Ufalme Wa Aina Mbili —Wa Dunia Na Wa Mbinguni

1y ago
13 Views
2 Downloads
2.04 MB
8 Pages
Last View : 16d ago
Last Download : 3m ago
Upload by : Nadine Tse
Transcription

ToleoToleo26XUFALME WA AINA MBILI—WA DUNIA NA WA MBINGUNIKwa maana sisi, wenyeji [uraia, serikali] wetuuko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamiaMwokozi, Bwana Yesu Kristo. —Wafilipi 3:20Mashujaa wa imani ambao wanatajwakwa mapana na marefu katika kitabu chaWaebrania walitoka nchi mbali mbali, waliishikatika vizazi tofauti tofauti, walikuwa vifo vyaaina tofauti tofauti, lakini wote walishirikijambo moja: macho yao wote yalifunguliwa namwanga wa kiroho ambao uliwafanya kukirikwamba “walikuwa wageni, na wasafiri juuya nchi.” Na wakati wakitafuta nchi yao yambinguni lengo lao halikuwa kuwa makini aukusumbuka na mambo ya nyumba zao za humuduniani.Watoto wa Mungu ambao wanaishi sasahawana budi kuelewa kwamba wao ni watotowa falme mbili. Ufalme mmoja ni wa hapaulimwenguni na ufalme ule mwingine niwa kiroho. Mtu huingia ufalme mmoja kwakuzaliwa kimwili, na ule ufalme mwinginehuingiwa kwa mtu “kuzaliwa tena” kwa Rohowa Mungu (Yohana 3:3). Yesu Kristo ndiyemtawala wa ufalme wa pili, na Yeye alisemakwamba, “Ufalme wangu sio wa ulimwenguhuu. Kama ufalme wangu ungekuwawa ulimwengu huu, watumishi wanguwangenipigania” (Yohana 18:36). Ufalme waMungu uko ndani ya kila mtoto wa Munguambaye ameoshwa na damu yake Yesu (Luka17:20-21). Huu sio ufalme wa kisiasa bali niufalme wa “haki na amani na furaha katikaRoho Mtakatifu” (Warumi 14:17).Watoto huwa raia wa nchi ambayowamezaliwa. Ni jambo la kawaida na linalofaakwa watoto kukua huku wakiwa na upendowa kuitambua nchi zao. Uraia ni sehemu mojaya vile watu hujitambua na ni moja ya mamboyanayowezesha watu kujitambua kibinafsi.Kujifunza Biblia:Mafundisho ya BibliaKuhusu Msimamo waMkristo wa KutopingaUkweli wa Injeli Toleo 24Mtu Mwovu4Tahariri3Lakini wakati mwingi watu huvutwa na rohoya utaifa wao na pia roho ya kujitolea kwa nchiyao. Watoto wao hufanya nadhara na uaminifuwao kwa nchi yao ya kidunia na hata kuilindahivi kwamba wakati mwingine wanafikia hatakumwaga damu kwa ajili ya nchi zao. Wakatimwingi upendo huu kwa taifa huandamana naroho ya watu kujisikia kwamba wao ni borakuliko watu wale wengine, jambo ambalo nikinyume na Roho wa Mungu. Mara nyingimaslahi ya nchi moja huwa kinyume kabisa namaslahi ya nchi nyingine. Je, ni serikali ganiau ni watu gani ambao wanafaa zaidi machonipake Mungu? Je, ni taifa gani au ni malengogani ambayo Kristo anaweza kutoa nadhiri aukujitoa kwayo? Ukweli ni kwamba katika Kristo“Hamna Myahudi au Myunani” (Wagalatia3:28) kwa maana hata ingawa haya ni mataifatofauti watu wote wa nchi hizo ni wa kiwangosawa katika Ufalme wa Mungu kupitia kwampango mkuu wa wokovu.Hata ingawa watakatifu wa Mungu ni wananchiwa ufalme wa kidunia ambao ni nchi zao waowameitwa kuwa wageni na watembezi dunianiwakati wakitafuta mambo ya kiroho katikaupendo na utumishi wao kwa Mungu. Watotowa Mungu huwajibika kwa mwito wao wa juuzaidi na kwa jambo ambalo linahitaji uaminifuna kujitolea zaidi kuliko matakwa ya mataifa yaulimwengu huu.Sisi kama wananchi wa ufalme wa duniani nawa kiroho moja ya falme hizo ndiyo ambayotutatilia umuhimu zaidi. Hata ingawa nimuhimu kwa watakatifu kuheshimu nchi zaona kuwa wananchi wenye bidii ambao wanatiisheria za nchi zao, wao wanahitaji kujitoleamhanga na kufanya imani zao, tabia zao,maisha yao ya kila siku, ulingana na ufalme wa“Kwa kweli kufunga ninjia ya mtu kufunguaakili na roho yake nakunyenyekea mbelezake Mungu, jamboambalo linamwezeshakushirikiana naBwana kwa njia yakaribu zaidi katikamambo ya kiroho.”(Endelea katika Ukurasa 2)Mafundisho ya Biblia:Mafundisho ya BibliaKuhusu MkristoKutopinga MtuMwovu5Maswali na MajibuJe, Wajua?Neno Linalofaa kwaMsimu Huu78

