Dhima Ya Vyombo Vya Habari Kwako

2y ago
169 Views
2 Downloads
2.25 MB
104 Pages
Last View : 2d ago
Last Download : 3m ago
Upload by : Konnor Frawley
Transcription

dhima ya vyombovya habarikwakoMwongozokwa Mashirika ya Kiraia

IMPRESSUM Uamilifu wa Vyombo vya Habari KwenuMwongozo kwa Mashirika ya KiraiaUmetolewa na:European Journalism CentreOranjeplein 106, 6224 KV Maastricht the Netherlands,www.ejc.netWaandishi:Lisa Essex y Brandon OelofseMwandishi Mwenza:Oliver WatesWahariri:Oliver Wates, Josh LaPorte,Melissa Rendler-Garcia, Odongo Eric MukoyaTranslator:Dr. Sellah Kingo’roPicha:Picha zimetolewa kwa hisani yaThomson Reuters Foundationna Samir M KhanUsanifu na mpangilio:Sharl de WetUmepigwa chapa:Agosti 2015ISBN/EAN:978-90-819305-1-2 Januari 2015 – Matini ya mwongozo huu imeidhinishwa kwa mujibu wa leseniya usambazaji sawa usio wa kibiashara wa kazi za ubunifu wa kawaida.

fahirisidibajiutangulizi0506kuelewa vyombo vya habarikuelewa mitandao ya kijamii0814mawasiliano kupitia vyombo vya habaritaarifa kwa wanahabarivikao vya wanahabarimahojiano223036mawasiliano kupitia mitandao ya kijamiitwitterfacebookkublogumkakati wa mkondoni44546472usimamizi wa mawasiliano yakomaandalizi ya kampeni katika vyombo vya mawasilianomawasiliano kwenye hali ya hatariwajibu wa afisa mawasiliano828896

Picha ya Reuters/ David Mdzinarishvili /kwa hisani ya Wakfu wa Thomson Reuters04

dibajiSuala hili limekuwa chanzo cha kukatishatamaa kwa yeyote anayefanya kampeniya kuboresha hali ya maisha ya watukama vile wanaojitolea, wanaharakati, auwanaofanya kazi katika mashirika yoyoteya kiraia: kwa nini masuala muhimuya kibinadamu hayapati umaarufuyanayostahili miongoni mwa umma?Kimapokeo, tabaka aali la watu wenyeuwezo ndilo lilolaumiwa, yaani makundiyaliyodhibiti vyombo vya habari - matajiriwa magazeti, wakiritimba wa biasharakubwa, serikali za kimabavu, vyama vyasiasa na makundi yenye maslahi maalumuya kitabaka, kidini au kimbari. Wanahabariwangelalamika kwamba walichapisha nakutangaza tu yale ambayo watu walitaka.Hata hivyo, tabaka tawala liliendelewakutuhumiwa kuwa ndilo lililoweka ajendaya habari.Mapinduzi ya mawasiliano yaliyotuleteaintaneti, simu ya mkononi, Facebook,Twitter na Google, yamedhoofisha hojahiyo. Kadiri watu wengi zaidi wanavyopatanyenzo za kufikia intaneti, ndivyo njiazetu za kupata habari zinaendeleakugeuzwa. Uwezo wa tabaka aali, iwapolilikuwepo,umepotezamaana,aukutoweka kabisa. Hawawezi kulazimishakile tunachokitazama. Tunao uwezo wakuchagua vyanzo vyetu vya habari, taarifana maoni kwa kiwango ambacho babuzetu hawangeweza kuota.Na bado twapata kwamba habari muhimuaghalabu ama hupuuzwa au huwa ngumukupatikana. Vyombo vya habari huwavimejaa mambo ya kipuuzi, burudani,uvumi na michezo. Tovuti na vipindi vyahabari huelekea kusheheni hadithi zilezileza zamani - kashfa, siasa, migogoro,michezo na sifa za watu maarufu. Je, hiindiyo gharama tunayolipa kwa kuwa namfumo wa habari wa “kidemokrasia” zaidi?Ni dhahiri kwamba mwongozo huu mfupihauna majibu yote. Mara nyigi huwavigumu kupata umaarafu kutokana na kaziau kile kinachotetewa na asasi za kiraiaau mashirika yasiyo ya kiserikali. Kamaingekuwakuwa rahisi, makundi kampenikama hayo pengine hayangehitajika.Bado ni vigumu kuvutia mabadilikoyanayohitakika, na kwa hakika haliitaendelea kubaki hivyo.Mfumo mpya wa habari duniani wenye“uwazi” zaidi ni jangwa la mahitaji ambayoyanashindana kukidhiwa na umma.Wafanyabiashara hushindana kwa pesazao, wanasiasa kwa kura zao, wasanii kwaendorsement yao, wajuaji kwa pongeziyao. Na wanaharakati hushindana kwamsaada wao, ushiriki wao, uanaharakatiwao, michango yao ya muda na pesa.Wengi kati ya hawa wana utaalamumkubwa mno katika kile wanachokifanya.Wanajua jinsi ya kutania, jinsi ya kunyakuamakini yako, jinsi ya kukushawashi katikaulimwengu wa msisimko wa kijuu juu, siasaza “sound bite” na utoshelezaji wa papokwa hapo. Unahitaji mbinu za kisasa ilikuifanya sauti yako isikike katika makelelehayo. Haitoshi kujali kwa undani tu, balini shauku inayoweza kukufikisha umbalihuu. Unahitaji kichwa kizuri na ujuzi wakuwasilisha harakati na asasi yako kwaufanisi.Asasi ya kiraia (CSO) yenye ufanisi inahitajimkakati wa vyombo vya habari uliofikiriwavizuri, wafanyakazi wa mawasilianowaliopata mafunzo, muda na pesa zakugharamia shughuli zao. Ili kuuwasilisha“ujumbe” wako, haitoshi kuwa sawa;unahitaji kuwa na ujuzi pia. Haitoshikutegemea msaada wa wanahabariwachache wenye ushawishi mkubwaau watu maarufu, inabidi ushindanekwenye vyombo vya habari jadi pamoja namitandao ya kijamii, dunia ya zamani nampya. Uzoefu na mafunzo ni muhimu.Anza na mwongozo huu.Oliver Wates05

