katika mwaka 2016/17 ni 64:35 (kawaida:maendeleo). Uwiano unaendana na viwango vinavyotakiwa ukilinganisha na ule2

wa mgawo wa mwaka uliopita wa 84:16. Chati ya chini inaonyesha uwiano huo:Chati Namba 4: Mwenendo wa Mgawo wa Bajeti ya Sekta ya Elimu:Kawaida dhidi ya MaendeleoKawaidaMaendeleoChanzo: Bujeti ya Taifa 2015-16 & 2016-17Kwa mujibu wa malengo ya bajeti na vipaumbele vilivyopangwa, lengo kuula bajeti ya sekta ya Elimu katika mwaka 2016/17 ni kutekeleza elimubure ya msingi kwa nchi nzima; kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu yajuu; ujenzi; ukarabati wa miundo mbinu ya elimu; kuboresha thamani yaelimu kwa kujenga ujuzi unaotakiwa katika ngazi zote; kuimarisha Utafitina Maendeleo na matumizi ya sayansi na teknolojia ili kuchochea ukuaji wauchumi. Kutekeleza na kufikia malengo haya yaliyopangwa; fedha za sektaya elimu husambazwa kupitia Wizara zifuatazo ambazo hupokea kiasi tofautikutegemeana na shughuli zinazofanyika:·Shilingi Bilioni 2,871.6 hupelekwa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikaliza Mitaa·Shilingi Bilioni 1,397 hupelekwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia·Shilingi Bilioni 500.1 hutengwa na Serikali kuu kupitia Wizara mbali mbalizinazoshughulika na elimu, yaani Wizara ya Wanawake, Jinsia na Maendeleoya Mtoto na Wizara ya Afya na Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo3

Chati Namba 5: Mgawo wa Bajeti ya Sekta ya Elimu Ki-WizaraOR-TAMISEMIWESTWizara NyingineChanzo: Bujeti ya Taifa 2016-17Matumizi mengine muhimu kutokana na bajeti ya sekta ya elimu yanajumuishaShilingi Bilioni 3,069.5 zilizopangwa kutekeleza“Mpango wa Elimu Bureya Msingi”; ambapo Shilingi Bilioni 2,871.6 zimetengwa kama ruzuku zakuhawilishwa kwa Mamlaka ya Serikali za Mitaa (LGA’s). Shilingi Bilioni 197.89hutengwa na Serikali kuu kupitia wizara mbali mbali. Mpango wa Mafunzo yaTeknolojia na Ufundi hupokea Shilingi Bilioni 44.61, Maendeleo ya sayansi nateknolojia hupokea Shilingi Bilioni 69.66; wakati Shilingi Bilioni 431.71 huendakatika utoaji wa mikopo kwa wanafunzi walioingizwa kwenye elimu ya juu naBilioni 43.75 zitatumika kwa uhakiki wa thamani, ukarabati wa Vyuo vya Walimu,kuimarisha ukaguzi na kuanzisha Tume ya Huduma ya Waalimu (TSC).Bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ya Mwaka 2016/17Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ni mshauri mkuu wa Serikali kuhusumfumo wa elimu, hivyo hutoa miongozo kwa taasisi za elimu na mashirikayanayochangia katika malengo ya Serikali kuhusu elimu. Majukumu yake makuuni kupanga mikakati, sera, na mipango ya mageuzi na maendeleo ya elimu;na kuandaa rasimu ya kanuni na taratibu, na kusimamia utekelezaji wake.Kufanikisha majukumu hayo Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia mwaka2016/17 imeomba na kuidhinisha kutumia kiasi cha jumla ya Shilingi Bilioni1,397 katika kugharamia ya shughuli za kawaida na za maendeleo kwa mwakawa fedha wa 2016/17.4

Hili ni ongezeko la Shilingi Billioni 407.5, sawa na asilimia 41.2 kutoka ShilingiBilioni 989.5 zilizoombwa na kuidhinishwa katika mwaka wa fedha wa 2015/16.Bilioni (TZS)Chati Namba 6: Jumla ya Mgawo wa Bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansina TeknolojiaWEST* BajetiChanzo: Bujeti ya Taifa 2015-16 & 2016-17Kati ya jumla ya Shilingi Bilioni 1,397, Wizara imepanga kutumia Bilioni 499.3sawa na asilimia 35.7 ya jumla ya bajeti yote kwa matumizi ya kawaida ikiwani pamoja na fedha kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa Wizara na gharamanyingine. Hata hivyo, Wizara imetenga Shilingi Bilioni 897.7, sawa na asilimia64.3 ya bajeti yote kwa matumizi ya maendeleo katika mwaka wa fedha wa2016/17. Shughuli za maendeleo zinajumuisha ujenzi na ukarabati wa miundombinu na miradi mingine chini ya wizara.Wachambuzi wa bajeti na baadhi ya wadau wanafikiri kuwa uwiano baina ya bajetiya kawaida na ya maendeleo ni mzuri sana; kwani juhudi nyingi zimeelekezwakatika matumizi ya ki-mtaji (maendeleo) kuliko matumizi ya kawaida.*West-Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia5

Chati Namba 7: Matumizi ya Wizara: Kawaida Dhidi ya MaendeleoKawaidaMaendeleoChanzo: Bujeti ya Taifa 2015-16 & 2016-17Hata hivyo bajeti ya Wizara hugawanywa tena katika matumizi ya Bodi yaMikopo na matumizi mengine ya ki-mtaji chini ya wizara. Kwa kugharamia elimuya juu kupitia mikopo kwa wanafunzi walioingizwa katika taasisi za elimu ya juu,Serikali imetenga Shilingi Bilioni 431.71; hii ikiwa sawa na asilimia 31 ya jumlaya bajeti ya Wizara na asilimia 47 ya jumla ya bajeti ya Wizara kwa matumizi yamaendeleo, wakati Shilingi Bilioni 465.9 (sawa na asilimia 53) zimetengwa kwaajili ya matumizi halisi ya wizara kwa mwaka wa fedha wa 2016/17.Chati Namba 8: Mgawo wa Fedha za Matumizi ya Maendeleo yaWizara ya ElimuChanzo: Bujeti ya Taifa 2015-16 & 2016-176