(Inaendelea kutoka Ukurasa 1)Mambo AmbayobibliaInafundisha Kuhusu.Neno la Mungu2 Tim. 3:6, 2 Pet. 1:20-21, Mt. 24:35Uhusiano wa UpendoMt. 22:37-40, Yn. 14:21-23, 1 Yoh. 4:7-21TobaMdo. 3:19, 17:30, 2 Kor. 7:10Uzao MpyaYn. 3:3-7, 2 Kor. 5:17, Rum. 6:1-4,Efe. 2:1, 5-6Uhuru Kutokana na Dhambi1 Yoh. 5:18, Mt. 1:21, Yn. 8:11Ujazo wa Roho Mtaka fuMdo. 19:2, 15:8-9, 1:8Utaka fuLk. 1:73-75, Ebr. 12:14, 1 Pet. 1:15-16,Tit. 2:11-12, Rum. 6:22Ufalme wa MunguLk. 17:20-21, Rum. 14:17, Yn. 18:36KanisaMdo. 2:47, Efe. 4:4-6, 1 Kor. 12:12-13,Kol. 1:18UmojaYn. 17:20-23, Gal. 3:28, Ufu. 18:2-4Kanuni za KanisaMt. 28:19-20, 26:26-30, I Kor. 11:23-27,Yn. 13:14-17Uponyaji wa KiunguLk. 4:18, Isa. 53:4-5, Yak. 5:13-16Utaka fu wa NdoaMt. 19:5-6, Lk. 16:18, Rum. 7:2-3,I Kor. 7:10-11Urembo wa NjeI Tim. 2:9-10, I Kor. 11:14-15, Kum. 22:5Mwisho wa Nyaka 2 Pet. 3:7-12, Yn 5:28-29, 2 Kor. 5:10,Mt. 25:31-46Kupenda AmaniLk. 6:27-29, 18:20IbadaYn. 4:23-24, Efe. 5:19, 2 Kor. 3:17Wajibu MkuuMk. 16:15kiroho badala ya ufalme wa kidunia. Wakati Yesu alipowaombea wanafunziwake, katika Yohana 17:14-16 alisema kwa wazi kwamba wafuasiwake hata ingawa walikuwa wangali ulimwenguni, wao hawakuwa waulimwengu huu.Wafuasi wa Yesu watakuwa na malengo na nia tofauti na zile ambazozinaonekana katika falme za ulimwengu huu. Watakatifu wa Munguwanahitaji kujikinga dhidi ya moyo yao na maisha yao kuambatana na nchizao ili misimamo ya nchi zao isingongane na kanuni za kimsingi kuhusuupendo na unyenyekevu ambazo ndizo zinahitajika katika ufalme wakiroho. Roho inayoleta misimamo mikali ya kisiasa au roho ya kimwili yakuipinga serikali sio mambo ambayo yanalingana na Maandiko, hata iwe nikwa sababu yoyote ile.Hata ikiwa watakatifu walioko ulimwenguni kote ni wa tabaka, taifa, nalugha tofauti, umoja wao unapatikana ndani yake Yesu Kristo. Umoja huokamwe hauhitaji kuvunjwa, na kamwe watakatifu hawastahili kuwa naubishi wa mmoja kwa mwingine kwa ajili ya falme za kidunia. Watakatifuni watu “walioitwa kutoka (duniani)” nahivyo wanahitaji kuishi kwa msingi huo.“Kuna msimamo ambaoWakristo wanawezakuwa nao ambaokupitia kwake tutawezakuishi katika amani nakutambua kwamba hataingawa sisi tunaishikatika falme za kiduniautaifa wetu ulio mkuu naMtume Paulo akisema kuhusu vita vyakiroho katika 2 Timotheo 2:4 alisema,“Hakuna apigaye vita ajitiaye katikashughuli za dunia, ili ampendeze yeyealiyemwandika awe askari.” Watoto waMungu wanahitaji kuwa waangalifu iliwasifungwe na mambo ya ufalme huuwa kilimwengu. Siasa, utaifa, upinzanin.k. ni mambo ambayo yanaweza kuanzakutuongoza na kututawala na kumfanyamtu kwenda kinyume na kanuni zile kuuza milele za Bwana wetu Yesu Kristo.Ni jambo ambalo linafaa Mkristokumpatia Mungu shukrani kwa ajili yanchi ile ambayo ametoka, kwa barakaule wa ufalme wa kiroho.”na mema ambayo amepata kutokakwa ufalme huu wa kidunia. Watotowa Mungu wanastahili kuwa wenye shukrani kutokana na uhuru waaina yoyote ambao umetolewa na serikali ambazo wao wanaishi ndaniyake kama raia. Lakini shukrani hizo hazistahili kuandamana na ahadi zabure na hata kumfanya Mkristo kufanya nadhiri ambazo ni kinyume nauaminifu na kujitolea kwao kwa Mwana Kondoo wa Mungu. Sisi ni wasafirina wageni nchini humu ambako tulimo, lakini baraka za utaifa wetu wambinguni ni kuu zaidi ya baraka zinazotolewa na serikali za kilimwengu.wa kutambulika kabisa niKuna msimamo ambao Wakristo wanaweza kuwa nao ambao kupitiakwake tutaweza kuishi katika amani na kutambua kwamba hata ingawasisi tunaishi katika falme za kidunia utaifa wetu ulio mkuu na wakutambulika kabisa ni ule ufalme wa kiroho. Gazeti la Ukweli wa Injili ni jalida ambalo linatolewa kila robo ya mwaka kwa manufaa yaKanisa la Mungu kwa ajili ya mafundisho na kwa ajili ya kuwahimiza Wakristo ili washikekweli za Biblia. Tutembelee katika tovuti yetu ya www.thegospeltruth.org na ujiandikishe iliuwe ukitumiwa notisi kwa njia ya barua pepe kila wakati jalida hili likiwa tayari ili uwezekupata toleo la kila kipindi. Gazeti hili la Ukweli wa Injili linachapishwa katika nchi nyingi ililisambazwe katika nchi hizo. Kazi hii inawezekana kupitia kwa matoleo yanayotolewa kwahiari. Pia wewe ukitaka unaweza kutumiwa risiti ya vile tumelipa ushuru kutokana na zawadiyako.—Mhariri, Michael SmithGospel Truth, P.O. Box 2042, Nixa, MO 65714 USAeditor@the gospeltruth.org2Ukweli wa Injili Toleo 26

TahaririNayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, baliyanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni.—1 Wakorintho 10:13Somo la robo hii ya mwaka ni kuhusu swala la Mkristo kuwa na msimamo wakutompinga mtu mwovu, au Mkristo kukataa kushiriki vita kwa sababu ya imaniyake. Lakini kuna tofauti ya maana katika jambo hili, wakati mwingine likichukuliwakuwa na maana ya mtu kuwa na mwelekeo wa kupinga vita vyote au mwelekeo wa kuipinga serikali,jambo ambalo liko kinyume na Mafundisho ya Agano Jipya kuhusu mwelekeo huo wa Mkristo wakutompinga mtu mwovu. Basi katika jarida hili maana ambayo imekusudiwa ni Mkristo kukataakuwa mwanajeshi anayebeba silaha kwa sababu ya kidini.Mafundisho haya kuhusu msimamo wa Mkristo kutompinga mtu mwovu yanapatikana katikaTutembeleeAgano Jipya na sio Agano la Kale. Lakini jambo hili halimaanishi kwamba mafundisho hayowww.thegospeltruth.orghayana msingi kwa sababu mambo mengi yalibadilika kwa ukubwa wakati Kristo alipokuja.Lakini mafundisho hayo ya kutompinga mtu mwovu sio mafundisho ambayo watu dhaifu katikaili kujiandikisha naimani yao katika Kristo wanaweza kukubali. Kuna watu ambao wakisikia mafundisho hayakupata jaridawanaweza kucheka huku wakidhihaki na kusema kwamba mwanaume wa kweli hujikingawakati amekutana na adui. Lakini ukweli ni kwamba ni jambo ambalo linahitaji nguvu na uwezoza mbele.zaidi kwa mtu kuwa na msimamo wa kupenda na kusamehe kuliko msimamo wa kupigana namakonde na silaha. Basi hata ingawa kanuni ya kutopinga mtu mwovu huangazia zaidi swala lakutoshiriki vitani; lakini kanuni hiyo pia inafundisha kuhusu njia bora zaidi ya kuishi, njia ambayoina manufaa zaidi, njia ambayo kwa kuitumia tunaweza kuangusha na kubadilisha maadui zaidiya vile ambavyo silaha hatari sana zinaweza kuwaangusha. Nguvu za msalaba (ambazo hazitumiisilaha), na ambazo hupatikana kwa njia ya kunyenyekea, kamwe hazisalimu amri kutokana na wogawa kidunia. Badala yake nguvu hizo hukumbatia ulimwengu kwa upendo na wema.Wakristo wataelewa kwa njia ambayo haifai mwito wa kumfuata Yesu huku wakiwa na msimamowa kutompinga mtu mwovu kama hawataelewa vizuri kazi na wajibu wa kuweko na falme mbilitofauti. Hata ingawa Mungu ndiye ana haki ya kulipiza kisasi, Yeye hutumia serikali za kidunia kuletahukumu duniani na kudumisha sheria na utaratibu mwema katikati mwa watu wasiomcha Mungu.Kwa kweli tunaweza kuheshimu na kufurahia serikali zetu na uhuru ambao zinatupatia, lakinikufanya hivyo sio lazima sisi tuwe na mwelekeo wa kujitolea kwa serikali hizo, mwelekeo ambaohuenda ukawa kinyume na kujitolea kwetu na nadhiri yetu ambayo tunastahili kumpatia Mungupeke yake. Wakristo ni wageni na wasafiri duniani. Sisi ni wapita njia ambao hatustahili kushikamanasana au kujishughulisha sana na maswala ya ulimwengu huu wa sasa. Siasa na jitihada za kuwaletawatu pamoja kwa ajili ya jambo fulani ambalo linawaletea watu hao shauku nyingi silo jambo ambalolinaonyesha roho wa Kristo. Huu ulimwengu ni nyumbani kwetu kwa muda tu, lakini tunastahilikutumia wakati mwingi na juhudi zaidi kujiandaa kwa ajili ya makao yetu ya milele.Katika mambo yote ambayo tutashiriki tunastahili kujiuliza swali kwamba, “Je, Yesu angewezakushiriki jambo hili?” Tunahitaji kujibu swali hilo sio kulingana na maoni yetu ya kibinafsi balikulingana na mfano ambao tuliachiwa na Kristo. Kamwe hatumwoni Yesu akipigia debe harakati zauhuru wa kisiasa kwa njia ya kutumia vita au kwa kuandamana barabarani. Yesu hakuwaita Wakristopamoja ili wafanye safari kuelekea mji wa Roma, wala hakuwaambia kusimama wima kujilinda dhidiya wale ambao walikuwa wanawatesa. Lakini tunamwona Kristo ambaye alienda hatua zaidi kulikoalivyoamrishwa, huku akiwafanyia mema maadui zake na kuwapenda. Basi mfano ambao Kristoalitupatia hauambatani na matumizi ya mabavu, aidha ikiwa mtu ni mwananchi wa kawaida aukama mtu anaitumikia serikali. Sisi kama kanisa tunahitaji kutimiza wajibu wetu wa kibinafsi na wapamoja, wajibu wa kueneza injili ya amani, na tuiachie serikali kufanya kazi yake bila kuingiliwa kwamabavu.Yohana D. Roth alitoa muhstasari wa jambo hili katika maandishi yake ya Kuamua Kwenda Kinyumena Vita (Choosing Against War), “Mwishowe, msimamo wa Mkristo wa kutoshiriki vita sio jambo lamabishano ambalo lazima mtu ashinde, na pia sio silaha ya mtu kufikia malengo mazuri ya kisiasa,na hata silo jambo la maadili mema ambayo kamwe hayatingisiki. Hili ni jambo hasa la mtu kumfuataYesu kwa moyo wa kweli ambao umejitolea mhanga, hata ikiwa safari hiyo itamfanya mtu huyokufika msalabani.”Michael SmithOktoba, 2018Toleo 26 www.thegospeltruth.org3