utanguliziWewe ni Mkuu wa Mawasiliano wa NGO yakimataifa ijulikanayo kama KosAid, ambayoinajitahidi kutokomeza ugonjwa hatari waAizrah unaoenezwa na maji machafu katikanchi zinazoendelea. Ugonjwa huo, ambaoumeua na kulemaza mamilioni ya watu kwazaidi ya karne iliyopita, ni hatari hasa kwawatoto wenye utapiamlo. Hali ni mbaya zaidiLucidia, nchi kubwa inayoendelea ambayoimesambaratishwa na miongo kadhaa ya vita,utawala mbaya na ufisadi.Mvua nyingi ambazo zimekuwa zikinyeshakwa kipindi cha miezi sita zimesababishamafuriko katika maeneo makubwa ya Lucidiana mfumuko wa ugonjwa huo. Unaenea kwakasi isiyomithilika miongoni mwa mamilioni yawatu ambao wamelazimika kuacha nyumbazao kwa sababu ya mafuriko. Kwa sasawanaishi katika mabanda ya muda au kambiza wakimbizi.KosAid inaamua kuzindua kampeni kubwa yakupambana na janga hili. Inaandaa mkakatiwa mawasiliano wa miezi sita kwa lengo la: 06kuchangisha pesa kutoka kwa umma wakimataifa na wafadhili wakuu kugharamiauanzishwaji wa timu za matibabu bingwa.kuhamasisha wananchi wa Lucidia juu yahatari inayowakabilikuwataarifu watu katika maeneo yamaambukizi kuhusu jinsi ya kupunguzahatarikushauri wagonjwa na jamaa zao kuhusujinsi ya kutibu ugonjwa huo kuhamasisha jumuia ya kimataifa namashirika ya misaada kufadhili kampenihiyo, nakushinikiza wanasiasa wa Lucidia kuhimizauchimbaji wa mifereji ya maji na hatua zakitabibu kupambana na Aizrah.KosAid inazindua kampeni yake kwa kikaocha wanahabari kinachohudhuriwa namwanaharakati maarufu mjini Atlantida(jiji kuu Magharibi mwa nchi). Uzinduzi huounapeperushwa moja kwa moja kwenyemtandao wa intaneti. Tukio hilo linaambanana taarifa kwa vyombo vya habari na ufunguziwa sehemu mpya ya tovuti iliyotengewakampeni na ugonjwa huo. Data, pichana video zinawekwa kwenye tovuti hiyo.Mwanaharakati mtajika na Mtendaji Mkuuwa KosAid wanahojiwa na wanahabari watelevisheni, redio na magazeti.Kikao hicho cha wanahabari kinapeperushwamoja kwa moja kwenye intaneti na tweetkutumwa mara kwa mara. Tovuti mpyainafunguliwa kwenye Facebook. Anwaniza intaneti na namba za simu maalumuzinaanzishwa kujibu haraka maswali na maoniyote kuhusiana na janga hili.Kadiri kampeni zinavyozidi kupamba moto,habari mpya kuhusu michango ya pesana mafanikio katika uanzishwaji wa timuza matibabu zinat marolewa kadhaa kwawiki. Tweet na habari mpya zinatokea/zinasasaishwa kwenye Facebook kila siku.Pindi timu ya kwanza ya wataalamuwa matibabu inafika Lucidia, kikao chawanahabari sawa na kile kilichofanyikaAtlantida, kinaitishwa ila wakati huukinahudhuriwa na waziri mmoja wa Lucidia.Tweet zinatolewa mara kwa mara kwa lengola kufikia watumiaji wa simu za mkononi.Mkuu wa KosAid anaandika makala ya “oped” kwa minajili ya gazeti kuu la kila siku. Hii nimojawapo ya msururu wa makala za aina hiizitakazosambazwa kweye magazeti magazetimaarufu nchini Lucidia.Kadiri timu za wataalamu zinapoanza kazikatika maeneo ya Lucidia yaliyoathirika zaidi,habari zaidi kuhusu ya kuenea kwa ugonjwahuo na jitihada za kuudhibiti zinaendeleakupatikana. Habari hizo zinawekwa kwenyetovuti KosAid na kurasa za Facebook. Mkuuwa KosAid nchini anaandamana na kundi lawanahabari kutoka vyombo vya habari kitaifakuzuru kliniki ya Aizrah. Wanaonyeshwamadaktari na wauguzi wakiwa kazini,wagonjwawaliotibiwanawasiotibiwa,maeneo yenye mafuriko ambako ugonjwahuo unashamiri na uendeshaji wa shughuli zakuutokomeza.Madaktari kutoka nchi mbalimbali wanaanzakuandika blogu kwenye lugha zao juu yakazi wanayoifanya huku wakiweka picha zamaeneo na watu. Hizi zinaenda kwenye tovutipamoja na Facebook na Instagram. Videofupi zenye filamu za mafuriko, wagonjwa namadaktari kazini zinapakiwa kwenye YouTube.Timu hiyo pia inazindua huduma ya simu zamkononi kutuma ujumbe kwa watu walioachamakazi yao kutokana na mafuriko kuhusuugonjwa wa Aizrah, jinsi ya kuutambua,kuzuia maambukizi na kutafuta msaada iwapowameambukizwa. Baada ya shughuli za kikazinyanjani kwa kipindi cha miezi mitatu, viongoziwa kidini hapo wanamshutumu mmoja katikatimu yako kwa kubaka wanawake. Mashtaka