Dondoo Muhimu za Kisera:· Bajeti zilizoidhinishwa zitangazwe baada ya kuzingatia deni la taifa kuepukakutoeleweka kwa kuzingatia uwezo halisi wa matumizi ya bajeti ya mwakahusika. Mwaka 2016/17 bajeti iliyoidhinishwa haikujumuisha deni la taifa;hali hii ilifanya takwimu ya bajeti ionekane kuwa kubwa wakati hali halisi siyokubwa kwa sababu sehemu ya bajeti iliyoidhinishwa itatumika kulipa deni lataifa.· Uwiano kati ya bajeti ya kawaida na ya maendeleo umeboreshwa na umekaribiakabisa uwiano unaopendekezwa wa 60:40. Tumeifurahia nia hii ya serikali natunasisitiza kwamba iwe endelevu.· Hata hivyo, bajeti ya Wizara kwa matumizi ya maendeleo bado imechangiwagharama na kiasi cha fedha zilizojumuishwa kwa ajili ya huduma ya mikopo yawanafunzi wa elimu ya juu ambayo tunaiainisha kama matumizi ya kawaida.· Mpango wa bajeti hauna uhusianao na mipango iliyopita kama vile MatokeoMakubwa Sasa ambayo kwao Serikali ilifanya umma kuamini kuwa ni mpangomzuri sana na unaofaa kuboresha elimu.· Usambazaji wa bajeti ya sekta ya elimu kwa wizara mbali mbali kunapinganana misingi ya uwazi na uwajibikaji. Tunapendekeza kuwa sekta ya elimuiendeshwe na wizara moja au kwa kushirikiana na wizara moja tu yenyejukumu la Mamlaka ya Serikali za Mitaa (LGAs).7

Kimeandaliwa na Hakielimu kwa niaba ya Kikundi Kazi cha Policy Forum cha BajetiPolicy ForumS.L.P 38486, Dar es SalaamSimu: 255 22 2780200/255 782317434Baruapepe: info@policyforum.or.tzTovuti: www.policyforum.or.tz8

Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi. Kiasi hiki ni sawa na asilimia 22.1 ya jumla ya bajeti yote ya Taifa ambayo ni Shilingi Bilioni 29,539.6. Takwimu hizi hazijumuishi deni la taifa. Kutokana na takwimu

Related Documents:

Sheria ya Elimu Na. 25 ya mwaka 1978 na Rekebisho Na. 10 la mwaka 1995 ikisomwa pamoja na Waraka wa Elimu Na. 4 wa mwaka 2016 unaohusu mwongozo wa uundaji wa Kamati ya Shule. Ibara ya 3 kifungu cha 39 cha Sheria ya Elimu Na. 25 ya mwaka 1978, inazitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa kuunda Kamati ya

elimu ya juu, Sayansi na Teknolojia. Ilitoa jumla ya tuzo 119 kwa wanafunzi wa kike kutoka shule 20 zilizofanya vizuri katika masomo ya Sayansi na Hisabati katika mitihani ya kumaliza kidato cha nne mwaka 2006 (18); kidato cha sita mwaka 2006 na 2007 (25); vyuo vikuu, taasisi za serikal

katika bajeti ya sekta ya elimu ya Mwaka wa Fedha 2016/2017 ili kutekeleza kwa ufanisi azma yake ya utoaji wa elimu bure, vinginevyo utakuwa ni usanii mtupu, na dhana ya elimu bure inaweza kuwa chanzo kingine cha anguko kuu la ubora

3 RASIMU YA BAJETI YA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 UTANGULIZI Mhe. Mwenyekiti, Maandalizi ya Bajeti ya mwaka 2017/18 yameanza mwezi November 2016 kwa wakuu wa

MUHTASARI WA RIPOTI YA KAMATI YA BAJETI YA BARAZA LA WAWAKILISHI- ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 . kutoa elimu maskulini na michezo. . ambapo Serikali imemuekea sharti la kuanza kuendeleza eneo alilopat

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekuwa ikiboresha Mtaala wa Elimu ya Msingi kuhakikisha kwamba elimu inayotolewa ni bora na inayomwandaa mwanafunzi kumudu maisha katika mazingira yake. Muktadha huu umeifanya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia iboreshe mchakato wa kufundisha

RIPOTI YA DUNIA YA UFUATILIAJI WA ELIMU ilIcMUHTASARI Dibaji Ripoti yaDunia ya Ufuatiliaji wa Elimu ya mwaka wa 2019imeandaliwa kwa kuwashirikisha timu ya wahamiaji wa kimataifa. Wanne kati yao ni watoto wa wakimbizi. Ha

ONLINE REGISTRATION: A STEP-BY-STEP GUIDE CONTENTS OVERVIEW 3 HOW TO LOG IN TO ONLINE REGISTRATION 6 PERSONAL DETAILS 7 1. Personal Information (Gender, Marital Status, Mobile Phone No.) 8 2. Social Background (Occupational Background, No. of Dependants). 9 3. Country of Origin/Domicile 9 4. Home Address 10 5. Term Time Address 11 6. Emergency Contact Details 12 7. Disabilities 14 8. Previous .