Mwongozo wa Kujifunza BibliaSomo: Mafundisho ya Biblia KuhusuMsimamo wa Mkristo wa KutopingaMtu MwovuSomo la Biblia: Mmesikia kwamba imenenwa, jicho kwa jicho, na jino kwa jino; Lakinimimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume,mgeuzie na la pili. Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie najoho pia. Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili.—Mathayo 5:38-41Muhstasari: Mafundisho na mfano ambao Yesu Kristo alitupatia unadhihirisha haja ya Mkristo kuishi maisha ya upendona ya kutompinga mtu mwovu. Yesu amewaita wanafunzi wake ili wafuate mfano wake wa kukabiliana na uovu nakutotendewa haki kwa kutumia silaha ya maombi, upendo, na kusameheana, badala ya silaha za kutumia nguvu namabavu. Katika historia ya kanisa na hata sasa kanisa la Mungu limekuwa na msimamo wa kupinga Wakristo kushirikikatika jeshi.Maana: Kutoshindana na mtu mwovu—Kanuni au mazoea ya Mkristo kutoshindana na mpinzani ambaye anatumiamabavu, au kutoipinga serikali kwa kutumia nguvu, hata ikiwa serikali hiyo inatumia ukatili na udhalimu.Kukataa kushiriki Vita—Mtu kukataa kutumia silaha kama mwanajeshi kwa ajili ya imani yake kuhusiana na maadilibora au kutokana na mafundisho anayoamini ya kidini.I. UnabiiA. Yeremia 31:31 Agano Jipya (Waebrania 8:13)B. Mika 4:2-3 Watu wa Mungu hawatajifunza vitatena.II. Falme MbiliA. Wafilipi 3:20 Uraia wetu ni wa Mbinguni.B. Yohana 3:3 Mtu huingia Ufalme wa Mungukupitia kwa kuzaliwa kwa njia ya kiroho.C. Luka 17:20-21 Ufalme wa Mungu ni ufalme wakiroho (Warumi 14:17).D. Yohana 18:36 Ufalme wa Yesu sio waulimwengu huu.E. Yohana 17:14-16 Wanafunzi wa Kristo wakoulimwenguni lakini wao sio wa ulimwengu huu.F. Waebrania 11:13-16 Sisi ni wageni na wasafiriduniani.G. Waefeso 2:19-20 Sisi tu raia pamoja nawatakatifu wale wengine.III. Mafundisho ya Kristo—Sheria ya UpendoA. Mathayo 22:36-40 Upendo ndio amri kuu zaidi(Warumi 13:9-10).B. Mathayo 5:38-41 Usimpinge mtu mwovu(Luka 6:27-29).C. Mathayo 5:43-48 Miongozo ya jinsi mtu anahitajikumpenda adui yake.IV. Vita vya WatakatifuA. Mathayo 26:51-52 Rudisha upanga wako.B. 2 Wakorintho 10:3-4 Silaha za watakatifu sio zakimwili.C. Waefeso 6:11-12 Mapigano yanahitaji kuwa yakiroho, sio ya kimwili.4Ukweli wa Injili Toleo 26V. Wajibu wa SerikaliA. Danieli 2:21 Mungu huondoa na kuwekawafalme mamlakani (Zaburi 75:7).B. Danieli 4:17 Aliye Mkuu Zaidi ni mtawala katikafalme za wanadamu.C. 1 Petro 2:13-14 Viongozi wa kidunia hupewawajibu wao ili kuwaadhibu wenye kutendamaovu.D. Warumi 13:1-4 Lengo la kuweka serikalimamlakani ni kuleta hukumu kwa yule ambayeametenda maovu (Yeremia 25:8-9).VI. Wajibu wa WatakatifuA. 1 Petro 2:21-24 Tumeitwa ili kufuata mfano waKristo wa kutompinga mtu mwovu.B. 1 Petro 3:9 Wakristo hawastahili kulipiza uovukwa uovu.C. 1 Petro 2:1-3 Kunyenyekea chini ya sheria naserikali za kidunia.D. 1 Timotheo 2:1-3 Waombeeni wale wotewalioko kwenye mamlaka ili watakatifu waishimaisha yenye utulivu na amani.E. 2 Timotheo 2:3-4 Msijiingize sana kwa shughuliza kidunia.F. Warumi 12:14-21 Wabariki wanaokutesa.Usijilipizie kisasi.TamatiKwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwaajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake.—1 Petro 2:21