Picha ya Reuters/ Thomas Mukoyakwa hisani ya Wakfu wa Thomson Reutersyenyewe hayana msingi bali yanatokanawanakijiji kutotaka wanawake wagonjwakutibiwa na wageni. Hata hivyo, jambo hililinachukuliwaa na idhaa ya redio ya upinzanina mtandao ya kijamii ya kimataifa. KosAidinaanzisha operesheni ya mawasiliano ya haliya hatari mara moja. Wakurugenzi wa mpangoLucidia na Atlantida wanahojiwa mfululizokubatilisha ripoti hizo. Hatimaye, kisa hichokinafifia na kutoweka baada ya siku.Msururu wa Tweets, uwekaji wa habarimpya kwa Facebook na usasaishaji kwenyetovuti unaendelea. Miezi miwili baadayeziara nyingine kwenda Lucidia inapangwa, ilawakati huu inahusisha kundi la nzi mtendaji na waziri wanashiriki nakuhojiwa, kupigwa picha na kufilamiwa katikaeneo lililofurika vibaya.Kwa vile ziara hii inaadhimisha miezi sitatangu kampeni ilipoanza, KosAid inatoa taarifakwa vyombo vya habari kuhusu maendeleoyaliyofikiwa, ikiwa ni pamoja na jumla ya pesazilichangwa.Je, ungeweza kumudu hayo yote?Ikiwa sivyo, mwongozo huu wavyombo vya habari ni kwa ajiliyako.07

sura ya 1kuvielewavyombovya habari

Wanahabari wana shughuli nyingi namambo mengi hushindania muda namakini yaoSiku ya KaziHebu tuanze kwa kuangalia siku katika maishakikazi ya mwanahabari.Ni kosa kufikiri kwamba neno “habari” linamaana kwamba wanahabari hukaa, wakisubirimambo “mapya” yatendeke. Ingawaje kunamatukio ya ghafla yasiyotarajiwa (kwamfano, ajali ya ndege). Hata hivyo, “habarizinazochipuka” ni sehemu moja tu ya habariza siku.Wanahabari mara nyingi huwasili katikachumba cha habari ambacho tayari kinashughuli nyingi. Wakija asubuhi mapema,watakuwa wanawapisha wenzao wa zamuya usiku. Mashirika makuu ya habari huwana angalau watu wawili wanaokesha katikachumba cha habari, hata kama wana ofisinyingine katika eneo la wakati tofauti.Baadhi ya wanahabari huja ofisini kwa mudamfupi. Kwa hali hiyo, unaweza tu kuwasiliananao kupitia kwa simu ya mkononi, baruapepeau mitandao ya kijamii.Lakini wengi huja ofisini kwa sababuhuenda kukawepo mkutano wa wahariri, aukuhudhuria kikao cha mipango ya habari, aukuona tu kilichofika usiku. Hii ni mojawapo yafursa ya kuwasiliana nao.Mkutano wa wahariri hutumiwa kuchujahabari zote kwa ujumla kuwawezesha wahaririwafanye uamuzi kuhusu kiasi cha mudaau nafasi ya kutengea kila mojawapo. Hatahivyo, kufikiri kwamba uamuzi huu hufanywakwa misingi ya umuhimu wa habari iliyopo nikupuuza mambo.Sehemu kubwa ya habari hususani zatelevisheni, hupangwa awali ili kuratibushughuli za timu mbalimbali, wafanyakazi naruwaza za zamu ya kazi. Uchukuzi wa watu navifaa kuelekea eneo la tukio huchukua mudana wakati mwingine wanahabari huhitajivibali mbavyo huombwa mapema. Habari hiziambazo hupangwa awali mara nyingi huitwa“shughuli za kishajara”.Aina ya mambo ambayo yanaweza kupangwawiki, au hata miezi, mapema ni pamoja namaadhimisho ya siku ya ukumbusho, shughulirasmi na matukio ya kampuni yaliyopangwa.Hii ni fursa ya kipekee kwako kupata “kigingicha habari” – yaani tukio linaloweza kutumiwakupata habari inayoweza kuchapishwa kuhusumada au kampeni ya muda mrefu.Habari kuu - kwa mfano feri iliyotoweka- haitapewa kipaumbele iwapo itakosapicha, mahojiano ya nguvu na habari mpya.Habari yako inaweza kuwa na nafasi nzurikuzingatiwa iwapo utatoa habari muhimukutoka kwa mtaalamu au usafiri kwendaeneo linalohusika. Shirika la habari lenyewelinaweza kuwa na mwegemeo fulani - kwamfano kuunga mkono au kupinga serikali.Kwa hivyo, unahitaji kujua iwapo kuna maslahiyoyote yanayohitaji kufahamika. Na ikiwakuna habari inayochipuka, kama vile motoau ajali ya treni, usitarajie ya habari yakoizingatiwe siku hiyo!Ukikosa wanahabari mwanzoni mwa siku,kuna uwezekano watakuwa nje ya chumba chahabari wakifanya mahojiano, wakihudhuriavikao ya wanahabari, wakifanya vox Populi,utafiti au wakikusanya data. Ni muhali kwahabari kutokea katika chumba cha habari!Wanahabariwengihuwahawapatimapumziko ya chakula cha mchana, hatahivyo wanapopata, watakuwa radhi kukutananawe kupata uvumi wowote mzuri. Usiwena mazoea ya kushinikiza habari zako,unaweza kujenga mwamala mwema bilakutarajia kuchapishwa kwa habari yako.Iwapo utamaduni wako unaruhusu, unawezakuwa na bahati zaidi endapo utawaalika kwakahawa au kinywaji baada ya kazi.Alasiri mapema ni fursa nyingine nzuriya kukutana na wanahabari ofisini kwasababu mashirika mengi huwa na kikao chaalasiri kupanga mambo ya siku ifuatayo aukukamilisha habari za jioni.10