Mafundisho ya Biblia KuhusuMkristo Kutopinga Mtu MwovuMWITO WA KRISTO KWAMBA TUISHI KWA SHERIA YA UPENDOYesu Kristo ndiye alianzisha mafundisho ya upendo ambayo yanasema kwamba watoto wa Mungu wanahitajikustahimili kutotendewa haki bila kulipiza kisasi, na pia wasilipe maovu kwa maovu. Vita na umwagaji wadamu, mambo ambayo yalikuwa ya kawaida katika kipindi cha Agano la Kale sio mambo ambayo yanakubalikakwa watu wa Mungu ambao wanaishi katika kipindi hiki cha neema ambacho sisi tunaishi ndani yake.Agano JipyaHata ingawa vita na mafundisho ya kulipiza“jicho kwa jicho” yalikuwa mambo ya kimsingina ya mazoea kwa taifa la (kihistoria) la Israelikunalo agano jipya ambalo lilitabiriwa katikaagano hilo la kale. “Angalia, siku zinakuja, asemaBwana, nitakapofanya agano jipya na nyumbaya Israeli, na nyumba ya Yuda” (Yeremia 31:31).Nabii Mika naye alitabiri kwamba kutakujawakati ambapo watu wa Mungu “watafua pangazao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu;taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, walahawatajifunza vita tena kamwe” (Mika 4:2-3).Unabii huu ulitimia katika mpango wa wokovukupitia kwa Bwana wetu Yesu Kristo.Sheria ya Upendo“Ilikuwawakatimuhimu sanawakati Yesu,huku mautiikimnukia,akimwambiaPetrokurudishaupanga wake.”Katika Agano Jipya watu wa Mungu wameitwaili wafuate mafundisho na mfano wa YesuKristo. Kanuni la kimsingi la Kristo lilikuwamafundisho kwamba mtu ampende Mungukuliko kitu kingine chote na pia “Mpende jiraniyako kama nafsi yako” (Mathayo 22:36-40).Watoto wa Mungu wanahitaji kuwa na upendomkuu na kuwajali watu wale wengine wote,na kutaka watu wote wapate mema, hata waleambao wanatenda maovu. Ingawa wana waIsraeli walifuata sera za kivita hata kwa ajili yakufuata mwongozo wa Mungu, Yesu alifundishakwamba sisi tusishiriki vita na pia tusimpingemtu mwovu. “Mmesikia kwamba imenenwa,Jicho kwa jicho, na jino kwa jino; Lakini miminawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakinimtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na lapili” (Mathayo 5:38-39). Andiko hili halikutoamwongozo wa maisha ya mtu kibinafsi tu bali pialilitoa mwongozo kwa watu wa taifa la Kiyahudiambao waliishi chini ya himaya ya utawala wakiimla wa serikali ya Rumi. Hata ingawa watuwengi walikuwa wakimtafuta Masihi ambayeangeshikanisha watu pamoja kufanya vita dhidiya Warumi, Masihi halisi alitufundisha kwamba“tusishindane na mtu mwovu.”Mfano wa YesuJe, ni kweli kwamba Yesu alimaanisha kwambawatu wake hawastahili kushiriki vita? Manenoyake hayakuwa tu ya ufasaha wa usemi aulugha ya kupendeza tu. Ukweli ni kwambailikuwa ni wakati mgumu sana wakati ambapoYesu huku akinukia mauti alimwambia Petrokurudisha upanga wake (Mathayo 26:52).Badala ya kukabiliana na uovu kwa kutumiamabavu na nguvu Yesu aliteseka bila kujibukwa vitisho au matusi. Badala ya kutumiambinu za vita na mabavu Yesu alimwombaBaba yake kuwasamehe maadui zake. Basi Yeyeakadhihirisha kupitia kwa mfano wa maishayake (na wanafunzi wake pia wakadhihirishahayo) kwamba mateso na kuvumilia kutendewavitendo visivyo vya haki na kujibu vitendo hivyokwa upendo ni jambo ambalo ni bora zaidikuliko Mkristo kulipiza kisasi au kujipigana kwamaslahi yake binafsi au hata kwa ajili ya taifalake.Wajibu wa watoto (wa kweli) wa Baba nikuangusha mianzo yote ya vita na vurugu.“Wapendeni adui zenu, waombeeniwanaowaudhi, ili mpate kuwa wana wa Babayenu aliye mbinguni” (Mathayo 5:43-45).Vita vya KirohoMtume Paulo alizungumzia swala la vita vyakiroho na akasema wazi kwamba “Maana ingawatunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwajinsi ya mwili; (maana silaha za vita vyetu siza mwili, bali zina uwezo katika Mungu hatakuangusha ngome;)” (2 Wakorintho 10:3-4).Maisha ya Mkristo yanahitaji kuwa ambayoyametolewa mhanga kutimiza kusudi la Yesu nayenye manufaa kwa ajili ya injili ya amani. Hataingawa Wakristo wamo kwenye ubishi na vitakatika maisha haya ubishi huo na vita hivyo nivya kiroho na wala sio vya kimwili: “Kwa maanakushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama”(Waefeso 6:11-12)Ushahidi wa KihistoriaKulingana na nakala za kihistoria na kwa kufuatamafundisho ya Kristo, Wakristo wa kwanzawalikataa vita kabisa na pia wakakataa umwagajiwa damu. Wanahistoria wameashiria (hataingawa hawajasema kwa njia ya moja kwa moja)kwamba kanuni ya kutoshindana na mtu mwovuimekuwa msimamo wa kanisa tangu mwanzo.Wakristo wa kwanza walikataa kutumika jeshinikwa sababu ya imani yao na kwa ajili ya utiifuwao kwa Kristo. Mwandishi Justin Martyraliandika na kusema: “Sisi tumebadilisha vifaa(Endelea katika Ukurasa 6)Toleo 26 www.thegospeltruth.org5