Kumbuka kwamba kadiri mwisho wa sikuunavyokaribia, ndivyo makataa zinavyokaribiana kutisha zaidi. Makataa yenyewe inawezakuwa kipindi cha taarifa ya habari ya jioni,au wakati ambapo gazeti hupelekwa kwenyematbaa.UsimuliziKadiri inavyowezekana, jaribu kuwapigiasimu au kutumia baruapepe kwa wanahabariasubuhi. Kosa la kawaida huwa kutumiamchana kutwa kuandaa taarifa kwa vyombovya habari na kisha kuituma alasiri, wakatiambapo wanahabari na wahariri huwambioni kutimiza makataa yao. Wanahabariwa radio na mawakala wa habari huwasilishahabari muda wote, kwa hivyo, huwa vigumukuwapata. Iwapo unajishughulisha na gazeti lakila wiki, waulize kuhusu siku ya makataa yaokisha ujitahidi kuzungumza nao siku tofauti.Waulize kuhusu ratiba yao, watafurahia.Hakunasababukulalamikakwambawanahabari WANAPASWA kujali kuhusuhabari yako kwa sababu ni muhimu. Kwamwanahabari mwenye Inbox iliyojaa naanayezomewa na mhariri wake, habariyako haitamsisimua usipoiuza kwa bidii, nausimfanyishe mwanahabari kazi ngumu yakubaini maana ya habari yako.iwapo unafikiri kuhusu kutumia Twitter,kumbuka kwamba majira ni muhimu kwasababu arafa za Twitter hupita haraka mno.Sio baruapepe, kwa hivyo ukituma maramoja kwa siku kuna uwezekano kwambawatu watakosa ujumbe uliotuma kwa sababuhawakuwa wakiangalia wakati ulipotuma.Si jambo la busara kutuma arafa nyingikuhakikishakwambaujumbewakounaonekana, unachohitaji ni kutuma arafa zakowakati unaofaa. Fikiria iwapo mwanahabaribusy atakuwa anaangalia Twitter mchana,wakati ambapo wapo uwandandani wanahoji,wakiandika na kuchukua filamu.Kutuma tweet yako kama Jambo la kwanzaasubuhi kunaweza kuiweka katikati ya habarinyingi mno, kwa hivyo kuituma mwendo wasaa nne asubuhi kunaweza kuwa jambo labusara zaidi.Mara baada ya kumpata mwanahabarihuna budi kuteka makini yao. Hii ina maanakuwapa habari inayoweza kupita wahariri nakuchapishwa katika jarida au gazeti.Hakikisha ni wakati mzuri wa kuzungumzaunapowapiga wanahabari simu. Muulizemwanahabari, “Je, una muda wa kuongea?” au“Je, una makataa?” Maswali haya yataonyeshaunaelewa na kuheshimu shughuli zao nyingina wala sio utani.Ukizungumza na mwanahabari, aukuwasiliana naye kwa njia zingine,unahitaji kufanya “usimulizi”.Usimulizi ni ufafanuzi wa wazo la habariambayoungetakaitumike.Usimulizihubainisha umuhimu wa habari. Kimsingi,usimulizi hujenga hoja ni kwa nini habarifulani inawasilishwa wakati fulani. Usimulizimzuri unapaswa kufupisha kwa haraka habariambayo mwandishi anataka kuandika naueleze ni kwa nini habari hiyo ni muhimu KWAMWANAHABARI AU KWA JAMII, WALA SIO KWANINI NI MUHIMU KWAKO!Huu hapa ni mfanombaya:“Aisee, Bi Mwanahabari. Ninakutumiakurasa 300 za makala ya utafitiinayoelezaumuhimumajisafi.Unapaswa kuitumia.“Huu hapa ni mfanomzuri:(zingatia “umuhimu” wa habari NAusimulizi)“Umeona habari leo kwambaserikali inasema inacheleweshamipango ya kuweka mabomba yamaji katika sehemu ya kati ya nchi?Utafiti wetu unaonyesha kuwawatoto 100,000 watakuwa katikahatari ya magonjwa yanayotokanana maji. Tunaweza kukupelekakijijini ambapo watu wamekuwawakisubiri usambazaji wa majisalama kwa miaka 10.”Tumeona jinsi ambavyo siku mwanahabarihuwa na shughuli nyingi, kwa hivyo, ni dhahirikwamba wakati wa kufanya usimulizi wakosio siku ambayo tangazo limefanywa auripoti kutolewa. Usimulizi ufanywe siku mojakabla, siku mbili kabla au wiki moja kabla, ilimwanahabari afanye mipango ya kutenganafasi katika toleo la gazeti au kipindi chamatangazo kinachohusika.11

WanachotakaUmuhimu wa habari ni kile hufanya kisa kuwachenye thamani ya habari au cha wakati huo.Yawezekana umekuwa ukiendesha kampeniya chanjo kwa miezi, lakini serikali ndiyo hutoadata ya vifo vya watoto. Hiki ndicho kipengelekinachofanya habari hii kuwa ya wakati namuhimu sasa. Hiki ndicho kitakachowafanyawanahabari watake kuitumia hadithi yako.Wanahabari wengi huhitaji aina fulani yaumuhimu wa habari kabla hawajafikiriakutumia. Umuhimu huo usipokuwa dhahiri,huna budi kujaribu kuutafuta au uhatarishekazi yako kukataliwa kama isiyo na maana.Ukosefu wa umuhimu wa habari ni njiamojawapo ya kuwafanya wanahabari kuikinaihadithi yako.Mahusiano na WanahabariPamoja na kutolewa kwa data mpya, kunaaina nyingine za umuhimu wa habari. Kwamfano, mtu maarufu kutembelea mojawapoya miradi yako, au mabadiliko ya sera auufadhili mpya.Haitoshi kuchukulia kwamba utakuwa nauhusiano mzuri kitaaluma na wanahabarimashuhuri kwa sababu ya wadhifa wako tu,huna budi kuufanyia kazi kama ilivyo katikamaisha yako binafsi. Hebu tuanze na vidokezovichache kuhusu jinsi ya kukuza uhusianoimara na wanahabari.KunukuuWanahabari pia wanahitaji “nukuu la sauti” au“dondoo la kipekee”. Haijalishi ujumbe wakoni wa kushangaza namna gani, usipowapaangalau video ya sekunde 20, hawatautumia.Hili ni kweli hasa katika utangazaji watelevisheni na redio. Si lazima utoke kwako- kwa hakika ni bora hivyo - mtaalamuau mfanyakazi wa mstari wa mbele aumwanaharakati huaminika zaidi kuliko afisawa uhusiano mwema. Hata hivyo, kwa njiamoja au nyingine, huna budi kutoa habari hizokwao.12Unaweza kuipata njia hii ya “nukuu la sauti”fupi kuwa ya kijuujuu, na uhisi hadhira yakoinahitaji muda na kina zaidi – hata hivyoukweli ni kwamba hadhira ya watazamajihabari haiwezi kuwa makini kutazama taarifandefu. Filamu na makala yatakupa mudamrefu zaidi kuwasilisha ujumbe wako, lakinini ghali na huchukuwa muda kutekeleza. Kwasababu hiyo mashirika ya habari hayawezikuziwasilisha kwa wingi.Wanahabari wengi huwa na uhusiano msetona vyombo vya habari au wataalamu wauhusiano ya mwema. Wao hulalamikia halikwamba maafisa wa habari ni wasumbufu,hawajibu simu, au hushindwa kuelewa jinsiwanahabari walivyo na shughuli nyingi. Kutana wanahabari ana kwa ana. Waalikemshiriki kahawa na chakula cha mchana.Kwa kadiri wanavyokujua ndivyo kunauwezekano zaidi kwamba watatumiahabari zako. Usiwaite wanahabari tu wakati kunahabari kubwa. Piga simu katika nyakatitulivu pia. Mazoea hukuza imani nauaminifu. Uwe mwenye heshima na mzuri.usiscreamie wanahabari, hata kamaunahisi wamekukosea wewe binafsi aushiriaka lako. Toa habari. Wanahabari watakuwa na niaya kuzungumza na mtu wanayefahamuanajua habari wanazotafuta. Chukua muda wako na usitarajie matokeopapo hapo. Bainisha masharti ya kuzungumza nawanahabari. Kubaliana nao apishwa”. Endeleza uhusiano wa kibinafsi na kirafikina waandishi wa habari. Kwa mfano, jaribukutumia maslahi yoyote maalumu (muziki,michezo, nk) unayoweza kushirikiana nao. Chunguza ni wanahabari gani ambaoNGO zingine zinazungumza nao, kwa ajiliya mawasiliano nao iwezekanavyo. Patia magazeti / magazini za biashara/ tovuti kutambua ni nani anayeandikakuhusu eneo lako la taaluma. Timiza ahadi zako. Ukiahidi mwanahabaritaarifa, uwepo au mahojiano maalumukufikia wakati fulani, timiza; au angalaupiga simu kueleza kwa nini haitawezekana.Angalizo:“Wakati mwingine rafiki, daimamwanahabari”nimsemomuhimu.”Kumbuka - ajenda yako nikukuza shirika lako, ajenda yao nikuchapisha au kutangaza habariinayovutia. Haijalishi iwapo habarihiyo ni chanya au hasi kuhusumaslahi yako. Hicho ndichowanahabari hufanya - angalauwale ambao bado wana kazi.