(Endelea kutoka ukurasa 5)vyetu vya vita vikawa majembe, mapanga yetu yakawamiundu; na mikuki yetu ikawa vifaa vya kulima.” Nayomafundisho ya kale ya kanisa (ambayo yamenakiliwa)yalikataza Wakristo kutumika jeshini.Serikali Za “Kikristo” Ndizo ZililetaMchanganyikoKuna ushahidi kwamba wakatiWakristo walianza kuingilianana mambo ya kidunia ndipowalianza kujiunga na jeshi. Hiindiyo ilifanya mwandishi wakanisa Tertulian hapo mwakawa BK 174 kuandika na kusema,“Je, mtoto wa amani atashirikivitani ilihali hawezi kumshitakimtu mahakamani?” Hapo baadaye“Kuna tofauti kubwamwandishi huyo aliandika nakati ya majukumukusema kwamba ikiwa mwanajeshiataokoka yeye mara moja alihitajiambayo mtoto wakuachana jeshi, au kuwa tayarikupata adhabu ambaye alistahiliMungu ambayekupata kutokana na kuachanaanaishi katikajeshi. Wakati Kaisari Konstantiniwa Roma alipookoka (312 BK)neema kutokana nayeye ndiye alifanya Ukristo kuwadini ambayo ilitambuliwa kisheria.majukumu ambayoJambo hili lilifanya Wakristoserikali imepewa nakuanza kubadilisha msimamo waowa kutoipinga serikali, kwa maanaMungu, majukumusasa serikali haikuwa ya kipagani.Karibu mwaka wa BK 380 Kaisariambayo hufanyaTheodosius na Gratianus walifanyakazi katika mamboUkristo kuwa dini rasmi ya kitaifaya kimwili.” na mwishowe wakawalazimashaaskari jeshi wote kuwa Wakristo.Hii ilikuwa kinyume na msimamowa Wakristo wa kutoipinga serikali, msimamo ambao ndioulikuwa na Wakristo wa kwanza. Wale ambao walikuwaviongozi wa msimamo huu mpya ilikuwa ni viongozi wakijeshi, ambao sasa hata walifanya vita kwa jina la kuwaWakristo.Mgawanyiko Kati ya Mamboya Kidunia na ya Kiroho6Hata sasa Wakristo wengi wameingiliana na mambo yakidunia katika msimamo wao kuhusu swala hili. LakiniMsimamo wa mtoto wa Mungu kuhusiana na swala lakutompinga mtu mwovu hauhitaji kuwa umetokana nahistoria, bali unahitaji kuwa umetokana na mafundishorahisi ya Kristo. Ni jambo la kimsingi mtu kutambuakwamba kuna falme mbili—ufalme mmoja ukiwa wa mpitona mwingine ukiwa wa kiroho. Ufalme wa Mungu sio “waulimwengu huu” (Yohana 18:36) na hata ingawa Wakristowako ulimwenguni wao sio wa ulimwengu huu (Yohana17:14-16). Kama wageni na wapita njia watakatifu waUfalme wa Mungu wanastahili kuepuka vita vya kisasa vyakupigania mambo ya mpito na ambavyo hufanywa kwa jinala taifa, kwa sababu vita hivyo huwa kinyume na matakwaya uraia wa ufalme wa kiroho. Kuna tofauti kubwa kati yamajukumu ambayo mtoto wa Mungu ambaye anaishi katikaneema yakilinganishwa na majukumu ambayo serikaliUkweli wa Injili Toleo 26imepewa na Mungu, majukumu ambayo hufanywa kwanjia ya kimwili. Wakati mwingi majukumu hayo mawilikamwe hayaingiliani.Mungu Ndiye Ameweka Serikali MamlakaniKitabuli cha Danieli kinatufunza kwamba Mungu ndiye“huuzulu wafalme na kuwamilikisha wafalme” (2:21).“Aliye juu anatawala katika ufalme wa wanadamu,naye humpa amtakaye, tena humtawaza juu yake aliyemnyonge” (4:17). Hata ingawa serikali hazina uwezowa kuleta matangamano na amani kamili kwa kutumiasheria kutokana na sababu kwamba wanadamu wengiwamekataa neema ya Mungu, serikali huweza kusaidiakuzuia virugu kwa kutumia mbinu za kimwili. Hiindiyo sababu Mungu ametoa mweke kwa wafalme nawatawala kuadhibu watu wenye kutenda maovu (1 Petro2:13-14). Basi sio kazi ya watakatifu ambao wanaishichini ya neema na upendo kuwapatia adhabu wale watuambao wanatumia mabavu, au wale ambao ni wezihatari, au hata mataifa ambayo huwaletea wananchi waomadhara. Serikali za kidunia zimeitwa “watumishi waMungu” ambao wamewekwa mamlakani na Mungu iliwawe - “amlipizaye kisasi mtenda mabaya kwa ajili yaghadhabu” (Warumi 13:1-4).Wito Ambao Mkristo AmepataHuduma ya kanisa ni kuendeleza umisheni wa Kristoduniani. Huduma ya Kristo haikuwa ya kumwadhibumtenda maovu bali ilikuwa kuleta ujumbe wa wokovuna upendo kwa ulimwengu ulioanguka. Hata ingawaWakristo ni raia wa ulimwengu huu mwito wao ni kuishikulingana na mwito wa juu zaidi. Biblia imetaja waziwazi kuhusu wajibu na majukumu ya mtoto wa Mungu.“Tiini kila kiamriwacho na watu, kwa ajili ya Bwana”(1 Petro 2:13). Wakristo wanastahili kutii sheria zanchi yao mradi iwe kwamba sheria hizo hazihitilafianina sheria ya Mungu. Wakristo wanastahili kuombana kufanya sala “kwa ajili ya wafalme na wote wenyemamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katikautauwa wote na ustahivu. Hili ni zuri, nalo lakubalikambele za Mungu Mwokozi wetu”(1 Timotheo 2:1-3).Lengo letu ni kuishi maisha yenye utulivu na amani;na kama wanajeshi wa msalaba Wakristo hatustahilikuingiliana sana na mambo ya maisha sasa(2 Timotheo 2:3-4).Wakati huu ambapo vita vinaendelea duniani namataifa mengine yanapata nguvu na mengine kuangukawatakatifu wa Mungu wanastahili kuendelea kufuatanyayo zake Kristo (1 Petro 2:21-24)—nyayo zakutolipisha “baya kwa baya” (1 Petro 3:9),kusimama wima kuwapenda wenzao, kufanya memakwa maadui zao (wa kibinafsi na wa kitaifa), kuwabarikiwatesi wao, na kushinda uovu kwa kutenda wema(Warumi 12:14-21).Msimamo wa watakatifu wa kukataa kutumika jeshinini jambo ambalo msingi wake ni mafundisho na mfanowa Mfalme wa Amani. Ni kweli kwamba msimamo wakutompinga mtu mwovu ni jambo ambalo ulimwenguhautaelewa, na ni jambo ambalo litaleta mateso, nahata wakati mwingine litaleta mauti; lakini hayo yoteni matokeo ya kufuata njia nyembamba, njia ambayohumwongoza mtu hadi katika uzima wa milele.