picha/ Samir M Khan /www.behance.net/sk5sami13

sura ya 2kuelewamitandaoya kijamii

kuelewa mitandaoya kijamiiWataalamu wa mahusiano ya vyombo vyahabari wanapaswa kukabiliana na hadhirazote mbili. Watumiaji wa mitandao ya kijamiiwanaweza kuwa na usuli na motisha tofautina wanahabari wa kitaaluma. ijapokuwautatumia habari na mbinu zilezile kutungakile unachotaka kukisema unapokabiliana nahadhira zote mbili, kila kundi hushughulikiwakwa njia tofauti.Kabla ya mwanzoni mwa miaka ya 2000“mitandao ya kijamii” ilimaanisha kundi lawatu wanaotazama filamu au kuwasilianawakiwa wanacheza mchezo wa video pamojakwenye jumba la michezo. Leo hii dhanahiyo inajumuisha majukwaa ya kidijitaliambako mamilioni ya watu hubadilishanamawazo, wanavyopenda na kuchukia, kuundajamii za mtandaoni na kuitikia matukioulimwenguni kote.Tumeunda jamii changamano ya kidijitaliinayoonyesha mahusiano ya mtu binafsina ulimwengu anamoishi na mawazo yakekuhusu ulimwengu huo kupitia mazungumzoyake. Mitandao ya kijamii ni pamoja naTwitter, Facebook, blogu, YouTube, Instagram,Linkedin na mingine mbalimbali iliyoundwakuchochea mazungumzo na kuunda jamiiza mtandaoni.Ni wakati mgumu kwa wataalamu wamahusiano ya vyombo vya habari kuuongozaulimwengu wa mitandao ya kijamii isipokuwawafahamu hadhira yao, wakutane nao kwenyemajukwaa wanayotumia, na kujiunga katikamazungumzo.16Mojawapo ya mambo muhimu ya kuzingatiaunapotumia mitandao ya kijamii ni kwambaunaanzisha mazungumzo. Mazungumzo nimchakato wa njia mbili ambao wewe, kamamshiriki katika mazungumzo, husikiliza nakujibu. Mashirika mengi hutumia mitandao yakijamii kama ambavyo wangetumia tangazo laTV au bango - tangazo kwa hadhira au mlio wabaragumu kutangaza mambo kuhusu shirikalenyewe.Shirika linapotumia mitandao ya kijamii kwanjia hii, aghalabu huwa halina na mwonekanomkubwa: tweet zao hazitumwi tena wafuasiwao, ukurasa wao huonwa lakini haupendwina jamii za mtandaoni ambazo huelekeahuwatenga badala ya kukubali kuwajumuishakatika marafiki zao.Unapotazamia mitandao ya kijamii ifikiriekama kuingia kwenye dhifa, kaida zilezile zakijamii hutumika, jiunge na mazungumzo,usisimame pembeni ukipayuka chochotekijacho akilini mwako, hususani kama niajenda.Jamaa asiyependwana wengi chumbaniMtu anaingia kwenye tukio kijamii,anatangazia kila mtu “Mambo! jinalangu ni Tim, niko hapa”.Umati wa watu anamwona Tim nakwenda kumwamkia.Tim anasema “Je, mngetaka kuonanilivyo mkuu? Wiki iliyopita niliandaakikao cha wanahabari. Kilikuwa chakufana mno.”Tim anaendelea kusema, “Shirika langulilishinda tuzo, hii hapa ni picha yake”.Wachache kwenye umati wa watuwanasonga mbali.Mtu anauliza Tim iwapo aliona makalaambayo inaweza kunufaisha shirikalake. Tim anampuuza mtu huyo nakuendelea kuzungumza kuhusu jinsishirika lake lilivyotia saini mkataba namfadhili mpya. Tim anadai umpende.Wenginekwenyekundihilowanajiondoa na kwenda kuzungumzana mtu mwingine. Wale walioachwawanaanza kuzungumza kati yaokumhusu Tim.Tim anatoa taarifa “Tunaenda kwenyekongamano wa wiki ijayo!”.Hatimaye wachache wa mwishowanaondoka, lakini Tim anasimamapembeni akijizungumzia mwenyewe.