Maswali naMajibuJe, ni jambo ambalo halifai Wakristokutumia nguvu ili kujilinda?Swali hili huzua hisia na ubishi mwingi. Ni jambo muhimu kukumbukakwamba Wakristo (kwa makosa) walizua dhana ya “vita vya haki” iliwapatanishe vita na mafundisho ya kutompinga mtu mwovu. Dhanahiyo inaweza kutumika katika maisha yetu ya kibinafsi. Yesu mwenyewehakujikinga wakati akichapwa na kusulubishwa. Nao mitume wa Kristo namaelfu ya watu wengine ambao waliuawa kwa ajili ya dini hawakulipizakisasi au kufanya vita ili kujilinda wakati wakiuawa kwa njia isiyo ya haki.Ni jambo ambalo si la akili timamu mtu kukosa kujilinda wakati yumohatarini. Basi ni kwa njia ya neema tu na ya kiungu na ya kutokana nauwezo wa Mungu ndipo mtu huweza kukabiliana na hali kama hiyo kwakutumia nguvu zaidi ambazo amepewa na Mungu, nguvu za upendo namsamaha.Kuna wakati ambapo halaiki ya watu walijaribu kumshika Yesu ili wamuue. Lakini Yeye aliweza kuwahepa na kutorokambali nao kwa zaidi ya mara moja. Basi tendo la Mkristo la kumhepa mtu mwenye kuleta madhara sio kitu moja nayeye kutumia nguvu za kimwili ili kujilinda. Lakini kuna hali nyingi ambazo zinaweza kuelezewa kwamba ziko kinyumena ukweli huu. Mimi mwenyewe ninakubali kwamba siwezi kuwaambia watoto wasitumie nguvu za kimwili ili kuhepana kumtoroka mtu ambaye amewateka nyara. Mungu ameahidi kwamba hatatuletea majaribu ambayo ni zaidi ya yaleambayo tunaweza kustahimili, basi ninaamini kwamba tukijipata katika hali mbaya zaidi kutakuwa na neema kubwazaidi na hekima kubwa zaidi kutoka kwake Mungu ambayo itatuwezesha kuendelea kuishi maisha ambayo yanalinganana mafundisho yake Kristo.Je, ni vipi Mkristo anaweza kuunga mkono utawala wa sheria na kazi ya wanajeshi?Kama Wakristo wazuri silo jambo la kinafiki sisi kufurahia kazi na wajibu wa serikali wa kuhakikisha kwamba sheriainafuatwa, na pia kufurahia kazi ya wanajeshi, hata ingawa sisi wenyewe hatushiriki vitani ambako inatubidi tuwaue watu.Kama hakungalikuwa na wadumishaji wa amani wa kitaifa na hata wa kilimwengu kungalikuwa na vurugu ulimwengunikote na uhuru tulio nao ungekuwa hafifu kabisa. Sisi tuko na uhuru ambao tuko nao kwa sababu ya kujitolea kwa watuambao kila siku wanahatarisha maisha yao kwa ajili ya manufaa yetu. Ukweli ni kwamba kuna mambo ambayo tunawezakufanya ili kuunga mkono walinda usalama, mambo mengine yakiwa vitendo vya kiroho vya kuwanufaisha walindausalama. Ni jambo muhimu kwetu kukumbuka kwamba sisi ni raia wa nchi mbili. Huduma yetu ya kwanza kabisa namwongozo wetu maishani unahitaji kuwa kwa ajili ya manufaa ya mambo ya kiroho, lakini hivyo si kusema kwambahatuwezi kufurahia kazi ya watu wale wengine.Pia ni jambo muhimu kwa Wakristo kutotilia umuhimu mkubwa kazi ya serikali, hata ingawa kazi ambazo serikali hizohufanya ni muhimu kwa ajili ya manufaa ya watu wale ambao hawaishi kwenye neema. Basi si jambo bora sisi kupigia debekwa watoto wetu kufanya kazi katika huduma za kidunia ambazo hazilingani na maisha yetu ya Kikristo.JE, TUSEME NINI KUHUSU WATU WANAOKATAA KUTUMIKAJESHINI KWA SABAU YA DHAMIRI ZAO?Kumtii Mungu Badala ya Kumtii MwanadamuKuna watu ambao hukataa kutumika jeshini au kukataa kubeba silaha kutokanana msimamo au maadili yanayoongoza maisha yao, au kutokana na msimamowao wa kidini. Katika historia kuna rekodi ya watu wengi ambao walikumbatiamsimamo huo wa kutoshiriki jeshini, na kutokana na hayo wakafungwa jela auhata kuuawa wakati ambapo imani yao iligongana na msimamo wa serikali zao.Lakini baadhi ya watu hawa ambao walikataa ktutumika jeshini kwa ajili yadhamiri zao mara nyingi walikuwa tayari kufanya huduma jeshini ambazohazikuhusisha matumizi ya silaha, lakini kuna wengine wao ambao walipingautumishi wa aina yote jeshini. Katika siku za hivi karibuni baadhi ya nchi zimetoakibali na kuruhusu watu wanaokataa kushiriki jeshini kwa sababu ya dhamiri nadini zao kuweza kufanya hivyo. Baadhi ya nchi hizo zimetoa njia mbadala ya watuhawa kutumika, badala ya wao kubeba silaha, huduma kama ile ya wananchi wakawaida, badala ya wao kulazimishwa kutumika jeshini.Wakristo wanahitaji kufanya juu chini ili kufanya mambo yote wanayotendayalingane na sheria ambazo serikali zao zimeunda ili waweze kuwa raia wanaoletamanufaa kwa kufuata sheria. Lakini wakati jambo fulani linapohitilafiana na rohoyake Kristo basi Mkristo hana budi kwa unyenyekevu mkubwa kuitiii sheria yaMungu badala ya kutii sheria ya mwanadamu. Toleo 26 www.thegospeltrut