Picha ya Reuters/ David Mercado /kwa hisani ya Wakfu wa Thomson Reuters17

kanuni muhimu za mitandao ya kijamiiUtendakazi wa mitandao ya kijamii kwa kiasi kikubwa hutegemea uundaji wa jamii. Jamii ni watu watakaopenda au kufuata mtandao wa kijamiiwako, watakaoingiliana nawe, wakaoshiriki katika majadiliano yako na kukusaidia kufikia malengo ya kampeni zako.Maslahi Sawia Umoja JamiiHizi hapa ni kanuni tatu za kuzingatia unapopanga mkakati wa mtandao wa kijamii wako.WajueWataalamu masoko walio wengi hubainishawanayezungumzanayewanapoandaamatangazo au vifaa vya mawasiliano /kampeni kwa ajili ya mashirika yao.Hawa wanaitwa “hadhira lengwa” yao.Hadhira lengwa ni bayana. Wanapoundanyezo za mawasiliano, kila mtaalamu wavyombo vya habari anapaswa kufahamu kwauhakika shirika lake linazungumza na nani.Je, unazungumza na wafadhili, wanahabari,wanasiasa, wanajumuiya ambapo shirika lakolinafanya kazi, au watu wanaohusika katikamradi wako? Kujua ni nani ano. Linganisha jinsi vijana na watuwazima huzungumza. Hakuna mwanamasokoanayeweza kudhubutu kuzungumza na vijanakwa njia sawa na watu wazima. Vijana hutumialugha tofauti au mchanganyiko wa lugha.Kama shirika, njia nzuri ya kuielewa hadhiralengwa yenu kubungua bongo mawazomachache kuhusu mnayetaka kumfikia.Zingatieni kinachopendwa na hadhira yenu,wasichokipenda, wanachotazama, manenowanayotumia, mashujaa wao na namna yakuwavutia mashujaa hao upande wenu. Ninguo zipi wanazovaa, ni kitu gani huwasisimuana iwapo unaweza kupata picha za watu haona kujadilina na wanachama wa kundihicho.18Mara ukishaifahamu hadira lengwa yako,zingatia mtandao wa kijamii inayoatumiana jinsi unavyoweza kukutana nao walipo.Mitandao hiyo huenda isiwe majukwaamakubwa kama vile Twitter au Facebook.WahitajiHadhira yako haikuhitaji, unaihitaji. Kwakuonyesha hitaji lako au kuwa wazi kuhusuazma ambayo shirika lako linajaribu kufikia,utashangazwa na mwitikio wa hadhirayako kwako. Mahitaji yako yanaweza kuwakuhamasisha au au kusaidia kufikia lengofulani. Chochote kiwacho kile, iombe hadhirayako msaada kwa uwazi na uaminifu.Njia bora ya kufikia uaminifu ni kutoa habariya kihisia. Watu huitikia kunapokuwepouhusiano wa kihisia na kitu au mtu. Hadhiraitajibu uwasilishaji wa habari halisi, yakuaminika na yenye hisia.Mnamo mwaka 2013 kipindikidogo cha runinga cha Kiboliviakwa vijana kiitwacho “Pica,”ambacho kililenga masuala namaoni ya vijana, kilikuwa hatarinikuzimwa.Kilikuwakimevutiawafuasi wengi miongoni mwavijana nchini Bolivia. Hata hivyo,idhaa ya serikali haingepeperushakipindi hicho tena. Timu ya Pica,shirika lisilo la kibiashara, liliombamashabiki wake wa Facebook4,000 kuwasaidia kuchanga pesakatika mradi wa “Salvamos Pica!”(tuokoe Pica!).Vijana wa Bolivia waliitikia wito huowa msaada na kuchangisha pesa,wakatoa muda wao na kuandikabarua kwa serikali, idhaa ya serikalina mashirika mengine yaliyoungamkonoPicanchiniBolivia.Matokeo ya juhudi hizo yalikuwakwamba Pica ilipata ufadhili nakuendelea kupeperushwa.

WashirikisheLKampeni kubwa zaidi kwenye mitandaoya kijamii – The Arab Spring, The Occupycampaign au Kony 2012 - zinaonyeshauwezo wa mitandao ya kijamii kusababishamabadiliko. Kiini cha kampeni hizi ni wito wanguvu kwa hadhira kujihusisha kwa njia mojaau nyingine. Katika kampeni ya The ArabSpring hadhira ilishriki kwa kupakia ujumbewa video, kutuma ujumbe wa msaada nakusambaza taarifa, kila mtu akipaza sautikueleza kutoridhika kwake na kuishi chini yaserikali dhalimu. Katika kampeni ya Occupy(dhidi ya ulafi wafanyikazi wa benki wanyadhifa za juu) kushiriki kulikuwa kujiunga nakampeni na malengo yake maalumu. KatikaKony 2012 (kuhusu dhehebu la mauaji la AfrikaMashariki na ya Kati) mitagusano miongonimwa hadhira ilikuwa kumfanya Joseph Kony“maarufu” katika mji yao kupitia matukio ya“paka mji rangi nyekundu”.Kuishirikisha hadhara yako si lazima kuwekwa njia kubwa kama ilivyokuwa Arab Spring.Hata hivyo, unapaswa kujitahidi kujengamazungumzo, jamii na maingiliano bainaya shirika lako na hadhira. Msukumo wazihuwafanya watu kuchukua hatua; hakikishaunaiambia hadhira waziwazi jinsi unavyotakawahusike na kile wanachoweza kuchangia.Kumbuka, watumiaji wa mitandao ya kijamiisio wanahabari kitaaluma. Ingawa unawezakutumia nyingi katika mbinu zilezile kufumaunachotaka kuziambia hadhira zote mbili,kila mojawapo mara nyingi huwa na usuli namotisha tofauti sana.Mitandao ya kijamii ni mahali pa kuwambunifu. Kwa sababu kila mtu anawezakuifikia huduma hiyo, kila wazo linawezakujaribiwa. Baadhi yatachukuliwa na kuwa“virusi” - yatachukuliwa na kusambazwa namamilioni ya watu mtandaoni. Vikwazo vyavyombo vya habari vya jadi havina nafasi hapa.Mfano wa hali hii ni ukuaji wa “changamoto yandoo ya maji ya barafu” kuchangisha pesa zakupambana na magonjwa. Watu humwagiwandoo za maji baridi ya barafu kisha hutumavideo, kama changamoto kwa wenzaokufanya vivyo hivyo. Ilipoanza mnamo mwaka2014, pamoja na kuhamasisha umma kuhusumagonjwa, changamoto hiyo ilichangishamamilioni ya dola katika kipindi cha wikichache.Angalizo:Mitandao ya kijamii inaweza kuwa hatari pia. Maoni yasiyo kadiri yaliyotumwakutoka usiri wa chumba chako cha kulala kwenye utulivu wa jioni yana uwezo wakuwa dhahiri kama mahojiano ya moja kwa moja kwenye studio ya televisheni.Usiliwazwe katika hali ya usalama ya uongo.19