2 Ukweli wa Injili Toleo 26 Gazeti la Ukweli wa Injili ni jalida ambalo linatolewa kila robo ya mwaka kwa manufaa ya Kanisa la Mungu kwa ajili ya mafundisho na kwa ajili ya kuwahimiza Wakristo ili washike kweli za Biblia. Tutembelee katika tovuti yetu ya www.thegospeltruth.org na ujiandikishe ili uwe ukitumiwa notisi kwa njia ya barua pepe kila wakati jalida hili likiwa tayari ili uweze

Related Documents:

Zamani za kale, kabla kabisa ya ulimwengu kuwako, alikuwako mfalme, Mfalme wa utukufu. Mfalme huyu alikuwa mbali, juu sana na ng [ambo ya cho chote na ye yote tunayeweza kumfikiria. Kwenye kutokuwa na mwisho kwa umilele yeye pekeealikuwa Mfalme, na ufalme wake ndio uliokuwa ufalme pekee, enzi yenye hekima, upendo, furaha, na amani kikamilifu.

kama‘āina—has also been a cornerstone of settler colonialism in Hawai‘i. Settler colonialism has drastically refigured the concept of kama‘āina in various popular cultural texts, hapa-haole music being one of many examples, putting focus on the idea of becoming kama‘āina as an eas-ily attainable possibility. This paper will

Holomua, Ka Lei Momi, Ka Leo 0 Ka Lahui, Ka Makaainana, Ko Hawaii Pae Aina, and Nupepa Ka OiaioP The "Mele Aloha Aina" song first appeared in Hawaii Holomua on March 25, 1893, under the title "He Inoa No Na Keiki O Ka Bana Lahui" (A Namesong for the Children of the National Band). The lyrics were reprinted b

Maisha ndani ya Kristo Yako na: Dhambi Utengamano Kusumbuka Yako na: Amani Uzima wa milele Yesu Kristo. 7 . Kama vile buu anavyogeuka kuwa kipepeo na hamu mpya ya maisha mapya pia sisi tunageuzwa kutoka kwa "ufalme wa giza kuelekea katika ufalme wa Mwana mpendwa wa Mungu ". (Wakolosai 1:13, 14).

a) Dhihirisha kuwa ngano hii ni; (alama 3) i. Ngano ya usuli ii. Ngano ya kiayari iii. Hurafa b) Eleza sifa tano za ngano zinazojitokeza katika ngano hii. (alama 5) c) Hii ngano ina mafunzo mbalimbali. Eleza yoyote manne. (alama 4) d) Tambua shughuli zozote mbili za kiuchumi na mbili za kidini zinazojitokeza kwenye ngano hii. (alama 2)

kinachoandikwa kwa Kiswahili au Kiganda kinatoka bila shaka kuwa mali ya fasihi ya Kiswahili au ya Kiganda. Napendekeza na kutilia mkazo kwamba kazi ya tafsiri ifanyike kutoka lugha zote mbili. Pendekezo zaidi ni kuomba wenyeji wa lugha zote mbili watilie . Watafiti wageni ingawa huwa na

mawazo ya wanamsambao hususani katika ugawaji wa ngano bila kuchunguza kwa umakini sifa ya kila kundi. Propp anaamini kuwa ili kuchunguza asili ya ngano ni vema kuanza kuchunguza aina za ngano kwa kuangalia maumbo ya ngano. Hivyo mtazamo huu unaangalia asili ya ngano kwa kuchunguza maumbo ya ngano husika. Ubora wa nadhairia hii, nadharia hii inasaidia kujua aina za ngano kutokana na dhima zake .

The Community Medicine curriculum at Tufts University Family Medicine Residency will provide resident physicians with an understanding of the social, economic, and cultural contexts of health and an appreciation of the public health perspective on community well-being. The second year Community Medicine program includes a mix