mawasilianokupitiavyombovya habari

picha/ Samir M Khan /www.behance.net/sk5sami

sura ya 3taarifa kwawanahabari

Taarifa kwa Wanahabari ingali kiinicha Habari ya shirika kwa vyombovya habariSio kile kipande cha karatasi cha kizamanikilichotumwa kwa wote kwa njia ya posta aukilichotolewa kwenye “matukio” ya vyombovya habari, lakini toleo lililotayarishwa kwamakini kusema unachotaka kukisema kwaufanisi kadiri iwezekanavyo. Inaweza kuundakiini cha “ujumbe” utakaowasilishwa kwavyombo vya habari na mitandao ya kijamii.Pamoja na hayo, idadi kubwa ya taarifa kwavyombo vya habari huwa hazina habari, huwazimeandikwa vibaya na ni ndefu mno. Ipo hajakutumia muda kuziandaa vyema, ili kwambazihabarishe na kuvutia sio tu kwa vyombo vyahabari vya jadi, bali kwa hadhira ya mitandaoya kijamii vilevile.Uandishi wa taarifa kwa wanahabarihuonekana kuwa kazi ngumu. Mbali na kuwana mengi yanayofanana na uandishi mzuri wahabari, inahitaji kufanywa vyema. Ijapokuwaunaandika taarifa ili ichapishwe kwa manufaaya umma, mlengwa wako mkuu anapaswakuwa mwanahabari au mhariri, kwa sababuwao ndio huchuja kinachosomwa na hadhirapana.MuundoUnapoandaa taarifa kwa wanahabari, WA, ambao aghalabu hutumiwana mashirika ya habari katika uandishi wahabari. Sehemu pana ya chini ya umbo lapiramidi inawakilisha taarifa kubwa zaidi, yakuvutia na muhimu tunayojaribu kuwasilisha.Habari ya aina hii sharti iwe kichwa chamatini, ilhali sehemu ya chini iliyochongokainaonyesha kwamba habari nying

huo unashamiri na uendeshaji wa shughuli za kuutokomeza. Madaktari kutoka nchi mbalimbali wanaanza kuandika blogu kwenye lugha zao juu ya kazi wanayoifanya huku wakiweka picha za maeneo na watu. Hizi zinaenda kwenye tovuti pamoja na Facebook na Instagram. Video fupi zenye filamu za mafuriko

Related Documents:

Ndugu Waandishi wa habari, Awali ya yote, ninamshukuru Mwenyezi Mungu aliyetuwezesha kukutana mahali hapa leo. Pia, ninamshukuru Mh. . Ukaguzi wa Ufanisi kuhusu Upatikanaji usioridhisha wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi yenye ubora kwa Watanzania. 12. Ripoti ya ufuatiliaji wa mapendekezo ya ukaguz

Kwa hivyo hii ni sanaa ambayo haiwezi kupuuzwa kutokana na majukumu mbalimbali inayotekeleza. Vyombo vya habari virnetenga masaa kadhaa ya kuwabUiudisha watu kwa kuturnia nyimbo mbalimbali. Balisidya (1987) anakubali kuwa sanaa hii ni sehernu mojawapo ya fasihi K

3 Kuanzisha zaidi ya vituo 180 vya mafunzo ya awali ya mtoto vya Tucheze Tujifunze (Vituo vya TuTu) katika maeneo ambayo upatikanaji wa elimu, pamoja na elimu ya awali bado ni duni. Kuandaa video shirikishi kwa ajili ya kutoa miongozo ya kuwaimarisha walimu katika u

ya mwongozo na Novemba 2016, tulisambaza kwa wajumbe wa awali karatasi ya majadiliano inayoonyesha mifano ya kazi zilizopo ambazo zilikuwa tayari zinaendelea katika nchi zingine, kwa mdhumunj ya kuzalisha viwango vya maendeleo ya jamii. Kundi la

5.Kwa kutumia mifano ya sentensi eleza dhima tano (5) za mofimu "ku" (necta2007) 6.Viambishi awali na viambishi tamati vina uwezo wa kubadili umbo na maana ya neno. Katika maneno yafuatayo eleza dhima ya kila kiambishi. a)Watakapotupambanisha b)Sielekezi 7.Upatanisho wa kisarufi hufanya nomino mbalimbali kuwa katika kundi moja.

alikuwa ametakiwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kueleza ni kwanini alimruhusu mwandishi wa habari kuandika taarifa ambayo . Ibara 3 (e) ya Katiba ya MCT inataka Baraza kuwa na taarifa kimandishi za matukio yanayoweza kuzuia upatikanaji wa taarifa zenye manufaa na umuhimu kwa jamii, kuweka muendelezo wa mara kwa mara wa

njema. Aidha aliyeelimika anauw zo wa kufanya maamt1Zi ·tasawari kuhusiana na uchumi na siasa hususan kutokana na mbinu anu ii:zak pata habari na uwezo.wal uzitathmini. Uwezo wako wa kuwaiiahiambohupigwa msasakupitia elimu. Kinyume na siku za :; ' , ' ' kisogoni, kupata habari kurrierahisishwa na ukuiiji wa teknolojia m'athalan mtandao wa kijamii.

appointment before or immediately after accepting an appointment, bearing in mind the terms of the arbitration agreement, including any arbitration rules and the law of the place of arbitration (lex arbitri). 2. The terms of appointment should be recorded in writing and should address the nature of the appointment, arrangements for the arbitrators’ remuneration and any other material terms .